Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

SEHEMU YA 355

Mama Angel alijikuta akijiwa na moyo wa huruma tu, kwani huwa akisikia mtoto anaumwa anasikia kuteseka sana moyoni, basi akahitaji kwenda kumuona.
Ikabidi yeye na Tumaini huku wakiongozana na Siku wakaenda hadi chumbani kwa Sarah na kumkuta amekaa huku akilalamika tumbo, walipoingia tu alianza kutapika, wakati wanamuhamisha ili wamfute yale matapishi walikuta kuna damu nyingi sana zinamtoka.
Hapo wakaona kuwa huyu mtoto anahitaji tiba ya haraka sana, kwahiyo ilibidi mama Angel aanze kumuandaa kwaajili ya kwenda nae hospitali, yani Sarah hata hakuwa na maelezo yanayoeleweka juu ya hali yake.
Wakatoka nae na moja kwa moja kuanza nae safari ya kwenda hospitali, Siku alibaki nyumbani huku akiwaangalia tu maana alihitaji kubaki na kuangalia nyumba kwani alijua wazi kama mama yao angerudi na kutokuwakuta wote ingekuwa balaa.
Baada tu ya wale kuondoka, ndipo Elly aliporudi nyumbani na kumkuta Siku yupo nje anafua, alienda ndani kumuangalia Sarah aliyemuacha mgonjwa ila hakumkuta, ikabidi arudi nje kumuuliza Siku aliyekuwa anafua,
“Yuko wapi Sarah?”
“Oooh Sarah ni mgonjwa, yani anaumwa sana kwahiyo walikuja hapa wale wakina mama Erick ndio wamempeleka hospitali”
“Alizidiwa sana au?”
“Aaaah si unajua wale wana viherehere sana, mama si ameondoka kamuacha Sarah anaumwa hapa wala hakuwa na tatizo kwani alijua lazima atapona tu, ila wao sasa na viherehere vyao yani wamemchukua na kumpeleka hospitali”
“Sasa hata hujui ni hospitali gani wamempeleka, wasiporudi nae je?”
“Kwani kwao hapafahamiki? Tutaenda nyumbani kwao, waache wahangaike nae huko, watamrudisha tu”
Basi Elly akatamani kujua kuwa Sarah alikuwa akisumbuliwa na nini, ila kwa muda huo njaa nayo ilikuwa ikimsumbua maana aliondoka bila ya kula chochote, akamwambia Siku,
“Si chai ipo eeeh! Ngoja nikakoroge ninywe”
Muda huo huo Siku aliacha kufua na kumwambia Elly kuwa anaenda kumuandalia chai, basi moja kwa moja aliingia nae ndani, na kumuandalia chai kweli ambapo Elly alikunywa na kujihisi vizuri, baada ya hapo Siku alimletea Elly juisi na kumtaka ashushie kwa ile chai aliyokunywa,
“Mmmh nimeshiba sana”
“Aaaah kwetu kukataa mtu kitu alichokuandalia ni vibaya kabisa, naomba unywe hata kidogo”
Basi Elly alichukua ile glasi na kunywa kidogo ila baada ya kunywa tu alijihisi kulewa yani kama mtu aliyekunywa pombe, basi Siku alifunga milango na kumchukua Elly kwenda nae chumbani kwake, na kuanza kumpapasa, na kuweza kulala nae sababu tu Elly hakujielewa na ile hali ya kuwa kama amelewa.
Yani Elly alivyokuja kurejewa na fahamu zake aliumia sana kwenye moyo wake kwani hakutegemea kufanya kile kitu na Siku,
“Kwanini umenifanyia hivi dada?”
“Nilikuwa nakutamani sana Elly kwa muda wote, yani kila siku nilikuwa nakutamani sana. Nashukuru leo nimepata nafasi, huu ni mwanzo najua sasa utakubali kwa hiyari yako”
Elly alichukia sana, na kutoka mule chumbani kwa Siku na kwenda chumbani kwake huku akiwa amechukia sana.

Wakina mama Angel walifika hospitali wakiwa na Sarah na moja kwa moja alipelekwa kwenye matibabu, basi walitulia huku wakisikilizia kuwa itakuwaje. Mama Angel aliamua kumpigia simu mama Sarah ila ile simu iliita sana hadi kukatika yani hakuna cha maana alichokipata.
Baba Angel akasema,
“Haya mambo ndio huwa siyapendi, kweli mama wa mtoto anaondoka na kuacha mtoto wake anaumwa jamani”
“Labda alijua anaumwa kidogo”
“Kidogo, hakumuangalia vizuri, kwa zile damu zilizomtoka inaonyesha ni muda mrefu tatizo lilianza”
Waliongea kidogo pale huku baba Angel akifatilia hali ya yule mtoto Sarah, badae daktari alikuja na kuhitaji mzazi wa yule mtoto, sababu wale ndio walimpeleka na kudai kuwa ni ndugu wanaoishi na yule mtoto ilibidi tu awaambie kinachomsumbua yule mtoto,
“Ni hivi jamani, inaonekana mtoto alikuwa na mimba changa sasa imetoka”
Wote wakashangaa sana, mama Angel aliuliza,
“Jamani, mtoto mdogo kama Sarah anatoa wapi mimba?”
Tumaini akadakia na kusema,
“Kila siku huwa nasema sana kuhusu malezi mabovu, kwani Daima kapata vipi ile mimba aliyoipata? Watoto wa siku hizi wana mambo sana”
Basi daktari akaondoka kuendelea na huduma kwa yule mtoto kwani ilibidi wamsafishe, kwakweli baba Angel aliwaambia,
“Jamani, mimi naondoka mtaniambia yatakayojiri. Sitaki habari za watoto wasiojielewa kama huyo”
Baba Angel aliondoka zake na kumuacha pale Tumanini na mama Angel, ila muda kidogo Tumaini nae aliondoka zake na kumuacha pale mama Angel, yani mama Angel alishindwa kuondoka bila ya kuruhusiwa kuondoka na Sarah, kwahiyo hakutaka kuondoka kabisa.

Tumaini akiwa njiani akielekea nyumbani kwake, ndipo alipokutana na mama Sarah, alimsimamisha na kuanza kuongea nae,
“Kheee unajua nilikuwa sikujui kabisa mambo yako, kumbe wewe mwanamke ni mbaya kiasi hiki”
“Kwani nimefanyeje?”
“Unawezaje kuondoka na kumuacha mwanao mgonjwa ndani au ulikuwa ukijua ni kitu gani kinamsumbua mwanao?”
“Kwahiyo ulikuwa nyumbani kwangu?”
“Ndio, tulikuwa na kikao na wewe kwani tulikuwa tukihitaji kujua ukweli kuhusu mtoto Sarah, ila hatujakukuta na kumkuta mtoto akiumwa vile nyumbani kwako”
“Kheee jamani, Sarah alikuwa anaumwa tumbo tu wakati naondoka. Siwaelewi imekuwaje?”
“Imekuwaje kuhusu nini? Mwanao katoa mimba huko”
“Katoa mimba? Hiyo mimba Sarah aitoe wapi? Mbona mnataka kuchekesha walionuna”
“Ndio hivyo, nenda hospitali huko kamfate mwanao. Umemkuta Erica hana roho mbaya na ndio kabaki na mwanao hospitali, nenda kamuangalie huko. Nilikusema sana kwa malezi mabaya unayompa Sarah, nadhani umeona matunda yake sasa”
Tumaini akamuelekeza tu hospitali aliyolazwa Sarah na kuachana nae pale.

Walipomaliza kumuhudumia Sarah na kila kitu ndio wakampa ruhusa mama Angel aweze kurudi nae nyumbani, daktari aliongea tu na mama Angel kiasi kidogo pale,
“Mpeni mtoto elimu stahiki, kumbe alikuwa mjamzito halafu akaenda kuchoma sindano ya uzazi wa mpango, imeenda kuharibu ile mimba na ndiomana kaumwa sana, hebu muwe makini sana na hawa watoto wenu, mtawapoteza mjue.”
Basi akapewa na dawa zitakazoweza kumsaidia kwa kipindi hiko, mama Angel akaondoka sasa na Sarah yani alikuwa akimuangalia bila ya kummaliza kwakeli, basi akawa anaondoka nae huku akiendesha gari na kumuuliza baadhi ya maswali,
“Kwanza Sarah ulipata vipi hiyo mimba?”
Sarah alikuwa kimya tu huku akiinama chini, mama Angel alipumua kidogo na kumuuliza tena,
“Na ilikuwaje hadi ukaenda kuchoma sindano ya uzazi wa mpango?”
Bado Sarah alikuwa kimya tu, basi mama Angel akamwambia,
“Utaniambia vizuri ukiwa vizuri, nakuhurumia sana, wewe Sarah bado ni mtoto mdogo sana”
Basi walifika nyumbani kwakina Sarah na Sarah kuingia ndani na moja kwa moja mama Angel alimpeleka Sarah chumbani ili aweze kupumzika, ila wakati anatoka tu chumbani kwake alikutana na mama Sarah ambaye ndio alikuwa ametoka kufika,
“Yani nimetoka hadi kwenye ile hospitali mliyoenda nikaambiwa kuwa mmetoka, kwanza nakushukuru kwa hili ulilolifanya kwani mwanangu anaumwa nini?”
“Yani unakaa na mwanao kweli hujui tatizo lake? Mwanao alikuwa ni majamzito, kaenda kuchoma sindano ya uzazi wa mpango sijui basi ile sindano imeenda kuharibu ile mimba na kumfanya aumwe sana, na hiyo hali imefanya apoteze damu nyingi sana. Anatakiwa kula vizuri na kuna dawa nimemuachia hapo ambazo walimuandikia”
“Oooh nashukuru sana, sikutegemea kama ungefanya kitu cha namna hii, asante sana Erica”
“Usijali, watoto hawa ni wa kwetu sote. Ila dokta kasisitiza sana juu ya malezi tunayowapa watoto, tunatakiwa kuwa makini sana”
“Asante”
Basi mama Angel alimuaga na kuondoka zake, kwakweli hata yeye alishangaa mno kuona jinsi mama Sarah alivyokuwa mpole kwa siku hiyo.
Moja kwa moja mama Sarah alienda chumbani kwa mwanae na kumuangalia, basi alikaa karibu yake na kumuuliza,
“Mwanangu kwani hiyo mimba umepataje?”
“Sijui hata nimepataje”
“Nani alikupeleka kwenda kuchoma hiyo sindano ya uzazi wa mpango?”
“Sijui mama, nimechoka sana. Hali yangu sio nzuri kabisa, kwasasa nahitaji kupumzika”
“Pole sana mwanangu, Mungu atakusaidia utapona tu”
Kisha mama Sarah alitoka na kumtaka Siku amuandalie chakula Sarah ili aweze kwenda kumlisha kikiwa tayari. Siku hii mama Sarah hata hakujua kama ataweza kutoka kwa ile hali ya mtoto wake.

Mama Angel alirudi nyumbani kwake wakati hata giza limeanza kuingia na kumkuta mumewe akiwa amejilaza tu kwa muda huo, basi alienda kuoga na kurudi kuongea na mume wake,
“Ila mume wangu jamani, ndio kuniacha mwenyewe hospitali”
“Kiukweli huwa sipendi ujinga wa watoto wa kike kamavile kwakweli, mtoto anabeba mimba kwa umri mdogo vile! Na kwanini imetoka sasa?”
“Sijui alikuwa na mimba halafu akaenda kuchoma sindano ya uzazi wa mpango”
“Aaaargh katoto kana tabia mbaya hadi kamewaza kwenda kuchoma sindano ya uzazi wa mpango jamani!! Si umri wakina Erica yule aarrgh!”
“Unajua watoto tusiwalaumu sana vitu vingine hawajui”
“Hawajui wapi? Mtoto anajua kabisa nitapata mimba ndio kaenda kuchoma sindano ya uzazi wa mpango ili asipate na aendelee kufanya kwa raha zake, naye ni mtoto huyo? Hata sitaki tena awe karibu na watoto wangu maana atawafundisha tabia mbaya”
“Aaaah usiseme hivyo mume wangu, mimi nina uhakika Sarah hajapata mtu wa kuongea nae na kumuelewesha vizuri kwani nina hakika angeeleweshwa vizuri basi yote haya yasingetokea”
“Aeleweshwe nini na mtoto kashapata utamu wa tunda?”
Mama Angel alicheka tu, kisha baba Angel akauliza tena,
“Je umemuuliza nani muhusika wa hiyo mimba iliyotoka? Umemuuliza ni nani aliyempeleka kwenda kuchoma hiyo sindano ya uzazi wa mpango?”
“Nimemuuliza kabaki kimya tu, anaona aibu ila nasubiri apone vizuri nitamuuliza”
“Utamuuliza nini sasa? Si ndio wakina Daima hao? Toto limefata tabia mbaya ya mama yake lile aaargh”
Baba Angel alionekana kutokupenda kabisa lile jambo ambalo Sarah amelitenda kwahiyo kwa muda huo aliamua kulala tu wala hakutaka matatizo mengine.

Kulipokucha, Baba Angel alijiandaa na kwenda kazini kama kawaida na wakina Erica walienda shuleni kwahiyo pale nyumbani alibaki tu mama Angel, Vaileth na Ester kama kawaida.
Basi mama Angel alianza kumsimulia Vaileth kitu ambacho kimejiri kwa Sarah,
“Yani nimeumia sana kwa mtoto mdogo kama Sarah kupata ujauzito loh! Halafu kaenda kutumia sindano ya uzazi wa mpango jamani”
“Sasa nani kampa Sarah mimba?”
“Anataka kusema basi!! Sijui imekuwaje, yani mimi nina wasiwasi sana yasije kuwa mambo kama ya Daima”
“Jamani”
“Roho imeniuma sana, huwa namuona Sarah kama mtoto wangu, huwa namuona Sarah kama ninavyomuona Erica tu. Nimeumia sana”
“Kweli ni mdogo sana, kaanza mapenzi basi ndiomana akapata hiyo mimba, hadi imetoka dah!”
Mara mlango ulifunguliwa na aliyefungua mlango alikuwa ni Erica, basi mama yake alimuuliza kilichomfanya arudi mapema vile,

“Tumbo mama linaniuma sana”
Mama Angel akashtuka maana hofu ikamjaa kuwa isijekuwa mambo yale yale ya Sarah, basi alienda nae mwanae chumbani na kumuuliza vizuri,
“Ni tumbo gani linakuuma mwanangu”
“Tumbo la kikubwa mama”
Hapo mama Angel alielewa vizuri kabisa kitu kinachomsumbua mtoto wake.
Baada ya muda Erica alimfata Vaileth ambae kwa muda huu alikuwa chumbani kwake na kuanza kumuuliza,
“Ni nani mliyekuwa mnamzungumzia kuwa katoa mimba?”
“Ni Sarah huyo, yani kumbe mtoto mdogo ana mambo ya ajabu”
“Kheee Sarah kaanza mambo ya wanaume!! KWahiyo naye kapata mimba kama Daima?”
“Ndio ila imetoka, yani Sarah kafanya mchezo wa ajabu sana”
“Kheee kumbe!!”
Basi Erica aliridhika kwa muda kuipata habari hiyo maana alishindwa hata kupumzika kidogo bila kujua kilichokuwa kikizungumziwa na mama yake pamoja na Vaileth pale sebleni, kwahiyo alivyojua aliweza kuridhika na moyo wake sasa.

Baba Angel akiwa ofisini kwake leo alitembelewa na Sia, na kushangaa ila alimkaribisha na kumuuliza,
“Ndio ushapata jibu la utafiti wako juu ya aliniwekea sumu?”
Kidogo Sia alijiuma uma na kusema,
“Hiko sio kilichonileta ila kilichonileta ni swala lingine kabisa”
“Swala gani?”
“Hivi kwanza unajua kama Erica amewahi kuwa na mahusiano na Derrick? Ni ndugu yake ila amewahi kuwa na mahusiano nae”
“Hayo hayanihusu kabisa, kinachonihusu sasa ni kuwa Erica ni mke wangu halafu Derrick ni shemeji yangu”
“Duh!! Yani wewe Erick ni wa ajabu sana”
“Sema lingine ulilokuja nalo”
“Ni kuhusu mtoto Elly”
“Eeeeh una story mpya kuhusu Elly au kitu gani? Hebu sema ukweli kuwa Elly ni mtoto uliyezaa na Derrick”
“Hapana, mimi sijazaa na Derrick. Ngoja leo nikwambie ukweli”
“Haya, niambie nakusikiliza”
“Mimi kiukweli kabisa nilizaa na Steve yani huo ndio ukweli halisi”
Baba Angel alicheka kwanza na kusema,
“Ila wewe mwanamke jamani dah!! Nakusikiliza vizuri sana, na ulivyokuwa umekazana kuwa umezaa na mimi ni nini?”
“Sikiliza basi, ni hivi mimi siku nimeenda kujifungua nilienda kabla hata ya muda ila mwanangu alikuwa vizuri tu, sema hakuzaliwa kwa uzito ule uliotakiwa, basi ikapewa yule mtoto ila alikuwa akilia sanaalipokuwa kwangu. Baba yako mzee Jimmy alikuja kuongea nami, yani aliongea na mimi kabla sijajifungua na akaongea na mimi baada ya kujifungua, alipanga nami mpango wa kubadilisha mtoto wangu na mtoto wa Erica, nilikubali sababu ya shida yangu ya hela, mtoto alipofika miezi mitatu kasoro ndipo mzee Jimmy alipowabadilisha, kwamaana hiyo Elly ni mtoto wa Erica halafu Erick ni mtoto wangu ndiomana nilikuwa nakukazania kuwa nimezaa na wewe kwani nilijua hata mwanangu akipimwa damu atakutwa ni mwanao kweli yani Elly. Ila baada ya sokomoko hili la kusema kuwa Elly ni mtoto wa Derrick basi kuna uhakika kabisa kuwa Erica aliendelea na Derrick kwahiyo Elly na Erica mdogo wote ni watoto wa Derrick maana mtoto wangu mimi ni Elly”
“Uwiii sijakuelewa hata jambo moja ulilonieleza Sia”
“Hujanielewa kivipi? Ushahidi pia ninao kuwa mimi na baba yako tulibadilisha watoto”
“Mlibadilisha wakiwa na umri gani?”
“Miezi mitatu kasoro”
“Mbona wanangu walipomaliza mwezi tu niliondoka nao na mama yao tukaenda Afrika kusini na tulirudi huko baada ya miaka mitatu, unajua sikuelewi kabisa”
“Nitakuletea ushahidi basi, mimi sio chizi kusema kila siku kuwa Erick ni mtoto wangu. Ila ndio hivyo mkeo alikusaliti huyo ndiomana imekuwa hivyo”
“Nenda tu Sia, ila mke wangu awe alinisaliti au hakunisaliti bado nitampenda hadi mwisho wa maisha yangu”
“Duh!! Ni mzima kweli wewe?”
“Ni mzima kabisa, nilishasema hata nimfumanie hapo mke wangu basi nitamsamehe maana nampenda sana”
“Mmmmh!! Shukuru Mungu mkeo hana hayo mambo siku hizi”
“Ndiomana nimemuoa kwnai najua sio mwanamke wa kutangatanga tangu zamani”
“Sio wa kutangatanga wapi, angetembea na ukoo mzima huyo! Unamtetea tu”
“Alikuwa akitafuta penzi la kweli ila mke wangu katulia sana na nina mpenda sana, hakuna kinachoweza kututengenisha”
“Ngoja nikapekue vizuri ule ushahidi nikuletee”
Sia aliamua kuondoka zake maana aliona hakuna ushirikiano wowote kwa baba Angel ila alimuahidi kumletea ushahidi kwa yale aliyoyasema.

Baba Angel siku hii baada ya maneno ya Sia, aliamua kupitia dukani kumnunulia mkewe zawadi, kwnai yale maneno ya Sia yalimuingia sikio la kushoto na kutokea sikio la kulia, alienda moja kwa moja kwenye duka ambalo huwa ananunua na leo alimkuta baba Emma na kufurahi kwani alijua kuwa atamchagulia kitu ambacho mke wake atakipenda sana.
Alipofika pale tu baba Emma alimuonyesha zawadi ya kumpelekea mke wake,
“Leo mpelekee tu hiki kikoi nina uhakika atakipenda sana”
“Mmmh atapenda kikoi mke wangu kweli!”
“Kweli atakipenda sana, ni kizuri hiki hakuna mwanamke ambaye atakiona na kukichukia”
Basi baba Angel alimchukulia mkewe kile kikoi na moja kwa moja kurudi zake nyumbani kwa mke wake.
Leo alipofika tu ndani moja kwa moja alimuonyesha mke wake ile zawadi aliyomchukulia, kwakweli mama Angel alifurahi sana na kumwambia mume wake,
“Ulijuaje kama nataka kikoi jamani mume wangu? Kweli wewe ni kiboko yangu. Nimependa sana hiki kikoi mume wangu, asante sana.”
Muda wote mama Angel alikuwa akikitazama tu kile kikoi ilionyesha ni jinsi gani amekipenda kile kikoi.

Usiku wa siku hii, Erica alienda moja kwa moja chumbani kwa kaka yake Erick na kuanza kuongea nae kuhusu kile alichosikia kuhusu Sarah,
“Umesikia hayo yaliyopo huko”
“Mmmh umeanza Erica, mambo gani hayo?”
“Kumbe Sarah alikuwa na mimba kwahiyo imetoka”
“Mmmh alikuwa na mimba!! Jamani, Sarah kapata wapi mimba?”
“Kapata wapi? Kwani wewe hujui mimba inapatikanaje?”
Erick alimuangalia nduguye bila ya kumjibu kitu na kuamua kuanza kumueleza mambo mengine,
“Hivi zile karata siku hizi unacheza mwenyewe? Leo nije tucheze wote?”
“Hapana, leo sichezi karata”
“Kwanini?”
“Subiri baada ya siku tatu ndio nitacheza karata”
“Kwanini?”
“Siri yangu, usiku mwema”
Kisha Erica aliondoka zake na kumuacha Erick pale akimshangaa tu na kujiuliza kwanini Erica kasema vile kuhusu kucheza karata mpaka baada ya siku tatu, hakumuelewa kwakweli.

Leo Erick alipokuwa shuleni aliamua kumuuliza Elly kuhusu Sarah kwani ni kweli hakuonekana shuleni, basi alikaa nae na kuanza kumuuliza,
“Vipi Sarah anaendeleaje?”
“Kheee mbona umeniuliza mimi!”
“Nasikia anaumwa, na wewe ulisema kuwa upo nae karibu”
“Ndio anaumwa, ila twende ukamuone sio kuniuliza uliza maana hilo sio jukumu langu”
“Duh!! Basi tutaenda badae baada ya masomo”
Walirudi darasani na kuendelea na masomo kama kawaida, ila vipindi vilivyoisha, Elly alimkumbusha tena Erick swala la kwenda kumuona Sarah, ni kweli Erick alikubali na moja kwa moja kuondoka na Elly kuelekea nyumbani kwakina Sarah.
Walipofika, walimkuta Sarah yupo chumbani, basi Siku alienda kumuita na kumwamnbia kuwa,
“Erick kaja kukuona”
“Oooh mwambie aje kuniona chumbani”
Ikabidi Siku ampelekee ujumbe ule Erick, na muda ule Erick na Elly waliingia pamoja chumbani kwa Sarah ila Sarah aliomba kuzungumza na Erick kwahiyo alihitaji Elly asubirie kwanza, na Elly alifanya vile basi Erick alianza kuzungumza nae,
“Kwani ni kitu gani kinakusumbua Sarah?”
“Najua mama yako ameshakwambia”
“Kaniambia kuhusu nini?”
“Kuwa nilikuwa na mimba na hiyo mimba imetoka”
Erick akashtuka kidogo maana hizi habari alizipata kwa Erica ila hakuziamini moja kwa moja, ila muhusika alipomuhakikishia alishangaa sana na kumuuliza kwa makini,
“Sarah unazungumzia nini?”
“Kwani hujanisikia au hujanielewa? Ndio kama ulivyoambiwa kuwa nilipata mimba na imetoka”
“Ulipataje mimba Sarah?”
“Kwani mimba inapatikanaje?”
Sarah alianza kucheka tena alicheka sana na kusema,
“Erick usiniambie hujui hata mimba inapatikanaje?”
“Wewe ni mtoto mdogo sana Sarah! Unajua kama ulichokifanya sio sawa kabisa”
“Sio sawa kitu gani, kuna mtu ambaye huwa hafanyi mapenzi?”
Erick aliona ni vyema abadilishe mada na kuanza mada zingine kwahiyo alianza kumpa pole tu maana aliona kama angeendelea na mada ile basi ingekuwa ni ngumu sana kuelewana na Sarah,
“Pole sana Sarah”
“Ila haya yote umeyataka wewe Erick”
“Kivipi sasa?”
“Wewe ndio chanzo cha mimi kupata mimba na wewe ndio chanzo cha mimi kuchoma sindano na mwisho wa siku ile mimba ikatoka kabisa”
“Unaongelea nini wewe? Unadhani mimi naweza kufanya huo upuuzi? Kwanza hiyo kwangu ni dhambi”
“Dhambi unaijua wewe! Yani hata usijitetee kwa lolote, maana wewe ndio chanzo cha kila kitu”
“Duh!! Kwaheri”
Erick hakuweza kukaa zaidi, basi aliinuka na kutoka kabisa, aliwaaga na kuondoka zake kwani hata hakumuelewa Sarah na wala hakutaka kumuelewa. Muda huu aliingia Elly chumbani kwa Sarah na kuanza kuongea nae,
“Ulikuwa unaongea nini na Erick?”
“Nilikuwa namwambia ukweli kuwa mimi nilikuwa na mimba na imetoka ndio alikuwa akishangaa kuwa mimba nimeitoa wapi, yani huyu Erick huwa anaongea kama sio mwanaume vile”
“Mmmh usiseme hivyo, mimi naogopa mama akijua ukweli maana atanifukuza hapa”
“Kwa usalama wako nishakwambia usiondoke kabisa mahali hapa yani endelea kuishi hapa hapa sababu ukiondoka tu basi niotasema ukweli wa mambo ulivyo”
“Mmmmh hata nikiwepo, ukikazaniwa na mama yako hutonitaja!”
“Subiri wakikazana kuniuliza kuna kitu nitakifanya, tulia tu”
“Mmmh kitu gani Sarah?”
“Wewe tulia tu, utaona itakavyokuwa”
Basi Elly alimuangalia tu Sarah bila ya kusema kitu kingine chochote kile.
 
SEHEMU YA 356

Erick alirudi nyumbani kwao, na mtu wa kwanza kumuuliza kwanini kachelewa alikuwa ni Erica,
“Mbona leo umechelewa sana Erick, ulipita wapi?”
“Khaaa Erica nawe, nilipita kumuangalia Sarah”
Mama Angel akasikia na kumuuliza Erick vizuri,
“Eeeeh Sarah anaendeleaje?”
“Anaendelea vizuri mama”
“Unajua anachoumwa?”
“Hapana, kasema homa tu”
Erick aliogopa kusema kwani aliona hayo mambo kama ya kikubwa sana kuongelewa na yeye, basi mamake nae hakumuhoji zaidi.

Usiku wa leo mama Angel aliongea na mume wake kuhusu mtoto Sarah yani alijikuta akitamani sana kujua ukweli wa kuhusu mtoto huyu,
“Kwakweli mume wangu natamani sana kujua vingi kuhusu Sarah”
“Kwanini au kwavile umesikia kuwa ni shangazi yako?”
“Yani sijui kwanini? Natamani kujua vingi, halafu roho inaniuma sana kuona kaharibikiwa, najua tukiujua ukweli basi tutaweza kumlea na tutakuwa na uhuru nae tofauti na sasa ambavyo mama yake kamshikilia”
“Fatilia kwanza ujue ni nani alimpa mimba nadhani ndio mengine utayafahamu”
“Yani huyo mjinga wa kumdanganya Sara nikimjua dah sijui hata nitamfanya nini jamani!! Yule mtoto nampenda sana, hata sijui kwanini mama yake katokea kuwa Manka jamani, yani mimi yule Manka huwa sivutiwi nae kabisa haswaa yale maneno yake ya kujiona ni bora kushinda wengine. Sijui kwanini mtoto bora kama Sarah kumpata mama kama Manka”
“Ndio mama yake sasa, utafanya nini wewe?”
“Ila kesho nitaenda, najua Sarah nikiongea nae vizuri ataniambia mengi sana, natamani sana Sarah akae katika mstari ulionyooka”
“Haya, mimi hata sijishughulishi kwa hilo”
Baba Angel hakutaka kujifanya anashughulika sana na mambo yale kwani mkewe alimfahamu vizuri sana kuwa atamgeuka tu na kusema anashughulika vile sababu ya mama Sarah, kwahiyo yeye akajiepusha kabisa.
Basi moja kwa moja waliamua kulala tu kwa muda huo.

Leo Mama Sarah alikaa nje na mwanae huku akiongea nae mawili matatu kuhusu kile kilichomtokea,
“Eti mwanangu Sarah niambie jamani, nani muhusika wa yote hayo? Nafanya hivi kwaajili yako mwanangu”
“Kwani unataka kumfanya nini huyo muhusika mama?”
“Hakuna kitu ila nataka nikufundishe, najua Sarah mwanangu huelewi vizuri kuhusu mapenzi ndiomana imefikia hatua ya kufanya hivyo, sasa watu wote wamejua kuwa mimi sio mleaji mzuri ni bora ningekugundua mimi mwenyewe kuliko lile kundi lililokugundua kuhusu hili, hadi napata aibu”
“Sasa mama, niache kuona mimi aibu uone wewe mama yangu jamani!!”
Muda huo alifika mama Angel na kuwakuta pale nje, basi aliwasalimia pale na kuungana nao pale nje huku akimpa pole Sarah kwa yale yaliyomkuta na kumuuliza,
“Kwanza Sarah ni nani aliyekwambia kuhusu kwenda kuchoma sindano ya uzazi wa mpango?”
“Tulifundishwa shuleni njia za kuzuia mimba, na mchumba angu hakutaka nipate mimba kwa kipindi hiki wakati nasoma ndio tukashauriana nikachome sindano”
Mama Angel alipumua kwanza maana alikuwa kama haelewi vile, alimuangalia vizuri Sarah na kumuuliza,
“Kwani Sarah unamchumba?”
“Ndio ninaye na wote mnamfahamu”
Mama Angel na mama Sarah waliangaliana na kujikuta wakiuliza kwa pamoja,
“Nani huyo?”
Sarah alicheka na kusema,
“Ni Erick”
Yani mama Angel alihisi kama moyo wake ukipasuka kusikia kuwa mwanae ndio muhusika wa matendo yale.

Mama Angel alipumua kwanza maana alikuwa kama haelewi vile, alimuangalia vizuri Sarah na kumuuliza,
“Kwani Sarah unamchumba?”
“Ndio ninaye na wote mnamfahamu”
Mama Angel na mama Sarah waliangaliana na kujikuta wakiuliza kwa pamoja,
“Nani huyo?”
Sarah alicheka na kusema,
“Ni Erick”
Yani mama Angel alihisi kama moyo wake ukipasuka kusikia kuwa mwanae ndio muhusika wa matendo yale.
Alimuangalia vizuri Sarah na kumuuliza tena,
“Huyo Erick ni Erick mwanangu mimi au ni yupi?”
“Ndio huyo huyo”
“Kwahiyo ndio aliyekupa mimba, na ndio aliyekushauri kuhusu uzazi wa mpango?”
“Ndio, na hata jana kaja kuniona”
Halafu Sarah akainuka zake na kwenda ndani, kwahiyo alimuacha mama yake pale na mama Angel wakitazamana bila ya jibu, ni mama Sarah ndiye aliyeanza kuongea,
“Mbona makubwa haya, unajua Erick na Sarah ni ndugu!”
“Ni kosa lako Manka, kwanini hukutaka mtoto aujue ukweli? Hebu ona mambo kama haya kweli! Yani haijalishi Sarah ni mtoto wa mzee Jimmy au Derrick bado ni ndugu kwa Erick maana aaaarghh hata sijui nisemeje”
“Ila mwanao ana tabia mbaya jamani, kujifanya mpole vile kumbe kaanza mambo mabaya. Haya Manka hajui kulea mtoto, na wewe je umeleaje huyo wako?”
“Sikia nikwambie, hii ni ajali tu kama ajali zingine ila hata hivyo bado hainiingii akilini kabisa, mwanangu Erick namfahamu vizuri sana, hawezi kufanya kitu cha namna hii, kwanza Erick alikuwa akimuheshimu sana Sarah”
“Watoto wa kiume ni wa kuwakatalia basi!! Hebu nenda kaongee vizuri na kijana wako, mimi hizi habari zimenichanganya kwakweli, halafu tujue cha kufanya maana Erick na Sarah ni ndugu”
Mama Angel pia alihisi kama akili yake kwa muda huo haifanyi kazi vizuri, basi aliamua kuaga na kuondoka zake.

Leo usiku wakati baba Angel katoka kazini, mkewe aliamua kuongea nae chumbani kuhusu vile Sarah alivyosema, ila baba Angel alicheka kidogo hadi mkewe akamuuliza,
“Sasa unacheka nini? Ni habari ya kuchekesha hiyo?”
“Hapana, ila nimetambua kuwa mwanangu ni mwanaume rijali”
“Khaaa sikutegemea kama utafurahia huu ujinga baba Angel jamani, huu ni urijali au ujinga? Kwahiyo umefurahi kwa mtoto kurithi tabia mbaya kama hii? Halafu kaa ukijua kuwa Erick na Sarah ni ndugu”
“Hapana mke wangu sijafurahia kiivyo, ila nilichocheka ni kuwa alichokifanya Sarah ni sawa na alichokifanya Daima, yani hapo ni wazi kuwa Erick kasingiziwa”
“Kasingiziwa vipi wakati hata wewe ndio ilikuwa tabia yako hii!”
“Ni kweli mimi sikuwa kijana safi hata kidogo tena nilikuwa msumbufu sana, natakiwa nisishangae sana kuhusu kijana wangu kuwa hivyo maana nitaishia kusema tu amerithi kwangu ila nakataa hiyo kitu asilimia mia moja kwa kijana wangu Erick, nakataa kabisa mwanangu hajafanya hiko kitu hata kidogo. Huyo Sarah kafanya kitu kama alichokifanya Daima tu, ila huyo Sarah sijajua lengo lake nini ila mwanangu Erick hawezi kufanya kitu cha namna hiyo”
“Mmmh ila mimi nitamuuliza tu Erick, na hivi kesho ni mapumziko basi nitamuuliza Erick”
Baba Angel wala hakubisha sana alimuacha mkewe afanye vile atakavyotaka.

Kulipokucha leo, Erick na Erica walitoka nje na kuanza kufanya usafi wa nyumba yao, walisafisha ndani na kisha kwenda kusafisha nje ya nyumba yao, wakati Erick akikatakata maua, Erica alikuwa akikusanya yale majani ya maua na kuyaweka sehemu moja, muda huu baba yao alitoka nje na kuwakuta watoto wake wakiendelea na ile kazi kwakweli alifurahi sana na kuwaambia,
“Kwakweli watoto wangu mnajituma sana, hadi nahisi fahari kuwa nanyi, leo jioni nikirudi mjiandae maana nitaenda nanyi kutembea kidogo”
Erick na Erica walifurahi na kumuitikia baba yao, kisha baba yao pale aliwaaga na kuondoka zake, kwakweli alikuwa akijihisi ufahari sana kupata watoto wanaopenda kujituma kama wale.
Mama Angel nae alitoka nje kabisa muda huu na kukuta ndio wamemalizia ule usafi waliokuwa wakifanya,
“Oooh watoto wangu mmefanya kazi kubwa sana, nitamuita yule kijana aje tu kuyabeba hayo matakataka akayatupe, kwakweli watoto wangu mananifurahisha sana. Ila mkitoka kunywa chai nina maongezi kidogo na wewe Erick”
Erick aliitikia tu ila hakujua kuwa ni maongezi gani ambayo mama yake alikuwa nayo juu yake, basi waliingia ndani na moja kwa moja kwenda kuoga maana hata kuoga walikuwa hawajaoga, walipomaliza ndio walienda kunywa chai huku Erica akimwambia Erick,
“Natamani na mimi nikasikilize hayo maongezi ya wewe na mama”
“Khaaaa Erica jamani, unajua una mambo ya ajabu sana, sasa maongezi ya kwangu halafu unataka ukayasikilize kweli!!”
“Ndio, natamani kujua ni kitu gani yani roho inaniuma kweli kwa kutokujua. Basi nikuombe kitu Erick ukishaongea na mama naomba unihadithie ni kitu gani”
“Haya, baba si kasema tutaenda kutembea? Basi nitakuhadithia huko”
Yani Erica alitamani sana mama yao aseme hayo maongezi na yeye akayasikilize kuwa yanahusu nini.
Erick alipomaliza kunywa chai moja kwa moja alimfata mama yake ili aweze kuongea nae, ila mama Angel alimtambua mwanae vizuri, alimwambia asubiri kwanza atamuita mwenyewe, alitaka kwanza chai aliyokunywa imshuke maana hasira za mwanae alizitambua fika zilivyo, haswaaa kitu cha kusingiziwa huwa hapendi kabisa.

Kwenye mida ya mchana, mama Angel alimuita Erick kwenye bustani yao na kuanza kuzungumza nae kuhusu madai ya Sarah,
“Kwanza mwanangu samahani, ile juzi ulienda kumuona Sarah kwanini?”
“Mmmh mama! Ni vile niliambiwa Sarah anaumwa, nilimuuliza Elly akasema kwanini nisiende kumuona ndio nikaenda kumuona”
“Unajua anaumwa nini Sarah?”
“Mimi sijui mama”
“Hajakwambia chochote?”
“Mmmmh hajaniambia”
“Basi Sarah alikuwa mjamzito na hiyo mimba imetoka”
Erick alijifanya kushtuka kwani hakutaka kumuonyesha mama yake kuwa anafahamu hizo habari, basi mama Angel aliendelea kusema,
“Mimba ya Sarah imetoka sababu alienda kuchoma sindano ya uzazi wa mpango. Nilienda jana kumuuliza vizuri kuwa ni nani aliyempeleka kuchoma sindano ya uzazi wa mpango na ni nani muhusika wa mimba iliyotoka, akakutaja wewe”
Hapa ndio Erick alishtuka zaidi na kumuuliza kwa makini mama yake,
“Kanitaja mimi?”
“Ndio, mwanangu Erick naomba uniambie ukweli unajua mimi ni mama yako. Niambie ukweli tafadhari usinifiche”
“Mama, nakwambia ukweli wa moyo wangu. Mimi sijawahi kufanya hayo mambo kabisa, na hata hivyo nakumbuka uliniambia kuwa Sarah ni ndugu yangu, nawezaje kufanya huo ujinga nae!”
“Nimekuelewa mwanangu hata usijifikirie vibaya wala nini, nimekuelewa vizuri sana mwanangu. Naomba usifikirie vibaya, nilitaka tu ukweli na ushanipa ukweli, naomba usifikirie kuhusu hilo”
Kisha mama Angel aliachana na Erick kwani hakutaka kumlazimisha zaidi mtoto wake kwa kitu alichokataa kabisa kukifahamu. Kisha mama Angel aliamua kwenda kuendelea na mambo yake mengine.

Mama Sarah alijiandaa na kuondoka nyumbani kwake, maana alipanga kukutana na Rahim ili aweze kuongea nae kuhusu ya nyumbani kwake,
“Mwanangu Sarah nikuletee nini?”
“Hapana mama, hata sitaki chochote”
“Mmmh mwanangu jamani!!”
“Labda chokleti”
Basi akaagana nae na kuondoka zake, moja kwa moja alienda kukutana na Rahim kama ambavyo alipanga kukutana nae na kuanza kuongea nae,
“Yani binti yangu ana matatizo, sijui alipata mimba halafu akaenda kuchoma sindano ya uzazi wa mpango na ile mimba ikatoka”
“Ila watoto wa siku hizi wabunifu”
“Ubunifu wao nini sasa?”
“Hajataka shida, kaenda kujichomea sindano na mimba ikatoka, hapo katumia elfu mbili au elfu tatu maana alivyozidiwa mmeshughulika nae wenyewe”
“Sio ubunifu ule ni ujinga”
“Kwahiyo binti yako mjinga?”
“Ndio ni mjinga, ni kweli zile sindano zina uwezo mkubwa sana wa kutoa mimba ila mara nyingine ile mimba inaweza isotoke na kukupa shida sana na ukazaa mtoto asiyeeleweka mwanzo wala mwisho, au mara nyingine mimba ikatoka na kukusababishia matatizo makubwa sana. Ndiomana ni vyema mtu kwenda hospitali na kutumia njia nzuri ambazo madaktari wanatumia katika kutoa mimba”
“Kwahiyo unasapoti utoaji wa mimba?”
“Hapana, sisapoti hata kidogo. Kwanza roho inaniuma sana kuhusu mwanangu, tumempana kasema mimba kapewa na Erick”
“Erick yupi?”
Mama Sarah akaanza kumueleza Rahim kuhusu huyo Erick bila ya kujua kuwa Rahim anaielewa hiyo familia vizuri sana, basi Rahim akasema,
“Unachukua uamuzi gani?”
“Sijui nifanyeje sasa”
“Nipeleke nikaongee na binti yako, nataka niongee nae kama baba anavyoongea na mwanae”
Mama Sarah aliona kuwa ni sawa, basi akakubaliana nae na kuondoka mahali hapo kuelekea moja kwa moja nyumbani kwa mama Sarah.

Jioni hii ya leo, baba Angel alivyorudi nyumbani tu aliwataka watoto wake wajiandae kwaajili ya kwenda kutembea nao kwa muda huo.
Walijiandaa na kutoka na baba yao, moja kwa moja walienda ufukweni na kuanza kufurahi huku kwahiyo Erick na Erica walikuwa wakirushiana rushiana maji, muda huu baba Angel akamuona Steve akiwa ameongozana na kijana mwingine, basi aliwasogelea na kuwasalimia, ambapo Steve alimtambulisha yule kijana kwa baba Angel,
“Huyu anaitwa Paul, ni mtoto wa madam Oliva”
Basi baba Angel alisalimiana na mtoto yule pale na kuongea mawili matatu, kisha alimvuta Steve kwa pembeni na kumuuliza,
“Kwani madam Oliva ulizaa nae?”
“Hapana”
“Mbona huyu mtoto ni wewe mtupu?”
“Duniani wawili wawili, hata mimi huwa sielewi ni kwanini nimefanana hivi na huyu mtoto”
“Steve sikia nikwambie kitu hiki, huyu ni mtoto wako, yani ni mtoto wako kabisa napata hisi a hizo kuwa huyu Paul ni mtoto wako”
“Khaaa jamani, mimi na Oliva tumefahamiana rasmi mwaka huu, sasa tutoe wapi mtoto mkubwa hivi! Ila mimi mwenyewe huwa namuangalia sana huyu mtoto na huwa namuona kama mwanangu mzazi kabisa, yani najiona ni wazi kuwa mimi ni baba Paul”
“Duh!! Kwlei dunia ina mambo hii, yani mtoto kakuranda kila kitu, Steve chunguza vizuri ila huyu ni mwanao”
“Sasa nichunguze nini? Mama halali wa huyu mtoto sijawa nae kwa kipindi hiko, nimekuwa nae kwa kipindi hiki, je huyo itawezekanaje kuwa mwanangu?”
Baba Angel hakutaka kuongea zaidi ila bado alihisi kwa upana zaidi kuwa yule mtoto ni mtoto wa Steve. Waliongea kidogo pale na kuagana, halafu baba Angel aliwafata watoto wake ambao walikuwa wakichezea chezea maji na kuwataka kwa muda huo waweze kwenda kula sasa.

Mama Sarah alifika na Rahim nyumbani kwake, na kumkuta Sarah yupo tu nyumbani kama alivyomkuta, kisha Rahim alitaka kutoka nje ya nyumba na kuzungumza na yule mtoto, ambapo ilikuwa hivyo alitoka nae na kuanza kuzungumza nae,
“Unajua madhara ya kutoa mimba?”
“Sijui sema mimi sikupanga kutoa mimba yani imetokea tu bahati mbaya, sikupanga kitu cha namna hiyo”
“Ila ulipanga kubeba mimba?”
“Hapana sikupanga, mimi bado mdogo mimi ni mwanafunzi”
“Unasikitisha Sarah, unajua wewe ni binti mdogo sana. Huwa mambo ya kijinga namna hiyo yanafanywa na mabinti walioshindikana kwa wazazi wao, unakuta binti hajulikani popote wala lolote ndio hufikia hiyo hatua. Haya ni nani kidume aliyekudanganya yote hayo?”
“Ni Erick”
Rahim alimuangalia vizuri Sarah na kumuuliza tena,
“Ni nani?”
“Ni Erick”
Rahim akamuangalia tena na kumwambia,
“Hebu Sarah niangalie machoni”
Sarah akafanya hivyo kwa muda na kushusha macho yak echini, Rahim akashtuka kidogo na kusema,
“Basi, nakusihi tu upende masomo achana na mambo ya mapenzi yatakuharibu akili yako”
Rahim aliinuka na kumuita mama Sarah kisha akamwambia,
“Kuna kitu nimekigundua kuhusu binti yako”
“Kitu gani hiko?”
“Aaaah sijui hata nikwambiaje, ila kuna kitu sielewi sijui ni hisia zangu sijui ni nini?”
“Kitu gani?”
“Nimewahi kumuona binti mmoja mwenye macho kama Sarah miaka mingi iliyopita, sitaki kumuongelea binti huyo kwasasa, ila kuna tatizo kwa binti yako. Kaa nae vizuri, mfundishe kama mama, binti yako ni muelewa sana muelekeze vizuri atakuelewa”
“Unajua sikuelewi Rahim, kwani ni kitu gani umegundua kwa Sarah”
“Aaaah unajua mimi nina mahusiano na wewe!! Si vizuri kwakweli”
“Si vizuri nini? Sikuelewi”
“Ila naomba namba ya huyo mamake Erick”
Mama Sarah alimpatia Rahim namba ila bado hakumuelewa, Rahim aliaga na kuondoka na kumuacha mama Sarah akiwa haelewi chochote kile kilichoongelewa na Rahim, alienda kumuuliza binti yake moja kwa moja kitu ambacho alikuwa akizungumza na Rahim ila Sarah alimueleza tu vitu vya kawaida hata alishangaa ni kwanini Rahim kasema vile.

Wakati baba Angel na watoto wake wanarudi nyumbani, walikutana njiani na Sia, na yule Sia ndio aliliona gari la baba Angel kwani alilisimamisha ikabidi baba Angel ashuke kumsikiliza kuwa anasemaje,
“Yale niliyokwambia umeyafanyia kazi?”
“Yapi hayo?”
“Kuhusu Elly na Derrick na kuhusu Erick na mimi”
Baba Angel akakumbuka kitu na kujikuta akiunganisha matukio,
“Tena umenikumbusha kitu, hivi si ulisema kuwa wewe ulibadilishana na baba yangu watoto?”
“Ndio, na alinilipa kufanya hivyo. Sikutaka ila umasikini ndipo umepelekea haya”
“Kwahiyo hujui mwanao alipo?”
“Sijui kivipi wakati mwanangu ni Erick!”
“Erick sio mwanao, yani nakataa kabisa. Ila tusiandikie mate wakati wino upo. Mimi nitakupelekea wewe na Erick hospitali mkapime damu, najitolea kulipa kila kitu halafu tukipata majibu ndio utajua kuwa mtoto wako yuko wapi”
“Mmmmh unamaanisha nini?”
“Unajua katika maisha kuna ujinga mtu unaufanya ila hufikirii kuwa ujinga huo utakufanya nini badae, unaona sawa tu kufanya ujinga ulioufanya, mimi nina kuhakikishia kabisa Erick sio mtoto wako”
“Mmmmh!! Haya nipo tayari kwenda kupima nae”
“Kwenye ukweli, uongo hujitenga. Kesho tutaondoka wote ila usimwambie chochote Erick kuwa tunaenda kupima nini, tutamchukua tu damu halafu nitakuita nawe uchukuliwe damu, ikipimwa ndio nadhani utaweza kujiongeza sasa kuwa mwanao yuko wapi? Uache tamaa za kijinga, umasikini usiwe chanzo cha ujinga, kwaheri”
Baba Angel alimuacha Sia akijiuliza vitu vingi sana bila ya jibu lolote lile.

Usiku wa leo, baba Angel anaamua kuongea na mama Angel kuhusu kuonana kwake na Steve akiwa ameongozana na mtoto Paul,
“Yani yule mtoto ni moja kwa moja ni mtoto wa Steve, niliwahi kumuuliza Steve aliniambia kuwa yeye mtoto aliyezaa na Sia tu ndio aliamini kuwa ni mtoto wake. Sijawahi kuongea na Oliva ila napata hisia kuwa yule ndio mtoto wa Steve”
“Mmmmh mbona makubwa haya”
Halafu baba Angel alimuelezea mama Angel vile ambavyo Sia alimsimulia na jinsi alivyomwambia,
“Unajua Sia anakazana bado kusema Erick ni mwanae, mimi najua tu kuwa sio ukweli. Naenda kuvunja nae mzizi wa fitini kwa kupima damu yake na damu ya Erick kesho”
“Bora iwe hivyo maana anakera sana yule”
“Ila mimi nina hisia mbaya sana toka nimuone Steve na yule mtoto, nahisi yule mtoto wa madam Oliva ndio mtoto wa Sia na Steve”
“Kheeee basi itakuwa Elly ni mtoto wa madam Oliva na Derrick, ila imekuwaje hiyo?”
“Kumbe madam Oliva alizaa na Derrick?”
“Ndio hivyo”
“Basi itakuwa ni kweli maana kwa maelezo ya Sia ni kuwa alibadilisha watoto, kwahiyo kuna uwezekano mkubwa sana kuwa hao watoto walibadilishana”
“Mmmmh inawezekanaje?”
“Nasikia baba yangu ndio alifanya huo mchezo mzima, sijui ni kwanini alifanya hivyo, au baada ya kukosa mtoto wangu ndio akafanya hivyo sielewi, kuna siri kubwa sana kwa huyu mzee”
“Inatakiwa basi tumtafute bi.Aisha atakuwa anafahamu mambo mengi sana”
Mara simu ya mama Angel ilianza kuita, ikabidi aipokee simu ile na kuanza kuongea nayo,
“Rahim anaongea hapa”
“Kheee unataka nini?”
“Sikia, hebu jifunze kulea watoto basi unaachiaje watoto hadi wanaenda kupena mimba? Umewezaje kutokumfunza vyema huyo Erick mdogo?”
“Hapana, mwanangu si muhusika wa mambo hayo”
“Unamkatalia ulikuwa nae? Au unagtembea nae kila mahali?”
“Hapana, namfahamu vyema mwanangu, hana tabia hiyo”
“Hivi Erica unawezaje kukataa hilo, ikiwa baba na mama mmeoana ila wote mnafanana tabia, watoto je watakuwaje eeeh!”
“Kwani wewe shida yako nini, nishakwambia mwanangu hahusiki. Nakata simu sasa hivi”
“Hapana, usikate simu hata mimi najua kuwa mwano hahusiki na kitu chochote ila naomba nikupe kazi ndogo”
“Kazi gani?”
“Nenda kazungumze na Sarah, halafu ukiwa unaongea nae muangalie kwenye macho yake ndio utagundua ukweli wake na uongo wake”
“Kwahiyo wewe umeongea nae?”
“Nimekupa hiyo kazi, nilikuwa nakutisha tu kuhusu mwanao, namfahamu vizuri sana mwanao Erick, ni rafiki yangu mzuri tu naelewa wazi kuwa hawezi kutenda jambo hili. Kuna watoto hata ukiwaangalia unawahisi wanaweza kufanya lolote ila sio kwa mtoto kama Erick, mchunguze Sarah na utaweza kufahamu mambo mengi sana”
“Haya nitafanya hivyo asante”
Alikata simu ila kwa muda huu hakumueleza mumewe kitu alichokuwa akiongea wala baba Angel nae hakumuuliza mkewe kitu alichokuwa akikiongea kwenye simu.

Kulipokucha tu, wanafanya mambo yao mengine na kuamua kwenda Kanisani ila Vaileth anadai kuwa hayupo kwenye hali nzuri kwa siku hiyo, kwahiyo wote wanaondoke na yeye anabaki mwenyewe.
Muda kidogo tu alifika Junior pale nyumbani na kufurahi sana,
“Kwanza nimefurahi kwa yule jini kisirani kuondoka”
“Mjinga sana yule binti”
“Halafu unajua ubaya alioufanya? Kamsingizia baba kuwa anataka kumbaka”
“Khaaaa mjinga sana yule Daima”
Basi wakainuka na kwenda chumbani, ila Vaileth akakumbuka kuwa bado hajafunga milango, ndio akarudi sebleni ile anataka kufunga tu mlango akaingia mama Junior, ikabidi asalimiane nae pale na mama Junior akakaa pale sebleni,
“Yani sijakuta mtu eeeh!”
“Hawapo ndio wote wameenda Kanisani”
“Hawa watu nao kujifanya wanapenda sana Ibada hadi kero jamani, ila nitawasubiri hapa mpaka warudi”
Vaileth alitulia kimya kwani aliona ni jinsi gani swala lake linaharibika kwa muda huo, akakaa nae kidogo tu na kumwambia,
“Mama, samahani nataka niende kuoga”
“Kheee kumbe hujaoga? Mbona umejipodoa kabisa?”
Vaileth akajichekesha kidogo na kusema,
“Mwanamke kupendeza mama, si huwa mnasema hivyo sio nionekane mchafu tu muda wote”
“Mimi sikujua kama hujaoga, haya nenda kaoge”
Vaileth alienda chumbani kwake na kufunga mlango, na kuongea kidogo na Junior,
“Mama yako kaja Junior, balaa leo na kasema haondoki hadi warudi”
“Duh huyu mama nae sijui ana matatizo gani, sasa anataka nini tena?”
“Hapa nimekuja tu nimemdanganya kuwa naenda kuoga”
“Haya, itabidi leo tukaoge wote yani kashaniharibia tayari huyu mama”
Junior hakupenda kabisa kwa uwepo wa mama yake mahali hapo kwa wakati huo.

Leo Sarah alimgomea Elly kutoka kabisa kwahiyo Elly alibaki na Sarah nyumbani tu kwa siku hiyo, na walikaa nje pamoja huku wakiongea ongea,
“Unajua mimi nilishazoea kwa mama kwenda kwenye Ibada”
“Sasa unaenda kufanya nini kwenye Ibada na hizi dhambi tulizofanya?”
“Mmmh dhambi gani?”
“Inamaana hujui? Uzinzi ni dhambi halafu sisi tumefanya uzinzi, nimepata mimba nje ya ndoa, nayo ni dhambi. Tumeenda pamoja kuchoma sindano ya uzazi wa mpango na kusababisha mimba itoke kwahiyo tumefanya dhambi ya mauaji maana kutoa mimba ni uuaji, halafu tumesema uongo”
“Mmmh uongo gani tena?”
“Mimi nilimwambia mama Erick kuwa Erick ndio muhusika wa kila kitu”
Yani Elly hadi alihisi kupaliwa kabisa na kumwambia Sarah,
“Mbona unanizidishia dhambi jamani, huo uongo mimi nimeusema muda gani?”
“Mimi na wewe tumekuwa mwili mmoja, kwahiyo nikisema mimi uongo ni sawa na umesema wewe”
“Duh!!Sijategemea kusikia neno kama hilo”
“Ndio hivyo, mimi na wewe si tutaoana eti!!”
“Duh!! Sarah!”
Elly alihisi tena kukohoa na akaamua kwenda ndani kuchukua maji ya kunywa.

Ibada ilipoisha, walitoka ila mama Angel alihitaji kwenda kumuona Sarah kwani alitaka atomize ile azma ya kuongea nae kwa siku hiyo, kwahiyo aliwataka wale warudi nyumbani na mtoto, baba Angel aliongea nae kidogo tu,
“Nitarudi nao na kutoka kidogo na Erick kwa ile niliyokwambia jana”
“Oooh nakumbuka vizuri, haya mimi ngoja iende”
Mama Angel aliwaacha wale wameondoka kurudi nyumbani halafu yeye alianza safari ya kwenda kwa mama Sarah kama alivyopanga.
Mama Angel alivyofika alimkuta Sarah pale nje na moja kwa moja kwenda kuongea nae, na alipomuuliza kuhusu aliyempa mimba bado alikazana kuwa ni Erick,
“Una uhakika na hilo Sarah? Mbona Erick kakataa kabisa?”
“Anakataa tu ila ndio yeye”
“Hebu niangalie machoni Sarah”
Basi alianza kutazamana na Sarah, na alipomuangalia vizuri alishtuka pia, na kumwambia,
“Unajua Sarah tumefanana sana macho, yani tumefanana sana, sikugundua jambo hili ndio nagundua leo. Hupendi kutazama machoni Sraah sababu unaongea uongo, ila kaa ukijua kuwa wewe na huyo Erick ni ndugu”
“Mmmh ndugu kivipi?”
“Sarah, mimi ni shangazi yako. Yani hapa hakuna ubishi hata kidogo, kwa mfanano huu! Mimi ni shangazi yako Sarah, usimwambie ukweli mama yako ila nitakuja kukuchukua na kukupeleka kwa baba yako. Niambie ukweli Sarah, nani muhusika wa yote”
“Ni Erick”
Sarah akainuka na kwenda ndani kwani hakutaka kuongea sana, basi Sarah alivyoenda ndani ikabidi mama Angel nae ainuke ili aondoke ila nyuma aliitwa,
“Mama Erica”
Mama Angel alisimama na kugeuka nyuma, akamuona aliyemuita kuwa ni Elly, kisha alimsogelea mama Angel na kumkumbatia kisha akamwambia,
“Naomba msamaha, naomba niokolewe kwenye dhambi hii”
“Dhambi gani?”
“Sio Erick aliyehusika, ni mimi”
Mama Angel alimuangalia Elly na kumshangaa

Mama Angel alisimama na kugeuka nyuma, akamuona aliyemuita kuwa ni Elly, kisha alimsogelea mama Angel na kumkumbatia kisha akamwambia,
“Naomba msamaha, naomba niokolewe kwenye dhambi hii”
“Dhambi gani?”
“Sio Erick aliyehusika, ni mimi”
Mama Angel alimuangalia Elly na kumshangaa.
Kwakweli mama Angel alipenda kuongea zaidi na Elly, alimuomba asogee nae mahali ili waweze kuongea, nae Elly alikubali kwani alitaka kuisafisha dhamira yake.
Walipanda pamoja kwenye gari ya mama Angel na kuelekea sehemu ambayo kuna mgahawa kisha walishuka hapo kwani mama Angel alitaka kumsikiliza vizuri Elly,
“Eeeeh nieleze sasa, maana hata sijakuelewa, kwahiyo muhusika ni wewe?”
“Ndio ni mimi, namaanisha kuwa ni mimi ndiye nilimpa mimba Sarah, na ni mimi ndiye niliyeenda na Sarah mpaka kwenye kituo ambacho alichoma sindano ya uzazi wa mpango”
“Kheee hebu nielezee vizuri kwanza, ilikuwaje hadi ikawa hivyo Elly?”
“Sijui nikwambiaje yani, ila kwa kifupi ni umasikini ndio umesababisha haya”
“Hebu nielezee vizuri Elly?”
Yani Elly hakumficha kitu chochote, alianza kumueleza mama Angel toka siku ya kwanza ambayo alianza kushawishiwa na Sarah na hadi walipoenda kuchoma sindano,
“Mimi sikujua kama ana mimba, na tulinunua hadi kipimo cha mimba ila nilikuwa naogopa kweli kama akipima na kugundulika kuwa ana mimba itakuwaje? Siku ile uliyonikuta na kwenda nami hospitali kule ndio siku ile niliyoenda na Sarah kumsindikiza kwaajili ya kuchoma sindano na alisema kuwa tukifika kule niseme kuwa mimi ni mdogo wake ili yeye anaonekane mkubwa”
“Duh! Yani nimesikitika sana, unajua kitu gani?”
“Nini?”
“Wewe na Sarah ni ndugu”
Elly akashtuka ila aliikataa ile kauli,
“Haiwezekani”
“Ndio hivyo Elly usikatae, yule Derrick wa siku ile ndio baba yenu”
“Mmmh haiwezekani, sijui kama yule anaweza kuwa baba yangu, mbona mama amekataa jambo hilo”
“Tulia bado nafanya utafiti ila nitakuja na jibu zuri tu, sasa kuna kitu Elly. Ukiendelea kukaa kule lazima Sarah ataendelea kukusumbua”
“Tena sio Sarah peke yake, bali hata yule mdada wao wa kazi ananisumbua sana”
“Kheee hadi yule Siku anakusumbua?”
“Ndio, nimewahi kulala nae mara moja”
Mama Angel akaona hili ni tatizo tena ni tatizo sana, basi alimuomba kitu Elly,
“Naomba turudi wote nyumbani kwangu, naomba ukaishi kwangu kwanza”
“Mmmh naogopa maana mamake Sarah ndio anayenisomesha mimi”
“Hata mimi ninao uwezo wa kukusomesha Elly kuliko hiyo fedheha unayoipata, nakuomba ukubali. Halafu kesho tutaenda wote kwa yule baba wa siku ile pamoja na Sarah, tutaenda kumfata”
“Kwahiyo kesho nisiende shule?”
“Ndio kwa kesho itabidi tu usiende shule, najisikia kuweka sawa haya mambo kwanza, nimeumia sana moyo kwa hayo maelezo yako Elly, kama mama nimeumia sana”
Elly alikubali kuondoka nae, kwahiyo kwa muda huo yeye na Elly waliondoka kuelekea nyumbani kwake.
 
SEHEMU YA 358

Erick, Elly na Erica walijiandaa kwaajili ya kuondoka, ila gari walilotaka kutumia Erick aligundua kuwa halina mafuta ya kutosha, ila kwake

hilo halikuwa tatizo sana, aliondoka na wenzie na kupitia kituo cha mafuta ambacho baba yake huwa mara nyingine anaweka mafuta kwa

bili na kuwaambia hapo wamuwekee mafuta. Nao walifanya vile, ila yule mdada wa kwenye kituo cha mafuta alimuita Erick pembeni kidogo

na kuongea nae,
“Erick, siku nyingine ukija hapa ulizia Rose basi mimi nitakuja na kukuwekea mafuta”
“Oooh sawa, hakuna tatizo”
“Ila ungenipa na namba zako Erick”
Sababu Erick hakuwa na simu, basi alimpa namba ya simu ya mezani ya nyumbani kwao na kuagana nae.
Moja kwa moja walienda kwakina Sarah, na walimkuta Sarah sebleni ambae aliwakaribisha vizuri tu ila hakupenda kwa kumuona Erick na

Elly pamoja na Erica kufika pale kwapamoja, alikaa nao kidogo sebleni akiongea nao ila Erica alionekana kusinzia na mwisho wa siku alilala

kabisa pale kwenye kochi, muda huo Sarah alimuomba Erick na Elly akaongee nao nje kidogo, walitoka na kuanza mazungumzo,
“Sijapenda mmekuja wote, ila nimefurahi mmefika ili niweze kuzungumza ya moyoni. Kwanza kabisa Erick naomba unisamehe maana ukweli

utakuwa umeujua ndiomana Elly ameondoka kwetu. Halafu kitendo cha Elly kuondoka kwetu sijafurahishwa nacho kabisa kwani inaonekana

kama mimi nakulazimisha kufanya mambo mengine”
“Aaaah Sarah hujanielewa tu, ila hapa kwenu nimeondoka kwasababu nyingi sana”
“Haya niambie ni sababu gani iliyokufanya ukimbie nyumbani kwetu, je mama yangu ni tatizo kwako? Nimekufichia aibu kwa mama, na hata

akigundua basi nitamueleza ukweli wote bila hata ya kumficha”
“Aaaah Sarah jamani acha maneno kama hayo, haya sasa tunaongelea nini kwa wakati huu?”
Mara walishangaa kumuona Erica akitoka pale nje huku akiwa anathema, wote kwa pamoja walimuuliza,
“Tatizo nini Erica?”
“Nimeota vibaya sana?”
“Umeota nini?”
Erica alinyamaza kimya kidogo na kusema,
“Sijui kama nilichoota ni cha kweli ila naomba mnisamehe kama kitawakwaza, sema nahitaji kusema ili kama ni kweli basi huyu mtu apone”
“Sema basi, umeota kitu gani?”
“Samahanini, mimi simfahamu vizuri huyu dada wa kazi humu ndani, ila nimekaa pale kwenye kochi nikasinzia nikajiwa na ndoto kuwa yule

dada alikuwa mjamzito”
Wote waliangaliana, tena Elly ndio akashtuka zaidi maana alianza kuhisi vibaya muda huo, alihisi huenda hata Sarah akajua kuwa

alitembea na huyo dada, ila Sarah alimuuliza Erica,
“Mmmh Erica, sasa tumsaidiaje maana unasema hiyo ndoto unatusimulia ili tuweze kumsaidia”
“Nimeota kuwa hiyo mimba imetoka, sema inatoka vipande vipande na inamsumbua sana, yani anaumwa. Nimeota kuwa huyu mdada

apelekwe hospitali maana akikawia anaweza kupoteza maisha maana anazidi kupoteza damu”
“Mmmh Erica wewe jamani, tuko nae hapa siku zote hatujui hayo”
“Mimi sijui ila nimeota tu”
Basi Erick alikumbuka yale ya kutoka mimba ya Daima, aliamua kumwambia Sarah kuwa akamuulize huyo dada yake,
“Ngoja nikamuulize ila siku tatu hizi kapooza sana, hayupo kama zamani. Mara nyingi anakimbilia chumbani, sikujua tatizo ni nini”
“Aaaah sasa nilivyoota mimi kuwa anaumwa sana, ana hali mbaya sana”
Basi Sarah aliamua kwenda kumuangalia Siku, na kweli alikuwa yupo chumbani, Sarah aliingia na kumkuta akigalagala chini kuwa anaumwa

sana,
“Tatizo ni nini dada?”
“Sijui mdogo wangu, naumwa sana”
“Umeanza lini kuumwa?”
“Toka juzi ila leo imezidi, naumwa sana Sarah. Naumwa mimi, nadhani nitakufa mimi”
Sarah alisikia harufu ya damu mule chumbani na kugundua maneno ya Erica kuwa huenda ikawa kweli maana inaonyesha huyu dada

ametokwa na damu nyingi sana, basi aliwaomba wakina Erick na kuanza kumkongoja na kuingia nae kwenye gari na kwenda nae hospitali.

Walifika hospitali walitakiwa waandike kadi na vipimo vya awali, yani Erica alijikuta ile elfu ishirini ikimtoka maana kwa pale walipokuwepo

hakuna hata aliyekuwa na pesa ya kufanya chochote kile.
Kisha Sarah alimpigia simu mama yake ili kumpa taarifa ya pale hospitali,
“Tupo hospitali mama”
“Kwani kuna nini?”
Sarah alimsimulia mama yake kile walichoambiwa na Erica na mpaka kumpeleka pale hospitali, basi mama Sarah aliahidi kwenda pale

hospitali ili kuona kinachoendelea ni kitu gani.
Walikaa pembeni wakijadiliana maana hakuna aliyejua tatizo linalomsumbua ni nini, ila Sarah akasema,
“Mmmh inaonekana wewe ni noma sana Erica, khaaa nimekuogopa kwakweli. Inakuwaje unaota ndoto zinazotokea?”
“Hata mimi sijui kabisa inakuwaje ila hizi ndoto huwa zinanijia mara nyingi tu, na kama ni ndoto ya kusema hapo basi nasema hapo hapo.

Kuna kipindi niliacha kuota ndoto za namna hii ila nashangaa kwa jana zimeanza tena”
“Ila ni vizuri maana huyu dada angeendelea kuugulia ndani tu, halafu mimi sijaenda kutoa pesa sijui leo ingekuwaje bila ya wewe kuwa na

hela”
Mama Sarah alifika mahali pale na kwenda moja kwa moja kuongea na daktari, na kuelewana nae kuwa wamfanyie kila kitu maana gharama

zote atazilipa mwenyewe, halafu akarudi kuongea na hawa vijana wake. Ila alipomuona Erick alichukia sana kwani bado alikuwa na ile

dhana kuwa Erick ndio kaharibu fikra za Sarah, alisogea na kumzaba vibao Erick.
Kitu ambacho mama Sarah hakukijua ni kuwa Erick ni mtu ambaye huwa na hasira sana, wakati anamzaba vile vibao, Erick alikuwa akikunja

ngumi yake kwaajili ya kumpiga nayo mama Sarah, yani ni Erica ndio alimuona na kumuwahi Erick ule mkono huku akimsihi waondoke,
“Nakuomba Erick twende nyumbani, nakuomba sana”
Mama Sarah nae aligundua hili kwani alimuona Erick usoni akiwa hadi amesimamisha mishipa ya sura, kwahiyo aliamua kusogea nyuma

kabisa na kwenda mbali nao. Erick alimuangalia Erica, ila kwa leo alimsikiliza na moja kwa moja kwenda kwenye gari, basi Erica na Elly

walimfata nyuma na kuondoka nae ila wakiwa kwenye gari Erick alikuwa haongei kitu, yani alikuwa akiendesha gari huku machozi yakimtoka

maana bado alikuwa na hasira, hadi Erica alimuomba Erick aweke gari pembeni na kuanza kuongea nae,
“Sasa Erick ndugu yangu, hasira za nini kiasi hiko jamani eeeh!! Naomba ufurahi na mimi basi, yule mmama si tumeshamuacha pale?

Nakuomba Erick shusha hasira zako”
Basi Erica alifanya kazi ya kumfuta yale machozi, yani hata Elly aliweza kugundua ni kiasi gani Erick alikuwa ni mtu mwenye hasira sana.

Basi mama Sarah alimsogelea mwanae na kuongea nae kuhusu ugonjwa wa Siku na zile hasira za Erick, ila alianza kuongea nae kuhusu

hasira za Erick,
“Kwahiyo mwanangu Sarah kabisa ndio ukampenda mtu kama huyu?”
“Kwani ana tatizo gani mama?”
“Khaaa mwanaume wa hasira hivyo hafai kabisa mwanangu, mbona unaweza kulia na mtu kama huyo jamani. Unawezaje kuishi na mtu

kama huyo? Hebu fikiria mimi kumnasa kibao tu kabadilisha ile sura yake, mishipa imemtoka usoni balaa halafu kakunja na ngumi, khaaa

huyu Erick hapana aiseee hata hafanani na babake jamani”
“Unamfahamu vizuri yule baba yake mama? Labda nae alikuwa vile ujanani?”
“Namfahamu vizuri sana, ana hasira ila sio za namna ile kabisa. Yule Erick nimemfananisha na mkaka mmoja hivi, loh alikuwa akichukia

unaweza kulia, ila nasikia kaoa mke mpole sana, ndio inavyotakiwa kwa mtu mwenye hasira kiasi hiki, aaah hafai huyu mtoto tena hafai

kabisa”
“Mmmmh mama”
“Haya tuachane na hayo, huyu dada yako nae mtu mzima kwenda kufanya mambo ya kitoto kama uliyoyafanya wewe ndio nini?”
“Mambo gani mama?”
“Kumbe lilipata mimba halafu nalo likaenda kuchoma sindano ya uzazi wa mpango, si kunitia gharama tu jamani, leo hatotoka huyu ndio

atabaki hapa hapa hospitali nasikia kapoteza damu nyingi sana huyu mjinga kabisa. Anataka anifie ndani halafu mimi jopate lawama kwa

ndugu! Hii ndio shida ya msichana wa kazi kukuzoea sana basi anakupanda hadi kichwani kama huyu alivyofanya kwangu”
“Kwahiyo mama utamrudisha kwao”
“Mmmmh nimemzoea sana, halafu nilishasema nitaishi nae hadi atakapooelewa, unajua huyu Siku ni mtoto wa ndugu yangu kabisa!!

Ndiomana huwa namuamini sana ila kumbe akili zake ni finyu kama zako”
Basi mama Sarah alienda tena kuongea na daktari kisha aliamua kurudi nyumbani tu na Sarah maana waliambiwa kuwa Siku anatakiwa

kubaki pale hospitali kwaajili ya kumuangalia kwa karibu zaidi.
Kufika nyumbani ndio mama Sarah alichoka, aliingia jikoni na kukuta vyombo havikuoshwa wala nini,
“Khaaa huyu mjinga kumbe hakuosha vyombo jamani, hili sufurua si limepikiwa tambi juzi loh!”
“Kumbe tangu juzi alikuwa akiumwa mama”
“Kheee basi na humu ndani hakuna usafi uliofanyika, jamani kuwa na kazi nyingi napo loh!! Hata sijagundua hiki kitu, mlikula nini sasa

jana?”
“Aaaah mimi nilimuagiza yule dereva wa bodaboda atuletee chips ile jioni maana nilikuwa na njaa halafu dada alisema anaona uvivu kupika”
“Khaaa ndio masahani ya chips haya hapa, mweeeh jamani uchafu gani huu lakini! Na leo nimechoka sana wala siwezi kufanya chochote,

twende tu mahali tukale huko halafu nitajua cha kufanya nikirudi”
Ikabidi wajiandae kwa muda huo na kwenda kula kwenye mgahawa.

Leo usiku, mama Angel aliamua kumueleza baba Angel kile ambacho amezungumza na madam Oliva, hapo ndio baba Angel nae alipata

picha na kusema,
“Oooh hapo kuna uwezekano mkubwa sana kuwa madam Oliva alibadilishiwa mtoto, nina hisi tulichokuwa tunahisi ni kweli kuwa Elly ni

mtoto wa madam Oliva halafu yule mtoto wa madam Oliva ni mtoto wa Sia”
“Haya mambo jamani, ila mzee Jimmy kwanini afanye kitu cha namna hiyo? Kwani ana ugomvi gani na madam Oliva mpaka ambadilishie

mtoto?”
“Mmmh hapo sijui kitu, ila kwakweli kama baba yangu kafanya hiko kitu ni mbaya sana. Kesho nahitaji kwenda kaburini kwa baba mara

moja”
“Mmmmh unaenda kufanya nini? Twende wote basi”
“Hapana, wewe nenda Kanisani na watoto halafu mimi nitaenda huko. Kuna vitu nahitaji kuwauliza wale walinzi wa lile eneo, yani kuna kitu

kinanijia kichwani”
“Kitu gani?”
“Nitakwambia nikirudi, ila baba yangu kama alifanya hivyo kwa kudhamiria kwakweli hakufanya sawa kabisa”
Basi waliamua tu kulala kwa muda huo.

Kulipokucha tu, asubuhi na mapema, baba Angel alijiandaa na kuondoka zake kuelekea kwenye eneo ambalo kulikuwa na kaburi la mzee

Jimmy, maana yule mzee alizikwa kwenye eneo lake mwenyewe.
Basi baba Angel alifika pale, na kusogea karibu na kaburi la baba yake ila gafla alishikwa bega, alipogeuka nyuma alishangaa sana

kumuona bi.Aisha, basi bila hata salamu alimuuliza jambo moja kwanza,
“Nilipanga kuja kuongea na wewe, ila nilipokuona na Sia nikaishiwa nguvu kabisa ya kuja kukuona. Sia ashakwambia yaliyomkuta?’
“Kaniambia ndio, kuwa mtoto aliyefikiria ni wake, kakuta sio wake tena. Ila sijashangaa sana”
“Kwanini?”
“Kwani mzee Jimmy alikuwa na uwezo wa kufanya chochote alichojisikia na yote aliyafanya akiwa na maana nayo thabiti kabisa”
“Sasa alikuwa na maana gani kufanya kitu cha namna hiyo?”
“Unashangaa hayo tu, je ukigundua alichokufanya wewe kwa watoto wako utafanyaje?”
Baba Angel alimuangalia vizuri huyu bibi yani alikuwa kama hajamsikia vizuri

Basi baba Angel alifika pale, na kusogea karibu na kaburi la baba yake ila gafla alishikwa bega, alipogeuka nyuma alishangaa sana

kumuona bi.Aisha, basi bila hata salamu alimuuliza jambo moja kwanza,
“Nilipanga kuja kuongea na wewe, ila nilipokuona na Sia nikaishiwa nguvu kabisa ya kuja kukuona. Sia ashakwambia yaliyomkuta?’
“Kaniambia ndio, kuwa mtoto aliyefikiria ni wake, kakuta sio wake tena. Ila sijashangaa sana”
“Kwanini?”
“Kwani mzee Jimmy alikuwa na uwezo wa kufanya chochote alichojisikia na yote aliyafanya akiwa na maana nayo thabiti kabisa”
“Sasa alikuwa na maana gani kufanya kitu cha namna hiyo?”
“Unashangaa hayo tu, je ukigundua alichokufanya wewe kwa watoto wako utafanyaje?”
Baba Angel alimuangalia vizuri huyu bibi yani alikuwa kama hajamsikia vizuri vile.
Ikabidi baba Angel amuulize tena,
“Unasemaje?”
“Kwani hujanisikia Erick? Ukigundua alichofanya baba yako kwa watoto wako utafanyaje?”
“Kwani kafanya kitu gani?”
“Niliwahi kumdokezea mke wako, na nilimwambia kuwa asifike huku mwenyewe, ila nina haraka kidogo. Tuondoke kwanza eneo hili na

nitakwambia kwa kifupi tu”
Kwakweli baba Angel alijikuta akitamani kufahamu ni kitu gani haswaa ambacho kimeendelea kwa familia yake, akaondoka na huyu bibi.

Akapanda nae kwenye gari na kwenda kwenye eneo moja ambalo palikuwa na mgahawa na kuagiza vinywaji halafu wakaanza kuongea,

basi bi.Aisha akamwambia,
“Hebu kunywa kwanza hiko kinywaji maana tunaweza kuondoka hapa na hujanywa hata kidogo”
Baba Angel alihisi hata moyo wake kwenda mbio sana, akamuangalia huyu bibi na kumwambia,
“Naomba ieleze”
“Kunywa kwanza hiko kinywaji chako”
Baba Angel alikunywa kidogo na kuanza kumsikiliza huyu bibi,
“Kwanza kabisa, mimi na baba yako tumefahamiana kwenye harusi yako, nilialikwa na mtu mmoja hivi. Basi nikafahamina na baba yako,

katika maongezi ya mimi na yeye tuligunduana kuwa wote ni waathirika, basi aliniambia kuwa kama nipo tayari anioe, nikakubali na tulifunga

ndoa bomani. Kama ujuavyo, babako hakuwahi kuoa kwahiyo mimi ndio nilikuwa mke wake wa kwanza. Niliishi na baba yako ila niligundua

vitu vingi sana, ngoja nikwambie baadhi ya vitu hivyo. Hebu kunywa kwanza kinywaji chako ushushie na pumzi ndefu”
Kwakweli baba Angel aliona huyu bibi akizidi kumchanganya tu kwani yeye alihitaji kugundua ukweli, aliamua kunywa kile kinywaji ili

kumridhisha yule bibi,
“Ni hivi, kuna mwanamke alikuwa akiitwa Ester, mwanamke huyu alipendwa sana sana na baba yako, yani hiyo ndio ilikuwa ndoto yake, ila

hakuweza kuwa na mwanamke huyu na mpaka mwisho hakuweza. Ila baba yako alitokea kumpenda sana mwanamke mwingine, na huyu si

mwingine bali ni mke wako Erica, yani alitamani kufanya chochote kwaajili ya mke wako Erica, ile harusi yenu ameigharamikia sio sababu

yako ila ni sababu ya mke wako Erica, yani alimpenda sna. Na usifikiri baada ya wewe kuoanana Erica basi baba yako aliacha kumfatilia

Erica! Hapana, yani ndio alikuwa akimfatilia sana, ila mkeo najua hajawahi kukwambia haya sababu hakutaka ujihisi vibaya kwa baba yako.

Kuna siku hata alitaka kumbaka, najua mkeo hajawahi kukueleza jambo hili”
Baba Angel alipumua kidogo huku akiendelea kumsikiliza bi.Aisha,
“Sasa ule upendo wa kumpenda Erica na kumuona yupo na wewe ulimuumiza sana, na alipanga kufanya kitu cha kukufanya wewe ujute na

hata Erica ajute katika maisha yake”
“Kitu gani hiko?”
“Upo tayari kukisikia?”
“Ndio nipo tayari”
“Haya, kunywa tena kinywaji chako”
Kwakweli baba Angel alikuwa hamuelewi kabisa huyu bibi aliona kama anamchanganyia mada tu, basi akamwambia,
“Naomba uniambie tu, hizo habari za kusema kila muda ninywe kinywaji nashindwa kukuelewa kabisa”
“Ila wewe ni mbishi sana hata baba yako aliwahi kunilalamikia sababu hiyo, hivyo basi sitokwambia yote”
Baba Angel alikuwa akitamani hata kumzaba vibao huyu bibi ili aongee haraka ila alitakiwa tu kuwa mpole na kumsikiliza,
“Ni hivi, ni kweli kabisa baba yako alibadilisha watoto na mpango wake ulikuwa ni kubadilisha mtoto wa mke wako pamoja na mtoto wa Sia,

ila sijui nini kilitokea hapo maana hata yeye alilalamika kuwa kuna kitu kimekwama katika mipango yake, kwahiyo sijui kipi kilifanikiwa na

kipi kilikwama. Ila uhakika nilionao ni kuwa kuna sindano ya ajabu sana walichomwa watoto wako mapacha wakiwa wachanga kabisa”
“Unamaanisha Erica na Erick?”
“Kwani una watoto wengine mapacha zaidi ya hao?”
“Ni hao tu, inamaana kuna sindano aliwachoma wanangu baada ya kushindwa kuwabadilisha?”
“Kuhusu kuwabadilisha nisikuhakikishie maana sina uhakika sana kama alishindwa ila tu alilalamika kuwa hajafanya vile alivyotaka. Kitu cha

kusikia kuwa ameenda kuwachoma sindano watoto wako, niliumia sana na ndio ugomvi wa mimi na yeye ulipoanza”
“Kwahiyo hizo sindano aliwachoma za nini na ilikuwa ni kipindi gani?”
“Sikia, mtafute yule daktari wa ile hospitali. Yule daktari mkubwa yule mwenye jina kama la baba yako, anaitwa dokta Jimmy, ndio

anayeweza kukueleza kuhusu hiyo sindano”
“Duh!! Niambie vyote ili nijue cha kufanya”
“Nenda kafanyie kazi hilo ndio unitafute, sio ukiniona na Sia unadhani mimi ni msaliti, hata Sia sio msaliti wako ila baba yako ndio alikuwa

msaliti wako”
Yani baba Angel hata hakutaka kuongea zaidi, kwani kwa muda huo huo, alimuaga yule bi.Aisha na kuondoka zake kuanza safari ya

kuelekea nyumbani kwake.

Tumaini leo alivyotoka tu kwenye Ibada, moja kwa moja alienda nyumbani kwa mama Sarah kwani alihisi kuwa kuna mengi ya yeye

kuzungumza na huyu mwanamke, basi alifika pale na kumkuta mama Sarah nje ya nyumba huku akiosha vyombo,
“Kheeee naona mwanamke kujituma”
“Kujituma wapi? Mdada wangu wa kazi anaumwa, kwahiyo hii shughuli imeniangukia mwenyewe”
“Ila na nyie mnayataka, mpo wangapi ndani hadi umeosha vyombo vingi hivi!!”
“Mmmh toka majuzi hivi vyombo ndiomana unaviona vingi na hapa ndio namalizia, vilikuwa vingi sana. Nimechokaje hapa”
“Pole sana, ndio umama huo. Jikaze tu”
“Yani acha tu, umeona nguo zilivyojaa kwenye kamba hizo! Nilikuwa nafua ndiomana nimechoka sana”
“Duh pole, kwahiyo umezifua leo?”
“Ndio, asubuhi nimeamkia hizo nguo ujue, nilipomaliza ndio nikasafisha ndani halafu muda huu ndio naosha vyombo, nimechokaje hapa”
“Kwani Sarah hayupo?”
“Yupo ndani, saizi nadhani atakuwa anaangalia muvi”
“Kheeee hivi wewe ukoje? Si Sarah angeosha hivyo vyombo!”
“Weeee Sarah aoshe vyombo!! Hajawahi si atavitoa na mafuta!”
“Nalea watoto kijinga ila wewe mwenzangu umezidi, mtoto hata kuosha chombo hajui! Hapana hayo sio malezi kabisa, unamuharibu mtoto

sio kumpenda. Nilikusema siku ile, haya tukaja mtoto alipata mimba sijui kachoma sindano ya uzazi wa mpango, unafikiri hayo mambo

kayajulia wapi Sarah? Unafikiri ni wapi amepata ushawishi? Hayo masimu unayomuachia hayo”
Tumaini siku ile ilikuwa kama amepanga kumsema mama Sarah maana alimsema sana kwa ulezi mbaya wa mtoto wake.
Baada ya yale mambo sasa ndio Tumaini alikuwa akiongea nae vizuri,
“Hebu niweke wazi, Sarah ni mtoto wa nani?”
“Ngoja nikwambie ukweli, Sarah ni mtoto wa mzee Jimmy”
“Aaaah acha uongo wako bhana, baba nilikuwa namtambua vizuri, baba alikuwa na matatizo ya kizazi. Kama ulimsingizia sawa, mimi nipo

hapa kutaka kujua tu kama mtoto ni wa Erick na sio vinginevyo”
“Mtoto ni wa mzee Jimmy, kama unabisha sawa ila huyu ni mtoto wake”
“Kwahiyo wewe ulizaa na baba yetu?”
“Ndio, na huyu ndio mtoto mwenyewe”
“Haya nimekuelewa, unaweza kunipa mdogo wangu nikamlee kwa wiki mbili tu!”
“Hata siku mbili siwezi kukupatia, mimi niliapa kwa mzee Jimmy, kuwa sitokuja kumtesa huyu mtoto, sitokuja kumpiga wala kumfanya

chochote. Baba yake alipenda kumuona huyu mtoto kama yai na ndio niliapa kumlea hivyo Sarah”
Kwakweli yale maneno bado hayakumuingia akili kabisa Tumaini, aliondoka lakini alijihisi wazi kutokuelewa chochote kile.

Leo Sia anaenda moja kwa moja nyumbani kwa mama Angel maana na yeye alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, basi aliongea pale na

mama Angel kidogo na kumwambia,
“Naomba niitie Elly hata niongee nae kidogo tu”
Mama Angel aliamua kumuita Elly ambapo Sia alitoka nae nje na kuanza kuongea nae,
“Elly mwanangu, tatizo nini hadi umeondoka kule kwenye msaada?”
“Hata hawa wameahidi kunisaidia mama”
“Na mbona hujarudi nyumbani? Naomba kwa leo twende nyumbani tu mwanangu”
Elly alimuangalia mama yake ambaye alionyesha sura ya huruma sana kwa siku hiyo, kwahiyo ilibidi tu akubali na moja kwa moja kwenda

kumuaga mama Angel kuwa anaondoka na mama yake mara moja.
Wala mama Angel hakumkatalia jambo hilo, basi Elly aliondoka na mama yake huyu, wakiwa njiani Sia alianza kumuuliza mwanae,
“Hivi mwanangu kwa mfano akatokea mtu na kukwambia huyu sio mama yako mzazi, ni amekulea tu lakini sio mama yako mzazi

utafanyaje?”
“Kwanza nitamshangaa sana halafu nitaona amechanganyikiwa huyo mtu”
“Sasa utafanyaje? Utanikataa kuwa sio mama yako tena au utafanyaje?”
“Mama, haiwezekani kitu kama hiko. Wewe ndio mama yangu, hakuna kitu cha kusema wewe sio mama yangu”
Basi Sia alitamani amwambie ukweli ila aliogopa kwani huyu mtoto alishamzoea sana kama mwanae wa kumzaa tu.

Usiku wa leo, baba Angel alikuwa na mawazo sana, alifikiria sana vile alivyoongea na bi.Aisha, basi alimsimulia mkewe kila kitu ambacho

mama Angel anashangaa kiasi kwani huyu bibi alishawahi kumuelezea. Basi baba Angel akamuuliza mkewe,
“Ni kweli baba yangu aliwahi kutaka kukubaka?”
“Ndio ni kweli”
“Na mbona hukuniambia?”
“Mmmh sikutaka kukugombanisha na baba yako”
“Hebu nidokezee ilikuwaje maana hata sijaelewa kabisa”
“Nikiwa na mimba kubwa sana ya hawa mapacha, nakumbuka siku hiyo baba yako alikupigia simu kuwa twende kumsalimia, ila tulivyofika

pale tu akakutuma wewe kwenye ofisi gani sijui. Kwahiyo ndani nilibaki mimi na yeye tu maana mkewe alikuwa katoka kidogo, sijui alikuwa

akitafuta nini chumbani, akaniita ili nikamsaidie, sikujiuliza sana nilienda, uwiii mzee Jimmy alibamiza mlango na kutaka kuniingilia kimwili

kwanguvu tena bila kujali mimba niliyobeba, nakumbuka yule mkewe bi.Aisha ndio alikuja kunisaidia ili mzee Jimmy asinibake”
“Ila kwanini hukuniambia jamani Erica?”
“Sikuweza kwakweli kukwambia chochote kile, ningewagombanisha mapema sana, nami sikutaka kitu cha namna hiyo”
“Nasikia baba yangu alikuwa akikusumbua sana. Unajua yani vitu vingine nafikiria na kukosa jibu kabisa, baba nae anaumia kabisa moyo

wake kwa kukuona mimi na wewe kweli? Yani kuna vitu nafikiria na kuvikosea jibu kabisa”
“Kwanza kule kwenye kaburi, yule bibi alinikataza kabisa yani kuwa nisiende peke yangu. Kwahiyo kuna makubwa tu yapo hapo katikati”
Kiukweli mama Angel alikuwa akiongea tu ila aliona kuna kila sababu ya kuchunguza mambo yote yale, waliamua kulala tu kwa muda huo.

Asubuhi ya leo kulipokucha, mama Sarah alichelewa kumuamsha mwanae kwaajili ya kwenda shule na kumwambia,
“Oooooh kumbe Siku huwa anafanya kazi kubwa sana humu ndani, hivi kweli Sarah umeshindwa kuamka mwenyewe na kuwahi shule

mwanangu?”
“Aaaah mama, sijui imekuwaje ila nitaenda tu hakuna tatizo”
Sarah alienda kujiandaa na kuchukua hela kwa mama yake maana alisema kuwa atatumia usafiri wa kukodi siku hiyo ili aweze kuwahi

shule.
Ila Sarah alipoondoka pale hakwenda shule wala nini, moja kwa moja alienda nyumbani kwa mama Erica ambapo alimkuta amejiandaa

anataka kutoka ila alipomuona alimshangaa klidogo,
“Kumbe Sarah?”
“Eeeeh ndio mimi”
Basi mama Angel akasalimiana nae pale na kukaa nae kidogo huku akimuuliza kilichompeleka kwa muda ule,
“Naomba unisamehe kwa yote, labda unaujua ukweli au huujui ila naomba unisamehe nipo kwako kukiri”
“Nini tena?”
Mama Angel alitoka nae nje na kwenda nae kwenye bustani yao ili aweze kuwa huru katika kuelezea yanayomsibu, basi Sarah alimueleza

kila kitu mpaka swala la yeye kuanza kutembea na Elly, yani hakuacha kitu chochote,
“Kwanini ulikuwa ukifanya hivyo sasa Sarah?”
“Kiukweli, nilijikuta nikimpenda sana Erick, yani sana na kila nilipomwambia hakuonekana kunielewa kabisa. Mama alinifunza kuwa

nikimpenda mtu basi nimwambie moja kwa moja, na mimi nilimpenda sana nikajikuta nikimwambia ila Erick hakutaka. Sasa simu yangu hii

nina marafiki wengi sana, wakubwa kwa wadogo, kuna siku walinitumia video zilinisisimua sana na wakanielekeza zinapopatikana kwenye

mitandao, na hata mikanda yake wakaniletea, nilikuwa nikiangalia nasisimka sana. Kuna kipindi nikaanza na mimi kutamani kufanya

kamavile wanavyofanya kwenye video ila tatizo ni kuwa sina ukaribu na watoto wa kiume. Mama alipomleta Elly nyumbani nilifurahi sana,

naye nilimuonyesha hizi video na kujikuta tukiwa wote”
Kwakweli mama Angel alisikitika sana, na kumuhurumia Sarah kisha akamwambia,
“Pole sana binti yangu maana huwa nakuona wewe kama mwanangu kabisa vile, pole sana. Ila Elly ni ndugu yako hata Erick ni ndugu yako,

usinibishie maana huu ndio ukweli, mama yako hataki tu kukwambia ukweli ila huu ndio ukweli mwanangu. Hebu niambie kwasasa

unajihisije?”
“Yani mama, sijui nikwambiaje, ni kama nimeathirika hivi na hizi video, siwezi kulala bila kuziangalia, halafu muda mwingi natamani Elly awe

karibu yangu hata nifanye nae tu ndio niridhike na moyo wangu. Kwakweli nipo kwenye wakati mgumu sana, dada hayupo imefanya leo

nichelewe kwenda shule maana nimechelewa kuamka, nilimwambia mama kuwa nitaenda ila nimekuja huku, nikiamini unaweza kunisaidia

maana akili yangu haipo sawa, hata unaniambia Elly ni ndugu yangu sikuelewi kwa chochote wala kwa lolote”
“Dah pole sana”
Mama Angel alifikiria kidogo, ingawa alikuwa na safari zingine ila aliona ni bora ampeleke mtoto huyo kwenye maombi, akamkumbuka yule

mama aliyekuwa akifanya maombi basi alimwambia Sarah kwa muda huo waondoke na waelekee huko.
 
SEHEMU YA 360

Jioni ya leo, mama Angel alirudi toka sehemu aliyokuwa ameelekea, kwa kiasi Fulani alikuwa amechoka sana, basi akaanza kuongea na

Vaileth kuhusu mambo yaliyoendelea hapo nyumbani.
“Vipi habari a hapa? Hajasumbua leo Ester?”
“Hapana, leo alikuwa kimya tu”
Basi mama Angel akaenda chumbani ambako mwanae alikuwa amelala, sema kwa muda huu mama Angel alijihisi kuchoka sana kutokana

na mizinguko ya siku hii.
Alikuwa akipekua kitu kwenye kabati lake na ikaanguka picha ya Angel alipokuwa mtoto, basi mama Angel aliishika ile picha huku

akitabasamu na kusema,
“Mwanangu Angel, nakumbuka kipindi ulipokuwa mtoto, ulikuwa ukinifurahisha sana, muda mwingi ulitumia kuwa na mimi ila siku hizi

hakuna kabisa mambo ya kuwa karibu na mama”
Muda kidogo baba Angel nae alikuwa kawasili, basi mama Angel akaongea na mumewe,
“Nimemkumbuka Angel jamani, nimemkumbuka sana”
“Hata salamu mke wangu!”
Mama Angel alicheka kidogo na kuanza kusalimia mumewe, basi baba Angel akasema,
“Karibu shule itafungwa, atarudi nyumbani kwa kipindi hiki sio kama ile likizo aliyokaa kwa bibi yake. Atarudi nyumbani moja kwa moja,

hakuna tatizo”
“Ila miaka inaenda sana, nakumbuka kipindi hiko tukiishi mimi, wewe na Angel tu hata hatukufikiria kama tutakuwa na watoto wengine

jamani, ila Angel ni maisha yangu ujue”
“Naelewa ndio, na Angel ndiye aliyetuunganisha tena mimi na wewe. Najua bila kuzaa wewe, ungeendelea tu kushikwa akili na wengine na

kukuumiza tu moyo wako maana hawakufahamu vizuri kama mimi ninavyokufahamu na akili zako”
Mama Angel alicheka tu, ila ni kweli mumewe alimfahamu sana ndiomana aliweza kuishi nae kwa muda mrefu sana.

Usiku wa siku hiyo, Vaileth alikaa chumbani kwake huku akiwaza sana kuwa afanye kitu gani, hakupata jibu kabisa, aliwaza kuhusu ile

mimba ila uhakika wa kweli kuwa ana mimba hakuwa nao. Akakumbuka njia ya kupima mimba aliyoambiwa na bibi yake, akasema kuwa

ataifanya kesho yake asubuhi maana mkojo wa asubuhi ulikuwa rahisi sana kukufanya ugundue kuwa una ujauzito au la.
Muda huu aliamua kulala ila alikuwa na mawazo mengi sana hadi alihisi usingizi kutowe, palipokucha tu alienda jikoni na kuchukua chumvi

na vikopo vyake, kisha alienda tena chumbani kwake na kupima ule mkojo wake, kwakweli alishtuka sana kwani ilionyesha wazi kuwa ni

mjamzito, alianza kuwaza ni kitu gani afanye, huku wazo la kutoa ile mimba likichukua nafasi kubwa sana.
Mara akasikia mlango wake ukigongwa na kumfanya apatwe na hofu kiasi, akaenda kumwaga ile mikojo yake na kutupa kabisa ule ushahidi

maana hakutaka hata mtu kumuhisi vibaya, basi alienda kufungua mlango wake na kukuta aliyekuwa anagonga ni Erica ambapo moja kwa

Erica aliingia chumbani kwa Vaileth na kumwambia,
“Dada samahani, tukae kidogo tuongee kuna kitu nataka kukwambia”
Vaileth alikaa nae kitandani na kuanza kumsikiliza Erica huku akimuangalia kwa makini,
“Eeeh niambie”
“Nimeota kuwa wewe una mimba”
Vaileth alishtuka sana, na kushindwa hata kuongea, ila Erica aliendelea kusema,
“Tena nimeota kuwa hiyo mimba unataka kwenda kuitoa”
Yani Vaileth ndioT alihisi kuchanganyikiwa kabisa kwa muda huo.


Mara akasikia mlango wake ukigongwa na kumfanya apatwe na hofu kiasi, akaenda kumwaga ile mikojo yake na kutupa kabisa ule

ushahidi maana hakutaka hata mtu kumuhisi vibaya, basi alienda kufungua mlango wake na kukuta aliyekuwa anagonga ni Erica ambapo

moja kwa Erica aliingia chumbani kwa Vaileth na kumwambia,
“Dada samahani, tukae kidogo tuongee kuna kitu nataka kukwambia”
Vaileth alikaa nae kitandani na kuanza kumsikiliza Erica huku akimuangalia kwa makini,
“Eeeh niambie”
“Nimeota kuwa wewe una mimba”
Vaileth alishtuka sana, na kushindwa hata kuongea, ila Erica aliendelea kusema,
“Tena nimeota kuwa hiyo mimba unataka kwenda kuitoa”
Yani Vaileth ndio alihisi kuchanganyikiwa kabisa kwa muda huo.
Vaileth alinyamaza kimya bila ya kusema chochote, kisha Erica akaendelea kuongea na kumwambia Vaileth,
“Sikia dada, unajua kama kutoa mimba kuna madhara sana. Sio vizuri kutoa mimba, bora uvumilie uweze kuzaa uwe na mtoto wako”
Muda huu Vaileth alijikaza na kumuuliza Erica,
“Umepata wapi hiyo habari kuwa mimi ni mjamzito na ninataka kutoa mimba?”
“Nimepata hiyo habari kwenye ndoto, nimeota kuwa una mimba na unataka kuitoa”
“Una uhakika gani?”
“Kama unanibishia basi nikamwambia mama ili twende wote hospitali kupima, nina uhakika na ndoto zangu”
“Erica jamani usifanye hivyo tafadhari, nakuomba usimwambie chochote mama.”
“Ukitaka nisiseme niahidi kuwa hiyo mimba hutoitoa”
“Nakuahidi Erica, sitotoa mimba hii wala nini, nitailea hadi nitakapozaa ila usiseme Erica, nitafukuzwa kazi mimi, na kwetu maisha ni shida

sana”
“Naelewa, kweli mimi ni mbea sana na huwa nawashwa kukaa bila kusema ila niruhusu nimwambie mtu mmoja tu ambaye namuamini kuwa

yeye anaweza kukaa na jambo moyoni na hatolisema kwa yoyote”
Vaileth akaogopa kidogo, na kumuuliza Erica kwa uoga,
“Nani huyo?”
“Ni Erick, niruhusu nimwambie tu Erick yani nitakuwa sawa nikimpata hata mmoja wa kumwambia hili na sitosema popote tena”
Hapa kidogo Vaileth alipumua kwani kweli Erick hakuwa na tabia za umbea kabisa, yani huwa hata kumuuliza muhusika tu hamuulizi kabisa,

basi akakubali na kusema,
“Hakuna tatizo, naamini Erick hawezi kusema. Ila nakuomba usimwambie yoyote yule mwingine, sina maisha yoyote mimi, hii kazi ndio

tegemeo langu”
“Sawa, nimekuelewa”
Ilisikika sauti ya mama Angel akimuita Vaileth, ilibidi pale Vaileth aachane na Erica na kwenda kumsikiliza mama Angel anasema kitu gani.
Wakati huo Erica nae aliondoka na kwenda kufanya kazi zingine za pale ndani kwao, moja kwa moja alienda chumbani kwa Erick ili

akafanye nae kazi ila alimkuta kwa muda huo Erick akijiandaa,
“Kheee unaenda wapi kwani?”
“Naenda na baba kiwandani”
“Aaaah sawa”
Erica alitoka zake na kumuacha Erick akimalizia kujiandaa pale.

Siku ya leo, nyumbani kwa madam Oliva alikuwepo Paul na Steve tu, walikuwa nje wakijishughulisha na vitu mbalimbali, basi Steve

alimuuliza Paul,
“Vipi shuleni maendeleo yakoje?”
Ndipo Paul alipokumbuka kuwa kuna barua alipewa jana yake kuwa awapatie wazazi wake, waweze kwenda shule siku hii ya Jumamosi

kwenda kuongea na mwalimu wa paul. Basi Paul akaenda kumletea Steve ile barua ambapo baada ya muda kidogo Steve aliamua kumpia

simu madam Oliva ili ampe ule ujumbe,
“Kuna barua, Paul kanipatia hapa kuwa wazazi wake tunahitajika shuleni”
“Kheeee huyo Paul kafanyaje tena huko shuleni?”
“Sijui, inabidi kwenda”
“Sawa, si upo nae hapo nyumbani. Basi nenda nae huko shuleni, mimi nikiwahi pia nitafika hapo hakuna tatizo”
Basi Steve alijiandaa vizuri kabisa kwaajili ya kuondoka na Paul kwenda nae huko shuleni walikoitwa.
Kisha Steve na Paul waliongozana kwenda huko shuleni ambapo Paul anasoma, wakati wanafika tu pale na madam Oliva alikuwa kashafika

kwahiyo ilibidi tu wote kwa pamoja waende ofisini ila mwalimu mmoja alipowaona akaropoka,
“Kheee huyu Paul kumbe baba yake yupo? Anavyosemaga kila siku hana baba!!”
Wote wakaangaliana na kuguna tu, kisha madam Oliva akasema,
“Jamani walimu wenzangu, hebu acheni hiyo tabia mnadhalilisha taaluma yetu”
Basi wakabaki wanatazamana maana hawakujua kama mamake Paul ni mwalimu pia.
Moja kwa moja walienda kuzungumza na mwalimu aliyewaita, ambapo mwalimu alimtaka Paul kuwasubiri wazazi wake nje kwanza, halafu

Paul alivyotoka ndio alikaa vizuri ofisini na wazazi wa Paul na kuanza kuzungumza,
“Kwanza kabisa sikujua kama babake Paul yupo, nilijua ni ana mama tu kwani siku zote huwa anasema baba yake hayupo”
Madam Oliva alijibu kwa kujibalaguza pale,
“Babake yupo”
“Hata mimi naona aisee, basi kesi imeisha tayari ngoja niongee sasa”
“Eeeeh tunakusikiliza”
“Paul, nimemkuta mara nyingi tu akiwasimulia wenzie kuhusu ubaya wa mababa, yani kila mara anawaambia wenzie kuwa wababa ni watu

wabaya sana, wanatelekeza watoto wao hata hawana habari kuwa mtoto anakula nini au anavaa nini, yani yeye huwa anasifia tu kuhusu

mama yake, ila anasema mama yake ana mawazo sana sababu hana baba wa kuwa nae. Mimi kama mwalimu niliumia sana, kuna siku

mwanangu alikuja nyumbani, anasoma hapa ni rafiki wa Paul, aliniambia mama naomba tumpe Paul baba yetu hata mara moja akae nae,

alisema Paul anatia huruma sana sababu baba yake sio binadamu wa kawaida. Nikashtuka sana, halafu siku hizi huwa namuona Paul

anakuwa na mawazo muda wote, utakuta amekaa darasani kajiinamia chini akiwaza sana, ndiomana nikaamua nimuite mzazi wake ili

nikwambie na ujue cha kufanya”
Kisha alimwangalia Steve na kumwambia,
“Jamani, nyie wababa hebu acheni roho mbaya hizo. Mpaka mtoto anafiki hivi kweli!! Cheki ulivyomfananisha jamani, halafu umemuacha

anahangaika bila baba, ni bora ijulikane umekufa kuliko upo hai halafu humjali mtoto”
“Nimekusikia mwalimu”
Steve hakutaka kuongea sana, mwalimu aliongea pale na kuagana nao, kwakweli kwa upande mwingine Steve alijihisi vibaya, katika hisia

zake alihisi kabisa kuwa Paul ni mwanae wa kumzaa ila kwanini inakuwa vile? Hakuelewa kabisa.
Madam Oliva nae alijihisi vibaya sana, walitoka na kuondoka na Paul kurudi nae nyumbani ila hawakuongea kitu chochote kile, kisha

walivyofika nyumbani madam Oliva alienda chumbani na kuanza kuzungumza na Steve,
“Tufanyeje sasa?”
“Inavyoonyesha mlisha Paul sumu mbaya sana kuhusu wababa”
“Ni kweli, sababu ya hasira nilizokuwa nazo juu ya baba yake, alinitenda vibaya sana”
“Hata kama, ila si vizuri kumlisha mtoto sumu mbaya kiasi hiki. Yani mtoto ajue kuwa alikataliwa na baba yake, sijui hapendwi. Najua Paul

anachowaza sasa ni kitu gani! Ni hivi, anafikiria ukaribu uliokuwepo kati yangu na yake, anafikiria kuwa je mimi ndiye baba yake? Anafikiria

jinsi mama yake ulivyomwambia kuhusu baba yake ndiomana anakuwa na mwazo sana. Na maneno ukishatamka hayarudishiki mdomoni

yani ni kama maji yakimwagika vile, sasa hapa cha kufikiria tu kuwa tutafanyaje na huyu mtoto”
Madam Oliva akapumua kwanza na kusema,
“Unajua hadi nahisi kuchanganyikiwa mmmh!! Ila mtoto amekuwa kwasasa, sijui kama atanielewa nikimbadilishia maneno. Unajua mimi

nilikuwa na kidonda moyoni, ndiomana muda wote nilipokuwa naongea na mwanangu nilikuwa namwambia ubaya wa baba yake tena bila

kujali kuwa kuna wanaume wengine wanawapenda sana watoto wao wala nini, nilikuwa naumia sana, hebu fikiria toka nina mimba mtu

hataki kuniona na mimba ameikataa, nimejifungua bado akanikataa, kwakweli nilikuwa kwenye wakati mgumu sana ndiomana nimejikuta

nikimwambia maneno yote hayo Paul wangu jamani”
“Hasira hasara, umejenga kitu kibaya sana kwa Paul. Na bora ni mtoto wa kiume pia, ila angekuwa ni mtoto wa kike, angekuwa muda wote

anawaza mabaya tu kwa wababa. Nitajitahidi kuongea nae, nitajitahidi kuwa nae karibu ili aweze kuhisi uwepo wa baba katika maisha yake.”
Madam Oliva alimsihi tu baba Angel amsaidie jambo hilo maana yeye alihisi kutokuweza kabisa kumuelewesha tena mwanae kuhusu

wababa.

Baba Angel akiwa kiwandani na Erick baada ya kazi za hapa na pale, alifika Juma ambaye alibahatisha tu siku hiyo na kuwakuta kwakweli

alifurahi sana na kuanza kuongea nao,
“Kwanza nimefurahi mno kuwaona mpo pamoja”
Kisha Juma alimuomba kidogo baba Angel kuongea nae, kwahiyo walimuacha Erick aendelee na kazi zingine,
“Hivi ndugu yangu mbona huwa hutaki kunielewa kuhusu kipaji cha huyu mtoto? Hebu nipatie niwe nae japo kwa wiki moyo na mimi

akanisaidie kazi yangu”
“Hivi akili yako ni nzima kweli Juma? Yani mimi nikakupatie kijana wangu kweli!!”
“Kwani kuna tatizo gani jamani eeeh! Mambo mengine kusaidiana, sawa isiwe wiki moja, naomba hata kwa siku moja tu.”
“Kwa hutojali, twende wote hilo eneo la tukio”
“Hakuna tatizo, hayo ndio maswala ya kuongea sasa kuliko kubaniana riziki”
“Kwahiyo mtoto wangu ndio ridhiki yako?”
“Sinamaana hiyo, ila nina maana kuwa mwanao atafungua na kunionyesha njia vizuri kwenye biashara yangu kwani nimeshaona uelewa

wake ulivyo”
“Sawa nimekuelewa kwa hilo”
Basi wakaongea pale, na kisha Juma alimuaga baba Angel na moja kwa moja baba Angel alirudi ofisini kwake kumalizia kazi na kijana

wake, alipomaliza ndipo walipoenda dukani kwani baba Angel hakuwa ametembelea duka kwa siku nyingi kidogo.
Basi walimkuta Rama pale akiendelea na kazi zake vizuri kabisa, ila baba Angel wakati akiongea nae Rama alimwambia jambo ambalo

lilitukia mahali hapop,
“Kuna mwanamke Fulani alikuja hapa, alilia sana kwa muda mrefu halafu akaondoka”
“Mmmmh mwanamke gani huyo?”
“Alisema anaitwa Sia”
Baba Angel akacheka na kumwambia Rama,
“Huyo mwanamke huwa akili zake zinaenda na kurudi, usijaribu kumsikiliza anachokisema”
Waliongea kidogo pale huku wakipitia baadhi ya bidhaa za pale, ila Rama alikumbuka kitu na kusema,
“Alisema kuwa Jumapili baada ya kutoka Kanisani atakuja tena hapa”
Baba Angel alielewa vizuri akili za Sia zilivyo basi akasema kuwa kesho yake na yeye ataenda tena baada ya kutoka Kanisani.

Baba Angel na Erick walirudi nyumbani kwa siku hiyo wakati muda kidogo umeenda hivyobasi walifikia kupata chakula cha jioni tu moja kwa

moja, baada ya hapo kila mmoja alienda moja kwa moja kwenye chumba chake.
Baba Angel alimueleza mke wake kuhusu walipoenda leo na Erick na kila kitu kilichotokea, ila hakukumbuka kumwambia kuhusu Juma

kuhitaji siku moja Erick afike kwenye biashara zake.
Alimueleza tu jinsi walivyoenda dukani na jinsi alivyoambiwa na Rama kuwa Sia alikuwa mahali pale,
“Kheee sasa alifata nini dukani na kilio juu”
“Yule mwanamke ni chizi, ila nasikia Kesho anaenda tena, hakuna shida nitaenda pale ili nimuulize vizuri tatizo lake ni nini”
“Mjinga sana, sasa pale angepata msaada gani?”
“Sikia nikwambie kidogo malengo ya yule mwanamke yalivyokuwa, ni hivi aliamini kuwa kabadilishana mtoto na wewe, kwamaana hiyo

aliamini Erick ni mwanae halafu Elly ni mwanetu, ndiomana alikuwa akisema ile biashara ni ya mwanae, akimaanisha kuwa kama tukimpa

Erick ni sawa sababu ni mwanae, na kama Elly tungegundua badae basi lazima tungempa mali zetu ambapo Elly asingeweza kumtupa

mwanamke aliyemlea kwa siku zote. Ila kwasasa akili yake kama imegonga mwamba, sababu Erick sio mwanae, na ile kitendo cha

kumwambia kuwa unahisi Elly ni mtoto wa Derrick ndio anapata mawazo sana, sababu kazi ya Derrick aliitambua na siku zote alikuwa

akiitoa kasoro, kwahiyo lazima achanganyikiwe sana”
Mama Angel alicheka sana na kusema,
“Yani yule ana akili ndogo sijapata kuona, halafu yule tusipokuwa makini ataokota makopo, ingawa nahisi kuwa yule mtoto wa madam Oliva

atakuwa ni mwanae”
“Unadhani madam Oliva atakubali? Ni ngumu ujue”
Walijadiliana ila hawakupata jibu na kufanya wapate mawazo tu ya kuendelea kuchunguza.

Erica alimfata Erick chumbani kwake kwa muda huu na kuanza kuongea nae, kwanza alimpa pole kwa mizunguko,
“Ila nina usingizi sana Erica”
“Ni kweli una usingizi hata mimi naona ila nisipokwambia hili nitaumwa mimi”
“Nini tena Erica jamani!”
Erick alikuwa akiuliza huku akisinzia tu, basi Erica alitaka kumwambia ila akakumbuka kitu,
“Mmmmh haya ndio yale yale, najiropokea kumbe mama ananisikiliza”
Akainuka na kwenda kufunga mlango vizuri, na kurudi kitandani kwa Erick, ila bado Erick alikuwa amelala basi moja kwa moja alienda na

kuosha mkono wake na kushika maji kiasi kisha alienda na kumnawisha Erick usoni na kufanya Erick ashtuke tu,
“Jamani Erica kwanini lakini?”
“Mimi sitaweza kulala na hili, nisikilize tafadhari”
Basi Erick ilimbidi tu akae ila kiukweli alikuwa na usingizi sana ingawa aliamua kumsikiliza Erica, ambapo Erica alianza kumwambia,
“Nimeota kuwa dada Vai ana mimba na anataka kuitoa hiyo mimba”
“Aaaah sawa”
Kisha Erick akajilaza tena, na kumfanya Erica amtingishe pale kitandani kwani alikuwa akihitaji kusikilizwa,
“Erica nakuomba nisaidie jambo moja tu”
“Jambo gani?”
“Naomba tulale, lala tu hapa kitandani kwangu ulale na mimi kwa leo halafu nikishtuka wakati usingizi umeisha ndio uanze kuniambia yote

unayohitaji kuniambia, nakuomba dada yangu, nakuomba Erica”
Erick alikuwa akiongea kwa usingizi kabisa, basi Erica alikubali na kulala pembeni ya nduguye.
Kulipokucha, Erick ndio alikuwa wa kwanza kuamka, basi alimuamsha Erica kwani alikumbuka kile alichokuwa akimsumbua usiku,
“Erica, Erica, amka uniambie sasa”
Erica aliamka na kufikisha macho, ila hakusema kitu chochote bali aliinuka gafla kama mtu aliyepatwa na kitu sio cha kawaida halafu

akaondoka mule chumbani kwa Erick, kwakweli hata Erick hakumuelewa dada yake.

Junior bado alikuwa na uhitaji wa kupata pesa ya kuweza kumpatia Vaileth ili aende kutoa ile mimba aliyokuwa nayo, kwavile kwa baba

yake mlezi ilishindikana na kwa mama yake ilishindikana basi siku hiyo alijiandaa na kutoka shuleni halafu moja kwa moja alienda nyumbani

kwa Linah.
Alifika nyumbani kwa Linah na kumkuta muda huo akinywa chai,
“Ooooh nilijua tu kuwa utarudi”
“Naomba unisamehe”
“Yani hata usijali, nilijua tu kuwa utarudi ila kipindi hiki nitakupa sheria za kuwa na mimi”
“Sawa, nipo tayari kwa lolote lile. Nimepatwa matatizo na sina pa kukimbilia, nimekukumbuka wewe tu ndio msaada wangu”
“Una tatizo gani”
“Kuna mwanafunzi mwenzangu nilikuwa natumia simu yake, bahati mbaya njiani nikaibiwa na vibaka. Sasa mwenyewe anadai simu yake”
“Khaaa ulikuwa ukiongea na nani?”
“Na mama, halafu mama kakataa katakata kunikabidhi pesa nikamnunulie yule mwanafunzi simu yake”
“Kwani wewe simu yako iko wapi?”
“Mimi sina simu, iliharibika”
“Hebu kaa chini kwanza nikupe masharti yangu”
Junior alikuwa mpole kabisa akisikiliza masharti ya huyu mama,
“Safari hii ukivunja masharti yangu sidhani kama tutaelewana kwakweli, yani ole wako ukiuke masharti yangu. Kwanza hakuna kutoka shule

bila ruhusa yangu, ni mimi tu mwenye uwezo wa kukutoa shule na kukupeleka nitakapo, kila muda nikikupigia simu unatakiwa kupokea simu

yangu haijalishi kitu chochote, ole wako nikufumanie na mwanamke, nadhani utataja jina langu la utoto. Haya, hiyo simu uliyoibiwa

inauzwaje?”
“Laki mbili na elfu hamsini”
“Oooh tutaenda wote dukani kuinunua”
Junior hakuwa na usemi kwani hakutaka kuongea sana, kuepuka swala la yeye kuonekana ni muongo. Basi siku hiyo alishinda na huyu

mama kwa muda mwingi sana ila kuna simu iliingia kwa huyu mama na baada ya hii simu huyu mama akachukua pochi yake na kumkabidhi

Junior laki nne kisha akamwambia,
“Lete kwanza kitambulisho chako cha shule”
Junior alimkabidhi yule mama kitambulisho chake halafu huyu mama akamwambia tena,
“Nenda tu kanunue hiyo simu maana haitawezekana kuendelea kuwa hapa na haitawezekana kuondoka wote, ila nitakuja shuleni kwenu

kukukabidhi hiki kitambulisho. Hela itakayobaki kanunue simu yako ila hakikisha unanipigia ukirudi tu shuleni”
Junior aliitikia na kwa wakati huo aliondoka mahali pale, safari yake ilikuwa ni kuelekea moja kwa moja nyumbani kwa mamake mdogo yani

mama Angel.

Kama kawaida walijiandaa wote na kwenda kwenye Ibada, ila Vaileth alibaki nyumbani maana huwa anapata sababu kila ifikapo siku hiyo

kwani alitaka pia kuwasiliana na Junior kwa siku hiyo.
Walivyoondoka, ndipo alipoanza kumtafuta Junior, yani alimpigia sana simu Junior bila ya mafanikio yoyote, alijiuliza maswali mengi sana

kuwa kwanini Junior anafanya vile,
“Aliniahidi jana kuniletea pesa, ila jana imepita kimya, leo tena hata simu hapokei, sijui ana mpango gani na mimi! Ila Erica nae kaniambia

nisitoe hii mimba, hivi mimi nitakuwa ni mgeni wa nani ikiwa wakigundua kuwa nina mimba humu ndani?”
Aliwaza sana na kukosa jibu, basi alianza kujifanyia tu kazi zake ambazo zimebakia hapo na mwishoe akaenda kulala kwani alikuwa

amechoka kiasi.
Kwenye mida ya mchana, mama Angel na familia yake walirudi na kumkuta Vaileth pale basi alianza kuongea nae mawili matatu,
“Mbona baba hajarudi?”
“Aaaah kapitia kwenye biashara huko, tena nimekumbuka Vai, jioni utaenda buchani kununua maini”
“Sawa mama, hakuna tatizo”
“Unikumbushe basi maana mimi naweza nikasahau”
Basi walikuwa wakiongea pale huku mama Angel akionekana kupiga simu zake mbali mbali na kuwasiliana na watu wake, ila bado Vaileth

alikuwa na mawazo sana kuhusu junior kuwa ni kwanini hapokei simu zake halafu hajaonekana ile jana kama alivyomuahidi.

Junior alifika nyumbani kwa mama Angel na kuingia ndani ambapo alimkuta na kuanza kumsalimia pale,
“Kheee umeamua kurudi leo?”
“Nimewakumbuka ndio, nikaona nije kuwasalimia”
“Karibu, hapa ni nyumbani”
“Asante mamdogo ila njaa inaniuma, Vaileth yuko wapi?”
“Kuwa na adabu wewe, yule ni kama dada yako. Sema dada Vai sio kumuita Vaileth kamavile ni mtu unayelingana nae”
“Samahani mamdogo sijui mimi nimezoeaje, ila hata wakina Erick huwa hawaniiti kaka Junior labda ndiomana”
“Hawakuiti sababu ya tabia zako, rekebisha tabia kwanza uheshimiwe”
“Sawa, dada Vai yuko wapi?”
“Nimemtuma, kuna mahali ameenda, ila kama njaa inakuuma ngoja nikuitie Erica akupe chakula”
Basi mama Angel alimuita Erica pale ampe Junior chakula, halafu yeye akaenda zake ndani. Wakati huo Junior nae moja kwa moja alienda

chumbani kwa Vaileth na kuandika ujumbe kisha akamuachia zile hela akiwa amezifunga kwenye karatasi, akaweka kwenye droo halafu

akatoka nje, moja kwa moja alienda mezani ambako ndio kuliandaliwa chakula na Erica na kuanza kula kile chakula ila alikula kwa kiasi

kidogo sana, kwani kiukweli alishashiba toka kule kwa Linah alipokula.
Baada ya kumaliza kula, aliinuka na kumuaga Erica kuwa anaondoka,
“Kheee humsubirii dada Vai?”
“Aaaah nina haraka sana, akija msalimie”
Halafu Junior aliondoka zake, basi Erica alimuangalia na kujisemea,
“Ndiomana watu huwa wanasema kuwa wanaume wana tabia mbaya sana, kashampa mimba mwenzie, saivi anajifanya hata hawezi

kumngoja kidogo tu amsalimie jamani. Ila Mungu atamsaidia dada Vai”
Kisha Erica aliendelea na mambo yake mengine.

Vaileth akiwa anataka kurudi kutoka alipokuwa ametumwa na mama Angel, njiani alikutana na Sia ambaye alimsimamisha Vaileth na kuanza

kuongea nae,
“Unakumbuka kuna siku nilikuja pale kwenu na kukwambia kuwa inawezekana Erick akawa mtoto wangu sababu nilicheza mchezo wa

kubadilisha watoto, unakumbuka?”
“Nakumbuka ndio”
“Basi, Erick sio mtoto wangu ndio vipimo vilivyoonyesha hivyo na wala Elly sio mtoto wangu”
“Duh!! Kwahiyo vipimo vimeonyesha kuwa Elly sio mtoto wako?”
“Hapana, sijapima na Elly, kutokana na haya yaliyopo, kuna uwezekano mkubwa sana wa Elly kutokuwa mtoto wangu. Tamaa imeniponza

mimi, hapa nilipo najuta tu hata sijui cha kufanya kwakweli”
“Aaaah pole sana”
“Asante, nishauri cha kufanya basi. Namtafuta mwanangu halisi”
“Unadhani hata akikufahamu atakukubali? Akija kujua kuwa ulimbadilisha sababu ya pesa atakukubali? Sijui lakini, ila ulichofanya hakikuwa

sawa kabisa”
“Umetoka kununua nini?”
“Maini”
“Aaaah ya Erick eeeh! Maana huwa anapenda sana rosti ya maini na chapati. Naomba nifate”
Sia alimshika Vaileth mkono hadi kwenye banda lake na kutoka na mfuko kisha akampa Vaileth na kumwambia,
“Hizo ni chapati nne, leo asubuhi zilibaki, naomba mtakapomuwekea Erick chakula usiku basi umuwekee na chapati moja kati ya hizo.

Ipashe tu na uiweke. Huwa sipiki Jumapili, yani huwa sifungui biashara yangu ila leo nimefungua sio kwa kutaka bali kuna vitu vinanisumbua

sana. Naomba unisaidie kwa hilo”
“Kheee kwanza unamuongelea Erick yupi? Yule mdogo?”
“Hapana, namuongelea baba Angel. Naomba unifanyie hivyo. Humu sijaweka dawa wala kitu chochote, hakuna kibaya nilichoweka humu, ila

najua akila atanikumbuka japo kwa kiasi tu na anaweza hata kufikiria kunisaidia juu ya hili linalonitatiza, nisaidie Vaileth nakuomba”
Vaileth alimuangalia sana na kumuona anatia huruma kwakweli, kwahiyo alichukua zile chapati na kurudi nazo nyumbani.

Muda wa chakula cha usiku, ni kweli kabisa leo kwa mama Angel zilipikwa chapati na rosti la maini, basi Vaileth aliogopa kufanya kama

alivyoagizwa na Sia badala yake zile chapati za Sia alijiwekea yeye mwenyewe kwenye sahani yake ili kama kuna madhara yoyote basi

yampate yeye, ila walipokaa mezani kuanza kula, baba Angel alivuta ile sahani ya Vaileth na kumwambia aweke chapati zingine kwenye

sahani nyingine maana zile atazila yeye, basi baba Angel alianza kuzila zile chapati, muda huu mama Angel alikuwa chumbani na mtoto

wake mdogo akimnyonyesha maana alianza kulia muda kidogo tu baada ya wao kukaa mezani kwahiyo aliinuka na kwenda kumnyonyesha.
Basi Vaileth alikuwa akimuangalia tu baba Angel akila zile chapati, ila baba Angel alishtuka kidogo na kuuliza,
“Nani kapika hizi chapati?”
Vaileth akajibu kwa uoga sana,
“Mimi ndio nimepika”
“Nani aliyekutuma ulete chapati zilizopikwa na Sia humu ndani?”
Kwakweli Vaileth alitetemeka kwani hakutambua kama ingefahamika kuwa zile chapati ni za kutoka kwa Sia.


Basi Vaileth alikuwa akimuangalia tu baba Angel akila zile chapati, ila baba Angel alishtuka kidogo na kuuliza,
“Nani kapika hizi chapati?”
Vaileth akajibu kwa uoga sana,
“Mimi ndio nimepika”
“Nani aliyekutuma ulete chapati zilizopikwa na Sia humu ndani?”
Kwakweli Vaileth alitetemeka kwani hakutambua kama ingefahamika kuwa zile chapati ni za kutoka kwa Sia.
Baba Angel aliacha kula na kuinuka zake kuelekea chumbani, basi Erica alimuangalia Vaileth na kumuuliza,
“Dada, chapati za Sia kivipi?”
“Sijui”
“Hebu nipe nizionje”
Vaileth alimsogezea ile sahani Erica, ambaye alionja kidogo na kusema,
“Mbona nzuri tu”
“Hata mimi nashangaa kwanini baba kazikataa”
“Ila hujazipika wewe eeeh! Si ungeniambia nije nikusaidie!”
Vaileth aliinama chini tu, kwani alishindwa hata kujibu, basi Erica alimsogezea na Erick zile chapati huku akimwambia,
“Hebu zionje na wewe”
“Hilo jina la mtengenezaji tu, limezhaniochefua unadhani naweza kuendelea kula? Ngoja na mimi niondoke zangu”
Erick nae aliinuka na kuelekea chumbani, kwahiyo pale walibaki Vaileth na Erica tu ambapo Erica alimuuliza Vaileth,
“Kwani dada imekuwaje? Umetoa wapi chapati za huyo Sia? Kwanza Sia ndio nani?”
“Ni mama yake Elly”
“Khaaa jamani, ndio nyumba nzima hawamtaki yule mama jamani, wakati huo huo huwa tunaishi na Elly hapa ndani!! Ngoja mimi nile hizi

chapati na nione kama zitanidhuru”
Erica na Vaileth walikula kisha kila mmoja kuelekea chumbani kwake.

Erica alipokuwa yupo chumbani kwake tu, alifika kaka yake na kumwambia Erica,
“Mimi nina njaa sana”
“Si ukale zile chapati”
“Hapana Erica, naomba ukanisongee ugali”
“Kheee umenifanya kama mkeo”
Halafu Erica akainuka, kwakweli Erick alimuangalia tu na kushindwa kusema chochote kile ila aliinuka tu na kwenda sebleni halafu chakula

kilipoiva Erica alimuita ili aweze kula, basi Erick alienda mezani na kula ule ugali ambao ulisongwa na Erica kisha akainuka na moja kwa

moja alienda tena chumbani kwa Erica ambaye kwa muda huu alikuwa akijiandaa kulala,
“Asante kwa chakula Erica ila sijapenda ulivyoniambia”
“Nilivyokwambia nini?”
“Kuwa mimi nakufanya kama mke wangu, nitawezaje kukufanya mke wangu wakati wewe ni dada yangu?”
“Kwani dada na kaka hawaoani?”
“Hakuna kitu kama hiko, kwanza ni laana”
“Haya yaishe, umeshiba!”
“Ndio nimeshiba”
“Basi nenda chumbani kwako ukalale”
Kwakweli Erick alishindwa kumuelewa Erica toka asubuhi ya siku hiyo alionekana tofauti sana ukilinganisha na siku zote.
 
Simulizi Zinazorushwa na BURE SERIES

1. Simulizi: Kurudi Kwa Moza

Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi: Kurudi Kwa Moza

2. Riwaya: Kasri ya Mwinyi Fuad
Bonyeza hapa chini kusoma
Riwaya: Kasri ya Mwinyi Fuad

3.Simulizi: Nini maana ya mapenzi
Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi: Nini maana ya mapenzi

4. Simulizi : Nguvu Ya Mapenzi
Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi : Nguvu Ya Mapenzi

5. Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)
Bonyeza hapa chini kusoma
Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)

6. RIWAYA: Sauti Yake Masikioni Mwangu
Bonyeza hapa chini kusoma
RIWAYA: Sauti Yake Masikioni Mwangu

7. NDOA ILIVYOTETERESHA IMANI YANGU (Kisa Cha Kweli)
Bonyeza hapa chini kusoma
NDOA ILIVYOTETERESHA IMANI YANGU (Kisa Cha Kweli)

💥 💥 💥NEW 💥 💥 💥

8. RIWAYA: Mume Gaidi

Bonyeza hapa chini kusoma
RIWAYA: Mume Gaidi

9. STORY: Sitaki Tena

Bonyeza hapa chini kusoma
STORY: Sitaki Tena

10. Nilivunja Ndoa Zangu 3 Kulipiza Kisasi (Kisa Cha Kweli)

Bonyeza hapa chini kusoma
Nilivunja Ndoa Zangu 3 Kulipiza Kisasi (Kisa Cha Kweli)
 
SEHEMU YA 361


Vaileth akiwa amelala na mawazo mengi sana yakitawala kichwa chake, akachukua simu yake tena na kumpigia Junior, aliona hiyo sababu ni usiku basi Junior angepokea mapema simu yake, ila haikuwa hivyo kwani simu iliita sana hadi kukatika, kwakweli alikata tamaa ila kuna ujumbe mfupi uliingia kwenye simu yake,
“Vai mpenzi, najua unajiuliza kwanini nipo kimya na pengine unahisi ni makusudi au ni kitu gani, ila mimi nilikuwa nikitafuta pesa na yote haya nafanya sababu ya hiyo pesa. Angalia ndani ya droo ya kwenye kabati lako hapo, kuna karatasi nimeviringisha utaliona hapo. Ukifanikisha utaniambia, nipo sehemu mbaya kwasasa, siwezi kuongea na simu”
Vaileth alijiuliza sana kuwa hiyo sehemu mbaya ni sehemu mbaya ipi wakati anajua kuwa Junior ni yupo shule, halafu shule yao wapo huru sana kiasi kwamba huwa anaongea nae kwenye usimu hasa usiku kama huo.
Basi aliweka simu pembeni na kwenda kuangalia kwenye droo kweli alikuta kama Junior alivyomwambia, alihesabu ile hela na kuona Junior alimuwekea laki tatu. Akafurahi sana na kuona kuwa Junior anampenda kweli,
“Aaaah, sasa nimeamini kuwa Junior ananipenda sana. Sasa sijui niendelee na wazo la mimi na Junior yani wazo la kutoa mimba au nikazane na wazo la Erica kuwa nisitoe mimba? Ngoja niangalie madhara yake kwa yote mawili ili kama madhara makubwa niyaepuke. Kwanza kabisa, wakijua kama nina mimba kuna uwezekano mkubwa wa mimi kukosa kazi, ila kuna uwezekano mkubwa wa mimi kutetewa na Erica, nikitoa mimba basi Erica atanisemea na kuna uwezekano mkubwa wa mimi kufukuzwa kazi, ila si nakataa tu kuwa sikuwa na mimba! Mmmmh sijui ipi ni njia bora kwangu!”
Aliwaza kiasi na kuamua tu kulala kwa muda huo maana hakutaka kuwaza sana.

Kulipokucha tu, mama Angel ilibidi akampikie chakula cha asubuhi mume wake kwani alikuja kugundua ile asubuhi kuwa hakula kile chakula walichopika usiku, na alimuona mumewe kuwa kaamka akiwa na njaa, basi alimuandalia chakula na kwenda nae mezani ili aweze kula, basi baba Angel alikaa mezani na kuanza kula kile chakula alichoandaliwa na mkewe,
“Mbona usiku hukula mume wangu?”
“Umejuaje kama sikula?”
“Unajua nilikuangalia ule usiku tulivyokuwa tumelala nikahisi tu hukula chakula, vipi hukupenda chapati?”
“Aaaah sikuzitaka kwa jana”
Baba Angel hakutaka kumwambia mke wangu kuwa katambua zile chapati za jana ni za kutoka kwa Sia, kwani anajua lazima mkewe atachukia sana na kumfokea Vaileth, ingawa na yeye alitaka kujua ni kwanini Sia amempa zile chapati mdada wao wa kazi.
Basi alikula pale na kuongea mambo mengine na mke wake.
Kisha baba Angel alijiandaa na kuondoka zake, ambapo moja kwa moja alienda kwenye biashara ya Sia kwani alitaka kujua kwanini kafanya vile.
Alimkuta Sia akiwa makini na kazi zake za pale, ila Sia alipomuona baba Angel aliacha kazi zake na kumfata kuongea nae,
“Wewe kwanini umeweka chapati zako kwangu?”
“Ooooh nashukuru sana, kwani umezila na kugundua kuwa zimetoka kwangu”
“Mjinga wewe, umenilaza na njaa jana. Sikutaka tu kumwambia ukweli mke wangu maana angemgombeza bure yule msichana wa kazi”
“Kwanza naomba unisamehe, sikuwa na nia mbaya ila nilijua ukizila zile chapati basi utanikumbuka na kuja kama hivi kuongea nami. Unadhani naweza kukuwekea dawa kwenye chapati? Hapana, ila nilitaka tu unikumbuke na uje kuniona kama hivi. Unajua sikutaka kufika nyumbani kwako ndiomana nimefanya hivi”
“Haya ulikuwa na shida gani?”
Sia akamsogeza pembeni zaidi baba Angel na kuanza kuongea nae,
“Ni hivi, unajua mimi nipo kama nimechanganyikiwa hivi najiona kabisa siku hizi nipo kama kichaa, kuna siku nilishinda Kanisani ila nilipotoka nilikuwa naongea peke yangu, nikashikwa bega na kuropoka kila kitu kumbe nimeongea mbele ya Elly, kiukweli Elly hanielewi kabisa ndiomana hata hajaondoka tena nyumbani, anahisi mama yake nina matatizo. Yani akili yangu imeharibika kweli, na ninakubali kuwa nina matatizo kweli, ila jana wakati nimetoka kununua bidhaa za kupika, nilipita mahali na kumuona dokta aliyenibadilishia mtoto”
Hapo ndio baba Angel akashtuka kidogo na kumuuliza,
“Dokta gani?”
“Ni dokta Jimmy maana ndio alihusika na kunibadilishia mimi, alilipwa pia na mzee Jimmy. Ila ni kwavile sikuwa na usafiri na wala hela ya kumfatilia, sababu nilikuwa nishanunua bidhaa ila nisingenunua bidhaa ningemfatilia ili aniambie ukweli kuwa mwanangu yuko wapi”
“Kumbe dokta Jimmy ndio alifanya mchezo huo?”
“Ndio, tena yeye ndio alikuwa akinihakikishia kuwa mtoto tumebadilisha na mtoto wa Erica, kiukweli nimemlea Elly sijawahi kumlea vibaya hata mara moja, sina pesa ndio ila sijawahi kumlea vibaya Elly”
“Asante kwa ujumbe huo, maana nina muhitaji sana huyo dokta, nikimpata nitafurahi kwakweli. Nahitaji kuongea nae, haya jambo lingine ulilotaka kuniambia?”
“Nilitaka kukuona tu, ili niridhike na moyo wangu, hivi kweli Erick ungekuwa bega kwa bega na mimi kipindi kile haya yote yangetokea? Nina uhakika kusingekuwa na kitu kama hiki”
Baba Angel alimuaga pale na kuondoka zake, ila ujumbe kuwa dokta Jimmy yupo, aliupenda kwani aliona itakuwa ni rahisi zaidi kumfatilia dokta huyo.

Mama Angel akiwa yupo nyumbani kwake, alikuwa akijiandaa kwa muda huo na yeye aweze kutoka ila alifika pale Elly na kufanya aongee nae, Elly alimsalimia pale mama Angel na kuanza kuongea nae,
“Hujaenda shule leo Elly?”
“Sina raha ya kuwa shule kabisa, sina amani wala sina furaha”
“Tatizo ni nini kwani Elly?”
“Nimekaa na kutafakari siku zote hizi ila sina raha, nilimsikia wazi mama akiongea kuwa mimi sio mtoto wake. Roho inaniuma, inamaana aliniokota au kitu gani? Je wazazi wangu wako wapi? Na yule uliyenipeleka anayesema yeye ni baba yangu ni nani? Nimechanganyikiwa nahitaji kujua”
Mama Angel akapumua kidogo, basi alimwambia Elly amsubirie pale sebleni halafu yeye alienda chumbani moja kwa moja kumpigia simu madam Oliva kwani alitaka amkutanishe na Elly halafu aone itakuwaje maana alikuwa akiamini damu ni nzito. Alimpigia na kuanza kuongea nae,
“Madam Oliva, upo wapi leo?”
“Nilikuwa shuleni, ila muda sio mrefu nitakuwa kwenye saluni yangu”
“Aaaah basi nakuja huko kwenye saluni yako”
Basi mama Angel alikata ile simu na moja kwa moja alienda kuongea na Elly pale na kumtaka waende mahali, basi Elly alikubali yani kwa kipindi hiko hata shule alikuwa akiiona chungu yani hadi mama Angel alikuwa akimuhurumia sana.
Basi walifika mpaka kwenye saluni ya madam Oliva ambapo naye ndio alikuwa anafika, basi mama Angel alimsogeza Elly pale kwa madam Oliva na kumtambulisha,
“Huyu anaitwa Elly ni mtoto wa ndugu yangu”
“Ooooh sawa, nashukuru kumfahamu”
Kisha mama Angel akamwambia Elly akamsubiri kwenye gari yake ambapo Elly alifanya hivyo, halafu mama Angel alianza kuongea na madam Oliva sasa,
“Unapomuona huyu Elly unahisi anafanana na nani?”
“Mmmmh nimemfananisha na Derrick ujue, yani kafanana na Derrick kweli tena!!”
Mama Angel akapumua kidogo na kusema,
“Hujakosea, ni kweli yule Elly ni mtoto wa Derrick”
“Aaaah ndio mtoto aliyezaa na Manka eeeh!! Au alizaa na mwanamke mwingine tena?”
Mama Angel alikaa kimya kwa muda kwani alikuwa akitafuta la kuongea pale, kisha akamwambia kitu,
“Unajua nini, ile hospitali ambayo wewe ulijifungua ndio hospitali niliyojifungua mimi”
“Halafu nasikia imefungwa eti, ila sijui kwasababu gani?”
“Baba Angel alienda pale, na kuambiwa kuwa ile hospitali imefungwa sababu kuna watu hao wanadai kuwa walibadilishiwa watoto pale hospitali, kwahiyo wanahitaji kufahamu watoto wao halisi, halafu yule daktari kashindwa kuwaonyesha watoto halisi wa wale watu, halafu sijui kuna skendo zipi zingine zimefanya ile hospitali kufungwa”
“Mmmmmh mbona unanitisha? Ile hospitali walikuwa wanabadilisha watoto?”
“Ndio, nilivyosikia hivyo”
“Hivi kweli nije kusikia kuwa Paul wangu sio mtoto wangu wa kumzaa jamani? Wanaume ndio wanasingiziwaga watoto, kumbe na wanawake tunabadilishiwa watoto! Ila haiwezekani, Paul ni mwanangu”
“Sijakwambia Paul sio mwanao ila ile hospitali inatakiwa kufanya uchunguzi wa hali ya juu, wote tuliozalia pale inatakiwa tujitathimini”
“Kwani wewe huwa unahisi watoto wako sio wako?”
“Mmmmh hapana, wale ni watoto wangu”
“Sasa tuchunguze nini? Mimi hata naogopa kuchunguza. Nipate habari kuwa Paul sio mwanangu, hapana kwakweli sitaweza kuifanyia kazi hiyo habari. Nampenda sana mwanangu”
Mama Angel akapumua tena kidogo, ila hakutaka kuongea zaidi, basi alimuaga na kudai kuwa alienda pale kumsalimia tu.
Aliondoka moja kwa moja kwenda kwenye gari lake na pale alimkuta Elly amekaa tu huku kajiinamia, basi akaondoka nae mahali hapo na moja kwa moja alienda nae kwa Derrick kwani alijua ni wazi kule Elly ataweza kujihisi vizuri, ila kitu ambacho hakuelewa ni kwanini hata madam Oliva hajaonyesha tofauti yoyote ya kutamani hata kuwa karibu na Elly.
Basi walifika nyumbani kwakina Derrick, kwakweli siku hizi Derrick alikuwa kabadilika sana, kwani muda wote utamkuta akijishughulisha tu na kazi mbalimbali, alifurahi sana kuona mama Angel kampelekea tena mwanae, basi akamuomba jambo moja mama Angel,
“Naomba leo uniache na huyu kijana, naomba uniache nae niongee nae halafu kuna kitu nitakwambia”
“Hakuna tatizo, ngoja nimuulize Elly mwenyewe kama yupo tayari”
Mama Angel alimuuliza Elly, kiukweli Elly alikuwa akihitaji mtu wa kuongea nae kwa ukaribu zaidi kwahiyo alikubali kwa haraka sana kukaa hapo na kushinda na Derrick. Basi mama Angel akampatia tu pesa kidogo Elly kuwa akihitaji kurudi basi atakuwa na nauli kabisa, kisha mama Angel aliondoka zake na kurudi nyumbani kwake kwa muda huo.

Mama Angel kabla hajarudi nyumbani kwake, aliamua kwanza kupitia ofisini kwake maana hakwenda kwa siku kadhaa kidogo, basi alipitia na kuangalia mambo ya pale yanaendaje kisha alipomaliza aliamua kuondoka zake, ila wakati anatoka ofisini kwake tu, alikutana na rafiki yake Dora na kuanza kusalimiana nae ambapo waliingia tena ofisini na kuongea mawili matatu,
“Kheee siku hizi hushikiki ndugu yangu yani hupatikani kabisa”
“Jamani mbona nipo ndugu yangu”
“Sasa ndugu yangu, kuna siku nimemuona binti mmoja uwiiii umefanana nae jamani, kweli duniani wawili wawili”
Mama Angel alicheka na kuuliza,
“Nani huyo?”
“Sijui anaitwa nani, ila yote tisa kumi jana nimemuona tena yule mwanamke wa kuitwa Manka, yani yule anajidai na mali za mzee Jimmy ujue”
“Mmmh!!”
“Ndio hivyo, mzee Jimmy mpuuzi alimpenda sana yule mwanamke sijui alimpendea nini ila nahisi kuna mambo ambayo mzee Jimmy alikuwa akiyafanya halafu yule mwanamke anayafahamu vizuri. Hivi unamfahamu kwanza huyo Manka?”
“Mmmmh simfahamu, ndio kwanza nilikusikia wewe”
Mama Angel aliamua kujibalaguza,
“Ni hivi, ni mweupe peee peee, yani ule weupe umefanya awe mzuri sana. Kwakweli Manka ni mzuri ila bado mimi ni mzuri zaidi”
Dora alicheka na mama Angel alicheka pia, kisha Dora aliendelea kuongea,
“Kuna gari nimemuona analiendesha, kwakweli yule mwanamke kachukua mali nyingi sana za mzee Jimmy. Ila nadhani Manka alikuwa haelewi akili za mzee Jimmy zilivyo, yule mzee hawezi kukufanyia kitu ambacho badae hutokuja kukijutia, yani lazima anakufanyia mazuri halafu na majuto anakuandalia”
“Mmmh kama yapi? Sasa majuto gani atampa huyo Manka? Ukiangalia mzee Jimmy alishakufa, na kama mali kashampa huyo Manka!”
“Nakwambia hivi, mzee Jimmy ni baba mkwe wako ila hufahamu vitu vingi sana vya yule mzee. Kwanza lile zee ndio lilinipa mimi ukimwi halafu anasingizia mimi ndio nilimpa ukimwi, mzee ana mipango yule. Amekufa ndio ila aliowaacha huku nyuma sijui tu, ila yule Manka atakuwa anajua vizuri sana maana alikuwa karibu sana na mzee Jimmy”
“Itabidi tumfatilie huyo Manka vizuri ili tujue mambo ya mzee Jimmy, usikute kuna mengi nyuma ya pazia”
Mama Angel aliongea na Dora pale, hadi waliagana na kuondoka, ambapo mama Angel alimpeleka Dora hadi mahali karibu na kwake halafu yeye akaondoka zake, yani mama Angel kuna jambo jipya liliingia kwenye akili yake kuwa mama Sarah anafahamu vitu vingi sana vya mzee Jimmy ila hakujua kama mwanamke huyu anaweza kukaa chini na kuwaambia chochote kile.

Erica aliporudi kutoka shuleni leo, moja kwa moja alienda kumsaidia kazi mbalimbali za mule ndani kwao Vaileth huku akimuuliza,
“Ila dada kwanini jana ukaenda kuchukua chapati kwa yule mwanamke jamani! Si ungesema nikusaidie kupika?”
“Ila zingine nilipika”
“Humu ndani unajua watu wake vizirani, baba kagoma, Erick nae akagoma hadi kuja kuniambia nikamsongee ugali”
“Ila upo vizuri sana Erica, una roho nzuri sana wewe mtoto”
Kuna mgeni walisikia amefika pale kwao wakiwa jikoni, basi Erica alitoka na kwenda kumsikiliza huyo mgeni, akakuta ni Rahim yani baba yake Samia, basi alimsalimia na kumsahngaa,
“Kheee mbona umekuja kwetu?”
“Kwani vibaya mimi kuja kwenu?”
“Hapana”
“Nimekuja kumuulizia Samia, amefika huku”
Erica alishangaa kwa yule baba kumuulizia Samia kwa muda ule wakati Samia anamsimuliaga mambo yote ya yule baba, kwahiyo Erica alibaki akimuangalia kwa muda tu, mara mama Angel nae alitoka ndani, kwakweli mama Angel alipomuona Rahim pale kwanza hakupenda pili alishtuka kiasi na kumtaka Erica akaendelee na kazi zingine kisha alitoka nje na Rahim,
“Umefata nini nyumbani kwangu?”
“Nimekuja kumuulizia binti yangu Samia”
“Khaaa jamani, lini Samia wako kaja huku kwa muda huu! Hebu nenda kamfatilia huko, halafu giza linakaribia kuingia”
“Kiukweli sio Samia aliyenileta hapa, ila nilitaka tu kukuona”
“Unajua wewe una wazimu eeeh!! Akili zako kuna muda zinaenda na kurudi. Jichunguze. Kwaheri”
Mama Angel alitaka kurudi ndani ila Rahim alimvuta, na wakati huu alimvuta karibu na kumkumbatia, baba Angel alikuwa nae ameingia na alichukia sana akasogea pale na kumsukuma Rahim chini, kumbe muda ule Erica alikuwa akichungulia dirishani kwahiyo alikuwa akiona kinachoendelea.
Rahim aliinuka pale chini na kutikisa kihwa tu halafu akamwambia baba Angel,
“Dawa yako inachemka sijui sura yako utaificha wapi? Siku zote mwanaume wa kwanza kuzaa na huyo mwanamke basi huyo ndio mumewe, nakuhurumia sana kuchukua mizigo usiyoijua”
Baba Angel alichukia sana na kutaka kumfata Rahim ila mke wake alimshika na kumsihi waende ndani, wakati huo Rahim alisogea getini na kutoka nje na kuondoka kabisa.
Mama Angel aliingia na mumewe ndani hadi chumbani ili kumshusha zile hasira,
“Hizi huyu Rahim ananitakia nini mimi na familia yangu?”
“Naomba uachane nae tu mume wangu, asituumize kichwa huyu kabisa, tuwaze mambo mengine tu”
“Eti mtu wa kwanza kuzaa na huyo mwanamke ndio mumewe, kwahiyo yeye ni mume wa wanawake wangapi maana wengi kawazalisha, akili mbovu kabisa yule mtu jamani!! Sijui kama kuna siku ugomvi wangu na ugomvi wa Rahim utakuja kuisha”
“Naamini mambo yataisha haya na kila kitu kitakuwa sawa”
Mama Angel alijitahidi pale kushusha hasira za mume wake kwani alionekana kuchukia sana kwa muda huo.

Mama Angel alihitaji kujua kuwa Erica alikuwa akiongea nini mwanzoni na Rahim, basi alimfata Erica chumbani kwake, na kumkuta kajiinamia tu basi akamfata na kumuuliza,
“Tatizo nini mwanangu, mbona umejiinamia tu?”
Kabla ya kujibu, Erica alimuuliza swali mama yake,
“Mama, hivi Erick kachukua hasira za baba eeeh!”
“Kwanini umeniuliza hivyo?”
“Kuna siku tulikuwa njiani na Erick ila aliwasikia wamama Fulani wakitusema vibaya, basi Erick alienda kumpiga ngumi moja mama yule, halafu hataki kuondoka yani anataka kupambana nao wote, kuna siku nyingine kwa mama Sarah, wakati mama Sarah akimsema vibaya, uwiii Erick alitaka kumpiga ngumi mama Sarah hadi nikamzuia. Nimemuona baba leo akimsukuma baba Samia kwa hasira, kumbe hasira za Erick ni za baba?”
“Eeeh ndio, kafata hasira za baba yako. Ila na wewe Erica ni mbea jamani, kuchungulia nje ndio nini? Yani mtoto mbea wewe sijapata kuona”
“Ila mama, kwani umbea huu nimerithi wapi?”
“Sijui wewe na Mungu wako maana kwetu wala kwa baba yenu hakuna wambea kama wewe”
“Mmmh mama au mimi sio mtoto wenu?”
Erica alisema hivyo huku akiinama chini inaonekana ni kitu kilichoanza kumsumbua akili, basi mama yake alimuangalia vizuri na kuanza kuhisi kuwa labda zile mada za kubadilisha watoto basi moja kwa moja zimemfikia Erica, ukizingatia ni mbea sana, basi mama Angel akamuuliza Erica,
“Kwanini umesema hivyo?”
“Sijui mama, sijui ila kama sijarithi tabia zenu huenda mimi sio mtoto wenu”
“Erica, najua ni umbea wako ndio umepelekea kuanza kusema hayo. Najua huwa unasikia mimi na baba yako tukizungumzia kuhusu watoto waliobadilishwa hospitali, ila hii haihusiani kabisa na nyie watoto wangu. Kwani wewe unajiona ni tofauti?”
“Sijui mama, ila Erick kafanana na baba hasira, ila mimi umbea nimefanana na nani?”
“Sikia Erica, sio kila kitu utafanana na wazazi. Hebu fikiria ni watu wangapi wakikuona wanasema kuwa wewe ni mwanangu! Hata ambao hawajui kuwa mama yako ni mimi ila watakwambia wazi kuwa mama yako ni Erica eeeh! Sababu mimi na wewe tumefanana, na tumefanana vitu vingi sana, mfano kwenye kupika unafikiri umerithi kwanani kupenda kupika? Umerithi kwangu, huo umbea umerithi kwa mjomba wako mmoja hivi ni mbea sana, kuna siku nitakuonyesha pacha wako Erica”
Kisha mama Angel akasogea na kumkumbatia mwanae, akajua zile habari ambazo huwa anaongea na mumewe basi zimefika kwa mbea wake mashuhuri wa mule ndani, basi aliongea nae kidogo tu, mwisho wa siku hata hakumuuliza kuhusu alichokuwa akiongea na Rahim zaidi ya kumuaga tu usiku mwema na kuachana nae.

Mama Angel aliporudi chumbani kwa mumewe, aliamua kumueleza kile alichozungumza na Dora siku hiyo kuhusu Manka,
“Inamaana Manka atakuwa anafahamu vitu vingi sana vya baba yangu?”
“Ndio, yani hapo ni wazi kabisa kuwa Manka anafahamu vitu vingi sana kuhusu mzee Jimmy”
“Sasa tutawezaje kupata ukweli toka kwa Manka?”
“Hapo ndio pagumu ila kama tukiamua basi tutaweza tu kugundua ukweli wa mambo ulivyo”
Basi baba Angel alimgusia pia na swala la Sia kumuona dokta Jimmy,
“Ila yule Sia ni chizi sema tukimtumia kwa hili tutaweza kufanikiwa, yani kama tukimwambia Sia afatilie kuhusu dokta Jimmy anaweza yule na uchizi wake”
“Ni kweli, ila kesho nitaenda tena pale hospitali kuna kitu nimefikiria”
Baba Angel aliongea na mke wake kuhusu mipango yake na kwa muda huo waliamua tu kulala.
Kulipokucha baba Angel alijiandaa na kuondoka ile asubuhi na mapema kabisa maana alisema atapitia kwanza ofisini kwake halafu ndio ataenda kwenye ile hospitali kufatilia.

Mama Angel akiwa nyumbani kwake kwa muda huo, alitembelewa na wifi yake Tumaini basi alisalimiana nae na kuanza kuongea nae pale,
“Nikwambia mambo yaliyopo nyumbani kwa mama Sarah”
“Mambo gani tena?”
“Yule Sarah si ndio tulihangaika nae kipindi kile kwa kuchoma sindano ya uzazi wa mpango wakati ni mjamzito hadi mimba ikatoka”
“Ndio, ila kwasasa anaendelea vizuri”
“Ndio, ila yule mdada wao wa kazi nae kaenda kuchoma sindano ya uzazi wa mpango wakati ana mimba basi imemsumbua alilazwa na mimba imetoka”
Mama Angel alikumbuka mambo ambayo Elly alimwambia, basi moja kwa moja alipata jibu hapo kuwa Elly ndio muhusika wa ile mimba ya huyo dada wa Sarah pia. Ila alibaki kushangaa tu,
“Nani aliyewaambia kuwa kutoa mimba ji kuchoma sindano ya uzazi wa mpango? Wajinga hao watakufa wanajiona, huyo mdada mtu mzima nae anafanya mambo kama mtoto”
“Ndio hapo sasa, yani hata hajaona shida wala nini. Watoto wa siku hizi jamani, hapana kwakweli, haya yote tisa kumi ni mdada wangu wa kazi”
“Kafanyaje tena?”
Muda huu Vaileth alikuwa akimletea glasi ya juisi huyu shangazi yao wakina Erica, basi Tumaini alikuwa akimwambia mama Angel,
“Msichana wangu wa kazi ana mimba”
Vaileth aliangusha glasi na kufanya ile glasi ivunjike, basi wakamshangaa pale na Tumaini ndio akaanza kuongea pale,
“Wewe vipi, inaonyesha hii habari imekushtua au na wewe una mimba?”
Vaileth alikuwa kimya tu kama akimshangaa Tumaini, halafu Tumaini akasema,
“Itakuwa una mimba wewe, usije ukatuletea mambo ya Daima hapa kuwa mimba ya Junior!”
Yani Vaileth alijihisi kupatwa na baridi gafla kwenye mwili wake na kuanza kutetemeka.

Vaileth aliangusha glasi na kufanya ile glasi ivunjike, basi wakamshangaa pale na Tumaini ndio akaanza kuongea pale,
“Wewe vipi, inaonyesha hii habari imekushtua au na wewe una mimba?”
Vaileth alikuwa kimya tu kama akimshangaa Tumaini, halafu Tumaini akasema,
“Itakuwa una mimba wewe, usije ukatuletea mambo ya Daima hapa kuwa mimba ya Junior!”
Yani Vaileth alijihisi kupatwa na baridi gafla kwenye mwili wake na kuanza kutetemeka.
Mama Angel nae alimuangalia kwa makini Vaileth na kumuuliza,
“Una nini wewe? Una mimba kweli au?”
Vaileth akajibu kwa uoga,
“Hapana mama, sina mimba”
“Mbona hii mada inaonekana imekugusa sana”
“Nisamehe mama”
Kisha Vaileth akaenda kuleta tambara na kufuta pale alipoangusha glasi, basi Tumaini akamwambia mama Angel,
“Atakumalizia glasi zako huyu, kama ana mimba ondoa haraka asikuletee usiku”
“Na hiyo mimba anaitoa wapi?”
“Jamani, kwani mimba inatoka wapi? Si inatoka kwa wanaume”
“Unajua najiuliza hao wanaume Vai atakutana nao muda gani?”
“Wewe hujamuwekea gunzi huyu, unavyomtuma sokoni? Ukiwa haupo unadhani inakuwaje? Jitahidi ukampime mimba”
“Kwahiyo niende nae hospitali eeeh!!”
“Njoo na kile kikopo cha kupimia mwambie aweke mkojo wake, halafu uende ukapime. Asituletee ujinga sisi”
“Umenitisha, basi itabidi tufanye muda huu huu”
“Ndio, hawa wadada wa kazi wana siri nyingi sana. Halafu mwishowe anakuletea mabaa na mimba zao, yani ukigundua ana mimba ni nyumbani kwao moja kwa moja hakuna kumchekea wala nini. Usifanye masikhara na kulea mwanamke mjamzito”
“Naelewa, ila sidhani kama Vaileth anaweza kuwa na mimba”
“Usimkatalie wala nini, hawaaminiki hawa viumbe ujue”
“Sasa tufanyeje?”
“Ni kuchukua hatua muda huu huu, huyu msichana akapimwe mimba”
“Ila hiko kikopo cha kuchukua mkojo na kwenda nao hospitali nitakipata wapi?”
“Ngoja kwanza”
Tumaini alianza kupekua mkoba wake na kutoa kikopo ambacho huwa kinatumiwa hospitali kupima haja ndogo,
“Chukua hiki hapa, nenda kampe aweke mkojo wake humu asitutanie kabisa. Tena tutaenda wote huko hospitali kupima”
Basi mama Angel alichukua kile kikopo na kumpelekea Vaileth ili aweke haja ndogo mule.
Wakati Tumaini yupo sebleni, muda kidogo alirudi Erica kutoka shule na kumsalimia pale,
“Mbona mapema leo?”
“Naumwa tumbo shangazi”
“Wewe nawe sijui una chango jamani, kukua ndio kuumwa kila leo ukiona mambo jamani!!”
Mama Angel alitoka nae alimkuta Erica pale akilalamika kuhusu kuumwa na tumbo,
“Oooh ndiomana umewahi kurudi mwanangu, halafu si kuna zile dawa ulipewa wewe!! Hilo tumbo limekuanza tena! Pole mwanangu, nenda kapumzike kwanza halagfu nikupashie maji moto nije nikukande kidogo mwanangu”
“Asante mama”
Basi Erica aliondoka na kuwaacha wakiendelea na mazungumzo mengine.
Moja kwa moja Erica alienda chumbani kwa Vaileth na kuikingia ila akamkuta Vaileth kajiinamia tu, akilia, kwakweli huruma ilimjaa kwani hakupenda kumuona akilia haswaa kutokana na ile hali ya ujauzito aliyokuwa nayo, alimshika bega na kumwambia,
“Nini shida dada Vai?”
“Nimeambiwa nitoe mkojo ili wakanipime mimba, naogopa mimi maana ikigundulika ndio kazi sina tena”
“Lete hicho kikopo”
Halafu Erica alienda nacho chooni na kuweka haja ndogo yake halafu akampelekea vaileth kile kikopo halafu yeye alirudi chumbani kwake, kwakweli Vaileth hakuamini kile kitu aliona kama ni muujiza hivi.
Muda kidogo alifika mama Angel akidai ule mkojo ambapo Vaileth alimpatia halafu mama Angel alitoka nao kwenda sebleni ila Vaileth hakuwa na hofu yoyote tena maana kilichotendeka alikielewa vizuri sana.
 
SEHEMU YA 362


Mama Angel alipokuwa sebleni anamwambia wifi yake,
“Mkojo huu hapa, ila sasa nitaondokaje na kumuacha huyu mtoto anayeumwa? Sijui wifi utaniendea”
“Hakuna tatizo, naenda tu hapo duka la madawa kupima”
Basi muda huo huo Tumaini aliondoka na kile kikopo ili wajue kama Vaileth ana mimba kweli au la.
Basi mama Angel alibaki pale na kumuita Vaileth na kuanza kuongea nae,
“Hebu Vaileth niambie ukweli, una mimba kweli?”
“Hapana mama sina mimba”
“Usiniaibishe Vai, unajua nimempa wifi yangu akapime huku nina mashaka sana moyoni. Naomba iwe kweli maana hii aibu siitaki kwakweli”
“Kweli mama, sina mimba”
“Haya, kaendelee na kazi zako zingine”
Basi mama Angel alienda chumbani ila akapigiwa simu na Derrick muda huo huo, akapokea na kuanza kuongea ne,
“Ndio Derrick, ni nini tena?”
“Kuna kitu nimegundua kuhusu huyu Elly”
“Mmmh kitu gani hiko?”
“Huyu Elly ni mtoto wangu tena ni mwanangu kabisa, ila kila nikijaribu kumuangalia naona haendani kabisa na Oliva, sijui labda kuna mwanamke mwingine nilizaa nae, si unajua ujana tena. Kwahiyo huyo Sia anasema mamake Elly ni nani?”
“Mmmh huyo Sia hata hajui kwakweli, basi wewe hebu jaribu kupitia wanawake wote ambao uliwahi kuwa nao na pengine mmoja wapo ndio atakuwa mama wa Elly”
“Inawezekana, ila huyu ni mwanangu nina uhakika asilimia moja. Na mlivyosema hana baba basi ndio nimepata jibu wazi kuwa huyu ni mwanangu. Piga ua galagaza ila huyu ni mwanangu kabisa”
Mama Angel alikuwa akicheka tu ila akasema,
“Kama sio wa Oliva atakuwa wa nani maana kuna uhakika wa asilimia zote kuwa mtoto anayelelewa na Oliva ni mtoto wa Sia ila tu hatujamwambia kwani uchizi wake tunaujua na hatujui ni kitu gani kitatokea, kwahiyo Elly yuko wapi?”
“Kaondoka jana jioni kwenda kwa huyo mama yake Sia”
“Ila hujamwambia chochote kama Sia sio mama yake?”
“Hapana sijamwambia, ila tu nazidi kumsisitiza kuwa mimi ni baba yake ili asinichukie wala nini”
“Basi tutaongea vizuri, ila jaribu kuweka macho karibu kwa huyo mtoto ili uweze kugundua mama wa huyo mtoto ni nani”
“Nitafanya hivyo”
“Loh na wewe Derrick ulizidi jamani, hebu ona unavyohangaika! Yani wewe loh!”
Basi waliongea pale na kukata ile simu ambapo mama Angel aliamua kuendelea na mambo mengine tu.
Ila mama Angel alipigiwa simu na wifi yake na kwenda kuonana nae mahali kuhusu majibu ya Vaileth.

Baba Angel alipotoka kwenye kazi zake, moja kwa moja anaongoza kwenye ile hospitali ili ajaribu kuchunguza zaidi, basi alifika na kuanza kuongea na walinzi,
“Jamani, mimi nina shida sana na huyu dokta Jimmy, mnavyoniambia hamna mawasiliano yake mnazidi kuniachangaya”
“Ni kweli hatuna mawasiliano yake kabisa”
Mara baba Angel alishangaa mahali pale akifika madam Oliva, basi alianza kusalimiana nae pale na kuulizana kwa mshangao kuwa wote wanafanya nini pale, basi madam Oliva alianza kujieleza,
“Mimi nina shida na dokta Jimmy kwakweli, nahitaji aniambie ukweli tu kuhusu mtoto wangu, je mtoto aliyenipa ni wangu au sio wangu? Kila siku nazidi kupatwa na mawazo tu juu mambo ambayo huwa naongea na mkeo. Na wewe je umekuja kufanya nini?”
“Dah!! Mimi ni mambo mengi, unajua mke wangu nae alijifungulia hapa, nataka tu kujua ni kitu gani aliwafanya wanangu wakati wadogo, sababu nasikia kuna sindano aliwachoma”
“Kheee huyu dokta, kumbe ana makubwa kiasi hiko. Haya tutampataje sasa?”
Baba Angel na madam Oliva walijadiliana kwa muda kidogo na kisha madam Oliva akasema kitu,
“Nina uhakika kwa asilimia kubwa hawa walinzi watakuwa wanajua huyu dokta alipoa”
“Wanasema hawajui”
Madam Oliva aliwauliza pia, na walimjibu vile vile ambavyo walimjibu baba Angel, basi madam Oliva akawaambia,
“Sikieni, ni nani aliyewaajiri kulinda hapa na ni nani anayewalipa mishahara yenu?”
“Mdogo wake dokta Jimmy”
“Ni nani huyo?”
Wale walinzi walitoa zile namba za mdogo wake dokta Jimmy na kuwaambia kuwa wamtafute huyo ndio atawajulisha, kwa muda huo walimpigia simu ila iliita sana hadi ilikatika, basi wakapanga kumpigia tena kwa muda mwingine, kisha baba Angel na madam Oliva waliagana na kila mmoja kuondoka zake.
Kwakweli baba Angel alikuwa na mawazo sana, hivyobasi moja kwa moja alienda nyumbani kwake, na alipofika hakumkuta mke wake maana alikuwa kwa muda huo ametoka.
Akaagiza chakula tu, ambapo Vaileth alimuwekea chakula na alijitahidi na kula kile chakula huku akijiuliza baadhi ya vitu kwenye kichwa chake.
Baba Angel aliamua kwenda kujilaza kwa muda huo, ila muda kidogo mkewe alirudi na kuanza kuongea nae,
“Ulienda kwenye kazi leo?”
“Haoana, ila Tumaini alikuja hapa”
Basi mama Angel alianza kumueleza mumewe kuhusu hofu ya Tumaini ya kusema kuwa Vaileth ni mjamzito,
“Ila yale majibu aliyoniitia ni kwamba Vai hana mimba, nimeshukuru sana kwakweli. Maana sipati picha ambavyo Tumaini angenisema”
“Oooh dada yangu nae muda mwingine, anajijuaga mwenyewe”
“Haya yote tisa, kumi ni kuwa kule aliponiita Tumaini kuna jambo jipya nimeedna kukutana nalo”
“Jambo gani hilo?”
“Unamkumbuka Moses? Yule Moses aliyekuwa akiuza duka lako kipindi kile? Yule Moses ambaye mimi nilijua ndio mmliki halali wa lile duka lako mpaka akampenda Angel na kufanya Angel awe balozi wa duka lako unamkumbuka?”
“Namkumbuka ndio, alikuwa ni muaminifu sana yule mtu”
“Unajua yuko wapi siku hizi?”
“Hilo sijui maana sijawasiliana nae siku nyingi sana toka kipindi kile alivyoondoka wala sijawasiliana nae tena”
“Jamani, leo nimemuona. Moses kawa Moses kweli, kwanza kanenepa sana, nimumuona kwenye gari nzuri ya gharama anatembelea, inaonyesha Moses ana maisha mazuri sana kwasasa, sikuweza kuongea nae maana anaonekana alikuwa na haraka, kabadilika hatari”
“Yeye alikuona?”
“Hapana, yani alikuwa na haraka huyo. Jamani Moses kabadilika, na nisingemkumbuka bila Tumaini kunikumbusha jamani, Moses kawa Moses kweli. Ana mali nyingi, pesa nyingi. Gari aliyokuwa nayo ni zile gari nzuri za gharama”
“Kama ya pesa ngapi?”
“Mmmh ile gari kama milioni mia tano”
“Duh!! Kweli huyo katoka kimaisha, kapata wapi hela yote hiyo?”
“Duniani kuna mambo unajua vitu vingine sio vizuri kuviwaza ila mtu unaviwaza na kuona mmmh kuna kitu katikati. Hebu fikiria jambo Fulani, lile duka lako ni Moses ndio alikuwa amelishikilia vilivyo yani hakuna kilichokuwa kinafanyika bila yeye. Halafu kumbuka kuwa lile duka ulilifunga na kuacha biashara ile baada ya Moses kuondoka pale, hapo akili kichwani mwako”
“Si unajua tuliibiwa pale”
“Mmmmh mume wangu, ukifikiria zaidi utayaona mambo ya Derrick ujue kwenye hili!!”
Baba Angel aliwaza kiasi na kuona ataumia kichwa zaidi, basi alibadili mada na kuanza kuongea mengine na mke wake.

Basi Vaileth akiwa anamalizia zile kazi za Usiku, alifika mama Angel na kumwambia kuhusu majibu ya ile mimba yake,
“Kwanza Vai, nakushukuru kwa kuwa msichana bora kwangu. Yani nilijua kweli u mjamzito, oooh nimefurahi sana Vaileth”
“Nashukuru kwa kuniamini mama”
Basi mama Angel alimuaga Vaileth na kuondoka zake, ambapo moja kwa moja Vaileth alienda chumbani kwa Erica ili akamshukuru kwa kile alichomfanyia, ila alipofika kabla hajaingia alikuta mlango wa Erica haujafungwa vizuri basi alisimama na kuangalia kinachotendeka, ambapo alimuona Erick akimpa huduma Erica yani alikuwa akimkanda tumbo lile lililokuwa linamuuma, basi Vaileth aliangalia sana na kujisemea,
“Hawa watoto mbona wana mambo ya ajabu sana, mapacha gani hawa wanafanya hivi. Yani kama wapenzi vile mmmh!!”
Aliendelea kuwaangalia ila mwishowe aligonga na kukaribishwa ndani, aliingia na kuwasalimia pale huku akisema anataka kuongea na Erica,
“Unataka kuniambia nini kwani? Niambie tu”
“Nataka niongee na wewe peke yako”
Erica alicheka kidogo na kusema,
“Unamuogopa Erick? Unamuogopa bure tu maana hata ukiniambia peke yangu basi nitaenda kumwambia tu”
Erica alicheka tena, yani inamaana kuwa umbea wake alishaukubali kwa asilimia zote, ni kweli Vaileth aliona hata akimwambia Erica peke yake basi ile habari lazima moja kwa moja itafika kwa Erick, basi alimwambia,
“Asante sana kw akuniokoa siku ya leo”
“Usinishukuru mimi, mshukuru Mungu aliyenirudisha nyumbani kwani aliniotesha kuwa leo siri itabumbuluka ndiomana nilivyofika tu nilianza kuja chumbani kwako”
Vaileth alimuangalia Erick na Erica kwa aibu ila bado aliendelea kumshukuru Erica kisha Erica akamwambia,
“Ninachotaka ni huyo mtoto azaliwe, halafu sisi tutalea. Si mtoto wa ndugu yetu, kwahiyo ni damu yetu. Si eti Erick tutalea eeeh!”
“Ndio tutalea”
Vaileth aliwashukuru tu pale kwa aibu na kuondoka zake maana alihisi kuaibika sana kwa wakati huo.

Siku ya leo, kuna jambo linamjia sana kichwani anaona ni vyema kama akipanga safari na kwenda kuongea na mama Sarah, basi alijiandaa na kuondoka nyumbani kwake moja kwa moja kuelekea kwa mama Sarah.
Mama Angel alipofika pale tu alimkuta mama Sarah akiendelea na mambo yake mengine kwani kwa siku hiyo alipanga kutoka jioni ndiomana hadi muda huo alikuwepo nyumbani kwake.
Mama Sarah alipomuona alimkaribisha vizuri tu ila alitoka nae nje na kumwambia,
“Najua lazima kuna mada umekuja kuongea nami, haya tuongee hapa nje”
“Asante, kuna mambo nahitaji kukuuliza ili niyajue”
“Mambo gani tena hayo? Kuhusu baba mzazi wa Sarah au kitu gani?”
“Hapana, siwezi kuuliza kuhusu baba wa Sarah wakati inajulikana wazi, huyu Sarah ni mtoto wa nani. Ila ninachotaka kuuliza ni kuhusu mzee Jimmy”
“Unataka kusikia nini kuhusu mzee Jimmy?”
“Nahitaji kujua ukweli tu, ni kitu gani kipo kati yako na mzee Jimmy!”
“Hivi una wazimu wewe? Mzee Jimmy alikuwa kwangu kama Erick alivyo kwako nadhani unanielewa kwa hilo. Nadhani pia unanielea nikisema kuwa mzee Jimmy ni baba wa Sarah”
“Usibadilishe mada Manka, kuna vitu vingi mzee Jimmy alivifanya ambavyo sio sahihi kwakweli, lazima wewe unaelewa mambo mengi sana yaliyofanywa na mzee Jimmy kabla ya umauti wake. Naomba uniambie”
“Hivi Erica unachekesha sana, naanzaje mimi kukwambia kuhusu mzee Jimmy, kabisa mimi nikwambie wewe jamani!! NI mzima kweli wewe? Ni hivi, kwanza mrudishe Elly hapa kwangu ndio uongee huo utumbo wako”
“Huyo Elly anarudi vipi kwako? Unajua ni kwanini kaondoka?”
“Nitajuaje ikiwa wewe ndio umemchukua bila ruhusa yangu”
“Kwanza tambua Elly na Sarah ni mtu na dada yake maana wote ni watoto wa Derrick”
“Kama mtu na dada yake kuna ubaya gani wakiishi nyumba moja? Si ndio undugu wao utajengeka zaidi”
Mama Angel alimuangalia mama Sarah kwa hasira kidogo na kumjibu,
“Huo undugu utajengwa vipi, ikiwa watoto wanatamaniana? Unajua kama mimba ya Sarah iliyotoka ni mimba ya Elly?”
Mama Sarah alishangaa sana kwani kitu hiki hakukijua kabisa, siku zote alikuwa akimuhisi vibaya Erick sasa kuambiwa kuwa ni Elly alishangaa sana.
“Kumbe ni Elly, haya nashukuru kufahamu. Mama Angel naomba uondoke nyumbani kwangu”
Mama Angel hakuongea zaidi, kwani aliamua kuondoka tu kwa muda huo kuelekea nyumbani kwake.

Mama Angel alipokuwa njiani aliona kuwa mama Sarah anaweza kwenda kumfanyia fujo Sia, kwahiyo aliona ni vyema kwenda kumwambia Sia ukweli, ila alijilaumua sana kuwa kwanini kamwambia mama Sarah ukweli ulivyo.
Moja kwa moja mama Angel alienda kwenye biashara ya Sia na kuanza kuongea nae,
“Kheee kwahiyo Elly alimpa mimba Sarah?”
“Ndio hivyo”
“Kweli Elly sio mtoto wangu, ni lazima atakuwa mtoto wa huyo huyo asiyejielewa Derrick. Haiwezekani mwanangu akawa Elly halafu akafanya ujinga namna hiyo kwa jinsi ninavyomfundisha kuhusu kuwa mtoto mwema halafu akafanye huo ujinga jamani!!”
“Hapana, yule kalazimishwa tu na huyo Sarah wala sio kosa lake, ndiomana nilivyoenda aliniomba niondoke nae”
“Kheee hako kaSarah nako kahuni kama mama yake, kweli mtoto wa nyoka ni nyoka tu. Ila na wewe ulifata nini kwa mama Sarah?”
“Nilihitaji kuongea nae kwani yeye anafahamu vitu vingi sana kuhusu mzee Jimmy”
“Aaaah kumbe!!”
Mama Angel alimueleza Sia kwa kifupi tu kuhusu mama Sarah na mzee Jimmy, ila Sia alishaelewa kwa haraka sana, kisha mama Angel akamwambia tena,
“Usimfokee Elly, ila ujue jinsi ya kumlinda ili huyo Manka asiweze kufanya chochote kwa Elly maana ana hasira sana yule mwanamke. Halafu wewe ingawa Elly sio mwanao ila kumbuka umemlea Elly kwa kila hali akijua kuwa wewe ndiye mama yake basi kuwa nae kwa makini sana hata akija kuujua ukweli bado aendelee kukuthamini kama ambavyo anakuthamini sasa”
“Nimeelewa, siwezi kumtupa Elly kwakweli”
Basi mama Angel aliamua kuondoka tu kwa muda huo na kumuacha Sia pale.

Muda ule ule Sia aliondoka na moja kwa moja kwenda ofisini kwa baba Angel, kwani yeye huwa akifikiria kitu anahisi ni rahisi zaidi kusaidiwa na baba Angel kuliko mtu mwingine yoyote.
Alimkuta pale na kuanza kuongea nae,
“Erick kuna kitu nataka kukwambia”
“Kitu gani hiko?”
Sia alianza kumueleza kile ambacho aliongea na mama Angel kwa siku hiyo, kisha alimwambia baba Angel,
“Unajua kwanini nimekwambia yote haya?”
“Ili nikuone wewe na mke wangu mnapatana siku hizi”
“Hapana sio sababu hiyo, unajua mimi sio mbaya wa Erica wala nini. Mapenzi yangu kwako ndio yalikuwa kitu kibaya kwa Erica. Ila tuachane na hayo, nimekueleza yale kwasababu kubwa moja, kama mama Sarah yani Manka ndiye anayefahamu vitu vingi kumuhusu mzee Jimmy, basi njia pekee ya kupata siri hizo ni kwa kupitia wewe”
“Mmmmh kwa kupitia mimi kivipi?”
“Yani wewe ndio uwe karibu na mama Sarah, wewe nio umuulize kwa hakika atakwambia ukweli wa kila kitu na atakuweka wazi kwa kila kitu klabisa”
“Mmmh!”
“Ni kweli sababu aliwahi kukupenda”
“Hiyo sio sababu, aliwahi kunipenda ndio, ila sio kwasasa ambapo kila mtu ana masisha yake. Ila nitajaribu kumdadisi”
“Ila nimekumbuka kitu, naomba unisamehe sana kwa kuchelewa kukwambia kuhusu jambo hili, ni hivi kuhusu wewe kuwekewe sumu ni huyo huyo Manka ndio muhusika mkuu ila usinitaje kama nimesema”
“Unaongelea nini? Sikuelewi”
“Kipindi kile ulipopewa sumu, nilifatilia na kugundua kuwa ile sumu uliipata kwenye matunda ambayo ulipewa na huyo mama anayewauzia matunda nje hapo, ila yule mama sio kwamba yeye ndio alikuwekea sumu! Hapana, yule mama alitumwa na huyo Manka kukupa yale matunda ambayo yalikuwa na sumu tayari. Nilipokuwa nachunguza, ndipo Manka mwenyewe akanibamba na kunipa onyo kali sana kuwa nisifatilie maisha yake, ukizingatia yeye ndio anamsomesha mtoto wangu, basi sikuwa na namna yoyote ya kutenda zaidi ya kukubaliana na hali halisi tu ya kutokufatilia maisha yake, na niliogopa kuja kukwambia ukweli. Ila kuwa nae makini sana”
“Duh!! Kumbe Manka alifikia hatua hiyo! Sikufikiria kwakweli, huyo mama nae muuza matunda aliwezaje kukubali matunda kwa mtu na kuniletea mimi!!”
“Aliahidiwa hela ya mtaji ndiomana alifanya vile, unajua sisi masikini huwa tunajikuta tunatenda vitu vingine na kuja kujutia badae”
“Umasikini gani wa kuniwekea sumu? Ningekufa je! Ndio angesema umasikini wake umeniua au? Kwanza masikini unawajua vizuri au? Mfano kama wewe, mambo mengine huwa unayataka mwenyewe, hivi Sia uambiwe jambo kama hilo uje kunitendea mimi sababu umeahidiwa hela hiyo ni sawa kweli? Mwishowe usingizie umasikini! Umeauza mtoto umesingizia umasikini, halafu kwasasa unataka kuniambia kumuwekea mtu sumu ni umasikini kweli!!”
“Hapana mimi siwezi kuweka sumu, hata kama nina shida kiasi gani siwezi kufanya hivyo, hata yule mama nina uhakika asilimia zote hakujua kama ni sumu. Yani kuna kitu kingine mtu unaamua kusema kuwa hizi shida zinimalize ila sio nifikie hatua ya kutoa uhai wa mtu sababu ya pesa, hiyo ni tamaa tu, mtu awe na pesa au asiwe nazo ila akiingiwa na tamaa ya hivyo basi atafanya tu”
“Na kwasasa uache kusingizia umasikini basi, lini umekwama kwenye biashara ukaniambia nikaacha kukusaidia? Mimi nipo vizuri sana ila huwa sipendi tu uchizi wako ambao ukiuanzisha hadi zimamoto waje kuuzima. Kitu kingine nakushukuru kwa uchunguzi wako. Nakupa kazi nyingine, ukimuona dokta Jimmy popote pale naomba umfatilie hadi tumpate kwani ana mengi sana ya kujibu, licha ya kubadilisha watoto ila kuna mengi anatakiwa kujibu”
“Sawa, hakuna tatizo”
Baba Angel leo alimpa na hela kidogo Sia, ambapo Sia alifuirahi sana na kumuaga halafu akaondoka zake ambapo cha kwanza kabisa alienda kwa yule mama muuza matunda ingawa aliwahi kukatazwa na mama Sarah.
Alimkuta pale yule bibi akiendelea na mambo yake na kumsalimia pale kisha alianza kuongea nae,
“Vipi ulishapewa mtaji?”
“Mmmh ndugu yangu, yamenishinda”
“Kwanini?”
“Kuna siku yule tajiri alikuja na chakula kizuri sana alisema nimpelekee bosi Erick, nikamwambia kuwa bosi Erick siku hizi hata matunda yangu hali, akaniambia kuwa bosi akiona kile chakula atakipenda na kukila tena nisiondoke hadi amalize kula. Kisha akanipa laki moja ya kufanya hivyo, mmmh niliogopa yani kazi ya kupeleka chakula tu ndio anipe laki moja! Nikamwambia kuwa siwezi kufanya vile, alichukia na wala hakuniambia kitu zaidi zaidi aliondoka na hela yake na chakula chake”
“Duh! Pole sana, yani mabosi wana mambo sana”
Basi Sia alimuaga yule mama ila pale alipata kitu kuwa bado mama Sarah anaendelea kumfatilia baba Angel, ila tu hakujua ni kwasababu ipi.

Usiku wa siku hii, mama Angel alikuwa akiongea na mume wake kuhusu yaliyojiri yani vile alivyoenda kwa mama Sarah kwahiyo aliongea nae vitu vilivyotokea pale, kisha baba Angel alimwambia ushauri aliopewa na Sia na jinsi Sia alivyomwambia kuhusu mama Sarah na kufanya mama Angel ashtuke kiasi,
“Mmmh hata usimfatilie, kumbe ni yeye aliyetaka kukuwekea sumu?”
“Ndio, yani Sia kanihakikishia kila kitu”
Muda kidogo simu ya baba Angel ilianza kuita, kuangalia mpigaji ni madam Oliva ila alipokea tu hivyo hivyo,
“Samahani kwa kukupigia usiku huu”
“Bila samahani, nini tatizo madam”
“Kuna mlinzi niliongea nae, nilimwambia kuwa mdogo wake dokta Jimmy akienda anipe taarifa, anasema kuwa kaongea nae huyo mdogo wake dokta Jimmy kasema anaenda kesho. Kwahiyo kama inawezekana twende kesho”
“Sawa hakuna tatizo, itabidi kesho twende”
Baba Angel aliongea na mke wake kuhusu jambo hilo, mama Angel aliona ni vyema kwa mume wake kufanya vile na alimsapoti kwa jambo lile.

Leo baba Angel alijiandaa na kuwasiliana na madam Oliva kisha alimpitia na kuondoka pamoja nae kuelekea kwenye ile hospitali.
Na kweli waliwakuta walinzi, na huyo mdogo wake dokta Jimmy anaonekana nae alifika ile asubuhi maana huwa sio mkaaji wa eneo lile.
Basi wakina baba Angel walionyeshwa tu na kumsogelea ambapo huyo mdogo wake dokta Jimmy alikuwa kawapa mgongo kwa muda huo, basi walimsalimia pale ambapo aligeuka na kuwatazama ila baba Angel na yule mdogo wake dokta Jimmy walishangaana kwani ni watu wanaofahamiana.

Basi wakina baba Angel walionyeshwa tu na kumsogelea ambapo huyo mdogo wake dokta Jimmy alikuwa kawapa mgongo kwa muda huo, basi walimsalimia pale ambapo aligeuka na kuwatazama ila baba Angel na yule mdogo wake dokta Jimmy walishangaana kwani ni watu wanaofahamiana.
Baba Angel ndio alianza kutamka jina la yule mdogo wa dokta Jimmy kwa mshangao,
“Moses ni wewe!!”
Moses nae alionekana kumshangaa baba Angel kwani hakutegemea kumuona kwa wakati ule mahali pale, basi madam Oliva alimuuliza baba Angel,
“Kumbe unafahamiana nae?”
“Ndio, namfahamu vizuri sana huyu mtu”
Baba Angel aliendelea tena kuongea na Moses,
“Za siku Moses”
“Nzuri tu”
“Naomba tuongee kidogo”
“Nina haraka sana kwa muda huu”
Yani Moses alisema vile huku akielekea kwenye gari yake na kupanda na kuondoka, huku madam Oliva na baba Angel wakiwa pale wakimshangaa,
“Sasa anamaana gani?”
“Nadhani hakutegemea kukuona mahali hapa, ndiomana unamuona hivyo. Ngojea tumuulize vizuri yule mlinzi”
Basi walimuita tena yule mlinzi na kumuuliza,
“Kwani unafahamu anapoishi?”
“Hapana, huwa sijui anaishi wapi na hakuna anayejua anapoishi kati yetu”
“Mmmh! Na huwa anaondoka kwa haraka hivi?”
“Hata nashangaa kaondoka bila hata ya kutuaga maana sio kawaida yake kabisa, huwa akija lazima aende kwenye ile ofisi ya dokta ambayo yeye ndio ana funguo zake na huwa sijui anaenda kufanya nini maana sisi tunalinda tu”
“Hivi ni kweli hii hospitali imefungwa na serikali au ni kitu gani? Ndio wasije kuikagua kweli?”
“Sisi hatujui ila ndio tulivyoambiwa kuwa imefungwa na serikali”
“Mmmmh hapa kuna siri kubwa sana tena sana”
Basi madam Oliva alimvuta pembeni baba Angel na kumuuliza,
“Kwahiyo huyu kijana unamfahamu vizuri sana?”
“Tena sana, ila kwasasa kanenepa sana. Huyu kijana alikuwa akiuza duka langu moja hivi lilikuwa ni kubwa sana, nadhani kwasasa ndio lingekuwa duka pekee kubwa sana hapa nchini kwa vifaa na vitu vya watoto maana lilikuwa na bidhaa nzuri na kufanya wengi walipende, kule kote ninakofungua maduka kwasasa, nanusanusa tu ila ile ndio ilikuwa biashara yangu kubwa sana”
“Kwahiyo imekuwaje? Ulifunga au imekuawaje?”
“Ni historia ndefu kidogo, kwanza ile biashara kwa asilimia zote ilikuwa ikifanywa na huyu kijana, yani kama hujui hata unaweza sema ni duka lake sababu nilimuamini sana kwenye biashara yangu ile, na ilikuwa na faida haswaaa kwani tulikuwa na wateja wengi. Mwanangu Angel wakati mdogo ndio alikuwa balozi wa duka langu lile, sasa badae mke wangu alivyojifungua na kupatwa matatizo mbalimbali, niliamua kwenda nae Afrika kusini kwaajili ya matibabu, basi nilisafiri na familia yote yani mimi, mke wangu na watoto wetu wote na tulikaa huko kwa miaka mitatau huku biashara yangu kubwa ikiendeshwa na Moses kwani huwa hata nikiwa mbali basi yeye anaendesha biashara yangu vizuri kabisa. Nakumbuka tulivyorudi nchini na kuanza maisha hapa tena, ndio hapo tatizo lilianza kwani biashara ile ilianza kuyumba sana na baba alinilaumua kuwa nimefanya uzembe, kuondoka na kuacha biashara, moses aliandika barua ya kuacha kazi na kuondoka zake, sikuwa na usimamizi mzuri kwakweli. Baada ya Moses kuondoka, wiki moja nilishusha mzigo mpya kwa kutumia akiba yangu nyingine ili duka nilisimamie mwenyewe, ila duka lilivamiwa na majambazi ambao walikomba kila kitu yani unajua kila kitu! Ni kila kitu hadi taa, duka lilibaki jeupe kama halijawahi kuwa na kitu. Ndio toka kipindi hiko niliacha hiyo biashara na sikuonana tena na huyu jamaa hadi leo, fikiria toka wakina Angel wadogo hadi leo! Ni muda mrefu sana umepita”
“Ni kweli ni muda mrefu sana, ila hakuna mtu mliyekuwa mnamshuku kwa wizi huo?”
“Nimshuku nani ikiwa hadi walinzi wangu waliuwawa? Yani kwasasa ndio unaona nakuwa na duka la kawaida tu kama lile, ila duka langu hilo lilikuwa ni kubwa sana, nilikuwa nafanya biashara ya jumla na rejareja”
“Ooooh pole sana kwakweli, wezi huwa wanajua kurudisha mtu maendeleo nyuma. Pole sana”
Wakaongea kiasi pale na kuamua kuondoka ambapo baba Angel alimpitisha hadi shuleni maana madam Oliva alikuwa akienda shuleni kwa wakati huo, basi madam Oliva akamuuliza,
“Ushuki kuja kusalimia mwanao?”
“Aaah Erick!! Atashtuka akiniona kwa muda huu, acha niende ofisini tu”
Basi waliagana oale, halafu baba Angel aliondoka zake.
 
SEHEMU YA 363


Njiani, baba Angel aliwaza kuwa aende kwa Sia, kwahiyo moja kwa moja aliongoza mpaka kwenye biashara ya Sia ambapo alimkuta pale akiendelea na biashara yake basi akaongea nae,
“Kwakweli Sia kwa uchunguzi nakukubali sana, nakuomba fanya juu chini uweze kuchunguza kuhusu dokta Jimmy. Halafu unajua kitu kingine nilichogundua?”
“Kitu gani?”
“Unamkumbuka yule Moses aliyekuwa anauza duka langu kipindi kile, lile duka langu kubwa la vitu vya watoto”
“Oooh lile duka ulilomfanya Angel kuwa balozi?”
“Ndio lile lile, sasa kumbe Moses ndio mdogo wake na dokta Jimmy na kwasasa Moses ndio mtu pekee anayejua dokta Jimmy alipo”
“Kheee umejuaje Erick?”
Baba Angel alimueleza Sia vile alivyoweza kugundua kuhusu Moses, na jinsi alivyoondoka upesi upesi pale hospitali,
“Mmmmh huyo itakuwa ana siri kubwa sana ila ndiomana mimi sijawahi kumuamini huyo kiumbe jamani! Kumbe ni ndugu yake dokta Jimmy!!”
“Ndio, ni ndugu yake kabisa. Nasikia ni ndugu yake wa damu”
“Sasa unanifungua ufahamu wangu kidogo, ndio naanza kuelewa zile hisia zangu. Unajua Erick, usikute ule wizi wa duka lako ni Moses ndio alihusika!!”
“Hapana jamani, biashara na Moses nilianza nae miaka mingi sana, kweli kwa muda ule ndio aamue kuniibia? Haiwezekani”
“Sisemi sana ila nahisi hivyo, ila kitu kingine yule Moses sasa naelewa ni kwanini niliwahi kumkuta mara kadhaa akiwa na mzee Jimmy”
“Naona unataka kuniletea mada zingine sasa, kumbuka baba yangu hayupo halafu mnavyomuongelea kila mara sio picha nzuri”
“Ila kumbuka yote haya mimi nahangaika nayo sababu ya baba yako, yani Erick huwezi kukwepa maovu ya baba yako aliyoyafanya kipindi cha uhai wake. Mimi nitamfatilia huyo dokta Jimmy ila natakiwa niwe na pesa, kwasasa sina hela za kutosha”
Baba Angel hakutaka pesa ndio zikwamishe kile anachotaka yeye kufahamu, hivhobasi akampa Sia laki tatu ili zimsaidie na kumwambia kuwa atamuongeza zingine bila kujali kuwa akigundua kuhusu dokta Jimmy itakuwa ni msaada na kwake pia. Kisha baba Angel alimuaga pale na kwenda ofisini kwake.

Mama Angel akiwa nyumbani kwake, leo alipigiwa simu na mama yake na kuanza kuongea nae,
“Kheee nyie watoto wabaya, hivi kweli Erica ndio wakukaa kipindi chote hiki bila kuja kuniona kweli!!”
“Mama, naomba unisamehe bure. Kesho nitafanya juu chini nitakuja kukuona na Ester”
“Hapo nitafurahi sana nikimuona mjukuu wangu, najua amekuwa sana kwasasa”
Basi alimaliza kuongea na mama yake, kisha alimuita Vaileth na kumuuliza,
“Hivi ndugu zako huwa hawakuulizi pia kuhusu kwenda kuwasalimia?”
“Na yale mambo ya kipindi kile, si unaona hata kuja wanakuja kiuoga, wala hata hawasemi chochote”
Wakawa wanaongea pale, muda kidogo Erica alirudi kutoka shuleni na kuwasalimia pale kisha alimuomba mama yake kuwa ana mazungumzo nae, mama Angel alijua tu kuwa Erica atakuwa amerudi na maneno yake ya umbea kwahiyo anatafuta pa kuyafikisha, basi mama Angel moja kwa moja alienda chumbani kwa Erica na kumsikiliza,
“Mama, hivi kweli mimi ni mtoto wako?”
“Hivi wewe mtoto una wazimu au kitu gani? Swali gani hilo unaniuliza sijui mara ya ngapi leo! Si nilishakujibu wewe, unaniletea kichaa eeeh!”
“Sasa mama, nimetoa wapi umbea?”
“Sitaki ujinga, umbea ni tabia kama tabia zingine, hiyo ni tabia yako haina kurithi hiyo. Umeipata mwenyewe, jifunze tu kuirekebisha maana umbea sio mzuri, ipo siku utasutwa hadi ukosee njia”
Erica alipumua na kumuuliza tena mama yake,
“Mama, wakati mimi na Erick tumezaliwa, tulikuwa na alama gani wakati wadogo? Au mimi nilikuwa na alama gani?”
“Alama kivipi?”
“Kuna kidude mwilini mwangu sikielewi mama”
“Kidude gani?”
Erica aliondoa shati lake na kuinua mkono juu ambapo chini ya mkono wake wa kushoto yani kwenye sehemu karibu na kikwapa mama Angel aliona kuna kakinundu,
“Kheee tuseme kile kinundu kimerudi tena!!”
“Ndio, sikipendi mama, nimerithi kwa nani?”
“Sijui, hayo ni matatizo tu. Inatakiwa tujue tiba ili utibiwe, hayo mengine matatizo tu. Sio kila jambo ni kurithi. Nakumbuka tulikikata kipindi kile hospitali, sikujua kama kitarudi tena. Nitakupeleka tena hospitali”
Mama Angel aliona Erica hana maneno ya maana basi aliamua kuondoka tu chumbani kwa Erica kwa muda huo.

Usiku wa leo, baba Angel aliamua kumueleza mkewe kuhusu mambo yaliyojiri kwenye hospitali ambayo alienda kwaajili ya kumfatilia huyo mdogo wake dokta Jimmy,
“Kheee kumbe Moses! Umemuona alivyonenepa eeeh!”
“Nimemuona, kabadilika sana hajataka hata kuongea na mimi”
“Basi ukweli wote anaujua, yani yeye ndio wa kumshikilia nadhani pia hakutegemea kama angekutana na wewe”
“Hakutegemea kabisa, ila kabadilika sana kwanza sijategemea pia kama Moses angegoma kuongea na mimi kwa kisingizio kuwa ana kazi nyingi!!”
“Ila ndio wanadamu walivyo mume wangu”
Waliongea sana pale, hadi kwa siku hiyo walichelewa kulala kwakweli.
Kulipokucha, ni mtoto ndio aliwaamsha baada ya kuanza kulia, ikabidi baba Angel ajiandae na kwenda ofisini.
Mama Angel nae aliamka na kumuandaa mwanae ili aende kumuona mama yake kama ambavyo alimuahidi.
Basi alipomaliza alienda kujiandaa alienda kumuaga Vaileth,
“Leo, naondoka na mtoto maana naenda kwa bibi yake”
“Kheee kwahiyo mama, leo kurudi jioni?”
“Ndio, ni jioni kabisa ndio nitarudi. Basi upike vile vile kama kawaida ila hawa wakitoka shule wakute chakula”
“Sawa mama, hakuna tatizo”
Basi mama Angel alitoka na kuondoka zake, ila siku hiyo alitoka na dereva kwani asingeweza kuendesha mwenyewe na mtoto mkononi.

Vaileth alishukuru kuona wote pale nyumbani wameondoka, basi alimpigia simu Junior, ambaye alimuahidi kufika kama kawaida, kisha yeye aliendelea na kazi mbalimbali za hapa na pale.
Na kweli baada ya muda tu Junior alifika na kuanza kuongea na Vaileth,
“Unajua nilikuwa nakujaribisha tu kama utafika, Junior jamani huwa unasoma muda gani?”
“Aaaah nasoma, halafu leo si Ijumaa”
“Inamaana muda wote huwa upo na simu?”
“Yani hujui tu Vai ukinipigiaga simu jinsi akili yangu inavyopoteza uelekeo, kwanza niambie ushatoa mimba? Ushatumia uzazi wa mpango?”
“Vyote tayari”
“Oooh kwahiyo ni kujiachia tu kwasasa? Ndiomana watu huwa wanasema kuwa wanawake wakubwa wana akili sana, na hizi ndio akili sasa”
“Akili kutoa mimba Junior?”
“Hapana, sio akili kutoa mimba ila akili yako ni kwamba unawaza mambo ya mbali, mfano mimi bado nasoma, je ukizaa mtloto itakuwaje? Hapa ndani wakigundua kuwa una mimba si watakufukuza? Na je mimi si nitachukiwa sana hapa nyumbani? Kwahiyo kwa kitendo chako cha kutoa umenifurahisha sana”
Vaileth alipumua kiasi na kumuangalia huyu Junior kwa makini, na kuona hapa huyu kijana yupo kwake kwaajili ya starehe tu na si vinginevyo. Kwahiyo aliona ni vyema aishi kwa akili. Basi Junior alisema aende kuoga kwanza, kwahiyo alienda kuoga na muda huo huo Vaileth alishika simu ya Junior ambapo ujumbe uliingia kutoka kwa jina lililoandokwa ‘Mama Linah’
Ujumbe ulisema,
“Junior mpenzi, ulisema nikutumie kiasi gani?”
Vaileth akafikiria kidogo na kumjibu,
“Naomba nitumie laki sita mpenzi”
“Nitume zote kwenye simu yako au nitume kwenye namba uliyosema unadaiwa?”
Vaileth akafikiria tena na kumwambia,
“Tuma laki tani kwenye ile namba halafu laki moja kwenye namba yangu, ngoja nikutumie namba ya kutuma na jina kamili ili usikosee”
Basi muda ule ule Vaileth alimtumia mule namba yake na jina lake, ambapo baada ya muda kidogo kuna ujumbe kwenye simu yake kuwa amepokea laki tano uliingia, halafu yule mama alituma ujumbe mwingine,
“Natumaini umepata, hata huyo mdai wako amepata”
“Ndio nashukuru sana, kanipigia simu muda huu huu”
“Basi muda sio mrefu nitakufata halafu nitakurudisha shule Jumapili jioni, sawa mume wangu mpendwa!”
“Hakuna tatizo mke wangu”
Basi Vaileth alifuta zile jumbe zote na kuweka pembeni simu ya Junior, hata Junior alipotoka kuoga alienda nae sebleni ili aweze kula chakula maana alimuandalia na kuongea nae vizuri kabisa, kisha baada ya kula aliamua kuongea nae kidogo,
“Hivi Junior ni kweli unanipenda?”
“Ndio, nakupenda sana, tena sana”
“Sawa, je huna wanawake wengine?”
“Ila wanawake jamani, huwa hamjiamini kabisa, sijui kwanini lakini. Mimi nakupenda wewe, sasa mwingine wa kazi gani? Sina haja na mwanamke mwingine mimi”
“Sawa nimekuelewa, sasa tunaongea sana leo. Twende tukajipumzishe kidogo”
“Hapana, leo sijisikii kwakweli nilikuita tu nikuone”
“Aaaargh ndio mambo gani hayo lakini Vai?”
“Kweli tena, sijisikii kabisa leo”
Mara simu ya Junior ilianza kuita na aliipokea, na kuongea nae kwa kifupi tu kisha akainuka na kumwambia Vailet,
“Natakiwa shuleni mara moja, ngoja niende tutawasiliana”
Kisha Junior alisogea karibu na Vaileth na kumbusu halafu akaondoka zake, yani Vaileth alimuangalia kwa hasira sana huyu Junior ila akawa za kitu,
“Hivi kweli kabisa niendelee kukaa na mimba ya Junior kwa akili kama hizi alizokuwa nazo kweli jamani!! Natamani kwenda kuitoa hii mimba, sijui nifanyeje?”
Akawaza, akaona sana akaona bora atamtafute nduguye Prisca na kumuuliza baadhi ya mambo,
“Prisca ndugu yangu, kuna jambo nataka nikuulize”
“jambo gani tena?”
“Hivi kipindi kile nilikusikia ukiongea na bibi kuwa mtu ukipata mimba halafu hiyo mimba huitaki, sasa ukitaka itoke unafanyaje?”
“Mmmmh Nyanda usiniambie kuwa una mimba? Ni mimba ya huyo baba mwenye nyumb? Unatoaje mimba ya tajiri hivyo?”
“Hapana, sina mimba ila kuna mtu nataka kumsaidia ndio ana mimba”
“Mmmmh mtu gani huyo?”
“Niambie kwanza halafu nitakwambia ni mtu gani”
“Nitafute usiku nikuelekeze vizuri, ila kama ni wewe pia uniweke wazi”
Basi Vaileth alikubaliana nae kuwa atamtafuta usiku ili aweze kuongea nae kuhusu jambo hilo.

Mama Angel alifika nyumbani kwa mama yake, kwakweli mama yake alifurahi sana kumuona mtoto wake maana ni siku nyingi sana hakukutana nae, kwahiyo walifurahiana pale na kukaa pamoja huku wakiongea mambo mbalimbali,
“Yani Angel huwa naenda kumuona hadi anasema mama na baba ndio kama wamenitupa huku maana hata hawaji kuniona”
“Mama, tumepanga likizo ndefu ndio tutamrudisha nyumbani, si unajua yule mtoto alivyojua kuchanganya vichwa vyetu yule, yani mpaka nilikuwa najihisi kupata ugonjwa wa moyo. Kwanza natamani hata akae huko huko hadi amalize shule kabisa, mambo yake na Samir mimi hata siyawezi. Ila wale masister sasa wanawachunga wale watoto hata ujinga haiwezekani”
“Ni kweli, ile shule ni nzuri sana. Ila Angel alikuwa anaelekea pabaya, nadhani kapata macho juu juu kama baba yake, ila tabia sio yako kabisa”
“Mmmh jamani mama”
“Ndio, naona Erica ndio kachukua tabia yako maana hana mambo ya ajabu yule”
“Ila umbea ni moto, katoto ni kambea hadi shetani anaogopa sijui umbea ule kaupata wapi”
Bibi Angel alicheka sana, tena sana na kuanza kuongea na mama Angel,
“Sikia nikwambie, babu wa baba yenu yani baba yake mzazi na babu yenu. Jamani yule babu alikuwa ni mbea hadi basi, Mungu amrehemu tu huko alipo ila alikuwa ni mbea hakuna mfano. Halafu ubaya ni mmoja, alikuwa na mtindo wa kuota mambo ya ukweli, yani yeye utakuta anaota kitu kilichopo, akishaota sasa anakueleza kila kitu, na aliyekaribu anamwambia, yani siri yako peupeee, yule babu nasikia watoto wake karibia wote waliachana na waume zao na wengine waliachana na wake zao maana yule babu alikuwa noma. Unapanga kitu mwenzio kashakiota, ukija anakuumbua mwanzo mwisho. Vipi Erica kapona na ndoto?”
“Zamani ndio alikuwa na mtindo huo, ila kwasasa ameacha”
“Kheee basi yule babu, alikuwa na nundu Fulani kwenye kwapa, yani hadi wajukuu zake wanampa ushauri kuwa apelekwe kukatwa ila anakataa na kusema kuwa lile nundu ndio linamfanya aote siri za watu”
“Kheee!!”
Mama Angel kidogo akashtuka na kumwambia mama yake,
“Hata Erica ana kinundu Fulani kwenye kwapa, tuliwahi kumkata wakati yupo mdogo ila jana kaniopnyesha kile kinundu kimerudi tena”
“Duh!! Hebu mfatilie Erica vizuri”
“Ila mama mbona hata Derrick ni mbea ila huwa hasemi kama anaota?”
“Derrick ni mbea kweli, ila pia ni muongo ndiomana hata kazi ya utapeli aliiweza, kwanza anaendeleaje?”
Ndipo mama Angel alipoanza kumueleza mama yake hadi mambo ya mtoto Elly aliyekuwa kwa Sia kuwa ni mtoto wa Derrick, kwakweli bibi Angel alishangaa sana na alipoambiwa kuwa jambo hilo lilifanywa na mzee Jimmy alishangaa zaidi na kusema,
“Yani yule mzee akili zake anazijua mwenyewe, nilitaka nishangae kafa tu na kuacha salama mambo yote!! Nilijua lazima kuna ujinga atakuwa amefanya. Umenikumbusha kitu, kuna siku alisema kuwa ipo siku hata akifa wewe Erica utaenda kwenye kaburi lake na kulia sana”
“Kheee mzee ana wazimu huyo eeeh!!”
“Ni kweli ana wazimu tena haswaa, ila maneno yake yalishakufa nae kashashindwa yule”
Waliamua kubadilisha mada na kuanza kuongea vitu vingine kwa wakati huo, kwani waliona mada za mzee Jimmy zingewachanganya akili.
Ila muda wakati mama Angel anakaribia kuondoka ndipo alipogundua kuwa simu yake haina muda wa maongezi,
“Unajua nini mama? Nilimwambia dereva nitampigia muda wa kuondoka aje anichukue, ila muda wa maongezi kumbe sina”
“Kheee na mimi sina yangu haina muda wa maongezi pia”
“Basi ngoja nikanunue vocha”
Mama Angel alimuacha pale mama yake na yeye kuondoka zake kuelekea dukani kwani kwa muda huo mtoto wake mdogo alikuwa amelala.

Mama Angel, alipotoka nje ya nyumba yao alishangaa kuona kuna gari imesimama hapo, alijiuliza sana kuwa ile gari ni ya nani ila hakuelewa kuwa ni ya nani kwa muda huo, basi aliamua kuachana nao na kuendelea na safari ila alisikia sauti ikimuita,
“Erica”
Akasimama na kugeuka nyuma, alishangaa kumuona Rahim, ambapo Rahim alimsogelea na kuanza kuongea nae,
“Mambo vipi Erica?”
“Kilichokuleta huku kwetu leo ni nini?”
“Hata mimi sijui ni kitu gani? Nilikaa nyumbani kwangu ila nikajisikia tu kuwa kuja huku kwenu nikuone”
“Kweli akili yako haina akili kabisa, yani kipindi kile nina mtoto mdogo hapa, ulishindwa hata kuja kumtazama mtoto wako mwenyewe, halafu kwasasa unajifanya una hamu sana ya kuja kuniona mimi!!”
Kisha mama Angel alikuwa akiendelea kwenda dukani huku Rahim akimfata nyuma na kuongea nae,
“Zilikuwa ni akili za ujana zile, kwasasa nimejua thamani yako. Yani nina hamu kweli ya kuishi nawe pamoja na mtoto wetu Angel, natamani kweli watoto wote ulionao ingekuwa umezaa na mimi”
Mama Angel alifika dukani na kununua vocha kisha kuanza kurudi nyumbani, basi Rahim aliendelea kuongea tu,
“Unajua nini Erica, mimi bado nakupenda tena nakupenda sana”
Mama Angel alisimama na kumwambia Rahim,
“Hebu nisikilize Rahim tena nisikilize kwa makini sana, mimi nimeolewa kwasasa na nina maisha yangu, na wewe umeoa na una maisha yako. Unatakiwa kumuheshimu mke wako kama mimi ninavyomuheshimu mume wangu. Nampenda sana Erick, ndiye mwanaume aliyefuta machozi yangu, mwanaume aliyeondoa aibu yangu, mwanaume aliyenifanya nijione mwanamke kati ya wanawake, mwanaume aliyefanya wengi wanaotuona kutamani mapenzi yetu na kuniona kuwa mimi ni mwanamke mwenye bahati sana. Kweli nina bahati sana kumpata Erick kwenye maisha yangu, nampenda sana kupita chochote”
“Dah! Umeamua kunimaliza kabisa leo kwa maneno yako. Huwezi jua siri za ndani ya nyuma, nyumba zinja siri kubwa sana Erica. Nikikueleza ya mke wangu kwa hakika utachoka kutasikiliza kabisa. Ila hakuna tatizo, najua ni jinsi gani unapendana na Erick ila ukweli utabaki pale kuwa na mimi nakupenda sana wewe”
Mama Angel akafikiria kitu na kukumbuka jambo, basi alimwambia Rahim,
“Kama kweli unanipenda au ulikuwa na upendo wa dhati juu yangu naomba ufanye jambo moja kwaajili yangu”
“Jambo gani hilo?”
“Najua kwasasa una mahusiano na mwanamke aitwaye Manka, ila kuna jambo kubwa sana kuhusu huyo Manka. Alikuwa yupo karibu sana na baba mkwe wangu aliyeitwa mzee Jimmy, nadhani unamfahamu vizuri sana. Naomba umchunguze huyu mwanamke ujue yeye na mzee Jimmy ni kitu gani kimejificha”
“Eeeeh baada ya kazi hiyo ndio nitakupata?”
“Halafu wewe una kichaa kweli, hivi unajisahaulisha kuwa umeathirika au kitu gani!”
Kisha mama Angel aliingia ndani kwao na kumuacha Rahim pale nje kwani alihitaji kumpigia dereva wao simu ili aweze kwenda kumchukua.

Mama Sarah, toka siku ameujua ukweli alisikia roho kumuuma sana, na kwavile siku hizo Elly hakurudi nyumbani kwake basi akaona ni vyema akamfate shuleni kwao.
Alienda mpaka shuleni na kumuita Elly, ambaye alienda kumsikiliza kisha alimwambia kuwa anahitaji kuondoka nae, kwakweli Elly alishindwa kukataa kwani ni huyu mama ndiyo anayemtegemea kwenye elimu yake.
Aliondoka nae huku mama Sarah akiongea nae kwenye gari,
“Ulianza lini mchezo mchafu Elly?”
“Mchezo gani?”
“Unajifanya hujui au? Mchezo wa kuwapa wanawake mimba”
Elly alikaa kimya kwani aliogopa kiasi, kisha mama Sarah aliendelea kumwambia,
“Nadhani hunijui vizuri, mimi ni mwanamke mwenye huruma sana pia ni mwanamke mwenye roho mbaya sana, nimekereka mno kusikia kuwa wewe ndio kidume ambaye umempa mimba binti yangu. Yani nikusomeshe, mama yako ategemee pesa yangu, mle chakula changu halafu uje kumfanyia vibaya binti yangu? Sijapenda hata kidogo”
Elly alikuwa akitetemeka tu bila kujua cha kujitetea wala kujua kitu chochote cha kufanya, basi moja kwa moja mama Sarah alienda nae mahali Elly na kumkabidhi kwa mtu akimtaka mtu huyo amuadhibu Elly atakavyo ambapo yule mtu alianza kwa kumchapa viboko visivyokuwa na idadi, yani Elly alikuwa akilia sana huku akilaani vikali umasikini uliokuwepo kati yake na mama yake.
Yule mtu alipomchapa sana Elly alimuuliza mama Sarah,
“Adhabu zingine sijui kama utapenda kuona nitakavyompatia! Niruhusu niende nae kule mtoni nikamuadhibu vizuri”
“Sawa hakuna tatizo”
Mama Sarah alikaa pembeni ya gari yake huku amekunja sana sura yake na akifurahia vile Elly alivyoenda kuadhibiwa, akatoa na kinywaji kabisa kwenye gari lake na kuanza kunywa taratibu. Ila baada ya muda mfupi tu, yule kijana aliyekuwa akimuadhibu Elly, alikuja mbio hadi kwa mama Sarah na kumwambia,
“Mama, kuna kitu sio cha kawaida nimekiona kwa huyu kijana”
Mama Sarah alishtuka kuwa ni kitu gani hiko.


Mama Sarah alikaa pembeni ya gari yake huku amekunja sana sura yake na akifurahia vile Elly alivyoenda kuadhibiwa, akatoa na kinywaji kabisa kwenye gari lake na kuanza kunywa taratibu. Ila baada ya muda mfupi tu, yule kijana aliyekuwa akimuadhibu Elly, alikuja mbio hadi kwa mama Sarah na kumwambia,
“Mama, kuna kitu sio cha kawaida nimekiona kwa huyu kijana”
Mama Sarah alishtuka kuwa ni kitu gani hiko.
Basi mama Sarah ilibidi aongozane na yule kijana, ambapo Elly alikuwa chini huku akivuja damu nyingi kwa kipigo alichokipata kwa yule kijana, basi mama Sarah akaanza kumfokea yule kijana,
“Imekuwaje umpige mpaka aanze kuvuja damu hivyo?”
Kisha mama Sarah alijikuta akijiwa na huruma ya hali ya juu, na kwenda pale chini alipokuwa Elly, kisha yule kijana alimwambia,
“Kilichonishangaza sio hizo damu nyingi zilizomtoka, ila angalia mbele ya hizo damu”
Mama Sarah alipoangalia aliona kuwa hizo damu za Elly, zimeenda kuzunguka kwenye mti ambao umeandikwa kwa kukwanguliwa jina ‘Manka’ kwakweli mama Sarah alishtuka sana, hakujua ile inamaanisha nini, ila alimuomba yule kijana wasaidiane kumchukua Elly na kumpeleka hospitali.
Walimbeba na kumkimbiza kwenye gari, kisha kumpeleka hospitali. Huko mama Sarah hakusema kama wamempiga ila aliongea na daktari tu amuhudumie maana yeye kamsaidia, akampa pesa yule daktari ambapo alianza tu kumuhudumia Elly bila kutaka kujua kama waliompeleka hospitali ndio waliompiga.
Kwakweli mama Sarah alikuwa haelewi kitu, na muda nao ulikuwa umeenda sana kwa siku hiyo, yani alizunguka zunguka pale hospitali na aliumia sana moyo wake.
Aliondoka pale hospitali kwenye mida ya saa tano usiku na kurudi nyumbani kwake huku akiwa na mawazo sana haswaa ni kwanini jina lake limechorwa kwenye ule mti!! Yani hapo ndio hakuelewa kabisa.
Mama Sarah alipoingia ndani kwake na kwenda kuoga tu, akafatwa na Sarah ambaye alimsubiria mama yake amalize kuoga kisha akamuuliza,
“Mama, mbona siku hizi sikuelewi!”
“Kwanini mwanangu?”
“Yani huwa muda mwingine unaonekana ukiwa na mawazo sana, unaonekana huna raha. Siku hizi unaenda sana kwenye mikesha yani huwa sielewi, na yote kwa yote leo ndio sijakuelewa kabisa, kwanza umechelewa kurudi halafu umerudi ukiwa na hofu kubwa”
“Hebu kwanza niambie ukweli, ni kweli Elly alikubaka hadi ukapata mimba ile?”
“Hapana Elly hajanibaka mimi, ila mimi ndio nilitaka kuwa nae, yani kwa tatizo hili wala sio kosa la Elly kabisa”
Mama Sarah alipumua kiasi kwa muda maana alihisi kama mawazo yake kukatika, kisha Sarah akamuuliza,
“Nani kakwambia kuwa Elly alinibaka?”
“Hapana, hakuna kitu mwanangu”
Basi mama Sarah aliamua kuagana na binti yake tu kwani aliona kwa muda huo akili yake kutokufanya kazi kabisa.

Vaileth kama ambavyo aliwasiliana na ndugu yake, basi alimtafuta tena kwa usiku ule na kuanza kuongea nae ili kujua cha kufanya kuweza kuitoa ile mimba aliyokuwa nayo. Basi alianza kuwasiliana nae,
“Eeeh Prisca niambie ile dawa sasa”
“Kwanza niambie ukweli ili nikupe dawa ya uhakika”
“Basi tuache masikhara, ni kweli mimi ndio nina mimba ila ni mimba ya mlinzi”
“Oooh hiyo toa haraka sana, haifai hata kulea hiyo mimba”
“Haya, nakusikiliza hiyo dawa”
“Kuna dawa za aina mbili, kuna moja ni uhakika yani lazima itoke na kuna nyingine ni bahatinasibu, unahitaji ipi?”
“Niambie hiyo ya uhakika ndio ninayoihitaji”
“Sasa hiyo unatakiwa kuifanya mchana halafu wakati watu wote hawapo, inawezekana?”
“Inawezekana ndio”
“Kuna yale majani mekundu, nadhani unayakumbuka yale sijui kama huko yapo au nikuletee?”
“Mmmmh ngoja niangalie maana huyu mama kapanda maua mengi sana, nitayaangalia kesho, nikipata nifanyeje?”
“Yani unatakiwa hiyo dawa wakati unaichemsha asiione mtu halafu unainywa taratibu, ngoja nikutumie ujumbe wa vitu vya kuchanganyia humo. Ni chungu ila mambo fasta tu”
“Sawa sawa, nitumie huo ujumbe”
Kwakweli Vaileth alikuwa na hamu sana ya kufanikisha lile jambo ili ajihisi sawa kabisa kwani mambo ya Junior yalimchosha sana.

Kulipokucha, mama Sarah alishtuliwa na sauti ya mwanae ambaye alimuuliza mama yake,
“Mama Elly yuko wapi?”
“Kwanini unaniuliza hivyo?”
“Mama, mamake Elly kanipigia simu kuwa Elly hayupo nyumbani kwao na amejaribu kuulizia kote alipodhani yupo ila kaambiwa kuwa hayupo. Je Elly yuko wapi mama?”
“Naomba leo nikamtafute huyo Elly halafu nitakupa jibu mwanangu, nenda shule tu halafu nitafanyia kazi jambo hilo”
“Ona sasa mama, umesahau hata kama leo sio siku ya shule, leo ni Jumamosi ujue!”
“Oooh samahani mwanangu, labda kuchanganyikiwa tu. Nitamtafuta usijali, vipi leo utashinda siku nzima nyumbani?”
“Hapana, nitaenda kwa mama mkubwa kumsalimia nimemkumbuka sana”
“Sawa, kamsalimie sana”
Mama Sarah kwa muda huo, alijiandaa na kuondoka zake na safari yake ya kwanza ni hospitali kumuangalia Elly ambaye bado hakuwa na hali nzuri kutokana na kile kipigo alichokipata, basi mama Sarah alimuomba daktari ajitahidi sana katika kumpa huduma zote huyo Elly, kisha akamuachia hela nyingine. Na kwa wakati huo aliondoka moja kwa moja na kwenda mpaka kwenye biashara ya Sia ili kuweza kuongea nae kuhusu Elly, alimkuta kwenye biashara na kumuita pembeni na kuanza kuongea nae,
“Ndugu yangu, mama mwenzangu naomba tuongee jambo hili”
“Yani kabla ya hilo jambo, sipo sawa kabisa ujue, mwanangu Elly hajulikani alipo, nimeenda hadi shule kumuulizia ingawa leo sio siku ya shule, cha kushangaza nimeambiwa na mlinzi wa pale kuwa jana aliondoka na wewe. Niambie kwanza yuko wapi mwanangu Elly?”
“Ndio hilo jambo nililokuwa nataka kuongea na wewe, ni hivi Elly anaumwa na yupo hospitali”
Sia alishtuka sana na kuuliza kwa makini,
“Anaumwa nini tena?”
“Tulia kwanza, usiwe na papara utajua tu ukweli”
Mara mama Sarah alipigiwa simu na daktari na kupewa ujumbe kuwa Elly anahitaji damu kwani katokwa na damu nyingi sana, kwahiyo ikabidi mama Sarah amwambie Sia waende nae hospitali kwa muda huo.
Kwakweli Sia alikubali kwani kwa siku hiyo hata hakuwa akifanya biashara kama siku zote kwani alikuwa akiwaza kuwa mtoto Elly yuko wapi.
 
SEHEMU YA 364



Leo, baba Angel aliona ni vyema kwenda ofisini kwake kwani alikuwa na mambo mengi ya kufanya huko ofisini, pia aliona kuna umuhimu wa mtu kwenda kiwandani basi alimuomba Erick aende ambapo Erick aliomba kwenda na Erica huko kiwandani, kwahiyo walijiandaa na kwenda kiwandani, halafu baba Angel nae ndipo alipoondoka na moja kwa moja kwenda ofisini kwake. Kwahiyo nyumbani alibaki tu mama Angel pamoja na Vaileth, basi mama Angel alianza kuongea na Vaileth,
“Hivi Vai, nasikia huko kwenu watoto huwa wanatembea haraka sana, huwa mnawafanya nini?”
Vaileth alicheka kidogo na kusema,
“Ni bibi zetu hao ndio wanadawa za kimila hatari, yani mtoto ili atembee haraka huwa wanamchanjia na mavi ya panya”
“Kheee Vai, mavi ya panya tena!!”
“Ndio, kule panya ni wengi sana, si unajua kijijini tena, tofauti na hapa kwako hata mende tu kumpata ni adimu”
Mama Angel alicheka na kusema,
“Naogopa mende mimi balaa jamani, yani ndiomana huwa nawaita wale wa kupulizia dawa kwenye chemba za vyoo ili nisiwapate hao mende kabisa, nawaogopa sana. Ila mimi hayo mambo ya kumchanja mwanangu na mavi ya panya mmmh siyawezi”
Vaileth akacheka na kusema,
“Hata ukitaka mtoto aongee upese dawa ipo”
“Mmmh nyie nadhani mna dawa hata ya kutolea mimba nyie”
Vaileth alicheka kiasi na kuomba akaendelee na kazi zingine huku akitamani sana mama Angel aweze kuondoka kwa siku hiyo ili yeye aweze kufanya dawa zake alizoambiwa na ndugu yake Prisca.

Baba Angel akiwa ofisini, siku ya leo alimuita yule mama muuza matunda ili kuongea nae kuhusu kile alichokuwa ameambiwa na Sia maana hata alishindwa kuamini vizuri, basi alimuita ofisini kwake na kuanza kuongea nae,
“Mama, unakumbuka matunda ya mwisho kunipatia mimi?”
“Nakumbuka ndio”
“Uliyatoa wapi yale matunda? Na unajua kwanini siku hizi sili matunda yako?”
“Hapana sijui ni kwanini huli, ila yale matunda kiukweli kabisa kuna mama aliniletea ili nikupatie na aliniambia kuwa atanisaidia kuniongezea mtaji na alisema wewe ni rafiki yake sana ila hakutaka ujue kama ni yeye amekupatia yale matunda”
“Ila kwanini hukujiuliza kabla ya kuniletea mama yangu? Unajua ungeniua?”
Yule mama alikuwa kimya kwa muda huku akitoa macho yake, kisha baba Angel aliendelea kuongea,
“Kwenye yale matunda kulikuwa na sumu, kwani baada ya kula tu nilirudi nyumbani nikiwa na hali mbaya. Mke wangu aliniwahisha hospitali na kufanya niweze kupata matibabu haraka ila bila ya hivyo ningekufa mimi”
“Aaaaah naomba unisamehe baba yangu”
Huyu mama alipiga magoti huku akimsihi baba Angel amsamehe na machozi yakimtoka, huku akisema,
“Tamaa hii jamani, tamaa ya pesa ndio iliyoniponza. Naomba unisamehe sana, nilitaka kutanua biashara yangu, hata sikujua kama kuna kibaya kwenye yale matunda”
Baba Angel alimuinua pale na kuendelea kuongea nae,
“Ila huyo mwanamke hakukwambia lengo lake kwangu ni nini?”
“Hakuniambia, na kama ningejua basi kwa hakika nisingethubutu kukupatia yale matunda. Naomba unisamehe sana”
“Haya, amekupatia hiyo hela ya kuongeza mtaji wako?”
“Hapana, mwanzoni alikuwa anakuja mara kwa mara ila kuna siku alikuja na chakula na kutaka nikuletee kile chakula, akanipatia laki moja kwa kazi hiyo, hapo nilishtuka na kukataa kwani sio kitu cha kawaida kusema nikuletee chakula halafu anipe laki moja ya kazi hiyo, nilivyokataa ndio akaondoka na hakurudi tena”
“Duh!! Kuna kitu umenifungua, huyo mama yukoje?”
“Ni mweupe sana, ana mwili kiasi, pia ni mrefu. Halafu ni mzuri, hata sikumtegemea kama anaweza kufanya kitu kama hiko”
“Asante kwa taarifa hiyo, nashukuru. Basi hiyo ndio sababu ya mimi kutokula matunda yako tena”
Huyu mama alikazana kumuomba baba Angel msamaha ila baba Angel alimwambia kuwa ameshamsamehe na kufanya huyu mama aweze kwenda kuendelea na kazi zake zingine.

Mchana wa siku hiyo, mama Angel alipigiwa simu na kudai kuwa inabidi aondoke kwa muda huo, basi alimuaga Vaileth na kumuachia mtoto kama kawaida.
Kwa Vaileth lile swala la mama Angel kuondoka lilikuwa ni swala la muhimu sana kwake, kwani alipoondoka tu, ndipo na yeye alipoanza kufanya ile dawa ambayo alielekezwa na Prisca kuona kama itafanya kazi mapema kama alivyoambiwa, alienda kutafuta na kupata majani aliyoambiwa, alichanganya vyote alivyoambiwa maana vyote vilikuwepo kule ndani, kisha alibandika jikoni na kuanza kuchemsha.
Wakati yupo jikoni, alishangaa kuna mgeni ameingia ndani na moja kwa moja kuingia kule jikoni, ambapo alishtuka sana kwani hakumtegemea mgeni huyu kwa wakati huu, alimuangalia kwa mshtuko,
“Kheee Sarah!”
“Ndio ni mimi, unapika nini dada?”
Kabla hata Vaileth hajamjibu, tayari Sarah alishasogelea hadi lile sufuria ambalo lilikuwa jikoni likichemka ile dawa na kumfanya Vaileth achukie sana ila hakuwa na cha kufanya kwa Sarah, na yeye Sarah alishangaa sana kumuona Vaileth kachukia kwa namna ile,
“Kwani tatizo nini dada mbona unaonekana umechukia?”
“Hakuna kitu”
Basi Vaileth aliipua ile dawa maana hata hakuona umuhimu tena wa kuendelea kuichemsha ile dawa maana ishakosewa masharti tayari, basi akatoka na Sarah mpaka sebleni na kumuuliza,
“Kwani tatizo lako nini Sarah?”
“Mbona unaniuliza kwa ukali hivyo?”
“Nisamehe, samahani nimekuuliza tu kuwa tatizo ni nini?”
“Leo, nimeenda kwa mamangu mkubwa kumsalimia na lengo langu siku ya leo nimalizie huko ila nimemkuta Junior”
Kidogo hii habari ilimshtua Vaileth na kumfanya aulize vizuri zaidi kwani aliweza kupata picha kuwa huyo mtu atakuwa ndio mama Linah,
“Duh! Huyo mamako mkubwa anaitwa nani?”
“Jina lake halisi anaitwa Linah”
“Duh! Kwahiyo ndio umemkuta Junior huko?”
“Ndio, tena hana hata habari nilitaka nije nimwambie mama hapa”
“Mmmh usimwambie hiko kitu atachukia sana”
Mara mama Angel nae alikuwa amerudi muda huo na kuuliza kwa makini kuwa ni kitu gani ambacho anatakiwa kufichwa na Sarah, ni hapo hapo Sarah aliporopoka kuwa Junior yupo kwa mamake mkubwa na kumfanya mama Angel achukie sana huku akifikiria kitu cha kufanya ili kumtoa Junior kwa huyo Linah.

Baba Angel akiwa anaendelea na kazi zake pale ofisini alipigiwa simu na mke wake na kuambiwa ule ujumbe kuwa Junior yupo kwa Linaha alichukia sana na kwa muda huo huo aliamua kwenda nyumbani kwake, kisha alipofika kwake tu aliomba kuondoka na Sarah ili kwenda kuonyeshwa nyumbani kwa Linah, kwahiyo Sarah aliondoka na baba Angel na moja kwa moja kwenda nae nyumbani kwa mamake mkubwa.
Basi baba Angel, alisimamisha gari na kumtaka Sarah amsubiri kwenye gari lake halafu yeye ndio alishuka kwenda kumfata Linah ambaye alionekana nje ya nyumba yake kwa muda huo.
Baba Angel alimsogelea pale karibu na kumsalimia kisha akamwambia,
“Naomba niitie Junior”
Linah alienda ndani na kumuita Junior, kisha baba Angel aliondoka na Junior kwenda nae kwenye gari lake, yani hata Linah hakusema jambo lolote lile kuwakatalia kuwa wasiondoke wala nini.
Moja kwa moja baba Angel aliondoa gari lake hadi nyumbani kwakina Sarah ambako alimuacha Sarah huko halafu yeye alienda nyumbani kwake.

Mama Sarah na Sia walipofika hospitali, moja kwa moja mama Sarah aliongea na Sia ili waweze kuona kama anaweza kumchangia Elly damu, kwakweli Sia alikubali tu na daktari muda ule ule aliamua kumpima damu Sia aone kama ataweza kumchangia mtoto wake, ila cha kushangaza damu ya Sia haikuendana na damu ya Elly, ikabidi watafute njia nyingine, ndipo mama Sarah alipouliza kama yeye ataweza kumchangia,
“Kama inawezekana basi mimi nitolewe damu nimchangie”
Basi walienda kumpima na kukuta damu yake inaendana na Elly, ikabidi atolewe yeye damu na aende kuongezewa Elly.
Basi mama Sarah alikaa na Sia kwa muda huu na kumuuliza swali,
“Inawezekanaje mama na mtoto msiendane damu?”
“Inawezekana ndio, labda karithi kwa baba yake?”
“Oooh kweli lakini usemayo, inawezekana hiyo kitu. Ila nashukuru nimeweza kumtolea damu Elly natumai atakuwa mzima kabisa”
“Ila hujaniambia kuwa alifanya nini?”
“Unajua nini kuna mahali nilienda kumuonyesha Elly ila alikazana kusema kuwa anataka kurudi nyumbani basi nikamruhusu kuwa arudi, cha kushangaza sasa wakati anarudi sijui vijana gani huko wakampiga sana, kwa bahati nzuri nami ilirudi eneo lile ndio nikamuokoa”
“Ooooh jamani, mtoto wangu mpendwa dah! Nimeumia sana”
“Pole, ila atapona kabisa”
Basi walikaa kaa kidogo na kisha mama Sarah alimlazimisha Sia kuhusu kumrudisha nyumbani kwake kwa muda huo kwani muda ulikuwa umeenda sana.

Baba Angel alifika na Junior nyumbani kwake moja kwa moja yani alikuwa na hasira kiasi kwamba alishindwa hata kuongea na Junior kuhusu jambo lolote, basi mama Angel ndio aliamua kwenda kuongea na Junior,
“Hivi wewe mtoto una nini lakini? Yani unaacha kuwa shule kweli unaenda kwa huyo mwanamke mtu mzima? Unajua umuhimu wa elimu wewe!”
“Nisamehe mamdogo”
“Unadhani hiyo nisamehe yako inasaidia kitu gani? Hiyo nisamehe yako ndio inaenda kukufaurisha mitihani au kitu gani? Hebu niambie ukweli kwanza ni kitu gani kinakufanya hadi unakazana kuwa kwa huyo mwanamke?”
“Nisamehe mamdogo, sitarudia tena”
“Ulisema hivi hivi mwanzoni na kitu gani umefanya sasa? Yani Junior tunahangaika kukusomesha halafu unaenda kufanya ujinga kweli!! Sijapenda kabisa kabisa, kesho nitakupeleka mwenyewe shule mjinga sana wewe”
Mama Angel hata hakufurahishwa na majibu yale ya Junior ya kutokusema ukweli, ila alipotoka kuongea nae hapo aliamua kumpigia simu dada yake ili kumueleza jambo lililotokea, kwakweli mama Junior alichukia sana na kuahidi kuwa kesho ataenda pale nyumbani ili na yeye amseme pia mtoto wake na wampeleke wote shuleni kwao,
“Kwakweli huyu Junior kanikera sana, yani hata nimejikuta kutokujua cha kufanya kwakweli. Hivi hilo jinga litamaliza shule kweli jamani!”
“Tumuombe tu Mungu kwakweli, maana karudi kwa yule yule mwanamama tuliyegombana nae jamani dah!! Nimechukia sana”
Basi mama Angel aliongea na dada yake pale na kukata simu.

Usiku wa siku hii, Erica kabla ya kulala alienda moja kwa mona chumbani kwa Erick na kuanza kuongea nae,
“Hivi yule tuliyekutana nae leo umemuelewa?”
Erick alifikiria kidogo kwani alishasahau ni mtu gani ambaye walikutana nae kwa siku hiyo, kisha alimuuliza Erica,
“Yupi huyo?”
“Si yule aliyekuwa akitushangaa pale njiani”
“Oooooh nimemkumbuka, yule aliyesema kuwa hatuna adabu eeeh!”
“Ndio, hivi kwanini watu wakituona mimi na wewe wanatuhisi tofauti? Yani kwanini huwa hawahisi kuwa sisi ni ndugu na wanahisi sisi ni wapenzi?”
“Nadhani ni sababu ya kile kiapo ambacho tulisema kuwa mimi na wewe tusiwe na marafiki wengine”
“Basi inabidi tukavunje hiko kiapo au unasemaje?”
Erick alibaki kimya kwa muda kidogo mpaka Erica alimshtua na kumwambia tena,
“Inabidi tukavunje hiko kiapo”
“Kwakweli sipo tayari kwa hilo, sitaki kuona ukizungukwa na marafiki kama Bahati na Abdu kwahiyo siwezi kuvunja hiko kiapo kwakweli”
Erick alionyesha hadi kunyong’onyea wakati Erica akimkazania kuvunja kile kiapo, basi ilibidi Erica atoe ushauri kuwa wacheze karata, halafu Erica akaenda kuchukua karata chumbani kwake na kurudi kuanza kucheza na Erick na kama kawaida walicheza hadi usiku sana na mwishowe walijikuta wakipatwa na usingizi tu mule mule ndani kwa Erick.

Junior alipatwa na aibu sana, kwahiyo aliona ni vyema kumuomba msamaha hata Vaileth maana aliona ni wazi kuwa amemkera kila mtu mule ndani, basi alitoka chumbani kwake na kwenda kugonga chumbani kwa Vaileth ila hakufunguliwa mlango, basi alirudi chumbani kwake na kuanza kumtafuta Vaileth kwa njia ya ujumbe mfupi maana simu alimpigia sana ila Vaileth hakupokea simu za Junior kabisa, akamtumia ujumbe,
“Vaileth mpenzi wangu kwanini lakini umekuwa hivyo?”
“Mjinga wewe tena usinizoee kabisa”
“Ndio yamekuwa hayo kweli? Umesahau kila nilichokifanya kwaajili yako?”
“Usinibabaishe huko, ni kipi ulichofanya kwangu chenye umaana zaidi ya uhuni wako tu!!”
“Hujui tu Vaileth ni kwanini nimekutwa na yule mama, nilikuwa na shida na pesa mimi kwaajili ya kutoa ile mimba yako, sikuwa na pengine pa kupata pesa zaidi ya kwa yule mama”
“Mjinga wewe, ulishindwa vipi kusema gtulee tu!”
“Sasa tutaleaje Vai wakati bado nasoma?”
“Usinizoee, endelea na kusoma kwako”
Muda huu Vaileth alizima na simu kabisa kwani zile jumbe kwa Junior zilikuwa haziendi tena kwa Vaileth, kwakweli Junior alijihisi vibaya sana na kusema,
“Haya ndio matatizo ya wanawake, yani mtu namsaidia mwenyewe halafu anaona kamavile nimefanya makusudi, mjinga kweli huyu mwanamke. Aaaargh hawa wanawake wananichanganya akili mno, ningejua ningemuacha na mimba yake ajijue nayo mwenyewe”
Alichukia na kuamua kulala tu kwa muda huo.

Mama Angel aliamka mapema sana kwa siku hii sababu ya kuamka kwa mtoto wake mdogo, basi alianza kushughulika nae pale, muda kidogo baba Angel nae aliamka kutokana na kelele za yule mtoto,
“Oooh mume wangu pole jamani, endelea kupumzika”
Mama Angel alitoka na yule mtoto kwani alitaka amuandalie maziwa, basi moja kwa moja alienda nae chumbani kwa Erica ili Erica amshike mdogo wake ila alishangaa kutokumuona,
“Kheee mapema yote hii haka katoto kameenda wapi jamani!”
Akapata wazo la kwenda kumuangalia chumbani kwa Erick na kweli alimkuta kalala huko akiwa hana hata habari na karata zao zikiwa pembeni, yani mama yake alimshtua pale na kufanya hata Erick ashtuke pia,
“Hivi nyinyi kwanini mnapenda kucheza karata hadi usiku sana, mna matatizo gani? Au ndio midawa mliyopewa kuwa mchzage karata!”
Erica na Erick walishangaa maana hawakuwa wakijua kuhusu hiyo mada ya dawa, basi Erica alimuuliza mama yake,
“Dawa gani mama?”
“Mnajiona mpo sawa? Watu gani nyie mnacheza karata hadi usiku halafu mnajikuta mmelala, mimi sijawahi kuona hili jambo kwakweli, sijapata kujua kama nyie watoto mtakuwa wajinga kiasi hiki. Haya Erica mshike mdogo wako”
Alimpa mtoto Erica na kutoka zake, basi Erica alikaa na yule mtoto, na wakati huo hata Erick alikuwa ameamka na kukaa kwahiyo walianza kuongea,
“Dawa gani anazozisema mama kuwa tumekunywa?”
“Mmmh hata sijui, ila kwanini tukicheza pamoja karata basi tunacheza hadi usiku sana na mwishowe tunajikuta tumelala yani kama hatujalala chumbani kwako basi tutalala huku kwangu kwanini?”
“Hata sielewi pia, tunatakiwa kujua ni dawa gani zinazosemwa na mama”
Kisha Erica aliinuka na yule mdogo wake hadi sebleni huku akijiuliza kuhusu dawa alizoambiwa na mama yake.
Ila alipokaa pale sebleni na mtoto alijikuta akisinzia na kujiwa na ndoto ambapo alikuja kushtuliwa na mama yake,
“Yani Erica umeshika mtoto huku umelala jamani!!”
“Nisamehe mama, ila nimeota”
“Umeota nini?”
“Nimeota kuwa jana kaka Junior mlienda kumfata na kumkuta kwa yule mama wa siku ile, halafu nimeota ulirudi na kumsema sana Junior”
Mama Angel alishtuka kidogo, kwani wakaina Erica waliporudi hawakujua chochote kilichoendelea kwani muda huo hata Junior alikuwa amelala, basi akaanza kukumbuka kitu alichoambiwa na mama yake kuhusu huyu mtoto wake, basi alimsogelea karibu na kumuuliza,
“Umeota nini kingine?”
“Nimeota Junior akipewa hela na yule mama, yani Junior anamfata yule mama sababu ya pesa zake”
Muda huu Junior nae alikuwa akitoka chumbani, kwahiyo alijikuta akisimama tu kwenye ngazi huku akimsikiliza Erica alivyokuwa akifunguka kuhusu mahusiano yake na yule mmama.

Leo mama Sarah alifikiria sana jambo na aliona ni vyema kama akienda kwenye ilea lama ya jina lake kugundua ukweli, kwani alitaka kujua imekuwaje jina lake kuwepo sehemu ile, basi alijiandaa na kuondoka pale nyumbani kwake.
Moja kwa moja alienda kwenye ule msitu mdogo na kwenda karibu na mto ule mdogo ili kujua ni kitu gani kilitokea, ila alikuta kuna mtu amesimama karibu na ule mti akiuangalia basi mama Sarah alishtuka na kumsalimia yule mtu, ambapo yule mtu aligeuka na kumfanya mama Sarah ashtuke sana kwani hakutegemea kumuona mahali hapo, mtu huyu alikuwa ni Derrick.


Moja kwa moja alienda kwenye ule msitu mdogo na kwenda karibu na mto ule mdogo ili kujua ni kitu gani kilitokea, ila alikuta kuna mtu amesimama karibu na ule mti akiuangalia basi mama Sarah alishtuka na kumsalimia yule mtu, ambapo yule mtu aligeuka na kumfanya mama Sarah ashtuke sana kwani hakutegemea kumuona mahali hapo, mtu huyu alikuwa ni Derrick.
Mama Sarah alimshangaa sana na kusema kwa mshangao,
“Derrick!!”
“Ndio, ni mimi. Derrick nipo hapa, nimefurahi kukuona, umekuja kufanya nini hapa?”
“Kwani wewe unafanya nini hapa?”
“Si unaona huu mti unajina lako!”
“Kwahiyo kama una jina langu?”
“Nakumbuka siku niliyoandika jina hili ni siku nilipogundua kuwa Elly ni mtoto wangu halafu sio mtoto niliyezaa na Oliva, niliwaza sana kuwa itakuwa nimezaa na nani Elly maana nina hisia asilimia zote kuwa ni mtoto wangu. Ila nilikuja na kuandika jina lako kwenye mti hapa, kuna kitu kiliniambia kuwa kama ikitokea damu ya Elly ikazunguka mti huu basi huyu ndio atakuwa mama mzazi wa Elly, na pia Elly atahitaji damu sababu damu yake imetoka halafu huyu mama atamuongezea damu. Sijui hilo jambo litatokea lini, ila nimekuja leo na kuona mti umezungukwa na damu iliyoganda sijui ndio ya Elly au ni nini”
Mama Sarah alipumua kwanza kwasababu kama alikosa usemi hivi, alijikuta akikaa pale chini kabisa na kumuuliza Derrick,
“Umejuaje kuwa vyote hivyo vimetokea?”
“Kwahiyo ndio ilivyokuwa? Elly ni mwanao Manka, ni furaha sana kugundua hilo”
“Hebu nisikie tena unisikie kwa makini. Mimi sio mwanaume kusema nilimpa mwanamke mimba akazaa huko halafu sijui kuhusu mtoto ndio nije kugundua badae, ila mimi ni mwanamke niliyebeba mimba kwa miezi tisa kamili, nikashikwa na uchungu na kwenda kuzaa. Katika maisha yangu sijawahi kuzaa mtoto mwingine zaidi ya Sarah tu, ndio mtoto niliyezaa, nikamnyonyesha, nikamlea na nimemkuza, sikuelewi unavyoniambia kuwa Elly ni mwanaungu, unasema hivyo kwa vigezo gani?Mbona Elly ni mtoto wa Sia na Erick!!”
“Sikia nikwambie, labda kama Sia hajakwambia ukweli, ni hivi yule mtoto sio wa Sia hata yeye mwenyewe hakujua wazazi wa yule mtoto, ila Mungu ni mwaminifu, kamleta kwangu kwanza na kunifanya nimtambue kuwa ni mtoto wangu, na sasa nimetambua kuwa nimezaa na wewe”
“Loh!! Kwakweli unanichanganya yani sikuelewi hata kidogo kabisa, unanichanganya haswaaa”
“Sijui ni kitu gani kipi, ila nina uhakika kuwa wewe ndio mama mzazi wa Elly”
“Na Sarah je?”
“Huenda ulipata mapacha, labda hospitali waliiba mtoto mmoja”
“Uwiii mbona nitakuwa nimeumbuka mimi!”
“Umeumbuka kivipi?”
Mama Sarah hakujibu, kwani moja kwa moja alirudi kwenye gari lake na kupanda kisha alijisemea,
“Nimezaaje mapacha bila kujua? Inamaana mwanangu mmoja walimuiba? Kama ni hivyo inamaana Sarah alitembea na kaka yake wa damu? Oooh nimeumbuka mimi jamani, watoto wangu kweli watembeleane? Inamaana mimi nimemuadhibu kiasi kile mwanangu? Nahisi kuchanganyikiwa kwakweli”
Alihisi akili yake kutokuwa sawa kabisa, hivyobasi moja kwa moja alienda kwenye hoteli moja na kukodi chumba kisha aliagiza pombe humo na kuanza kuzinywa, alichukua simu kwa muda huo na kumpigia dokta ambaye alihusika na kujifungua kwake,
“Eti dokta, inawezekana mimi nilijifungua mapacha?”
“Inawezekana ndio”
“Kivipi? Niambie ukweli, nilijifungua mapacha eeeh! Wa kike na wa kiume?”
Huyu dokta alikata simu na kumfanya mama Sarah akili yake iwe mbovu kabisa kwa wakati huo, basi aliagiza vinywaji na kunywa sana kama mtu aliyechanganyikiwa kabisa.

Mama Angel leo anaamua kukaa na Erica kwani aliona anatakiwa kuongea vitu vingi sana na huyu mtoto kwani hakumuelewa ndoto aliyosema ameiota,
“Erica mwanangu, huwa unaota nini na nini?”
“Naota mambo mengi tu”
“Mfano”
“Kabla hamjapata ukweli kuhusu kutoka kwa mimba ya Daima niliota kuwa mimba hiyo imetoka”
“Kheee mbona huwa husemi sasa?”
“Vingi huwa namwambia Erick”
“Mwanangu, naomba unieleze mambo yote ambayo huwa unaota kuhusiana na familia hii”
Mama Angel alitaka kufahamu hiko kilichopo kwenye akili ya mwanae, ila Erica hakutaka kusema kwani angeweka wazi kuhusu mimba ya Vaileth na kumfanya Vaileth kuwa vibaya.
Muda kidogo alifika mama Junior kama ambavyo walipanga ile jana yake, alimuita mwanae na kumsema sana kuhusu lile jambo ambalo amelifanya,
“Mwanangu hakuna faida yoyote utakayopata kwa kufanya huo ujinga, zaidi zaidi unanidhalilisha mama yako na kufanya nizidi kutukanwa na baba yako. Kwanini lakini unafanya hivi mwanangu?”
“Nisamehe mama”
“Kuna muda hata hawa wanaokusomesha watachoka na kukuacha ukihangaika na maisha tu, kwakweli sijapenda kabisa”
Kisha mama Angel nae alijiandaa na kuondoka pale nyumbani wakiwa wameongozana na Junior kwa lengo la kumrudisha shuleni.
Kwahiyo nyumbani alibaki tu Vaileth pamoja na Erica na kuanza kuongea mambo mawili matatu yaliyopo pale, kwanza Vaileth alianza kwa kumshukuru Erica,
“Kwanza nashukuru sana kwa kuendelea kunifichia siri yangu”
“Lakini masharti ya hii siri yangu si unayajua?”
“Ndio, nayajua”
“Na mbona jana ulitaka kujaribu kuitoa hiyo mimba sababu wakati unachemsha dawa alikuja Sarah hapa nyumbani”
“Khiiii ila wewe Erica sio mtu wa kawaida kabisa dah!! NImekutoa kwenye kundi la watu wa kawaida”
“Hapana mimi ni wa kawaida sana, sema huwa naota hayo mambo yote ninayokwambia”
“Sitarudia tena kutoa mimba, wala sitoitoa. Nitabaki nayo tu hii mimba na nitazaa ingawa nina mawazo sana kuwa nitaleaje?”
“Utalea kama jinsi utakavyozaa, usiitoe hiyo mimba kabisa”
Yani Erica alikuwa akiongea huku akimaanisha kitu alichokuwa akikiongea.
Muda kidogo simu yao ya mezani ilikuwa ikiita, basi Erica alienda kupokea na kufurahi sana kwani alikuwa ni dada yake,
“Jamani dada Angel nimekukumbuka sana, wote nyumbani tumekukumbuka sana. Sijui tutakuona lini?”
“Mtaniona tu hata msijali, nampigia simu baba hapokei”
“Yupo Kanisani umesahau leo ni lini?”
“Kheee baba nae, siku hizi anachelewa kutoka namna hii. Akirudi nyumbani mwambie anipigie”
Erica alifurahi sana kuongea na Angel kwa siku hiyo, basi aliagana nae huku akiwa na furaha sana.

Siaalipotoka kanisani kwa siku ya leo, moja kwa moja alienda hospitali kumuona Elly kwani alijikuta akimkumbuka sana mwanae huyu ukizingatia alishazoea kuishi nae.
Alipofika hospitali, kabla ya kwenda kumuona Elly kuna mtu alimuona na kumgundua, mtu huyu alikuwa ni dokta Jimmy, basi Sia aliamua kutumia muda huo kuanza kumfatilia dokta Jimmy hata hakuendelea tena na swala la kumuangalia mtoto pale hospitali.
Dokta huyu alionekana na haraka sana kwani alipanda gari lake na kuondoka, muda huo Sia nae aliita bodaboda na kumtaka wamfatilie dokta yule hadi alipokuwa akielekea, ni kweli walimfatilia na moja kwa moja waliingia kwenye hoteli ambapo Sia alishuka na kuanza kumfatilia, ila kuna chumba alimuona akiingia ila yeye hakuweza kuingia ingawa alitamani kuingia humo. Ila alijibanza mahali na kuona dokta akitoka, na kuna mwanamke aliyefunga mlango ambapo Sia alimtambua vizuri sana yule mwanamke, basi moja kwa moja alimuacha yule dokta aondoke halafu yeye alienda hadi kugonga pale ambapo yule mwanamke alimfunbgulia mlango na Sia aliingia moja kwa moja ndani, kwakweli huyu mwanamke alimshangaa kidogo ila Sia alimwambia,
“Bila shaka unaweza ukawa unanikumbuka kuwa mimi ni nani?”
“Mmmh hapana”
“Mimi naitwa Sia, niliwahi kuwa mpenzi wa boss wa mume wako”
“Unamaanisha Erick?”
“Ndio huyo huyo, kumbe boss wa mume wako unamfahamu eeeh!! Kuna nini kinachoendelea kati yako na huyu aliyetoka yani dokta Jimmy?”
“Mmmh ni shemeji yangu huyu”
“Unajua kama anatafutwa na watu wengi sana kutokana na aliyoyafanya?”
“Mimi sijui kitu”
“Na mbona unaishi hotelini inamaana siku hizi mna utajiri wa kuishi maisha haya?”
“Kheee ndio maswali gani hayo umeniuliza?”
“Mumeo yuko wapi? Hivi unajua nakuuliza maswali ya msingi sana”
“Ila mimi nilimwambia Moses, haya mambo nilijua tu siku moja itakuwa tatizo”
“Nadhani unaelewa ninachoweza kufanya, basi nisikilize ni hivi, naomba namba za dokta Jimmy ila usimwambie kama tumeonana mimi na wewe na wala usimwambie kama nimechukua namba kwako”
Huyu mwanamke alikuwa akimtambua Sia vizuri kabisa ingawa mwanzoni alidai kuwa hamtambui Sia, basi muda huo huo alitaja namba za dokta Jimmy na kumfanya Sia aondoke akiwa amepata mawasiliano ya dokta huyo.
Moja kwa moja alirudi kwa yule dereva na kumtaka ampeleke tu nyumbani kwake, kwakweli huku walipoenda ilikuwa ni mbali sana, na kiukweli dereva alifanya kazi kubwa ya kufatilia na kupoteza muda kwenye eneo moja.
Walifika nyumbani kwa Sia ambapo tayari kulikuwa na giza, Sia alimuuliza yule wa bodaboda kuwa amlipe pesa ngapi,
“Hapa labda laki moja na elfu hamsini”
“Duh! Kama nilikodi kosta kumbe bodaboda”
“Sasa unadhani ni pesa ngapi? Nimefanya kazi kubwa sana, jumlisha na mafuta yangu”
“Ila kumbuka wakati tunarudi nilitoa elfu ishirini ukajaza mafuta pale”
“Ndio, ila mafuta niliyotumia wakati wa kwenda je? Tena mimi nimekuhurumia kufanya kazi yako bila ya maswali mengi”
Sia aliamua kwenda tu kutoa hiyo hela kwani alijua wazi kama akimwambia baba Angel basi atapata hela zaidi ya hiyo.
Aliamua tu kupumzika kwa muda huo, maana alikuwa kachoka na ule upepo wa pikipiki katika kumfatilia dokta Jimmy.

Usiku wa leo, mama Angel anakaa na mumewe chumbani na kuanza kuzungumza kuhusu habari za Erica na ndoto alizosema huwa anaota, ni hapo baba Angel alipokumbuka ujumbe aliopewa na Erica kuwa amtafute, basi moja kwa moja baba Angel alimpigia simu mwalimu mlezi wa pale na kuuliza kama kwa muda huo ataweza kuongea na Angel,
“Ooooh Angel kwa muda huu! Wamelala, labda umpigie simu kesho”
“Basi nitajitahidi na kuja mwenyewe huko ili nimuone”
Basi alikata simu kisha baba Angel akamwambia mke wake,
“Ngoja kesho niache mambo yote niende kumtazama Angel kwanza, itakuwa katukumbuka sana. Dah sijui shule anamaliza lini maana hata mimi nimemkumbuka sana”
Waliongea sana na baba Angel alipanga kuwa asubuhi na mapema wakati wakina Erica wakienda shuleni na yeye ndio aondoke na kwenda moja kwa moja kwenye shule ya wakina Angel ili kuweza kumsalimia.
Ila katika ile mada ya kuhusu Erica, baba Angel akasema jambo,
“Ila mke wangu kama mtoto wetu huwa anaota mambo ya ukweli, inatakiwa tumshirikishe kwenye vitu vingi. Inawezekana hata haya tunayohangaika nayo ikawa yeye akapata jibu mapema, tunapomshirikisha ndio atapata mwanga”
“Mmmh tumshirikishe kuwa walichomwa sindani! Mbona hapo pagumu sana mume wangu!”
“Hapo pagumu kweli, na hakuna namna ila cha muhimu ni kumuuliza mara kwa mara ili tujue ni kitu gani ambacho huyu mtoto huwa anakiota kwani itasaidia kwasisi kufahamu yanayoendelea juu yake”
Basi waliongea na kuamua kulala tu kwa muda huo.
Kulipokucha, baba Angel aliamka na kuanza kujiandaa ili kwenda kumsalimia mtoto wao ila mama Angel nae akaona ni vyema aongozane na mume wake na kumwambia,
“Twende wote kwakweli, mbona na mimi nimejikuta nikitaka kwenda kumsalimia”
“Sawa, hakuna tatizo lolote”
Mama Angel alianza kujiandaa, wakati huu baba Angel alitoka kabisa sebleni kumsubiria mke wake.
Akiwa pale sebleni alimuona Erica akiwa ametoka na sare za shule, akamsalimia pale basi baba Angel alimuuliza,
“Wewe mbona umechelewa hivi!! Si gari la shule litakuwa limekuacha?”
“Ni kweli nimechelewa hata hilo gari limeondoka, ila baba naomba usiende leo kumuona dada Angel”
“Kwanini unasema hivyo?”
“Nimeota vibaya, nimeota kuwa wewe na mama mkienda huko leo mtapata ajali”
Baba Angel alishtuka kidogo na kumuangalia kwa makini binti yake, kisha akamuuliza,
“Umejuaje kama naenda na mama yako?”
“Sijui ila nimeota tu kuwa unaenda na mama”
“Duh!! Wewe mtoto hapana kwakweli”
“Sasa nimeota baba ndiomana nimeshindwa hata kuondoka bila ya kuwaambia hiko kitu”
Mama Angel alitoka ndani akiwa kamaliza kujiandaa, ila na yeye alishtushwa na ile taarifa ya Erica, basi mama Angel alimuuliza zaidi,
“Yani Erica umeona sisi tukipata ajali?”
“Ndio mama, nimeota. Mara nyingine sioni sura kwenye ndoto ila naelewa inaponielekeza”
“Duh! Kwahiyo umeota tukienda huko tuitapata ajali?”
“Ndio, tena katika hiyo ajali wewe mama utaumia sana, haswaa mkono wako wa kulia yani hadi mfupa utateguka”
“Duh!!”
“Sijui ni wapi anasoma dada Angel ila nimeota kuwa hiyo ajali mnapata kwenye njiapanda ya karibu na shule ya wakina dada Angel”
“Duh!! Basi mwanangu, kweli kuna njiapanda pale. Hatuendi tena tumeahirisha, ngoja nimwambie dereva tu akupeleke shule”
Kisha Erica alitoka nje kwani baba Angel aliwasiliana na dereva kwenye simu, baba Angel na mama Angel walibaki wakitazamana tu yani hiyo safari waliihairisha kabisa yani kilichoendelea hata kwenda kazini pia baba Angel alihairisha yani akaona ni vyema kwa siku hiyo kubaki tu nyumbani bila kwenda popote pale.
 
SEHEMU YA 365


Mama Sarah anaamka akiwa hotelini na kukumbuka kuwa jana yake hakurudi kabisa nyumbani kwake, nasi aliinuka na kuoga kabisa kisha akaenda moja kwa moja hospitali kumuangalia Elly, na kweli alimkuta akiendelea vizuri basi aliongea na daktari ambaye alimpa ruhusa na kumfanya mama Sarah kuamua kwenda nae nyumbani kwake.
Yani walipanda kwenye gari la mama Sarah ila Elly hakuwa na amani kabisa yani alijiona kama anaenda kutupwa tena, ila mule kwenye gari mama Sarah alianza kuongea nae,
“Elly naona huna amani kabisa kuwa nami karibu, hebu naomba usahau yote yaliyopita na tunaenda kuanza maisha mapya, utasoma na kufurahi kama zamani”
Elly aliitikia tu kwa kichwa ila alikuwa akiogopa hata kuongea kutokana na kipigo alichokipata hapo kabla.
Basi moja kwa moja wanenda hadi nyumbani kwa mama Sarah na kufika pale ambapo mama Sarah anampeleka Elly moja kwa moja chumbani huku kichwani akijiwa na dhana kuwa huenda Elly akawa ni pacha wa Sarah.
Anamngoja Sarah arudi jioni, na anapofika tu anaanza kuongea nae,
“Sarah, nakuomba mwanangu huyu Elly umuheshimu kama kaka yako kabisa”
“Lakini mama, Elly sio kaka yangu”
Mama Sarah alitokwa na machozi na kumwambia binti yake,
“Kuna mambo mtu huwezi kuyaelewa na utaona kama wanaoyaongea wapo kupiga kelele tu, ila kiukweli wewe na Ellu ni ndugu tena ndugu wa damu”
“Kwahiyo yule wa siku ile ndio baba yetu?”
“Yupi huyo?”
“Mama Erick alitupeleka kw ambaba mmoja hivi, mimi na Elly na kudai kuwa yule ni baba yetu ila mimi sikubali hilo swala kabisa. Najua baba yangu alishakufa, usiniambie vingine mama sijui kama naweza kukuelewa”
“Na wala sina haja ya kukwambia vingine na sijasema kuwa huyo sijui nani ndio baba hyako hapana, ila nimesema kuwa Elly ni ndugu yako. Muheshimu kama kaka yako”
“Ila nimempenda mama”
“Usiniletee wazimu huo Sarah, nimekwambia muheshimu Elly kama kaka yako”
“Hapana mama, nampenda Elly na siwezi kusahau nilichokuwa nimefanya nae”
“Hivi wewe mtoto una wzimu au kitu gani?”
“Hapana mama, siwezi kukuelewa kwa wewe kuniambia kuwa Elly ni ndugu yangu ikiwa nishafanya nae vingi, nishamtunuku usichana wangu”
Mama Sarah alijikuta akichukia sana, kwa mara ya kwanza alijikuta akimnasa kibao mwanae na kumfanya Sarah akimbilie chumbani kwake akilia, kwakweli mama Sarah alijikuta tu akifanya vile ingawa hajawahi kumpiga Sarah toka alipokuwa mdogo kwani alimpenda sana mtoto huyu na alimuona kama ndio maisha yake, Ila kwa siku hiyo hata yeye alikaa chini na kujishangaa kwa muda kwa kitendo chake cha kumpiga Sarah wakati hajawahi kufanya hivyo hata mara moja.
Alitoka chumbani kwake na kwenda mlangoni kwa Sarah na kumgongea ila Sarah hakufungua mlango wala hakusema chochote kile na kumfanya mama Sarah apatwe na uchungu sana moyoni mwake.

Sia alienda moja kwa moja ofisini kwa baba Angel ili amueleze yale yaliyojiri ila hakumkuta, ikabidi aende nyumbani kwa baba Angel ili hata kama akimkuta mama Angel amwambie yale mambo maana aliona ni sawa pia kufanya huvyo.
Alifika nyumbani kwa mama Angel na kuingia ndani ambapo alimkuta Vaileth na kumuuliza,
“Yuko wapi mama mwenye nyumba?”
“Yupo kule kwenye bustani na baba”
Basi Sia alienda moja kwa moja walipo, na kweli aliwaona kwenye bustani, roho ilimuuma ila hakutaka kuwaza hayo kwa muda huo, aliwasalimia pale na kuanza kuwaeleza kile ambacho alikutana nacho, kwakweli baba Angel alifurahi sana na kumpongeza Sia,
“Kuna muda huwa upo vizuri sana Sia, unaweza kutupeleka kwenye hiyo hoteli?”
“Ndio, napakumbuka vizuri sana”
Mama Angel akachangia hapa,
“Mmmh mnadhani tutawakuta tena!! Hivyo lazima yule atakuwa amewaambia na wamehama, hebu tuanze na hiyo namba kupiga”
“Tumieni simu yangu maana kuna laini yangu ipo tu huwa haijulikani kirahisi kuwa ni yangu”
Basi baba Angel alifanya hivyo na kuchukua simu ya Sia, kisha akapiga ile namba ambapo baada ya muda kidogo tu simu ilipoita ilipokelewa,
“Hallow, nani mwenzangu?”
“Nina shida na wewe dokta”
“Kwani wewe ni nani?”
“Tuonane kwanza ndio utajua mimi ni nani”
“Kama hujitambulishi kwaheri”
Ile simu ilikatwa muda ule ule, baba Angel alipojaribu kupiga tena ile simu haikupokelewa basi waliangaliana pale na kuanza kujadiliana,
“Lazima kuna kitu kikubwa sana, ila nakuamini Sia huwezi kuacha kumfatilia huyu hadi tujue vingi zaidi”
“Ninachohitaji kufahamu ni sehemu wanayoishi kwani nikifahamu hapo itakuwa ni rahisi zaidi kumpata”
Walijaribu kupanga mambo kadhaa kisha Sia aliondoka zake na kurudi nyumbani kwani baba Angel alimuahidi kumpelekea pesa nyingine kwaajili ya kazi yake ya uchunguzi.
Baada ya Sia kuondoka, ndipo mama Angel alipomwambia mume wake,
“Unajua kwanini nimekataa tusiende huko kuwatafuta?”
“Kwanini?”
“Naogopa ndoto ya Erica, mmmh tusijepata ajali kweli bure”
“Mmmh mke wangu, umeanza kuishi kwa hofu sasa. Kweli kuna kutoka hapa mmmh!!”
Walijikuta wote wakicheka kwa pamoja maana kwa wakati huo wote walijikuta wakitawaliwa na hofu.

Usiku huu mama Sarah akiwa chumbani kwake akiwaza jinsi ambavyo hapati ushirikiano mzuri na mwanae, muda huo huo alipigiwa simu na Rahim na kuanza kuongea nae,
“Sijakusikia kwa siku hizi mbili tatu, upo sawa kweli!!”
“Nipo sawa tu”
“Nakuja nyumbani kwako, niandalie chakula”
Mama Sarah alimkubalia tu, kwani kwa kiasi Fulani aliona kuwa ile kwake ni jambo jema ukizingatia alikuwa na mawazo mengi sana ambayo yalikuwa yakichanganya akili yake kwa kipindi hiko, basi moja kwa moja aliinuka na kwenda jikoni kupika ila alipika tu ilimradi maana hata hakuwa na furaha ya kufanya hivyo.
Kweli baada ya muda kidogo Rahim alifika tena akiwa na begi la mgongoni, basi mama Sarah alimkaribisha vizuri kabisa na Rahim aliomba kupewa chakula alichodai kuwa aandaliwe, alitengewa na kula kile chakula na baada ya hapo alienda chumbani na mama Sarah kwani muda ulikuwa umeenda sana, halafu akatoa vinywaji kwenye begi alilokuwa amebeba,
“Oooh halafu sikukuuliza kuwa umebeba nini humo?”
“Ni nguo na hii mizinga mitatu tu”
“Kheee hii si pombe kali? Unakunywaga pombe Rahim?”
“Kwanini nisinywe? Nimemkosea nini Mungu hadi nisinywe pombe!”
Mama Sarah alicheka na kwenda kuchukua glasi kisha yeye na Rahim walianza kunywa huku wakiongea kuhusu zile nguo ambazo Rahim amezibeba,
“Na nguo hizi za nini?”
“Nimepanga kuja kukaa huku wiki mbili kwa safari hii”
“Duh!! Ya sasa kali”
“Ni kali kweli, nimeamua kujitoa muhanga kwako maana nakupenda sana”
Basi walikunywa sana zile pombe, na mpaka wakajikuta wamelewa na kulala pamoja.
Kulipokucha asubuhi, mama Sarah alikuwa akijiangalia vizuri na kuwa kama mtu anayejuta kitu Fulani, basi Rahim alimuuliza,
“Nini mawazo tena mpenzi?”
“Unajua hatujatumia kinga usiku?”
“Kinga ya nini? Unahofia kupata mimba au kitu gani?”
“Kinga ni bora maana tunajitenga na ukimwi pia”
“Inamaana siku zote hizi huniamini jamani au nini? Hivi inawezekanaje mtu kama mimi kupata ukimwi? Wapo wa kupata ukimwi jamani Manka na sio mtu kama mimi”
“Ila na mimi je unaniamini vipi?”
“Nakuamini, ikiwa unakumbuka kinga muda wote inamaana upo vizuri na unajiamini, basi unatakiwa uniamini na mimi kama na mimi ninavyokuamini wewe”
Mama Sarah alitulia tu ila kiukweli alikuwa na mawazo sana, kwani kwa upande wake alikuwa ameweka kinga ni jambo la muhimu sana kutokana na mtu mmoja aliyemuamini sana halafu akakuta ameathirika, basi toka hapo alianza kutumia kinga tu, mpaka siku hii aliyosahau kutumia kinga sababu ya kulewa sana na Rahim.

Siku ya leo, mama Angel alipatwa na ugeni ambao hakuutaraia kwakweli maana alifika rafiki yake wa chuo, ila hakujua kama angefika kwa siku hiyo,
“Kheee jamani Fetty, karibu sana”
Basi walikumbatiana pale na kufurahia huku Fetty akimwambia mama Angel,
“Naona leo timu nzima ipo nyumbani!”
“Si unajua tena!! Leo ni sikukuu ya kitaifa!!”
“Najua maana na wanangu wapo nyumbani ila watoto wale jamani, Mungu anisaidie tu”
“Vipi tena?”
“Kuna kale kanaitwa Abdi dah huyu mtoto ni pasua kichwa hatari, leo ndio nimejua maana ana ugomvi na kaka yake Bahati wa muda mrefu sana”
“Ugomvi gani?”
“Kumbe wanamgombania binti yako Erica”
Mama Angel alishangaa sana na kuuliza kwa mshangao,
“Kheee wanamgombania Erica? Kivipi?”
“hata mimi sikuwaelewa kwakweli, ila wanamgombea binti yako, kila siku huwa wanagombana yani leo ndio nimejua chanzo cha ugomvi wao”
“Kwani ndio uliozaa na Bahati hao?”
“Nizae nae wapi? Yule nae si ndio mzazi mashuhuru! Ana watoto kila kona yani, huyo Abdi ni mtoto wa mdogo wake Nasma ambaye anaitwa Siwema, na huyo Bahati ndio mtoto wa Siwema, hapo sikutajii timu nyingine aliyoniwekea pale nyumbani. Mwanaume hafai yule namvumilia tu, kwani ni mimi ndio nimembadilisha tabia yake mbovu”
“Sasa umegundua vipi kuwa wanamgombania Erica wangu?”
“Leo wakati natoka, nilimuaga baba yao pale ndipo kila mmoja alisema mtaa ninaoelekea ni mtaa anaokaa Erica wake, nilipowadadisi ndio nikagundua ni mwanao ndio anatajwa. Ila mimi nimepitia tu hapa ingawa haikuwa safari yangu ya leo”
“Kwani ulikuwa unaenda wapi?”
“Sio naenda wapi! Nimetoka kumuangalia rafiki yangu mmoja huko amepata ajali na ameumia sana hadi huruma jamani”
“Kheee jamani, lini tena?”
“Jana hiyo, kaumia sana yani”
“Kwani alikuwa akienda wapi jamani! Pole yake kwakweli”
“Kuna mtoto wao anasoma, sasa walipanga kwenda kumuona mtoto wao shuleni ila mumewe akapata dharula kwahiyo hakwenda, ndio akaenda huyo rafiki yangu jamani, kaumia sana hadi huruma”
Mama Angel aliuliza tena,
“Ni shule gani hiyo aliyokuwa anaenda?”
Fetty alimtajia na kumfanya mama Angel ashangae sana kwani ndio shule anayosoma Angel pia, kisha akamuuliza tena,
“Kwahiyo ajali kapata maeneo gani?”
“Yani nasikia karibu na hiyo shule kuna njiapanda, basi ndio hapo hapo kapata ajali hiyo na kuumia sana”
Mama Angel alishangaa sana kwani ni kitu hiki hiki waliambiwa jana yake na Erica.

Fetty alimtajia na kumfanya mama Angel ashangae sana kwani ndio shule anayosoma Angel pia, kisha akamuuliza tena,
“Kwahiyo ajali kapata maeneo gani?”
“Yani nasikia karibu na hiyo shule kuna njiapanda, basi ndio hapo hapo kapata ajali hiyo na kuumia sana”
Mama Angel alishangaa sana kwani ni kitu hiki hiki waliambiwa jana yake na Erica.
Basi mama Angel aliyasikiliza maelezo ya Fetty kwa makini ila alikuwa akitafakari vitu vingi sana, na hakuweza kusema zaidi kwani alihisi yale maelezo kumchanganya, basi alimuuliza tena Fetty,
“Huyo rafiki yako huwa anaishi huku? Maana sijawahi kukusikia kuwa unaenda kumuona rafiki yako huku”
“Hapana haishi huku wala nini, ila kutokana na ile ajali imebidi arudi kwa dada yake mkubwa ambaye ndio kama mama yao kwahiyo ndio anamuhudumia kwa yale majeraha”
“Hospitali je?”
“Walienda ndipo walipotoka walirudi moja kwa moja huku ndiomana mimi kuja kumuona imebidi nije huku”
“Hapo nimekuelewa”
Baada ya muda kidogo, Fetty aliaga na kuondoka zake, na moja kwa moja mama Angel alienda kuongea na mumewe ili kumpa hiyo habari,
“Mmmh umesikia hii?”
“Nini tena?”
Mama Angel alimsimulia kila kitu ambacho Fetty amesema na kufanya baba Angel ashangae pia, alimuuliza mkewe,
“Kwani Erica alituambiaje jana?”
“Alisema sisi ndio tutapata ajali halafu mimi nataumia sana, eneo alilolitaja Erica ndio lile lile ambalo rafiki wa Fetty kapatia ajali”
“Dah!! Unajua mwanetu anaanza kuwa mtabiri sasa?”
“Kivipi?”
“Maana katabiri vile ambavyo ilivyo ila katuokoa maana hiyo ajali ingekuwa ya kwetu ila ndio imeenda kwa huyo”
“Dah! Unajua mume wangu umefikiria mbali sana! Mimi sikufikiria huko”
“Ulifikiriaje?”
“Yani moyo ulianza kunienda mbio wakati Fetty ananisimulia, nakumbuka Erica kasema kuwa kaota sisi wazazi wake tukienda huko tutapata ajali, basi Fetty alivyosema vile nikaanza kuwaza au sisi sio wazazi wa Erica!!”
Baba Angel alimuangalia mkewe na kumuuliza kwa mshangao,
“Kwanini sasa umewaza hivyo?”
“Weee na hayo matimbwilitimbwili ya dokta Jimmy ya kubadilisha watoto lazima vitu vingine vinipe mshtuko mkubwa sana”
“Walibadilisha watoto wa wengine ila sio watoto wetu sisi, kwanza hebu muangalie Erica au huwa humuangalii vizuri yule mtoto mke wangu? Mtoto umefanana nae yule jamani kila kitu hadi kupika, kasoro yenu ni kuwa Erica ana maneno mengi ila vingi umefanana nae, yani hata mimi ningekuwa simjui Erica basi ningemuona lazima ningesema ni mtoto wako”
“Ila kweli, kwa asilimia mia moja Erica ni mwanangu. Unajua mambo ya hiyo ndoto ya ajali ndio yamenishtua”
“Ila mke wangu unachekesha, kipindi kile Sia amekazana kusema Erick ni mwanae, ulikuwa ukipinga vikali hadi mishipa ya ufahamu inakusimama ila sasa hivi ndio unaanza kuwa na mashaka mwenye kuhusu Erica jamani!!”
“Hapana mume wangu, kuna mambo Erica anayo huwa yananishangaza sana. Erica anaweza kuwa na kitu halafu asiniambie mimi mama yake, akaenda kumwambia Vai huko au hata Sia akikutana nae njiani anamwambia kuliko kuniambia mimi”
“Aaaah usitake kujisahaulisha huko, kila siku nilikuwa nikikusikia ukimkemea mtoto kuwa asikuletee umbea wake, nilikuwa namuona anavyoondoka amenyong’onyea, ila alikuwa anajitahidi kuja kukwambia na mara nyingi ulikuwa ukimfokea, kwani unadhani na yeye hasomi alama za nyakati? Anajua hupendi umbea na yeye na umbea ndio damu damu, ndiomana hakwambii ila wewe ndio umesababisha yote hayo mke wangu”
Mama Angel alianza kukumbuka na kuona ni kweli kuwa huwa anamfokea sana mtoto wake kuhusu kumletea habari za umbea, basi aliongea pale na mumewe na kuahidi kuwa atabadilika ili kuwa karibu tena na mwanae na aweze kujua vitu vingi alivyonavyo Erica.

Usiku wa leo, Erica alitoka chumbani kwake na moja kwa moja alienda chumbani kwa Vaileth na kuanza kuongea nae,
“Dada Vai, hivi karibuni ushawahi kuongea na yule ndugu yako mchawi?”
“Kheee ndugu yangu mchawi? Kivipi?”
“Si yule dada yako, sijui anaitwa nani?”
“Aaaah Prisca, ndio nimewasiliana nae”
“Basi nimeota amekuja, kakuletea dawa kuwa unywe uweze kutoa mimba ila hiyo dawa kama ukiinywa itakutoa hiyo mimba na kizazi”
Vaileth alishtuka sana na kumuuliza Erica,
“Ila watoto wa siku hizi mnajua vitu vingi eeeh!”
“Ndio, ila kwani mimba ni jambo jipya sana kusema mtu kama mimi nisijue?”
Vaileth hakusema kitu zaidi, basi Erica alimuaga na kuondoka zake.
Vaileth alilala huku akiwaza sana, kuwa huyu Erica huyu ana makusudi gani na maisha yake? Yani aliona kama mimba hii ni kikwazo kikubwa sana kwenye maisha yake, na kuwaza kuwa atafanyaje pale tumbo litakapokuwa limetangulia mbele? Aliwaza bila ya jibu na kujitahidi kulala tu kwa muda huo.
Kulipokucha, Vaileth aliamka na kufanya shughuli za hapa na pale, ila kwa kipindi hiki alikuwa akichoka haraka sana kutokana na ile mimba aliyokuwa nayo, kwahiyo alifanya kazi nyingi kwa uvivu sana.
Muda kidogo, mama Angel nae alitoka siku hii na kumuacha Vaileth na mtoto kama kawaida,
“Ila leo nitawahi kurudi tofauti na siku zote”
“Sawa mama, hakuna tatizo”
Basi mama Angel aliondoka zake na kumuacha pale Vaileth.
Baada ya masaa machache kuna mgeni alifika pale, na mgeni huyo alikuwa ni Prisca yani dada wa Vaileth, basi alivyofika tu alianza kumsema mdogo wake,
“Ila na wewe Nyanda ulianzaje kutembea na mlinzi jamani!”
“Sijui ila si unajua mapenzi ni upofu”
“Upofu wapi? Ujinga huo, unaacha kutembea na mwenye nyumba unaenda kutembea na mlinzi loh!! Najua dawa ya siku ile ilishindikana, chukua hii ni kiboko kabisa ndani ya muda mfupi kitu kitakuwa tayari”
“Oooh asante, ila dada ondoka tu sitaki huyu mwenye nyumba akukute hapa”
Kwahiyo ilibidi Prisca aondoke tu kwa muda huo na kumuacha Nyanda akifikiria kuhusu ile dawa kama ainywe au la, huku akikumbuka maneno ya Erica ya kumpa onyo.

Muda wa mapumziko kama kawaida, Erica na rafiki yake Samia walikaa na kuanza kusema kwanza watu wa shuleni kwao, kisha kuanza kuongelea kuhusu familia zao, ila Samia ndio alikuwa na mtindo wa kumuelezea Erica kuhusu baba yake nyumbani,
“Jamani, baba kasafiri”
“Kheee kumbe kasafiri baba yenu?”
“Ndio, kidogo maneno yamepungua. Nadhani mama yangu alichoka ndiomana alianza kuongea yani ni kweli kabisa wanaume ni watu wasiofaa”
“Hadi wewe Samia unawajua wanaume?”
“Sikia nikwambie, mimi nina yule kaka yangu yani na yeye ni balaa, kuna wadada pale wa kutosha wanakuja kumlilia kaka, inamaana wote wale kawadanganya”
Basi walijikuta wakiwajadili watu wote kwa muda ule, mpaka waliporudi tena madarasani na kutangaziwa kuwa wanakaribia kujiandaa kwaajili ya mitihani walishukuru sana kwani kutokana na kile kidato walichopo basi hata likizo zile ndogo ndogo walishindwa kukaa nyumbani kwani walitakiwa kuwa shule tu muda wote.
Ila muda wa kutoka shule siku hiyo, Samia alimshawishi Erica kuwa wasitumie gari la shule, badala yake, waende kupanda daladala ya kurudi nyumbani. Walikubaliana kufanya hivyo.
Daladala walilopanda, kuna mtu akamshika bega Erica alipogeuka akakutana na Daima na kuanza kuongea nae,
“Kheee umetoka wapi Daima?”
“Nimetoka hospitali”
“Unaumwa nini?”
“Kiukweli sina hali nzuri, unajua ile mimba yangu ilitoka, basi toka kipindi hiko nimekuwa nikipata matatizo mengi sana, mpaka leo nimetoka hospitali naumwa”
“Pole sana Daima”
Kisha Daima alianza kuuliza kuhusu habari za Junior na kumfanya hata Erica amshangae kwasababu kwa mambo yale hakufikiria kabia kama huyu Daima angepata ujasiri wa kumuuliza Erica kuhusu Junior.
Basi wakati wapo mule kwenye daladala, kuna mkaka mmoja alipanda pia, ni Daima ndio aliwatonya Samia na Erica,
“Kheee mmemuona yule kijana alivyo mzuri?”
Samia nae alimuangalia kwa makini na kusema,
“Kheee jamani ni mzuri sijapata kuona mimi”
Erica alikuwa akiwaangalia tu, sababu mambo kama hayo yeye hakuwa nayo, basi walifika stendi ya kushuka ambapo alikuwa akishuka Erica, na yule kaka nae alishuka na kufanya Daima na Samia washuke pia pale stendi huku kila mmoja akimsakizia mwenzie kwenda kumuuliza kitu yule mkaka ila Erica aliona ule ni ujinga na kuamua kuondoka zake kuelekea nyumbani kwao huku akimuacha Samia na Daima wakimfatilia yule mkaka.

Mama Angel moja kwa moja alifika nyumbani kwakina Derrick na kuanza kuongea nae maana siku hii Derrick alimuita tena ili kuongea nae,
“Najua uliniuliza sana kuwa naelewa kitu gani kuhusu Elly”
“Eeeh niambie”
“Ninachoelewa ni kuwa Elly ni mtoto wangu, na kwasasa nimeelewa kuwa mtoto Elly nimezaa na Manka”
Mama Angel alishangaa kidogo na kumuuliza vizuri Derrick,
“Sasa, huyo Manka si umezaa nae mtoto wa kuitwa Sarah? Au yule Sarah si mwanao?”
“Yule ni mwanangu pia?”
“Umezaa na nani sasa? Kama Elly unasema kuwa umezaa na Manka, je Sarah umezaa na nani maana ndio mtoto wa Manka tunayemtambua!”
“Kwakweli sijui ila ninachojua ni kimoja tu kuwa Elly ni mwanangu ambaye nimezaa na Manka”
“Mmmh au Manka alizaa mapacha ila mtoto mmoja akaibiwa? Ila mbona hiyo habari naona inazidi kuchanganya akili”
“kwanini?”
Mama Angel alimwambia ukweli Derrick kwa kilichotokea baina ya Sarah na Elly, kwakweli Derrick alijihisi vibaya sana hata moyo wake ulimuuma, na kukaa chini kabisa huku akisema,
“Sikutegemea kama yale makosa yangu ndio Mungu angeniadhibu kiasi hiki!”
“Makosa yako gani tena!!”
“Umesahau kuwa mimi nilikulazimisha wewe! Nadhani imejirudi tena kwa watoto, hii ni laana kwakweli, ila si tulifanyiwa tambiko?”
“Ila nadhani kama ni laana basi imesababishwa na mdomo wako huo mchafu maana kila uliyekutana nae ulimueleza kama mimi na wewe tuliwahi kuwa na mahusiano bila kujali hata kama mimi na wewe ni ndugu!!”
“Usiseme hivyo Erica!”
“Yani hapo ndio ujijadili wewe mwenyewe na roho yako, watoto ndio wameshatembeleana, itakuwa unavuna ulichokipanda, na unaambiwa huyo Sarah anampenda Elly balaa, kwahiyo kazi kwako”
Mama Angel alimuaga Derrick na kumuacha Derrick pale akiwa na mawazo sana.

Usiku wa leo, Rahim alikuwa amekaa ndani na mama Sarah na kuanza kuongea nae kwani kwa hizo siku chache tu aliweza kugundua kuwa huyu mwanamke kwa kipini hiko hakuwa sawa kabisa. Basi alimuuliza,
“Kwani tatizo nini Mank? Inaonhyesha haupo sawa kabisa kipenzi”
“Ngoja nikwambie kitu labda utanielewa, mfano uwe na watoto wawili yani watoto wako mwenyewe halafu kwa bahati mbaya umkute mtoto wako kalala na huyo nduguye na wamepeana mimba”
“Duh!! Ni ndugu yako yamemtokea hayo?”
“Hapana, nijibu kwanza ungefanyeje?”
“Najua hilo jambo haliwezekani kwangu, yani watoto wangu wajazane mimba kweli!! Haiwezekani, kwanza nina damu kali mimi haiwezi kuwa hiyo kitu”
“Mmmh hongera zako”
“Basi, niambie tatizo ni nini?”
“Ni hivi, Sarah ni binti yangu kabisa. Ila sikujua kama nilizaa mapacha, kuna kijana nilimleta na kuishi nae hapa nyumbani kwangu kumbe ndio pacha wa Sarah, basiSarah alitembea na huyo kijanahadi wakapeana mimba”
“Duh!! Wewe hujui kama ulizaa mapacha?”
“Sijui, sababu mimi nilizimia baada ya kujifungua”
“Duh!! Wanawake mna kazi kumbe. Ila daktari aliyekuzalisha unamfahamu vizuri?”
“Ndio namfahamu na hadi huwa nawasiliana nae”
“Basi huyo ndio wa kumshikilia akwambie ukweli, maana yeye ndio anajua kama alikuzalisha mapacha na atakuwa anajua ukweli halisi wa watoto wako. Kwani wewe umejuaje kama huyo mwingine ni pacha wa huyo?”
“Aaaah ni historia ndefu”
“Sawa, basi naomba kesho tukamfate huyo daktari ili atuambie ukweli, sipendi kuona ukiwa na mawazo kiasi hiko kipenzi”
Basi mama Sarah alikubaliana na Rahim kuwa kesho yake wamtafute yule dokta na waweze kuongea nae vizuri.

Kesho yake kama ambavyo mama Sarah alipanga na Rahim, alimpigia simu dokta wake na kupanga kukutana nae mahali.
Kisha aliondoka na Rahim kwenda kukutana na yule dokta waliyepanga kukutana nae, walifika na kukuta dokta ameshafika basi Mama Sarah alimtambulisha pale,
“Dokta samahani, huyu ni mume wangu mtarajiwa anaitwa Rahim. Halafu Rahim huyu ni daktari aliyenizalisha, anaitwa dokta Jimmy”
Basi dokta Jimmy na Rahim walifahamiana pale na kukaa kuanza kuongea, kisha mama Sarah alianza kuongea,
“Najua umeshangaa sana kwa mimi kuja na mtu leo katika kuonana na wewe, usiwe na wasiwasi nae. Ni hivi nimepata mkanganyiko sana juu ya uzazo wangu, dokta niambie ukweli sasa, ni kweli nilizaa mapacha? Kama ulivyoniambia kwenye simu?”
“Kwani kwenye simu nilikwambiaje?”
“Nilikuuliza dokta, kuwa mimi nilizaa mapacha, ukanijibu kuwa nilizaa mapacha, ndio nipo hapa nikitaka ukweli”
“Aaaah Manka jamani, hivi uzae mapacha kweli halafu mimi nikwambie ni mtoto mmoja!! Inamaana siipendi kazi yangu au kitu gani? Halafu inamaana huyo mtoto mwingine nimempeleka wapi?”
Mama Sarah alipumua kidogo na kumuuliza tena,
“Unajua kuna mtloto kajitokeza na kusema kuwa ni mtoto wangu, mimi ni mwanamke siwezi kusingiziwa mtoto. Katika maisha yangu nimezaa mara moja tu. Iweje niwe na mtoto Sarah halafu atokee na mtoto mwingine aseme kuwa ni mtoto wangu?”
“Kwani imekuwaje kwanza? Niambie ukweli maana sikuelewi”
Basi mama Sarah alianza kumueleza huyu dokta kuhusu tukio la Elly na jinsi alivyokutana na Derrick, basi dokta alimuangalia kwa makini sana mama Sarah na kumuuliza,
“Kwani wewe huyo Sarah ulizaa na marehemu mzee Jimmy au ulizaa na nani? Sikuelewi ujue, unawezaje kusema sijui Derrick ndio baba wa mtoto sijui ikaenda ikarudi yani hadi sikuelewi, ulizaa na nani Manka, hebu niweke wazi”
Hapo mama Sarah alinyamaza kwa muda kidogo na kumfanya huyu dokta aongee tena,
“Mnajua nyie wanawake mna mambo ya ajabu sana, nadhani hayo mambo ya ajabu hata nyinyi wenyewe huwa yanawapa mashaka sana. Sasa wewe siku zote unasema mtoto ni wa mzee Jimmy, hadi anakufa mzee wa watu anajua kuwa amezaa na wewe, halafu wewe unaniambia habari za Derrick, vipi wewe ni mzima kweli kichwani! Umezaa na nani? Mzee Jimmy au Derrick!”
“Basi yaishe”
Mama Sarah alimgeukia Rahim na kumtaka waondoke tu, kwahiyo waliondoka zao kwa muda huo na kurudi nyumbani.

Samia na Erica wakati wanatoka shule siku ya leo, Samia alianza kumueleza Erica kuhusu yule mkaka waliyekuwa wamemfata jana yake,
“Erica, yule makaka wa jana ni noma”
“Mmmh umeanza hivyo!! Ndiomana mama yangu huwa hapendi nipande daladala sababu ya mambo kama haya haya”
“Hujui tu Erica, hivi umemuona vizuri yule mkaka? Kwanza ni mtanashati sijapata kuona”
“Kheee kwahiyo kwasasa, huoni tena uzuri wa Erick!”
“Erick sio kitu kwa yule mkaka, ila ana maringo huyo hapana jamani, hivi mkaka unamuuliza unaitwa nani halafu anakuangalia bila ya kukujibu, yani anaondoka zake bila hata ya habari kuwa umemuuliza chochote”
Basi Erica alicheka sana kwa lile aliloambiwa na Samia, kisha akamwambia Samia,
“Hamuwezi kujua jamani, usikute kaka wa watu ni kiziwi ndiomana imekuwa hivyo!!”
“Mmmh halafu Erica umeongea kitu jamani, kweli usikute ni kiziwi, sie tumekazana kusema ana maringo halafu kumbe mkaka wa watu ni kiziwi”
Muda huo Samia alicheka sana na kusema tena,
“Mimi na yule Daima tulibaki tukimshangaa yule mkaka tu, maana hajatujibu hata jambo moja, kumbe mkaka wa watu ni kiziwi loh!! Mkaka mzuri vile anakuwa kiziwi jamani! Kweli hujafa hujaumbika”
Basi waliingia kwenye gari ya shule na kuelekea makwao, muda Erica aliposhuka tu nyumbani kwako alimkuta kijana bahati yupo nje ya geti lao huku kashika mfuko mkononi na kumfanya Erica aulize,
“Umebeba nini?”
“Ni zawadi yako Erica, nimekulea”
Erica alichukua ule mfuko na kuangalia kwa makini na kuona ni viatu, alitabasamu na kumwambia bahati,
“Asante sana, ila kwanini umeniletea zawadi hii?”
“Nimejisikia tu kufanya hivi Erica, kwani vibaya jamani?”
“Hapana hakuna ubaya”
Erica alimkaribisha ndani kwao Bahati ila Bahati alikataa na kuaga kisha akaondoka zake, na kufanya Erica aingie ndani kwao.

Ila Erica alipoingia tu kwenye mlango wao wa kuingia sebleni alimkuta mama yake amekaa sebleni na kitu cha kwanza kabisa mama Angel alimuuliza Erica,
“Umebeba nini kwenye huo mfuko?”
“Ni viatu mama”
“Umevituoa wapi? Hebu tuvione?”
Erica alimpa mamake ule mfuko ambapo mama Angel alitoa vile viatu na kuviangalia halafu akasema,
“Ni vizuri ila umevitoa wapi Erica?”
“Mama, nimekutana na Bahati hapo nje ya geti ndio amenipa kasema ni zawadi yangu”
“Aaaah kumbe!! Hebu viache kwangu, nenda kabadili sare za shule huko”
“Aaaah mama, hata kuniacha nivijaribishe kidogo?”
“Huo ujinga sitaki kusikia Erica, naomba uende zako ndani. Mimi naelewa ni kwanini nimevichukua hivi viatu, na mambo ya kupokea pokea zawadi kwa wanaume sitaki kusikia kabisa”
Muda huu Erick nae alirudi kutoka shule na kumkuta mama yake akimsema Erica, basi aliipenda ile mada pia kwani mama yao alimwambia Erick,
“Nakuomba Erick uwe mlinzi wa huyu ndugu yako, kwakweli hii tabia ya kupokea pokea zawadi kwa wanaume sijui kaitoa wapi jamani!”
“Basi atakuwa kapewa hiyo zawadi na yule wa kuitwa Bahati!”
“Umejuaje mwanangu?”
“Nilimuona jana akijitapa, ila Erica huwa hasikii nilishamwambia kuwa asiwe karibu na hao watu ila hasikii kitu”
“Wewe Erica wewe, hebu nisikilize kwa makini mama yako. Maswala ya marafiki wa ajabu ajabu sitaki kabisa, rafiki yako ni Erick tu nimemaliza”
Erica hakuongea neno zaidi kwa mama yake, kwani muda huo huo aliondoka zake kuelekea chumbani kwake, hata Erick alielekea chumbani kwake pia. Mama Angel akainuka tu na vile viatu kisha akaenda chumbani na kumpigia simu rafiki yake Fetty,
“Kesho nakuja nyumbani kwako, naomba nikutane na huyo kijana wako wa kuitwa Bahati”
“Mume wangu au?”
“Hapana, huyo Bahati mdogo”
“Kuna nini kwani?”
“Hapana, hakuna kitu ila nahitaji tu kuonana nae tafadhari”
Basi waliongea kidogo na kukata ile simu, huku mama Angel akifikiria kuwa kesho yake aende huko kwa Fetty maana aliona ni vyema kama akiongea moja kwa moja na huyu kijana.
 
SEHEMU YA 366


Usiku wa siku hii mama Angel na mumewe walianza kuongea ambapo baba Angel alimueleza mkewe kuhusu mambo yanavyoendelea maana bado alikuwa akichunguza yale yaliyotokea na yanayoendelea, muda huo kuna simu ilianza kuita kwa mama Angel basi aliipokea maana aliyepiga alikuwa ni mama Derrick, akaanza kuongea nae,
“Erica mwanangu, nduguyo Derrick sijui ana matatizo gani yani muda wote anaongea peke yake, sijui tutamsaidiaje”
“Duh hatari hiyo mama, ngoja niwasiliane na dada Mage, atawatafuta Kesho anaweza akaja”
Basi alikata ile simu na kwa muda ule, alimtafuta dadake mage hewani na kumtaarifu tu kuwa awasiliane na familia ya wakina Derrick alijua kuwa itakuwa rahisi kwani alihisi Derrick atamueleza kinachomsumbua ila mama Angel alielewa wazi kuwa kinachomsumbua Derrick ni lile swala la kugundua kuwa watoto wake yani Sarah na Elly wametembea pamoja.
Basi mama Angel aliendelea na maongezi mengine na mume wake kwani hakutaka kumwambia kuhusu mambo hayo ya ndugu yake.
Waliamua kulala tu kwa muda huo, kwani ilikuwa ni usiku sana.
Kulipokucha tu, baba Angel alijiandaa na kuondoka zake ila aliongea na mke wake jambo ambalo anahitaji kufanya kwa siku hiyo,
“Nataka leo niende na Sia kwenye ile hoteli aliyompata mke wa Moses”
“Ila na sisi ni wazembe jamabi, toka tumepewa ujumbe ndio tunakumbuka leo dah!!”
“Ndio hivyo mke wangu, mambo mengi sana ila leo ni siku nzuri”
Mama Angel alikubali swala hilo, basi muda kidogo baba Angel aliondoka nyumbani kwake na kuelekea kwanza ofisini kwake.

Mama Angel, leo alienda nyumbani kwa rafiki yake Fetty kama ambavyo alipanga jana yake kuwa ataenda, kwahiyo alibeba na ule mfuko wa viatu na kwenda nao hadi kwa Fetty, alifika pale na kumkuta rafiki yake na kuanza kuongea nae,
“Bora umekuja kweli, nataka kujua tatizo ni nini rafiki yangu?”
Mama Angel alimtolea vile viatu ambavyo Bahati alimpa Erica na kusema,
“Yani huyo Bahati ndio kaanza kumuhonga binti yangu jamani!”
“Kheee jamani, viatu vizuri hivyo, nadhani kanunua bei hivi, ila kwanini kampelekea mwanao?”
“Sijui yani hebu niitie”
Fetty alianza kumuita Bahati, kisha Bahati aliitikia kuwa anaenda, ila muda huu Fetty alichukua vile viatu na kutaka kuvijaribisha maana alivipenda ila kabla hajavijaribu alisikia sauti ya Bahati ikimwambia,
“Mama, nakuomba usijaribu hivyo viatu”
Kisha Bahati akakimbia pale na kuchukua vile viatu, kwakweli mama Angel na Fetty walishangaa sana.

Fetty alianza kumuita Bahati, kisha Bahati aliitikia kuwa anaenda, ila muda huu Fetty alichukua vile viatu na kutaka kuvijaribisha maana alivipenda ila kabla hajavijaribu alisikia sauti ya Bahati ikimwambia,
“Mama, nakuomba usijaribu hivyo viatu”
Kisha Bahati akakimbia pale na kuchukua vile viatu, kwakweli mama Angel na Fetty walishangaa sana.
Fetty alijaribu kumuuliza pale Bahati,
“Wewe mtoto una matatizo gani? Kwani hivyo viatu vina nini?”
Bahati hakujibu zaidi ya kuweka vile viatu vizuri na kuondoka navyo, Fetty alimuangalia mama Angel na kumwambia,
“Haya ndio matatizo ambayo nakumbana nayo kwakweli kwa hawa watoto, wamechukua tabia za mama zao huko wananisumbua balaa”
“Kheee pole sana, bora wangechukua tabia za baba yao”
“Yani wangechukua tabia ya baba yao naona ingekuwa heri kwangu, kwanza baba yao ni mpole, ni mwenye huruma, halafu ni mtu wa kujishusha na kusikiliza ushauri, sasa hawa watoto wapo masikio waruwaru kama antena za chuma”
Mama Angel akacheka kidogo na kusema,
“Yani nacheka kama mazuri, ila kwakweli huyu mtoto kaonyesha dharau za hali ya juu”
“Bora hili shoga yangu, navumilia mengi ujue usione hivyo, huyu Bahati ndio ana kiburi hatari, hivyo mara nyingi namtimua hapa aende kwa mama yake. Ukija kwa upande wa huyo Abdi nae kila leo kazua jipya huko mtaani, ila Bahati akiwepo ndio anamtuliza Abdi maana Abdi akiwa hapa ndio anajifanya kidume wa familia, mitoto ya laana hii inasumbua hatari”
“Pole mwaya, ila bado huyu mtoto kaaacha maswali kichwani mwanangu, ni kwanini kampa mwanangu zawadi ya viatu? Halafu kwanini kakukatalia wewe usijaribu, isije ikawa ndio mambo ya waganga!”
Fetty alicheka kidogo na kusema,
“Itakuwa mambo ya babu wa Bagamoyo hayo, yale mambo ya Dora na rafiki yake Sia”
“Ila mtoto mdogo hivi mambo ya waganga ya nini?”
“Weeee uliza kwanza, mama wa huyu mtoto ni kupuliza madawa kwa waganga kila leo. Babu yake huyu mtloto alifia kwa mganga sababu ya ushirikina, huyo mamake hajaacha ushirikina hadi leo ingawa anajua wazi kuwa haumsaidii, hajua kama nyumba yangu naifanyia dua kila leo, hayo madawa yake yanagonga mwamba hapa, yani mamake huyu anafanya biashara Fulani hivi ila kwa ndumba, yani ningekuwa sio mtu wa ibada kwa hakika ningeshaachana na mume wangu. Si unajua kipindi kile nimekuja kukulalamikia kuhusu mume wangu kuwa ameanza kukutaja wewe tena, yani haeleweki wala nini hadi na mimi nilihisi kuchanganyikiwa nikawa naenda hotelini huko na kukaa hadi usiku ndio narudi nyumbani kwangu, ila sasa nilikutana na yule mama wa kuitwa Ester yule ambaye huwa anawafanyia maombezi, nilijikuta nikiongea nae kuhusu mume wangu, alinishauri mambo mazuri sana, alisema hakuna kinachoshindikana kwa Mungu, kila kitu ni kuomba maana kama mpaka nimefunga nae ndoa na ninaishi nae hadi leo basi niamini kuwa ni mume wangu, nisikubali shetani anitenganishe nae, ukizingatia nampenda. Basi yale maneno yake yaliniingia sana, tulikutana tu njiani ndio kuongea yote hayo, basi nilivyorudi nyumbani nikasema sasa nabadilika, nilianza kufanya ibada upya. Kuna siku nilichukua pesa na kwenda kutoa msaada kwa watoto yatima, yani nilifanya vile kama sadaka kwangu yani nilitoa sadaka kwaajili ya mume wangu, kisha tukafanya dua na wale watoto, mbona mume wangu alianza kubadilika mwenyewe, hadi sasa kabadilika kabisa. Kwakweli mume ndani ukimuona kabadilika sio na wewe unaota pembe na kubadilika ili umkomeshe, huwezi jua anapitia kitu gani ndiomana kabadilika, cha muhimu ni kufanya maombi tu”
“Ooooh kweli uminiambia kitu kikubwa sana, hata mimi yule mama huwa ananifundisha mambo mengi sana, namshukuru Mungu kwa maombi ninayofanya kwaajili ya mume wangu inasaidia kwa yeye kutokutamani wanawake wengine”
“Ila wanawake tulioolewa tuna nini lakini, yani tumeacha hata kuzungumza yaliyotukutanisha na kuanza kuzungumza kuhusu waume zetu, dah wanaume wanatutoa akili hawa”
Mama Angel alicheka sana, maana kweli waliacha mada zao na kuanza kuzungumza kuhusu waume zao. Basi waliongea sana na Fetty aliahidi kumsemea Bahati kwa baba yake maana hakurudi tena hadi mama Angel aliaga na kuondoka zake.
Mama Angel akiwa kwenye gari lake, kuna mtu alimuona na kuamua kusimamisha gari kisha kushuka na kumfata alimshika bega ambapo yule mtu aligeuka na alikuwa ni mke wa Moses, basi mama Angel alimsalimia pale ila yule mwanamke aliitikia ile salamu kwa uoga kiasi, basi mama Angel akamuuliza,
“Hajambo mumeo?”
“Hajambo”
“Unajua nini, kuna mambo mtu huwezi kuyaficha milele kuna kipindi lazima yatakuwa wazi tu”
“Ila mimi sijamtuma kufanya hayo, usinifikirie vibaya”
Mama Angel alimshangaa mwanamke huyu kwa kuanza kujishuku, basi alimuangalia kwa makini na kumuuliza,
“Kwnai wewe ulimtuma kufanya nini sasa mpaka kafanya kinyume?”
“Sikia, mimi ni mwanamke tu. Mimi nimeolewa tu wala sina sauti katika ndoa yangu, ni mwanaume ndio anaamua cha kufanya. Nadhani Sia kakwambia kuwa kaniona na yule dokta, yule ni shemeji yangu nawezaje kumkwepa? Ila sikumtuma mimi Moses kufanya kazi na baba wa Erick ila hatukufikiria kama baba wa Erick atakuwa na jambo lolote baya”
“Ngoja nikuulize swali, mfano umelea mtoto wako vizuri kabisa halafu unakuja kupata habari kuwa yule mtoto sio wako ila alibadilishwa hospitali, kama wewe ungejisikiaje?”
“Mmmh sijui, ila kwanini umeniuliza hivyo?”
“Kamuulize mume wako, kwakweli huu mlioufanya kwa kushirikiana na huyo dokta wenu sijui shemeji yako sio uungwana kabisa wala sio utu. Kwakweli Mungu anawaangalia tu kwa jambo hili”
“Unasema? Yani watoto wako walibadilishwa?”
“Sio watoto wangu, ila kila aliyezalia ile hospitali ya kijinga kabadilishiwa mtoto, sijui kwanini wamefanya huo mchezo jamani!! Na mumeo ameshiriki kwenye hujuma hiyo”
Mke wa Moses alikaa kimya kwa muda kwani hakuelewa kuwa ajibu kitu gani kwa muda ule, ila aliamua kuondoka tu hata mama Angel alipomuita tena hakuitikia na kumfanya mama Angel ahisi pale kuna namna zaidi, basi alirudi kwenye gari lake na kuendelea kurudi nyumbani kwake.

Leo mume wa Fetty alivyorudi tu, aliamua kumueleza kuhusu mtoto wao Bahati na jinsi alivyompokonya vile viatu,
“Mmmh, unahisi nini mke wangu?”
“Nihisi nini hapo zaidi ya ndumba? Hiyo ni ndumba hakuna ubishi ni ndumba hiyo”
Basi baba Bahati aliamua kumuita mwanae pale mbele ya mama yake mlezi na kuanza kumuuliza kuhusu hivyo viatu,
“Haya wewe mtoto usiyejielewa yani unajifanya umekua sasa hadi umefikia uwezo wa kumuhonga kitu mwanamke, haya kwanini ulimpelekea viatu huyo Erica?”
Huyu Bahati kidogo alikuwa akimuogopa baba yake maana alikuwa mkali, aliona akichekea hawa watoto wake basi watafanya ujinga sana ukizingatia walikuwa na ujinga mwingi nyumbani, basi Bahati alianza kwa kumuomba msamaha,
“Naomba unisamehe baba, ila mimi sikuwa na nia mbaya, nilimpelekea vile viatu kama zawadi tu”
“Alikwambia kuwa anahitaji zawadi ya viatu?”
“Hapana, ila siku ya kwanza kufahamiana nae yule ilikuwa ni siku ambayo alikuwa akiulizia bei ya kiatu”
“Yani nyie watoto hata sijui hizo tabia mmerithi kwa nani, halafu Bahati sikukufikiria ujue, nilijua huo ujinga anafanya ndugu yako Abdi tu. Huyu Abdi si ndio alifanya niitwe shuleni kwa kutaka kumbaka huyo huyo Erica, halafu leo hii na wewe huyo kiguu na njia kwenda kupeleka viatu kwa Erica. Kama mnajiona mmekuwa basi muhame nyumbani kwangu mkajitegemee huko sio kuniletea ujinga tu hapa, mnadhani mnafundisha nini wenzenu?”
“Nisamehe baba”
“Haya, na hivyo viatu uliweka nini maana hata mama yako umegoma asijaribishe”
“Sijaweka kitu baba”
“Usikatae wakati mamako anapenda sana ushirikina, labda kashakupa madawa ya kukufanya uweze kumpata huyo Erica, kwakweli leo umenichefua sana. Niambie umeweka nini kwenye viatu”
“Kweli baba sijaweka kitu”
Baba Abhati aliona kuwa anadanganywa na mtoto wake, basi aliinuka na kuvua mkanda wake huku akimshika mwanae, yani hapo Bahati alijua wazi kipigo kitakachomuangukia hapo sio cha kawaida, ilibidi amwambie baba yake ukweli,
“Baba usinipige, ngoja nikwambie ukweli ulivyo”
“Haya niambie na usinifiche chochote maana ukinificha nitajua”
“Siku moja mama alinikuta nikiwa na mawazo, aliniuliza ni nini, niliamua kumwambia ukweli kuwa kuna binti anaitwa Erica nampenda sana, basi mama akaniambia kuwa nisijali. Aliniuliza tu, Erica anapenda nini kama zawadi, nikamwambia anapenda viatu, aliniuliza tu namba ngapi anavaa nikamtajia, basi kesho yake mama akaniletea vile viatu akasema nikampe Erica na atakapoenda kuvivaa atanipenda sana ila sijui ni sababu ya nini na mimi sijaweka chochote ndiomana nilimkataza hapa mama asivivae vile viatu asije akanipenda yeye”
Yani hadi baba Bahati alijikuta tu akicheka na kusikitika, kisha kumtimua mwanae na kumwambia kuwa akamrudishie mamake vile viatu,
“Na umwambie kuwa baba kaujua ukweli wote”
Fetty alidakia,
“Nilijua tu, maana yule mwanamama haaminiki kabisa, ila mimi siruhusu avirudishe kwanza, mwambie avilete”
Basi Bahati akaambiwa avilete ilibidi akavichukue na kuwapelekea, moja kwa moja Fetty alivichukua na kutoka navyo nje kisha akavimwagia mafuta ya taa na kuvichoma moto, kisha akamwambia bahati,
“Mwambie mama yako, mama kule nyumbani kachoma moto vile viatu, najua atakuja tu akipata hiyo habari”
Bahati hakuongea neno zaidi zaidi ya kuondoka tu, ila kiukweli Fetty na mume wake walisikitika kuona mtoto mdogo kama Bahati kaanza kufundishwa vitu vya kupendwa na mwanamke.

Basi usiku wa leo, mama Angel anaamua kumuelezea mumewe alivyoenda kwa Fetty maana anamwambia na jinsi Erica alivyopewa viatu, na jinsi alivyokutana na mke wa Moses,
“Naona kuna mengi sana nyuma ya pazia ambayo hatuyajui maana ni ngumu kutaona kwa macho ya kawaida”
“Ni kweli mke wangu kuna mengi sana, kuna muda nawaza hata sijui cha kufanya, unajua hata kule tulipoenda na Sia hatujawakuta tena!!”
“Nilijua tu lazima watakimbia, halafu leo nilivyomuona mke wa Moses nikasahau kama na wewe ulipanga kwenda kumtafuta, ila ningekuwa mtekaji ningemteka yule mwanamke maana najua ana mambo ya mumewe aliyoyafanya, na sasa nazidi kupata picha kuwa Moses ndio alihusika kwenye wizi wa duka lako”
“Mmmmh ila kwanini Moses afanye hivyo? Mbona siku zote hakufanya hivyo?”
“Sijui ila nina hisia mbaya kwakweli, kama Moses ameweza kushirikiana na huyu dokta aliyeharibu maisha ya watu wengi, je anashindwa kushirikiana na wabaya katika kuharibu biashara yako? Halafu nadhani walijua utafilisika maana ndio biashara uliyokuwa unaitegemea sana”
“Na kweli niliyumba si masikhara, isingekuwa mke wangu upo vizuri basi kipindi kile ndio ningekuwa naumbuka jamani, nakumbuka mama hakuwepo, halafu baba aligoma kabisa kunisaidia, yani niliyumba hatari. Ila mke wangu kwakweli Mungu akuzidishie yani wewe ni mwanamke kweli uliyeumbwa kwaajili yangu, kumbe kuna wajinga wakila tu pesa na kuhisi wananikomesha”
“Umekubaliana na usemi wangu eeeh kuwa Moses kahusika?”
“Hapana, sijasema hivyo”
Mara simu ya mama Angel ilianza kuita, na aliyekuwa akipiga alikuwa ni Fetty basi mama Angel alipokea simu ile na kuanza kuongea nayo ambapo Fetty alimueleza yale yaliyojiri yote wakati Bahati alipoulizwa na baba yake,
“Kheee makubwa, kwahiyo karudi na huyo mama yake?”
“Arudi wapi? Nadhani kamsimulia na kumfanya ashikwe aibu, yani yule mwanamke sijui ataacha lini ushirikina. Na bora umegundua mapema”
Kwakweli mama Angel alishangaa sana na kuagana na Fetty, kisha alimsimulia kiasi mume wake na kusema,
“Ngoja nikamueleze na huyo Erica”
“Jamani, kuna mambo duniani. Ila usisahau kesho kama tutaenda wote kiwandani, si unajua ndio ile Jumamosi tuliyopanga?”
“Naelewa, hakuna tatizo”
Basi mama Angel aliongea kidogo na mume wake pale kisha kuinuka na kwenda chumbani kwa binti yake.

Muda huu Erica alikuwa chumbani kwake ila alitaka kutoa karata zake ili aanze kucheza maana alikuwa amechukia jana yake kwa Erick kusaidiana na mama yake kumsema, kwahiyo hakutaka hata kwenda kucheza zile karata na Erick kwa muda huo wala nini.
Ila kabla hajazitoa, aliingia mama yake na kumfanya ashtuke,
“Mbona umeshtuka sana?”
“Aaaah hapana mama, hamna kitu”
“Nilijua tu bado hujalala na hivi leo ni Ijumaa nahisi unawaza kucheza karata tu hapo”
Erica aliinama tu na kuangalia chini, basi mama yake alianza kumpa habari za Bahati jinsi alivyoambiwa na Fetty,
“Unaona mwanangu, kumbe walikuwekea dawa, ungejikuta taratibu unaanza kumpenda huyo Bahati”
“kwahiyo mama, hiyo dawa ndio kama ile ambayo dada Vaileth alipewa na ndugu zake kwaajili ya baba”
“Aaaah wewe nawe unaleta habari gani, mimi nakwambia mengine halafu wewe unaleta habari zingine, nakueleza mambo ya huyo mleta viatu wako Bahati”
“Basi mama nimekusikia, nashukuru kwa kuniponya maana nisingejua ningevaa tu vile viatu”
“Haya mwanangu, ila safari nyingine jitahidi uwe makini sana na hayo mambo mwanangu, sitaki kukupoteza kizembe. Muombe Mungu kila utokapo na uingiapo, ukiwa shuleni muombe Mungu, ukitoka shule muombe Mungu, jitahidi kufanya sala kila muda”
“Sawa mama”
Basi mama Angel alimuaga mwanae na kuondoka zake kwa muda huo, kwakweli Erica nae aliacha kucheza karata kwa muda huo na kuzibeba hadi chumbani kwa Erick ambapo alimkuta ndio anajiandaa kulala basi alimshtua na kumtaka wakae na wacheze karata, ingawa Erick alikuwa amechoka ila alishindwa kumkatalia Erica kucheza nae karata, ambapo wakati wakicheza karata ndipo Erica akamsimulia kuhusu alichoambiwa na mama yake kuhusu vile viatuambavyo aliletewa na Bahati,
“Kheee kumbe ndio ilikuwa hivyo?”
“Ndio, eti ili nimpende jamani!! Duniani kuna mambo ya ajabu”
“Ila na wewe kwanini ulichukua viatu vyake kama humpendi?”
“Mimi simpendi kweli jamani”
“Haya unampenda nani?”
“Mimi nakupenda wewe”
Erick alitabasamu na kumwambia,
“Ila mimi ni ndugu yako?”
“Kwani ndugu hawaruhusiwi kupendana jamani Erick?”
“Aaaah kumbe unasemea upendo wa ndugu”
“Wewe ulijua ni upendo upi?”
“Hukuna kitu, tucheze tu karata”
Basi waliendelea kucheza karata, na mwisho wa siku kama kawaida walijikuta wakiwa wamelala pamoja kwenye kitanda cha Erick.
Kulipokucha, Erica ndio alikuwa wa kwanza kuamka na muda kidogo Erick nae aliamka ila Erica alimuangalia Erick na kushtuka kisha alimuuliza kwa mshangao,
“Nini hiko kimetuna hapo mbele ya kaptula yako?”
Erick aliona aibu kiasi na kuchukua shuka kujifunika huku akimjibu Erica,
“Ndio huwa hivi kila asubuhi”
“Mmmh mbona sijawahi kukuona?”
“Labda leo ndio umeniangalia”
“Hebu nionyeshe, yani vua nguo nione imekuwaje hadi kukatuna”
Erick alicheka tu na kutokujibu chochote,
“Kisha aliinuka na kutaka kama kuvua kaptula yake”
Gafla ikasikika sauti ya mama Angel akimuita Erica, kwahiyo kwa haraka Erica alitoka mule chumbani kwa Erick na kukimbilia ambapo mama yake kamuita.
“Erica, mimi na baba yenu tunatoka muda sio mrefu kwahiyo make mumuangalie mtoto. Leo zamu yenu sio kumuachia Vaileth tu”
“Sawa mama”
Basi moja kwa moja Erica alienda chumbani kwake kwaajili ya kuoga na kuondoa uchovu wa usiku.

Basi mama Angel na baba Angel wanafika kiwandani na kuanza kufanya mambo mbalimbali ya pale kiwandani, ila baada ya muda kidogo anafika pale rafiki wa baba Angel ambaye ni Juma kisha Juma anamuita baba Angel na kuongea nae,
“Ndugu yangu, tulipanga vizuri kabisa ila kwanini umenigeuka hivyo?”
“Nini tena?”
“Nilikuomba twende wote na kijana wako kwenye ile kazi yangu ila ukanigomea, kwakweli ulichonifanyia sio kizuri”
“Hivi ni kosa langu au kosa lako Juma? Ni lini ulisema kuwa twende leo?”
“Nilikupigia simu sana ila simu zangu hukupokea na wala hukujisumbua kunipigia tena. Sijapenda kabisa ndugu yangu”
“Naomba unisamehe tu yani kichwa hiki kina mambo mengi sana, naomba siku unayopanga uje nyumbani moja kwa moja halafu tutaenda huku kwenye biashara yako”
“Nitampata Erick?”
“Utampata ndio, hata shule tutamfata. Mimi mwenyewe nimekuruhusu kuhusu hilo”
Basi Juma aliongea kidogo tu na kuaga pale na kuondoka zake, kisha baba Angel alirudi ofisini na kuendelea na mambo mengine na mke wake, ila muda kidogo yule mteja ambaye huwa wanamuita mwarabu alifika pale kwenye ofisi ya baba Angel kuagiza mzigo kama kawaida yake, ila mama Angel alipomuona huyu mzee alishtuka kidogo ingawa aliongea nae mawili matatu,
“Oooh wewe ndio mama wa yule mtoto mrembo wa kuitwa Erica!”
Mama Angel akatabasamu kidogo na kusema,
“Ndio, mimi ndiye mama yake”
“Nimependa sana yule mtoto anavyoongea, nilimuomba siku anikutanishe na ndugu zake wengine, alinionyesha tu yule kijana mzuri Erick, halafu alisema ana dada yake anaitwa Angel na mdogo wake anaitwa Ester”
“Kheee kumbe alikutajia wote!”
“Ndio, yupo vizuri sana yule binti kwakweli, halafu ana akili sana. Natamani kumuona dada yake huyo Angel najua nae atakuwa ni mzuri sana kama yeye”
“Karibu sana, tutakukaribisha nyumbani kwetu”
Waliongea ongea pale na yule mzee kisha yule mzee aliweka oda yake na moja kwa moja kuaga mahali pale na kuondoka.
Wakati mama Angel na baba Angel wanaondoka, njiani mama Angel alimwambia mume wake,
“Ila yule mzee jamani kafanana na Rahim ujue!”
“Yule mwarabu?”
“Ndio, nahisi ni ndugu wa Rahim na huenda ni baba yake”
“Mmmmh!”
“Ndio, mimi simfahamu baba yake Rahim inawezekana akwa yule, sijaongea sana na baba yake ila nahisi maana Rahim alishawahi kunieleza kuwa baba yake ni mkarimu sana na yule mzee ndio yupo hivyo, anaonekana kuwa mkarimu sana”
“Duh!! Inawezekana lakini”
“Halafu yule mzee anataka kumuona Angel”
“Kheee kamjuaje Angel?”
“Si huyo mwanao chaumbea Erica, amemtajia orodha nzima ya watu kwenye familia hadi Ester”
“Kheeee kweli mwanangu yupo kwenye viwango vingine vya umbea”
“Ni kweli kabisa, yule ni kiwango yani umbea wake kungekuwa na shule ya umbea ukimpeleka akasome utakuta amekuwa mwalimu wao”
Baba Angel alicheka sana maana pia hakutegemea kama binti yake Angel aliweza kupiga Stori na huyo baba hadi kufikia hatua ya kumtajia orodha ya watu kwenye familia yao.
 
SEHEMU YA 367


Leo madam Oliva anafikiwa na mgeni wa muda mrefu ambaye ni rafiki yake, kwahiyo anafurahi sana kufika pale na kuanza kumwambia madam Oliva,
“Natumai leo nimemkuta mtoto wako!”
“Ndio, mwanangu yupo leo siku hizi nakaa nae”
Basi madam Oliva anamuita Paule ambaye alifika kwa haraka na kuanza kumtambulisha kwa rafiki yake huyu,
“Mwanangu mwenyewe ndio huyu anaitwa Paul, halafu Paul huyu ni rafiki yangu ni mwalimu pia anaitwa mama Yusra”
Basi Paul anamsalimia pale na kumfanya huyu mama amsifie sana kuwa Paul anaonekana ni kijana mpole,
“Yani inaonyesha Paul ni mpole sana, hongera kwa hilo madam”
“Asante”
Kisha madam Oliva alimruhusu Paul kuendelea na kazi zake, muda kidogo anafika Steve ambapo madam Oliva alimtambulisha pia kwa rafiki yake huyu na kufurahi pale huku wakiongea mambo mbalimbali.
Wakati wakiondoka, ndipo mama Yusra alipomuuliza rafiki yake,
“Hivi nakumbuka si ulisema babake Paul alimtelekeza mtoto?”
“Ndio, wanaume wana mambo ya ajabu sana. Tunawavulia basi tu”
“Kwahiyo umeamua kurudiana nae?”
“Nirudiane nae wapi? Huo ujinga siwezi kuufanya hata nikiwa nimekufa, yani siwezi kufanya kitu kama hiko kabisa, yule mwanaume sitaki hata kumuona kwenye uso wangu”
“Mmmh ila mbona ndio umenitambulisha pale kwako”
“Kivipi?”
“Kwani yule Steve si ndio babake Paul?”
“Hapana, yule sio”
“Acha masikhara bhana madam, yule ndio baba wa mtoto wako, hata chizi huwezi kumdanganya, mtoto kafanana kila kitu na yule baba”
Madam Oliva alishindwa hata kutia neno pale, moja kwa moja alimsindikiza rafiki yake hadi alipopanda basi.
Wakati anarudi alijiuliza sana kwanini inakuwa hivyo? Hakupata jibu kabisa, wazo la mama Angel kuwa huenda alibadilishiwa mtoto linaanza kufanya kazi kwenye akili yake, basi anaona ni vyema aanze kumchunguza Steve ili ajue kama kuna mwanamke Steve alizaa nae ili aweze kupata ukweli.

Ilipita kama wiki, ndipo mama Sarah alikuwa huru kwani kwa siku hiyo Rahim aliondoka yani siku ambazo Rahim alikuwepo alishindwa kufanya chochote sababu muda mwingi Rahim alionekana kumfatilia kwa mambo yote anayoyafanya.
Basi kwa siku hiyo aliamua kumpigia simu dokta Jimmy na kuanza kuongea nae,
“Ila dokta Jimmy, kwanini ulianza kuniambia vile mbele ya yule mtu?”
“Mtu gani?”
“Yule niliyekuja naye na nikakutambulisha kuwa ni mume wangu mtarajiwa”
“Mume mtarajiwa wakati yule ni moto”
“Moto? Moto kivipi?”
“Yule jamaa sio mzima, au na wewe ni moto?”
“Sikuelewi dokta, unazungumzia nini kwani?”
“Sikia nikwambie, mara kadhaa nimewahi kumuona yule jamaa hospitali moja hivi akifata vidonge vya ARV”
“Unaongelea nini kwani? Ni vidonge gani?”
“Uko wapi wewe hujui ARV? Wa wapi wewe jamani? Hujui mtu akianza kunywa hivyo vidonge kapatwa na nini?”
“Sielewi kweli, hebu nieleweshe”
“Kwa kifupi yule jamaa yako ni muathirika, ana ukimwi”
“Unasemaje?”
Yani mama Sarah aliona hata simu ya moto, alijikuta tu akiikata ile simu yani aliiona haifai. Ila baada ya muda kidogo alipigiwa tena simu na dokta Jimmy,
“Basi tukutane ili tuweze kuzungumza, nitakushauri cha kufanya usijali hata kama umekutana nae kimwili”
“Utanishauri nini? Jamani si ndio nitakuwa nimeubeba mimi!!”
“Sikia Manka, usipaniki wala nini. Tukutane halafu huyo jamaa itakuwa amekufanyia makusudi, ila atajuta kutufahamu, tulia tu Manka najua unanijua vizuri, siwezi kuacha uteketee. Halafu tutaongea vizuri na kuhusu yale madai yako”
Mama Sarah aliitikia tu ila kiukweli hakuwa na furaha yoyote ile.

Sia kama kawaida yake katika harakati za kumfatilia dokta Jimmy, kwa bahati anamuona mahali na kuanza kumfatilia kwa karibu zaidi, mara dokta akamuona mzee Jimmy kasimama mahali anaongea na simu,
“Ndio, tukutane kule kwenye kaburi la mzee kama baada ya masaa matatu maana mimi ndio naondoka huku muda sio mrefu”
Yani moja kwa moja Sia akahisi tu kaburi linalosemwa ni kaburi la mzee Jimmy, yani muda huo alihisi kama akili yake ikipaa kwani aliondoka hapo na kumpigia simu baba Angel na kuomba akutane nae mahali ambapo muda mfupi tu walikutana hapo na baba Angel,
“Muda sio mrefu nimemsikia dokta Jimmy akiwasiliana na mtu kuwa wakutane kwenye kaburi la mzee Jimmy, kama inawezekana twende muda huu huko huko”
“Basi ngoja niende huko, ila wewe Sia ubaki”
“Mmmh hapana, twende tu wote hata sijui usalama wa huko, naomba twende wote”
“Usalama gani kwani kuna vita?”
“Mtu akifikia hatua ya kubadilisha watoto ni sawa na vita hiyo, sio wa kumuamini mtu huyo, twende wote tu”
“Kwahiyo wewe ndio unakuwa kama bodyguard wangu!!”
Baba Angel alicheka kiasi kisha aliingia kwenye gari na Sia na kuondoka kuanza safari ya kuelekea kwenye kaburi la mzee Jimmy.
Kwenda kwenye kaburi la mzee Jimmy kulikuwa na mwendo kiasi, kwahiyo baba Angel ilibidi aongeze mwendo ili aweze kufika kama wale walivyopanga baada ya masaa matatu, walifika na kusimamisha gari pembeni kwanza kisha walishuka na kuanza kuelekea kwenye eneo la lile kaburi.
Kabla hawajafika kabisa walimuona dokta Jimmy na mama Sarah ndio wamesimama pale kwenye kaburi wakiongea, yani pale baba Angel ndio alipoamini vingi alivyosikia kuhusu mama Sarah

Kabla hawajafika kabisa walimuona dokta Jimmy na mama Sarah ndio wamesimama pale kwenye kaburi wakiongea, yani pale baba Angel ndio alipoamini vingi alivyosikia kuhusu mama Sarah.
Kwakweli baba Angel alipaniki sana kwa muda ule na kumwambia Sia,
“Kwakweli mimi naenda pale ili waniambie mbivu na mbichi”
Baba Angel akataka kwenda ila Sia alimzuia na kumwambia,
“Hapana Erick usiende, tujibanze tu na kuangalia kinachoendelea, huwezi jua kuwa wale watu wana ajenda gani!”
“Sio ajenda gani, hebu kumbuka yule dokta kafanya mambo mangapi? Halafu yule Manka kama mjinga kabisa, anawezaje kushirikiana na mtu kama yule!”
“Ni kweli kabisa usemayo, ila tusisonge popote, tusimame hapahapa tuendelea kuchunguza”
“Kwakweli uchunguzi usio na majibu huwa siuwezi kwakweli, siku zote hizi nipo tu makini na uchunguzi hata mambo mengine sifanyi, yani hapa natakiwa kupata jibu au kuacha haya mambo kama yalivyo. Natakiwa nionane nao kabisa ili nijue mbivu na mbichi”
Baba Angel alikuwa bado akihitaji kwenda ila bado Sia alimzuia kwa kumshika mkono, baba Angel ilibidi amsukume Sia pembeni na moja kwa moja kwenda waliposimama dokta Jimmy na mama Sarah hata wao walimshangaa kwani hawakutegemea kumuona, basi baba Angel akasema,
“Bora nimewakuta, niambie ukweli dokta kuhusu watoto wetu uliwafanya nini?”
“Kwani wewe unataka kitu gani? Kama kilichotokea tayari kilishatokea huwezi kubadilisha chochote, unataka nini kwani?”
Baba Angel alijikuta akijawa na hasira sana kwa lile jibu la dokta, basi moja kwa moja alimkunja dokta na kumpiga ngumi moja ya sura na kufanya yule dokta hata aanguke chini, mama Sarah alijaribu kumtoa baba Angel pale na kumwambia,
“Ondoka wewe, unataka kujitafutia matatizo”
“Matatizo gani? Na wewe usinijibu muuwaji mkubwa wewe”
Muda ule ule baba Angel alimnasa kibao mama Sarah maana alijikuta akikumbuka yale mambo ya yeye kuwekewa sumu, kwakweli mama Sarah alichukia sana na kusema,
“Nadhani Erick hunijui vizuri mimi, hivi kweli wa kunizaba kibao wewe!!”
Erick hakumsikiliza ila alimkunja dokta Jimmy na kumwambia,
“Leo sikuachii hadi umeniambia ukweli wa kila kitu”
Sia alikuwa yupo kule kule kwa mbali akiangalia kila kinachoendelea, gafla aliona kama mama Sarah akitoa ishara kwa mtu, vile Sia alipokuwa akiangalia vizuri ilia one ni mtu gani aliyepewa ishara alishtuka kumuona kashika bastola halafu kailengesha kwenye kichwa cha baba Angel, kwakweli kwa muda ule ule Sia alisema kwa nguvu sana,
“Erick, inamaaaaaa….”
Kisha akageuka upande aliokuwepo baba Angel, muda ule ule alishangaa kuona baba Angel akiwa chini huku damu zikimtoka, yani hapo Sia alihisi kama moyo wake unalipuka hivi na kuanza kupiga kelele za kuomba msaada sasa,
“Tunakufaaaa, tusaidieni….”
Na kwavile Sia alikuwa na sauti kali, zile kelele zilifanya hata dokta Jimmy na mama Sarah wakimbie halafu Sia alienda eneo lile huku baadhi ya wananchi nao wakisogea mahali pale.
Kwakweli baba Angel alikuwa akitokwa na damu nyingi sana, kwahiyo ilibidi wasiulizane pale kuwa imekuwaje zaidi ya kuanza kumpa huduma ya kwanza baba Angel ambaye walipomuangalia vizuri ilionyesha kapigwa risasi kadhaa miguuni, basi wale wananchi walijitahidi kuweza kumbeba hadi kwenye gari yake kisha kijana mmoja ndio alijitoa kwaajili ya kuendesha na kuwapeleka hospitali.

Mama Angel akiwa nyumbani kwake, leo aliona ni vyema akatoka kidogo na kwenda kuangalia kinachoendelea kwenye ofisi yake, ila alipofika tu ofisini alikutana na mwanamke mmoja ambaye alimsalimia kwakweli mama Angel alimshangaa kiasi ingawa alikuwa akimtambua mwanamke huyo, basi alisimama na kuongea nae kidogo ila yule mwanamke alimuomba wakae eneo kidogo na apate kuzungumza nae, ikabidi mama Angel akubali na walikaa eneo ambalo sio mbali na ofisi ya mama Angel kisha yule mwanamke alianza kumwambia,
“Unajua sikuwa najua unapoishi wala unapofanyia kazi, ila nikajaribu kukuangalia mtandaoni na kugundua ofisi yako hii ilipo basi nikaamua kuja kwa haraka ili kukwambia hili”
“Niambie tu”
“Ingawa najua mume wangu hataki kabisa swala hili niseme ingawa nilimwambia kuwa nitasema”
“Yani Moses hataki? Niambie tu ni kitu gani?”
“Nisikilize kwa makini, ni hivi Moses ndiye aliyesababisha hadi duka la mumeo likaibiwa kila kitu”
Mama Angel alishtuka kiasi na kuendelea kumsikiliza huyu mama ambaye ni mke wa Moses na aliendelea kueleza,
“Usishtuke tu kuhusu hilo, ila shtuka hili. Mume wangu hakujiamulia tu kufanya vile, ila aliombwa na mkwe wako kufanya vile”
“Kheeee babake Erick!!”
“Ndio, mzee Jimmy. Yeye ndio alimuomba Moses kumuibia mumeo kwa lengo kuwa mumeo atachanganyikiwa kabisa baada ya ule wizi na atafilisika na kuomba msaada tena kwake”
Mama Angel alipumua kidogo na kusema,
“Kheee makubwa, eeeh ikawaje tena?”
“Mimi nilimkataza Moses kukubali ila mume wangu hakutaka kuelewa ni kwavile aliahidiwa pesa nyingi sana na yule mzee ila ndio baada hapo tulianza kuwa watumwa wa mzee yule yani tulifanya kitu ambacho alikitaka yeye”
“Duh!! Niambie tu hata usiogope”
“Kama una kumbukumbu nzuri, kuna siku mumeo alivamiwa akiwa kwenye gari na aliibiwa kila kitu na kurudi nyumbani kwa miguu”
Mama Angel alikumbuka hilo tukio ambalo huwa hata halikumbushi maana huwa linamtia uchungu sana na kuendelea kumsikiliza huyu mwanamke tu kuhusu kitu anachokizungumzia,
“Sasa pale ni vijana ambao walitumwa na Moses, na aliagizwa na mzee Jimmy kufanya vile. Nakumbuka mliamua kwenda kuishi kwa mzee Jimmy ila mliishi kidogo na wewe kumshawishi mumeo kuondoka, kisha akaondoka na kurudi kwenu. Pale ndipo mlipomchanganya mzee Jimmy maana sijui ilikuwaje mkauza ile nyumba yenu na kwenda mbali bila kumwambia yoyote yule kati ya ndugu zenu. Pale ndio palikuwa pagumu sana kwa mzee Jimmy, sijui hata mlifikiria nini hadi kufanya yote yale ila ndipo mlipomchanganya mzee Jimmy, hamjui tu ni jinsi gani mliweza kumchanganya baada ya pale na aliumia sana roho. Sikujua ni kwanini mzee Jimmy alikuwa akifanya vile kwa mwanae mpendwa ila badae alisema kuwa alitaka siku Erick aende kumpigia magoti na kulia kwa maisha kumshinda ila haikuwa hivyo, sijui ni kwanini alitaka kuombwa msamaha na Erick sielewi kabisa. Je unajua kilichosababisha kifo chwa mzee Jimmy?”
“Kitu gani hiko?”
“Ukikijua utashangaa sana maana kifo cha mzee Jimmy kimemfika baada ya maisha yenu kubadilika kabisa na kuanza maisha mapya, kwanza hakutegemea kabisa. Kuna siku alikuja na kucheza na wajukuu zake nyumbani kwako, ila kuna jambo alifanyiwa na yule mtoto wako mdogo wa kike na jambo lile lilimsababishia kifo chake”
Mama Angel alishangaa sana,
“Unamaanisha Erica? Alifanyiwa nini na Erica? Maana ndio alikuwa mtoto wangu mdogo wa kike kwa kipindi kile”
“Ndio huyo huyo Erica, kuna jambo la ajabu sana alimfanyia babu yake na jambo hilo lilimsababishia kifo chake, sijui kama mwanao anaweza kukumbuka ila unaweza kumuuliza”
“Kheee hebu niambie ni jambo gani maana sijui chochote kile, yani hapa ni kama unaniamsha toka usingizini, hakuna ninachoelewa”
Yule mke wa Moses, alivuta pumzi kiasi kwanza huku akitaka kuanza kumueleza mama Angel sasa,
“Ilikuwa, siku ya mwisho kwa mzee Jimmy kuja nyumbani kwako kabla ya kufikwa na umauti wake, sasa……!!”
Mara simu ya mama Angel ilianza kuita hata mama Angel aliogopa maana kwa muda ule alihisi kama kapigwa ganzi mwilini vile, akifikiria ni kwanini baba mkwe wake awe katili kwao kiasi kile hakupata jibu kabisa, basi alimuomba samahani kidogo mke wa Moses na kupokea ile simu ambapo alikuwa akipigiwa na Sia, alipoanza kuongea nayo tu mke wa Moses nae aliinuka na kuondoka zake kwani naye ilionyesha simu yake kuita.
Kwakweli mama Angel alishtuka sana kuambiwa kuwa mumewe yupo hospitali, akiwa hoi kabisa, yani mama Angel alihisi kupagawa kwa muda ule, hata hakufatilia tena mke wa Moses kaenda wapi, bali alikuwa akihangaika namna ya kumfikia mumewe kwenye hospitali aliyopelekwa.

Moja kwa moja mama Angel anaendesha gari lake kama mtu aliyechanganyikiwa vile kwaajili ya kumuwahi mumewe hospitali.
Mama Angel alifika hospitali wakati giza likiwa tayari limeanza kuingia, moja kwa moja alienda kuulizia kuhusu mumewe na kupelekwa alipo mumewe kwakweli alimuona mumewe akiwa na hali mbaya sana hata aliomba wampe uhamisho wa hospitali ili aende na mumewe kwenye hospitali kubwa ingawa pale napo walianza kumuhudumia ila alijikuta kutokuamini maana tayari alihisi kuchanganyikiwa kabisa.
Hata hivyo alikuta pale hospitali napo ndio walianza kumuandikia ruhusa ya kupata huduma kwenye hospitali kubwa zaidi, basi moja kwa moja walipanda kwenye gari la wagonjwa pamoja na mgonjwa wao, kwa wakati huo alikuwepo mama Angel na Sia kwenye lile gari yani mama Angel alimpigia simu tu dereva wake ili aende kwenye ile hospitali kuchukua gari zao ambazo zipo kule.
Walifika kwenye hospitali kubwa, na baba Angel alipelekwa moja kwa moja kwenye chumba maalum ili madaktari waweze kumuhudumia.
Kwakweli mama Angel alikuwa nje hajielewi kabisa, alimuangalia Sia na kumuuliza,
“Kwani imekuwaje?”
Sia alimueleza kila kitu yani hakuacha jambo lolote lile katika maelezo yake, ila kiukweli mama Angel hata hakuwa akielewa vizuri kwa muda huo maana akili yake ilikuwa kwa mumewe tu.
Walikaa pale hospitali hadi asubuhi yani mama Angel alishindwa hata kuwasiliana na familia yake kwa jinsi alivyochanganyikiwa kuhusu mume wake.

Wakina Erica nyumbani walishangaa sana kwa kutokupata mawasiliano yoyote toka kwa wazazi wao, kiasi kwamba hawakuweza hata kwenda shule kwa siku ya leo maana hawakujua kitu chochote kile kinachoendelea, ukizingatia usiku kucha, Erica ndio alikuwa akimbembeleza mdogo wake. Muda mwingi walikuwa wakimpigia simu mama yao kwa kutumia ile simu ya mezani alikuwa hapokei simu yao. Basi ile asubuhi ndio walimuona dereva wao akiwa kaongozana na mtu mwingine wakileta gari za wazazi wao, ilibidi Erica awafate kuwauliza,
“Hata hivyo tungekuja kuwaambia”
“Kuna tatizo gani kwani?”
“Nasikia mzee kapatwa na matatizo, hata sisi hatujamuona bado, tumeenda tu kuchukua hizi gari halafu ndio twende hospitali waliyo”
“Ni wapi huko? Naomba twende wote”
“Hapana Erica, bakini tu nyumbani”
Erica alisononeka na wale madereva waliondoka zao, moja kwa moja Erica aliingia ndani na kuanza kuwaeleza wenzie,
“Inasemekana wazazi wetu wamepatwa na matatizo”
Erick akamuuliza Erica,
“Hujaota Erica ni matatizo gani wameyapata?”
“Ningeotaje wakati usiku mzima nilikuwa macho nikimbembeleza mtoto”
“Oooh pole, nadhani ni zamu yetu sasa nenda tu kapumzike”
Muda uke, Erick alimchukua mtoto ila muda kidogo mtoto nae alilala na kumfanya hata Erica kwenda kulala kwa amani sasa kwani alikuwa na usingizi wa kutosha tu.
Muda kidogo, Erica alishtuka na kwenda moja kwa moja kwa Erick na kumwambia,
“Nimeota baba yupo hospitali, eti alipigwa risasi”
Erick alishtuka sana kusikia vile, ila baada ya muda kidogo mama yao nae alirudi nyumbani na walimfata kumuuliza vizuri, ambapo aliwaambia vile ambavyo Erica alisema kuwa baba Angel kapigwa risasi,
“Jamani baba yetu, hali yake ikoje kwasasa?”
“Mungu atusaidie kwakweli apone kabisa, naamini Mungu ni mwema na baba atapona kabisa ila tuzidi kumuombea baba jamani, haya matatizo sio madogo ni makubwa haya wanangu”
Kisha mama Angel alienda ndani sasa kuoga na kumchukulia mumewe baadhi ya vitu ili ampelekee kule hospitali, baada ya muda mama Angel alitoka tena ila muda huu ilibidi aondoke na watoto na wao waweze kwenda kumuona baba yao hospitali.

Walifika hospitali na kwenda kumuona, kwakweli bado hali yake haikuwa sawa, ila waliendelea kumuomba Mungu tu. Muda kidogo alifika pale hospitali ni rafiki wa baba Angel ambaye alikuwa ni Juma, maana alipata habari baada ya kumpigia simu mama Angel.
Basi aliwakuta pale na kuanza kuongea na mama Angel,
“Ilikuwaje kwani hadi Erick akapigwa na risasi?”
“Hata naelewa basi!! Yani sielewi kitu”
“Unajua nashangaa sana kuona Erick ana maadui wa kufikia hatua hiyo”
“Maadui anao ndio maana aliwahi hata kuwekewa sumu kwenye chakula”
“Duh!! Sikutegemea, kumbe!! Nadhani ni mambo ya biashara haya, dah sikufikiria kabisa kama jambo kama hili litampata Erick, wamefanikiwa kumtoa risasi lakini!”
“Ndio, wamemtoa moja ila wanasema bado moja, kuna operesheni nyingine watamfanyia kumtoa hiyo risasi”
“Dah nimesikitika sana”
Basi Juma alikaa kidogo pale hospitali, na muda wa kuondoka mama Angel alimuomba aweze kurudi na watoto wake nyumbani, kwahiyo Juma aliongozana nao na kuwarudisha nyumbani kwao.
Baada ya hapo Juma aliomba wasaa wa kukaa na Erick mdogo na kuanza kuzungumza nae, walienda kukaa kwenye bustani,
“Sasa Erick, baba yako amepatwa na matatizo. Hapo ndio unatakiwa kuelewa ni kwanini Mungu alikuumba mwanaume katika familia hii, unatakiwa kusimama kiume, unatakiw akuonekana kwenye mstari wa mbele kuhakikisha baba yako anakuwa sawa. Biashara zake nyingi zitasimama kama wewe hutoweza kuziendesha, kumbuka itamchukua baba yako muda mrefu sana kuwa sawa kabisa, sisemi kuwa hatopona hapana, ila itachukua muda mrefu sana kwa baba yako kupona kabisa, unatakiwa kuwa makini. Simamia vyema biashara za baba yako,
“Ila mimi nakaribia kufanya mitihani”
“Nakwambia kuwa ndio hapa ule usemi wa wanaume tumeumbwa mateso hutimia, huwezi kusongesha biashara za baba yako kama usipokubaliana na hayo mateso. Najua kuwa baba yako anapenda usome kwa bidii na ufike mbali, mimi nakwambia kuwa soma huku ukisimamia biashara za baba yako kwa bidii, yupo hospitali na atahitaji matibabu pale tena matibabu ya hali ya juu na yatahitaji pesa, bila kukazana basi hamtoingiza pesa yoyote na kila kitu kitashindikana katika maisha yenu hapa nyumbani. Unatakiwa kuwa makini sana, nadhani unanielewa Erick”
“Nakuelewa ndio”
“Sitokuacha, nitakuwa nakusaidia kwenye kila kitu, najua unajua ni jinsi gani ninavyokupenda na ninavyopenda ubunifu wako na kazi zako. Nitakusaidia na kukupeleka sehemu mbalimbali ili kukuza biashara ya baba yako”
Erick aliitikia tu kwani aliyokuwa akielezwa yalikuwa na ukweli mtupu kwani lazima gharama kubwa zitatumika kwaajili ya baba yao hospitali, kwahiyo alijiona kwa muda huo kuwa anatakiwa kushughulika kwa hali na mali kwaajili ya kusaidia familia yake.
Basi Juma alimuaga na kumwambia kuwa atilie maanani aliyomwambia kisha aliondoka zake.

Familia ya baba Angel ilikuwa kwenye wakati mgumu sana kwasasa, kwani muda mwingi mama Angel alionekana kushinda hospitali kwaajili ya mumewe kiasi kwamba hata mtoto wao mdogo Ester ilibidi tu aachishwe ziwa, muda mwingi Erica mdogo alikuwa nyumbani kushinda na mtoto halafu Erick nae alikuwa na swala moja la kwenda shule na kwenda kufatilia biashara za baba yake, na wakati huo huo kumfundisha Erica vitu vingine ambavyo utakuta amevikosa shuleni sababu ya muda mwingi kuwa nyumbani akimlea mdogo wake, kwahiyo alikuwa haendi shule kwa siku zingine yani kwa kipindi hiko hata kitu kucheza karata alikiacha kwa muda kwani alijikuta akipatwa na mambo mengi na akipata wasaa wa kulala alikuwa akilala sana.
Siku hiyo Erick kama kawaida, alienda shule na alipotoka shuleni alienda moja kwa moja kiwandani kwa baba yake ili kuendelea kusimamia vyema biashara za baba yake, basi siku hii alifika yule mteja wao mkubwa sana yule mwarabu na kuanza kuongea nae,
“Niambie kijana Erick, sijawasiliana na baba yako kwa siku nyingi, kwani kasafiri?”
“Hapana, hajasafiri ila baba yangu amepatwa na matatizo”
“Kheee, matatizo gani tena?”
Erick alimwambia tu kwa kifupi huyu mwarabu na kumfanya ashtuke sana,
“Ni majambazi walimvamia au kitu gani? Yani imekuwaje hadi akapigwa risasi?”
“Itakuwa ni majambazi walimvamia maana alienda kutembelea kaburi la babu yetu”
Yule mwarabu alisikitika sana na kuomba kupelekwa huko hospitali siku ya kesho yake ili aweze kumuona huyo mgonjwa maana ni mtu aliyemfahamu vizuri.
Basi waliagana nae na kupanga kukutana nae kesho yake asubuhi ili waende hospitali.

Kesho yake kama walivyopanga, yule Mwarabu alikutana na Erick na moja kwa moja kwenda hospitali ambapo walimkuta pale mama Angel na kwenda kumuona baba Angel ambaye bado hali yake haikuwa nzuri, basi yule Mwarabu akauliza vizuri,
“Wamemtoa risasi zote lakini?”
“Wanasema bado moja”
“Ngoja niongee nao ili tufanye utaratibu wa kumuhamishia hospitali nyingine, kuna hospitali nzuri sana huko na wanaweza kufanya hili”
Yule mwarabu alienda kuongea na daktari, ila huyu mzee ni mtu anayefahamika sana na anafahamiana na watu wengi kwahiyo iliwezekana kwa kila alichokisema na siku hiyo hiyo baba Angel alihamishwa kwenye hospitali nyingine, na huko alipewa huduma kwa siku hiyo hiyo na kutolewa ile risasi iliyobaki.
Kwakweli mama Angel alimshukuru sana huyu mwarabu na alifurahi kufahamiana nae, yani kwa kipindi hiki mama Angel hata hakufatilia ni wakina nani wamempiga mumewe na risasi, je wako wapi kwani yeye alichokuwa akifatilia ni kimoja tu kujua hali ya mumewe inaendeleaje maana ndio ilikuwa ikimpa shida.
Ila baada ya ile huduma ambayo baba Angel aliipata, taratibu alionekana kuanza kuwa sawa kwani alikuwa akiweza hata kukaa na kuongea mawili matatu na mke wake, na hilo lilikuwa ni jambo la furaha sana kw amama Angel.
 
SEHEMU YA 368


Mama Angel siku hii aligundua jambo kuwa watoto wake wanapata shida kwenye masomo yao kwani muda mwingi wamejikuta na mambo mengi kama yeye,
“Oooh jamani, hata wewe Erica huwa huendi shule?”
“Huwa siendi kama mtoto akisumbua sana”
“Kheee hapana mwanangu, huyu Ester nitakuwa namuhudumia mwenyewe kuanzia sasa. Baba yenu anaonyesha matumaini. Namshukuru sana yule Mwarabu, kwakweli katupeleka kwenyehospitali kubwa, na siku sio nyingi baba yenu ataruhusiwa ila tu hatoweza kutembea kama zamani kwanza, atakuwa akitembea kile kiti cha matairi.”
“Dah! Namuhurumia sana baba”
“Ila yote haya yataisha tu, Erica naomba kesho uanze kwenda shule vizuri kama zamani na hata Erick nitamwambia hili. Msome watoto wengi, tutafanya tu haya mengine.”
Erica alikubaliana na mama yake, na kweli kuanzia kesho yake walianza kwenda shule kama kawaida kwani mama yao afadhari alikuwa akipata muda wa kulala na mwanae mdogo nyumbani tofauti na kipindi wakati akilala hospitali sababu ya hali ya mumewe ambayo ilikuwa mbaya, ila kwa kipindi hiko hali ya mumewe ilimridhisha na kumfanya aweze hata kulala nyumbani na mtoto wao mdogo.

Siku hiyo ndio ilikuwa furaha sana nyumbani kwa mama Angel kwani baba Angel aliruhusiwa kutoka hospitali na kurudishwa nyumbani, kwahiyo walikuwepo pale nyumbani na kufurahi sana huku wakiongea mambo mengi mengi, kwa wakati huo alikuwepo pale mama mzazi wa mama Angel, ndugu zao wengine, pamoja na mama mzazi wa baba Angel, na Tumaini pia alikuwepo pale kwani walifurahi kwa kiasi Fulani kwa baba Angel kuruhusiwa kutoka hospitali.
Basi baba Angel aliongea kiasi na mama yake mzazi na mama mkwe wake,
“Mama zangu, naomba kwasasa Angel asifahamu chochote ambacho kimenitokea, najua ni kwa kiasi gani swala hili limewazorotesha wanangu hawa kimasomo, nisingependa Angel nae apate simanzi, hivyobasi akiwa likizo muwe mnamuacha huko huko kwenu yani sitaki aelewe chochote kile, mwambieni nataka kuonana nae hadi atakapomaliza shule”
“Sawa hakuna tatizo, na hivi Angel anavyokupenda nadhani ni wazi kabisa atashindwa hata kufanya mitihani”
“Naelewa, hapa nyumbani tu huyu Erick na Erica naona wamekonda sana, najua ni sababu ya mawazo ila nitaongea nao pia ili wasome kwa amani”
Basi mama yake akauliza,
“Ila Erick ni kitu gani haswaaa kilitokea maana nashindwa kuelewa”
“Mama, ukimpata Sia atakueleza mengi sana maana ni yeye ndiye nilikuwa nae siku ya tukio”
“Usiniambie kuwa yule mwanamke alianza tena matatizo yake!”
“Hapana mama, siku hizi Sia kawa mtu mzuri kabisa hana matatizo wala nini. Tena naweza kusema kuwa amenisaidia sana, kwani yeye ndiye aliyemuona aliyekuwa akitaka kunipiga risasi na kuwahi kuwa niiname, sasa yule mpiga risasi aliamua kunilengesha nitakapoinama na kufanya zile risasi zinipate miguuni kisha nikaanguka, inaonesha alilenga kunipiga kichwani ila baada ya sauti ya Sia kuwa niiname ndio yeye akaamua kunipiga miguuni akijua ningeinama”
Walipumua kiasi,
“Duh!! Kwahiyo dhamira hapo ilikuwa ni kukuua?”
“Kwakweli sijui hata kidogo, ila mama nimewahi kuwekewa hata sumu kwenye chakula. Nadhani ni watu wenye mpango wa kuniua kwa muda mrefu”
“Kheee nahitaji kuwafahamu”
“Hapana mama, usijiingize kwenye matatizo”
Aliongea nao pale ila kiukweli hawakuridhika wala nini, na muda wa kuondoka mahali pale ndipo Sia nae alipofika kwenda kumuona baba Angel maana alikuwa akienda mara kwa mara hospitali, basi alivyowasalimia pale ndio mama mzazi wa baba Angel aliamua kuondoka na Sia ili aweze kumsimulia vizuri.
Waliondoka nae na kuongea nae, kwakwlei Sia hakuwa na sababu ya kuficha jambo lolote, yani alieleza kila kitu toka mwanzo alivyopanga na mzee Jimmy kubadilisha watoto,
“Kheee ndioma ulikuwa umekazana kusema umezaa na mwanangu sababu ulijua akipima damu atakuta ni mwanae sababu mlimbadilisha?”
“Ndio, yani nilikuwa najua hivyo ila sijui yule mzee alinichezea mchezo gani ila hakuwa mtu mzuri kabisa”
“Unajua umenishangaza sana, yani kwanini aligeuka na kuwa mbogo kiasi hiko? Yani abadilishe watoto ili iweje? Kumbe ndiomana alipoona Erica anakaribia kujifungua basi akaona ampeleke Erick mbali, aaaah kweli mume nilipata jamani, yani anafanya kitu kama hiko kwa mtoto wake mwenyewe!! Na aliyempiga Erick risasi ni nani?”
“Nilimuona kwa macho yangu wala siwezi kumsingizia, alikuwa ni Moses”
Huyu bibi alishangaa sana kwani huyo Moses alimfahamu vizuri sana na kusema,
“Haiwezekani, yani Moses ndio kawa mnyama kiaski hiko kwa Erick jamani!! Inaonyesha kuna mengi huwa yanaendelea kwenye kaburi la mzee Jimmy eeeh!”
“Ndio mama, ni mengi sana yanaendelea”
“Basi sikia, wala msifatilie tena jambo hilo yani msijisumbue tena. Kila kitu niachieni mimi. Usinione hivi, hata huyo mzee Jimmy alikuwa akiniogopa maana nikiamua langu basi naamua tu. Kama niliweza kusimama mwenyewe kama mwanamke na kufanya vyote nilivyovifanya basi naamini hakuna kitu kinachonishinda. Sia nbiachieni mimi na kila kitu kitakuwa wazi hapa mbele yenu, yani ukweli utapatikana tu”
“Oooh asante mama, yani hivi hata sijui mtoto wangu wa kweli ni yupi”
“Aaaah usiniambie hilo, maana huo ni ujinga wako. Uliona wapi mwanamke uzae kwa uchungu halafu ukubali kwa hiyari yako kubadilisha mtoto na kuchukua mtoto wa mwenzio? Ukiulizwa wako alikuwa na matatizo unajibu hapana, yani njaa na shida zikufanye ufanye ujinga namna hiyo!! Huo ni ujinga hata sio umasikini bali ni ujinga, kuna wanawake utakuta hawajiwezi kabisa ila wanakazana kulea watoto wao katika hali yoyote ile na wanawapenda hatari, halafu wewe upate nguvu ya kubadilisha mwanao kwa hiyari halafu upo kulalamika ni pesa!! Huo ni ujinga, labda useme kuwa mzee Jimmy alikuroga”
Sia hakuweza kuongeza neno lolote kwa huyu mama zaidi zaidi alikubaliana nae tu kwa kile ambacho alikiongea.

Miezi ilipita na mimba ya Vaileth ilizidi kukua, sema ilikuwa ngumu kugundulika na mama Angel kwani muda mwingi alijifunga kwa khanga kifuani halafu mama Angel nae alikuwa na majukumu mengi ukizingatia mumewe alikuwa bado akitembelea kiti cha matairi kwa kipindi hiko maana miguu bado haikuwa sawa.
Basi Vaileth alikuwa akitumia kila namna kuweza kuficha ile mimba yake, alipoona anakaribia mwishoni alianza kumuomba mama Angel ruhusa ili akasalimie kwao,
“Vai jamani utaondokaje katika kipindi hiki? Yani hapa nahitaji msaidizi wa hali na mali. Unajua kabisa nina matatizo, utaondokaje, yani sitaki kukukosa hata kwa siku moja. Naomba univumilie Vaileth, kwenu utaenda tu hakuna tatizo binti yangu”
Vaileth aliogopa kumwambia ukweli mama Angel kuwa ana mimba kubwa kabisa, kwahiyo aliamua kuendelea kuvumia tu ile hali.
Siku hiyo usiku, alihisi kushikwa na uchungu wa hali ya juu ila alikuwa akijikaza, yani alikuwa akiugulia sana chumbani kwake na akaona akifanya ujinga basi anaweza kujikuta hata akijifungulia pale pale nyumbani.
Aliandaa nguo zake na kubeba begi lake ili ikiwezekana awahi hospitali kujifungua na moja kwa moja aende nyumbani kwao maana hakutaka kujilikana na mimba ile ndiomana muda wote alivaa nguo kubwa kubwa na kujifunga khanga kifuani, na kwavile hakuwa na tumbo kubwa sana kwa ile mimba kwahiyo ilikuwa sio rahisi kumgundua kwani alijitahidi kwa kila hali isionekane. Basi alitoka sebleni na kumuomba mama Angel ruhusa kwa mara nyingine,
“Mama, nahitaji kwenda kuwasalimia nyumbani”
“Mbona unaongea huku umekunja sura Vai? Una tatizo gani kwani?”
Vaileth aliinama chini akiugulia maumivu ya uzazi aliyokuwa akiyapata, alisema kwa kutazama chini,
“Naomba niruhusu mama”
Mama Angel alimsogelea karibu, na muda ule Vaileth alishindwa kusimama tena, alijikuta tu akikaa huku damu na maji zikimuanguka miguuni.

Vaileth aliinama chini akiugulia maumivu ya uzazi aliyokuwa akiyapata, alisema kwa kutazama chini,
“Naomba niruhusu mama”
Mama Angel alimsogelea karibu, na muda ule Vaileth alishindwa kusimama tena, alijikuta tu akikaa huku damu na maji zikimuanguka miguuni.
Hapo ndio mama Angel alipohisi wazi kuwa Vaileth alikuwa ni mjamzito ila muda ule haukuwa muda mzuri wa kuanza kumuhoji maswali kwani alikuwa kwenye hali mbaya tayari, mama Angel alimuita tu dereva na kisha kumsaidia Vaileth kupanda kwenye gari halafu kumpeleka hospitali yani alikuwa akimshangaa sana kwa Vaileth kujificha kwa siku zote hizo kumbe alikuwa ni mjamzito.
Walipofika hospitali tu, yani ile kupokelewa Vaileth alijifungua na moja kwa moja kumkumbiza leba, kwahiyo mama Angel alibaki akiandikisha tu, yani hakuna jambo alilokuwa akilielewa kwa muda ule, kisha mama Angel alipomaliza kuandikisha ilibidi aondoke ili arudi nyumbani kuweka mazingira sawa ukizingatia aliondoka kwa haraka tu kumuwaisha Vaileth hospitali.
Yani njiani alikuwa na mawazo sana huku akijiuliza maswali mengi,
“Huyu Vaileth jamani kwanini kanifanyia hivi!! Haya si ndio mambo aliyokuwa akiyasema Tumaini mweeeh jamani huyu mtoto kaniweza kwakweli, sijui hata nitafanyeje na hapa nina majukumu hatari sijui nitafanyeje jamani”
Mama Angel aliwaza sana maana alihisi huduma zote kumuelemea kwa muda huo, basi alifika nyumbani kwake moja kwa moja, alipoingia getini tu akamuona Erica na kumuuliza,
“Wewe usharudi shule? Ila afadhari maana hata sikujua nianzie wapi”
“Nimerudi mama sababu ya dada Vaileth”
“Usiniambie na hilo umeota?”
“Ndio, nimeota kuwa kajifungua”
“Kheee, haya kajifungua mtoto gani?”
“Wa kiume”
“Khaaaa, wewe mtoto hapana jamani kama mfalme njozi, haya twende ndani ili nimpikie chakula mgonjwa”
“Aaaah nimempigia mamkubwa simu, kashakuja yupo jikoni kupika”
“Khaaaaa”
Basi mama Angel aliingia ndani hadi jikoni, ambapo alimkuta dada yake yani mama Junior akishughulika na zile kazi za pale,
“Khaaaa dada, kwani huyu Erica kakwambiaje?”
“Huyu mtoto jamani loh!! Unajua kanifata nyumbani, kasema nije nikusaidie kuna matatizo, nimetoka huko hai hai maana nimeogopa matatizo ya shemeji tena. Kufika hapa ndio ananiambia kuwa Vaileth kajifungua kwahiyo mimi nimpikie, kwanza kanichosha nimeona nisiongee kwanza, nipike tu. Hiyo na wewe mdogo wangu unawezaje kuishi na bingti wa kazi mwenye mimba katika nyumba yako? Sasa atakusaidia nini? Atakuwa msaada gani kwako jamani!”
“Acha tu dada, unadhani nilijua basi! Hata sikujua chochote yani mimi sikujua kitu kama vaileth ana mimba. Unajua majukumu yangu ya sasa, mume wangu bado ni mgonjwa, mambo kibao yameniandama yani hapa ndio naujua ugumu wa maisha ulivyo. Kwa kifupi nachanganyikiwa yani, huyo Ester mwenyewe saivi amekua kingangari maana kunyonya aliacha kipindi kile kile, ila Mungu ni mwema maana mtoto anatembea vizuri tu na kula vizuri. Leo sasa si ndio nikakutana na hili balaa la Vaileth, jamani mikosi ikiamua kukuandama inakuandama hadi akili ikukae sawa”
“Ila mdogo wangu kuwa makini sana, huyu binti akirudi aende kwa huyo muhusika”
“Nitakachomuhurumia hapa ni kusubiri tu mwanae akatike kitovu basi, nimruhusu kwenda kwao maana nikimtoa sasa sitakuwa nikimfanyia mazuri. Kumbe alikuwa akifanya kazi zote za humu na mimba yake dah nimeshangaa sana”
“Ila subiri, nitakwambia cha kufanya wanaona wewe ni mpole mdogo wangu”
Basi walikaa pale na kupika na kumsaidia mdogo wake kazi zingine, ila mama Junior alipigiwa simu na mume wake, kwahiyo ilibidi amuage mdogo wake na kuondoka maana kazi karibia zote pale walishafanya.

Mama Angel muda huu aliondoka na moja kwa moja kwenda zake hospitali kwaajili ya kumuona Vaileth na kumkuta akiwa na hali nzuri, akaongea nae kidogo pale,
“Pole na hongera ila bado sijamaliza maneno yangu kwako”
“Asante mama”
“Wamelikupa uji eeeh!”
“Ndio, walinipa uji na maandazi”
“Hii hospitali ipo vizuri sana, ngoja nikaongee na daktari aweze kunipa ruhusa tuondoke maana naona upo sawa”
Basi mama Angel alienda kuongea na daktari, ili ampe ruhusa. Kwa muda huo alikutana na yule daktari rafiki yake yani dokta Maimuna basi alianza kuongea nae pale,
“Mimi sina tatizo na wewe mama Angel ila nina tatizo na yule mume wako, sikujua kama ni mumeo yule”
“Ila amepatwa na matatizo, alipigwa risasi miguuni yani hawezi kutembea kwasasa, anatembelea kiti cha matairi tu. Huyu aliyejifungua ni mdada wangu wa kazi, yani naona nitashindwa hizi safari za kuja hospitali ndiomana nikaja kumuombea ruhusa maana naona yupo sawa”
“Weeee Erick alipigwa risasi na nani?”
“Watu wabaya tu”
“Jamani, hata kwa mambo yote ambayo Erick amenitenda bado siwezi kufikia hiyo roho mbaya ya kumpiga risasi au kumtumia watu wafanye hivyo. Erick hana roho mbaya kiasi hiko mpaka apate maadui wa hivyo, kwakweli nimeingiwa imani na hilo swala jamani dah!!”
“Ndio hivyo ndugu yangu”
“Nitamuandikia ruhusa huyu mdada wako halafu tutawasiliana kesho maana nitakuja kumuona Erick mara moja”
“Nashukuru sana dokta Maimuna”
Basi waliongea kiasi na yule daktari alienda kumuangalia kwanza Vaileth na kisha kumuandikia ruhusa mama Angel ilia pate kuondoka nae.
Kwahiyo mama Angel sasa aliondoka na Vaileth na kurudi nae nyumbani kwake.

Walifika nyumbani na kukuta Erica ameandaa mazingira mazuri kabisa chumbani kwa Vaileth kwaajili ya kukaa na mtoto yani alisafisha kila kitu, kwakweli kwa uchapakazi aliokuwa nao huyu mtoto ilimfanya mamake amsifie sana,
“Kwahili mwanangu hongera sana, yani dada yako Angel sasa uwiiii nisingekuta kafanya chochote na uvivu wake”
“Ila mama tumemkumbuka Angel”
“Atarudi tu, akishamaliza kabisa shule atarudi, sijataka achanganye masomo yake na hii hali ya baba yenu kwasasa”
Basi mama Angel alienda kumkanda Vaileth kwanza na kuoga, kisha kumpatia tena chakula, halafu alimuacha na mtoto wake chumbani.
Kwakweli Vaileth alijikuta akitokwa na machozi tu kwa huduma ile aliyopewa na mama Angel maana alimajali kama ni mwanae kabisa, alimpatia huduma zote muhimu, Vaileth alijihisi uchungu kwakweli kwa namna moja au nyingine.
Ila bado alijisemea kuwa swala hilo ataendelea kulifanya kuwa siri kabisa kwani hakutaka kueleza kwa uwazi kuwa yule mtoto ni wa Junior, alitaka adanganye tu maana aliona kusema ukweli atasababisha tatizo kubwa sana.

Basi mama Angel aliongea na mumewe chumbani kuhusu Vaileth,
“Yani balaa zimetupata mume wangu, na hii purukushani sijui itakuwaje”
“Ila hata hukuweza kumuhisi kuwa ni mjamzito!”
“Yani huwezi amini, Tumaini alisema hili jambo na nilimktalia katakata kuwa Vaileth ni mjamzito halafu na yeye Vaileth sijui akanifanyia mchezo gani maana kumpima nikakuta kweli hana mimba kumbe mimba anayo jamani!! Wasichana wa kazi hawa mambo yao loh!!”
“Ila ni nani muhusika wa hiyo mimba?”
“Sijamuuliza, ila umeniambia jambo jema itabidi nimuulize ila nimechoka hatari, nitaongea nae kesho tu”
“Pole mke wangu jamani”
Yani baba Angel alikuwa akimuhurumia sana mkewe, haswaa kwa siku kama hiyo alizidi kumuhurumia maana mambo yote yalimuelemea pale nyumbani kwao.
Yani siku hii mama Angel alilala kama mzigo yani hadi alikuwa akikoroma kwa uchovu wa siku hiyo.
Kulipokucha tu, alishukuru sababu ilikuwa ni Jumamosi, kwahiyo wakina Erica walikuwa nyumbani na waliweza kumsaidia baadhi ya kazi, ambapo kwa asubuhi ile tu Erick alienda zake kiwandani yani kwa kipindi hiki familia ilikuwa ikijishughulisha sana na hata hapakuwa na muda wa kupumzika.

Kwenye mida ya mchana wa siku hii, mama Angel aliamua kwenda kuzungumza na Vaileth ambapo alihitaji kujua baba wa mtoto ni nani,
“Eeeeh vai, huyo baba mtoto ni nani?”
“Nisamehe mama, kuna kijana mmoja ila alikataa mimba”
Vaileth aliinama chini na kutoa machozi, kisha mama Angel akamuuliza,
“Kwani Vaileth wewe si una mtoto huko kijijini kwenu?”
“Ndio nina mtoto”
“Imekuwaje upate mtu mwingine wa kukudanganya na kukujaza tena mimba bila ya ndoa? Unajua nini, mtu uking’atwa na nyoka basi ukiona jani lazima ushtuke, sasa wewe mwenzetu vipi eeeh! Yani upate mtoto wa kwanza asiye na baba halafu uje uzae mtoto wa pili asiye na baba, akili zako ni timamu kweli? Haya una mpango gani?”
“mama, naomba tu unisaidie kwa siku chache halafu nitaenda kumpeleka mtoto kwa wazazi wangu”
“Sababu wazazi wako ndio kituo cha kulelea watoto wasiokuwa na baba? Hebu muda mwingine muwe na akili nyie mabinti, hivi mnajua kama mnatuvuruga akili wazazi? Yani huwa tunachanganyikiwa, uzae mtoto wa kwanza nyumbani na baba asiyeeleweka, tunasema hili ni kosa ila ni kosa la kwanza labda mtu hajajua kadanganywa kwenye mapenzi. Ila bila hata ya kufikiria unapata tena nguvu ya kubeba mimba nyingine na kuzaa mtoto mwingine na unawaza kuwapelekea wazazi wako watunze, halafu inakuwaje? Unarudi tena kufanya kazi hapa kwangu ili upate mimba nyingine na uwapelekee wazazi wakatunze mtoto!!”
Vaileth alikaa kimya na kuinama chini huku machozi yakimtoka kwani ni kweli alikuwa amefanya kosa, basi mama Angel akamwambia tena,
“Vai, mimi ni mpole sana tena nina huruma sana ila katika maisha yangu ujinga sipendi. Ninapofanya ujinga mara moja huwa namuomba Mungu nisirudie tena huo ujinga, ni kweli sisi wanawake kuna muda tuna ujinga unatusumbua kichwani ila ni kumuomba Mungu ili huu ujinga ututoke. Vai, nitakapokuja kukuuliza tena kuhusu huyo mwanaume basi uwe na taarifa kamili zake, kama hataki tutaenda kupima damu na mtoto, yani naomba siku nitakayokuuliza tena uwe na jibu kamili juu ya huyo mjinga aliyekuambukiza ujinga binti mpole na mstaarabu kama wewe”
Kisha mama Angel aliinuka na kuondoka zake, kwakweli yale maneno yalimuingia sana Vaileth, alijihisi vibaya ila muda mwingine aliona mama Angel kamwambia maneno ya ukweli kwani alichokifanya ni ujinga kweli.
Mama Angel muda huu alipotoka tu alikutana na Erica ambaye alimuuliza mama yake,
“Kwani mama unataka kumfukuza dada Vai?”
“Nitamfukuza ndio, ujinga gani huu alioufanya? Hata wewe ukipata mimba nitakufukuza”
“Kheee mimi nikipata mimba? Nikipataje?”
“Aaaah usinichanganye Erica”
“Ila mama, kabla hujafikia swala la kumfukuza dada Vai, naomba ukumbuke yale mazuri aliyoyafanya kwenye familia yetu”
“Siwezi kumfukuza ila namtishia tu ili akae sawa”
Mama Angel aliondoka zake na kuendelea na mambo mengine.

Jioni ya siku hiyo ndipo dokta Maimuna alipowasiliana na mama Angel, kisha aliweza kufika pale nyumbani kwa mama Angel ili kuonana na baba Angel, kwakweli alipofika pale na kumuona baba Angel hata yeye alijikuta tu akimuhurumia na hata kile kinyongo alichokuwa nacho juu yake kikaisha, aliakaa nae chini na kuanza kuzungumza nae,
“Ilikuwaje lakini?”
“Hata mimi sielewi yani ila ndio hivi”
“Aaaah pole sana, hapa kwasasa kinachotakiwa ni mazoezi kwasana halafu kuna dawa Fulani hivi ni nzuri kwakweli nitakuletea ili uwe unatumia naimani utapona kabisa na kuwa kama zamani”
“Nashukuru sana”
“Nitaongea na mke wako, halafu nitakuwa nakuja kila asubuhi kukufanyisha zoezi Fulani hivi, ni zuri kwaajili ya kurudisha miguu katika hali yake, yani alivyoniambia mke wako nilijikuta nikisikitika sana”
“Ndio hivi, hujafa hujaumbika kwahiyo tupo tu katika maisha haya”
“Nitakuwa najitahidi, siku ninazopata muda nitakuwa nakuja kukupa hilo zoezi, yani kila nikipata muda nitakuwa nakuja”
“Aaah sikutegemea kwakweli, una roho nzuri sana Maimuna”
“Unanielewa vizuri sana, hata kama nikiwa na roho mbaya bado sitohitaji baya likufike. Nakumbuka siku ile uliyoletwa umepewa sumu niligoma kukuhudumia ila nilikuwa naumia sana moyoni, yale matendo yako yalinijia kwa kasi sana kichwani, ila bado asingetokea wa kukuhudumia basi ningekuhudumia tu. Sina roho mbaya kiasi hiko cha kumtoa mtu uhai”
Waliongea pale, kisha dokta Maimuna kwenda kuongea na mama Angel pia kuhusu hiyo huduma kwani alikuwa akimuhabarisha ila mama Angel hakukataa kwani kwa wakati huo alichokuwa akikihitaji ni uzima wa mume wake tu na si vinginevyo na ndiomana alishirikiana na yeyote aliyesema kuwa atamsaidia kwa mumewe.

Usiku wa leo madam Oliva anazungumza na teve kuhusu kwenda kumuona baba Angel maana hata wao lile tukio lilikuwa kubwa sana,
“Yani kwakweli ni jambo kubwa sana kwa mtu mzima kama Erick kukalishwa chini sababu ya wajinga wasiopenda maendeleo yake, inauma sana. Kesho naomba twende wote familia nzima kumuona”
“Unamaana twende na Paul?”
“ndio, twende na Paul kumuona baba Angel yani najua kuwa atafurahi sana kutuona”
Basi waliongea mambo mengi mno kwa usiku ule, ila muda kidogo madam Oliva alipigiwa simu na namba ngeni ambayo hakuijua mwanzoni na kuipokea huku akijiuliza kuwa ni nani, alipopokea tu alimuuliza,
“Nani wewe?”
“Mbona umepokea simu kwa uoga kiasi hiko?”
“Hapana, ila nauliza wewe ni nani?”
“Unaongea na dokta Jimmy hapa”
“Kheee dokta Jimmy? Eeeh niambie ukweli”
“Kwanza nilitaka kukuuliza, huwa unaenda pale hospitali kwangu kuniulizia ili iweje?”
“Nilikuwa nataka kujua ukweli, hivi mliyenipa ni mtoto wangu au kitu gani?”
“Unajua wewe mwanamke usilete kichaa chako eeeh!! Sikia, wewe mwenyewe ulitaka hadi kushtaki watu pale kwa madai kuwa mtoto wako amepotea, tuliacha shughuli zote kwa muda na kukutafutia mtoto wako, ambaye ni uzembe wako mwenyewe ndiomana alipotea. Tukampata na kukukabidhi, unaacha kushukuru kwa kazi tuliyoifanya eti upo kuulizia kama ni mwanao tulikupa au la! Ni kitu gani kinakufanya useme kuwa huyo si mwanao? Umempi DNA au ni kitu gani?”
“Hapana, nilikuwa nauliza tu”
“Halafu acha kuniwekea sifa mbaya, nitakuchafua. Kuna mwenzio mmoja naye anajifanya kujua sana, kaniwekea sifa mbaya eti nimebadilisha watoto wake hospitali. Mungu si Athumani, kapata ajali huko yupo kuuguza majeraha. Hebu fanya mambo yako, vitu vingine mtapata laana bure”
Ile simu ilikatika, basi madam Oliva alibaki kushangaa tu ile simu sababu hakuitegemea wala nini kwa muda ule yani hakufikiria kama angepata ujumbe kama ule, hakuweza hata kumsimulia vizuri Steve zaidi ya kuamua kulala tu kwa muda huo.

Leo, Sia alikuwa akiwaza mambo mengi sana haswaa mambo ya kuhusu mama Sarah, alikuwa ashaenda nyumbani kwa mama Sarah mara kadhaa ila alikuta nyumba imefungwa, basi leo aliamua kwenda tena, alihisi kama anahitaji kuongea na mama Sarah,
“Mimi ni muoga ndio, ila nikiamua basi huyu mwanamke nitaongea nae tu. Haiwezekani, nakumbuka vizuri kuwa ni yeye ndiye aliyetoa amri ya kupigwa kwa Erick, halafu ni Moses ndiye aliyemshuti Erick, nadhani bado nahitaji kuufahamu ukweli.”
Basi alijiandaa na kuondoka nyumbani kwake, moja kwa moja alienda nyumbani kwa mama Sarah, sababu aliona siku ile ni Jumapili basi alihisi kuwa anaweza kumpata nyumbani kwake.
Ila alipofika pale alikuta mlango umefungwa na kila kitu kikiwa kimya kabisa, ilionyesha ni kwa muda mrefu sana hakuna mtu aliyeonekana kuishi katika nyumba ile.
Alizunguka ile nyumba huku akiangalia huku na huku, wakati anataka kuondoka ndio alipokutana na dada wa mama Sarah yani alikutana na Linah na kuanza kusalimiana nae pale kisha kuongea nae,
“Wewe unajua alipo mama Sarah?”
“Nijue wapi? Yani sijui imekuwaje hadi kaondoka bila hata kututaarifu ndugu zake”
“Kheee hadi ndugu zake hajawaambia kumbe!!”
“Hajatuambia ndio, hatujui lolote lile”
“Duh!! Basi hatari”
Sia hakutaka kuongea zaidi kwani alimuaga Linah na kuondoka muda huo ila badae alikumbuka kuwa anatakiwa kwenda kumuangalia baba Nagel kwanza, basi aliamua kuongoza kwa baba Angel tu.
 
SEHEMU YA 369


Sia alipofika kwa baba Angel, alipoingia tu getini alimuona Paul akiwa amekaa kwenye kibaraza na Erica, kwakweli alijikuta akimuangalia sana mtoto huyu hata alipowasogelea alikuwa akimuangalia sana na kuwasalimia pale, kisha alimuuliza Erica,
“Samahani, huyu ni ndugu yenu?”
“Hapana, huyu ni mtoto wa madam Oliva anaitwa Paul”
“Aaaah”
Basi Sia alimuangalia Paul kwa muda mrefu kidogo hata Paul alimshangaa ila muda kidogo Sia aliingia ndani ili kusalimia waliopo mule ndani na kweli aliwakuta wote wamekaa tu na kuwasalimia pale, ila muda kidogo madam Oliva nae aliaga kuondoka na familia yake kwahiyo walimuita Paul ili awaage pia kwani madam Oliva hakupenda kukaa karibu sana na Sia.
Basi Paul alifika ndani na kushikana nao mkono wa kwaheri, wakati Sia ameshikana mkono na Paul alijihisi kitu kingine kabisa, yani alijikuta kama akitokwa na machozi kwenye macho yake kiasi kwamba aliamua tu kumkumbatia Paul kwa muda huo, mama Angel na baba Angel walielewa ila wengine walibaki kushangaa kwa muda.
Baada ya tukio hilo, madam Oliva na familia yake wakaondoka, ila Sia alimuita mama Angel pembeni na kuanza kuongea nae,
“Unajua nini ndugu yangu sijui nini kimenitokea, wakati namshika yuele mtoto mikononi nilihisi damu mwilini ikinikimbia, nilihisi machozi yakinitoka na hadi nikajikuta nikimkumbatia, msinihisi vibaya”
“Kwanza niambie umehisi nini?”
“Sijui, ila nimehisi kama nimemuona mtoto wangu wa halali”
Mama Angel alimuangalia kwa muda na kutamani hata kumweleza kilichopo ila alisita kwa muda na kumuuliza,
“Je unahisi kuwa Elly ni mtoto wa madam Oliva halafu mtoto wa madam Oliva ndio wako?”
“Mmmmh sijui kwakweli, ila inawezekana Elly akawa mtoto wa madam Oliva maana mbona Elly mpole kama yule madam”
“Aliyekwambia yule madam ni mpole nani?”
“Ila Elly angekuwa wa madam Oliva, basi angehisi kitu kwa siku zote hizi ambazo yupo shule anasoma kwa huyu madam. Sijui lakini, ila natamani kumuona mwanangu mimi”
“Pole sana”
Kisha Sia aliamua kumueleza mama Angel kuhusu swala la mama Sarah kutokuonekana kabisa, na vile vile kwa maelezo yale aliweza kumkumbusha tukio la baba Angel kupigwa risasi,
“Dah!! Huwa sisahau hilo tukio kabisa, ila naamini mume wangu atapona tu”
“Ni kweli atapona, nitaendelea kufatilia mambo mbalimbali na tutajua tu mbivu na mbichi hakuna tatizo juu ya hilo”
Sia aliongea kidogo na kuamua kuaga tu ili kurudi zake nyumbani kwake.

Basi kesho yake, alifika dokta Maimuna mapema kabisa na kumpatia baba Angel dawa alizoahidi kumletea kisha kuanza kumfanyisha baadhi ya mazoezi,
“Usijali Erick, utakaa sawa tu”
Kwakweli baba Angel alishukuru sana, na hii ikawa ndio mtindo wa huyu dokta mara kwa mara kwenda kumpa baba Angel mazoezi kwaajili ya kumuweka sawa.
Siku hiyo baba Angel aliamua kumuuliza dokta Maimuna,
“Ila Maimuna, unajua nini kwanini umeamua kujitoa hivi kwaajili yangu?”
“Kuna siku utagundua kwanini nimefanya hivi baada ya yote yale”
“Mmmh Maimuna, niambie ukweli”
“Ukweli utauopata pindi ukitembea kabisa, yani ukishapona ndio itakuwa furaha yangu na hapo nitaweza kukwambia ukweli kuwa kwanini nafanya hivi”
Kisha dokta Maimuna akamuita mama Angel na kuanza kumuelekeza baadhi ya vitu vya kufanya, huku akimwambia,
“Mimi natarajia kusafiri kesho, ila huyu asibaki bila mazoezi yani haya mazoezi yafanyike kwake mara kwa mara ili aweze kufunguka na kuwa mzima kabisa yani. Nitakuelekeza baadhi ili usiache kumfanyia, halafu nikirudi tutaangalia hali yake, natumai atakuwa akiendelea vizuri”
“Nashukuru sana kwakweli, kwahiyo wewe unaenda wapi?”
“Kuna mahali huko naenda, yani kuna tukio Fulani lilitokea. Kuna mtu alikufa na nilikuwepo kule, na tuliweza kumfanyia uchunguzi yule marehemu ambaye ilionyesha wazi kuwa ameuwawa, niliwaambia kuwa nipo tayari kutoa ushahidi basi ndio ninaenda huko kesho. Ila sio hiko tu kinachonipeleka bali kuna kazi pia ambayo naenda kuifanya huko”
“Oooh sawa, kwakweli Mungu akutangulie. Una moyo wa kipekee sana, Mungu akuzidishie dokta Maimuna”
Aliongea kiasi pale na kuagana nao.

Usiku wa leo, baba Angel na mama Angel walianza kuongea baadhi ya mambo ambayo yametokea,
“Unajua yule dokta alivyosema anaenda kuchunguza kuhusu kifo sijui kutoa ushahidi ndio nimekumbuka kitu”
“Kitu gani?”
“Kabla ya ile habari kuwa wewe umepiga risasi, nilifatwa na mtu ofisini kwangu ambaye alikuwa ni mke wa Moses. Nilienda kuongea nae kwenye mgahawa wa karibu na ofisini pale, na aliniambia mambo mengi sana”
“Mambo gani hayo mke wangu?”
“Najua hata wewe yatakushangaza haya mambo”
“Niambie tu”
Mama Angel alianza kumueleza kuhusu ujumbe aliopewa na mke wa Moses kuhusu biashara yake ile, yani baba Angel alishangaa sana kwakweli, pia alimwambia kuhusu kifo cha mzee Jimmy,
“Hapo kwenye kifo ndio alinichanganya kwakweli, sijui kivipi Erica alisababisha kifo cha babu yake”
“Hebu kamuite atuambie maana hata mimi nimehisi kuchanganywa na hizo habari sasa”
Ikabidi mama Angel ainuke na kwenda kumuita Erica, ambapo moja kwa moja alienda nae chumbani kule na kumtaka akae kwenye kiti na kuanza kumuuliza, basi baba Angel alianza kumwambia,
“Mwanangu usiogope tumekuita wala usianze kufikiria mambo mengine, tumekuita kwa uzuri tu. Unamkumbuka babu yako yani baba yangu mimi?”
“Ndio namkumbuka, si wewe baba umepigwa risasi ulipoenda kutembelea kaburi la baba!!”
“Oooh kweli una kumbukumbu nzuri, je unakumbuka siku ya mwisho babu yako kuja hapa kabla ya kushikwa na umauti wake?”
“Nakumbuka ndio”
Wazazi wake wakapumua kidogo na kumuuliza kwa pamoja,
“Ulimfanya nini”
“Nilimfanya nini kivipi? Mbona sikumfanya kitu”
Baba Angel ikabidi abadilishe swali,
“Yani ni kitu gani unakumbuka kutokea kati yako wewe na babu yako ile siku ya mwisho kufika mahali hapa”
“Mmmmh hakuna kilichotokea baba”
“Au ni nini uliongea nae, yani kuna kitu nahitaji kufahamu mwanangu ndiomana nimekuuliza”
“Ninachokumbuka ni hivi, babu alifika siku ile na alikuja moja kwa moja sebleni na kutusalimia na tuliongea nae kiasi tu, kisha aliondoka na kwenda kukaa kwenye bustani. Nakumbuka siku hiyo kuna sinema Fulani ilikuwa ikionyeshwa kwenye tv, kulikuwa na mtoto anacheza na babu yake nikajikuta nimeipenda sana ila sisi babu yetu hakuwa vile, basi moja kwa moja nilienda kwenye bustani na kumvizia babu ila nilimkuta akiongea na simu, sijui alikuwa akiongea nayo nini ila nilichogundua ni kuwa babu hatupendi, basi nilienda mbele yake babu na kumwambia babu sikupendi, aliniuliza kwanini? Nilimwambia sikupendi, sikuweza kuizuia chuki yangu mbele ya macho yake, nakumbuka nilirudia hilo neno kama mara tano hivi halafu niliondoka kwa kukimbia, nisameheni wazazi wangu ila mimi nilimwambia ukweli wa moyo wangu, sikuwahi kumpenda babu toka siku namtambua kuwa ni babu yetu”
Baba Angel na mama Angel walitazamana kwa muda kidogo bila ya kusema neno ila badae walimruhusu Erica aende kulala tu kwa muda huo, basi Erica akaondoka na wenyewe wakaongea kidogo.
“Hivi umemuelewa mtoto?”
“Unajua mimi huwa simuelewi huyu Erica kabisa, kwanza kana mambo ya ajabu sana. Mtoto kama huyu alianza kumchukia babu yake toka siku ya kwanza kwasababu gani?”
“Mke wangu, kumbuka huyu Erica huwa anaota inawezekana amewahi kuota matukio ya baba yangu ndiomana alijikuta kutokumpenda toka siku ya kwanza, tusimlaumu sana. Ila najiuliza kama hilo neno la sikupendi ndio lililomfanya baba afe? Mmmh!”
Walijadiliana pale ila hakuna jibu walilolipata.

Kesho yake mapema kabisa, mama Junior alienda tena pale kwa mdogo wake kumuangalia baba Angel pamoja na kumuangalia Vaileth aliyejifungua maana hata siku ile hakuweza kumsubiri.
Basi alifika na kumkuta mama Angel pale,
“Pole mdogo wangu, pole kwa mambo mengi ya hapa kwako. Vipi huyo mzazi hajaenda kwao tu!”
“Hapana, nipo nae, nimeona bora mtoto achangamke kwanza”
“Basi ngoja nikamuone kidogo”
Basi wakaongozana hadi chumbani kwa Vaileth ambapo alikuwa akimyonyesha mtoto, na aliwasalimia alipowaona, basi alipomaliza kumnyonyesha mtoto alimpa mama Junior ili amshike kidogo ila mama Junior alipomtazama yule mtoto alishtuka sana na kusema,
“Kheee mbona huyu mtoto kafanana sana na Junior!!”
Mama Angel nae akamuangalia vizuri na kuona kuwa ni kweli yule mtoto kafanana sana na Junior.

Basi wakaongozana hadi chumbani kwa Vaileth ambapo alikuwa akimyonyesha mtoto, na aliwasalimia alipowaona, basi alipomaliza kumnyonyesha mtoto alimpa mama Junior ili amshike kidogo ila mama Junior alipomtazama yule mtoto alishtuka sana na kusema,
“Kheee mbona huyu mtoto kafanana sana na Junior!!”
Mama Angel nae akamuangalia vizuri na kuona kuwa ni kweli yule mtoto kafanana sana na Junior.
Mama Angel alikaa kabisa na kumuangalia Vaileth kisha akamwambia,
“Eeeh Vaileth hebu sema ukweli mtoto ni wa nani?”
Mama Junior akasema,
“Aseme mtoto wa nani wakati ni chata ya Junior hii!! Atuthibitishie tu ukweli kuwa mtoto ni wa Junior”
Kwakweli Vaileth aliona aibu sana, ila kwavile walimuuliza sana ilibidi tu akubali,
“Ni kweli mtoto ni wa Junior”
Alikuwa akiongea huku ameinamia chini, mama Angel akasikitika kiasi na kusema,
“Yani Vaileth, binti mwerevu kweli unadanganywa na Junior? Halafu ulikuwa hutaki kusema ukweli kwanini? Je ningekufukuza wakati baba wa mtoto ni mwanetu? Kwanini ulikuwa hutaki kusema ukweli?”
“Nilikuwa naona aibu”
Mama Junior akasema,
“Ndio lazima uone aibu maana Junior ni mdogo kwako, wewe ndio wa kumfundisha Junior”
Mama Angel akasema,
“Ni kweli Junior ni mdogo kiumri kwa Vai ila Junior ni mkubwa sana kuliko hata huyu Vai, maana Junior anahangaika na wamama watu wazima wenye umri mkubwa kushinda hata wewe mama yake, sembuse haka kavaileth!! Tena usikute Junior alimbaka huyu. Eti Vai, ulibakwa na Junior au ulikubaliana nae?”
Vaileth alikuwa akihisi aibu sana yani alihisi aibu kupitiliza,
“Hajanibaka”
“Kwahiyo ulikubaliana nae? Vitu vingine vinachekesha na kusikitisha, kwahiyo Junior akakupa maneno matamu kuwa nitakuoa hata usijali na kukufanya wewe umuamini kabisa, bila kujali kuwa Junior ni kavulana kadogo kanakochipukia”
Mama Junior akaongezea,
“Yani Junior akakuoe wewe!! Khaaa jamani haya mashikolo mageni, yani wewe ukaolewe na Junior!! Siku ile mmekuja nyumbani kwangu kumbe ndio mmekuja kutambulishana loh!!”
“Tena Daima alituambia humu ndani kuwa Junior na Vai kuna kitu kinaendelea tukamkatalia binti wa watu na kumuona chizi, kumbe ni kweli. Nashangaa sana kwakweli”
Vaileth alikuwa ameinama chini tu kwa muda huo huku machozi yakimtiririka, basi mama Angel alijiwa na imani kiasi na kumwambia,
“Vai, nyamaza yani hata usilie kitu. Naelewa uliyopitia au unayoyapitia, ila umekosea sana maana tayari umezaa mtoto wa kwanza nyumbani, ulitakiwa kuwa makini sana hata kabla ya kuamua kuzaa tena. Kwakweli mnatufanya wazazi tupate aibu kwasana. Ila hilo swala la Junior niachie, kama alipanga kukuoa wala hiyo ndoto yako usiitoe kichwani mwako”
Basi mama Angel alimtoa dada yake pale na kwenda nae kuongea nae.

Mama Junior alimuuliza mama Angel kwa makini sana kwani hakumuelewa kwa ile kauli yake,
“Unajua kuwa sijakuelewa, ulikuwa unamaanisha nini? Kwahiyo Junior atamuoa Vaileth?”
“Dada, naomba uniachie hili swala mimi. Natambua maumivu aliyonayo yule binti, kafanya makosa ndio ila mara nyingine mapenzi yanatufanya tusione vya mbele, thamani ya yule binti imeshuka. Ni kweli ana mtoto ila ni binti aliyetulia sana, nina uhakika bila Junior basi huyu Vaileth yasingempata haya yaliyompata. Mwache tu Junior aserebuke huko, ajiachie na kujidai ila akirudi kuna mke wake huku hata asitake kunitania”
“Mmmh Erica jamani, unajua yule Vai ni mkubwa kwa Junior”
“Huyo Junior angeona Vai mkubwa basi asingemtongoza, kaona ni rika lake na atamuoa tu”
Mama Junior alimuangalia sana mdogo wake, ingawa hata na yeye alichoshwa na tabia za mwanae ila bado ilikuwa ngumu sana kwa yeye kukubali kuwa mwanae Junior amuoe Vaileth.
Waliongea kiasi pale ila mama Junior inaonyesha hakufurahi wala nini kwa lile swala, basi alimsaidia baadhi ya kazi pale mdogo wake halafu mama Junior akaondoka zake ila njiani akakutana na Linah ambaye alimuita mama Junior,
“Niambie mama mkwe”
“Mama mkwe!!”
“Unajifanya hujui kama wewe ni mkwe wangu kwa Junior au!! Junior ni mwanao halafu mimi ni mume wangu”
“Ila jamani, hivi huna watoto kweli wewe! Kwanini kumfanyia hivyo mwanangu?”
“Hata watoto wangu wote wamekubali kuwa Junior ni baba yao sasa sijui wewe ni nani wa kupinga na kukataa hilo. Unatakiwa kukubali tu kuwa mimi ndio mkwe wako”
Mama Junior alimuangalia sana Linah na kushindwa hata kumjibu kwa muda ule, kisha aliamua tu kuondoka zake huku akiona bora hata ya Vaileth kuliko huyo mkwe wake mama mtru mzima Linah.

Erica leo akiwa anatoka shule, alishukia njiani na kuanza kutembea kuelekea nyumbani kwao ila mbele yake kuna mtu alimuona, huyu mtu alikuwa ni kijana ambaye aliwahi kumuona kabla, alijaribu kutafuta kumbukumbu na kugundua kuwa yule kijana alimuona kwenye daladala kidha Daima na Samia walishuka kumfatilia na ambapo hakuwajibu kitu, basi Erica alijisemea,
“Si ndio huyu kaka kiziwi”
Akapita karibu sana, akagongana macho na yule kijana, basi Erica akasimama kumsalimia ili atambue kama kweli yule kijana ni kiziwi,
“Mambo vipi?”
“Poa, unanifahamu?”
“Hapana sikufahamu ila nimeona umeniangalia ndio nilitaka nikuulize na mimi unanifahamu?”
“Hapana, mimi naitwa Emmanuel. Je wewe unaitwa nani?”
“Mimi naitwa Erica”
“Ooooh jina zuri sana, unaishi wapi Erica”
Erica alimuonyesha kwa kidole tu, kisha huyu Emmanuel akampa Erica mawasiliano yake ili wapate kuwasiliana,
“Nadhani ninahitaji muda zaidi wa kuongea na wewe”
“Sawa hakuna tatizo”
Basi Erica aliagana nae na kuondoka zake, ila alianza kuhisi huenda huyu kijana anahitaji kumtongoza, ila kitu ambacho hakuelewa ni kwanini huyu kija a hakuitikia salamu za Daima na Samia hadi walihisi ni kiziwi ila leo kaongea vizuri kabisa na Erica,
“Mmmh au sio mwenyewe? Hapana ndio mwenyewe yule yule, namkumbuka vizuri sana”
Erica kwa muda huo aliongoza tu moja kwa moja na kurudi nyumbani kwao ambapo alianza kufanya shughuli za pale kwao maana kwa siku hizi alikuwa akirudi tu basi anaanza shughuli za nyumbani.

Usiku wa leo, Erica alienda kuongea na Erick maana siku hizi huwa hawaongei mara nyingi ila leo alijikuta akitamani sana kumueleza Erick kuhusu kijana aliyekutana nae,
“Jamani Erick kuna kijana tulijua mwanzoni ni kiziwi na bubu ila leo kaniongelesha”
“Ni kijana gani na kwanini mlimuhisi ni kiziwi na bubu?”
Erica alianza kumueleza ilivyokuwa hadi wakamuhisi hivyo yule kijana kuwa ni kiziwi na bubu,
“Aaaah kumbe alifatwa na hao vichaa, sasa huyo Samia na huyo Daima lazima mtu mwenye akili zake timamu asiwasikilize kabisa, ila huyo kijana ana shida gani na wewe?”
“Sijui ila kasema atahitaji kuongea nami zaidi”
“Nipatie namba zake”
Erica alimpa Erick lile karatasi la namba ambapo Erick alilichanachana lile karatasi na kumwambia Erica,
“Hakuna kuwasiliana nae, kumbuka hata mama kasema nikulinde kwa kadiri niwezavyo, nami nasema kuwa hakuna kuwasiliana nae”
“Ila kwanini Erick unakuwa hivyo jamani!! Unajua kuna wakati huwa sikuelewi, hebu niambie kitu gani unachoptaka kwangu”
“khaaaa usiniulize swali kama hilo mimi usije kunitendesha dhambi bure, ni usiku sasa unaweza kwenda kulala au umekumbuka karata leo!”
Erica hakujibu kitu kwani alichukia na moja kwa moja kuondoka zake na kwenda kulala.

Palipokucha, leo ilikuwa ni siku ya mapumziko kwahiyo hawakwenda shule, Erick aliona ni vyema kama akienda kumuamsha Erica maana jana yake aliondoka akiwa amechukia.
Basi moja kwa moja Erick alienda hadi chumbani kwa Erica, ila alimkuta amelala vibaya, yani kalala huku nguo imemfunuka, yani Erick alijikuta akimtazama kwa muda kisha alienda na kumfunika na shuka na hapo Erica alishtuka toka usingizini,
“Kheee Erick umekuja muda gani humu chumbani kwangu?”
“Muda sio mrefu, nilikuja kukuamsha”
“Umejiona kwanza hapo mbele?”
Erick aliinama kujiangalia, yani aliona aibu na kuondoka mule chumbani kwa Erica ila Erica alibaki akicheka tu kwa muda ule sababu yeye alihisi kama ni kichekesho kile.
Moja kwa moja Erica aliinuka na kwenda kuoga kisha alienda kumsalimia baba yake, maana kwa siku hizo ndio ilikuwa tabia yake kwa kila asubuhi kwenda kumsalimia baba yae.
Ila leo alivyoenda kumsalimia baba yake akamuuliza,
“Hivi Erica hakuna kingine ulichofanya kwa babu yako zaidi ya kumwambia kuwa humpendi?”
“Mmmh sikumbuki baba”
“Na ulivyomwambia kuwa humpendi ilikuwaje?”
“Nilimuona ameinama kwa muda kidogo na kuniangalia, halafu aliniuliza unasemaje Erica, nilimjibu sikupendi Babu basi sikuongea nae tena kwani niliondoka muda ule ule. Nisamehe baba ila kiukweli sikumoenda babu”
“Ila hujanipa sababu, kwanini humpendi?”
“Sababu yeye hakutupenda”
“Kivipi? Ulijuaje kama yeye hakutupenda?”
“Kwanza toka siku ya kwanza mnanitambulisha kwa babu sikumpenda, kuna siku niliota kuwa anataka kukuua. Nakumbuka ndio kesho yake akaja, kwahiyo ile filamu nilivyoiona, niliipenda kuona yule mtoto anacheza na babu yake, ila kwanini babu yetu alitaka kukuua? Ndio hapo nilimfata na kumsikia akiongea na simu ambayo sikumbuki ila ninachokumbuka ni kumfata na kumwambia kuwa simpendi”
“Mmmmh, wewe unaaminije kuwa alitaka kuniua? Unajua yule ni baba yangu kama nyie mlivyo kwangu, kanilea, kanisomesha na vyote kanifanyia, ni baba yangu ambaye ananipenda sana, utasemaje hakuwa akinipenda na alitaka kuniua?”
“Sijui baba, mimi niliota tu kuwa anataka kukuua”
“Je mimi naweza kuwaua ninyi? Huoni kama hiyo ilikuwa ni ndoto tu!”
“Ni ndoto tu ila matukio niliyoota yalikuwa ni yale yale”
“Kivipi?”
“Niliota kuwa babu amekuja vizuri kabisa hapa nyumbani, kisha akatusalimia na kwenda kwenye bustani ambapo aliongea na simu halafu sisi tulikuwa tukiangalia sinema halafu wewe ulikuwa kazini, ila ulivyorudi tu babu akakuita kwenye bustani na kukupulizia dawa usoni ambapo ukaanguka na kwenda kulazwa hospitali na ukafa. Ila kitendo cha mimi kwenda kuongea na babu kule kwenye bustani ni kama kilimfanya ajue kuwa ni kitu gani kinaendelea, unaweza usinielewe baba ila ndio ilivyokuwa. Sikuwa na nia mbaya kumwambia babu kuwa simpendi”
“Hivi ulimjua lakini kama neno lako sikupendi lingemaliza maisha ya babu yako?”
“Hapana sikujua, kwani babu amekufa kwasababu hiyo?”
“Sasa ni sababu gani iliyomuua babu yako?”
“Ni dawa aliyotaka kukupulizia wewe, alijipulizia mwenyewe na kufa”
“Mmmmh Erica jamani, babu yako aliondoka hapa akiwa mzima kabisa, utasemaje alijiwekea dawa?”
“Huwezi kunielewa, babu hajajiwekea dawa hapa, ila aliweka dawa baada ya kufika nyumbani kwake”
Kwakweli baba Angel bado hakumuelewa kabisa huyu mtoto wake na wala hakufikiri kama anaweza kumuelewa kwani aliona anachoongea kama hakihusiani vile na kifo cha baba yake, bado alikuwa na maswali mengi sana baba Angel kuhusu kifo cha mzee Jimmy toka mkewe kamuambia kuwa kifo cha mzee Jimmy kilisababishwa na Erica mdogo, basi akajisemea,
“Hapa watakaokuwa wanajua ni wafuasi wa mzee Jimmy tu maana huyu Erica nae hata sidhani kama anajielewa kwa kitu anachokisema”
Basi baba Angel alikaa tu pale kwenye kiti chake huku akitafakari mambo mbalimbali, kwanza kuhusu ndoto aliyoisema Erica kuwa baba yake alitaka kumuua aliikataa kabisa kwani aliona ni jambo lisilowezekana wala nini.

Mama Angel kama ambavyo alielekezwa na dokta Maimuna, basi muda huu alienda kufanyisha zoezi mume wake kama kawaida, na alipomaliza alikaa chini na kuongea nae,
“Sijawahi kufikiria katika maisha yetu hata mara moja kuwa kuna siku itakuwa hivi!!”
“Je ushawahi kufikiria kuwa kuna siku utabaki mjane”
“Jamani Erick naomba usiseme maneno hayo, naomba usiseme kabisa. Unanimaliza nguvu, naomba nitangulie mimi kufa kabla yako”
“Jamani mke wangu hapo unakosea, unajua sisi wanaume hatuwezi majukumu mazito ya familia ndiomana huwa tunakufa mapema, usiniombee kuniacha mke wangu maana nitakuwa kwenye wakati mgumu sana”
“Mungu atusaidie ili tuzeeke pamoja”
“Sasa hayo ndio maneno mke wangu, ili tulee pamoja familia yetu hii maana bado wanatuhitaji. Naamini nitainuka na nitatembea kabisa kama zamani”
Basi mama Angel alikuwa akitabasamu pale huku akiongea na mume wake, mara kuna simu iliingia kwenye simu ya mama Angel, alipoiangalia aliona namba ngeni ila aliipokea na kuanza kuongea nayo,
“Pole sana Erica”
“Kwani nani wewe?”
“Mimi ni Manka, pole sana”
“Kheeee Manka? Yani unajua wewe umefanya jambo la ajabu sana, kweli kumpiga risasi Erick kwa kosa gani?”
“Hapana, si mii niliyempiga na wala sijasema kuwa apigwe. Huwezi ukaniamini ila si mimi”
“Kama uliweza kumuwekea sumu Erick unashindwa vipi kusema apigwe risasi?”
“Hata sumu si mimi niliyemuwekea, aliyempiga risasi ndio anajua kila kitu”
“Moses!!”
“Ndio Moses, mimi siwezi kufanya hivyo unajua. Ni kweli nina roho mbaya ila siwezi kufanya hivyo”
“Na umewezaje kushirikiana na watu wanaomfanyia hivyo Erick kama wewe huna nia mbaya kwake?”
“Hayo sio niliyokupigia simu, ila nilichopiga simu ni kuuliza hali ya Erick anaendeleaje kwasasa?”
Mama Angel alipatwa hata na hasira kwakweli, alijikuta akijibu kwa hasira tu,
“Alikufa”
Kisha akakata ile simu, na kuanza kumueleza mumewe kuhusu aliyepiga, kwakweli hata baba Angel alimsifu mkewe kwa kumjibu kuwa alikufa,
“Hilo ndio lilikuwa lengo lao kuniua, sasa ananiulizia naendeleaje wakati waliniua!! Huyo mwanamke ni mjinga sana sijapata kuona dah!!”
Basi mama Angel aliamua kwa muda huo kumrudisha mumewe ndani baada ya yale mazoezi ya asubuhi ambayo alimfanyia.

Kwenye mida ya mchana, mama Junior alifika tena pale kwa mama Angel ila leo alibeba na zawadi za mtoto yani hata mama Angel alifurahi kuona vile kwani ilionyesha kuwa kwa muda huo dada yake alikuwa amekubaliana na hali halisi kuwa yule mtoto wa Vaileth ni mjukuu wao,
“Naona umejiongeza sasa dada!”
“Nisijiongeze mchezo!! Mwenzio si nilikutana na yule mtu mzima jamani, akaanza kuniita mama mkwe tena anasema intake nisitake yeye ni mkwe wangu tu”
“Kheee yule Linah!!”
“Ndio huyo huyo, yani nilichukia kweli kwa ile kauli yake”
“Khaaa halafu ana wazimu yule mmama jamani. Ila lazima tufanye jambo tu kuwa Junior amuoe Vaileth”
“Hata mimi nipo tayari kwa hilo kuliko yule mtu mzima kunizidi mimi kuniita mama mkwe dah nilijihisi vibaya sana”
Mama Angel alicheka kidogo,
“Yani nacheka kama mazuri, ila huyu Junior huyu dah!! Kwakweli katushinda tabia huyu mtoto”
Basi mama Junior, moja kwa moja alienda chumbani kwa Vaileth na kumshika mtoto kisha kumpa Vaileth zile zawadi ambazo alimbebea mtoto, kwakweli Vaileth alifurahi na kumshukuru sana kwa jambo lile.
Kisha mama Junior alianza kuongea nae,
“Eeeeh niambie kwanza, utaweza kuishi na mwanangu?”
Vaileth alijibu kwa uoga uoga,
“Nitaweza”
Mama Angel nae aliingia muda ule mule ndani na kuwakuta wakiulizana hivyo, basi akasema,
“Asiweze kuishi nae kwanini? Mtu kaweza kulala nae na kupata mimba, ndio atashindwa kuishi nae kweli!!”
“Mmmh Erica siku hizi umekuwa mjanja mdogo wangu yani unaongea kijanja janja, halafu sikutegemea kama unaweza kukubali Junior kuishi na huyu mwanamke”
“Dada, huyu Vaileth ni mwanamke mwenzetu, najua unaelewa ambavyo anajisikia kwa hili alilolipitia. Muache apate faraja kidogo, Vaileth usijali huyo Junior atakuoa tu, ilimradi amekuzalisha basi atakuoa tu”
Kiukweli Vaileth alitabasamu na kufurahi sana kwenye moyo wake kwani hakutegemea kama wale wamama wawili wangekuwa upande wake.

Kuna kitu Sia alikuwa akikiwaza sana, haswaaa kuhusu mtoto wa madam Oliva, yani alikuwa na hisia zote kuwa huenda yule mtoto akawa mtoto wake maana hakuona kama kule kufanana na yule mtoto ni kwa kawaida.
Basi leo, aliamua kwenda kwa madam Oliva sababu alikuwa akipafahamu hakupata shida kwenda pale ila alijisihi kwanza moyo wake kuwa anatakiwa kuwa mstaarabu na sio kukurupuka kama alivyofanya kwa Erick wakati anang’ang’ania kuwa ni mwanae.
Moja kwa moja alienda nyumbani kwa madam Oliva, ila muda huu hakumkuta madam Oliva na hata Steve alikuwa amelala kwa muda huu kwahiyo ni yule yule mtoto Paul ndiye aliyemkaribisha na kuongea nae kiasi,
“Kwani kaenda wapi mama yako?”
“Kwenye biashara zake, mama yangu ni mwanamke shupavu. Anapenda kujishughulisha na mambo mengi, hapendi mimi nipate shida”
“Na baba yako je?”
“Mmmh huwa simuelewi, ila nampenda. Sema simuelewi kabisa, muda wote anashinda nyumbani na kufanya kazi za nyumbani na kulala, sijui kama wanaume wote wapo kama baba”
Sia akagundua kuwa anachofanya Steve hakikuwa sahihi mbele ya macho ya mtoto kwani alikuwa akijifunza kile kitu ambacho hakikuwa na maana, basi Sia alimwambia,
“Kwani baba yako hajawahi kufanya kazi?”
“Mimi sijui maana baba mwenyewe nimemjua ukubwani hivi. Ila mimi nakumbuka wakati naishi kwa bibi, ni bibi ndio utamkuta muda wote nyumbani na akiondoka sana basi yupo kwenye bustani yake ila babu alikuwa akipenda kujishughulisha, na ukimkuta nyumbani basi atakuwa akisoma vitabu. Nakumbuka hata kwa mama mkubwa nilipoishi ndio ilikuwa balaa huwezi kumkuta baba mkubwa akishinda nyumbani muda wote. Ila toka nimekuja hapa, ni mama ndio anahangaika ila baba muda mwingi tunafanya nae shughuli za nyumbani hapa halafu na kwenda kulala”
“Sawa, unaweza kuniitia baba yako kidogo niongee nae na nimuage maana nitakuja siku nyingine”
Ni kweli Paul aliinuka na kwenda kumuita Steve, yani Steve alivyotoka na kumkuta Sia kiukweli alichukia kiasi ila aliamua kutoka nae nje kabisa ili aondoke,
“Umefata nini nyumbani kwangu Sia?”
“Sijaja kwa lengo baya wala sijaja kwa ugomvi, nimekuja kwa mema tu. Nashukuru umenitoa nje ili niweze kuongea hili”
“Lipi hilo?”
“Steve, najua unaishi vizuri na huyu madam, najua kama madam anajiweza maana ana biashara zake na kazi yake. Ila kuna muda mwanaume unatakiwa kuwa mwanaume, hebu simama kwenye nafasi yako Steve, hili ndio jambo hata ndugu zako waliweza kukutoa kwangu, ni mwanaume gani wewe unashindwa kusimama kwenye nafasi yako?”
“Kivipi?”
“Laiti ungemsikia yule mtoto alivyokuwa akisema, nadhani akili yako ingekukaa sawa”
“Alikuwa anasemaje?”
Sia alimwambia kwa kifupi tu na kumuongezea,
“Sasa unatakiwa kujishughulisha, usitegemee kulishwa na kulelewa na mwanamke kwa kila kitu. Unatakiwa kusimama kama mwanaume. Acha ujinga Steve”
“Nimekusikia, ila nini kilichokuleta!”
“Nitakwambia tu kilichonileta nikija tena, mtunze sana Paul ni mtoto mwenye akili ambaye kagundua kuwa mwanaume hufai kukaa nyumbani na kulala lala kama mwanamke, wenzio huko hata kama hawana shughuli za kufanya wanashika vitabu au magazeti wanajisomea, sio kulala tu na hakuna ulichofanya. Hayo ni mambo ya kike, mwanaume analala sababu kachoka, katoka kufanya kazi ngumu huko amechoka na kuamua kujilaza mchana, sio unakuwa kama mwanamke unaamka asubuhi na kufanya kazi za nyumbani halafu kulala. Kusaidiana kupo hatukatai ila sio ndio unakuwa kama mwanamke jamani unatia aibu”
Sia hakuongeza neno la zaidi kwani muda huo huo tu akaondoka zake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom