Abdallahking
JF-Expert Member
- Mar 19, 2018
- 3,983
- 10,804
- Thread starter
- #441
SEHEMU YA 388
Rahim alimkaribisha baba Angel kwenye ile ofisi ambapo walikuwa wawili tu na kuanza kuongea nae alichotaka kuongea nae, ila kabla ya yote baba Angel alimshukuru kwanza kwaajili ya kumtambulisha baba yake kwenye biashara yake,
“Nashukuru sana Rahim, sikujua kama ungefanya kitu kama hiki”
“Sina ugomvi na wewe, najua ugomvi wetu mkubwa huwa upo kwenye mapenzi sababu wote tumempenda mwanamke mmoja ila bado sio sababu ya mimi kugombana na wewe kila mara. Mara nyingi huwa nipo na pombe kichwani ndiomana nakujibu vibaya na kugombana na wewe ila sio kwa akili zangu timamu. Usijali kuhusu hilo, kumbuka kabla ya yote tumewahi kuwa marafiki wazuri sana, na tukiambiana kila kitu, kwahiyo bado nakumbuka mazuri tuliyotenda pamoja”
“Oooh sawa, ni vizuri sana”
“Sasa nilichokuitia ni kuhusu Angel”
Baba Angel akashtuka kidogo na kumsikiliza Rahim ambapo Rahim aliendelea kuongea,
“Yule binti kawa mkubwa kwasasa, nakumbuka pale shuleni hata nilivyomfata kumsalimia alinikwepa. Kama mzazi iliniuma sana ile kitu, na jinsi Angel alivyokaribu na wewe nikaumia zaidi, nakuomba jambo moja mwanaume mwenzangu, naomba Angel atambue ukweli, naomba Angel anitambue baba yake halisi na anipokee kama baba yake halisi, yani Angel ajue kama mimi ni mwanae”
Baba Angel akapumua kidogo na kusema,
“Dah, ila hilo swala ni gumu sana kuongea mimi”
“Najua ni ngumu sababu Angel amekuzoea sana, siku zote anajua kuwa wewe ni baba yake, hana wazo kuwa kuna kiumbe sijui baba mwingine wa kuitwa Rahim, naomba fanya lolote ili Angel atambue uwepo wangu”
“Labda niongee na mama yake ndio amwambie”
“Sijui kama atakubali ila najua wewe ni mwanaume pekee unayeweza kumshawishi Erica kuongea na mwanae ukweli wa mambo yote”
“Ila Rahim, unajua una makosa sana, kipindi kile niliweka utaratibu mzuri tu wa mtoto kuweza kukutambua wewe kama baba yake ila wewe ukataka kufanya mambo mengine”
“Sikatai, ni kweli nilifanya makosa yani hilo nakiri kabisa, nisamehe na Mungu anisamehe. Kweli ni mara nyingi sana nilitaka kumbaka Erica, sababu bado nilikuwa na mapenzi nae, nilijilaumu sana kuoa mwanamke ambaye hakuwa chaguo langu sababu yule alikuwa chaguo la baba, na mimi nilikubali tu kwa kutumiwa picha zake, niliporudi nikawa nae yeye, huwa najiona mjinga sana kumuacha mwanamke kama Erica ambaye kwa kipindi kile alikuwa tayari kwa chochote kile kwaajili ya mtoto ila mimi nilikuwa mjinga sana. Naomba hayo yaishe, ila naomba ongea na Erica amwambie ukweli Angel, amueleze kuwa mimi ni baba yake halisi ili Angel anithamini na kuniamini”
“Sawa, nitajaribu kuongea nae kuhusu hilo kwani Angel kawa mkubwa kwasasa anatakiwa kujua ukweli”
“Asante sana Erick, nashukuru sana kwa hilo yani utakuwa umenisaidia kwa kiasi kikubwa sana, natamani sana mtoto wangu anifahamu”
Basi baba Angel aliagana na Rahim kisha yeye kuondoka zake na kurudi nyumbani kwake huku kichwa chake kikiwa na mawazo mengi sana.
Usiku wa leo, wakati baba Angel yupo chumbani na mke wangu akaamua kumueleza lile swala la kukutana na mwarabu ya kuwa Rahim ni mtoto wa yule mwarabu na kitu ambacho Rahim kakifanya kumjulisha yule mwarabu kuhusu bidhaa zao,
“Mmmh Rahim huyo ndio kamfahamisha yule mwarabu kiwanda chetu!”
“Ndio, ni yeye. Mwarabu mwenyewe kasema hilo”
“Basi Rahim huwa anajichetua tu, kumbe mara nyingine anajielewa. Tunamshukuru kwa hilo”
“Ila kuna jambo lingine”
“Lipi hilo?”
Baba Angel aliamua kumwambia mama Angel kuhusu kile ambacho Rahim amekisema kuhusu kutambulishwa kwa Angel, basi mama Angel akasema,
“Kheee ndiomana kumbe kumtambulisha baba yake kiwanda chetu ili tuweze kumfahamisha kuhusu Angel! Aaaargh alivyokuwa akifanya ujinga hakujua kama kuna siku itabidi amfahamu Angel kwa undani zaidi?”
“Kaomba msamaha, ila mke wangu ni kweli ana haki ya kufahamiana na mtoto wake”
“Mimi simtambui Rahim, ninachojua ni kuwa Angel ni mtoto wako”
“Ila mama Angel twende mbele na kurudi nyuma, wakati unamwambia Rahim kuwa una ujauzito wake alikataa?”
“Hapana”
“Kipindi cha mimba alikuwa hakuhudumii?”
“Hapana, alikuwa akinihudumia vizuri tu hata akanipangia chumba maana niliogopa kurudi nyumbani na mimba, mama algundua siku ya mwisho mimi kwenda kujifungua”
“Ila unajua kuwa kuna mabinti wanabeba mimba na kukataliwa pindi anapomwambia mwanaume tu kuwa nina ujauzito wako?”
“Najua”
“Wewe chanzo cha Rahim kuacha kuhudumia mtoto na mengine ni kitu gani?”
“Kwakweli sijui, ila nakumbuka kila nikimwambia njoo kwetu anasema nitakuja nitakuja, halafu toka nilipojifungua ndipo Rahim alipoanza kupunguza matumizi kwangu kanakwamba hakumtaka tena mtoto. Hata nimwambie kitu gani hakuwa na muda wa kunisaidia kabisa, nakumbuka niliongea na dada zangu wakaniambia kama mwanaume ana pesa, muombe basi hela ya mtaji ili angalau upate cha kujishikisha uweze kulea mtoto wako, kwakweli hela Rahim alikuwa nayo wala sio hela ya kubabaisha, nikamuomba hela ya mtaji. Nakiri kwamba nilimuomba hela kubwa ila hakutakiwa kunijibu kitu ambacho alinijibu”
“Ulimuomba pesa ngapi?”
“Nakumbuka wazi, nilimuomba milioni kumi na tano ili nifungue biashara ya kuuza vitu vya watoto. Ni bora Rahim angenijibu kiustaarabu kuwa sina hiyo pesa au mimi nina kiasi kadhaa kwahiyo fikiria biashara nyingine, ila hapana alianza kunikejeli alinitusi sana, niliumia sana moyo wangu hadi akasema nimemfanya yeye ndio tegemeo langu na familia yangu kwasababu sisi ni masikini, akaniambia badala nimuombe elfu kumi ya mtaji eti namuomba milioni kumi na tano, nafikiri pesa inaokotwa, yani alinijibu kwa kejeli sana. Toka hapo ikawa ndio kama nimemfukuza kwani hakutaka tena kuwasiliana na mimi, hakutaka kujua habari za mtoto wala kumsaidia mtoto. Nilikuwa nalia tu, kumbuka ndio nilitoka kumaliza chuo, sikuwa na kazi wala chochote cha kuniingizia pesa, niliona maisha mabaya sana, nikikaa kidogo mama ananisema sana kuwa mimi ni mjinga kwa kuzaa mtoto asiye na baba. Yote aliyoyafanya Rahim sikuhesabia kama ni kosa ila swala la kutokutaka kumuona mtoto liliniuma sana, hakuwa na mpango wa kuja kujionyesha kwetu na wala kusema kuwa Angel ni mwanae. Nakumbuka hadi nilimwambia Rahim kama kikwazo ni dini basi mimi nipo radhi kubadilisha dini ili tulee mtoto pamoja, ila Rahim alinikataa kabisa. Unadhani ningefanya nini? Kumpeleka mtoto kwa baba asiyemtaka kweli?”
Baba Angel alipumua kidogo na kuongea tena na mke wake,
“Hilo kweli ni kosa, tena kosa kubwa tu alilolifanya ila nadhani ni upepo mchafu ambao ulimpitia kiasi cha kukataa kufahamishwa vizuri kwa mtoto aliyemuhudumia toka tumboni. Ila mimi kama mwanaume najua ni jinsi gani wanaume tulivyo na makosa, nakuomba mke wangu shusha moyo na upunguze presha, mwambie Angel ukweli wa mambo ili amjue baba yake halisi”
“Kwani umechoka kumlea Angel?”
“Hapana sijasema hivyo ila Angel ana haki pia ya kujua ukweli, yani yeye ndio atakuwa na maamuzi ya mwisho ila muweke wazi aufahamu ukweli”
“Dah!! Hiyo kitu naiona ni ngumu sana kwangu”
“Jitahidi mke wangu”
“Nitajaribu, ila sijui kama nitaweza kwakweli”
Kwa siku hiyo mama Angel alijihisi hata kutokupata usingizi kabisa, alikuwa akigeuka huku na huko akiwaza jinsi ambavyo Angel atachukulia hilo swala la kuambiwa ukweli halisi wa maisha yake.
Siku hii, mama Angel baada ya kazi za hapa na pale alimwambia Angel kuwa anahitaji kutoka nae sababu ana maongezi nae, hakufikiria kama lile jambo anaweza kuongea na Angel pale nyumbani.
Basi alitoka na Angel moja kwa moja alienda nae ufukweni na kuanza kuongea nae,
“Mwanangu Angel, leo nataka kukwambia ukweli”
“Ukweli gani huo mama?”
“Nisikilize kwa makini”
Angel alitulia na kumskiliza mama yake,
“Katika maisha yangu, kuna mwanaume mmoja nilikutana nae, niliamini ananipenda sana kwani alikuwa akionyesha mapenzi ya kweli kwangu na hata pesa alikuwa akinipatia, ila nikaja kupata ujauzito wake hapo ndio palianza kuwa na utata. Baada ya kujifungua alikataa kabisa kuja nyumbani kwetu na kufanya nitukanwe sana, nidharauliwe na kuitwa malaya kuwa niliyezaa nae simfahamu, nililia sana ila ni kosa kweli nilifanya kukubali kuzaa na mwanaume ambaye sifahamu hata nyumbani kwao. Nilikuwa nawasiliana nae na ananijibu vibaya sana, na mwisho wa siku alikata kabisa mawasiliano na mimi. Kwakweli niliona dunia ikinishurutisha sana na kunikosesha furaha kabisa kwani muda mwingi nilikuwa nikilia na kumshika mwanangu aliyekuwa akijaa machozi yangu, ila Mungu mwema akatokea mwanaume mwingine na kunipenda sana, huyu mwanaume akasema kuwa yupo tayari kumlea mtoto wangu na kumpa jina lake ni kweli kamlea kwa mapenzi yote, ila sasa kajitokeza yule mwanaume wa kwanza anamtaka mtoto wake”
Hapo mama Angel alinyamaza kwanza na kuinama chini huku machozi yakimtoka, Angel alimuangalia mama yake na kumuuliza,
“Unamaanisha huyo mtoto ni mimi? Unamaanisha baba sio baba yangu?”
Mama Angel alikuwa akilia na kusema,
“Nina uchungu mwanangu Angel nina uchungu sana, sikujua kama kuna siku kama ya leo itatokea katika maisha yangu. Nilifanya makosa sana, naomba unisamehe mwanangu”
“Sijakuelewa mama, naomba unieleweshe”
“Mwanangu, Erick sio baba yao mzazi. Baba yako mzazi anaitwa Rahim”
“Hapana mama, sitaki kusikia jambo kama hilo”
“Huo ndio ukweli mwanangu”
“Yani baba sio baba yangu! Hapana mama sitaki, sitaki kusikia hivyo”
Angel aliinuka na kuziba masikio kwa mkono halafu alianz akukimbilia baharini, hapo mama Angel akaona ni jambo lingine linataka kutokea, yani aliinuka na kumkimbia Angel, alipotaka kufika kwenye maji alimdaka kwa nguvu na kurudi nae nyuma ila Angel alisema,
“Ni heri nife kuliko kuniambia kuwa baba sio baba yangu”
“Jamani Angel mwanangu kwanini lakini, nisikilize kwanza”
Kwa muda huu mama Angel hakutaka kumuacha Angel mwenyewe, zaidi zaidi alimchukua hadi kwenye gari na kumpandisha huko, kisha naye akapanda na kumwambia,
“Mwanangu Angel jamani hebu jaribu kunielewa mama yako, nina maana thabiti kukueleza sasa”
“Sitaki kukuelewa na sitakaa nikuelewe juu ya hilo, ninachojua mimi ni kuwa baba ni baba yangu na si vinginevyo”
Mama Angel alijaribu kuongea ila kwa muda huu Angel hakumjibu chochote kile mama yake, yani alikaa kimya tu ilibidi mama Angel arudi nyumbani tu na mtoto wake.