Simulizi: Nilipanga nyumba moja na majini

Simulizi: Nilipanga nyumba moja na majini

SIMULIZI: THE HOUSE OF THE DEVIL (Nyumba
ya kishetani)
MSIMULIAJI: HUMULI SAMAKI
MWANDISHI: METECK DERTHOD
Sehemu ya 05
Endelea...!
"Humu ndani kuna mtu anaingia kufanya mambo
yake, lini mimi nimekula chipsi na kuku humu
ndani?" nilijiuliza, nikasikia kicheko kutoka kwa
wenzangu.
"Haa! Haaa! Ha! Haaaah."
Niliinua macho kuangalia juu kwenye silingbodi'
kama vile niliyekuwa nimeona kitu, akili yangu
ikawaza kitu cha dakika chache nyuma, nacho ni
hiki:
"Humuli."
"Naam."
"Ni kweli yule binti humjui?"
"Simjui mama."
"Kuna mawili hapo, humjui au humkumbuki."
"Vyote mama, simkumbuki na pia simjui."
"Lakini wewe si alikutaja kwa jina?"
"Mwenyewe nilishangaa sana."
"Basi Humuli nimeshaelewa, kwaheri, nimeelawa
ni kwa nini nimeugua kichwa na yule ni nani, pole
sana wewe kijana."
Je, ni kwanini Humuli aliyarejea mazungumzo
yake na yule mwanamke aliyeumwa kichwa
ghafla? Nilianza kuamini kwamba, kuna uhusiano
mkubwa kati ya yule msichana na wale
wapangaji wa pale ndani nilipo, inawezekana
alinijua jina kwa sababu naishi nao na wana
uwezo wa kujua jina la mtu kulingana na
mazingira yao.
Pia niliwaza kwamba, kuna uwezekano mkubwa
yule msichana alitokea baada ya maono yao
kuniona mimi na yule mama wa jirani tukitaka
kuwazungumzia wao kama wapangaji wenye
maajabu hivyo hawakupenda iwe hivyo ndiyo
maana msichana akaibuka na kusababisha
mvurugano.
"Itakuwa kweli, ndiyo maana yule mama naye
alisema ameshajua ni kwa nini aliugua kichwa
ghafla, alijua yule msichana ni nani na kwa nini
yeye kasikia maumivu ya ghafla vile."
"Lakini pia kuna wale wauza chipsi, nao
niliwakumbuka hasa yule mmoja aliyesema yule
msichana wanamjua, anaishi mtaani, lakini
hawajawahi kubaini anaishi nyumba gani na kwa
mzee nani wala anajishughulisha na nini," hayo
yote niliyawaza mimi.
Nilisimama, nikachukua sabuni ya kuogea
ambayo haijafunguliwa, nikaipiga chini kwenye
kapeti kwa hasira huku nikisonya, nikasema kwa
sauti ya chini:
"Humu ndani naishi na majini."
Kule chumbani nikasikia wakicheka.
"Si unaona, nimes mimi, lazima naishi nao
humu ndani, da! Najuta sana," nilisema. Kicheko
kikasikika tena, safari hii kilikuwa cha juu zaidi
kuliko kile cha awali.
Moyo ulijaa mawazo, akili ilihisi uchungu wa
maisha, niliwaza fedha nilizozilipa kwa ajili ya
kupanga mle ndani, nikamkumbuka dalili,
niligundua alichofanya ni kunitapeli na hakuna
lingine wala hakuwa msaada kwangu.
"Mimi ni mwanaume, kama niliweza kupata fedha
za kupanga hapa, sishindwi kupata nyingine za
kupanga sehemu nyingine tena mbali na hapa,"
nilisema kwa moyoni.
***
Usiku nikiwa nimelala, nilichelewa sana kupata
usingizi, ghafla nikaona taswira za watu ukutani,
wawili tena wakiwa wamesimama, ni mwanamke
na mwanaume. Niliogopa sana, nikainua kichwa
polepole kuwaangalia kwa umakini, japo kulikuwa
na giza, lakini niliweza kuona vizuri lakini si kwa
uwazi mkubwa kama ambavyo taa ingekuwa
inawaka.
Ni kweli walikuwa watu wawili kama nilivyoona,
tena weupe nikimaanisha si watu weusi.
Walikuwa wakionesha vitendo vya kucheka huku
wakijinyonganyonga.
Kuna wakati walitembea mpaka jirani na kitanda
changu kisha wakageuza na kurudi pale ukutani.
Nilipeleka mkono hadi kwenye swichi ya kitanda
(bed switch), nikawasha, cha ajabu sikumwona
mtu wala dalili pale ukutani.
Niliamka nikiwa nahema kwa kasi mpaka
nikajishika kifuani, nikafungua mlango na kutoka
nje ili nijifanye nakwenda chooni lengo langu
lilikuwa kupata picha kwa wenzangu kukoje
maana niliwashuku wao na wale walioonekana
chumbani kwangu.
Kwa wenzangu niliwasikia wakikoroma kwa
zamu. Nikajiuliza ina maana si wao waliokuja
chumbani kwangu? Niliona ni utani wa hali ya
juu.
Niliamua kurudi chumbani na kukatisha safari ya
kwenda chooni, nikafunga mlango wangu kwa
funguo na kupanda kitandani, nilizima taa ili
nione kama yale mauzauza yatatokea tena.
Ukimya ulitawala kwa muda bila kujitokeza
chochote, nikaanza kupitiwa na usingizi kwa
kusinziasinzia, ghafla ukutani nikawaona tena
wale watu wawili.
Safari hii walikuja hadi kitandani, wakakaa,
wakasimama, wakaenda kwenye kabati,
wakafungua, wakatoa mashuka na kujifunika,
wakayarudisha, wakaenda nyuma ya mlango,
wakatungua mashati yangu mawili, wakagawana
na kuyavaa kisha wakayavua, mmoja mwanaume
akaenda sehemu yenye redio, akapeleka mkono,
nikajua anataka kuiwasha, lakini hakufanya hivyo.
Nilichoamua kukifanya akilini ni kuwasha taa kwa
ghafla na kuwavamia na nilipanga kumvamia
mwanamke nikiamini ndiye aliyekuja kule kwenye
chipsi. Polepole nilipeleka mkono hadi kwenye
swichi, nikawasha taa kwa ghafla huku macho
yangu yakiwa kwao, lakini sikumwona hata
mmoja! Kwangu haikuwa mapambano bali
nilichukulia kama changamoto za maisha.
Asubuhi, niliamka nikiwa nimechoka sana, lakini
kabla sijatoka kitandani nilisikia nje ya mlango
kukiwa na hali ya watu kutembeatembea tena
kwa kasi, niliinua shingo ili nione kama nitasikia
zaidi, lakini kukawa kimya.
Niliamka, nikatoka, nilikwenda sebuleni kwanza
kuangalia kama kuko salama.
Nilishangaa kukuta mezani kuna mfuko wa rambo
uliojaa chipsi kuku kama nilivyonunua mimi, lakini
zangu nilikula, sasa zile sikujua zilitoka wapi.
Niliubeba ule mfuko nikatoka nao, nilifungua
mlango mkubwa wa nje nikautupia pembeni
kidogo, niliporudi, nikaenda chooni, mlango
ulikuwa umefungwa kwa ndani kwani hata
niliposhika kitasa na kukivuta kilikuwa kigumu.
Hii iliashiria kwamba kuna mtu, kwa hiyo moyoni
nilisema nisimame palepale nje ya mlango hadi
atoke. Nilisimama eneo ambalo akitoka tu, uso
kwa uso na mimi.
"Tuone leo, wao si wajanja, leo nimemnasa
mmoja wao," nilisema moyoni. Dalili zote
zilionesha kwamba mle chooni mlikuwa na mtu
kwani niliweza kusikia hata kuhema kwake, mara
mlio wa maji, mara alikohoa, tena kwenye
kukohoa nikabaini mtu mwenyewe alikuwa ni
mwanamke ndiye aliyekuwa mle.
"We kohoa mpaka utapike, lakini mimi nipo hapa
mpaka utoke," nilisema moyoni. Nilikaa sana,
ikafika mahali nikachoka, lakini moyoni nikasema
siondoki hata iweje, lakini nilishtuka kitu,
niligundua muda mrefu sijazisikia zile dalili kama
maji au kuhema, nikafunguka akili. "Mh! Siyo
kwamba ametoka?"
Ile namalizia kusema ametoka?' nikasikia kicheko
kutoka kwenye chumba chao. Vicheko vikubwa
sana cha kike na kiume.
Nilirudi chumbani mwili ukinisisimka, hapo ndipo
niliamini mia kwa mia kwamba, nilikuwa nadili na
watu wasiokuwa wa kawaida.
Niliingia chumbani, nikampigia simu dalali.
"Haloo," niliita.
"Haloo. Halooo," nilirudia lakini sikupokelewa.
Nikiwa nimeachana na simu, mara iliita yenyewe,
alikuwa ni dalali nikapokea.
"Haloo," niliita.
"Haloo," niliitikiwa lakini sauti haikuwa ya dalali.
"Mzima bwana?" nilisalimia.
"Tuone leo, wao si wajanja, leo nimemnasa
mmoja wao."
Ha! Nilishtuka sana, nilisikia sauti yangu
mwenyewe ikisema hivyo. Ikaendelea.
"We kohoa mpaka utapike, lakini mimi nipo hapa
mpaka utoke."
Nilikata simu, nilikuwa nahema sana, mapigo ya
moyo yalikuwa yakienda kwa kasi ya ajabu huku
nikishindwa kuona sawasawa.
"Hii ni hatari sasa," nilisema.
ITAENDELEA..!
: THE HOUSE OF THE DEVIL (Nyumba
ya kishetani)

MSIMULIAJI: HUMULI SAMAKI

MWANDISHI: METECK DERTHOD

Sehemu ya 07

Endelea...

Hakunijibu, alianza kwa kutumbukiza mkono
kwenye mfuko usiokuwa na kitu, akahamia wa
nyuma ambao una waleti, akapeleka wa kulia
kwangu ambao ndiyo wenye bangi, aliposhika,
akakunja sura, alipotoa akashtuka sana na
kusema:

"Haa! Hii bangi siyo?"

Sikumjibu kwani niliamini ameshaijua, wenzake
waliokuwa kaunta wakaacha mambo yao na
kunigeukia mimi, nao wakashangaa sana. Mmoja
alikuwa amekaa juu ya stuli, akashuka huku
akiniangalia kwa kunikazia macho.

"Unakuja kituo cha polisi na bangi, wewe
unatutafuta nini sisi?" aliuliza yule aliyeshuka
kwenye stuli.
Niliambiwa nafunguliwa kesi ya pili, ya kwanza
kupigana na kujeruhi ya pili kukutwa na bangi!
Nilijitetea nikisema bangi ile si kwa ajili ya
kuvuta bali nilikuwa nina shida nayo.

''Wewe usitufanye sisi watoto wadogo, tunawajua
ninyi raia," alisema yule afande aliyenisachi.
Lakini afande mmoja wa kike ambaye muda wote
alikuwa akiangalia tu, akawaambia
wenzake:

"Lakini huyu kaka mbona hafanani na kuvuta
bangi, muulizeni ana shida nayo gani?"

Wale wenzake wakanigeukia na kuniuliza:

"Haya, wewe mwananchi, raia kabisa, unaweza
kuwa na shida gani na bangi mbali na kuvuta?"

Niliwasimulia kila kitu, tena nilifika mahali
nikawaambia kama kuna asiyeamini, tuongozane
hadi nyumbani, Magomeni akaone maajabu
ambayo hayahitaji kuelekezwa sana ili kuamini
kama yapo au la!

Palipita ukimya wa sekunde kadhaa, mmoja wao
akaniuliza:

"Kama ni kweli au tufanye ni kweli, ni kwa nini
umemuumiza huyu?"

Nilisema kilichotokea, yule chinga niliyemsaidia
naye akanitetea kwa kusema hivyohivyo, lakini
afande mmoja akasema nilijichukulia sheria
mkononi ambapo ni kosa kisheria.
Niliomba sana wanisamehe kwa yote, nikasingizia
kwamba ni kwa sababu kichwa changu hakipo
sawa kwa kuishi nyumba moja na majini.
Namshukuru mmoja wao aliniambia niondoke
lakini nihakikishe situmii bangi katika kujitibu
kwani serikali haiamini kama bangi ni dawa.
Nilipotoka, nilikwenda kununua nyingine, lakini
akili iliingia hisia kwamba, huenda yule dada wa
ajabu mle ndani ndiye anayecheza michezo ili
kunikwamisha kwenda na bangi ndani ya
nyumba, nikasema moyoni ngoja ninunue hii
nione kitakachotokea, nikanunua tena misokoto
miwili.
Nilitembea kuelekea kituo cha daladala. Njiani
nilimpigia simu yule mfanyakazi mwenzangu
aliyenijulisha kuhusu dawa ya kutibu nyumba
yenye majini, nikamwambia sitaweza kurudi
kwani nilipata wakati mgumu kidogo njiani.
Alinielewa, akaniuliza kama nimepata, nikamjibu
kila kitu kimekwenda sawa, lakini sikumwambia
kuhusu timbwili lililojitokeza.
Nilipanda daladala nikashuka Magomeni, niliingia
ATM kutoa fedha kidogo, kisha nikatoka. Wakati
natafuta mwelekeo wa kwenda nyumbani,
nilimkumbuka dalali, nikampigia simu.

"Halo."

"Halo habari za kazi bwana?"

"Nzuri, pole na kazi na wewe mwenzangu?"

"Nimepoa. Bwana vipi kuhusu nyumba?"
nilimuuliza.

"Nyumba imefanyaje?"

"Si nilikusimulia matatizo yake, umesahau?"

"Kwani ulisema matatizo yake yakoje vile?"

Nilimwelezea kwa kirefu, nikafika mahali
nikamwambia hadi nilivyompigia simu halafu
ikapokelewa na sauti ya ajabuajabu, alicheka
sana.

"Wewe bwana acha kunichekesha.

"Kwa nini unasema hivyo?"

"Yaani simu yangu mimi halafu apokee mtu
mwenye sauti ya ajabuajabu, kwa nini sasa?"

"Mimi pia sijui."

"We ulikosea namba."

"Labda bwana mi siwezi kukazania sana,"
nilimjibu kwa kinyongo kwani namba yake
niliisevu na ninapompigia huwa nasachi jina tu,
sasa nilikosea kivipi?

"Enhe, unasemaje bwana?" aliniuliza.

"Nimeshakwambia bwana."

"Kwa hiyo unashauri nini?"

"Nataka pesa zangu nikapange kwingine."

"Da! Hilo halitawezekana kirahisi bwana, maana
mpaka nimpate mpangaji mwingine atoe fedha
ndipo nikulipe wewe na mpangaji atakayekuwa
tayari kutoa fedha lazima akute nyumba tupu,

sasa wewe utalikubali hilo?"

"Naweza kulikubali, ila tuandikishiane."

"Kwamba?"

"Kwamba unajikomiti nikiondoka, akiingia
mpangaji mwingine tu unanilipa pesa zangu."

"Ngoja nitakupigia," alisema dalali na kukata
simu.
Nilipokuwa nakaribia nyumbani, nikakutana na
yule msukuma mkokoteni wa maji.

"Kaka za kazi?"

"Nzuri, vipi wewe?"

"Niko sawa, ndiyo unarudi?"

"Ndiyo."

"Najua jamaa hawajarudi, nitakuja muda uleule
tuliopanga."

"Sawa, karibu sana."

"Asante sana."

Niliingiza funguo ili kufungua mlango, lakini
nikagundua kwa ndani kulikuwa na funguo
nyingine maana nilichungulia.
Nilipousukuma, ulifunguka. Hii ina maana wale
watu wa ajabu walikuwa wamesharudi, wako
ndani. Niliingia ndani, nikafungua mlango wa
sebuleni, nikaingia humo.
Nilifikia kwenye kochi kubwa, nikajilaza.
Sikuangalia kama kweli wenzangu walikuwa
wamesharudi, ila nilisikia sauti ya muziki wa
redio, nikajua wapo.
Mara nikasikia mlango wao mmoja ukifunguliwa,
nikasikia mtu akitoka. Kwa mara ya kwanza
nilisikia akisema:

"Kama utamkamata anavuta bangi apelekwe
polisi, ndiyo dawa yao watu wa aina hii."
Nilishtuka, nikakaa. Nikawaza kama ninachosikia
ni cha kweli au?

Huyo aliyekuwa akisema hayo ni mwanamke na
ilionekana alitoka kuelekea uani. Nikatoka ghafla,
nikaona kisigino cha mguu mmoja kikimalizia
kuingia chooni.
Nilirudi chumbani huku najiuliza kama hawa watu
walisema vile kwa sababu wamejua mimi
nimenunua bangi au? Na ni kwa nini wazungumze
Kiswahili kwa mara ya kwanza siku hiyo?
Baada ya dakika mbili, nilimsikia akirejea
chumbani kwake huku akisema:

"Mimi mtu anayevuta bangi siku yoyote na
mahali popote pale, nikimwona nampeleka polisi
ajue mimi ni nani. Haiwezekani watu wawe
wanavuta bangi hovyo tu.
Moyoni nikasema hata iweje, hii bangi leo lazima
niichome humu ndani. Mkienda polisi msipoenda
mtajua wenyewe.

"Mimi siwezi kuishi katika mazingira magumu
namna hii wakati pesa ni yangu. Kwa nini
ustaarabu usiwepo?" nilisema moyoni nikipeleka
mkono mfukoni ili kutoa ile bangi niliyonunua
mara ya pili.

Niliipata, nikaitoa. Niliiweka kwenye meza kisha
nikaendelea kulala nikiusaka usingizi kwa nguvu
zangu zote maana nilijisikia kuchoka sana. Hapo
nilikuwa sijaenda chumbani kwangu.
Sikumbuki ni muda gani nilipitiwa na usingizi, ila
nakumbuka wakati nalala ilikuwa saa kumi na
moja. Nilipokuja kushtuka
ilikuwa saa kumi na mbili na nusu. Ina maana
nililala kwa saa moja na nusu.
Jicho langu moja kwa moja lilitua kwenye bangi
pale mezani, sikuiona.
ITAENDELEA...!
Hapo Kuna kaujinga flan....bangi ushaingia nayo ndan, unasubir nn kuiwasha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom