Simulizi: Soka Lilivyonikutanisha Na Shetani

Simulizi: Soka Lilivyonikutanisha Na Shetani

Sehemu ya 77

Nilitembea nikipita mjini Malindi, Mji Mkongwe kisha Darajani. Nikapanda daladala ya Kiembe Samaki. Muda mfupi badaye niliwasili nyumbani kwa Sheikh Majeed Mapaka.

Nilimkuta sheikh huyo akiwa nje ya nyumba yake anasikiliza redio. Aliponiona akanilaki kwa ukarimu. “Ni wewe!” “Naam! sheikh ni mimi.

Asalaam alyekum.” “Walyekum wasalaam, karibu sana, habari za siku.” “Siyo salama ndugu yangu,” nilimwambia. Mganga huyo wala hakuniuliza kwa nini nasema siyo salama. Alichofanya ni kunikaribishia ndani, katika chumba cha kiganga kisha akaanzisha maongezi: “Haya nambie hujambo?” “Mimi mzima kimwili sheikh ila kiakili siko sawa”

“Nini tena?” “Ina maana hukuwahi kupata taarifa zangu sheikh?” badala ya kujibu na mimi nikamtupia swali. “Nizipatia wapi? Wewe na mwenzio hamkuwahi kurudi tena hapa.” “Sasa iko hivi... “ nilianza kueleza. “Jamaa walijibu mashambulizi bwana. Tena mashambulizi yao ilikuwa nusu nife.

Walinipiga kipapai nikawa kichaa aliyeshindikana huko mtaani.” “Acha wewe!” “Alaa! Washenzi sana wale watu wa Mbeya.” “Huyu huyu Mnyakyusa tuliyemzika jina makaburini! Kawezaje huyu mtoto lakini!!” “Huyo huyo!” “Eboo! Aliwezaje?” “Nitajulia wapi?” “Siyo bure wametumia uchawi wa kiwango kikubwa sana.” Mtaalamu yule alisema.

Nilimweleza kila kitu kilichonitokea maishani. Kadhalika, sikuacha kumueleza ukweli wa mambo mawili yaliyonipeleka Zanzibar siku hiyo. “Kwa hiyo unataka ufanyiwe kazi mbili tofauti?” Sheikh Majeed Mapaka aliniuliza baada ya kusikiliza maelezo yangu kwa makini.

“Tawire.” “Kumrudisha mchumba aliyeolewa nchini Yemen na kulipiza kisasasi kwa watesi wako?” Shekh Majeed Mapaka alihoji kwa msisitizo. “Swadakta.” “Sasa huyo mwanamke unayemtaka wa nini ilihali umenieleza unaye mke, tena ndiye alikusaidia kukupeleka kwa mtaalamu wa huko Kigoma.”

“Joto la penzi linalofukuta moyoni mwangu dhidi ya Lawalawa najua mwenyewe ninavyoteseka kwa kumkosa huyu mwanamke. Niko tayari kufanya lolote lakini Lawalawa arudi mikononi mwangu.”

“Gharama yake itakuwa kubwa kidogo, hasa kwa kazi ya kumrudisha mpenzi aliyeko mbali. Unajua kazi yenyewe ni kuvunja ndoa ya mtu? Mara nyingi kazi za hivi huwa zinasumbua sana.”
 
Sehemu ya 78

“Itakuwa kama gharama kiasi gani kwa kazi zote mbili?” nilimuliza. “Kabla ya kukutajia gharama. Hili la kisasi unataka hao Wanyakyusa akina ‘Kamwene’ wapewe adhabu gani?”

“Ikiwezekana hata kifo, wote waliohusika wakafie mbali.” “Kifo itakuwa ngumu, huwa siuwi. Chagua adhabu nyingine.” Sheikh Majeed Mapaka aliniambia kwa ukali. “Basi watie uchizi, yeyote aliyehusika kuniroga, mtie uchizi sambamba na donda lisilopona sehemu yoyote mwilini, yanii liwe ni donda ndugu.”

“Sawa, kwa kazi zote mbili pamoja na vifaa itabidi ulipie laki tano.” “Mbona nyingi. Haiwezi kupungua, maana kama nilivyokueleza, sasa hivi nafanya kazi za jua kali, faida kiduchu.” “Hapo haipunguki hata senti, ” Sheikh Majeed Mapaka alinijibu bila kuniangalia usoni.
Mpumbavu mimi sikuwa na jinsi. Maji nilikwisha yavulia nguo ilikuwa ni lazima niyaoge.

Mfukoni nilikuwa na shilingi laki tano taslimu, ambazo zilikuwa ni fedha za kuchukulia mzigo wa dagaa. Lakini kwa kuwa nilikuwa na wahaka na jambo langu, hakuna nilichojali.

Nilikuwa ladhi nilipie fedha yote. Kama kurudi Dar hata kwa kuogelea ningekubali, lakini siyo kumkosa mpenzi wangu Lawalawa na kuwaadabisha washenzi walinipa ukichaa na kuzima ndoto zangu.

Hata hivyo, nafsi yangu ilibaki kwenye ukinzani wa ndani kwa ndani. Nikawaza: “Nikilipa fedha yote ile. Nitarudi vipi Dar es Saalam, vipi kuhusu mke wangu Pili, naye nitamweleza nini kuhusu fedha za biashara tulizosaidiwa na babu Mo na mkewe bibi Mo kwa ajili ya biashara? Nitamdanganya vipi huyu kiumbe? “Ah! Potelea mbali, siwezi kukosa la kusema, katika makubwa ya kuhofia, sio hili la eti nitamwambia nini mke wangu.

Nilijitia moyo na kujipumbaza kwa kiburi cha uhayawani. Mpumbavu mimi nikalipa laki tano kwa mganga Sheikh Majeed Mapaka.

Baada ya kumpa mzigo ule wa fedha mganga huyo akanieleza: “Kuna mambo machache ambayo nitahitaji nipate.” “Kama mambo yapi?”

“Kwanza nitahitaji picha ya huyo binti na majina ya wazazi wake. Hiyo ni kazi ya kwanza, kadhalika kwa hii kazi ya pili, ningependa nipate jina la yule mchezaji kutoka Mbeya. Huyo hasimu wako huyu.”
 
Sehemu ya 79

“Jina la huyu mchezaji anaitwa Felix Kisu. Lakini kuhusu picha ya Lawalawa, nakuapia kwa jina la Mungu wangu wa mbinguni. Sioni pakuipatia picha yake.” Sheikh Majeed Mapaka alifikiria kidogo kisha akanieleza:

“Sawa, nitajie majina ya wazazi wake wote wawili.” Nilimtajia majina ya wazazi wa Lawalawa kisha akaniambia niondoke nirudi siku inayofuatia kwa ajili ya kuanza kazi pamoja.

Niliondoka nyumbani kwa mganga huyo nikiwa sina fedha yoyote iliyosalia. Hata hivyo sikupenda kumweleza Sheikh Majeed Mapaka hali yangu. Sio vizuri katika maisha kutangaza dhiki kwa mtu ambaye ni nadra kupata msaada utakao.

Nilichofanya baada ya kuondoka nilimpigia simu mke wangu. “Niko kwenye matatizo mke wangu!” nilianza kumdanganya mwanamke huyo aliyekuwa akinipenda kwa moyo wake wote. “Mungu wangu kuna nini tena, umepatwa na nini wewe!”

“Nimevamiwa, nimeibiwa fedha! Niongeavyo nawe nipo hospitali ya Temeke, hali yangu ni dhoofu.” “ Toba! Pili mimi! Jamani kwa nini niwe mimi tu miaka yote!!!” mke wangu alichanganyikiwa.

“Sikiliza mama...Unasikia Pili. Nisikilize..” Eeh unaendeleaje....” nilimsikia Pili akiwa anaongea huku kwikwi za kilio zikimtoka. “Hapa nilipo sina hata senti ya dawa, nifanyie mpango nipate japo laki moja muda huu huu. Yanii sasa hivi.” “Sawa, sawa, sawa...Ninayo akiba yangu.

Nakutumia sasa hivi mume wangu.” Namna alivyozungumza baada ya kumpa taarifa za uongo sauti yake ilitoa ujumbe mzito nafsini mwangu. Mwanamke huyo alikuwa ananijali kwa kiwango cha mwisho.

Laiti kama angalijua nilikuwa Zanzibar nikifanya matendo ya kishirikina ili tu kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, Lawalawa, bila shaka mke weangu Pili angeweza hata kujito roho yake.
Dakika chache badaye, laki mbili ilitumwa kwenye simu. Kisha akanipigia.

“Umeona?” “Nimeona mke wangu. Ahsante.” “Hawajakuumiza hao wavamizi?” “Kiasi fulani.” “Ilikuwaje, mbona simu yako ipo...?” “Subiri, tutaongea zaidi badaye.” Nilimkataishia. Nikakata simu.

Baada ya kupata ile fedha nilitafuta hoteli na kulala siku hiyo. Akili yangu ilikuwa inawaza jambo moja tu, kumrudisha Lawalawa mikononi mwangu.
Asubuhi ya siku ya pili nilirudi kwa mganga. Sheikh Majeed Mapaka.
 
Jamaa utadhani alitoka utumbo mmoja n shetani,,,,sio kwa roho mbaya hyo anayo mfanyia mkewe

#dunian kuna watu waxenge km ajbu !!
#***** !!
 
Sehemu ya 80

Asubuhi ya siku ya pili nilirudi kwa mganga. Sheikh Majeed Mapaka. “Kazi zako zote zitakwenda vizuri, mke wako itabidi nimtupie jini la kumleta.” Sheikh Majeed Mapaka aliniambia.

“Eeh!” “Ndio, popote atakapokuwa duniani. Jini ninayemtumia akishamwingia tu, siku tano nyingi.

Utamwona atakavyo kusaka.” Maneno yake yalinifurahisha sana.
Alitoka nje ya kilinge kile, punde akarudi na njiwa mwesi tii. “Huyu mdudu ndiye atakuletea mali yako” alisema.

Alichukua hirizi fulani, akamfungia yule njiwa mweusi shingoni, akachukua karatasi nyeupe akaandika jina langu na la Lawalawa kwa wino mwekundu unaomwagika.

Maandishi hayo aliyandika kwa lugha ya Kiarabu. Akaandika maneno mengine nisiyoyafahamu. Baada ya hapo ile karatasi akailoweka kwenye maji safi. Wino wote katika karatasi ukaishilizia kwenye maji ambayo yalibadilika rangi na kuwa mekundu kama damu.

Baada ya tukio hilo alimkamata yele njiwa akamfungua mdomo na kumnywesha kwa nguvu yale maji.

Akaniambia nimnuize yule ndege jambo lolote nitakalolitaka kuhusu Lawalawa. Nikasema: “Namtaka Lawalawa arudi kwangu, mlete haraka iwezekanavyo, asifikirie jambo lolote zaidi yangu,” niliongea kumwambia yule njiwa.

“Tayari?” Sheikh Majeed Mapaka aliniuliza. “Ndio, tayari.” Alimchukua yule njiwa mikononi mwangu, kisha akamwachia. Ndege huyo alibakia amezubaa. Muda mchache badaye, akatoka kupitia mlangoni. Tukawa tukimwangalia tu. Akatoka nje kisha akapaa angani na kupotelea mtaani.

“Kazi ya kwanza imekwisha. Imebakia hii.” Sheikh Majeed Mapaka aliniambia.
Akaanza kufanya kazi ya kumwadabisha Felix Kisu, mchezaji mwenzangu aliyenitia uchizi.

Kwanza lazima niangalie alitumia uchawi wenye nguvu kiasi gani, mambo haya siyo ya kuingia kichwa kichwa, tunaweza kufa wote hapa,” Sheikh Majeed Mapaka aliniambia.

Alimwita mkewe, ambaye kama nilivyowahi kusimulia huko nyuma alikuwa ni moja ya wanawake wenye sura nzuri na shepu ya kuvutia, ambao kwa bahati mbaya maisha yake yaliangukia kwa mganga wa kienyeji, anayeroga na kuponya.

Baada ya mkewe kuingia ndani, akiwa kwenye vazi la baibui. Sheikh Majeed Mapaka alichukua ubani akauchoma kwenye kichezo, kisha akajifunika shuka jekundu.
 
Sehemu ya 81

Baada ya mkewe kuingia ndani, akiwa kwenye vazi la baibui. Sheikh Majeed Mapaka alichukua ubani akauchoma kwenye kichezo, kisha akajifunika shuka jekundu. Akaanza kuimba wimbo fulani hivi huku akipiga chakachaka.

Mara majini yakampanda. Kwa sauti ya kuunguruma akaniambia nimpe kiganja cha mkono wangu. hakuwa yeye bali jini. Nikampa mkono.

Akanishika na kuniangalia, halafu akashika kichwa changu kisha akaniambia: “Mshukuru sana mganga aliyekutibia maradhi yako, Jini ulilokuwa umetupiwa ni hatari sana. Lakini pia...”alisema akaendelea:

“Naona siyo rahisi kumrudi hasimu wako. Analindwa na viumbe hatari mno.” “Kwa hiyo?” “Ngoja tujaribu.” Sikuongeza kitu, nilichokuwa nataka ni kuona wabaya wangu wanateseka.

Jini lililokuwa limepanda kwenye kichwa cha mganga sheikh Majeed Mapaka, lilianza kumpa maelekezo ya mazindiko na dawa mke wa mganga.

Miongoni mwa mambo aliyoelezwa mke wa mganga ni kwenda makaburini usiku wa manane kwa ajili ya kuchukua kivuli cha maiti.
Toba!!. Baada ya dakika kadhaa, jini likamuondoka sheikh Majeed Mapaka. Mkewe akamsimulia kila kitu alichoambiwa.

Sheikh Majeed Mapaka alionekana kushitushwa na baadhi ya mambo aliyotakiwa kufanya. “Watu ninaotakiwa kupambana nao ni hatari sana, hii kazi ni ngumu zaidi ya nilivyokuwa naifikiria. Kuchukua kivuli cha maiti makaburini si mchezo. ” Sheikh Majeed Mapaka, aliniambia.

Shiit!. “Kwahiyo?” nilimuliza mganga yule. Kauli yake ilionesha ni kama aliogopa kufanya kazi hiyo. “Nitajaribu,” alinijibu.

Alinitaka usiku wa siku hiyo niambatane naye hadi makaburini, huko tungechukua kivuli cha maiti ambacho ndicho kingetumika kama silaha ya kumwangamiza Felix Kisu.

Ingawa nilikuwa naogopa kwenda makaburini, hasa majira ya usiku, hata hivyo, sikuwa na la kufanya. Maji nilikwisha yavulia nguo, sikuwa na budi kuyaoga. Ilikuwa ni lazima nimfunze adabu Felix Kisu.

Nilishinda pale nyumbani kwa mganga kusubiri usiku uingie ili tuongozane makaburi. Ilipotimu saa mbili usiku mtaalam aliniambia lazima tuendelee kungoja hadi usiku uwe mkubwa ndipo twende huko. “Kivuli cha maiti tutakipta vipi?” hatimaye niliuliza baada ya jambo hilo kunifikilisha kwa muda mrefu.
 
Sehemu ya 82

“Kivuli cha maiti tutakipta vipi?” hatimaye niliuliza baada ya jambo hilo kunifikilisha kwa muda mrefu. Kupata kivuli cha maiti.

“Ni mchakato unaogopesha kidogo, na itakupasa uwe jasiri alijibu,” sheikh Majeed Mapaka alisema, ingawa hakuwa amejibu swali langu.

“Sijakuelewa mtaalamu.” “Ninamaanisha mchakato wa kukipata kivuli sharti uwe na roho ya chuma.” “Kwa nini?” “Kwa sababu tunafukua kaburi na kuitoa maiti, kisha kivuli chake kinachukuliwa.”

“Whaat!” nilimaka. Macho yalinitoka kama kinyonga. Nikamwambia: “Siwezi hiyo kazi.” “Kazi hutaifanya wewe. Nitaifanya mimi.” “Sasa mimi naongoza na wewe kufanya nini?” “Ili unisadie kubeba mwili wa mtu atakayekuwa amefukuliwa.” “Niniiiii!!” “Ndiyo.

Na ili tuweze kupata kivuli chake, ni kazi ya dakika tu.” “Nibebe maiti?” “Kuna kazi gani hapo?” sheikh Majeed aliongea katika namna ya kunionesha tukio alilokuwa akilielezea lilikuwa ni la kawaida sana.

“Ni kazi ngumu na ya kuogopesaha mtaalamu, hakuna mtu anayeweza kufanya hicho ambacho natakiwa nikakifanye mimi?” “Huyo tu mwingine unayemuongelea unamjua? Ni yeye ndiye mwenye matatizo ama wewe?” Sikuwa na jibu na kauli hiyo. Sikuwa na jinsi ilikuwa ni lazima nifanye kazi aliyoisema sheikh Majeed Mapaka.

Kuanzia majira yale ya saa nne nilikosa kabisa amani, tuliendelea kukaa na mganga huyo tukizungumza mambo mengi kuvuta muda wa kwenda makaburini, katika kipindi chote mganga huyo alikuwa akinisimulia kazi mbalimbali za kuogofya ambazo amekwisha wahi kuzifanya tkushinda ya siku hiyo.

“Kazi yako haiogopeshi sana ingawa inaoensha ni ya hatari, kuna kazi zinatisha bwana wewe!” “Wacha wee!” “Ndio. Kuna kazi zingine masharti yake sharti uzikwe ukiwa hai ndani ya siku saba. Ungeweza wewe.” “Duuh!” “Ndio.

Kuna kazi zina masharti magumu sana, ipo nyingine inakubidi uende mochwari ukafanye mapenzi na maiti ya mwanamke.” Kwa kweli mganga huyo alinieleza mambo mengi sana. Kufumba na kufumbua saa saba usiku ikaitimu.

“Hatimaye muda wa kuondoka umefika,” jamaa alinieleza, nilihisi tumbo zima likilipuka kwa woga. Lakini ningefanya nini? Njia niliyokuwa nimechagua kupita dhidi ya watesi wangu ni hiyo.
Tulijiandaa.
 
Sehemu ya 83

Tulijiandaa. Majeed Mapaka akachukua vifaa vyake vya kazi, kisha tukatembea hadi makaburini. Sikumbuki vizuri jina la makaburi ya pale Kiembe Samaki Unguja, ilikuwa panajulikanaje, makaburi yalikuwa yamezingirwa na vichaka na miti mikubwa.

Ninaposema mganga yule alikuwa amechukua vifaa vyake vya kazi ninakuwa na maana, kwamba alikuwa amebeba baadhi ya ndumba kama hirizi, pembe fulani kama ya ngo’mbe, sambamba na koleo la kuchimbulia kaburi. Koleo nilipewa mimi nibebe.

Japokuwa ililikuwa ni usiku, upepo ulikuwa ukivuma, lakini maungo yangu yalikuwa yakichuruzika jasho. Kufukua kaburi na kutoa maiti kisha kuchukua kivuli chake ilikuwa ni kazi ya aina yake maishani.

Mbalamwezi ilikuwa iking’aa angani, lakini hilo halikufanya eneo lile la makaburi lisiogopeshe. Tulitembea hadi katikati ya makaburi. Tukasimama chini ya mti wa mwarobaini uliokuwa umechipua. “Kama nilivyokwambia yakupasa uwe jasiri.” Mganga yule akaniambia.

Sikumjibu kitu, nilitikisa tu kichwa huku jasho jembamba likizidi kunichuruzika maungoni. Jamaa alivaa hirizi, akavaa na shanga fulani shingoni mwake. Akavua nguo zake zote na kuvaa kaniki.

Kisha akanieleza kwamba anatafuta kaburi ambalo ni la siku za hivi karibuni.

Akanieleza natakiwa kuendelea kusimama hapo kwenye mti wakati yeye anafanya kazi ya kulitafuta hilo kaburi.
Sikujua anatumia njia gani kulijua kaburi jipya, hasa kwa kuwa muda huo ulikuwa ni usiku. Sikutaka kuhoji sana. Nilibakia pale chini ya mti, jamaa akiendelea kulisaka kaburi jipya.

Nikiwa pale peke yangu nilikuwa naogopa vibaya sana, ungeniuliza nilikuwa ninaogopa nini kamwe nisingeweza kuwa na majibu ya msingi. Hata hivyo nakiri moyo wangu uligubikwa na mashaka na wasiwasi.

Muda mfupi badaye, mganga alirudi. “Nimepata kaburi jipya, haya twende.” Tuliongozana hadi kwenye hilo kaburi jipya alilolizungumzia.

Hatua chache tukalifikia kaburi hilo, lilikuwa ni kaburi la mtu mzima, kweli lilionekana ni kaburi la ambalo mtu aliyezikwa ndani yake hakuwa na siku tatu.

mganga Majeed Mapaka,alichukua unga unga fulani kama ubani, akautia kwenye kichezo, kisha akawasha njiti ya kiberiti na kuwasha unga huo. Ulitoa mlipuko mdogo kisha moshi mwingi ukafuka.
 
Sehemu ya 84

mganga Majeed Mapaka alichukua unga unga fulani kama ubani, akautia kwenye kichezo, kisha akawasha njiti ya kiberiti na kuwasha unga huo. Ulitoa mlipuko mdogo kisha moshi mwingi ukafuka.

Alilizunguka kaburi lile akiwa na kichezo cha ubani ambacho kilikuwa kinatoa moshi wa unga ule ambao kwa kweli hadi leo sijui ilikuwa ni kitu gani.

Baada ya kulizunguka kaburi mara tatu, akasimama upande wa miguuni mwa kaburi lile, kisha akaniambia mimi nisimame upande wa kichwani.

Baada ya tukio hilo, mganga akawa kama ananua maneno fulani ambayo sikuwa nayasikia kaburini hapo. Bado lile chepe ama koleo lilikuwa bado mikononi mwangu. Sikupenda kabisa mimi ndio nifanye kazi ya kufukua kaburi.

Kama nilivyosema mwanzo, ningefanya nini, maji nilikwishayavulia nguo, sina budi kuyaoga. Baada ya kumaliza kunuia maneno fulani kaburini hapo, akaniambia nianze kuchimbua kutoa udongo. “Mungu wangu. mimi ndio nafukue kaburi?” nilijikuta naongea kwa hamaniko kubwa.

“Nani mwenye shida na kazi hii ambaye unataka afanye kazi hii?” Maneno ya mganga Majeed Mapaka yalinikata maini, nilitamani hata nighairi zoezi lile. Hata hivyo bado nilikuwa na chembe ya ujasiri iliyokuwa imesalia kifuani mwangu.

Mpenzi msomaji huwezi kuamini nilianza kufukua kaburi, nikawa natoa udongo na kuuweka kando. “Haraka haraka,” Majeed Mapaka alinikoromea.

Nikaongeza kasi ya kuchimbua, nilipochimba kama makoleo kumi, akaniambia nisubiri. “Shika hii, vua nguo upake mwili mzima.” Alinipa kichupa cha mafuta fulani ya maji, kama ya griselini. Nilivua nguo nikabaki na ya ndani kisha nikapaka mafuta hayo mwili wote kama nilivyotakiwa. “Endelea kuchimbua bila nguo,” aliniambia. Yanii niendelee na zoezi la kufukua kaburi nikiwa uchi.

Ningefanya nini kupinga masharti hayo ilihali nilikuwa nataka cha uvunguni.
Nikaendelea kuchimbua kaburi. Jambo la ajabu kabisa kadirili nilivyokuwa nikiendelea kuchimbua shimo lile nidvyo hata ule wasiwasi wangu ulivyozidi kupotea. Bila shaka ni kutokana na mafuta niliyokuwa nimepaka mwilini.

Nilichimbua kwa muda mrefu kidogo, sikufika futi sita nikawa nimegota kwenye kilele, nilibaini hilo baada ya kukita koleo kwenye ubao ambao ulitumika kutengenezea mwanandani......... Toba.
 
Mkuu shunie samahani. Kama una part 2 .3.4 ya Siri. Naomba .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom