Simulizi: Nilipanga nyumba moja na majini

Simulizi: Nilipanga nyumba moja na majini

SIMULIZI: THE HOUSE OF THE DEVIL (Nyumba
ya kishetani)

MSIMULIAJI: HUMULI SAMAKI

MWANDISHI: METECK DERTHOD

Sehemu ya 06

Endelea...

"We kohoa mpaka utapike, lakini mimi nipo hapa
mpaka utoke."
Nilikata simu, nilikuwa nahema sana, mapigo ya
moyo yalikuwa yakienda kwa kasi ya ajabu huku
nikishindwa kuona sawasawa.
"Hii ni hatari sasa," nilisema.
Usiku wa siku hiyo sikulala kusema kweli kwani
kila nilipofikiria maisha yale sikuona sababu ya
kuendelea kuishi pale. Moyoni nilisema kwamba,
ni afadhali ningeishi na watu ambao ni
majambazi kuliko hawa, nafuu ningepanga
nyumba moja na makahaba kuliko kupanga
nyumba moja na majini.
Nilichoamua, asubuhi nikifika kibaruani tu niombe
ruksa kisha nianze kumsaka yule dalali na pia
nitafute dalali mwingine ambaye atanitafutia
vyumba kwingine na si maeneo yale tena kwani
niliyaona yana nuksi.
Asubuhi kulikucha salama kabisa, tena usiku wa
siku hiyo sikuona mauzauza wala dalili zake.
Nilikwenda kuoga bila kukagua mazingira, moyoni
nilisema liwalo na liwe kwa maana kwamba,
wawepo wasiwepo sawa tu.
Bafuni niligundua wameshaoga kwani kulikuwa
na majimaji ya muda mfupi uliopita. Nilipomaliza
kuoga, nilijiandaa na kutoka. Nje nilikutana na
mtu ana mkokoteni, akanisalimia.
"Za asubuhi bwana mkubwa?"
"Salama, karibu sana."
"Asante, kuna watu fulani wanaishi humu nina
shida nao."
Aliposema hivyo nilishtuka sana, niliamini yeye ni
mmoja wa wale ila amejigeuza kwa kujifanya ana
shughuli za mkokoteni.
"Unawajua kwa sura?" nilimuuliza huku nikiwa na
wasiwasi maana alinikazia macho.
"Siwajui."
"Sasa una shida nao kivipi watu usiowajua kwa
sura?"
Ni kwamba, kuna binti mmoja huwa wanamtuma
niwaletee maji, nikifika hapa huyo binti anabeba
madumu kupeleka ndani, sasa jana nilikutana na
huyo binti nikamuuliza kuhusu malipo yangu ya
mwezi sasa, akasema nije nifuatilie mwenyewe."
Nilishangaa sana kusikia hivyo. Nijuavyo mimi
mle ndani mna watu wawili, mwanamke na
mwanaume, sasa kama kuna binti hilo lilikuwa
jipya kwangu, labda lakini.
"Huyo binti naye anaishi humu au?" nilimuuliza.
"Sidhani, inaonekana kama huwa wanamtuma
tu."
"Kwa nini huamini kama anaishi humuhumu
ndani? Hafanani na wao wenyewe?" hili swali
niliuliza likiwa na mtego mkubwa sana, nilitaka
nijue uhalisia wake.
"Siwezi kusema hafanani wakati wao siwajui kwa
sura."
Hapo ndipo nilipopataka, nilidhani atasema
hafanani nao, ningejua ni walewale.
"Oke, nadhani wameondoka kwenda kazini."
"Ah! Sasa mimi fedha zangu nitazipataje jamani?"
"Subiri wakirudi jioni."
"Wewe utakuwepo?"
Nililishangaa swali hilo, hakuwa akinidai mimi
lakini anataka niwepo?
"Unataka niwepo?"
"Ee."
"Kwa nini?"
"Naamini utanisaidia kuzipata fedha zangu."
"Uliwahi kuja wakagoma kukupa?"
"Siyo hivyo, ila kila nikija, nikigonga mlango huwa
hawafungui."
"Basi nitakuwepo."
"Asante kaka. Nije saa ngapi?"
"Saa moja nitakuwa nimerudi."
Aligeuza mkokoteni na kuondoka zake huku
akisema:
"Muda huo nitakuwa nimefika kaka."
Niliondoka kwenda kazini kuomba ruksa. Lakini
wakati naondoka, mfanyakazi mwenzangu mmoja
aliniuliza nakwenda wapi, nikaamua kumsimulia
kwa ufupi kisa changu.
"Kha! Sasa hapo tatizo liko wapi, mbona dawa
ipo rahisi sana."
"Rahisi! Ni ipi hiyo?"
"Sikia, twende pembeni nikakusimulie," aliniambia
yule mfanyakazi mwenzangu huku akiangalia
kulia na kushoto kama mabosi watatokea.
Tulikwenda kusimama pembeni, akaanza
kuniambia:
"Sikiliza, kama unaishi nyumba ya namna hiyo,
unachotakiwa kufanya, kila siku asubuhi na jioni
au usiku unapuliza bangi ndani ya nyumba, kama
ni majini, mapepo sijui nini, utaona mambo poa
kabisa."
Sikuamini maneno hayo, nikamuuliza mara
mbilimbili kama ni kweli.
"Khaa! Nina mjomba'ngu aliwahi kuishi kwenye
nyumba ya hivyo, akaenda sehemu akaelekezwa
dawa ni hiyo, akaitumia, mpaka sasa anaishi kwa
raha hakuna cha majini wala mapepo," alisema.
Nilimsikiliza nikianza kuamini kwa mbali, lakini
nilifika mahali nikamuuliza hiyo bangi mimi
nitavuta au nitaiwasha ili itoe moshi yenyewe?
"Ukishaiwasha, utaiweka mezani au popote ndani
kwako, lakini angalia isizimike ili moshi wake
usambae chumba kizima au sebule nzima."
"Hilo linawezekana," nilimwambia nikimtumbulia
macho.
Kwa sababu nilikuwa nimeshaaga, ilibidi niondoke
tu na kurudi baadaye. Nilikwenda mtaani,
nilitafuta bangi nikapata maeneo ya Kariakoo,
nikaitia mfukoni.
Nilizurura sana siku hiyo, saa tisa kamili nilikuwa
njiani narudi kazini. Nilipiga hesabu za kufika
kazini na kuondoka, maana muda wa kazi ni saa
tisa na nusu.
Wakati napita pale Kituo cha Polisi Msimbazi,
fujo zikazuka, kuna machinga wawili walikuwa
wanapigana kwa sababu ya kugombea sehemu
ya kufanyia biashara, katika ugomvi huo mimi
nilibaini mmoja wao ndiyo mwenye kosa.
Nikampa laivu kuwa yeye ndiye mwenye tatizo,
alikuja juu, akachukua boksi lenye viatu na
kunirushia, likanipata kwenye bega la kulia,
sikukubali, nikaokota jiwe na kumrushia,
likampata mkononi.
Polisi walifika haraka sana, wakanikamata mimi,
yeye na yule machinga niliyeona anaonewa,
tukapelekwa Msimbazi polisi.
Tulipofika pale, afande aliyetukamata alituamuru
kuvua viatu, mikanda, simu kuweka pembeni.
Halafu mmoja alianza
kutusachi mifukoni. Wakati tendo hilo linaanza
kwa wenzangu, ndipo nikakumbuka mimi mfukoni
nina vipisi viwili vya bangi.
Nilitaka kutoka mbio kituoni hapo, lakini sehemu
tuliyokaa, ningesema nitoke, nisingefika nje au
hata kama ningefika ningekamatwa au kupigwa
risasi kama mhalifu, nilitetemeka, mwili uliisha
nguvu.
Ilipofika zamu yangu kusachiwa, askari
mwenyewe alishangaa kuniona nachezesha
miguu kama niliyebanwa na haja ndogo,
akaniuliza:
"We vipi, unaumwa?"
Nikamjibu naumwa afande.
"Unaumwa nini?"
"Sijui, nadhani homa."
Hakunijibu, alianza kwa kutumbukiza mkono
kwenye mfuko usiokuwa na kitu, akahamia wa
nyuma ambao una waleti, akapeleka wa kulia
kwangu ambao ndiyo wenye bangi, aliposhika,
akakunja sura, alipotoa akashtuka sana na
kusema:
"Haa! Hii bangi siyo?" ITAENDELEA..!
S
Umeirudia hii
 
: THE HOUSE OF THE DEVIL (Nyumba
ya kishetani)

MSIMULIAJI: HUMULI SAMAKI

MWANDISHI: METECK DERTHOD

Sehemu ya 07

Endelea...

Hakunijibu, alianza kwa kutumbukiza mkono
kwenye mfuko usiokuwa na kitu, akahamia wa
nyuma ambao una waleti, akapeleka wa kulia
kwangu ambao ndiyo wenye bangi, aliposhika,
akakunja sura, alipotoa akashtuka sana na
kusema:

"Haa! Hii bangi siyo?"

Sikumjibu kwani niliamini ameshaijua, wenzake
waliokuwa kaunta wakaacha mambo yao na
kunigeukia mimi, nao wakashangaa sana. Mmoja
alikuwa amekaa juu ya stuli, akashuka huku
akiniangalia kwa kunikazia macho.

"Unakuja kituo cha polisi na bangi, wewe
unatutafuta nini sisi?" aliuliza yule aliyeshuka
kwenye stuli.
Niliambiwa nafunguliwa kesi ya pili, ya kwanza
kupigana na kujeruhi ya pili kukutwa na bangi!
Nilijitetea nikisema bangi ile si kwa ajili ya
kuvuta bali nilikuwa nina shida nayo.

''Wewe usitufanye sisi watoto wadogo, tunawajua
ninyi raia," alisema yule afande aliyenisachi.
Lakini afande mmoja wa kike ambaye muda wote
alikuwa akiangalia tu, akawaambia
wenzake:

"Lakini huyu kaka mbona hafanani na kuvuta
bangi, muulizeni ana shida nayo gani?"

Wale wenzake wakanigeukia na kuniuliza:

"Haya, wewe mwananchi, raia kabisa, unaweza
kuwa na shida gani na bangi mbali na kuvuta?"

Niliwasimulia kila kitu, tena nilifika mahali
nikawaambia kama kuna asiyeamini, tuongozane
hadi nyumbani, Magomeni akaone maajabu
ambayo hayahitaji kuelekezwa sana ili kuamini
kama yapo au la!

Palipita ukimya wa sekunde kadhaa, mmoja wao
akaniuliza:

"Kama ni kweli au tufanye ni kweli, ni kwa nini
umemuumiza huyu?"

Nilisema kilichotokea, yule chinga niliyemsaidia
naye akanitetea kwa kusema hivyohivyo, lakini
afande mmoja akasema nilijichukulia sheria
mkononi ambapo ni kosa kisheria.
Niliomba sana wanisamehe kwa yote, nikasingizia
kwamba ni kwa sababu kichwa changu hakipo
sawa kwa kuishi nyumba moja na majini.
Namshukuru mmoja wao aliniambia niondoke
lakini nihakikishe situmii bangi katika kujitibu
kwani serikali haiamini kama bangi ni dawa.
Nilipotoka, nilikwenda kununua nyingine, lakini
akili iliingia hisia kwamba, huenda yule dada wa
ajabu mle ndani ndiye anayecheza michezo ili
kunikwamisha kwenda na bangi ndani ya
nyumba, nikasema moyoni ngoja ninunue hii
nione kitakachotokea, nikanunua tena misokoto
miwili.
Nilitembea kuelekea kituo cha daladala. Njiani
nilimpigia simu yule mfanyakazi mwenzangu
aliyenijulisha kuhusu dawa ya kutibu nyumba
yenye majini, nikamwambia sitaweza kurudi
kwani nilipata wakati mgumu kidogo njiani.
Alinielewa, akaniuliza kama nimepata, nikamjibu
kila kitu kimekwenda sawa, lakini sikumwambia
kuhusu timbwili lililojitokeza.
Nilipanda daladala nikashuka Magomeni, niliingia
ATM kutoa fedha kidogo, kisha nikatoka. Wakati
natafuta mwelekeo wa kwenda nyumbani,
nilimkumbuka dalali, nikampigia simu.

"Halo."

"Halo habari za kazi bwana?"

"Nzuri, pole na kazi na wewe mwenzangu?"

"Nimepoa. Bwana vipi kuhusu nyumba?"
nilimuuliza.

"Nyumba imefanyaje?"

"Si nilikusimulia matatizo yake, umesahau?"

"Kwani ulisema matatizo yake yakoje vile?"

Nilimwelezea kwa kirefu, nikafika mahali
nikamwambia hadi nilivyompigia simu halafu
ikapokelewa na sauti ya ajabuajabu, alicheka
sana.

"Wewe bwana acha kunichekesha.

"Kwa nini unasema hivyo?"

"Yaani simu yangu mimi halafu apokee mtu
mwenye sauti ya ajabuajabu, kwa nini sasa?"

"Mimi pia sijui."

"We ulikosea namba."

"Labda bwana mi siwezi kukazania sana,"
nilimjibu kwa kinyongo kwani namba yake
niliisevu na ninapompigia huwa nasachi jina tu,
sasa nilikosea kivipi?

"Enhe, unasemaje bwana?" aliniuliza.

"Nimeshakwambia bwana."

"Kwa hiyo unashauri nini?"

"Nataka pesa zangu nikapange kwingine."

"Da! Hilo halitawezekana kirahisi bwana, maana
mpaka nimpate mpangaji mwingine atoe fedha
ndipo nikulipe wewe na mpangaji atakayekuwa
tayari kutoa fedha lazima akute nyumba tupu,

sasa wewe utalikubali hilo?"

"Naweza kulikubali, ila tuandikishiane."

"Kwamba?"

"Kwamba unajikomiti nikiondoka, akiingia
mpangaji mwingine tu unanilipa pesa zangu."

"Ngoja nitakupigia," alisema dalali na kukata
simu.
Nilipokuwa nakaribia nyumbani, nikakutana na
yule msukuma mkokoteni wa maji.

"Kaka za kazi?"

"Nzuri, vipi wewe?"

"Niko sawa, ndiyo unarudi?"

"Ndiyo."

"Najua jamaa hawajarudi, nitakuja muda uleule
tuliopanga."

"Sawa, karibu sana."

"Asante sana."

Niliingiza funguo ili kufungua mlango, lakini
nikagundua kwa ndani kulikuwa na funguo
nyingine maana nilichungulia.
Nilipousukuma, ulifunguka. Hii ina maana wale
watu wa ajabu walikuwa wamesharudi, wako
ndani. Niliingia ndani, nikafungua mlango wa
sebuleni, nikaingia humo.
Nilifikia kwenye kochi kubwa, nikajilaza.
Sikuangalia kama kweli wenzangu walikuwa
wamesharudi, ila nilisikia sauti ya muziki wa
redio, nikajua wapo.
Mara nikasikia mlango wao mmoja ukifunguliwa,
nikasikia mtu akitoka. Kwa mara ya kwanza
nilisikia akisema:

"Kama utamkamata anavuta bangi apelekwe
polisi, ndiyo dawa yao watu wa aina hii."
Nilishtuka, nikakaa. Nikawaza kama ninachosikia
ni cha kweli au?

Huyo aliyekuwa akisema hayo ni mwanamke na
ilionekana alitoka kuelekea uani. Nikatoka ghafla,
nikaona kisigino cha mguu mmoja kikimalizia
kuingia chooni.
Nilirudi chumbani huku najiuliza kama hawa watu
walisema vile kwa sababu wamejua mimi
nimenunua bangi au? Na ni kwa nini wazungumze
Kiswahili kwa mara ya kwanza siku hiyo?
Baada ya dakika mbili, nilimsikia akirejea
chumbani kwake huku akisema:

"Mimi mtu anayevuta bangi siku yoyote na
mahali popote pale, nikimwona nampeleka polisi
ajue mimi ni nani. Haiwezekani watu wawe
wanavuta bangi hovyo tu.
Moyoni nikasema hata iweje, hii bangi leo lazima
niichome humu ndani. Mkienda polisi msipoenda
mtajua wenyewe.

"Mimi siwezi kuishi katika mazingira magumu
namna hii wakati pesa ni yangu. Kwa nini
ustaarabu usiwepo?" nilisema moyoni nikipeleka
mkono mfukoni ili kutoa ile bangi niliyonunua
mara ya pili.

Niliipata, nikaitoa. Niliiweka kwenye meza kisha
nikaendelea kulala nikiusaka usingizi kwa nguvu
zangu zote maana nilijisikia kuchoka sana. Hapo
nilikuwa sijaenda chumbani kwangu.
Sikumbuki ni muda gani nilipitiwa na usingizi, ila
nakumbuka wakati nalala ilikuwa saa kumi na
moja. Nilipokuja kushtuka
ilikuwa saa kumi na mbili na nusu. Ina maana
nililala kwa saa moja na nusu.
Jicho langu moja kwa moja lilitua kwenye bangi
pale mezani, sikuiona.
ITAENDELEA...!
 
Safi sana...

Ila jamaa ameniudhi, yani anaingia na bangi badala ya kuichoma analala tena...


Cc: mahondaw
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom