Simulizi: Penzi ama kaburi?

Simulizi: Penzi ama kaburi?

Sehemu ya 45.

Shadya alijikaza mpaka chumbani kwake, akapanda kitandani na kuanza kulia kwa maumivu makali kama mtu aliyefiwa na mtu muhimu katika maisha yake.

Hakuamini kama kweli alichana na Gibson baada ya kumuona mwanaume huyo haeleweki hata kidogo. Kipindi hicho alihitaji sana kubembelezwa, alifikiria mtu sahihi wa kumbembeleza, akahisi kaka yake, Rahim alifaa lakini akagundua hakuwa mtu sahihi.

Mtu wa mwisho kabisa kuja akilini mwake akawa Alex, aliamini kwa jinsi alivyokuwa mshauri mzuri basi angeweza kumliwaza kwa maneno matamu na kumwambia ni kitu gani alitakiwa kufanya.

Akachukua simu yake na kumpigia, ikapokelewa na kuanza kuzungumza naye. Alimwambia ukweli kwamba aliachana na mpenzi wake, ilimuuma mno moyoni mwake, alikuwa na maumivu kupita kawaida.

“Pole sana! Ila mwanaume amekuacha wewe?” aliuliza Alex kwenye simu huku akionekana kushangaa.
“Ndiyo!”
“Kuna wanaume wapumbavu sana! Kumbe mpaka karne hii kuna wanaume wajinga kiasi hiki! Mungu wangu!” alisema Alex.


“Kwa nini unasema hivyo?”
“Yaani mwanaume amekuacha wewe?”
“Ndiyo!”
“Ni ujinga ulioje? Pole sana. So nikusaidie nini?”
“Nahitaji nikuone! Tuzungumze mengi, unishauri ya kunishauri!”
“Basi haina shida.

Nakuja,” alisema kijana huyo na kukata simu, kidogo sana Shadya akajisikia ahueni, ila bado moyo wake ulikuwa na maumivu makali ya Gibson, yaani mwanaume huyo alimuumiza vilivyo.
.
.
.
Je nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 46.

Kulikuwa na mambo magumu sana duniani, mambo ambayo hata kama ungetumia muda mrefu kiasi gani usingeweza kufanikisha. Kulikuwa na wanawake wagumu duniani ambao hata kama ungetumia maneno laini usingeweza kuwatia mikononi mwako.

Hiyo haikuwa kwa Shadya, alionekana kuwa msichana mwepesi kwa Alex kwa sababu tayari moyo wake ulijeruhiwa na kipindi hicho alikuwa akihitaji sana faraja kutoka kwa mwanaume yeyote yule.

Ndani ya bajaji aliyopanda kijana huyo alikuwa akifikiria mambo mengi, kwanza uzuri wa msichana huyo, jinsi alivyovutia na kuonekana kuwa msichana wa tofauti kabisa, lakini pia akaanza kufikiria njia mbalimbali ambazo angetumia kumnasa Shadya, aliamini angefanikiwa katika hilo.

“Mtoto wa Kimanga! Wallahi huyu simuachi,” alijisemea.
Haikuchukua muda akafika mahali alipokuwa Shadya na kuanza kuzungumza naye. Kwa kumwangalia tu machoni hakuonekana kuwa sawa hata kidogo, aliumizwa, macho yake yalikuwa mekundu kwa sababu alitumia muda mwingi kulia kuliko hata kutabasamu.

Alex aliligundua hilo, kitu cha kwanza alichokifanya ni kuonyesha sura ya majonzi mno, alionyesha kuumizwa kwa kilichotokea kwa kuwa naye mwenyewe alikuwa akihitaji sana kuwa na msichana huyo mrembo.

“Yaani kuna mwanaume anaweza kukuumiza namna hii?” aliuliza Alex, miongoni mwa watu walioonekana kuumizwa na kile kilichokuwa kikiendelea kwa Shadya, alionekana kuwa wa kwanza.
“Ila kawaida tu! Wanaume mpo hivyo!” alisema msichana huyo.

“Hapana! Usitufananishe sisi wengine na wapumbavu kama hao. Hivi inakuwaje mpaka unamuumiza mwanamke kiasi hiki? Machozi ya mwanamke ni laana, akiamua kupiga goti na kulia kwa ajili yako, laana zote za mababu zitakufuata wewe,” alisema Alex, kwa jinsi alivyokuwa akizungumza, naye alionekana kuwa kama alikuwa upande wa Shadya.

“Nyie wanaume nyie! Hata Gibson alisema hivyohivyo!” alisema Shadya.
“Kuna kitu unakosea sana Shadya!” alisema Alex, akaanza saundi zake kama kawaida.
“Kitu gani?”
 
Sehemu ya 47.

“Kwa nini ulitokea kumwamini huyo fala haraka sana?” aliuliza, ili kumpata msichana yeyote duniani kwanza ni lazima utengeneze uadui na mtu aliyemuumiza, yaani aone kama na wewe umeanza kumchukia kumbe hakuna lolote.

“Unamuita fala tena!”
“Kila mwanaume anayediriki kumuumiza mwanamke yeyote kwangu ni fala tu! Haiwezekani umuumize mtoto wa kike namna hii, kila wakati awe analia kwa ajili yako, kama humtaki, kwa nini ulimfuata?” aliuliza huku uso wake ukiendelea kuwa vilevile, unafiki mwanzo mwisho.

“Kwa sababu alipata alichokitaka!”
“Kuna wanaume wangapi wanapata wanachokitaka lakini mwisho wa siku wanaamua kutulia na watu hao? Shdaya, nikwambie ukweli tu, hakuna kitu ambacho kimeniumiza mno kama wewe kuumizwa na huyo jamaa. Hebu naomba namba yake kwanza,” alisema Alex.

“Wewe ya nini?”
“Naomba tu!”
“Unataka umtukane!”
“Wewe naomba Shadya! Kuna mambo mengi ya kuvumilia, kuna wapuuzi wengi sana ambao tunaweza kuwavumilia lakini si wapuuzi kama hawa! Inaniumiza sana kwa sababu sijawahi kumuona hata baba yangu akimuumiza mama, kwa nini huyu pimbi mmoja afanye hivi?” alisema Alex.

“Lakini si una....”
“Usimtetetee...naomba namba yake!” alisema Shadya.
“Kwa namba siwezi kukupa!”
“Bado unampenda?”
“Hapana! Simuhitaji!”
“Basi naomba namba yake!”
“Haiwezekani! Sitaki kuona ukimtukana, siwezi,” alisema Shadya.

Mpaka hapo Alex alijiona kuwa mshindi, hakuamini kama alifanikiwa kwa kiasi kikubwa namna hiyo. Mwanamke anahitaji kutetewa kwa vyovyote vile, kwa kitendo cha kuhitaji namba ya Gibson kwa lengo la kujifanya kutaka kumtukana kisa tu alimuumiza Shadya, msichana huyo tayari aliona kama alikuwa upande wake.

Akakataa kumpa, Alex hakutaka kujali, alichomwambia ni kwamba alihitaji kukaa naye, wazungumze mambo mengi na kumsahaulisha kwa yale yaliyotokea.

Hilo halikuwa tatizo, Shadya akakubaliana naye na hivyo kuondoka na kuelekea katika Ufukwe wa Kunduchi.
Walipofika huko wakatafuta sehemu nzuri pembeni ya boti iliyopakiwa na kutulia hapo. Wakaanza kuzungumza mambo mengi yaliyotokea katika maisha yao.
 
Sehemu ya 48

Kama kawaida Gibson hakutakiwa kuwa mkweli kwa lolote lile, ilikuwa ni lazima kumfanya msichana huyo ajue alikuwa hana kosa, ajifanye kabisa alikuwa mtu mwema kuliko wanaume wote katika dunia hii.

“Ila unaposema sisi wanaume wote tupo hivi huwa unakosea sana,” alisema Alex.
“Kwa sababu gani?”

“Niliwahi kuwa na uhusiano na msichana mmoja aitwaye Upendo. Nilimpenda sana, nilimpa kila kitu alichokuwa akikihitaji katika maisha yake. Huwa ninapokuwa na msichana ninapenda mno kujitoa kwa kila hali ili awe na furaha,” alisema, kama kawaida alikuwa akitunga kauongo fulani kazuri sana.

“Ikawaje?”
“Yaani sijui nisemeje. Baada ya siku kadhaa, nikawa nimeamua kumnunulia zawadi fulani hivi, nikaenda kumpelekea nyumbani kwake. Akaipokea, nikamwambia ninataka tutoke kidogo kwa ajili ya dinner, akakubali hivyo akaenda kuoga,” alisema huku Shadya akisikiliza kwa makini kabisa.

“Ikawaje?”
“Sasa alipokuwa bafuni nikasikia simu yake imelia kama kuna ujumbe, si unajua hizi touch, meseji ikapop up pale juu, nilichokisoma, niliumia sana,” alisema Gibson, kwanza akanyamaza, akaangalia chini halafu akatingisha kichwa chake kuonyesha kuumizwa.

“Ikawaje?”
“Hawa wanawake hawa! Dah!”
“Ikawaje?”
“Tuishie hapo!”
“Hapana! Hebu niambie! Ujumbe ulisemaje?” aliuliza Shadya.

Kitu muhimu alichokifanya kijana huyo ni kuuchukua utulivu wa Shadya, alihitaji kumuweka katika hali ambayo ingemfanya kuwa makini sana kumfutilia kwa kile alichokuwa akikizungumza na kukiweka akilini mwake.

“Kuna jamaa alikuwa akidate nae, alimtumia meseji kumsifia jinsi walivyofanya ngono usiku uliopita. Unajua nilisikia maumivu ambayo sikuwahi kuyasikia,” alijibu Alex.

“Jamani poleeee...”
“Nashukuru! Ila ndiyo maisha! Kuumizwa ni kawaida, huwezi kuwa kwenye furaha kila siku na ndiyo maana uliponiambia kuhusu ishu yako, ilinigusa sana, imeniumiza mno na ndiyo maana nilihitaji namba ya jamaa ili nimtukane,” alisema, akaunganisha matukio.

Mpaka kufikia hapo tayari Shadya akahisi huyo alikuwa mwenzake, upande mmoja kumbe haikuwa hivyo, kama walivyokuwa wanaume wa vyuo vikuu, nae alitaka kupata alichokihitaji na kuondoka zake.
 
Sehemu ya 49.

Walikaa na kuzungumza mambo mengi, ilipofika jioni, wakaingia baharini kuogelea, walifurahia mno na walipomaliza, wakaondoka ufukweni hapo kurudi chuoni.

Wakawa pamoja kwa mawazo na kupeana ushauri wa mambo mengi kuhusu mapenzi. Kwa jinsi walivyokuwa karibu, Shadya akaanza kuhisi kwamba kwa mwanaume aliyekuwa akimtafuta katika maisha yake alikuwa huyo Alex kwani alikuwa na kila sifa.

Kwanza mpole, mcheshi, mkarimu na hata alipokuwa akiongea aliongea kwa huruma nzito kama padri aliyekuwa akihubiri kanisani.

Alihitaji kuiteka akili ya msichana huyo hivyo kwenye kila neno alilokuwa akilizungumza, kitu cha kwanza kabisa lilikuwa ni kuwaponda wanaume ambao hawakuwa waaminifu, kwake walionekana kama wavunja amani nchini Tanzania.
.
.

. “Hii ni mimba yako!” ilisikika sauti ya msichana mmoja kwenye simu.
“Yangu! Yangu kivipi yaani?” alisikika mwanaume naye akiuliza.

“Hivi unajifanya umesahau!”
“Ndiyo unikumbushe!”
“Siku ile nilikwambiaje?”
“Ndiyo nikumbushe! Siku gani?”
“Tulipofanya mapenzi!”

“Sikumbuki Angelina! Hebu nikumbushe!”
“Nilikwambia nipo kwenye siku zangu za hatari, ukatafute mpira, halafu ukaniambiaje?” aliuliza msichana huyo.
“Daah!”

“Alex! Yaani umenipa mimba halafu unataka kukataa kwamba hii si mimba yako! Nimesema sikubali!” alisikika msichana huyo.

“Hebu naomba tuonane kwanza!”
“Si unajifanya kukataa! Sasa subiri!”
“Rose! Usiwe mkali kwanza, hebu tuonane! Mimba ishu ndogo tu!” alisema Alex.

Alikuwa akizungumza kwa simu, alipigiwa na msichana Rose ambaye alikuwa mpenzi wake na kwenda pembeni kuongea naye huku akimwambia Shadya asubiri kidogo.

Alipomaliza kuongea, akamrudia msichana huyo na kumwambia alipigiwa simu na kuambiwa mama yake hakuwa na hali nzuri, hivyo alitakiwa kwenda kumuona.

Kwa kuwa Shadya alikuwa rafiki yake, akaomba kwenda naye lakini akakataa kwa kuleta visingizo vingi mpaka akakubalika na kwenda huko peke yake.

Njiani alikuwa na mawazo tele, alimfikiria huyo Rose.

Alikuwa msichana wake, aliyekuwa akimtumia kama chombo cha starehe, kila alipokuwa na hamu ya kufanya mapenzi, wanawake wote walipokuwa wakimzingua, msaada wake wa mwisho alikuwa huyo Rose.
 
Sehemu ya 50.

Alimtumia alivyotaka na siku ya mwisho kufanya naye mapenzi alimwambia kabisa kwamba alikuwa kwenye siku zake za hatari na hakuwa amechoma sindano za kuzuia mimba ila Alex akamshawishi na hatimaye kulala naye.

Akampa mimba na ndipo hapo alikuwa akipewa taarifa. Alitaka kuruka lakini mwisho akaamua kukubaliana naye hivyo kutaka kuonana.

Alichohitaji si kukubaliana na mimba hiyo ila alichohitaji hasa kilikuwa ni kumshawishi na hatimaye akubali kuitoa. Hakuwa tayari kuwa na mtoto, ni kweli alitembea na wanawake wengi lakini suala la kuwa na mtoto aliliweka kando kabisa.
Hakuchukua dakika nyingi akafika kwa Rose na kuanza kuzungumza naye.

Alimwambia vilevile kwamba alikuwa na mimba hivyo alihitaji kupata ushauri ni kitu gani walitakiwa kufanya.
“Inabidi itolewe!” alisema Alex, yaani aliongea simpo sana kama alikuwa akimsalimia mtu.

“Unasemaje?”
“Sasa Rose, wewe upo tayari kuitwa mama?” aliuliza.
“Hapana!”
“Sasa unadhani ni kitu gani tunatakiwa kufanya! Inabidi itolewe tu!” alisema Alex.

“Ila naogopa!”
“Kwani wewe ni wa kwanza mpenzi? Kuna wanawake zaidi ya milioni mia tano wametoa mimba, tena wengine mpaka tano, lakini ni wazima wa afya tele, tena baada ya kuolewa, wakaja kuzaa tena,” alisema alex.

Rose alibaki kimya akimsikiliza mwanaume huyo aliyekuwa na maneno mengi ya ushawishi. Aliongea sana na hatimaye wakakubaliana kwamba mimba ilitakiwa kutolewa.

“Ila mimi siwajui wanaotoa mimba!”
“Usijali! Nitawasiliana na madaktari ninaowafahamu!” alisema Alex, kichwani mwake kukaja madaktari kama watano hivi, wote hao aliwahi kuwatumia katika suala nyeti kama hilo, tena kwa mafanikio makubwa.
.
.
Tukutane Jumanne.
 
Sehemu ya 51.

Muda huo Alex alikuwa bize na Shadya, hakutaka kusikia la mwanamke mwingine. Kulikuwa na kitu alikihitaji na aliona kabisa mara baada ya kukipata, asingeendelea kuwa naye.

Alimjali msichana huyo, alimsikiliza na kumuheshimu, alimuonyesha mapenzi yote ambayo mwanamke alitakiwa kuonyeshwa, aliaminiwa kwa kuwa alionekana kama alikuwa mkweli kwa kile alichokuwa akikifanya kumbe haikuwa hivyo.

Japokuwa mara nyingi Shadya aliteswa na mawazo juu ya Gibson lakini baada ya wiki moja ya ukaribu na Alex akaanza kumsahau mwanaume huyo, taratibu akaanza kumtoka moyoni mwake.
Akawa na furaha tele, kwa jinsi Gibson alivyokuwa hakuamini kabisa kama kuna siku naye angeweza kubadilika.

Mpaka kipindi hicho Gibson hakutaka kumwambia jambo lolote lile kuhusu mapenzi, aliuandaa moyo wa msichana huyo, kwenye kitu ambacho hakutakiwa kumfanyia basi la kwanza lilikuwa ni kumtongoza.

Yaani alihitaji wajikute tu wakifanya mapenzi, alihitaji hilo kwa kuwa alikuwa na maana yake kubwa, yaani hata likitokea la kutokea, awe na la kujitetea, amuulize kwani nilishawahi kukwambia nakupenda?

Kila siku walikuwa pamoja, waliendelea na maisha yao. Moyo wake ulijeruhiwa kwa ajili ya mapenzi lakini badala ya kujiweka pembeni, avute pumzi lakini hakutaka kuelewa kabisa.

Lile jiji la Dar es Salaam ambalo alionywa sana ajitenge nalo kwani kulikuwa na wanaume waliokuwa na kila aina ya saundi ya kumtokea msichana, likamchukua, kila aliyekuja mbele yake alionekana kama ana mapenzi ya kweli kumbe haikuwa hivyo kabisa.

“Wewe ni mzuri sana,” alisema Alex, hayo yalikuwa maneno aliyoyarudia kila siku, na kila alipokuwa akiyatamka, Shadya aliachia tabasamu pana.

Hakuwahi kumwambia alikuwa akimpenda hata mara moja, yeye kazi yake ilikuwa ni kuusifia uzuri wake, macho yake, ngozi yake na mambo mengine mwilini mwake.
Ilipofika wiki ya pili baada ya kuonana na kuongea hapo ndipo mambo mengine yakaanza kuibuka.

Kila walipokuwa wakikaa darasani, Alex alitumia muda wake kupitisha mikono yake kwenye mapaja ya msichana huyo na kuanza kuyachezea.
 
Sehemu ya 52.

Kwa Shadya hapakuwa na tatizo lolote, angeweza vipi kumzuia mwanaume ambaye alimwambia alikuwa mzuri kama malaika? Hivyo akamwachia afanye lolote alitakalo.

“Unakwenda wapi huko?” aliuliza Shadya, mkono wa Alex ulianza mapajani, sasa ukawa unahama na kwenda juu.
“Subiri kwanza!” alisema Alex, Shadya akaangalia huku na kule darasani, hamukuwa na watu wengi, tena wale wachache kila mmoja alikuwa bize na mpenzi wake.

“Hebu panua miguu kidogo!” alisema Alex, cha kushangaza, Shadya akafanya hivyo.

Mkono ukaenda mpaka katikati ya mapaja na kutulia hapo kwa dakika kadhaa. Shadya alibaki akiugumia kwa raha ya kipekee, mkono ule uliweza kutalii vizuri maeneo hayo.

Zoezi hilo lilichukua kwa dakika tano nzima na baada ya hapo Alex akamwambia waende sehemu kupumzika, na kwa kuwa Shadya akawa hajiwezi, akakubaliana naye, wakaondoka na kwenda kuchukua chumba katika lodge moja iliyokuwa nje ya chuo hicho.

Hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Shadya kulala na Alex, walifanya ngono kuanzia majira ya saa kumi na moja mpaka saa tatu usiku, tena hawakuishia hapo, wakalala wote mpaka asubuhi.

Moyo wake ukafunguliwa kwa mwanaume huyo. Japokuwa Alex alikuwa na mademu wengi kutoka sehemu mbalimbali lakini aliweza kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha Shadya hagundui ilo.

Msichana huyo akamwamini Alex, yaani kwake hapakuwa na mwanaume mwaminifu kama huyo. Wakawa pamoja, Alex akatambulishwa kwa Rahim.
Ndugu yake huyo alimshangaa dada yake lakini akakubaliana naye kwa kuwa mambo ya mapenzi hakutakiwa kabisa kuyaingilia.

Moyo wa Shadya ukawa na furaha tele, hakukuwa na kitu kilichompa raha na furaha ya moyo kama kuwa na mwanaume huyo aliyejua kumuhendo mwanamke kama alivyokuwa akifanya.

“Nitataka niishi na wewe maisha yangu yote!” alisema Shadya huku akimwangalia Alex.
“Hakuna shida. Nakuahidi hakutokuwa na mwanamke mwingine zaidi yako!” alisema Alex.
 
Sehemu ya 53.

Mapenzi hayo yaliendelea mpaka mwaka wa kwanza chuo ulipokwisha na hivyo vyuo kufungwa. Shadya na Rahim wakarudi Ilala ambapo walikaa siku moja na iliyofuata kuondoka kuelekea Unguja.
Alipofika, bandarini kulikuwa na ndugu zao wachache na Ngwali ambao walikuja kuwapokea.

Shadya hakutegemea kumuona mwanaume huyo mahali hapo, alishtuka kwani alitoka kabisa moyoni mwake na hakumfikiria hata mara moja.
Wakapokelewa, wakasalimiana na kuondoka mahali hapo. Njiani, Ngwali alikuwa kimya, moyo wake ulikuwa na furaha kumuona mpenzi wake lakini kwa jinsi alivyokuwa, alihisi kabisa kulikuwa na tatizo.

Alitamani kuuliza lakini alishindwa. Moyo wake ulimuuma mno, alihisi mpenzi wake alibadilika na inawezekana kabisa alimpa mwanaume mwingine huko Dar alipokwenda.
“Ila niliongea naye na kuniambia hawezi!” alijisemea.

“Mh! Kama ni kweli, moyo wangu utaniuma sana,” aliendelea kujisemea.
Hawakuchukua muda mwingi wakafika nyumbani, wakateremka na kuingia ndani. Ngwali hakutaka kusubiri, moyo wake ulikuwa na shauku ya kutaka kujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, hivyo akatafuta nafasi ya kuwa na Shadya na kuanza kuzungumza naye.
“Mbona umebadilika hivyo?” aliuliza Ngwali.

“Nimekuwaje?”
“Umeonana na mimi ila huna furaha kabisa, yaani ni kama hukupenda kuniona, tatizo nini? Umempata mtu mwingine zaidi yangu?” aliuliza Ngwali, macho yake yalianza kuwa mekundu, yaani hakuwa na mwanamke aliyetegemea kulala naye zaidi ya huyo Shadya.

“Hapana! Nimechoka tu!”
“Ila unanipenda?”
“Ndiyo! Mbona leo unauliza mambo yanayonichanganya? Yaani hata kuuliza za masomo, imekuwaje huko, wewe unaulizia mapenzi tu, sijui unanipenda, sijui nimebadilika, hivi unajali kuhusu masomo yangu?’ aliuliza Shadya.
“Nisamehe mpenzi!”
“Unajali?”

“Ndiyo maana nimesema nisamehe!” alisema Ngwali, hapohapo Shadya akarudi ndani huku akijifanya kukasirika.
Hakumtaka tena Ngwali, mwanaume huyo hakuwa na kitu, alikuwa kapuku tu, mwalimu wa madrasa ambaye pesa zake alitegemea mpaka michango ya wanafunzi wa madrasa ama pale ambapo wangepata shughuli ya kichuo kwenda sehemu.
 
Sehemu ya 54.

Kila alipomwangalia hakuona kama kungekuwa na maisha naye hapo baadaye na ndiyo maana muda mwingi alitafuta nafasi ya kuachana naye.

Huyo Ngwali hakuwa mwanaume sahihi kwake, hakusoma, alikuwa ustaadhi tu, ila kila alipomfikiria Alex, moyo wake ulikuwa na shauku ya kutamani kuendelea kuishi naye maisha yake yote kwa kuwa tu walifanana.

“Hii mijanaume mingine...” alijisemea kwa hasira na kuelekea chumbani kwake.
Ngwali alibaki akiwa amesimama tu, moyo wake ulichoma kama pasi, hakuamini kilichokuwa kimetokea. Ni kweli Shadya alibadilika lakini yeye kama mpenzi wake alitakiwa kumuonyesha mapenzi na si kumuuliza maswali yaliyoonekana kumtia hofu nzito.

“Ila nilitaka kujua! Mungu wangu! Hivi huyu Shadya akiniacha nitampata nani mie? Ngoja nimuombe msamaha!” alijisemea.

Hilo ndilo alilolifanya siku hiyo, siku nzima alimwandikia meseji za kumuomba msamaha na kumwambia asingerudia tena kufanya ujinga wa namna hiyo.
Alituma meseji ndefu zaidi ya hamsini lakini hapakuwa na meseji yoyote ile iliyojibiwa. Hilo lilimuumiza, mapenzi yakaanza kuonekana kuwa machungu kwake.

Usiku wa siku hiyo akabaki akilia kitandani mwake, moyo wake ukatokea kulichukia Jiji la Dar es Salaam kuliko sehemu yoyote ile duniani kwa sababu iliyaiba mapenzi yake ndani ya moyo wa mpenzi wake.

Wakati akilia chumbani, moyo wake ukisononeka, upande wa pili Shadya alikuwa akiwasiliana na Alex kwenye simu, mapenzi yalimteka na hakufikiria kitu chochote kile zaidi ya kuwa na mwanaume huyo maisha yake yote.

Siku ziliendelea kukatika, Ngwali alitamani sana kuonana na Shadya lakini hakuweza kuonana naye tena kwani simu hazikupokelewa wala meseji kujibiwa mpaka kipindi cha likizo kilipokwisha na kurudi chuoni huku akiwa amefaulu masomo yote vizuri.

“Nilikukumbuka sana,” alisema Alex huku akimwangalia Shadya.
“Nilikukumbuka pia! Leo nataka nije kulala kwako!” alisema msichana huyo.
“Haina shida. Karibu!” alisema.
***
 
Sehemu ya 55.

“Nisikiliza Bhoke,” alisema mwanaume mmoja, alikuwa daktari, alivalia koti kubwa jeupe huku uso wake ukiwa na miwani ya macho.
“Moyo wangu unaniuma!”

“Kuathirika si mwisho wa matatizo, wengi wameathirika na bado maisha yanaendelea. Kuna dawa zitakazokufanya kuishi kwa kipindi kirefu,” alisema daktari huku akimwangalia msichana aliyekuwa akiongea naye.

Kwa jina aliitwa Bhoke Ahmed, alikuwa miongoni mwa wanawake warembo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kila alipokuwa akipita wanaume walimwangalia kwa macho ya matamanio, walimpenda kwa kuwa alikuwa na sura nzuri na walimtamani kwa kuwa alikuwa na wowowo kubwa.

Alifanya mapenzi na wanaume wengi chuoni hapo, hakuamini kutumia mpira, siku zote aliwaambia wanaume kwamba utamu wa pipi ni kuila bila ganda hivyo kufanya nao kwa kuamini angekuwa salama.

Baada ya kuhisi kama alikuwa na tatizo ndipo akaenda kupima na kugundulika alikuwa na virusi vya ugonjwa wa UKIMWI.

Hilo lilimuumiza mno, hakujua ni mwanaume gani ambaye alimwambukiza kwani alifanya na wengi, idadi yake ilikuwa kubwa kupita kawaida. Wanaume wote aliofanya nao mapenzi tangu aingie hapo chuoni wakaanza kujirundika kichwani mwake, walikuwa kama ishirini na mbili, na hakukumbuka hasa ni yupi alikuwa na tatizo hilo.

“Kenny, Maliki, John, Godwin, Alex, Jafari, Omar na wengine wengi,” alijisemea.

Hakuwa na nguvu za kubadilisha ukweli, alikubaliana na vipimo hivyo kwamba aliathirika na muda huo ulikuwa ni wa kutumia vidonge vya ARV kwa ajili ya kuongeza maisha yake na kuonekana kuwa na afya tele.

Hakutaka hilo lijulikane na mtu yeyote, aliwafikiria watu aliotembea nao, marafiki zake na hata maadui, kulikuwa na watu wengi ambao wangefurahia yeye kupata virusi hivyo na wachache mno wangehuzunishwa na hicho.

“Kuathirika kwangu kutakuwa siri yangu milele,” alijisemea wakati akiondoka ndani ya hospitali aliyokwenda kupima.
.
.

JE NINI KITAENDELEA?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom