Simulizi: Nilipanga nyumba moja na majini

Simulizi: Nilipanga nyumba moja na majini

Mwisho was simulizi ni kuisha njiani


Bado Naendelea Kujifunza
 
dah, ningepata pdf version ya izi riwaya ingekua poa sana
 
SIMULIZI: THE HOUSE OF THE DEVIL (Nyumba
ya kishetani)

MSIMULIAJI: HUMULI SAMAKI

MWANDISHI: METECK DERTHOD

Sehemu ya 06

Endelea...

"We kohoa mpaka utapike, lakini mimi nipo hapa
mpaka utoke."
Nilikata simu, nilikuwa nahema sana, mapigo ya
moyo yalikuwa yakienda kwa kasi ya ajabu huku
nikishindwa kuona sawasawa.
"Hii ni hatari sasa," nilisema.
Usiku wa siku hiyo sikulala kusema kweli kwani
kila nilipofikiria maisha yale sikuona sababu ya
kuendelea kuishi pale. Moyoni nilisema kwamba,
ni afadhali ningeishi na watu ambao ni
majambazi kuliko hawa, nafuu ningepanga
nyumba moja na makahaba kuliko kupanga
nyumba moja na majini.
Nilichoamua, asubuhi nikifika kibaruani tu niombe
ruksa kisha nianze kumsaka yule dalali na pia
nitafute dalali mwingine ambaye atanitafutia
vyumba kwingine na si maeneo yale tena kwani
niliyaona yana nuksi.
Asubuhi kulikucha salama kabisa, tena usiku wa
siku hiyo sikuona mauzauza wala dalili zake.
Nilikwenda kuoga bila kukagua mazingira, moyoni
nilisema liwalo na liwe kwa maana kwamba,
wawepo wasiwepo sawa tu.
Bafuni niligundua wameshaoga kwani kulikuwa
na majimaji ya muda mfupi uliopita. Nilipomaliza
kuoga, nilijiandaa na kutoka. Nje nilikutana na
mtu ana mkokoteni, akanisalimia.
"Za asubuhi bwana mkubwa?"
"Salama, karibu sana."
"Asante, kuna watu fulani wanaishi humu nina
shida nao."
Aliposema hivyo nilishtuka sana, niliamini yeye ni
mmoja wa wale ila amejigeuza kwa kujifanya ana
shughuli za mkokoteni.
"Unawajua kwa sura?" nilimuuliza huku nikiwa na
wasiwasi maana alinikazia macho.
"Siwajui."
"Sasa una shida nao kivipi watu usiowajua kwa
sura?"
Ni kwamba, kuna binti mmoja huwa wanamtuma
niwaletee maji, nikifika hapa huyo binti anabeba
madumu kupeleka ndani, sasa jana nilikutana na
huyo binti nikamuuliza kuhusu malipo yangu ya
mwezi sasa, akasema nije nifuatilie mwenyewe."
Nilishangaa sana kusikia hivyo. Nijuavyo mimi
mle ndani mna watu wawili, mwanamke na
mwanaume, sasa kama kuna binti hilo lilikuwa
jipya kwangu, labda lakini.
"Huyo binti naye anaishi humu au?" nilimuuliza.
"Sidhani, inaonekana kama huwa wanamtuma
tu."
"Kwa nini huamini kama anaishi humuhumu
ndani? Hafanani na wao wenyewe?" hili swali
niliuliza likiwa na mtego mkubwa sana, nilitaka
nijue uhalisia wake.
"Siwezi kusema hafanani wakati wao siwajui kwa
sura."
Hapo ndipo nilipopataka, nilidhani atasema
hafanani nao, ningejua ni walewale.
"Oke, nadhani wameondoka kwenda kazini."
"Ah! Sasa mimi fedha zangu nitazipataje jamani?"
"Subiri wakirudi jioni."
"Wewe utakuwepo?"
Nililishangaa swali hilo, hakuwa akinidai mimi
lakini anataka niwepo?
"Unataka niwepo?"
"Ee."
"Kwa nini?"
"Naamini utanisaidia kuzipata fedha zangu."
"Uliwahi kuja wakagoma kukupa?"
"Siyo hivyo, ila kila nikija, nikigonga mlango huwa
hawafungui."
"Basi nitakuwepo."
"Asante kaka. Nije saa ngapi?"
"Saa moja nitakuwa nimerudi."
Aligeuza mkokoteni na kuondoka zake huku
akisema:
"Muda huo nitakuwa nimefika kaka."
Niliondoka kwenda kazini kuomba ruksa. Lakini
wakati naondoka, mfanyakazi mwenzangu mmoja
aliniuliza nakwenda wapi, nikaamua kumsimulia
kwa ufupi kisa changu.
"Kha! Sasa hapo tatizo liko wapi, mbona dawa
ipo rahisi sana."
"Rahisi! Ni ipi hiyo?"
"Sikia, twende pembeni nikakusimulie," aliniambia
yule mfanyakazi mwenzangu huku akiangalia
kulia na kushoto kama mabosi watatokea.
Tulikwenda kusimama pembeni, akaanza
kuniambia:
"Sikiliza, kama unaishi nyumba ya namna hiyo,
unachotakiwa kufanya, kila siku asubuhi na jioni
au usiku unapuliza bangi ndani ya nyumba, kama
ni majini, mapepo sijui nini, utaona mambo poa
kabisa."
Sikuamini maneno hayo, nikamuuliza mara
mbilimbili kama ni kweli.
"Khaa! Nina mjomba'ngu aliwahi kuishi kwenye
nyumba ya hivyo, akaenda sehemu akaelekezwa
dawa ni hiyo, akaitumia, mpaka sasa anaishi kwa
raha hakuna cha majini wala mapepo," alisema.
Nilimsikiliza nikianza kuamini kwa mbali, lakini
nilifika mahali nikamuuliza hiyo bangi mimi
nitavuta au nitaiwasha ili itoe moshi yenyewe?
"Ukishaiwasha, utaiweka mezani au popote ndani
kwako, lakini angalia isizimike ili moshi wake
usambae chumba kizima au sebule nzima."
"Hilo linawezekana," nilimwambia nikimtumbulia
macho.
Kwa sababu nilikuwa nimeshaaga, ilibidi niondoke
tu na kurudi baadaye. Nilikwenda mtaani,
nilitafuta bangi nikapata maeneo ya Kariakoo,
nikaitia mfukoni.
Nilizurura sana siku hiyo, saa tisa kamili nilikuwa
njiani narudi kazini. Nilipiga hesabu za kufika
kazini na kuondoka, maana muda wa kazi ni saa
tisa na nusu.
Wakati napita pale Kituo cha Polisi Msimbazi,
fujo zikazuka, kuna machinga wawili walikuwa
wanapigana kwa sababu ya kugombea sehemu
ya kufanyia biashara, katika ugomvi huo mimi
nilibaini mmoja wao ndiyo mwenye kosa.
Nikampa laivu kuwa yeye ndiye mwenye tatizo,
alikuja juu, akachukua boksi lenye viatu na
kunirushia, likanipata kwenye bega la kulia,
sikukubali, nikaokota jiwe na kumrushia,
likampata mkononi.
Polisi walifika haraka sana, wakanikamata mimi,
yeye na yule machinga niliyeona anaonewa,
tukapelekwa Msimbazi polisi.
Tulipofika pale, afande aliyetukamata alituamuru
kuvua viatu, mikanda, simu kuweka pembeni.
Halafu mmoja alianza
kutusachi mifukoni. Wakati tendo hilo linaanza
kwa wenzangu, ndipo nikakumbuka mimi mfukoni
nina vipisi viwili vya bangi.
Nilitaka kutoka mbio kituoni hapo, lakini sehemu
tuliyokaa, ningesema nitoke, nisingefika nje au
hata kama ningefika ningekamatwa au kupigwa
risasi kama mhalifu, nilitetemeka, mwili uliisha
nguvu.
Ilipofika zamu yangu kusachiwa, askari
mwenyewe alishangaa kuniona nachezesha
miguu kama niliyebanwa na haja ndogo,
akaniuliza:
"We vipi, unaumwa?"
Nikamjibu naumwa afande.
"Unaumwa nini?"
"Sijui, nadhani homa."
Hakunijibu, alianza kwa kutumbukiza mkono
kwenye mfuko usiokuwa na kitu, akahamia wa
nyuma ambao una waleti, akapeleka wa kulia
kwangu ambao ndiyo wenye bangi, aliposhika,
akakunja sura, alipotoa akashtuka sana na
kusema:
"Haa! Hii bangi siyo?" ITAENDELEA..!
S
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom