gemplatnumz
Senior Member
- Jan 24, 2017
- 133
- 371
- Thread starter
- #61
Nishushe dude like nione wangapi mmeipendaaaaaaaa
Weka Basi mkal, ukitak kujua wanaofuatilia Mbona ni rahisi tuNishushe dude like nione wangapi mmeipendaaaaaaaa
😂😂😂😂😂😂😂😂 alaf kweli eeWeka Basi mkal, ukitak kujua wanaofuatilia Mbona ni rahisi tu
Wengn wanasoma kimya kimya na kusepa zao
Sent using Jamii Forums mobile app
alaf kweli ee
It's like sio akili yake.Safi sana...
Ila jamaa ameniudhi, yani anaingia na bangi badala ya kuichoma analala tena...
Cc: mahondaw
Mie ndio nimejiunga na kibando cha mia 5 hapa nifaidi uhondo. Kumbe nimetoka kapa.Kesho naimalizia yote
Mie ndio nimejiunga na kibando cha mia 5 hapa nifaidi uhondo. Kumbe nimetoka kapa.
Haya usiku mwema bhana
Kabisa mie mwenyewe nilishawahi kuisoma siku nyingi sana ila cha ajabu humu inaonekana mpyaHii hadithi ilikua inatoka kwenye gazeti la ijumaa au kiu sikumbuki vizuri...
Ila ipo mtandaoni tangu 2012 ikiwa inapatikana kwenye website ya gazeti husika.
Leo imeletwa humu mwandishi kabadilika na watu wote wanaonesha hawaijui.
Jamaa umefanya plagiarism.
Kama vile itaishia kwa wachungaji na walokole!?SIMULIZI: THE HOUSE OF DEVIL
(Nyumba ya
kishetani)
Sehemu ya 01
MWANDISHI: METECK DERTHOD
MSIMULIAJI: HUMULI SAMAKI
TYPE: TRUE STORY (Simulizi ya kweli)
UTANGULIZI:
Kama kuna watu hawayajui haya
nitakayoyaongea basi nawataka kuanzia sasa
wajue kwamba, hapa Dar kuna mambo makubwa
sana ambayo ukisimuliwa unaweza kusema si ya
kweli, lakini wale wanaoyapata hayo mambo
wanajua na wewe usiombe yakukute hata siku
moja," ndivyo alivyoanza kusimulia Bw. Humuli
Samaki (43), mkazi wa Buguruni (kwa sasa)
ambaye alipata mkasa mzito akidai alipanga
nyumba moja na majini Magomeni, Dar es
Salaam.
SASA ENDELEA MWENYEWE
"Si zamani sana mkasa huu uliponitokea, ilikuwa
mwaka 2009 tu, kwa hiyo naweza kusema ni
juzijuzi tu. Kwa sasa naishi hapa Buguruni, baada
ya kuhama kutoka Magomeni ambako nilipata
mkasa mzito na wa kuogopesha. Nilipanga
nyumba moja na majini."
Mwaka huo (2009), awali nilikuwa nikiishi
Mwanyamala Mwinjuma, jirani kabisa na Makao
Makuu ya Bendi ya TOT, hata Kapteni John
Komba nilizoeana naye kwa kuonanaonana naye
pale CCM-Mwinjuma, ingawa jina langu najua
hakuwa akilifahamu.
Ile nyumba niliyokuwa nikiishi pale
Mwananyamala iliingia kwenye mgogoro wa
kifamilia na kufikishana mahakamani kwa ajili ya
kugawana mirathi. Hukumu ilipotoka ikaamriwa
iuzwe kisha ndugu wagawane fedha.
Kwa maana hiyo, mimi na wapangaji wenzangu
watano, tulipewa notisi ya kuhama baada ya
mteja kupatikana. Huyu mteja anaitwa Masawe
anafanya kazi Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) lakini sijui ofisi za wapi.
Ilibidi mimi niangalie mwelekeo mwingine,
niliamua nibadili upepo, nikaishi Magomeni. Kwa
wakati huo nilikuwa sina familia. Sina mke wala
mtoto hata wa kusingiziwa, kwa hiyo nilikuwa
naishi peke yangu. Ni mwaka jana ndiyo nimeoa
mke wangu huyu, anaitwa Hadija Mashada.
Rafiki yangu mmoja anayeitwa Mohamed Kombe
alinipa namba ya dalali kwani yeye anaishi
Magomeni hata sasa. Nilimpigia simu dalali wake,
anayeitwa Yusuf Mwamba, akaniita Magomeni
pale kwenye nyumba wanayosema aliwahi kuishi
Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Nilikwenda mpaka pale, nilimkuta amesimama nje
ya nyumba hiyo, tukasalimiana, akaniuliza nataka
nyumba yenye sifa gani, nikamweleza.
Niliwajibu mimi mwenyewe sijui, lakini sikumaindi
sana. Akaja mama mmoja aliyesema anaishi
nyumba ya pili, akasalimia na kuniuliza maswali.
"Hamjambo wanangu?"
Tuliitikia wote, akauliza nani anahamia pale kati
ya sisi wote, tulikuwa watano mbali na dereva.
"Ni mimi."
"Ooo, mzima baba?"
"Mimi mzima mama."
"Unaitwa nani?"
"Humuli Samaki."
"Unahamia peke yako au uko na mke na watoto?"
"Peke yangu mama."
"Humuli Samaki ni mwenyeji wa wapi?"
"Usukumani."
"Haya, naamini uliaga wakati unaondoka
nyumbani."
"Hilo lilikuwa la kwanza mama."
"Haya, kila la kheri."
Tuliendelea na kazi ya kuingiza vyombo ndani
hadi tukamaliza. Wale wenye gari wakaondoka,
nikabaki mimi peke yangu.
Nilijiwekea malengo kwamba, nihakikishe naweka
sawa kila kitu ili kesho yake nisiwe na kazi hiyo
zaidi ya kwenda kazini. Niliifanya kazi kwa muda
wa saa tatu, mpaka kwenye saa saba na nusu
usiku nikamaliza.
Nilibadili nguo, nikavaa taulo na kwenda kuoga.
Nilikuta bafu limetoka kutumika kama dakika
kumi nyuma, sikushangaa kwani si kuna
wapangaji wengine ambao tulitakuwa tunatumia
bafu moja.
Usiku kabla ya kuzima taa, nilizima taa,
nikapanda kitandani. Kabla sijapata usingizi,
niliwasikia wenzangu wakicheka sana na kuongea
huku wameweka muziki. Lakini ule muziki
haukuwa wa kiarabu, kizungu wala kiswahili.
Hata maongezo yao, mimi nilisikia sauti tu lakini
kusema walikuwa wanatumia lugha gani si rahisi.
Kuna wakati kama walikuwa wakiongea kihindi,
pia niliwasikia kama wanaongea kiarabu, nikajua
ni watu wa namna hiyo.
Lakini sikulala mpaka nikampigia simu dalali
kumuuliza kama wale wapangaji wenzangu ni
weupe au waswahili kama mimi, akasema hata
yeye hajui kwani hakuwahi kuwaona hata siku
moja..
.! ITAENDELEA
Hatalikaa mkao wa kuenjoy balaa like kwa sana
True story ndo haihitaji likes!!??unataka LIKE wakati hadithi yenyewe umesema ni TRUE STORY!
maliza kwanza
= Hatari
Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
Ujuaji umekuzidi, kama ushaisoma tulia. Watu wengine....Nakumbuka hii story nilisoma mwishoni huyo dalali kumbe ndio anamfanyia michezo yote ila jina la YESU likatenda
Malizia hapo watu wengine wakufanye nini?