Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

SEHEMU YA 371


Muda huu baba Angel aliingia chumbani ila alihitaji maelezo kwa mke wake kuwa kamfahamu vipi baba Emma yani ni nani katika maisha yake kwani bado alikuwa akijiuliza maswali mengi sana sababu akikumbuka zawadi alizokuwa anaenda kumnunulia mkewe kwa baba Emma siku zote ni huyu baba ndio alimchagulia mama Angel zawadi, kwahiyo leo alishangaa sana kuona huyu mtu anafahamiana na mke wake tena inaonyesha wanafahamiana vizuri sana, basi alimuuliza,
“Mke wangu naomba unieleze kuwa huyu mtu mmefahamiana nae vipi, unajua nimeshangaa sana jinsi mlivyojuana, naomba niambie ukweli ili niweze kuelewa”
mama Angel alipumua kidogo na kuanza kumueleza mume wake,
“Ni hivi, huyo uliyesema ni baba Emma, namfahamu kwa jina la John. Nilikutana nae miaka ya nyuma sana wakati nimemaliza kidato cha tano, nakumbuka nilikuwa narudi likizo ndio nikakutana nae kwenye zile basi kubwa za mkoani na tuliongea mengi sana, ila kitu alichonipatia kilikuwa ni ukumbusho mkubwa sana kwangu, alinipa zawadi ya simu, yani nilifurahi sana ukizingatia simu nilikuwa na uhitaji nayo sana”
Baba Angel akamkatisha kidogo,
“Kwahiyo alikuwa ni mpenzi wako!! Si ndio”
“Nisikilize kwanza mume wangu, ni kweli nilianza mahusiano na John ila katika mahusiano yetu hatukufanikiwa kuwa pamoja kimwili kabisa, kwanza tulikuwa wote tunasoma halafu tulipotezana kimawasiliano”
“Ulimpenda sana?”
“Mmmh mume wangu jamani, katika maisha yangu hakuna mwanaume yoyote ninayempenda zaidi yako, najua unatambua hilo. Najua unatambua ni jinsi gani nakupenda ila huyu John ni mmoja katika mapito yangu kama wewe ulivyopita kwakina Sia, inamaana ulikuwa unawapenda sana au ndio unawapenda sana kuliko mimi!!”
“Hapana, mimi nimekuuliza hivi kwa maana yangu. Unajua nini, huyu jamaa ndio mwenye lile duka la nguo na kila siku nikikuletea zawadi basi huwa nimezotoa dukani kwa huyu kijana na huwa ananichagulia yeye, kwa hakika huwa unazifurahia sana na kuzipenda sana, ushawahi hadi kuniambia kuwa siku hizi nakuchagulia zawadi nzuri sana. Kuna siku nilienda na Erick dukani kwa huyu jamaa, kisha yeye na mkewe wakachagua zawadi tofauti, Erick alisema nikuletee zote hapa nyumbani ila bado ulichagua ile ya huyu jamaa bila kujua kuwa nachukua kwake zawadi. Nakumbuka siku nyingine nilikuchukulia viatu, huyu jamaa sikumkuta bali nilimkuta mke wake ndio alinichagulia vile viatu, vilivyofika hapa nilitaka tutoke ukiwa umevaa vile viatu ila ulidai vinakubana na kukuumiza miguu na hadi leo hujawahi kuvaa tena vile viatu, ndiomana nimekuuliza mke wangu, huyu John ndio ulimpenda sana”
“Unajua hadi nashangaa na kujikuta nikikosa kabisa cha kuongea, yani sina kabisa cha kuongea. Mimi sio kwamba nilimpenda sana John, kwakweli hilo siwezi kukubali. Ila ninachokumbuka kuwa John ndio mwanaume wa kwanza mimi kuanza nae mahusiano ila hata hivyo sijawahi kulala nae, kingine John ni mwanaume wa kwanza kunipa mimi zawadi ambayo nilikuwa na uhitaji nayo kwa kipindi hiko na niliipenda, ila kusema kuwa John nilimpenda sana hapana mume wangu. John kwangu ni wa kawaida tu, labda kitu ambacho hufahamu ni kuwa John ni mdogo wake Rahim”
“Mdogo wake Rahim!! Kivipi?”
“Hata mimi mwanzoni sikujua kama ni ndugu, ila mama yao ana watoto wawili tu yani John na Rahim ila baba zao ni tofauti yani Rahim ana baba yake halafu John pia ana baba yake. Na ndio yule mama aliponigundua alisema kuwa mimi ni malaya sababu nimetembea na watoto wake wote”
“Aaaah kumbe ndio ilikuwa hivyo, ila bado najiuliza kwanini huyo John akikuchagulia zawadi ndio unapenda?”
“Hilo sijui mume wangu, hata sijui ni kwanini yani utakuwa unaniuliza tu na hata sielewi chochote kile”
Ilibidi baba Angel aache kumbana mkewe kwa maswali na kuanza kupanga mazoezi yatakayoendelea kesho yake.

Basi kila siku iliyoendelea mama Angel aliendelea kumfanyisha mazoezi mume wake ili aweze kuwa sawa kabisa maana alitamani sana kuona siku ikifika ambayo mumewe atainuka na kutembea kabisa kama zamani.
Siku hiyo baada ya mazoezi walikaa wakiongea,
“Unajua mke wangu nimechoka hii hali, yani nimechoka kabisa, nachoka sana kufanya mazoezi na kuzunguka na magongo, natamani siku moja Mungu aniinue niweze kusimama na kutembea tena”
“Mungu ni mwema mume wangu, naamini kuwa utapona kabisa, uzima upo njiani mwako”
“Asante ila hivi ni kitu gani kimetokea kwa dokta Maimuna maana ni wiki ya pili sasa hajaja wala hajapiga simu”
“Halafu sio kawaida ujue, maana toka aondoke siku ile ndio imekuwa basi tena. Nakumbuka siku anasafiri alituaga vizuri kabisa na wakati yupo safarini alikuwa akitupigia simu na kuulizia kuhusu maendeleo yako, na amerudi tu moja kwa moja alikuja, tuseme kasafiri tena au ni nini!”
“Hata angesafiri tena ni lazima angetuaga tu, sijui alichukizwa na nini”
“Mmmh na wewe mume wangu usitake kusahau hapa, nilikwambia yale maneno yako ya kunisifia sana mimi inawezekana kuwa sababu kubwa sana ya kumchukiza”
“Sasa na yeye si amwambie mumewe amsifie huko!! Mambo mengine ni ya ajabu hata kufikiria, tulikuwa vizuri tu hapa, sasa nisisifie ninachokipenda kwasababu ipi?”
“Hata kama unasifia angalia na mazingira na pia angalia moyo wa mtu mwingine, ngoja nikupe mfano, tuseme mimi nimeolewa na mwanaume mwingine na wewe huwa unanipenda sana ila sijaolewa nawe nimeolewa na huyo mwingine. Halafu tunakutana naanza kukwambia kuhusu ninavyompenda mume wangu, unajua lazima uumie sababu ulinipenda sana. Ni heri tuongee mada zingine ila kumsifia umpendae mbele ya mtu aliyekupenda sana sio vizuri, labda kama yule mtu kakusumbua ila sio vizuri”
“Hapo nimekuelewa mke wangu, ni kweli inauma hasa pale umeoa au kuolewa na mtu ambaye hakuwa wa ndoto zako halafu unakutana na yule uliyekuwa unamuwazia sana anakwambia kuwa anampenda sana aliyemuoa au kuolewa nae, ni kweli inauma ni heri kuzungumza mada zingine. Ila kwa lile alilolisema siku ile ndio lilipelekea mimi kusifia kuwa wewe ni mwanamke wa kipekee sana na ninakupenda sana, sikufanya kwa ubaya kabisa ila nilifanya vile kutokana na kile ambacho yeye alikisema mwanzo”
“Nimekuelewa pia mume wangu”
“Leo utapenda kula nini ili nikupikie upendacho, haya mavyakula ya kupangiwa nayo ushakula sana jamani, leo tubadili”
“Sijala pilau siku nyingi sana, natamani ningekula pilau leo”
Mama Angel alitabasamu na moja kwa moja kwenda jikoni ili kuanza mapishi.

Wakati mama Angel yupo tu jikoni, alifika Erica muda huo na kumfanya mama yake amuulize,
“Mbona leo umewahi sana kurudi shule?”
“Tumetolewa mapema mama, halafu leo ni Ijumaa”
“Oooh hapo nimeelewa, haya bora umerudi. Najihisi uchovu balaa, baba yako leo anahitaji kula pilau, nina uhakika utapika ya kumfanya baba yako ajilambe. Unataka kupika pilau nini maana ndio hapa nilikuwa nafikiria tu nipike pilau nini!”
Erica alitabasamu na kumwambia mama yake,
“Naomba nipike pilau kuku”
“Mmmh kwa kupenda vitu vizuri tu mwanangu hujambo, haya jiko lako hilo kama kuna cha kukusaidia utaniambia”
Sababu Erica alishatoa sare zake za shule, moja kwa moja alianza kupika pale jikoni kama alivyoagizwa na mama yake.
Alivyomaliza Erica, muda anaandaa kile chakula ndio muda ambao Erick nae alikuwa amerudi shule, ila kwa harufu ya kile chakula akasema,
“Naomba kabla hata ya kwenda kubadili hizi sare, nile kwanza hiko chakula maana sio kwa kunukia huku”
Erica alitabasamu na kufurahi tu, ila Erick alienda kubadili sare kwanza maana alijua akikaa vile kula ingekuwa balaa kwa mama yake.
Basi Erica alimpakulia baba yake chakula na kumpelekea, ambapo baba yake alimwambia
“Erica mwanangu asante sana, haya kaa uombee hiki chakula”
“Nimeombea jikoni baba”
“Aaaah sawa, ombea na hapa”
Basi Erica aliombea tena kile chakula na baba yake kuanza kula, yani mama Angel aliingia ndani na kukuta mumewe ndio akila kile chakula na kukisifia sana,
“Mke wangu, yani kwa hiki chakula ni hakika huyu Erica umejizaa mwenyewe jamani. Aaaah mtoto mdogo anafanya mambo makubwa kiasi hiki!! Ni ajabu sana”
“Ndiomana nilipoona tu amerudi nikamsakizia apike mwenyewe, unajua kwenye mapishi Angel sio sana ila kimbembe kipo hapa kwa Erica, hata mimi kanizidi”
“Aaaah mtoto ana balaa huyu, yani mahari yake kwa hakika naozesha kwa milioni ishirini hapa”
Mama Angel alicheka sana na kumwambia mumewe,
“Sasa itakuwa kuozesha au kumuuza hapo!!”
“Kheee hiyo ni mahari, unauzaje mtoto kwa milioni ishirini!! Thamani ya mwanangu ni kubwa sana, hata kwa bilioni tano siwezi kumuuza mwanangu, hiyo ni mahari yani sitaki mwanaume wa kumuoa Erica awe ngonjwa ngojwa, nahitaji awe ni mwanaume mwenye wadhifa na pesa yake”
Mama Angel alicheka sana jinsi baba Angel alivyomsifia binti yake, yani alikula kile chakula huku akisifia muda wote, mpaka pale Erica alipoenda kutoa vyombo bado alikuwa akisifia na kumshukuru sana huyu binti yake kwa kupika chakula kitamu. Baada ya Erica kuondoka, baba Angel alianza kumwambia mke wake,
“Yani mimi ni baba mwenye bahati, kwakweli sisi ni wazazi wenye bahati sana. Hawa mapacha wetu wawili, ni watoto ambao wamebadili maisha yetu kwa kiasi kikubwa sana, angalia Erica ni mtoto msikivu, mpole, mcheshi na mpishi mzuri sana, tukiacha sifa ya umbea aliyonayo bado Erica anabaki kuwa binti mzuri na bora katika maisha yetu. Tunakuja kwa Erick sasa, ni kijana mwerevu, mpole na msikivu. Naumwa siwezi kwenda kazini wala kutembelea biashara zangu ila Erick anafanya yote hayo yeye mwenyewe, nabaki tu kupigiwa simu kuwa kila kitu kinaenda vizuri na wengine wakinisifia sana kuwa nimepata mtoto haswaa ambaye anaonekana kubadilisha maisha yangu kwa kiasi kikubwa. Tukitoa hasira na kisirani cha Erick ila bado anabaki kuwa kijana bora sana katika maisha yetu. Hawa mapacha najivunia sana kuwa nao”
“Kweli mume wangu, yani huwa nikikumbuka kuanzia siku niliyopata mimba ya hawa watoto, misukosuko tuliyoipata, halafu leo tupo nao tukiwa na furaha tele huwa nafurahi sana moyoni. Kwakweli hii ni dhahabu safi katika maisha yetu”
Siku hii baba Angel na mama Angel walijikuta wakisifia sana uwepo wa Erica na Erick katika maisha yao.
 
SEHEMU YA 372


Usiku wa leo, Erica akiwa chumbani kwake, aliwaza pia kuhusu Emmanuel na kuona kuwa anahitaji kuzungumza na mtu huyu, moja kwa moja aliamua kwenda chumbani kwa Erick ili amuombe simu aweze kumpigia Emmanuel.
“Erick naomba simu ili nimpigie yule Emmanuele tena maana mbona hajanitafuta hadi leo?”
“Sikia nikwambie kitu Erica, kuna kitu tufanye halafu nitakupa simu uongee na huyo Erick utakavyo”
“Kitu gani hiko?”
“Kalete karata”
Basi moja kwa moja Erica alienda kuleta karata, na kumpatia Erick, basi Erick alimtaka waanze kucheza karata na kumwambia,
“Ukinifunga goli tano za karata basi nakupa simu unaenda kulala nayo kabisa chumbani kwako na unaongea na yeyote utakaye”
“Ila na wewe Erick, umeanza masharti kama mganga wa kienyeji”
“Mmmh Erica, mambo ya mganga wa kienyeji umeyajulia wapi wewe?”
“Si huwa naona kwenye sinema, halafu hata Samia huwa ananihadithia sana. Alishawahi kuniambia kuwa, wao wangekuwa na baba mwingine. Mama yao aliwahi kuwasimulia kuwa kuna mwanaume alipendana nae sana ila yule mwanaume alirogwa na mwanamke mwingine, basi mama yao ndio akaamua kuanza na baba yao wanayeishi nae sasa, kwahiyo mambo ya waganga yapo nayajua”
“Duh!! Wewe ni noma”
Pale walianza na maongezi mengine, ambapo Erica alikumbushia pia maongezi ambayo baba yao alikuwa akiongea na mama yao maana alikuwa akisikiliza vizuri maongezi yale,
“Erica jamani, kumbe ulikuwa ukiwasikiliza?”
“Ndio, si walikuwa wakiongea pale sebleni nisisikilize kwanini? Nimemkosea nini Mungu hadi nisisikilize?”
Yani Erick alicheka tu, na kuendelea kucheza karata ila walicheza sana karata hata Erica alisahau mambo ya kupiga simu kwa Emmanuel na ile ilikuwa ni furaha kwa Erick maana alitaka kumgelesha Erica kuhusu hayo mawasiliano yake.
Basi walicheza sana karata na mwisho wa siku kama kawaida walijikuta wakilala hoi pamoja pale kitandani.

Kulipokucha, mama Angel alitoka chumbani kwake na kuelekea chumbani kwa Erick kwani alikuwa akitaka kumuagiza ofisini kwa baba Angel kwa siku hii, kwahiyo moja kwa moja alienda chumbani kwa Erick, alipoingia ndani alishangaa sana kuona Erica na Erick na leo wamelala pamoja, basi aliwaamsha na kuwaambia,
“Yani nyie bado tu hii tabia yenu ya kulala pamoja inaendelea?”
Hawakujibu kitu zaidi ya kumsalimia na kufikicha macho tu, kisha mama Angel aliendelea kuwasema,
“Nyie mmekuwa wakubwa sasa, sio wadogo tena kama zamani. Kwasasa, wewe Erick umekuwa na wewe Erica umekuwa haifai kulala pamoja kabisa. Mnajua madhara yake?”
“Hatujui mama?”
“Nyie ni ndugu, sasa mnawezaje kulala pamoja na ukubwa huu!! Haya mkilala hapo halafu Erick ukakosea na kumshika dadako ziwa unadhani itakuwaje?”
“Kwani kuna ubaya mama? Si itakuwa bahati mbaya hiyo?”
“Hebu achene ujinga, bahati mbaya kumshika ziwa dada yako!! Sitaki huu ujinga wa kukuta mmelala pamoja tena, nyie ni wakubwa kwasasa, mmelala udogoni ila sio kwasasa. Nadhani tumeelewana, haya Erica nenda chumbani kwako huko”
Basi muda ule, Erica aliinuka na kwenda chumbani kwake halafu mama Angel alibaaki kumuagiza Erick ofisini kwa baba yake,
“Leo naomba uende ofisini kwa baba yako, halafu ukienda pale ofisini unatakiwa kupitia mikataba ya watu watatu, jitahidi upitie kwa makini mwanangu”
“Sawa mama, hakuna tatizo”
Basi mama Angel aliondoka zake na kumuacha pale Erick ajiandae kwenda huko ofisini.
Mama Angel alirudi kwa mume wake moja kwa moja na kumwambia,
“Kwakweli leo hawa watoto wamenichukiza sana”
“Wmefanyaje?”
“Eti nimewakuta wamelala pamoja hawana hata habari”
“Kivipi?”
“Yani Erick na Erica nimewakuta wamelala pamoja chumbani kwa Erick na hawana hata habari”
“Walikuwa wanafanya kitu gani kibaya?”
“Hakuna, walikuwa wamelala tu”
“Sasa umechukia nini mke wangu?”
“Unaona ni kawaida kwa watoto wakubwa vile kulala pamoja? Unajua yule ni mtoto wa kike na wa kiume?”
“Kwnai unahisi nini kitatokea wakilala pamoja mke wangu?”
“Sijui ila sipendi halafu nahisi wanaweza hata kutamaniana na kutuletea balaa sie”
“Kheee jamani, ndugu watamaniane tena kweli mke wangu!! Au yale niliyokuwa nasikia ni kweli, kuhusu wewe na Derrick!”
Hapo mama Angel aliamua kubadilia mada kwani huwa hapendi kuzungumzia kilichotokea kati yake na Derrick.

Erick akiwa ofisini mule kwa baba yake, alichukua ile mikataba na kuanza kuipoitia maana ameshakuja mara kadhaa hapa ofisini ila huwa hakai kwa muda mrefu sana, mara nyingi anafika kwa kuagizwa na baba yake, basi wakati akipitia mkataba wa mwisho, kuna mtu aligonga ule mlango wa ofisini, alimruhusu kuingia na alimuona kuwa ni mwanamke wa makamo ambaye alikuwa amebeba sahani ambayo imefunikwa juu kwa lailoni nyeupe yenye kuonekana, kwenye sahani hiyo kulikuwa na matunda, basi yule bibi alifika na kukaa karibu na kumsalimia Erick kisha akasema,
“NBilijua boss Erick amekuja”
“Hapana, mimi ni mtoto wake”
“Mmmh sijawahi kukuona kabla, ila umefanana sana na binti yangu”
“Binti yako? Kivipi?”
“Wewe utakuwa ni mjukuu wangu tu lazima”
“Sikuelewi, mjukuu wako kivipi?”
“Umefanana sana na binti yangu, halafu binti yangu hajabahatika kupata mtoto, kwakweli wewe ni mjukuu wangu kabisa. Unaitwa nani?”
“Naitwa Erick”
“Wow na wewe ni Erick kumbe!! Nimekupenda bure mjukuu wangu, naomba uwe mjukuu wangu kweli, mimi ni bibi yako, naitwa mama Juli”
“Kheee haya sawa”
“Niite bibi, nitaridhika sana, unajua sijawahi kukuangalia ila leo nimekuona vizuri sana, kwa hakika unafanana sana na binti yangu. Karibu matunda”
Yule bibi alimuachia Erick yale matunda aliyokuwa ameyabeba, kisha Erick aliweka yale matunda pembeni na kuendelea na kazi yake.
Alipomaliza moja kwa moja aliondoka pale ofisini na kuelekea dukani kwa baba yake, alibeba na yale matunda maana hakutaka kuyala kabisa akihofia mambo aliyoambiwa ya kula kula hovyo kuwa sio mazuri.
Alifika pale dukani na moja kwa moja kuanza kufatilia mambo yanayoendelea pale dukani na kuangalia vitu mbalimbali, ila alipotaka kuondoka tu alitokea Juma pale dukani na kuanza kuongea na Erick,
“Kumbe umekuja huku leo! Kwakweli baba yako lazima ajivunie sana kwa kumpata kijana kama wewe, yani wewe ni kijana wa tofauti sana”
“Asante”
Erick alikuwa akielekea kwenye gari lake ambalo alienda nalo, ila alipofungua mlango wa gari, Juma aliweza kuona yale matunda ambayo Erick aliyaweka karibu na kioo, basi Juma alimwambia Erick,
“Dah nimeona hayo matunda nimejikuta nikiyatamani jamani, unaweza kunipatia kidogo”
Erick alichukua yote na kumpatia kwani kiukweli hata hakuyataka yale matunda, basi Juma aliyapokea na pale pale alianza kula huku akimuongelesha Erick, ila alipokula tunda la kwanza tu alishtuka sana na kumwambia Erick,
“Kweli wewe ni mwanangu, nimeamini sasa”
“Hivi huwa unamaanisha nini? Unajua huwa sikuelewi, yani yule sio baba yangu?”
“Hapana, sina maana hiyo ila kuna kitu nahisi unajua ladha ninayoipata kwenye haya matunda? Kuna siku nitakwambia. Ila sijakwambia kuwa Erick sio baba yako, hapana. Maana hata mimi nikiwa baba yako, je nimezaa na nani? Sijawahi kuwa na mahusiano na mama yako. Nadhani unaelewa ila mimi huwanakupenda yani napenda hata ungekuwa kijana wangu, ipo siku nitakwambia ladha niliyoipata kwenye haya matunda”
Erick hakutaka kufikiria sana kwani muda ule ule aliaga na kuondoka zake.
 
SEHEMU YA 373


Baba Angel, muda huu alitamani sana kupata maziwa yale ambayo huwa yanauzwa kwenye pakti, kwahiyo kwa muda huo waliamua kumuagiza Erica ili aende akawanunulie hayo maziwa.
Erica alipotoka tu kununua maziwa, alikutana njiani na Emmanuel ambaye alikuwa ameongozana na pacha wake Emmanah, kwahiyo pale pale aliamua kumtambulisha Emmanah kwa Erica kwahiyo walifahamiana pale na kufurahiana, kisha Erica aliwaambia jambo moja,
“Jamani, mwenzenu baba yangu naumwa miguu yani nashuhudiwa kwenye moyo wangu kuwa nikifanya maombi pamoja nanyi, basi baba yangu atapona, kwahiyo nawaomba kama hamtojali basi twende wote nyumbani kwetu ili tufanye pamoja maombi kwaajili ya baba yangu”
Yani Emmanuel alijikuta akimfurahia sana Erica na kumuitikia kwa haraka,
“Kwakweli upo vizuri sana, nimefurahi kukutana na binti unayependa maombi kiasi hiko, na mwenye imani kubwa hivyo. Basi naomba hayo maombi tufanye siku ya kesho maana leo kuna mahali tulikuwa tunaenda”
“Sawa, hakuna tatizo. Mtakuja muda gani nyumbani?”
“Kwenye saa kumi jioni tutakuja huko nyumbani kwenu, hakuna tatizo”
“Sawa, nimefurahi sana kunikubalia jambo hili. Mbona Emmanah huongei kitu?”
“Aaah mimi nimekubali tu”
“Inaonyesha wewe sio muongeaji eeeh!”
Emmanuel akasema,
“Sio nini!! Weee anasoma mazingira kwanza, huyu anaongea kinanda nyuma”
Wote walicheka tu, kisha Erica aliagana nao hawa na moja kwa moja alienda nyumbani kwao kumpelekea baba yake yale maziwa aliyokuwa amembebea.
Alifika nyumbani na moja kwa moja kumuwekea baba yake yale maziwa kwenye kikombe kisha kumpatia ambapo alianza kuyanywa yale maziwa huku akiyafurahia, Erica alitaka kuondoka ila baba yake alimtaka akae pale waweze kuongea nae ambapo Erica alikaa,
“Unajua nini! Nakumbuka zamani, ulikuwa na mtindo wa kuja na kunielezea kila kitu ila siku hizi umebadilika mwanangu au ndio ukubwa!”
Erica alitabasamu tu na kusema,
“Mbona nipo kawaida baba”
“Haya niambie mwanangu, hebu nielezee na mimi mambo ambayo huwa unayaota.”
“Mmmh mengine nasahau baba”
“Sasa, ngoja nikuombe kitu. Kwasasa ukiota tu basi kesho yake hakikisha unanihadithia kila kitu kuhusu hiyo ndoto uliyoota, au utashindwa kufanya hivyo?”
“Nitaweza baba”
“Ndio uweze kama ambavyo unapenda kucheza karata maana nasikia wewe bila karata basi siku yako sio nzuri”
“Hapana baba, huwa nacheza tu kujifurahisha”
Basi baba Angel kwa siku ya leo aliongea mambo mengi sana na Erica maana alikuwa akitamani kwa muda mrefu sana kuweza kuzungumza na binti yake.

Usiku wa leo kama kawaida, Erica anaenda tena chumbani kwa Erick na kumkuta ndio anajiandaa na kulala, basi Erick anamwambia
“Ila mama si amekataza wewe kulala huku?”
“Kakataza kulala ila hajasema nisiwe nakuja huku, hata hivyo baba kasema hakuna ubaya maana hata yeye alikuwa akilala chumbani kwa dada yake hata alipokuwa mkubwa kabisa”
“Aaaah kumbe ni kawaida”
“Ni kawaida ndio, mama alichukia sababu hapendi karata, kwahiyo kitendo cha kuopna karata karibu yetu kilimfanya aongee sana utadhani kitu gani. Ila kuna muda yale maneno yake yana maana”
“Kwanini?”
“Kwakweli, kwasasa tumekua wakubwa, kuna vitu kwenye mwili wako hata sivielewi jamani huwa natamani kuviona hasa hiko ambacho huwa kinatuna hapo”
Erick alijitazama na kucheka, kisha Erica akaendelea kuongea,
“Tubadilishe mada, kilichonileta ni kuwa leo nimekutana na huyo Emmanuel na pacha wake Emmanah”
Hapa Erick alijihisi aibu kidogo ukizingatia alimkatalia simu ila ameweza kukutana nao, yani hapo alijihisi vibaya, na kumuuliza tu kwa upole,
“Ulikutana nao wapi?”
Erica alimueleza kisha alimuomba,
“Nakuomba kesho tushiriki maombi na watu hawa kwaajili ya baba yetu, moyo wangu unanishuhudia kuwa kama tukifanya hivi basi baba atapona”
“Mmmh haya, mimi nakubali. Kwahiyo tutamuombea baba humu ndani? Kwanza nahisi baba atacheka tu, maana sisi na kuombea wapi na wapi?”
“Ni kweli baba atacheka, mama nae atacheka na tutawavunja imani bure ila kinachotakiwa ni sisi kuwa na imani thabiti kuwa baba atapona tu. Nimefikiria na kuona kuwa wale wakina Emmanuel wakifika basi tutaenda nao kule kwenye bustani na kufanya maombi kule”
“Mmmh tukiomba kule mbali halafu baba yupo ndani atapona kweli?”
“Kila kitu ni imani Erick, kuna watu wapo Marekani ila anamuombea mtu wa Tanzania na anapona, yote ni sababu ya imani. Unaambiwa imani inaweza kuhamisha milima, kwahiyo tuamini tu kuwa atapona hata bila ya chochote, ila sisi tutashirikiana na kuomba kwa kumaanisha”
“Kwahiyo tutamwambia ajiandae”
“Ajiandae kufanya nini sasa? Sisi tutabeba mzigo wote, na tutajitolea kwaajili ya hili, nimewaomba sana wale wakina Emmanuel na wamekubali kwa moyo wote, kwahiyo nao wamekuwa na imani juu ya hili. Naomba nawe uwe na imani”
Erick alikubali tu na kisha waliagana halafu Erica alirudi chumbani kwake kulala.

Jumapili ile kama kawaida ya ile familia, wachache walienda kwenye ibada maana kwa kipindi hiko ilikuwa ni ngumu sana kwa familia nzima kuondoka mahali hapo, na hata wakiondoka walikuwa wanawahi kurudi.
Kwenye mida ya saa kumi jioni, kama ambavyo walikubaliana ni kweli Emmanuel na Emmanah walifika na aliyewapokea alikuwa ni Erica ambaye moja kwa moja alienda nao kwenye bustani yao na kumuita Erick, kisha walisalimiana pale na moja kwa moja Erica alianza kusema,
“Jamani, kama nilivyoongea nanyi, hili jambo tunaenda kulifanya kwa imani. Sisi sio wachungaji wala viongozi wa dini, sisi ni watu wa kawaida kabisa, ila nina imani kuwa tukifanya jambo hili kwa imani basi litafanikiwa tu. Naamini nanyi mnaamini kama mimi ninavyoamini”
“Ndio tunaamini”
“Basi tushikane mikono na tufanye maombi huku tukiamini kuwa Mungu atatenda kwa baba yetu”
Basi walishikana mikono na kuanza maombi mahali pale.

Muda huu baba Angel na mama Angel walikuwa wamekaa sebleni huku wakiongea ongea kuhusu mambo mbalimbali,
“Unajua ule mkataba wa mwisho Erick anasema amekuta una matatizo sana”
“Upi huo?”
“Ule wa mwisho kusainiwa”
“Kheee haiwezekani jamani, wananifanyia ujinga sababu naumwa ila naamini muda utafika na mimi nitainuka tena na kutembea kama zamani bila maumivu yoyote huku nikifanya shughuli zangu zote”
“Mungu ni mwema, tuwe na imani”
Mara gafla baba Angel aliinuka na kuanza kutembea, kwakweli lile jambo lilikuwa ni la kustaajabisha sana machoni pa mama Angel.

Mara gafla baba Angel aliinuka na kuanza kutembea, kwakweli lile jambo lilikuwa ni la kustaajabisha sana machoni pa mama Angel.
Baba Angel aliongea kwa furaha huku akitembea tembea,
“Jamani natembea, kweli Mungu katenda miujiza kwangu, kwasasa natembea”
Mama Angel nae aliongea kwa furaha sana,
“Mungu ni mwema sana, mume wangu umepata uponyaji. Oooh Mungu ashukuriwe kwakweli”
Yani baba Angel alikuwa na furaha ya ajabu, yani ile furaha aliyokuwa nayo ilimfanya moja kwa moja aende chumbani kumpigia simu mama yake maana aliona ndio wa muhimu kwanza kabla ya yote, ila mkewe alimfata nyuma na kumwambia,
“Kabla ya yote mume wangu tunatakiwa kumshukuru Mungu maana ni Mungu tu ametenda haya”
“Sawa mke wangu, nina furaha sana ujue”
Kisha mama Angel aliingia kwenye maombi ya kumshukuru Mungu kwaajili ya uponyaji kwa mumewe, ila tu hawakujua kama Erick na Erick waliita wenzao kwaajili ya maombi hayo pia.
Baada ya yale maombi sasa, ndipo baba Angel alipompigia simu mama yake ambaye nae alifurahi sana kwa kupewa taarifa na mwane kuwa amepona kabisa mguu,
“Jamani Erick, huwezi amini nilivyofurahi. Naomba nije tufanye tafrija fupi hata tule wote chakula cha mchana hapo kwako”
“Hakuna shida mama”
“Alika na baadhi ya watu wako wa karibu, unajua nina furaha sana yani siamini kabisa hiki ninachokisikia”
“Ukiniona ndio utaamini zaidi mama yangu maana mimi ni mzima wa afya kabisa sasa”
“Kwakweli Mungu ni mwema sana”
Basi baba Angel alimaliza kuongea na mama yake, na muda huo akampigia dada yake yani alikuwa na furaha sana juu ya kupona kwake, basi akaanza kuongea na mkewe,
“Yani kesho tu naenda ofisini, unajua sina maumivu yoyote yale niliyokuwa nayasikia. Huu uponyaji ni wa viwango vingine, siamini mimi nimebaki nastaajabu”
“Mungu anaweza yote mume wangu, kesho tutaenda wote basi huko ofisini”
“Ila kwa daladala, yani nina furaha hata natamani nitembee kutoka hapa hadi ofisini”
Mama Angel alifurahi tu kwani aliweza kuiona furaha ya mume wake kwa wakati huo, akamwambia,
“Sikia mume wangu, kesho tutaondoka wote hakuna tatizo tutaondoka wote kwa daladala kama usemavyo halafu mimi nitarudi nyumbani na badae nitakuja kukufata na gari lakini”
“Aaaah hapo sawa, ila nina furaha sana jamani khaaa kweli natembea mimi!! Au na leo tutoke mke wangu?”
“Jamani mume wangu, labda tuzunguke nyumba ila sio kutoka jamani!! Najua furaha yako mume wangu”
Ile wazo la kuzunguka nyumba, baba Angel aliliafiki na muda huo huo wakainuka ili watoke nje na watembee kuzunguka nyumba yao.
 
SEHEMU YA 374


Muda huu Erica alikuwa akiwashukuru sana wakina Emmanuel kwa kuungana nao kwaajili ya kumuombea baba yao, kwahiyo walianza kuongea ongea pale kawaida ambapo sasa Erica alitaka kuwakaribisha ndani kwao ili waweze kusalimia wazazi wao ila muda ule ule Emmanuel alipigiwa simu, na alipomaliza kuongea nayo alimuangalia Emmanah na kumwambia,
“Mama huyo anatupigia, kasema twende haraka sana”
Basi wakawaangalia wakina Erica pale na kuwaomba ruhusa tu ili waweze kuwahi kwao, hawakuweza kuwakatalia na kuanza kuondoka nao ila walipokaribia getini Erica akasema,
“Ila mama na baba walikuwa hapo sebleni tu, twendeni basi mkawasalimie”
Waliongozana pamoja hadi sebleni ila wazazi wao hawakuwepo, Erica alimuuliza Vaileth ambaye alionekana kuingia jikoni muda ule,
“Eti dada, mama na baba wako wapi?”
“Sijui, mimi sijawakuta hapa”
Basi Emmanuele akasema,
“Tutawasalimia siku nyingine”
Ilibidi tu wakubaliane nao na kuwasindikiza huku wakiongea ongea, basi Emmanah akasema,
“Mtatupa taarifa sasa ya jinsi ilivyokuwa”
“Sawa hakuna tatizo”
“Namba ya simu je? Ngojeni niwape namba yangu ili kama mkikosa ya Emmanuel mnipigie mimi”
Emmanah alianza kutaja namba yake, ambapo Erick alitoa simu yake na kuandika ile namba iliyokuwa ikitajwa na Emmanah, basi baada ya kuwasindikiza kidogo waliagana nao huku wakipanga siku nyingine kwenda na pia kuwakaribisha wakina Erica nyumbani kwao ili na wao wapate kufahamu wanapoishi.
“Asanteni sana, ipo siku tutafika huko hakuna tatizo”
Waliagana pale, halafu wakina Erica walirudi nyumbani kwao.

Erica na Erick walipoingia tu wanamuona baba yao anatokezea na mama yao huku wakiwa na furaha sana kwani baba yao anawapa ushuhuda na watoto wake kuwa amepona, hilo jambo linawafurahisha sana Erica na Erick ingawa hawakumwambia baba yao kuwa walikuwa wakifanya maombi ili apone ila walifurahi sana kwa jambo lile, na moja kwa moja Erick alivyoingia ndani kwake tu alianza na ile namba ya Emmanah sababu ndio ilikuwa juu na kuwapa ushuhuda wa baba yao kuwa amepona,
“Jamani, baba Amepona na kwasasa antembea vizuri kabisa”
“Oooh hiyo ni habari njema sana, kwakweli Mungu ni mwema”
“Tumefurahi sana, asanteni sana”
Erick alivyomaliza kuongea na simu, Erica nae alikuwepo pale chumbani kwa Erick na kuendelea na furaha yake,
“Umewaambia eeeh!!”
“Ndio, wamefurahi sana pia, kweli kila kitu ni imani. Nimefurahi sana, wewe Erica ni mtu mwingine kabisa”
“kwanini?”
“Ulifikiria nini kwanza kabla ya haya yaliyotokea?”
“Nilikumbuka ya kwamba kila kitu kinafanyika kwa imani, basi siku niliyokutana na Emmanuel nikawaza kuwa hatuwezi kuungana nae na kufanya pamoja maombi? Nilipowaona tena njiani na pacha wake ndio ikabidi niwaombe tena na tumefanikiwa kwa hili”
“Aaaah hongera sana, je wazazi hatutawaambia hili lilolofanyika”
“Wala tusiwaambie ila watajua tu, yani wewe tulia halafu utaona, baba na mama watajua wenyewe na wao ndio watatuambia sisi”
Basi Erick hakuwa na cha ziada cha kuongezea maana alikuwa na furaha, kisha kila mmoja sasa alielekea kwenda kufanya mambo mengine.

Usiku huu wakati Erick akijiandaa kulala, kuna ujumbe uliingia kwenye simu yake ukitoka kwenye ile namba ambayo Emmanah alisema ni yake,
“Mambo vipi Erick? Ni Emmanah hapa, baba anaendeleaje?”
“Kwakweli anaendelea vizuri tunamshukuru Mungu kwa hili, tumekula nae vizuri na wameenda vizuri kulala”
“Oooh hiyo ni habari njema, kwakweli nimefurahi sana. Mungu ni mwema”
“Amen”
“Ila zaidi ya yote nimefurahi sana kukufahamu”
“Hata mimi nimefurahi kukufahamu pia”
“Basi tuwe tunawasiliana Erick, nimejikuta napenda sana kuwasiliana na wewe. Nimekufahamu leo ila nimefurahi sana kukufahamu, nadhani Mungu alikuwa na lengo jema kutukutanisha. Naweza kukupigia simu muda huu?”
“Piga tu hakuna tatizo”
Basi baada ya muda kidogo simu ya Erick iliita ambapo aliipokea ile simu na kuanza kusikilizana nayo, sauti ya Emmanah ilikuwa kwa chini sana kiasi kwamba lazima amsikilize kwa makini sana,
“Unajua nataka kulala muda huu, ila nikajisemea kuwa nikupigie simu kwanza. Au nimefanya vibaya?”
“Hapana, halafu sikujua kama wewe ni muongeaji mzuri hivyo kumbe wewe ni muongeaji!! Nakumbuka ulikuwa unakaa kimya muda wote”
“Mimi huwa mara nyingi hadi mtu nimzoee sana, ila mimi ni muongeaji mzuri tu. Hata kukutafuta wewe, nimejitahidi sana kwani huwa naogopa kuwasiliana na watu wengi, yani mtu pekee ambaye huwa nawasiliana nae ni Emmanuel tu sababu ndio ananifahamu vizuri mimi”
“Aaaah sawa nimekuelewa, usiku mwema”
“Kheee mbona haraka hivyo, unaniaga kabla hata sijakuaga jamani!! Mimi bado nataka tuongee”
Erick alishangaa kidogo kwani hakuona kama ana mazongezi ya ziada ya kuongea na huyu Emmanah ila aliongea nae hivyo hivyo kuhusu mambo mbalimbali hadi alijikuta akichelewa sana kulala, na iliwezekana pale simu ya Emmanah ilipoisha muda wa maongezi, yani Erick alishukuru kwakeli na kuamua kulala ila muda ulikuwa umeenda maana ilikuwa ni saa nane usiku.
Kulipokucha kama kawaida, Erick aliamka na kujiandaa kwaajili ya kwenda shule ila alikuwa na usingizi kiasi kwani alichelewa sana kulala, basi hivyo hivyo alijitajidi na kwenda shule.

Baba Angel kama ambavyo aliongea na mke wake leo, walijiandaa vizuri kabisa na moja kwa moja kuondoka kwenda kupanda daladala na kwenda kwenye ofisi ya baba Angel kama ambavyo walipanga, kwakweli baba Angel alikuwa na furaha sana kwa siku hii na kuongea mambo mengi sana na mke wake,
“Yani natembea huku siamini kama ni mimi niliyekaa chini miezi mingapi sijui, siamini kabisa”
“Amini tu, Mungu ni mwema halafu mahafali ya Angel yanakaribia”
“Oooh wow, nimebata na bahati ya kwenda kuudhuria na mahafali ya binti yangu kipenzi. Hii ni furaha sana kwangu. Ila tunastahili pongezi kwakweli, mtoto anamaliza kidato cha sita sasa tumekuza sana”
“Na kweli tumekuza, mwingine amemaliza na kutupatia zawadi ya ujukuu. Jamani Junior mambo yake!!”
“Hivi bado hamjamwambia ukweli eeeh!!”
“Tumesema hatumwambii lolote, mwache tu amalize vizuri mitihani yake, halafu akirudi hapa nyumbani tumpatie zawadi yake ya kumaliza kidato cha sita, naamini atapendezewa na hii zawadi ya mtoto au ndio ataanza kuruka futi mia kama kawaida yenu wanaume”
Baba Angel alicheka na kusema,
“Hawezi kukataa bhana, kwanza mtoto kafanana nae halafu kila kitu kipo wazi”
“Nimesema na atake asitake atamuoa huyo huyo Vaileth hata asitutanie. Kale kabinti huwa nakahurumia sana ujue, kwanza ana mtoto tayari ambaye haeleweki baba maana baba wa mtoto alishakimbia majukumu yake, halafu apeleke mtoto mwingine kwao ambaye baba haeleweki jamani!! Aaaah sio nzuri, mimba yenyewe kapatia kwetu, yani Junior atake asitake ataoa tu huyu mwanamke”
Baba Angel alicheka tu na kusema,
“Najua ukiamua umeamua, yani Junior kama alijua kwa huyu Vai atapita kama kwa Daima alivyopita basi kakosea namba maana naona mama mwenye nyumba umecharuka, hutaki ujinga kabisa. Ila kweli yule binti wa watu ni mpole, na akionekana anazaa zaa hovyo watampa sifa mbaya ya umalaya wakati binti katulia tu. Msumbufu ni kijana wetu, ila dada yako amekubali kuhusu hilo?”
Leo ndio mama Angel alimsimulia mumewe kuhusu mama Junior alivyokutana na Linah, yani baba Angel alicheka na kusikitika kwani mambo aliyokuwa anayafanya Linah yalimsikitisha kwakweli.
Basi walifika ofisini na baada ya muda kidogo mama Angel alimuacha mumewe pale ofisini halafu yeye akaondoka zake kurudi nyumbani kama ambavyo walikuwa wamepanga kufanya hivyo.
Basi baba Angel alipokelewa vyema tu pale na wafanyakazi wake, ambao walionekana kufurahi sana kwa bosi wao kurudi tena kazini kama zamani, kisha baba Angel alianza kupitia faili zake ofisini kwake kwanza maana ni muda mrefu hajafika humo.
Muda kidogo, alienda yule bibi muuza matunda na kufurahi sana kumuona baba Angel kisha alimsalimia na kumwmabia,
“Nilikuja na kumkuta kijana wako, nilijua ni wewe upo kumbe ni yeye. Hongera sana, una kijana mchapakazi sana nimempenda”
“Asante”
“Ila kijana wako kafanana sana na mwanangu”
“Mmmh kafanana na mwanao tena!! Mwanao gani?”
“Mimi nina mtoto anaitwa Juli, kwasasa ni mtu mzima ila mwanangu yule hajabahatika kuwa na mtoto. Mara nyingi anabeba mimba zinatoka, utakuta anajifungua ila watoto bahati mbaya, yani mwanao kafanana na mwanangu hadi raha. Nilimwambia hata siku aliyokuja hapa kuwa kafanana sana na mwanangu, nikamuomba nimuite mjukuu wangu”
“Duniani wawili wawili”
“Ni kweli kabisa, duniani wawili wawili”
“Kwani huyo mwanao yuko wapi kwasasa?”
“Unafikiri ana maisha mazuri basi!! Yani yupo yupo tu. Yupo huko mkoani anafanya kazi sijui kwenye shirika gani, yule nae alijikatia tamaa ya maisha kabisa, huwa anasema anatafuta hela ya kula tu basi maana atafute hela nyingi ya nini wakati hana wa kumuachia urithi!! Mwanangu kajikatia tamaa yule, yupo yupo tu”
Kwa muda huu baba Angel alikuwa na kazi nyingi sana, basi akamwambia huyu bibi kuwa wataongea habari zile kwa siku zingine maana alikuwa na kazi nyingi sana,
“Ila bado nakupa hongera, kama kijana umepata, kwanza ana heshima halafu ni mchapakazi kama wewe”
“Haya, nashukuru”
Yule bibi aliinuka huku akimuangalia sana baba Angel ambaye aliendelea na shughuli zake tu, yani baba Angel toka ile mikasa ya kupewa sumu basi alijikuta hapendi kutumia muda mrefu sana kuongea na huyu bibi ukizingatia alimuamini sana ila bibi huyu aliweza kurubuniwa kirahisi kabisa na mama Sarah.
 
SEHEMU YA 375


Mama Angel akiwa njiani akielekea nyumbani kwake, maana aliposhuka kwenye daldala aliamua kutembea tu kuelekea nyumbani kwake, ila kuna mtu alimuita na kumsalimia, alipomuangalia mtu huyo alimkuta ni Elly, ikabidi asimame na kuanza kuongea nae,
“Mbona siku hizi huji nyumbani Elly? Hujui kama mimi ni shangazi yako!!”
“Tatizo hampo wazi kwangu, siambiwi vizuri, ni shangazi yangu sababu yule anayesema ni baba yangu ni ndugu yako, sasa mbona mama anakataa kumfahamu baba yangu?”
“Ukikua zaidi utaelewa Elly, hiyo ni kawaida kwa wanawake wengi sana, ila kaa ukijua kuwa mimi ni shangazi yako na yule ni baba yako”
“Haya nashukuru, ila nafurahi kukuona leo ili nikupe huuu ujumbe”
“Eeeh ujumbe gani huo?”
“Ni hivi, jana nilipigiwa simu na Sarah, alidai kuwa anahitaji sana kuongea na wewe ila hakuwa na mawasiliano yako”
“Mmmh nipe namba zake tafadhari”
Elly alimpa mama Angel namba zile za Sarah, kisha mama Angel alimsihi Elly kwenda tena kuwatembelea kisha alimwambia na habari ya baba Angel kupona,
“Mwambie mama yako kuwa baba Angel amepona na kwasasa anatembea vizuri tu”
“Aaaah hiyo ni habari njema sana, nitampa huo ujumbe. Asante sana”
basi mama Angel aliagana na Elly na moja kwa moja yeye kuelekea nyumbani kwake.

Mama Angel alipofika tu nyumbani kwake, muda huo huo aliamua kumpigia simu Sarah kwa ile namba aliyopewa na Elly ili aweze kuzungumza nae, muda mfupi ile simu ilipokelewa na mama Angel kuanza kujitambulisha kama ambavyo Sarah alimzoea kumuita,
“Mama Erick anaongea hapa, hujambo Sarah!”
“Nafurahi sana umenitafuta, nimechoka kuishi na mama”
“Tatizo ni nini kwani Sarah?”
Sarah aliongea huku akilia,
“Natamani kumtoroka mama ila sijui nitakapoelekea”
“Aaaah usiseme hivyo Sarah wakati hapa nyumbani kwangu papo, unaweza kuja hapa. Kwani mko wapi na mama yako kwasasa?”
“Siwezi kutaja maana mama akinisikia hata kwa bahati mbaya atachukia sana, kwa kifupi mama yangu kabadilika sana yani simuelewi kabisa mambo yake”
“Sasa sikia Sarah, naomba uje tu moja kwa moja huku nyumbani. Hata ukipata usafiri mwambie huyo mtu akulete halafu mimi nitamlipa, jitahidi ufanye hivyo”
“Sawa nashukuru sana”
Mama Angel alijua wazi kuna tatizo kubwa sana lipo kati ya Sarah na mama yake, ingawa alijua wazi kuwa ile ya yeye kumchukua Sarah itakuwa tatizo kwa mama Sarah ila bado alihitaji kufanya hivyo maana moyo wa imani ulimfikia kila alipoongea na Sarah na kuona ile hali ya kilio cha Sarah.

Mama Angel kama alivyopanga, jioni yake anaenda ofisini kwa mumewe na kumchukua na kurudi nae nyumbani huku wakiwa na tabasamu, leo walipofika nyumbani tu walimkuta Sia yupo pale maana alipopata taarifa kuwa baba Angel amepona aliamua kwenda kumuona tu, kwahiyo waliongea ongea pale kisha waliagana nae.
Usiku ule, mama Angel aliongea na mumewe kuhusu Sarah, na baba Angel alikubali vizuri kabisa,
“Ni bora aje hapa tuishi nae maana najua hata huyo Manka atafika tu hapa na tutajua mipango yake yote”
“Ndio, itakuwa rahisi sana kufahamu mengi yahusuyo kwa Manka”
Basi waliongea mambo mengi sana, na toka siku hiyo mama Angel ndio alikuwa akifanya jukumu la kumsindikiza mumewe kazini maana alikuwa haamini kwa mume wake kwenda mwenyewe.

Siku hiyo, mama Junior alifika tena nyumbani kwa mama Angel kwa lengo la kumuona mjukuu wake, alivyofika pale alimkuta tu Vaileth na mtoto wake pamoja na Ester yani mtoto mdogo wa mama Angel, basi aliuliza pale,
“Baba Angel na mama Angel wameenda hospitali nini mbona hawapo leo?”
“Hamna, mama kamsindikiza baba kazini”
“Oooh kumbe kaanza kwenda na kazini, Mungu amsaidie shemeji yangu apone kabisa”
“Mbona ameshapona tayari, anatembea vizuri kabisa kwasasa”
Mama Junior alishangaa sababu alikuwa hajui halafu mdogo wake hakumwambia habari hiyo dada yake, basi akamchukua mjukuu wake na kumuangalia huku akizidi kumuona kuwa kafanana na Junior,
“Jamani huyu mtoto kila siku anazidi kuwa Junior mtupu, hivi mmempa jina gani?”
“Mama wa humu ndani kasema tumuite Joseph, jina la babu yake”
“Oooh hilo ni zuri sana, jina la kipenzi baba yangu. Mungu amrehemu, sijui Erica kafikiria nini jamani dah!! Nimefurahi sana kusikia hivyo. Ngoja nimlee vya kutosha baba yangu mie”
Vaileth alikuwa akitabasamu, muda huu Ester alikuwa chini akila chakula hata mama Junior alipenda kwakweli kwani Ester alikuwa akila vizuri sana,
“Hadi raha, kumbe Ester anakula mwenyewe!! Kweli wewe ni dada mlezi mzuri wa watoto ndiomana mdogo wangu hataki kukuondoa hapa kwake. Upo vizuri sana”
Vaileth alitabasamu tu na waliendelea kuongea mambo mengi na mama Junior ambaye kwasasa alikuwa ni mama mkwe wake.
Basi mama Junior aliamua kumuaga Vaileth na kuondoka zake maana kuna mahali alikuwa akihitajika,
“Nitampigia simu badae mama yenu, nikisahau basi naomba umkumbushe anipigie. Au akirudi tu mwambie anipigie”
“Sawa mama, hakuna tatizo”
Kisha mama Junior akaondoka zake kuelekea alipokuwa anatakiwa kupitia kabla ya kurudi nyumbani kwake.
Mama Junior akiwa njiani, akashikwa bega, kugeuka akamuona Linah ambaye alimsalimia,
“Habari mama mkwe”
“Hebu jiheshimu basi, mimi siwezi kuwa mama mkwe wako”
“Huwezi kivipi wakati nipo na mwanao!”
“Hivi chukua nafasi yangu, yani wewe uwe mimi halafu mimi niwe wewe ungekubali?”
“Kwanini nikatae ikiwa watu wanapendana? Upendo wa kweli hauangalii umri bali ni ule upendo wa dhati kutoka moyoni, kwakweli mimi na Junior tunapendana sana hilo huwezi kupinga hata ufanyeje hapa Junior habanduki”
“Dah! Hujielewi ndugu yangu”
“Na sijielewi kweli ujue, haya tuachane na hayo. Jiandae kupokea ujukuu maana kwasasa nina mimba ya Junior”
“Unasemaje!!”
“Hujanisikia au hujanielewa? Jiandae kupokea ujukuu maana nina ujauzito wa Junior, kwa kifupi Junior ndio baba wa mwanangu mtarajiwa”
Yani mama Junior alihisi hata kichefuchefu kuongea na huyu mtu, kwani aliondoka tu bila ya kusema chochote na kumuacha Linah akiwa anacheka sana.

Mama Angel leo mumewe alivyorudi nyumbani, ilibidi waongee tena kuhusu habari ya Sarah,
“Hivi kwani umewasiliana nae tena?”
“Ndio, leo nimewasiliana nae tena, kasema atakuja tu. Alikuwa na mitihani kaona bora amalizie kabisa ndio aje”
“Aaaah hapo nimemuelewa, kwahiyo uhakika wa yeye kuja upo ila hajataka kusema alipo mama yake?”
“Yani hilo kakataa kabisa, sijui ni nini ila najua Manka anajificha sababu ya haya mambo aliyokufanyia wewe nadhani anahisi tunaweza kumfungulia kesi”
“Ila kunikalisha nyumbani mwaka mzima, kweli nina haki ya kuwafungulia keshi hawa watu jamani, wamerudisha nyuma vitu vyangu vingi sana. Ila sasa Mungu alivyomwema, yani kila kitu Erick amekifanya kwenye mstari ingawa alikuwa akisoma. Kila siku nitashukuru kwa kumpata mtoto huyu katika maisha yangu”
“Hivi Erick kafata akili zako au akili zangu?”
Baba Angel akacheka na kusema,
“Kafata akili zangu yule”
“Mmmh ila asifate matendo yako”
“Kwanini sasa?”
“Unaona matendo yako yalikuwa sawa?”
“Lakini si nimebadilika!”
“Erick umebadilika na maombi wewe, muda mwingi nilikuwa nakesha kwa maombi ili mume wangu usitamani hovyo wanawake wengine na hadi leo unahisi kamavile nimekuroga, mimi nilikuwa namuomba Mungu ubadilike. Unadhani bila maombi nyie wanaume mnawezekana”
“Aaaah jamani mke wangu unaanza kunifananisha mimi na hao wanaume wengine wasiokuwa na akili? Kuna wanawake wanakesha makanisani, wanalia hadi jasho ila mwanaume habadiliki wala nini, utakuta ni anakunywa pombe hadi anazima na bado anabadili wanawake kama nguo, na mwanamke anaomba hadi anapata homa, kwahiyo ukikuta mwanaume kabadilika basi naye amechagua kubadilika. Ila hata hivyo nashukuru mke wangu maana maombi yako yameniokoa kwa vingi”
Mama Angel alicheka na kusema,
“Unamkumbuka Bahati alivyokuwa akinisumbua mimi hadi sina amani wala raha nikimuona, basi Fetty kamfanyia maombi yule, katoa na sadaka kwaajili yake, Bahati katulia tuli wala ahangaiki tena nadhani huwa hanitamani tena mimi, kwahiyo hata kama unapenda kubadilika ila maombi nayo yanasaidia sana maana bila maombi nyie wanaume mnavutwa sana mara mwingine akufanyie dawa, mwingine akufanyie uchawi kwahiyo lazima tuombe”
“Hata mimi huwa naomba sana Mungu akulinde mke wangu”
Wakawa wanacheka tu huku wakiendelea na maongezi yao.
 
SEHEMU YA 376


Usiku wa leo, Erick akiwa chumbani kwake akijiandaa kulala muda kidogo aliingia Erica mule ndani na kuanza kuongea nae maana alikuwa akisikia wazazi wake wakiongea kuhusu habari za Sarah,
“Nasikia Sarah anakuja hapa nyumbani kuishi na sisi”
“Umesikia wapi habari hizo?”
“Nimesikia baba na mama wakiongea kuhusu hiyo kitu”
“Mmmmh hujaacha tu mambo yako”
“Naomba simu yako mara moja Erick”
Erica aliamua kubadili mada na kumuomba Erick simu yake, ila alipoichukua tu muda huo huo kuna ujumbe uliingia kutoka kwa Emmanah,
“Nakupenda sana Erick”
Erica alimuangalia sana Erick na kumfanya Erick amuulize,
“Tatizo nini Erica?”
Erica nae alijibu kama ujumbe wa kwenye simu ulivyoingia,
“Nakupenda sana Erick”

Erica aliamua kubadili mada na kumuomba Erick simu yake, ila alipoichukua tu muda huo huo kuna ujumbe uliingia kutoka kwa Emmanah,
“Nakupenda sana Erick”
Erica alimuangalia sana Erick na kumfanya Erick amuulize,
“Tatizo nini Erica?”
Erica nae alijibu kama ujumbe wa kwenye simu ulivyoingia,
“Nakupenda sana Erick”
Kwakweli Erick alihisi moyo wake kuripuka kwa muda huo, sio kwamba hajawahi kusikia hili neno akiambiwa na Erica ila leo lilionekana kutoka kwa tofauti sana yani tofauti na siku zingine zote, Erick alimuuliza tena Erica,
“Unasemaje Erica?”
Erica nae alirudia ujumbe ule ule wa kwenye simu,
“Nakupenda sana Erick”
Yani Erick alimfata Erica karibu na kumkumbatia sana, yani hata Erica alikuwa akishangaa sababu hakutegemea kuwa baada ya kusema vile angemfanya Erick kuwa na furaha sana.
Yani Erick alimkumbatia Erica kwa muda mrefu sana huku akimwambia,
“Erica nakupenda sana pacha wangu, tena sana nakupenda naomba unipende hivyo hivyo”
Erick alianza kumbusu Erica, ila Erica alimsukumia pembeni na kumwambia,
“Weee mjinga unadhani ni mimi ndio nimekwambia kuwa nakupenda sana!”
Hapo Erick alikaa kimya kwa muda, kisha Erica alimpa Erick simu yake na kumwambia,
“Chukua huo upuuzi wako”
Halafu Erica alitoka na kuondoka zake kuelekea chumbani kwake.
Ndipo Erick alipochukua simu yake na kuangalia vizuri na kuona ule ujumbe ulikuwa umetoka kwa Emmanah, yani alishindwa hata kujibu ule ujumbe kwani muda huo huo aliweka simu pembeni na kuamua tu kujilaza kwani hakutaka hata kuwasiliana na Emmanah.

Erick alipoamka asubuhi ya leo, cha kwanza kabisa aliona ni vyema kwenda chumbani kwa Erica kwani aliona ana kila sababu za kumuomba Erica msamaha ukizingatia ni kweli amemkosea, basi aliingia na kumkuta Erica amejiinamia tu na kusalimia pale huku akimwambia,
“Erica naomba unisamehe, nisamehe sana sikujua chochote ila naomba unisamehe”
“Ila kwanini unaomba msamaha?”
“Sikujua kama kuna ujumbe toka kwa Emmanah kwenye simu yangu, naomba unisamehe sana”
“Kwani kukiwa na ujumbe toka kwa Emmanah ndio unapaswa kuniomba msamaha? Huyo Emmanah si atakuwa wifi yangu au ni vipi?”
Erica aliongea huku akitazama chini, Erick nae alipumua kiasi na kumwambia Erica,
“Hapana hawezi kuwa, sijui nikwambiaje Erica ila naogopa kusema. Sijui hata naanzaje kukueleza”
Erica alimuangalia Erick na kumwambia,
“Nadhani tunahitaji tupate mahali na tuweze kuzungumza kwa upana zaidi, au unasemaje?”
“Ni kweli, nina mengi ya kusema ila huwa nashindwa maana mdomo wangu unakuwa mzito sana”
“Twende ufukweni, na huko tutazungumza mengi. Leo ni Jumamosi, tukiwaomba ruhusa wazazi wetu watakubali tu ukizingatia ni siku nyingi hatujaenda kutembea”
“Sawa ni kweli, ngoja nikaongee na baba nadhani atanielewa”
“Ngoja mimi nitamwambia mama hata usijali, najua kwenye kujieleza sio mzuri sana wewe. Naomba tukifika huko uwe huru niambie chochote kile unachohisi nami nitakwambia”
Erick alikubali tu maana kiukweli alihitaji kuongea mambo mengi sana na Erica.

Mama Junior akiwa nyumbani kwake akiendelea na shughuli zake, kuna simu iliingia kwake na moja kwa moja aliipokea na kuanza kuongea nayo,
“Habari mama mkwe”
“Nani wewe?”
“Kheee, mimi ni mkweo Linah au una wakwe wangapi?”
“Khaaaa hivi wewe mmama huchoki? Kwanza nani kakupa namba yangu?”
Linah alisikika akicheka, na kusema,
“Kabisa unajikakamua kuuliza swali kama hilo kweli!! Namba nimepewa na mume wangu kasema leo nikusalimie mama yake, unajua kuwa nipo nae huku!”
“Nitolee balaa mie”
“Nadhani huniamini”
Mara ilisikika sauti ya Linah ikiita,
“Junior mume wangu hebu njoo mara moja”
Halafu ikasika sauti ya Junior,
“Nipo hapa kipenzi changu”
“Kuna mtu naongea nae hapa halafu haamini kuwa tupo wote, hebu mwambie ni jinsi gani unanipenda”
Mara Junior akasema,
“Nampenda sana Linah, nipo tayari kufa kwaajili yake”
Halafu Linah akaongea kwenye simu,
“Nadhani umesikia mwenyewe, mtoto ndio kashaganda, chezea mimi eeeh!! Hapa haambiliki wala hasikii anatamani kunioa hata leo, nasubiri tu amalize mitihani yote tutangaze ndoa. Najua utatuandalia zawadi nzuri sana”
Mama Junior alihisi hasira sana na kukata ile simu, yani hata kazi aliyokuwa akifanya aliiacha na kukaa chini huku machozi yakimtoka na kujisemea,
“Huyu huyu Junior nilimzaa mimi kweli au ana mama mwingine? Yani limeacha kujiandaa vyema kwa mitihani akiwa shuleni limeenda kwa mwanamke kweli!!”
Muda huo huo akaamua kumpigia simu mdogo wake mama Angel ili kumwambia jambo lile angalau apumue kidogo,
“Kwakweli mdogo wangu huyu Junior ananikosesha raha kabisa, sina amani mimi”
“Sikia kitu dada, hata usipaniki wala nini. Tunatakiwa kufanya kitu pamoja”
“Kitu gani hiko?”
“Njoo nyumbani tuongee, nakwambia huyo Junior na huyo mama yake watakoma tu, hapa ni ndoa ya Junior na Vaileth, hiyo ndoa ya Junior na huyo bibi yake Linah hatuikubali wala hatuielewi hapa. Asitupande kichwani huyu mtoto”
Basi alikata simu na kuanza kujiandaa ili kwenda kwa mdogo wake kuongea nae.

Erica alimfata mama yake na kumuomba ruhusa ili yeye na Erick waweze kwenda kutembea ufukweni, cha kushangaza ni jinsi mama Angel alivyokubali kuwa waende tu hata muda huo,
“Najua watoto wangu mmekaa sana nyumbani, mimi nawaruhusu kabisa na hela nitawapa. Nenda kamwambie Erick ajiandae mwende mkatembee huko ufukweni”
Erica aliondoka akifurahi sana ila mama Angel alifurahi zaidi na kusema,
“Afadhari jamani, sijui wamejuaje hawa watoto kwenda kutembea yani hapa angekuja dadangu tungeanza kujibana bana kuongea kwa kuhofia umbea wa Erica ila kwasasa ni huru kabisa tutapanga kila kitu hapa hapa nyumbani. Yani hawa na hela nawapa kabisa wakajaze mafuta kwenye gari waende huko wakazurule wee watakavyo”
Baada ya muda Erick na Erica walikuwa tayari wameshajiandaa na kumfata mama yao ambaye aliwapatia pesa akasema waende kutumia na kuweka mafuta kwenye gari,
“Hata hivyo najua kama wanangu mmefanya kazi kubwa sana, najua baba yenu angekuwepo hapa basi angetaka hata kuwaongezea pesa, ila natumaini hii ninayowapa itawatosha”
Walimshukuru sana mama yao pale ambapo aliongezea,
“Kama mkipungukiwa na hela basi Erick nipigie ili niwatumie nyingine kwenye simu”
“Aaaah hii inatosha mama, mbona nyingi tu”
“Haya, nawatakia matembezi mema”
Basi Erick na Erica waliondoka zao, kisha mama Angel alimuita Vaileth kwanza na kuanza kuongea nae,
“Vaileth mwanangu, sijawahi kukuuliza hili maana huwa tunaongea tu. Upo tayari kuolewa na Junior?”
“Ndio mama nipo tayari”
“Aaaah sawa kama ni hivyo basi kazi itakuwa rahisi sana hii”
“Kazi gani kwani?”
“Wewe tulia tu, subiri ndoa mwanangu”
Vaileth alitabasamu tu kwani ile ilikuwa ni habari nzuri sana kwake.

Erica na Erick walifika kwenye ufukwe waliohitaji kuwa na kutafuta mahali ambapo walikaa huku wamenunua vitu vitu vya kutafuna na kuanza maongezi yao, ambapo Erica ndio alianza kuongea,
“Leo, Erick naomba utoe dukuduku lako lote la moyoni najua una mengi sana na usijisumbue kunificha lolote lile, nieleze kila kitu unachohisi kwenye moyo wako”
“Hadi naogopa kujieleza”
“Usiogope nileze ukweli ili nami nikwambie ukweli”
“Ni hivi Erica, mimi najua kama wewe ni dada yangu tena ni pacha wangu ila tatizo lililopo ninapatwa na hisia tofauti sana juu yako yani najikuta nikitamani uwe mpenzi wangu wakati ni kitu ambacho hakiwezekani. Kuna siku niliwahi kukwambia kuwa mimi sitakuja kuoa katika maisha yangu sababu ninayempenda siwezi kumfanya awe mke wangu kwani ni dada yangu ambaye ndio wewe. Sijui nikueleze vipi Erica ila ndio hivyo, jana uliponiambia ile kauli kuwa unanipenda sana nilihisi kuchanganyikiwa kabisa, mwili wote nilihisi ukionyesha hisia za mapenzi juu yako. Ndiomana asubuhi nimekuja kukuomba msamaha kwani najua wazi kuwa nitakuwa nimekukwaza Erica, nisamehe sana”
“Usijali kuhusu habari za msamaha, nimeshukuru kwa kuniambia ukweli. Ipo hivi, sijui ni nini ambacho huwa kinakuja katika akili yangu yani huwa najikuta nikikupenda sana kiasi kwamba sitaki mwanamke yoyote awe karibu na wewe, nikiona kuwa mwanamke anaanza kujisogeza kwako huwa naumia sana, ila swala linabaki kwanini inakuwa hivi wakati sisi ni ndugu? Yani huwezi amini ile jana baada ya ujumbe wa Emmanah nilijikuta nikikosa usingizi na kuanza kulia, hadi nilikuwa sijielewi, na kilichoniliza zaidi nikikumbuka ni ile hali uliyonikumbatia nayo ilizidi kunipa hisia ndiomana nilikutoa pembeni, kwakweli Erick sielewi pia”
“Dah!! Mimi huwa naumia sana nikiona kuna vijana wanakufatilia. Ni kweli nilimkatia simu Emmanuel kwa kuhisi kwamba atakuhitaji kumbe haikuwa hivyo, yani yote hii ni sababu naumia sana juu yako Erica, sijui tatizo ni nini?”
“Hapo kwenye tatizo ni nini ndio pa kujadili, mimi na wewe ni ndugu tena ni mapacha. Inawezekana kwa ndugu kujikuta katika mapenzi ila kama hawafahamiani kuwa ni ndugu, utakuta wamegundua badae sana ila tofauti na mimi na wewe, tumekuwa pamoja, tunajuana kuwa ni ndugu tena ni mapacha, kwanini tuwe na hisia za kimapenzi kati yetu?”
“Sijui, ila mimi nakupenda sana. Hadi huwa najiuliza ni kwanini hairuhusiwi kwa ndugu kuwa pamoja kwenye mahusiano”
“Sio hiruhusiwi ila ni heshima tu, ukiangalia hapa duniani binadamu wote ni ndugu kwahiyo ndugu hawawezi kuwa wapenzi sababu ya heshima tu na kuangalia mipaka ya undugu na mahusiano ya kimapenzi. Ila kwa mimi na wewe ni kesi nyingine, huwa nahisi kuna jambo ambalo sio sawa kati yetu”
“Erica huwa unaota mambo mengi sana, je umewahi kuota chochote kuhusu sisi?”
“Huwezi amini, katika ndoto zangu zote sijawahi kuota kuhusu mimi na wewe, natamani sana kujua ni kitu gani kimefanyika baina ya mimi na wewe hadi tunajikuta kwenye hali kama hii. Kwanini unitamani mimi wakati unajua wazi kuwa mimi ni dada yako!! Na kwanini mimi nikutamani wewe wakati najua wazi kuwa wewe ni kaka yangu! Hapa ndio kwenye tatizo, na ninashikwa na wivu balaa pale ninapokuona upo na mwanamke mwingine”
“Sasa tunafanyaje Erica kwa hili?”
“Tunatakiwa kuchunguza”
“Ila nakuomba usiwe na mwanaume mwingine”
“Dah!! Kweli hapa ni tatizo, tunaweza kuona ni kawaida ila ni tatizo na tusipoangalia tutafanya hata wazazi wetu watuchukie sana. Sikia Erick tusionyeshe chochote kwa yeyote, tuwe tu kawaida huku tukichunguza. Najua siku nitawabana mama na baba nao wataongea ukweli kuhusu jamabo hili maana imezidi sasa”
Kwa maongezi haya, ilifanya moyo wa Erica na Erick kuwa huru sasa maana kila mmoja aliongea ukweli wa kile anachokihisi katika moyo wake na kuomba pale kuwa kila mmona ajitahidi kutokuumiza hisia za mwingine huku wakiendelea na uchunguzi maana Erica aliona kuwa jambo lile linahitaji kufanyiwa uchunguzi ukizingatia si rahisi kwa ndugu tena mapacha wa damu kujikuta kwa pamoja wameingiwa na hisia za mapenzi.
 
SEHEMU YA 377


Mama Junior alifika nyumbani kwa mama Angel na kuanza kuongea na mdogo wake, ambapo mama Angel alimwambia kwanza mama Junior kuhusu mpango alioufanya kuhusu Junior,
“Sasa dada kwa hayo mambo ya Junior tunatakiwa kufanya juu chini amuoe Vaileth”
“Atamuoaje sasa maana nina uhakika yule Linah akijua ni lazima atavuruga tu”
“Sikia dada, mimi na wewe ndio tutaenda kwakina Vaileth kujitambulisha na mambo ya mahari tutashirikiana na kutoa. Kisha siku Junior anarudi nyumbani tu inakuwa ndio siku yake ya harusi, yani tutafatilia wanamaliza lini mitihani na kwenda kumchukua ili afunge ndoa na mwenzie”
“Vaileth kakubali lakini?”
“Unadhani anakataaje na mtoto kashazalishwa!!”
“Sawa, je mila za kwakina Vaileth sio nyingi za kutusumbua?”
“Hamna cha kutusumbua wala nini, kwanza tutaongea na Vaileth ili aongee na kwao waweze mupunguza masharti na iwe kwetu rahisi kwenye kumuozesha Junior. Yani Junior, atake ataoa na asipotaka ataoa”
“Ila ni vyema kuwa na msimamo hivyo, yule mama kanichefua sana jamani, hadi nilikosa amani kabisa kabisa”
“Ngoja tumuite Vaileth tunakamilisha kila kitu hapa”
Mama Angel alimuita Vaileth pale na kuanza kuongea nae kuhusu sheria za kwao ambapo mwanaume akaitaka kuoa kwao ni kitu gani kinafanyika. Vaileth alianza kuwaeleza pale kisha mama Angel akamwambia,
“Hatutaki haya mambo kuyavuta sana, tunahitaji yaende haraka haraka ili tuweze kufanya shughuli kwa wakati. Natumaini inawezekana kwenye kwa haraka, si unajua kwenu kulivyo mbali?”
“Kwetu ni mbali ndio, ila mnaweza kwenda kwa kupitia shangazi, halafu mimi nitawapigia simu kule nyumbani kwetu. Siku ya mahali tu ndio ikaenda kule kwetu.”
“Haya kwa shangazi yako sio mbali, tuandalie barua ya uchumba hapo tumpelekee leo leo halafu ongea nao huko wapange mahari upesi ili tuweze kwenda kutoa mahari hii wiki inayoanza tu.”
Kwakweli Vaileth alifurahi sana kusikia jambo lile, na moja kwa moja alienda kuandaa barua ya uchumba kwa niaba ya Junior ambaye bado alikuwepo shuleni.
Alipomaliza kuandaa ile barua, Vaileth aliwapelekea na kuwaelekeza kwa shangazi yake na kuwapa mawasiliano yake.
Waliisoma na waliona ni jinsi gani Vaileth ameweza kujiongeza kwenye ile barua, kisha muda huo huo mama Angel alienda kujiandaa vizuri na kutoka kuelekea kwa shangazi yake Vaileth.

Mama Angel na mama Junior walibahatika kufika nyumbani kwa shangazi wa Vaileth ambaye aliwakaribisha vizuri tu sababu alishapigiwa simu na Vaileth, kwa muda huu shangazi alijisahaulisha yote ambayo yaliwahi kutokea kuhusu yeye kwenye nyumba ya mama Angel wakati amepeleka dawa zake pale.
Basi alianza kuongea nao kuhusu taratibu zote za kwao na kila kitu kuanza kujitambulisha basi waliongea nae tu wafanye haraka kisha waliamua kuaga na kuondoka zao ila ile habari ilikuwa ni nzuri sana kwa shangazi wa Vaileth yani aliwasindikiza huku akiwa na furaha kubwa sana.
Basi mama Angel na mama Junior waliongozana, wakiwa kwenye gari walianza kuongea kuhusu hilo swala walilolianzisha,
“Hivi wakishataja mahari itakuwaje?”
“Itakuwaje vipi dada? Tutalipa tu”
“Sasa wakitaja kubwa sana?”
“Wataje kubwa sana kwa misingi ipi? Kwanza kumbuka hawajui kama binti yao ana mtoto maana nishaongea na Vaileth kuwa hilo swala afanye siri kwanza kama alivyofanya kwetu, najua wazazi wa kiafrika wataanza kudai faini ya mtoto”
“Sasa itakuwaje kwenda kutoa mahari? Huyo Vai si tutaenda nae?”
“Twende nae wapi? Hao wazazi wake wana shida balaa, nadhani huwajui tu. Tukienda kutoa mahari utaona watakavyofurahi, yani hapa ni kumpanga Vaileth tu na kumuweka kwenye mstari. Anataka kuolewa, anajua kabisa mwanaume ni mwanafunzi, hiyo mahari kubwa anakubaliana na kwao kwa misingi ipi? Nitaongea nae na nitampangia kabisa mahari ya kusema kwao, hapa kwenyewe tumetoka kwenye matatizo, hizo hela nyingi tunaziotoa wapi? Mambo mengine watatafuta na mumewe wakiwa ndani ya nyumba yao. Sisi tutafanya kwa upande wetu na kupumzika”
“Hapo nimekuelewa mdogo wangu”
Njiani mama Junior alishuka maana alitaka tu kuonganisha kwenda kwao.
Mama Angel alivyofika getini ndipo akakutana na Sarah naye akiwa anashuka kwenye gari ambalo lilimleta, basi mama Angel alishuka na kumfanya Sarah kumuona, kwakweli Sarah alimkimbilia huku akilia na kumkumbatia sana mama Angel, basi alimbembeleza pale na kuongea nae mawili matatu, kisha alitakiwa kumlipa yule dereva aliyemleta Sarah,
“Unamdai pesa ngapi?”
“Ni elfu laki moja mama”
“Duh!! Sarah umetokea wapi jamani!! Inaonekana ni mbali sana eeeh!! Ila sio tatizo, twende ndani nikamletee hela yake”
basi mama Angel aliingia ndani na Sarah kisha alitoka na kumpatia yule dereva hela yake na kurudi ndani.
Mama Angel alianza maongezi na Sarah sasa kuhusu alipotoka ila Sarah alikuwa akilia tu,
“Siku nilipomsikia mama akiongea kwenye simu na kusema kuwa wamempiga risasi baba Erick nilijikuta nikiumia sana moyo wangu, kwanini mama kafanya kitu cha namna hii? Ingawa kwenye ile simu alikuwa anasema kuwa hataki iwe vile ilivyokuwa ila ndio ilishatokea tayari”
“Pole sana, yani mama yako sijui huwa anawaza kitu gani, kwakweli akili ya mama yako ina matatizo sana”
“Sijaweza kuendelea kukaa nae, nimeamua kuondoka nyumbani, nitarudi kama akija tu kuomba msamaha mahali hapa”
Ila Sarah alionekana ana mengi sana ya kuzungumza ila muda huo alikuwa na hasira sana kiasi kwamba alikuwa hazungumzi vizuri, basi mama Angel ilibidi amuandalie tu kile chumba ambacho walikuwa wamemuandalia Elly aweze kupumzika mule na aweze kulala kwenye kile chumba.

Erick na Erica waliamua kurudi nyumbani muda huu ila walipanga pamoja mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na kutokutiana kwenye tamaa maana hakuna aliyekuwa akijua kuna tatizo gani kati yao, na pia hawakutaka kuumizana moyo maana kila mmoja kajua ni tatizo gani linamsumbua mwingine.
Erick alimuahidi Erica kuwa atamtafutia zawadi,
“Naomba uikubali zawadi yangu, kesho nitatoka kwenda kule dukani kwetu. Nitakujia na zawadi natumaini utaipenda”
“Hiyo zawadi inamaana ipo tayari au ni kitu gani? Umeiongea tu muda huu au ipo?”
“Hamna, ni kesho ndio nitaitafuta, haipo wala nini ila kesho nitainunua na kuja nayo”
“Haya nimekumbuka kitu ni kuhusu Sarah, akija nyumbani kweli je!”
“Hakuna tatizo Erica, yote nadhani tumemaliza, kwani kuna tatizo? Kumbuka Sarah nae ni ndugu yetu, mama alisema”
“Nakumbuka, halafu Sarah nae alikuwa akikutaka, mweeeeh ukoo una nini huu? Kuna tatizo lazima”
“Ni kweli, halafu Sarah na Elly wakapeana mimba na wote ni ndugu zetu”
“Mmmmh kweli kuna tatizo mahali, ila mimi na wewe isifikie huko”
“Haiwezi kufikia sababu kila kitu tumekiweka wazi baina yenu, ni swala tu la kutafuta tatizo lipo wapi. Ila sijui kwanini wanazuia mahusiano ya kimapenzi baina ya ndugu!”
Erica alicheka sana na kisha kuendelea na mada nyingine, ila aliuliza jambo,
“Ila wana haki ya kuzuia, unajua haileti maana eti, maana mtoto atakuwaje ikiwa wazazi ni ndugu? Hili ni pepo tunatakiwa kulikataa kabisa”
Waliendelea na mazungumzo mengine hadi walipofika nyumbani na walipofika tu walimkuta Sarah maana muda huo alikuwa akila chakula, walimpokea vizuri tu na kumkaribisha vizuri.
Leo Erica hakuwa na tatizo lolote lile kwa Sarah, hata Sarah aliweza kugundua kuwa Erica amebadilika kwa kipindi hiki.
Usiku wa siku hii, Sarah alienda chumbani kwa Erica na kumuomba walale pamoja ingawa anajua kwa siku za nyuma haikuwezekana hiyo kitu ila kwa leo Erica alikubali tu na walilala wote hadi asubuhi bila ya tatizo lolote lile.
Kulipokucha tu, ni Erica ndio alimwambia Sarah,
“Leo si tutaenda Kanisani eeeh!!”
“Aaaah kumbe ni siku ya ibada leo!! Tutaenda basi”
“Hadi hujui kama leo ni Jumapili!! Kweli kuna tatizo kwako”
“Yani kwenye familia yetu hakuna Jumapili wala Ijumaa”
“Kumbe!! Ila nilisikia wewe hupendi Ibada”
“Hapana, ila ni malezi niliyopewa na mama hatuna kawaida ya kwenda Kanisani. Ila mimi sina nguo za kuvaa huko ibadani maana mavazi yangu nayajua mwenyewe”
“Usijali, utavaa za kwangu mbona miili yetu inaendana tu”
Basi waliongea kidogo na kuanza kujiandaa, kisha waliweza kuondoka kwa pamoja na kuelekea huko kwenye ibada.

Erick alipotoka tu, moja kwa moja alienda dukani kwa baba yake ili kuangalia ile biashara ya duka inaendaje, alifika pale na kufanikisha yote ambayo alitakiwa yeye ndio ayafanikishe, kisha alitaka kuondoka ila kabla ya kuondoka alifika Juma mahali pale na kumsalimia kisha kuanza kuongea nae, ambapo Juma alimchukua Erick pembeni na kumuuliza,
“Samahani Erick, yale matunda ya siku ile uliyatoa wapi?”
“Kwanini unaniuliza hivyo? Yalikuwa na tatizo kwani?”
“Hapana ila yamenikumbusha mbali sana, nakumbuka miaka ya nyuma alikuwepo mama yangu ambaye alikuwa akinitengenezea matunda kwa kunichanganyia vile na alisema kuwa kile ni kitu kilichopendwa sana na babu yangu. Kwakweli Erick nazidi kupata ushahidi kuwa wewe ni damu yangu”
“Unahisi nimetengeneza mimi yale matunda?”
“Ndio, niliambiwa kuwa wewe huwa huli kitu hovyo, kwahiyo ninahisi kwa asilimia zote kuwa ni wewe ndiye uliyetengeneza yale matunda”
“Hapana, yale matunda nimepewa na bibi mmoja hivi yupo kule kwenye ofisi ya baba. Labda kama yule bibi ndio mama yako”
“Aaaah kwa bahati mbaya mama yangu alishakufa siku nyingi sana”
“Basi yule bibi utakuwa na undugu nae sababu ni yeye ndio aliyenipa yale matunda, lazi ma atakuwa ndugu yako tu ndiomana umehisi hivyo”
Juma alifikiria kiasi na kusema,
“Unachokisema kinauwezekano ila bado nahisi kuna kitu hapa, kwanini hayo matunda ni wewe ndio unipatie mimi! Nishaenda ofisini kwa baba yako mara nyingi tu, sijawahi kuonana na huyo bibi na hata mara moja hajawahi kuleta matunda hayo mule ofisini kwa baba yako. Lazima kuna kitu ndiomana umeniletea wewe, unaona kama huyo bibi amekupa ila kulikuwa na lengo madhubuti kuniletea ujumbe mimi”
“Ujumbe gani sasa?”
“Kuwa wewe ni damu yangu”
“Unajua unanikumbusha mwanamama mmoja hivi ambaye alinisumbua sana kipindi cha nyuma akidai kuwa mimi ni mtoto wake, yule mama aliniharibu sana kisaikolojia maana mimi nawaamini wazazi wangu kuwa ndio pekee wanaohusika na mimi na si vinginevyo. Nadhani na wewe unataka kuniletea mada mpya, ila unadhani itaniumiza kichwa hiyo? Yani ni hivi uliyoyasema ndio nayaacha hapa hapa dukani, wewe unashindwa kujitafakari, mimi niwe damu yako kwa misingi ipi? Mbona nalelewa kwingine na sio kulelewa na wewe? Msinisumbue jamani, kama una lingine sema lakini maswala ya kusema mimi ni damu yako sitaki kutasikia”
“Sijakwambia kwa ubaya Erick”
“Cha kukusaidia ni kuwa nenda ofisini kwa baba yangu utampata bibi mtengeneza matunda halafu ndio uulizane nae undugu wenu, usinihusishe mimi. Wazazi wangu ni Erick na Erica nimemaliza”
Erick alienda kupanda gari na kuondoka zake, kwakweli Juma alimuangalia bila kummaliza na kuzidi kuona kiburi cha wazi cha mtoto huyo kilivyokuwa.

Leo Sia alivyorudi nyumbani kwake tu, baada ya muda kidogo alitokea mama Sarah na kuanza kuongea nae,
“Wewe Sia umempeleka wapi mwanangu Sarah?”
“Sarah!! Jamani, mtoto mwenyewe sina hata mazoea naye, nimpeleke wapi mie?”
“Unajua huwa nakuangalia sana wewe, ila hujui kuwa mimi ni mtu wa aina gani? Hujui ni kitu gani naweza kufanya kwako”
“Unazungumzia kuhusu nini? Unataka kunitishia maisha?”
“Utishiwe maisha kwa lipi? Wewe ni kiumbe mdogo sana yani hata mtu hawezi kutumia muda mwingi na wewe”
“Sikia nikwambie Manka, leo nakuita kwa jina lako. Mimi ni mbea sana hilo sikatai, katika maisha yangu kitu pekee ninachokiogopa ni umasikini ila sio kifo, kwa kifupi mimi siogopi kufa kwahiyo kama unanitishia maisha umekosea kwa hilo”
“Ninaongea kingine unajibu kingine, kweli huna akili wewe. Haya na huyo Elly yuko wapi? Ushamueleza ukweli kuwa wewe sio mama yake ila ni tamaa zako ndio zilikufanya umbadilishe na mwanao wa kweli?”
Hapo Sia alipunguza sauti kwanza kwani katika kitu ambacho hakukitamani kukiona ni swala la Elly kujua ukweli kuwa yule sio mama yake mzazi, basi alianza kuongea na mama Sarah taratibu,
“nakuomba ndugu yangu tukaongee sehemu nyingine”
“Nini sasa tuongelee sehemu nyingine? Elly, Elly , Elly”
Mama Sarah alianza kuita jina la Elly na baada ya muda tu Elly alitoka ndani, na kusogea pale walipo kisha mama Sarah akamwambia Elly,
“Huyu unayeishi nae sio mama yako mzazi, kwa tamaa zake alikubadilisha na mtoto wake ili mwanae aishi maisha ya kitajiri”
Elly alimuangalia mama yake kwa makini sana huku akiendelea kusikiliza maneno ya mama Sarah.
 
SEHEMU YA 378



Mama Sarah alianza kuita jina la Elly na baada ya muda tu Elly alitoka ndani, na kusogea pale walipo kisha mama Sarah akamwambia Elly,
“Huyu unayeishi nae sio mama yako mzazi, kwa tamaa zake alikubadilisha na mtoto wake ili mwanae aishi maisha ya kitajiri”
Elly alimuangalia mama yake kwa makini sana huku akiendelea kusikiliza maneno ya mama Sarah.
Mama Sarah aliendelea kuongea,
“Najua Elly hujui ukweli, ila ukweli wa mambo ni kuwa huyu unayemuona ni mama yako, huyu unayemuita ni mama yako, sio mama yako mzazi, yani yeye kwa tamaa zake aliamua kukubadilisha wewe na mtoto wake wa halali ili amwanae alelewe kwenye maisha ya kitajiri, na usimuone hivyo mama yako anaumbuka kila siku”
Sia alikuwa ameinama chini huku akilia maana ni aibu sana kwake na hakutaka kitu hiko kiwe wazi kwa Elly kwa namna hiyo ukizingatia ukweli wa kuhusu Elly bado umeuwa ni kitendawili kigumu sana kwake.
Alikuwa akilia huku mama Sarah akiendelea kuongea,
“Huyo mama yako, alikuwa akidhani Erick ndio mtoto aliyembadilisha, yani yale maisha anayoyapata Erick alikuwa anataka mwanae ndio ayapate, muulize imekuwaje? Mambo ya Erick yameishia wapi? Muulize kwa makini akwambie imekuwaje? Huyo mama yako hafai, unamuona anakupenda ila hana cha upendo wowote na wewe alikuwa na maana yake. Kwa leo nimemaliza ila ukitaka ukweli zaidi nitafute, huwa sipendi uongo, siku zote ukweli humweka mtu huru”
Mama Sarah aliondoka zake na kumuacha pale Sia akiwa analia huku Elly akiwa na hasira sana, basi Elly alimfata Sia na kusema,
“Mama, naomba uniambie ukweli. Naomba usinifiche, kipindi kile umezimia sikuelewa kabisa mambo haya, yani sikuelewa kabisa. Nilijua umechanganyikiwa, ila nilikusikia kabisa ukisema kuwa Elly sio mwanangu na Erick sio mwanangu, nahitaji uniambie ukweli mama, kwanini imekuwa hivi? Usinidanganye mama, tafadhari naomba uniambie ukweli mama”
Sia alikuwa akilia tu, huku akiwaza ukweli atakaoenda kusema ni ukweli ambao utamfanya Elly asimsamehe kabisa, ila atafanyaje kama kila kitu kipo wazi mbele yake? Alikuwa akilia huku akisema,
“Elly mwanangu, naomba unisamehe”
“Sio muda wa kuniomba msamaha huu, niambie ukweli. Nahitaji ukweli toka kwenye minywa chako”
“Ni kweli mwanangu kuwa wewe sio mwanangu wa kumzaa”
“Unasemaje mama? Ilikuwaje ukawa na mimi? Ndio hizo tamaa alizozisema huyu mama? Ulitaka mwanao aishi maisha mazuri halafu mimi niishi vibaya?”
“Sikia Elly, sikupanga iwe hivi naomba unisamehe”
“Nimekwambia kuwa huu sio muda wa kuniomba msamaha ila ni muda wa kunielezea kwanini ulinibadilisha?”
“Nililazimishwa Elly”
“Kwa hakika sikupendi, sikupendi kabisa. Siamini kama mama yangu ungenitenda hivi”
Elly aliinuka kwa hasira na kuondoka zake, yani kile kitendo kilimfanya Sia alie sana hata akakumbuka vifo vya wazazi wake, akakumbuka enzi za ujana wake, akakumbuka vitu vingi sana ambavyo vilitokea katika maisha yake, akakumbuka jinsi baba yake alivyokufa na kusema kuwa Erick ndio mwanaume anayepaswa kumuoa yeye, akakumbuka pia mama yake alivyokufa na kusema vilevile, akakumbuka jinsi Erick alivyokuwa kwa Erica, akakumbuka jinsi alivyoshawishika kwenda kwa mganga wa kienyeji, akakumbuka siku aliyompelekea Erick tunda halafu likarushwa nje ya geti, akakumbuka jinsi alivyomkuta Steve akila lile tunda, na jinsi alivyoanza kuishi na Steve hadi kufikia hatua ya kuoana, akakumbuka jinsi alivyoshawishiwa na mzee Jimmy kuhusu kubadili mtoto na jinsi Steve alivyomkimbia kwani mtoto alikuwa haeleweki, jinsi Erick anavyomkataa kila siku. Alijikuta akilia sana na kuona dunia imemuelemea, aliona dunia ni mbaya sana kwa upande wake, yani alilia hadi alilala pale pale nje huku akilia tu.

Yani Elly hakufikiria hata kama muda umeenda sana, alikuwa na mawazo sana, hakuwa na raha ya maisha kabisa, aliona kama kaonewa na maisha alijiuliza maswali mengi sana,
“Sasa mimi wazazi wangu wako wapi?”
Hapo akili ikamtuma kuwa moja kwa moja aende kwa yule mtu ambaye huwa anadai ni baba yake yani aende kwa Derrick maana aliona wazi kuwa akili yake haifanyi kazi kwa muda huo.
Basi alienda moja kwa moja kwa Derrick na kugonga mlango, yani Derrick alitoka huku akishangaa tu kwani hakutegemea kumuona Elly kwa muda ule, basi alimkaribisha na kuanza kuongea nae,
“Karibu Elly, tatizo ni nini kwani?”
Elly alikuwa akilia tu, ikabidi Serrick amkumbatie na kumuuliza kwa karibu kuwa tatizo ni kitu gani,
“Nahitaji kuwajua wazazi wangu, nahitaji kumfahamu mama na baba yangu. Nahitaji kujua mimi ni uzao wa nani?”
“Nyamaza kwanza Elly na tuweze kuongea vizuri”
“Roho inaniuma sana, niliyemtegemea siku zote, niliyemuamini siku zote, niliyempenda kwa moyo wote leo nimegungua kuwa sio mama yangu mzazi, alinibadilisha tu ili sijui mwanae aishi maisha mazuri, nimeumia sana moyo. Mimi sikuwa na haja ya maisha mazuri ila ninahaja ya kutambua wazazi wangu”
“Pole sana Elly, nilijua siku ukitambua hayo utaumia sana”
“Inamaana unajua?”
“Najua sababu najua kuwa wewe ni mwanangu ila sijawahi kuwa na mahusiano na yule mama yako, kwahiyo moja kwa moja nikaelewa kuwa kuna namna imefanyika maana wewe ni mwanangu”
“Imekuwaje sasa? Kwanini imekuwa hivi? Mama yangu mimi ni nani?”
“Sikia nikwambie, mara nyingine unaweza kulaumu kila unayemuona mbele sababu ya kitu kilichotokea, ila tunatakiwa kuyakubali makosa halafu kujifunza kutokana na makosa. Kwa namna moja au nyingine hata mimi pia sijihesabii kuwa baba bora. Kuna wanawake zangu wawili tu ndio ambao nina uhakika walikuwa na mimba zangu, kuna mmoja anaitwa Oliva na mwingine anaitwa Manka, ila kiukweli sikuwa na uwezo wa kulea wote wawili katika ile hali ya mimba zao, ikanifanya nimkatae Oliva, ila Manka nae akanikimbia toka hapo hakuna niliyejua yuko wapi hata walivyojifungua sikuwa najua chochote kile, nilipokutana na mmoja wao nilidai mtoto wangu ila wote waligoma kuzaa na mimi, nilikuwa naumia sana moyo maana naamini kuwa watoto wangu wapo ila wote wanakataa kuzaa na mimi. Ila Mungu mwema akanifahamisha kuwa wewe ni mwanangu kwa njia ya tofauti sana, ile njia ya ugonjwa wangu ilinifanya kwa urahisi zaidi nitambue kuwa wewe ni mwanangu”
“Haya, mama yangu ni nani sasa?”
“Hapo bado nina ukakasi lakini nahisi wazi kuwa mama yako ni Manka”
“Manka? Ndio nani?”
“Yule mnamuita mama Sarah sijui”
“Aaaah hapana, sitaki kusikia, yule hawezi kuwa mama yangu. Sitaki kusikia hiyo habari, yule mama alinitesa sana alinipiga hadi nilipoteza fahamu halafu mnasema ni mama yangu? Hapana sitaki hata kidogo, sitaki yule mwanamke awe mama yangu”
“Nisamehe mimi mwanangu ila huo ndio ukweli”
“Inamaana Sarah ni ndugu yangu?”
“Ndio ni ndugu yako”
“Hapana, sitaki jamani, sitaki kukubali hiko kitu kabisa. Mbona ndio nimezidi kuchanganyikiwa jamani”
“Hebu tulia kwanza Elly, kesho tutajitahidi twende kwa mama yako aliyekulea, kwani najua utakuwa umeondoka kwa hasira sana na yule mama anafahamu vitu vingi sana, hutakiwi kumchukia kiasi hiko. Kweli sio mazi wako ila ni mlezi wako”
Elly aliitikia tu kwa shingo upande, basi Derrick aliandaa mazingira ili waweze kulala na Elly kwa siku hiyo maana Elly alionekana kutokuwa sawa kabisa.

Leo wakati Erica kalala, basi Sarah alimfata tena na kumtaka walale pamoja kisha walianza kuongea mambo mbalimbali ambapo Erica alimuuliza Sarah kuwa ilikuwaje hadi akajikuta akilala na Elly,
“Mmmh sijui ni nini, itakuwa ni huu ujana halafu hisia nazo zilinishika sana”
“Kivipi?”
“Sikia, mimi nilikuwa nampenda sana Erick kabla sijajua kuwa Erick ni ndugu yangu, nilitamani siku moja niweze kulala nae, ndio nikaamua kulala na Elly”
“Ilikuwaje kwanza niambie”
“Elly alikuwa akikataa kabisa jambo hilo, ila nilimuoshesha video za mapenzi”
“Kheee video za mapenzi ndio zipi hizo?”
“Zipo kwenye simu yangu, yani mwanaume na mwanamke wanavyofanya, tulipoangalia zile video basi tulijikuta tukifanya. Hujawahi kuziona?”
“Nizionee wapi?Mimi sina simu”
“Basi nitakuonyesha, kwenye simu yangu zipo hizo video, yani ukiangalia lazima utajikuta ukiingiwa na tamaa na ndivyo ilivyokuwa mimi na Elly. Unataka kuziona?”
“Mmmh naogopa kuziona, usinionyeshe kwa leo”
“Sio mbaya lakini, zingine mbaya ila kwenye simu ninazo nzuri yani ukiziona lazima uzipende, Halafu shule si zimefungwa? Ngoja nikuonyeshe kwa hakika utazipenda, ni nzuri sana. Basi nikajikuta hivyo. Ila unafikiri najutia kufanya kile kitendo na Elly?”
“Kheee hujutii?”
“Ndio sijuitii maana mimi ni mwanamke na Elly ni mwanaume”
“Lakini Elly pia ni ndugu yetu”
“Muda mwingine naumia sana roho kila nikifikiria hilo jambo, ila sasa lilishatokea nitafanyaje?”
“Ukimuona Elly je utafanya nae tena?”
“Hapana, kwasasa siwezi hata kumsumbua siwezi maana Elly ni ndugu yangu”
Kisha Sarah alichukua simu yake na kuanza kumfungulia Erica zile video, ila wakati video inaanza kuonyesha tu mule ndani kwa Erica aliingia mama yao,
“Kheee nilijua mmeshalala kumbe bado?”
Erica aliweka ile simu pembeni na kuanza kumsikiliza mama yao,
“Aaaah tulikuwa tunaongea mama”
“Sawa, nilitaka kuongea kidogo nawe Sarah. Maana kesho ni siku ya shule, inakuwaje kuhusu shule, au nikaongee na walimu?”
“Hapana mama, shule mbona tumefunga”
“Kheee kumbe mshafunga! Sina khabari mimi, kwahiyo na nyie wakina Erica mmefunga?”
“Ndio mama”
Mama Angel alimuona kama Erica akikazana kuficha ile simu, na huwa anajua wazi kama mwanae anamficha kitu ni lazima sio kizuri basi alimuuliza kwa ukali kwani anajua Erica ni muoga kwahiyo akiulizwa kwa ukali lazima aseme ukweli,
“Unaficha nini wewe eeeh! Hebu nionyeshe”
Erica alitoa ile simu na kumpa mama yake, kisha mama Angel akaamuuliza Sarah,
“Hii ni simu yako eeeh!!”
“Ndio”
“Simu kubwa hivi ndio ulikuwa unatumia wewe!”
“Ndio, mama alisema ndio nzuri”
“Haya mlikuwa mnafanya nini?”
Erica akajibu,
“Sarah alitaka kunionyesha video za mapenzi”
Mama Angel alishtuka sana na kumuangalia Sarah kisha akamwambia amuonyeshe yeye hizo video, yani Sarah alizifungua kwa uoga kisha mama Angel akawaambia,
“Haya laleni hapo, kwa leo Sarah naomba niende na hii simu yako”
Sarah hakubisha wala nini na kufanya mama Angel atoke mule ndani kwa watoto huku akisikitika sana.
Sarah akamwambia Erica,
“Kwanini umemwambia ukweli? Atachukia sana halafu atanichukia mimi. Zile video ni za tabia mbaya, huwa wakubwa wengi hawapendi kujua kama watoto wanaangalia”
“Sikuwa na cha kufanya, tulale tu Sarah”
Yani Sarah alikubali kulala huku akiwa na mawazo sana na ile simu yake ambayo mama Angel ameichukua.

Moja kwa moja mama Angel alienda na ile simu hadi kwa mume wake, maana ulikuwa ni muda wa kulala na mumewe alikuwa kashalala ila alimuamsha na kuanza kumuonyesha,
“Hebu ona video ambazo watoto wanakazana kuziangalia”
Baba Angel na mama Angel waliangalia kwa kifupi tu na kusikitika kisha mama Angel akasema,
“Huwa naonekana mshamba sana kwa kutokumkabidhi mtoto wangu simu, ila haya ndio mambo ninayoyaepuka. Kuna umri wa kumpa mtoto simu, haya Sarah akili zake hadi zimeraruka sababu ya mambo kama haya, hebu fikiria mtoto akiangalia mavideo haya kwa siku nzima hiyo akili yake inakuwaje? Lazima atakuwa anawaza ujinga na ndiomana hata kaweza kumlaghai Elly kuwa nae kimapenzi”
“Nimesikitika sana, sikufikiria kama mtoto kama Sarah anaweza kuwa na video hizi kwenye simu”
“Yani mimi nilihisi hata damu kuniruka wakati wananionyesha, yani ndio nimewakuta wanataka kuonyeshana na Erica huu ujinga. Mtoto mdogo kama Sarah unampa hii simu kubwa ya nini? Haya ndio madhara yake, unahitaji kuwasiliana nae tu, kwani simu za mawasiliano tu hazipo? Napo ni tatizo maana hawa watoto kushawishika ni rahisi sana. Hata kama akiwa anawasiliana na wewe, basi mzazi jitahidi usiku uwe unachukua ile simu ya mwanao na kuikagua na ikiwezekana uwe unamkabidhi kwa muda unaoona unamfaaa. Watoto wetu hawa wana akili mbovu sana. Ndio utakuta wengine hata kusoma hawasomi muda wote wapo kwenye mitandao ya kijamii, yani mtoto mmoja anakuwa na akaunti kibao kwenye mitandao, ukifatilia yupo kidato cha kwanza, cha pili sijui cha tatu au cha nne, mwingine utakuta ndio yupo shule ya msingi kabisa, halafu mzazi hata hushtuki jamani dah!! Haya mambo haya, mtoto aharibike kwa bahati mbaya ila sio kwa makusudi sababu mzazi umeshindwa kumuangalia vyema. Malezi ya Manka kwa huyu mtoto yalilenga kumuhatribu kwa asilimia zote, nimeumia sana”
“Basi jitahidi kukaa nae na kumuelewesha, naona Sarah ni mtoto muelewa sana, nina uhakika atakuelewa tu. Hizi video sio nzuri kwake na zina muharibu ubongo wake, ataacha kufikiria ya maana atakazana kufikiria watu wanavyofanya humu”
Kwakweli baba Angel na mama Angel walisikitika sana, ila mama Angel alipanga kuongea vizuri sana na Sarah kwa kesho yake ili aweze kujaribu kumuweka kwenye mstari.
 
SEHEMU YA 380


Mama Angel alipoingia chumbani kwake, alikuta mume wake ameshalala, ila alimuamsha ili kumpa ile habari ya dokta Jimmy, alimueleza kuhusu kumuona kwake dokta Jimmy na vile alivyoongea na Vaileth kuhusu dokta Jimmy,
“Kumbe ni kitambo kahamia huko eeeh!!”
“Ndio inavyoonyesha hivyo, ni kitambo yupo kule. Wanafahamu hadi watoto wake”
“Sasa hiyo ni vizuri tumefahamu anapoishi, kweli nimeamini katika maisha kila kitu kina sababu, hakuna kinachotendeka kwa bahati mbaya, yani kila kitu kinasababu tu. Mmeenda huko kwakina Vaileth tumeweza kujua mtu tuliyemtafuta kwa muda kumbe yupo anaishi huko, basi hiyo ni rahisi kwetu. Safari yenu haikuishia kwenye mahari tu, bali imezaa na matunda mengine”
“Dada Bite akaniambia ni kheri tuwasiliane na mama yako maana ndio alisema atalifatilia jambo hili”
“Hapo sawa, tutawasiliana nae tu na yeye atakuwa kapata mwanga, najua mama anatamani sana kujua ni kitu gani kilikuwa kikifanywa na mzee Jimmy”
Ila baba Angel na mama Angel walifurahi kupafahamu mahali anapopatikana dokta Jimmy, kisha baba Angel alimuuliza mkewe kuhusu mipango ya harusi,
“Nilitaka Junior akichukuliwa ni moja kwa moja Kanisani kufunga ndoa”
“Aaaah mke wangu, sikia Junior tutamchukua siku moja kabla, tuongee nae hapa tumkanye halafu kesho yake ndio atafunga ndoa. Uende kumchukua siku hiyo hiyo ukute lile jimama lake lishamnyakua hata tusijue pa kuanzia hapo!! Yule tutamchukua tumkanye itoshavyo halafu kesho yake ndio ndoa inafanyika, yani hakuna kumpa uhuru wa kuaga marafiki wala wakina nani, ni moja kwa moja anaingia kwenye ndoa, bila kufanya hivi yule mtoto atatukanyaga hadi kichwani”
Mama Angel aliona sawa kabisa kuhusu swala hilo kwani kwa kiasi kikubwa sana alikuwa amechoshwa na matendo ya huyu kijana.
Kulipokucha tu, leo baba Angel alitoka ila mama Angel alinaki kwani aliona ni vyema kwa siku hii akipumzika nyumbani ukizingatia siku karibia zote kashafanya mizunguko mingi sana, kwahiyo aliona ni vyema akiitumia siku hii kupumzika tu.
Ndipo alipopigiwa simu na Derrick na kupewa ile taarifa kuwa Elly ameshaujua ukweli,
“Kwahiyo mama yake Elly ni nani?”
“Ni Manka, si nilishakwambia”
“Ila Manka, ana mtoto wa kuitwa Sarah, inamaana Sarah sio mtoto wa Manka au Sarah na Elly ni mapacha?”
“Mimi sijui ila ninachojua ni kuwa Elly ni mtoto wa Manka ingawa Elly hamtaki Manka kabisa nasikia Manka alimpiga sana Elly hadi Elly akalazwa, basi Elly hamtaki kabisa Manka”
“Duh!! Kumbe kuna makubwa”
“Ndio, Elly kaujua ukweli ila anasema ni bora aendelee kuwa karibu na mama aliyemzoea kuliko kuwa karibu na Manka”
Mama Angel alisikitika kiasi, kisha aliagana na Derrick na kuendelea na shughuli zake zingine.

Mama Angel akiwa ametulia kwa muda huu, ndipo Sarah anaamua kumfata ili aongee nae kuhusu simu yake maana hakumrudishia toka ile siku aliyoichukua,
“Mama, samahani hujanirudishia ile simu hadi leo”
“Oooh nimekumbuka, hebu tuongee kwanza”
Mama Angel aliinuka na kumuongoza Sarah hadi kwenye sebule yao nyingine na kuanza kuongea nae, kwanza mama Angel alimwambia,
“Naomba kwa muda huu tuongee kama marafiki halafu ndio tutakuja kuongea kama mama na mtoto. Upo tayari kuwa rafiki yangu kwa muda huu?”
“Nipo tayari ndio”
“Haya rafiki, naomba uniambie ni kitu gani unajihisi ukiangalia zile video? Kumbuka mimi ni rafiki yako, kuwa huru usimdanganye rafiki yako eeeh!”
Sarah akapumua kidogo na kusema,
“Mimi napenda tu halafu huwa najihisi raha kuziangalia”
“Raha gani ambayo huwa unahihisi wewe?”
“Sijui, basi tu najihisi raha”
“Kwa mara ya kwanza uliona wapi hizo video?”
“Kwenye simu ya mama”
Mama Angel akapumua kidogo na kumuuliza tena Sarah,
“Kwahiyo mama yako kwenye simu yake ndio alikuwa na video za aina hiyo?”
“Ndio tena zilikuwa nyingi tu, nilikuwa namuomba mama simu yake nicheze game halafu nikikuta hizo video naanza kuangalia. Sababu ya kumuomba mara kwa mara nicheze game ndio akaamua kuninunulia simu yangu”
“Eeeh na kwenye simu yako ulizipataje?”
“Sasa mama alipochukua simu yake na kuninunulia simu, ndipo nilipojiunga na mitandao ya kijamii, siku hiyo nikiwa naperuzi instagram niliona ukitaka video za kikubwa nifollow, nikamfollow, nikakuta kuna mahali kaweka namba tulipie halafu anatuunga kwenye group la kuona video za kikubwa, basi nikajiunga humo na humo ndio nikagundua sehemu nyingi zinapopatikana hizi video”
Mama Angel alisikitika kiasi na kumuuliza tena,
“Hebu niambie ukweli Sarah, lazima hizi video ndio zilifanya ukalala na Elly, uongo?”
“Ni kweli, kila nilipoziangalia nilitamani sana kujaribu kufanya kile kinachofanywa ila sikujua kama naweza kujaribu na nani, ndipo mama alipomleta Elly niliona ni vyema kujaribu nae, nilimuonyesha hizo video akapenda basi tukajikuta tunafanya”
Mama Angel alipumua na kuanza kumfundisha Sarah sasa ili awe mtoto mzuri na aweze kurudi kwenye maadili,
“Najua ni ngumu sana kukuelewesha, ila mimi nitajitahidi kukuelewesha kama mwanangu. Sarah wewe bado mdogo, hapo ulipo una ndoto nyingi sana za maisha, sio ndoto za kutazama haya mavideo ya ngono hakuna kitu chochote kitakachokuwa msaada kwako kwa kutazama hizi video zaidi ya kuathirika kisaikolojia tu, kwamba ukizikosa uone kama kuna kitu muhimu sana kimepungua kwako katika maisha. Mimi nitakuwa sambamba na wewe Sarah kuhakikisha kuwa unarudi kwenye mstari, najua wewe ni mtoto mzuri, bado hujawa katika kiwango cha kuropoka na kujibu watu vibaya, kwahiyo tutaenda pamoja tu. Kwasasa naomba uniachie simu yako, nakuomba mwanangu. Halafu kadri ninavyokufundisha ndivyo nitakavyokuja kukuachia simu, kuwa na simu sio mbaya ila ubaya ni kile unachofanya na simu, mbona kuna mambo mengi tu ya kujifunza hata humo kwenye mitandao ya kijamii? Unaweza kujifunza mapishi, afya, kilimo, ujasiliamali yani kuna vitu vingi tu vya kujifunza na vyenye manufaa kwako. Vingine sio muhimu sana kwasababu vipo kwetu na vitakuja kwetu kwa hali ya uhalisia, kwahiyo mwanangu nitajitahidi walau kila siku nipate muda wa kuzungumza na wewe. Ila naamini hujakwazika?”
“Hapana sijakwazika”
Sarah alikuwa akimpenda sana huyu mama, alikuwa akipenda sana jinsi huyu mama alivyoongea kwa upendo alitamani hata siku itokee kuwa kalala na kuamka na kuambiwa kuwa huyu mama ndiye mama yake mzazi, yani alijikuta akimpenda sana na kumsikiliza kwa kila kitu alichokuwa akimfundisha.

Leo Erick alipotoka tu kiwandani aliwasiliana na baba yake na moja kwa moja baba yake alimwambia kuwa aende ofisini kwake, kwahiyo Erick alienda ofisini kwa baba yake, na alipoingia pale walianza kujadiliana kuhusu faili lile ambalo alilikuta kuwa lina makosa.
Muda kidogo alifika yule bibi wa matunda mule ofisini na kuwasalimia kisha kuanza kuongea nao,
“Nawaona leo baba na mwana, yani hadi raha”
Baba Angel alitabasamu tu na kumkaribisha huyu bibi, kisha huyu bibi akasema,
“Yani boss Erick, huyu kijana wako kafanana sana na binti yangu tena sana”
“Kheee, duniani wawili wawili”
Muda kidogo alifika Juma yani rafiki wa baba Angel pale ofisini, ni hapohapo Erick alipomwambia yule bibi,
“Mwanao mwingine huyo hapo”
Alikuwa akimuonyesha Juma kwa yule bibi, basi Juma na yule bibi waliangaliana kwa muda kiasi kisha wakachukuzana na yule bibi nje kwaajili ya maongezi, basi baba Angel alimuangalia mwanae na kumuuliza,
“Imekuwaje umemwambia huyu rafiki yangu kuwa yule ni mama yake?”
“Kuna siku nimekuja hapa, akaja huyu bibi na kukazana kuwa nimefanana sana na mwanae sijui niwe mjukuu wake, aliongea sana, basi akanipa na matunda ila sikula. Nilipoenda dukani nikakutana na huyu baba ambaye aliyataka yale matunda na kukazana kusema kuwa kweli mimi ni damu yake. Nadhani sijakwambia baba, huyu huwa anasema mimi ni damu yake. Alikula yale matunda na kukazana kusema mimi ni damu yake, maana yale matunda ndivyo ambavyo babuyake alikuwa anapenda. Basi leo ndio akutane na mama yake”
“Dah! Wewe mwanangu una balaa, duh sikufikiria hiko kitu. Ila nitamuuliza huyu rafiki yangu, kwanini anasema kuwa wewe ni damu yake ana maana gani?Sijaongea nae toka kipindi cha kukupeleka sijui kwenye kaburi la babu yake, ila nitaongea nae tu. Ngoja arudi”
Ila mpaka jioni wanatoka, Juma hakurudi tena pale ofisini. Ikabidi tu waondoke na kurudi nyumbani kwao.
Walipofika nyumbani, leo baba Angel aliongea na mke wake kuhusu swala la Juma na kuhusu Erick,
“Ila hawa watu wana matatizo gani lakini! Kamaliza Sia, kaanza Juma, hivi nae alibeba mimba kuzaa au kitu gani?”
“Usinichekeshe mke wangu jamani, hata usiumie kichwa na hawa watu wala nini, sisi tufikirie mambo yetu ya maendeleo tu. Nitajua mimi, nitaongea tu na Juma hakuna tatizo”
Basi walimaliza yale maongezi na kuendelea na mambo mengine.

Leo, mama Angel mapema kabisa alichukuzana na Vaileth ili kwenda kujaribu gauni la harusi kama ambavyo alipanga nae, kwahiyo kwa muda ule mchache walimuacha mtoto kwa Erica.
Basi mama Angel alipokuwa na Vaileth wakichagua nguo ya harusi na kujaribisha ndipo alipokutana na rafiki yake Dora,
“Kheee kwenye duka la nguo za harusi tena! Mara ya pili au?”
“Hapana, ni binti yangu wa kazi ndio anaolewa”
“Kheee hongera sana, umeishi vizuri na binti wa kazi hadi anaolewa nyumbani kwako! Hongera sana, harusi lini sasa?”
“Ni alhamisi hii ndio harusi yenyewe, karibu sana”
“Asante sana, nitakuja basi. Sijui nije nyumbani kwako au kanisani?”
Mama Angel alimuelekeza Kanisa hilo lilipo ili moja kwa moja afike hapo kanisani,
“Muda ni saa tisa alasiri”
“Basi nitakuja, yani nisingekutana na wewe najua haya mambo yangekuwa kimya kimya, loh mambo yako Erica jamani loh!”
Basi walicheka tu pale huku mama Angel akimuomba msamaha kidogo rafiki yake maana kwa kipindi hiko alikuwa na mambo mengi sana kwahiyo alisahau kuwapa taarifa rafiki zake wengine hawa wakati kulikuwa na umuhimu sana wa kumwambia mtu kama Dora.

Siku ya leo baba Angel alipokuwa ofisini kuna simu iliingia kwake, alipoiangalia ilikuwa ni namba ya mwalimu wa Angel, basi aliipokea simu ile na kuanza kuongea nayo,
“Ndio, mwalimu niambie”
“Wakina Angel wanamaliza mtihani leo, alikuwa anauloza utakuja kumchukua leo?”
“Aaaah atakuja bibi yake kumfata kesho maana mimi bado nipo huku mjini na sikujua kama mitihani wanamaliza leo. Kwani na mambo ya mahafali si mlisema tusubiri”
“Ndio, yani lengo la binti yako ni kuwa anataka kusherekea na wenzie leo jioni kumaliza mtihani, sasa kuna mchango wamekubaliana kutoa ndiomana aliniuliza kuwa nimuulizie kwako ili ajue kama atasherekea na wenzie”
“Kwani huo mchango ni pesa ngapi?”
“Wamekubaliana kuchangia elfu hamsini kila mmoja”
“Nakutumia mwalimu, halafu mwambia bibi yake atakuja kesho kumfata”
“Sawa”
Muda kidogo, baba Angel alimtumia huyu mwalimu wa Angel hiyo hela aliyoambiwa kwani huyu baba huwa hapendi mtoto wake asononeke.
Baada ya muda kidogo, baba Angel akakumbuka kitu kuwa lazima Junior nae ndio anamaliza mitihani siku hiyo, basi akawaza kuwa aende kumuwahi huko shule maana alihofia pia kwa Junior kuchukuliwa na Linah.
Baba Angel alimaliza kazi zake mapema kabisa na kuondoka pale kuelekea shuleni kwakina Junior, moja kwa moja alienda kwa mwalimu kuongea nae,
“Madam, naomba Junior akimaliza mitihani tu niondoke nae”
“Kheee huyu Junior leo jamani, na mamake mdogo nae kaja kumfata kasema akimaliza mitihani tu anamuhitaji aondoke nae”
“Mamake mdogo yupi huyo?”
Yule madam alimuonyesha baba Angel gari ambalo alikuwepo huyo aliyekuwa anamsubiria Junior, basi baba Angel alienda hadi kwenye lile gari, alishangaa sana kumuona Linah ndio ambaye alikuwa akimsubiria Junior, basi baba Angel alimshtua na kumwambia,
“Linah jamani, umeshindwa hata kuwa na aibu hata kwa mbali? Haya Junior nani yako?”
Linah hakujibu kitu ila aliona aibu, basi alifunga vioo vya gari lake na kuondoka zake.
Baba Angel alimsubiri Junior pale pale shuleni kwao, na alipomaliza tu mitihani akamchukua na kuondoka nae huku akimsema sana kwa vitendo anavyovifanya,
“Yani Junior kweli unaacha masoma na kuondoka na yule mama? Dah basi tu, tutaongea nyumbani”
Moja kwa moja baba Angel alienda nyumbani muda huo na Junior.
 
SEHEMU YA 381

Walivyofika nyumbani tu, mama Angel alifurahi sana kwa baba Angel kurudi na Junior, aliinuka na kumshika mkono Junior,
“Shikamoo mamdogo”
“Twende ukachukue shikamoo yako na wewe ili kama ni chakula uweze kushiba muda huu”
Mama Angel alimshika mkono Junior hadi chumbani kwa Vaileth ambapo Vaileth alikuwa akinyonyesha mtoto yani Junior alibaki kistaajabu maana hakufikiria kile kitu kabisa, basi mama Angel alimkalisha chini Junior na kumwambia,
“Umemuona mtoto wako?”
Junior alizidi kushangaa huku akitetemeka, basi mama Angel akamwambia tena,
“Unatetemeka nini sasa? Kwani ulipopanda mahindi ulitegemea kuvuna nini? Ila hongera kwa kuitwa baba na ujiandae kwa harusi”
Hapo ndio Junior akashtuka kiasi,
“Harusi!!”
“Ndio harusi, wewe unaenda kumuoa Vai. Usifikirie ni siku nyingi bado, ila ni kesho kutwa hapo”
“Kheee sijawahi kuona harusi ya hivyo”
“Ndio uione sasa, nenda kaoge uje huku kumshika mtoto na kuongea na mwenzio. Nimemaliza, jiandae sasa”
Yani Junior alishindwa hata cha kusema, na kuinuka kama alivyoambiwa kuwa akaoge kwanza.

Junior alioga huku akijifikiria sana, aliona kama akili yake haisomi vile yani hakuna alichokuwa anaelewa hata kimoja.
Alipomaliza, moja kwa moja alienda chumbani kwa Vaileth maana alikuwa na maswali mengi sana na hakusema asubirie kuvizia usiku lazima tu afanye vile inavyotakiwa.
Basi alienda na kumkuta Vaileth akiwa anakunja nguo za mtoto, alifika pale na kupumua kidogo kisha alimwomba msamaha Vaileth kwani alijua wazi kuwa anapaswa kumwomba msamaha,
“Naomba unisamehe Vai, nisamehe kwa yote. Nisamehe kwa kushawishi kutoa mimba, nisamehe kwa kukata mawasiliano na wewe, naomba unisamehe sana. Kwakweli nimefanya hiki kitu bila ya kujifikiria, nisamehe sana Vaileth”
“Nimeshakusamehe”
“Naomba nimshike mtoto”
Vaileth alimtoa mtoto kitandani na kumpa Junior huku akimwambia,
“Anaitwa Joseph”
“Oooh jina la babu, kapewa na nani?”
“Bibi yake mdogo”
“Aaaah halafu naomba unieleweshe hayo mambo ya harusi kesho kutwa”
“Ni hivi mama amwshaenda kujitambulisha kwetu, kashatoa mahari na walishaandikisha ndoa. Kwahiyo kesho kutwa tunaoana”
“Ila kwanini wamefanya hivyo bila ya kunishirikisha muhusika?”
“Kwani hutaki kunioa Junior?”
“Hapana, nina lengo jema tu ila kwanini hawajanishirikisha? Hapo ndio walipokosea ila sijachukia”
Kisha Vaileth akamtolea gauni la harusi ambalo lilikuwa kabatini na kumfanya Junior aamini wazi kuwa ndoa inafungwa kweli, alitabasamu tu ila alikuwa na mawazo mengi sana.
Baada ya hapo Junior alirudi chumbani kwake, ila muda ule ule alitumiwa ujumbe na Linah,
“Junior mpenzi wangu, nilifika kukuchukua leo kama ahadi yetu ilivyokuwa kuwa ukimaliza mitihani tu basi utakuja kukaa kwangu mwezi mzima. Babako mdogo kajifanya kuja kuniwahi hapo shuleni, kwahiyo Junior fanya kitu tuonane”
Junior alisoma ule ujumbe mara mbilimbili na bila ya kujibu chochote, kisha akaamua kulala tu.

Leo mapema kabisa, Sia akiwa nyumbani kwake alifatwa tena na mama Sarah ambapo mama huyu alianza kuongea nae,
“Mwanangu yuko wapi?”
“Hivi kweli kabisa unatoka huko na kuja kumuulizia Sarah hapa, una akili kweli wewe?? Unaamini kabisa kuwa Sarah ni mwanao?”
“Ndio, Sarah ni mwanangu”
“Pole sana, ulihisi mchezo ule mzee Jimmy kanichezea peke yangu, kwa taarifa yako mtoto wako ni Elly, wala Sarah sio mwanao”
“Haiwezekani”
“Haiwezekani nini? Nenda kapime huko, kapime na Elly na Sarah halafu mtafutie Sarah wazazi wake kama mimi nilivyotafuta wazazi wa Elly na kugundua kuwa mmoja wapo ni wewe usiyejielewa”
“Unaongea au unatapika? Hujui kama mimi nilijitolea kumsomesha mtoto wangu?”
“Umejitolea kumsomesha mtoto wako pia maana Elly ni damu yako, nilitaka nishangae yani mzee Jimmy akuache tu na amani wewe bila ya kukufanyia mchezo!!! Kitu hiko hakiwezekani, pole sana, huyo ndio mzee Jimmy bhana”
Sia alikuwa akicheka tu ila jambo lile lilimpa mawazo sana mama Sarah kiasi kwamba hakuweza tena kuendelea kuongea na Sia maana muda huo huo aliamua kuondoka zake.

Wakati baba Angel kaenda mjini na Junior, mama Angel aliwaita wakina Erica na kuwapa taarifa juu ya harusi ya kesho. Kidogo ilikuwa ni taarifa ya kushtukiza maana hawakujua kama kuna mipango ya harusi, basi Erica alimlaumu sana mama yake kwa kutowaambia mapema,
“Ila mama umefanya vibaya, kwanini hujatuambia mapema tufanye maandalizi?”
“Maandalizi ya nini sasa Erica? Ni harusi ya haraka hii, wala hakuna sherehe wala nini, tutapika tu hapa nyumbani na kula kama familia. Sherehe kubwa itaandaliwa na itafanyika kijijini kwakina Vaileth, huko ndio tutajipanga ila sio kwasasa”
“Haya, na kuhusu hiyo kesho ndio tumejipangaje? Chakula gani tutapika, vitu gani vitakuwepo?”
“Tutapika tu pilau, na vinywaji vitakuwepo maana baba atapita kuvichukua na Junior, halafu Erick nae nilimuagiza kuna vitu apitie kwahiyo akitoka tu kiwandani atapitia kwenda kuvichukua”
“Mama jamani, tupike na tambi za nyama ya kusaga”
“Ila tambi sijanunua labda nikuagize ukanunue hapo madukani”
Basi mama Angel alimuagiza Erica, na muda mfupi tu Erica alitoka kwenda kununua tambi alizoagizwa.
Wakati Erica anarudi, alikutana na Emmanuel, basi alimsalimia pale na kumualika kwenye harusi ya kesho yake kwani aliona kuwa na wao wana umuhimu wa kwenda.
“Jitahidi uje na Emmanah, tuanzie Kanisani”
“Sawa ingawa gafla mno”
“Hata sisi wenyewe tumeshtukizwa tu, naomba mjitahidi”
Aliagana nae na kurudi nyumbani.
Siku hii usiku walikuwa wakifanya maandalizi tu ya harusi ya kesho, walicheza na kufurahi pamoja.

Siku ya harusi ilifika, kwakweli Vaileth alipendeza sana ingawa ilikuwa ni harusi ya fasta fasta ila alipendeza sana.
Familia yote ya mama Angel ilikuwepo hapo kushuhudia hiyo harusi, basi taratibu zote zikafanyika kama kawaida.
Wakati mchungaji aliposema,
“Kuna mtu yeyote mwenye pingamizi hapa?”
Sauti ikasikika toka mlangoni,
“Mimi hapa nina pingamizi”
Mtu huyu alikuwa akija mbele na watu wote waligeuka kumuangalia, kwakweli mama Angel ndio alishangaa sana kwani huyu mtu alikuwa ni Linah.

Wakati mchungaji aliposema,
“Kuna mtu yeyote mwenye pingamizi hapa?”
Sauti ikasikika toka mlangoni,
“Mimi hapa nina pingamizi”
Mtu huyu alikuwa akija mbele na watu wote waligeuka kumuangalia, kwakweli mama Angel ndio alishangaa sana kwani huyu mtu alikuwa ni Linah.
Kila mtu alikuwa akimshangaa kwa waliomfahamu na wasiomfahamu, ila Linah hakuona aibu na kusogea moja kwa moja mbele hadi kwa mchungaji, kwakweli Junior alibaki kushangaa tu hata mtu aliyempa taarifa Linah hakumtambua kwakweli, basi mchungaji akamuuliza,
“Una pingamizi gani mama kwa hawa mahurusi”
“Haiwezekani ndoa ikafungwa maana mimi nina mimba yake”
“Mimba ya nani huyo? Unamsema huyu kijana?”
“Ndio, huyo bwana harusi mimi nina mimba yake”
Kila mmoja alibaki kushangaa, baba Angel alisogea mbele pia hata mama Angel na wakubwa wengine huku baba Angel akimlazimisha Linah kutoa nje maana pale anajiaibisha mwenyewe tu, ila Linah aliongea kwa ukali,
“Na wewe Erick naomba uniache, tena niache kabisa. Huyu Junior ataoa vipi wakati mimi na yeye tumeishi nae kama mke na mume kwa kipindi chote hiki na hapa nilipo nina mimba yake”
“Hivi Linah unaijua sheria wewe?”
“Sheria gani? Sheria ya mimi kupewa mimba halafu nifurahie? Siijui”
Mchungaji aliamua kuhairisha kwanza ili wale wenye mashtaka yao wakayamalize ofisini, na alitoa nusu saa tu kuwa kama haitawezekana kumaliza hiyo tofauti basi ndoa haitafuingwa na itahairishwa maana kunatakuwa na kasoro, kwakweli Vaileth aliinama akilia ni mama Angel ndio alimchukua pembeni akimbembeleza huku baba Angel akimwambia Erick akae na Junior wakati yeye anaenda ofisini ili huyo mwanamke aache hizo lawama zake.
Basi mama Angel alikuwa akimbembeleza Vaileth,
“Ni mkosi gani huu nilionao mama? Kwani kosa langu mimi ni nini? Nimekosea wapi nijue jamani? Kwanini imekuwa hivi”
“Hakuna ulipokosea, achana na huyu mtu mzima asiyekuwa na akili”
Kisha mama Angel alimuita mama Junior akae na Vaileth ili yeye akajaribu kuzungumza ofisini huko na wajue jinsi ya kufikia muafaka, wengine walibaki tu wakijadiliana na kushangaa kwani yale mambo yalikuwa ni ya ajabu halafu ni ya aibu kubwa sana.

Mama Angel alienda ambapo mumewe alikuwa akizungumza na Linah huku akitamani hata kumzaba vibao maana inaonyesha Linah alikuwa akimjibu baba Angel majibu mabaya,
“Sikia Erick huna cha kunibabaisha ujue, kwahiyo utaenda kufungua mashataka kuwa Linah alikuwa anambaka Junior? Toka lini mwanamke akambaka mwanaume? Hiyo kitu inapatikana wapi? Huyo Junior mtoto? Kashavuka miaka kumi na nane inamaana kuwa ni mtu mzima ndiomana hata nyie mmepata nguvu ya kuja kumfungisha ndoa. Sasa na mimi haki yangu iko wapi na niliishi na Junior kinyumba hadi kanipa mimba?”
“Yani wewe Linah unaongea utadhani ni mtu wa wapi sijui, Junior ni mdogo sana kwako. Junior ni sawa tu na mtoto wako hata wa tano huko, hivi huoni hata mchungaji kakushangaa kusema unapinga ndoa kisa una mimba? Mtu gani mwenye mimba ya mtoto wewe?”
“Uliona wapi mtoto akaweza kumpatia mwanamke ujauzito? Junior ni mwanaume aliyebalehe na ndiomana kanipatia mimi mimba. Na huo uwezo wa kumbaka Junior mimi nautoa wapi? Mnajijua kabisa wanaume mlivyo kuwa hakuna kinachowezekana bila ya mashine zenu kusimama, haya mimi nitaweza wapi kufanya hilo kama sio Junior kwa mapenzi yake na tamaa zake, kwanza Junior amekula vingi sana vyangu, lazima anioe, mimi ni mtu mzima ndio ila sina mume na mume wangu ni Junior. Kwahiyo msinichanganye kabisa, angejiona mtoto basi asingekuwa na mimi”
“Si kwasababu ulikuwa ukimlazimisha”
“Msinichekeshe mimi, toka lini mwanaume akalazimishwa? Msitake niwatusi hapa”
Linah aligoma kabisa kumaliza ule utata, basi Mchungaji aliwaita ofisini kwake na kuanza kuongea nao tena,
“Bado dakika tano, hamjafika muafaka?”
Linah alijibu kwa kujiamini kabisa,
“Hatuwezi kufika muafaka, Mchungaji najua kuwa wewe ni mtumishi wa Mungu, angalia jambo hili kwa undani. Huyo Junior nimemsomesha na kumlea kama mume wangu mtarajiwa, na tulipanga kuoana kabisa hadi mimba nikabeba sababu najua mume yupo. Mchungaji unataka nitoe mimba yani niue kiumbe cha Mungu?”
Mchungaji alisikitika na kusema,
“Unajua siku hizi mna mambo ya ajabu sana, yani kuna vitu vya ajabu ambavyo mtu huwezi hata kufikiria kama vinaweza kutokea. Ngoja nikuulize kwanza, una miaka mingapi mama”
“Miaka yangu ya nini Mchungaji? Mimi ninachotaka ni mume wangu”
“Aaaaah yani kuna mambo mengine hata kujadili hayana maana kabisa”
Mara pale kwenye ofisi ya mchungaji aliingia Dora na kufanya wamuangalie kwanza maana alichelewa na kuanza kusema bila kusalimia,
“Nimeaingia Kanisani nikaona mambo hayaeleweki na watu wametoka nje, nikaamua kuuliza ndio naambiwa sijui kuna mwanamke anasema kuwa ana mimba ya Junior, kwahiyo ndoa haiwezi kufangwa. Kwani yuko wapi huyo mwanamke?”
Maana aliona wote pale ni watu wazima halafu ni watu anaowafahamu, mama Angel akamwambia akimuonyeshea Linah,
“Huyu mwanamama hapo ndio mwenye mimba ya Junior”
Dora alihamaki kwa sauti,
“Linah!! Kheee unawezaje kubeba mimba ya mtoto wa binamu yako?”
Wote wakashangaa na kumuangalia kwa makini Dora, huku Linah akimuuliza Dora,
“Unamaanisha nini?”
“Kwani hujui kama Junior ni mtoto wa marehemu James?”
Hapa Linah alijikuta akiinuka ila walimshika mkono na kumuuliza,
“Unaenda wapi sasa? Bado unamtaka Junior?”
“Niacheni mie”
Linah alitoka nje ambapo alifatwa na Dora na kusimama mahali huku wakiongea, wakati huo baba Angel alimuomba tu mchungaji waweze kwenda kumaliza swala la ile ndoa ya Junior na Vaileth, na Mchungaji alikubali maana muda haukupita sana, ingawa muda aliosema ulipitiliza ila kutokana na ile kesi aliamua tu kuendelea na lile swala.
 
SEHEMU YA 383

Baba Angel alipomaliza kazi zake, alifunga ofisi na kuondoka zake ila alipokuwa njiani alikutana na Juma na kumsimamisha huku akianza kuongea nae,
“Hivi toka siku ile hatujaonana ndugu yangu, hivi imekuwaje kwanza? Ni kitu gani kipo kati yako na yule mama Juli?”
“Unajua kuna kitu cha ajabu sana nimekigundua ambachop sikukitarajia”
“Kitu gani hiko?”
“Unajua mimi, mama yangu alikufa na kuniacha mdogo sana, baba akaoa tena na huyo mama alizaa mtoto mmoja tu ndio huyo Juli sijui yupo wapi siku hizi ila familia ilitengana kidogo baada ya baba kufa. Kwahiyo yule mama ni mama yangu wa kambo, yani mke wa baba”
“Kheee kweli milima haikutani, binadamu hukutana umemjuaje sasa?”
“Ni hivi, siku moja Erick alinipa matunda, jinsi yale matunda yalivyokuwa ni kwamba babu yangu mimi alipenda vile kwenye matunda na kunigfanya moja kwa moja nihisi kuwa Erick anahusika na ukoo wangu kwa asilimia mia moja. Nilijua Erick ndio katengeneza yale matunda, ila ndio kaja kunikutanisha na huyu mama, kumbe ni mke wa baba kwahiyo na yeye alikuwepo kwa babu pale, ndiomana anamtindo ule wa kuweka matunda”
“Ila kwanini huwa unahisi Erick anakaa kwenye ukoo wako? Ni kipi kinachokufanya uhisi kuwa Erick ni mtoto wako?”
“Yani ni hivi, kuna matendo Fulani ya Erick yanafanana na babu yangu. Kuna kipindi babu yangu alipigwa na kuzimia, ila alipotoka hapo alikuwa na nguvu za ajabu halafu alikuwa na hasira sana nasikia alikuwa akimpiga kila mtu, nimekuwa nikimfatilia Erick kwa muda mrefu sana, nisamehe kwa hili. Kwanza kabisa nilihisi Erick ni mtoto niliyezaa na baby, yani nimeanza kumfatilia Erick hata wewe hujui kama namfatilia. Mimi Erick aivyochapwa na kuzimia, nilikuwa wa kwanza kupewa taarifa maana kulikuwa na mwalimu pale shuleni kwanina Erick ambaye nilimwambia amfatilie Erick na kila kinachompata aniambie kwahiyo ilikuwa wa kwanza mimi kupewa taarifa. Erick ana akili sana, kitu hiki kinanifanya nimfananishe na babu yangu, hata nimewahi kumshawishi mara kadhaa kuwa aache shule kwani najua akili zake ni zaidi na kukaa darasani”
“kwahiyo huyo Erick umezaa na nani? Unajua unanichanganya wakati najua wazi kuwa Erick ni mwanangu, ulizaa na mke wangu?”
“Hapana, nilidhani nimezaa na baby ila huyu baby niliwahi kukutana nae, aaah kumbe haitwi baby ni jina la uongo alinipa. Mwanamke ni muongo yule hakuna mfano, nilimkuta akilia peke yake akilalamika kuwa maisha yamemtenda. Namuuliza kuwa mwanangu yuko wapi, analalamika kuwa hata yeye hajui mwanae yuko wapi, aaaah wanawake wengine huwa tunazaa nao tu, kumbe ni wajinga”
Baba Angel alipumua tu maana hata hakuelewa vizuri, alimuangalia Juma na kumuuliza tena,
“Kwahiyo Erick sio mtoto wako?”
“Kwasasa nina haki ya kusema sio mwanangu, sikujua kama Mungu alitaka nifahamu maisha ya mama yangu wa kambo yalivyo na maisha ya ndugu yangu Juli. Natakiwa nimtafute ili arudi kwenye mstari, kwahiyo Erick alikuwa kama daraja la mimi kufahamu kuhusu ndugu yangu”
“Na huyo baby?”
“Mjinga yule, Mungu amempiga kofi. Nimemkuta kalewa, analia hovyop tu, nikamuacha hapo. Kwaheri ndugu yangu.
Basi baba Angel aliamua tu kuondoka zake kwa muda huo na kurudi nyumbani kwake.

Usiku wa leo, mama Angel na baba Angel walijadiliana habari za Juma kuhusu kijana wao Erick,
“Kheee kumbe ndio ilikuwa hivyo?”
“Ndio mke wangu, yani nimemshangaa sana”
Mara simu ya mama Angel ilianza kuita, baba Angel alimuangalia mkewe na kumuuliza,
“Nani huyo anapiga usiku huu?”
“Mmmh hata sijui”
“Hebu pokea”
Mama Angel alipokea ile simu na kusikia sauti ya Rahim,
“Rahim hapa anaongea, toka nje mara moja nina ujumbe wako”
“Kheee usiku huu!!”
“Ndio, ni ujumbe wa muhimu sana kuhusu familia yako”
Mama Angel na baba Angel walitazamana kwa mshangao kwanza.
Mama Angel alipokea ile simu na kusikia sauti ya Rahim,
“Rahim hapa anaongea, toka nje mara moja nina ujumbe wako”
“Kheee usiku huu!!”
“Ndio, ni ujumbe wa muhimu sana kuhusu familia yako”
Mama Angel na baba Angel walitazamana kwa mshangao kwanza.
Kisha mama Angel akamwambia mume wake,
“Niende nikamsikilize?”
“Ukamsikilize ili iweje?”
“Kasema ni jambo la muhimu sana, linahusu familia yetu”
“Saa ngapi saa hizi?”
Mama Angel aliangalia muda na kujibu,
“Saa sita kasoro”
“Hivi kweli saa sita kasoro usiku, mke wa mtu atoke kwenda kuongea na mwanaume aliyezaa nae nje eti huyo mwanaume ana jambo la maana, inakuingia akilini kweli!”
“Kheee yamekuwa hayo”
“Hata kama sio mwanaume uliyezaa nae, inawezekana vipi kwa mke wa mtu kutoka usiku na kwenda kuzungumza na mwanaume nje eti kuna jambo la muhimu!”
“Samahani mume wangu, ila ingependeza zaidi kama tungeenda wote”
“Wapi huko? Kuonana na Rahim kwa usiku huu, ili iweje? Mke wangu hebu tulia, nakupenda sana kama jambo la maana angetuambia mapema au asubiri hadi kesho au atume ujumbe basi ila kutoka nje muda huu nakataa kabisa”
“Ila huwezi jua mume wangu, anataka kuongelea kuhusu familia yetu”
“Erica sikia mke wangu, kwanza nimekukumbuka sana. Huu sio muda muafaka wa kwenda kuongea na watu nje, njoo tufanye yetu, mambo ya kuongea na watu tuyaache”
Basi kwa muda huo, mama Angel alitoa kabisa wazo la kuonana na Rahim na kuwa na mume wake.
Simu ya mama Angel iliita sana ila haikupokelewa tena na badala yake baba Angel aliizima kabisa maana aliona ni usumbufu.

Leo, Sia alipotoka Ibadani tu moja kwa moja alienda kwa mama Angel kwani aliona anatakiwa kuongea nae mambo mengi tu ambayo hajaongea nae.
Alipofika ndio akagundua pia na swala la Vaileth kuolewa na Junior, basi aliongea nae pale,
“Hongera sana, hiyo ni bahati ujue maana wanawake wengi wanaililia”
“Asante sana”
“Kuna wanawake huko wenye elimu zao na kazi zao ila wapo tu, hajatokea hata yule wa dada naomba tukaishi wote, achilia kupata ndoa. Kwakweli ukibahatika kupata ndoa ni swala la kushukuru sana. Hongera kwa hilo, sijui mama Angel yupo”
“Yupo ndio”
Vaileth alienda kumuitia mama Angel ambapo alitoka na kwenda kuongea nae kwenye bustani kwani alijua wazi kuwa Sia huwa ana mambo mengi sana, kwanza Sia alimueleza kuhusu mama Sarah na tuhuma za mtoto,
“Kheee basi Sarah yupo hapa kwangu”
“Aaaah kumbe!! Ila sijamuacha, nimemsema pia, anadhani Sarah mtoto wake!! Thubutu, mtoto wake ni Elly”
“Kheee kwahiyo Sarah ni wa nani? Nilihisi huenda kazaa mapacha!”
“Mapacha wapi? Hakuna cha mapacha wala nini, yule kajifungua mtoto mmoja tu ambaye ni Elly, pale mzee Jimmy kampiga changa la macho pia na yeye, huyo Sarah hata sio mwanae, mtoto hafanani nae hata ukucha”
“Mmmmh kwahiyo Sarah wa nani?”
“Mimi sijui, ila muulize Derrick anaweza kujua Sarah ni mtoto wa nani kama alivyojua kuhusu Elly”
“Wanawake aliozaa nao Derrick ni Oliva na Manka, ila hata mara moja Oliva hajawahi kushtuka kuhusu Sarah, halafu ni mwalimu wake pia, yani hajawahi hata mara moja, kama ni mwanae lazima angeshtuka”
“Mmmh kuna kitu naanza kufunuka, kwamaana hiyo, yule mtoto aliyepo kwa yule madam sio mtoto wake pia? Na yeye alijifungulia hospitali gani?”
“Ile ile ya majanga ya mzee Jimmy”
“Mmmh inawezekana yule ndio akawa mwanangu, jamani huyu mzee Jimmy alikuwa na maana gani lakini? Sasa Sarah ni mtoto wa nani kama Oliva sio mtoto wake?”
“Mimi sielewi”
“Haya mambo yalivyo unaweza kushangaa hata wewe Erica na Erick wote sio watoto wako sijui utafanyaje”
“Weeee ushindwe, wale ni watoto wangu, nina uhakika nao kabisa”
“Nimetania tu, ila kale kasarah umefanana fanana nacho”
“Nahisi ni mtoto wa Derrick maana Derrick ni ndugu yangu, ndiomana damu yangu na damu ya Sarah zimeendana”
“Kwahiyo unataka kusimamia huo msimamo kuwa Manka alijifungua mapacha?”
“Sijui, ila inawezekana”
“Kheee kazi ipi, ila jana usiku kuna mahali nilipita nikamuona Makna na Rahim”
“Mmmmh!! Walikuwa wakifanya nini?”
“Sijui maana sijafatilia, umbea nauogopa siku hizi. Ngoja niende, nilileta hayo tu”
Sia hakukaa sana kwani muda huo huo aliondoka ila hapo alishapata uhakika kuwa mtoto aliyepo kwa madam Oliva ni mtoto wake wa damu.

Usiku wa leo, moja kwa moja Erica alienda chumbani kwa Erick na kuanza kuongea nae,
“Jamani kwakweli nimekumiss sana, yani naona kama kuna kitu kimepungua kwangu, hakuna tena uhuru wa kuongea kama tuliokuwa nao zamani sababu ya Sarah”
“Ila hukuipenda zawadi yangu jamani Erica!”
“Sijaipenda wapi wakati Sarah ameng’ang’ania vile viatu”
“Basi nitakununulia vingine”
“Haya, nimekufata tucheze karata”
Erick hakukataa kwani ni muda mrefu hakucheza na dada yake, kwahiyo aliona ni sawa tu kwa siku hiyo kucheza nae karata, basi walianza kucheza zile karata ila kwa leo Erick alikuwa akimuachia Erica kushinda tu muda wote mpaka Erica akamuuliza,
“Kwanini leo hushindi wewe Erick?”
“Nina usingizi”
“Mmmh haya, ngoja nikuache ulale”
“Hapana, naomba leo ulale pembeni yangu kama unavyolala na Sarah”
“Mama katukataza lakini?”
“Najua ndio, ila nakuomba Erica leo tu ulale humu chumbani kwangu”
“Sawa, hakuna tatizo”
Basi Erica alilala pembeni ya Erick, ila kwenye saa nane ya usiku walisikia mlango ukifunguliwa wote wawili walishtuka ila aliyeingia alikuwa ni Sarah, basi walimwambia kwa mshangao,
“Sarah!!”
“Ndio, utaniacha vipi nilale mwenyewe wakati wewe umekuja kulala huku! Labda kama tulale wote huku”
Basi Erica aliinuka pale kitandani na kumshika mkono Sarah na kwenda nae chumbani kulala kwani alijua wakiendelea kuongea pale, huenda mama yao angetoka, walifika chumbani na kulala tu.
Kulipokucha, Erica alianza kuongea na Sarah,
“Kwani wewe ulikuwa ukifikiria kitu gani kwa mimi kulala chumbani kwa Erick?”
“Hapana sikufikiria chochote ila kwanini uniache mimi nilale mwenyewe? Hapo ndio pagumu Erica, wala hata sikufikiria chochote kibaya”
“Haya sawa, leo tutaenda kwenye biashara ya mama Elly uone jinsi ambavyo huwa anapika”
“Sawa, hakuna tatizo”
Walikubaliana vizuri pale na kuendelea na mambo mengine.

Asubuhi ya leo, wakati Sia anatoka kununua mahitaji yake, alikutana njiani na Rahim ambapo ni Rahim ndio alisimamisha gari na kumuita Sia,
“Wewe cha umbea”
Sia alishtuka kuitwa cha umbea, basi alipomuangalia alimtambua na kwenda kumsikiliza ambapo kitu cha kwanza alimuuliza,
“Kwanini umeniita cha umbea?”
“Nimepata taarifa zako kuwa wewe ni mbea sana na unapenda kufatilia mambo ya watu”
“Mmmh!! Haya niambie ulichoniitia”
“Najua kama uliniona nilipokuwa na Manka”
Sia akashtuka na kumfanya Rahim amshushue,
“Usijifanye kushtuka, au hukuelewa kama ningekuona au ni kitu gani?”
“Hamna kitu”
“Nilienda kwa huyo Erica ili kumwambia ukweli maana aliniambia nimfatilie Manka kama kweli ninampenda”
“Eeeeh!!”
“Umeshtuka sababu hujui, ni hivi mimi nimewahi kuwa na mahusiano na Erica najua kama hilo unalifahamu hadi tukabahatika kumpata mtoto Angel, najua pia unafahamu hilo. Ila ambacho hujui ni kuwa mimi hadi leo bado nampenda Erica tena ninampenda sana, bila mambo ya ujana kunisonga basi Erica ndio angekuwa mke wangu, nadhani sasa umepata umbea mwingine wa kukuongezea siku za kufanya umbea wako”
Sia alikuwa kimya tu, kisha Rahim aliendelea kuongea,
“Sikia nikwambie kitu, hata yule Manka hakujua kama Erick kamuoa Erica, anasema siku aliyojua ni siku ambayo alimfata mwane nyumbani kwa Erica, ndio hapo alikutana nae kwa mara ya kwanza na kufahamiana, ila alikuwa akijua kuwa Erica kaolewa na mtu mwingine kabisa tofauti na Erick. Kitu kilichokuwepo ni kuwa ule ukoo ambao Erica kaolewa humo, najua alikubali kuolewa na Erick sijui ni sababu ya pesa au ni sababu ya nini maana kama pesa hata mimi nilikuwa nayo, sio nilikuwa tu hata kwasasa ninayo, mimi nimezaliwa kwenye hela na nimekulia kwenye hela tofauti na Erick. Sijui ni nini kilimfanya akubali kuolewa na Erick ila yule baba yake Erick alikuwa ni zaidi ya mafia, mzee alikuwa na roho mbaya sana yule. Laiti Erica angejua kitu alichopanga yule mzee ukumbini kukifanya! Mimi mwenyewe sikujua ingawa nilikuwepo pale ukumbini ila nasikia yule mzee alibabaishwa na mama mmoja ambaye saivi unaweza kumuita bibi maana umri ushaenda, anaitwa bi.Aisha, huyu amebahatika kujua vitu vingi sana vya mzee Jimmy. Nilitaka kumwambia Erica mambo mengi sana zaidi ya haya ila sababu ya kiburi chake hakutaka kunisikiliza kitu, namuacha tu na ujinga wake na mume wake, au unataka nikueleze wewe!”
“Ndio niambie”
“Cheki ulivyotegesha masikio vizuri, unadhani naweza kukwambia wewe! Nilataka nionane na Erica mwenyewe nimueleze ujinga wa baba mkwe wake, ukikutana na Erica mwambie nina mengi sana ya kuongea nae, mimi sitamtafuta ila yeye anitafute mimi. Afanye kabla mambo hayajaharibika, maana akigundua kilichofanyika kwa hao mapacha wake anaweza akalia machozi ya damu. Ongea nae mwambie afanye hima kabla mambo hayajaharibika, ataumbuka na sijui ataweka wapi sura yake kwa hiyo aibu ambayo ataletewa na wale mapacha wake, watoto wamekuwa wale, asipokazana kwasasa, atalia na sijui atajificha wapi”
“Mmmmh!! Kwani ni kitu gani kipo kati ya Erick na Erica?”
“Kuna jambo kubwa sana limetengenezwa na yule mzee kwa wale watoto, hilo bomu likilipuka sijui huyo baba mtu na mama mtu wataweka wapi sura zao maana itakuwa ni aibu kubwa sana kwao. Haya sio kwa Manka, nimeyapata kwa mwenyewe dokta Jimmy ambaye ni muhusika wa mambo yote. Roho imeniuma kama mzazi halafu ukizingatia nampenda sana Erica, najua angekuwa mke wangu kwahiyo roho inaniuma mimi. Mwambie anitafute haraka sana”
Kisha Rahim akapanda kwenye gari yake na kuondoka zake, Sia alisimama kwa muda bila ya kuelewa kitu chochote kile.
Basi aliamua kurudi kwenye mgahawa wake kwanza ilia pike pike na badae aende kwa mama Angel kuongea nae kuhusu hiyo habari.

Mama Angel alitoka maana alipigiwa simu na Dora ili wakaangalie maendeleo ya nyumba ya James maana alikuwa akiitengeneza kwanza kabla ya kuikabidhi mikononi mwa Junior.
Kisha Erica alimwambia Sarah sasa kuwa wanaweza kutoka kwenda kule alipomwambia kwenye mgahawa wa mama Elly.
Basi moja kwa moja walienda kwenye ule mgahawa wa mama Elly na kumkuta pale akiwahudumia wateja wake, alipowaona aliwafata karibu na kusema,
“Wewe Erica umemleta Sarah huku hujui kama anatafutwa na mama yake?”
“Kheee kwahiyo haruhusiwi kutembea?”
“Hapana sio hivyo ila mama yake anamtafuta”
“Aaaah mimi nilimleta tu aone mgahawa wako au Sarah umewahi kuja hapa? Lakini kama umewahi kuja basi umesahau”
“Ila kabla hamjaondoka, hebu subiri kwanza”
Sia alienda kuandika ujumbe kwenye karatasi na kuuweka kwenye bahasha kisha akamwambia Erica kuwa ampagtie mama yake ule ujumbe,
“Oooh sawa, sasa si ndio mama atajua kama tulikuja huku, kwanini usimpigie simu?”
“Nimejaribu ila sijampata hewani”
“Duh!! Sawa basi nitampatia”
Kisha Sia alimwambia Sarah kuwa aonje chakula ambacho yeye anakipika ila Sarah na Erica waligoma huku wakidai kuwa wameshiba sana, kisha wakamuaga na kuondoka zao. Njiani Sarah akasema,
“Ila huyu mama Elly anajikaza tu, sema anaonekana ana shida sana”
“Ni kweli ana shida, ni baba ndio huwa ana msaidia, mwanzoni nilikuwa namuona ni mtu mbaya sana ila badae niliona hana tatizo lolote lile. Sijui ilikuwaje maana Erick alikuwa hampendi huyu mama hata kumsikia”
“Duh!! Erick nae ana matatizo sana yule, najua utamwambia sababu ni pacha wako ila ana matatizo sanba yule”
Njiani walikutana na Emmanuel ambaye alikuwa ameongozana na Emmanah, ndipo Erica alipoanza kuongea nao,
“Halafu nyie kwanini hamkutaka kuja kuhudhuria sherehe”
“Mama mkubwa alitukataza, ndiomana hatukuja”
“Basi, kesho naomba mje nyumbani kwetu”
Emmanah akauliza swali,
“Hivi wewe Erica, si Erick ndio pacha wako? Na huyu ni nani?”
“Aaaah huyu ni ndugu yangu anaitwa Sarah”
“Yani mlivyoongozana kama mapacha vile”
Erica alicheka, hata Sarah nae alicheka na kusema,
“Unajua mimi hata kuna watu huwa wananifananisha na mama yao na hawa, kipindi hiko sijui kama ni ndugu zangu ila kwasasa sina shida sababu ni ndugu zangu”
“Erick sasa, kawapita urefu maana nyie ni wafupi”
“Hapana, sisi sio wafupi ila sisi sio warefu. Jamani watu wafupi ni wafupi sana, yani sisi sio warefu kama Erick ila sisi sio wafupi. Ila ni sawa na wewe na huyu Emmanuel maana yeye mrefu na wewe sio mrefu”
Wote wakacheka tu, na Erica aliendelea kuwasisitiza kuwa wasikose kwenda nyumbani kwao kwa siku ya kesho kama alivyoongea nao. Kisha waliagana pale.
 
SEHEMU YA 384



Mama Angel akiwa na Dora kuangalia ile nyumba, alifurahi sana kwani Dora aliweka karibia kila kitu kilichohitajika katika ile nyumba,
“Kwakweli hapa Dora umefanya kazi kubwa sana”
“Asante, nashukuru kwa hiyo sifa”
“Itabidi hii hela nyingine tuwapatie wenyewe kwaajili ya maisha”
“Ila kwa tabia ya Junior ilivyo ndugu yangu, wanaweza kutumbua hiyo hela yote na maisha kuwashinda ingawa wana nyumba. Sikia kitu, kule ofisini kwa babake Junior nako wamesema wanachanga. Vitu hivi nimenunua mimi pamoja na yule aliyekuwa mshirika wa James kwenye kazi zao, naweza sema alikuwa ni bosi wa James, kwahiyo hapo lazima tufikirie kitu wanachoweza kufanya wakina Junior ili kuboresha maisha bila ya hivyo basi hata vitu vya ndani humu Junior atauza vyote, sijui akili mbovu kaitoa wapi yule, yani babake hata hakuwa na akili mbovu kiasi kile”
“Ila hata huko ofisini nawapongeza sana, ni ofisi chache sana ambazo muhusika anakufa ila bado wanakumbuka fadhila zake na kusaidia kizazi chake, ni ofisi chache sana, nawapongeza kwakweli”
“Yani james licha ya yale mauzauza yake ya uhuni ila alikuwa ni mtu wa watu sana, pale ofisini kila mtu ukimuuliza atakwambia kuwa ana historia ya kusaidiwa na James, mwingine utasikia James aliokoa maisha ya mama yangu, mwingine James alinitoa gerezani mimi, ningekuwa jela bila yeye. Kama huyu aliyenunua vitu vyote humu ndani huwa anaongea sana, sijui alifanya madudu gani, akahukumiwa kifungo cha miaka thelathini na tatu jela au dhamana ya shilingi milioni ishirini na nane, unaambiwa alijua lazima afie gerezani ila James alitoa hela hiyo na rafiki yake kuwa huru, kwakweli James alikuwa akisaidia sana kipindi alipokuwa na hela, starehe alifanya sana ila na misaada alitoa sana ndiomana wanakumbuka watoto wake”
“Duh!! Kweli lakini, James alikuwa na moyo wa kusaidia, namkumbuka vizuri isingekuwa kunitaka sababu ya tamaa yake basi siku zote angebaki kuwa shemeji bora kwangu”
“Haya, tujadiliane sasa cha kufanya na Junior”
“Naona ni vyema nikamuulize Vaileth kuwa anaweza kufanya biashara gani, halafu tufungue biashara ambayo itasimamiwa na Vaileth ili waweze kusonga mbale kimaisha.”
“Oooh hiyo nzuri, halafu mimi nitajaribu kuongea nao pale ofisini kwa baba yake ili kama inawezekana wamtafutie Junior kazi yoyote pale, maana akiwa busy itapunguza usumbufu wake na kuhangaika”
Waliongea mengi sana na kupatana juu ya hilo, kisha waliagana na kuanza kuondoka ambapo mama Angel alikuwa akielekea nyumbani kwake ila njiani alikutana na rafiki yake Johari ambapo alisimamisha gari na kusalimiana pale kisha Johari alimuuliza,
“Hivi mume wangu kaja huko kwenu hivi karibuni?”
“Hapana, kwani vipi?”
“Kwakweli haeleweki, kuna mambo anayafanya nyumbani haeleweki kabisa, utamkuta kasimama kasema aaargh Erick, huwa simuelewi kwakweli”
“Mmmh!! Hebu mfatilie kwa makini, mbona ni ajabu?”
“Unajua namshangaa, bora nimekutana nawe nimeweza kukuuliza, yani huwa simuelewi kwakweli kuwa ana maana gani kufanya vile”
Waliongea kidogo tu na kuagana.

Yani Erica alipokuwa nyumbani alijikuta akiwa na hamu sana ya kujua kile ambacho kimeandikwa kwenye ile barua na Sia, ila alishindwa kuichungulia sababu karibia muda mwingi alikuwa karibu na Sarah, kitu kile kilimfanya ashindwe kusoma.
Mama Angel aliporudi moja kwa moja aliamua kumpelekea ile barua ambapo mama Angel aliiweka na kwenda kuoga kwanza, kisha alienda kuongea kidogo na Vaileth ili ajue jinsi inavyoendelea hapo nyumbani kwani kwa siku hizo walimkatalia Junior kutoka walimwambia mtu akitoka kuoa kuna siku ambazo anatakiwa kukaa ndani kwahiyo lazima atomize siku hizo,
“Eeeh Vaileth, hapa nyumbani mnaendeleaje? Junior hasumbui kweli?”
“Hapana mama, hasumbui na tunaishi vizuri tu”
“Haya, ukikaa nae vizuri hebu jadiliana nae kuwa ni kitu gani anapenda. Kumbuka kwasasa, wewe na yeye ni mke na mume, wewe hutoendelea kufanya kazi hapa bali mtaishi pamoja, ila kabla ya kuishi pamoja sisi kama wazazi tunahitaji kuwaandalia nyie mazingira ya kuwawezesha kuishi pamoja kwa amani. Hebu nikuulize wewe, katika maisha yako kitu gani unapenda kufanya?”
“Mmmh mama, mimi sijasoma maana niliishia kidato cha pili tu na kupata mimba, kwahiyo sijui nitafanya kazi gani”
“Hamna Vai, mambop ya kufanya bado yapo haijalishi umesoma au hujasoma, katika maisha makosa huwa yanatomkea, ila yanapotokea ni muda wa kujifunza kutokana na makosa ili usiweze kuyarudia tena, kwahiyo usijali, kitu gani ulikuwa ukipenda kufanya?”
“Mmmh mimi nimewahi kutamani kushona nguo”
“Oooh kwahiyo unahitaji kujua cherehani?”
“Ndio mama”
“Sawa, ni vizuri kama ni hivyo, kwahiyo wewe ni kujifunza cherehani na kukununulia tu vifaa kisha uanze kazi ya kushona! Basi hakuna tatizo, tutafanikisha tu hilo swala”
“Kwakweli mama hata huwa sijui niseme kitu gani kwa jinsi ambavyo unanisaida, kwakweli unanifanya kama binti yako kabisa”
“Usijali, wewe ni binti yangu. Napenda uishi kwa amani, sijawahi kugombana na wewe, hujawahi kunijibu vibaya, kukiwa na kosa nitakufokea na utanielewa, halafu nakupenda sababu wewe ni mwepesi wa kuomba msamaha, kwahiyo naishi nawe kama binti yangu, sijakuona na kasoro yoyote sijui tabia mbaya, sijui manini huko, upo vizuri sana Vaileth, usijali yani usiniogope kabisa uwe unaniambia kila kitu halafu tutajua jinsi ya kusaidiana”
“Sawa mama, nashukuru sana”
“Hekima na nidhamu uliyonayo ndio silaha kubwa sana kwako na ndio kitu kinachofanya upendwe na kila mtu”
Basi mama Angel alimuacha Vaileth pale na moja kwa moja kwenda chumbani kwake kuendelea na mambo mengine.

Wakati wa kulala, mama Angel alimueleza baba Angel kuhusu alichokifanya Dora kwaajili ya wakina Junior,
“Kumbe kuna kipindi Dora uwa anakuwa na akili eeeh!!”
“Siku hizi Dora kawa vizuri sana”
Mama Angel akakumbuka ile barua aliyopewa na Erica na kuamua kuichukua muda ule na kuisoma, kisha kumpa mumewe,
“Hii barua, wakina Erica wanasema kuwa wameitoa kwa Sia, anasema eti niwasiliane na Rahim mmmh!!”
“Huyo Rahim kaonana muda gani na Sia?”
“Mimi sijui kwakweli, nadhani wenyewe ndio wanajua. Je vipi, nimpigie huyo Rahim?”
“Hakuna kumpigia usiku huu, kwanza anachofahamu yeye ni kitu gani mpaka kutaka kutafutwa mwenyewe? Mimi sitaki kabisa, kwanza huwa simuamini huyo Rahim”
“Mmmh ila anasema ni mambo ya familia yetu”
“Hata kama, siku akikupigi simu mwambie aje kuongea na mimi maana mimi ndio baba wa familia kwahiyo ndio mwenye familia, kila kilichopo hapa kipo chini yangu. Mwanaume huwa anaitwa nani katika viungo vya mwili!”
“Kichwa”
“Eeeeh mimi ndio kichwa, kwahiyo natakiwa niongoze familia nzima, kichwa ndio kinaonyehsa cha kufanya halafgu vingine vinafatia, mwambie Rahim aje kuongea na mimi na si vinginevyo”
“Sawa mume wangu, nimekuelewa”
“Tulale tu, hayo mambo ya Rahim huwa sitaki hata kuyasikia”
Basi waliamua tu kulala kwa muda huo.

Baba Angel alipoenda ofisini kwa siku ya leo, alipigiwa simu na mwalimu wa Angel akipewa taarifa kuwa siku ya Jumamosi ndio siku ambayo shule imepanga kuwepo kwa mahafali ya wanafunzi wao,
“Wanafunzi wetu wote tutawaaga hapa kwenye kiwanja cha shule yetu, ndiomana hawakuondoka. Karibuni sana”
“Sawa mwalimu tutakuja tu huko hakuna tatizo”
Basi baba Angel aliagana na mwalimu na kuanza kufikiria pale vitu vya kununua kwaajili ya zawadi ya Angel, ila muda sio mrefu alifika yule bibi ambaye huwa anauza matunda, baba Angel alifurahi kumuona ili amuulize maswali yake ambayo alikuwa ameyaandaa kwake, ila yule bibi ndio alianza kuongea,
“Kwanza ninakushukuru sana bosi kwa kunikutanisha na kijana wangu Juma”
“Oooh nashukuru, ila kuna maswali kadhaa nilitaka kukuuliza”
“Niulize tu”
Mara simu ya yule bibi ilianza kuita, na kumfanya yule bibi aombe samahani kwanza kwa baba Angel,
“Samahani, ni binti yangu Juli ndio anapiga”
Basi yule bibi alipokea na kuongea nayo kwa muda, kisha alimtaka baba Angel kuweza kusalimiana na huyo Juli, baba Angel alichukua simu na kusalimiana nae ila ile sauti ilikuwa kama sauti anayoifahamu na kuamua kuuliza,
“Mbona sauti yako kama naifahamu?”
“Hata mimi sauti yako kama naifahamu, wewe sio Erick kweli? Uliniambia mkeo anaitwa Erica na binti yako mkubwa anaitwa Angel!”
“Oooh kumbe wewe ni Juli yule uliyekuwa ukinifanyia usafi!!”
“Ndio mimi bhana”
Walianza kuongea mengi tu, kisha kuagana na baba Angel alimtazama mama Juli na kumwambia vile ambavyo anafahamiana na binti yake,
“Kuna kipindi nilikuwa mkoa Fulani huko, halafu huyu Juli ndio alikuwa akinifanyia usafi kwenye chumba changu. Nimefurahi sana kufahamu kuwa wewe ndio mama mzazi wa Juli”
Basi walichekeana pale na kuongea mengi sana hata baba Angel alisahau mambo ya kumuuliza maswali yule mama.

Baba Angel aliporudi alimwambia mkewe juu ya mahafali ya binti yao Angel, basi mama Angel aliona ni vyema kuanza maandalizi ya zawadi ya kumpatia binti yao,
“Ila hivi Angel tumpe zawadi gani afurahi?”
“Mmmmh sijui, maana Angel mara nyingine huwa haeleweki tofauti na huyo Erica”
“Ni kweli, Erica ni mtoto wa tofauti sana. Kwa kifupi Erica ni mtoto mzuri tukitoa tu hilo swala lake la umbea”
“Ila muulize Erica, tumnunulie zawadi gani dada yake halafu Erica atasema, najua zawadi ambayo Erica atamchagulia Angel ni lazima Angel ataipenda maana Angel huwa anampenda sana Erica”
“Kweli kabisa usemayo”
Walijadiliana mambo mengi sana.
Kulipokucha, mama Angel aliamua kwenda kuongea na Erica kama ambavyo baba Angel alimuagiza, basi alimwambia,
“Mwanangu, Jumamosi ni mahafali ya dada yako. Tumnunulie zawadi gani, tumefikiria hatuajua”
“Mmmh sijui ila ningekuwa mimi ningependa mninunulie zawadi ambayo inanikaa mwili mzima yani nikitoka navaa zawadi zenu tupu”
Mama Angel alicheka na kumuuliza,
“Zawadi gani hiyo?”
“Yani, kuanzia nguo ya ndani hadi kiatu na mkoba, nadhani mmenielewa”
“Duh!!”
“Kwahiyo hujapenda mama?”
“Hapana, ni sawa tu hakuna tatizo”
Basi mama Angel alipoondoka hapo aliwasiliana na mume wake na kwenda kufanya hiyo kitu pamoja hadi waliporidhika na kuongeza zawadi zao nyingine.

Siku ya mahafali, baba Angel aliondoka na mama Angel tu kuelekea shuleni kwakina Angel kwaajili ya mahafali, walifika pale na walikuta watu wamejaa sana tu ila kila wazazi walipofika walipewa namba za viti kwahiyo kila mzazi alikuwa na namba yake ya kiti cha kukaa.
“Baba Angel na mama Angel, namba zenu ni hizi nne na tano”
Wakapokea zile namba na moja kwa moja kwenda kukaa kwenye zile siti zenye namba zao, ila mama Angel alipotazama pembeni alishtuka kidogo kwani pembeni yao walikaa watu wanaowafahamu vizuri tu, mama Angel akamshtua mumewe ambaye nae alishangaa kuona pembeni yao wamekaa Rahim na dokta Maimuna.

Wakapokea zile namba na moja kwa moja kwenda kukaa kwenye zile siti zenye namba zao, ila mama Angel alipotazama pembeni alishtuka kidogo kwani pembeni yao walikaa watu wanaowafahamu vizuri tu, mama Angel akamshtua mumewe ambaye nae alishangaa kuona pembeni yao wamekaa Rahim na dokta Maimuna.
Baba Angel anamuuliza mke wake,
“Hii inamaana gani?”
“Hata mimi sielewi”
“Inamaana Rahim kajua kama leo ni mahafali ya Angel au ni kitu gani?”
“Sielewi kwakweli, unajua nabaki kushangaa tu. Hata hivyo angejuaje kama Angel anasoma shule hii na ikiwa tumejitahidi kumficha tuwezavyo!”
“Itakuwa umemwambia wewe Erica”
“Hapana, siwezi kufanya hivyo, na kwanini nifanye hivyo? Hapana kwakweli”
Basi baba Angel alimuomba mama Angel waondoke eneo lile maana hakutaka kukaa pamoja na wale watu, ila Rahim na mkewe dokta Maimuna hata hawakuwaona baba Angel na mama Angel maana walikuwa wanachezea simu zao tu, yani kila mmoja alikuwa makini na simu yake.
Basi baba Angel na mama Angel wakaenda kuomba nafasi nyingine na kubadilishana na wazazi wengine, ambapo walikaa na kuendelea kutazama kile kinachoendelea pale mbele,
“Ila natamani tu hii mahafali iishe turudi nyumbani, nimeboreka kwakweli kumuona Rahim”
“Hata mimi nimeboreka sana”
Mara wakamsikia mwalimu akitangaza,
“Kuna wanafunzi wawili wameandaliwa kwaajili ya kusoma lisala, mmoja kutoka shule ya wasichana na mwingine kutoka shule ya wavulana”
Basi mama Angel na baba Angel walitazamana, na walipoangalia vizuri ndio walijua kuwa kuna wanafunzi wa kiume na wa kike,
“Kheee kumbe wamefanya mahafali ya shule mbili!!”
“Naona, nilijua ni moja tu”
Kisha mwalimu akatangaza kwenu,
“Naomba niwakaribishe hawa wanafunzi, Angel Erick atasoma risala ya shule ya wasichana na Samir Rahim atasoma risala ya shule ya wavulana”
Hapa mama Angel na baba Angel waliangaliana kwa mshangao, ila walipowaangalia hawa watoto wao vizuri ndio walibaki kushangaa tu,
“Kumbe yule Samir kamfata Angel hadi huku!! Kwahiyo walisoma shule zinazohusiana!! Kheeee watoto hawa jamani!!”
“Unajua mpaka muda huu nashangaa, nimejitahidi kwa kila hali kumficha Angel kuhusu shule ambayo anaenda kusoma, ili asimwambie Samir, sijui imekuwaje tena wamesoma shule zinazokaribiana!!”
Yani baba Angel na mama Angel walijikuta wakiongea tu kiasi kwamba hata ile risala iliyosomwa na vijana wao hawakuisikiliza kwani walikuwa kwenye mshangao tu kwa muda huo.
Basi ratiba zingine ziliendelea kama kawaida, hadi muda ya kugawa vyeti na zawadi uliwadia ila bado mama Angel na baba Angel walikuwa wakiongea tu na kustaajabu yale yanayotukia mahali pale.

Muda wa chakula, ndipo Rahim nae alipowaona baba Angel na mama Angel na kuwafata, kisha aliwasalimia na kusema,
“Kumbe Angel mlimleta shule hii? Au Angel niliyemsikia sio mwenyewe!”
Walikuwa kimya kwa muda, kisha mama Angel alimuuliza,
“Kwani wewe umekuja kufanya nini hapa?”
“Kijana wangu Samir, kahitimu pia kidato cha sita, shule ya wavulana. Tumeambiwa wote tuje hapa maana mahafali inafanywa moja tu kwa wote”
“Kheeee kwahiyo Samir ni mwanao?”
“Ndio, ni mwanangu kwani unamfahamu?”
Mama Angel alibaki kimya kwa muda kidogo na kujidai kuwa hamfahamu Samir, basi Rahim akamwambia mama Angel,
“Hata hivyo nina maongezi na wewe”
Baba Angel alimuangalia Rahim na kumwambia,
“Huu sio muda wa maongezi”
Kisha akamvuta mkewe mkono na kwenda kukaa nae sehemu nyingine huku wakiendelea kupata chakula, ila kiukweli mama Angel alijikuta akipata mawazo ya gafla, kwani hapo ndio akatambua wazi kuwa Angel na Samir ni ndugu, kitendo kile kilimpa mawazo zaidi kwani anajua ni jinsi gani Angel na huyo Samir wanavyofatana fatana, maana hata kuwa hapo kwenye hiyo shule karibu hakujua kuwa imekuwaje.
“Mbona mke wangu unaonekana kuwa na mawazo?”
“Aaaah hapana sina mawazo wala nini”
“Upo sawa kweli?”
“Ndio nipo sawa hata usiwe na wasiwasi na mimi”
Basi waliendelea kula, na kisha kuwa karibu na binti yao na kumpongeza, ila baba Angel hakutaka kupoteza muda kwani aliona mahafali imeisha basi akamtaka Angel na mama yake aondoke nao ili kama kusherekea wakamalizie nyumbani, Angel alikubali tu ila aliwaomba kwanza akaage rafiki zake.
Wazazi wake walikubali ila walikuwa wakimuangalia anayemuaga, ambapo moja kwa moja Angel alienda alipo Samir na kuagana nae, kisha kukumbatiana nae, kwakweli mama Angel alisikitika tu.
Angel alirudi na moja kwa moja walipanda nae kwenye gari na safari ya kurudi nyumbani ilianza.

Wakiwa kwenye gari, mama Angel aliamua kumuuliza binti yake kuhusu Samir maana hakuelewa,
“Angel imekuwaje umeenda kusoma na Samir shule za karibu, ulimwambia?”
“Hapana mama, ila nadhani Mungu kuna kitu kaweka kati yangu na Samir”
“Kivipi?”
“Mimi na Samir tunapendana sana”
“Weee mtoto, huogopi kusema hivyo? Ndio shuleni mmejifunza hivyo?”
“Hapana mama, ila tumejifunza kujiamini, kwasasa najiamini na ninapenda kusimamia imani yangu”
“Imani ipi hiyo?”
“Kuwa nampenda sana Samir”
“Uwiiii hizi shule jamani, ndio tumeenda kusomesha mtoto hivi kweli!! Yani Angel huna hata uoga kuwa unaongea na mama yako!”
“Ila mama jamani, mimi ni binti mkubwa sasa, kumbuka nina miaka kumi na nane”
“Miaka kumi na nane ndio mkubwa Angel jamani!! Mimi na umama wangu huu lakini kuna mambo siwezi kumwambia mama yangu, ila naona wewe upo huru kabisa huna mashaka yoyote, amakweli tumesomesha mmmh! Kwahiyo ukamwambia Samir shule uliyopo?”
“Hapana mama, kwanza mimi nakuja shuleni sina kabisa mawasiliano na Samir, yani nilikuwa siwasiliani nae kabisa. Ila sikuhiyo tulikutanishwa shule yao na shule yetu kwenye marumbano ya hoja, pale ndio nikaonana na Samir kwa mara nyingine. Kwakweli nilifurahi sana na nimesoma kwa amani sana kwa kipindi chote hiki kwa kugundua kuwa Samir hayupo mbali na mimi”
“Duh!! Nimechoka kwakweli, kichwa kinaniuma, nitakuhoji kwa muda mwingine”
Mama Angel alichoka kwa majibu ya mtoto wake, yani kwa kipindi hiki Angel alionekana kujiamini kupita maelezo ya kawaida ndiomana alikuwa akimjibu mama yake bila uoga wowote wakati ingekuwa zamani basi angebaki kulia tu na kutetemeka.
Yani hapo hawakuzungumza tena hadi wanaingia nyumbani.

Wanafika na moja kwa moja kushuka kwenye gari, huku wakina Erica wakitoka ndani na kwenda kumlaki Angel huku wakimfurahia sana na kufanya iwe ni furaha kubwa pale nyumbani kwao kwa siku hiyo.
Hapo ndio akapewa na taarifa mbalimbali kuwa Vaileth na Junior wameoana hata wana mtoto tayari, alibaki tu kushangaa ila aliwapongeza sana, yani ilikuwa ni furaha, wakiwa sebleni, baba Angel alifatwa na mlinzi kuwa kuna mgeni wake nje, ikabidi baba Angel atoke kwenda kuzungumza na huyo mgeni, akakuta kuwa huyo mgeni ni Rahim na kumuuliza,
“Umefata nini?”
“Nimekuja kumpongeza mwanangu, kwani kuna ubaya?”
“Mtoto hakutambui Rahim, kila kitu huwa kinaenda ngazi kwa ngazi, subiri mtoto aambiwe ukweli ndio utakuwa huru kumpongeza kwa wakati wowote”
“Lini mwanangu ataambiwa ukweli? Hata mimi natamani sana kuwa karibu na mwanangu, pale shuleni nimejaribu hata kwenda kumpa mkono ila amekataa kupokea mkono wangu, yani angel ana maringo kama ya mama yake jamani”
“Sawa nimekusikia ila huu sio muda muafaka wa kuongelea hilo swala”
“Haya naomba tuongee kuhusu watoto wako”
“Watoto wangu wamefanyaje?”
“Usiwe mkali wewe, wanao watapeana mimba”
Baba Angel alicheka sana na kumwambia Rahim,
“Unafikiri mimi ndio nilizaa hovyo hovyo kama wewe, maana wewe kila mwanamke uliona uchomeke mbegu zake ndio uzae nae, sasa wewe ndio watoto wako watapeana mimba na sio watoto wangu, maana mimi wangu wote wametoka kwenye familia moja”
“Yani Erick, unajua ulikuwa rafiki yangu mkubwa sana wewe. Hivi bila kulazimisha vidada vya watu kutoa mimba ungekuwa na watoto wangapi wewe? Nadhani ungefungua shule yako kabisa ambapo wangekuwa wanasoma watoto wako tu, unaniona mimi muhuni sababu nina watoto wengi, mimi sijawahi kuwatoa wanawake mimba ndiomana nina watoto wengi sio wewe. Halafu nataka kuongea nawe mambo mengine halafu wewe unaongelea vitu vingine sijui vya kuzaa hovyo, mambo yameingilianaje hapo?Utajijua mwenyewe na familia yako”
Kisha Rahim aliondoka zake na kufanya baba Angel nae arudi tu ndani na kuendelea kufurahi na familia yake.
 
SEHEMU YA 385


Leo muda wa kulala, Erica alienda kulala chumbani kwa dada yake kwani alimkumbuka sana ukizingatia ni kipindi kirefu alikuwa yupo shule.
“Dada jamani, nakumbuka kile kipindi ambacho wewe ulikuwa ukituambia sisi kuwa wewe ndiwe mama yetu”
“Ndio, mimi ni mama yenu maana mimi ni dada yenu wa kwanza”
“Eeeeh nipe habari za shule?”
“Kabla ya yote, nasikia siku hizi umekuwa mpishi hodari sana, nasikia unapika hadi watu wanajing’ata”
“Nani kakwambia dada?”
“Huko bibi yako anakusifia kila kukicha, kwakweli mdogo wangu umekuwa noma”
Erica alicheka na kusema,
“Jamani dada!”
“Ndio, basi kesho naomba unitengenezee keki ili niwapongeze Vaileth na Junior kwa kuoana, najua na mimi ya kwangu itakuwa nzuri balaa”
“Ya kwako na nani dada?”
“Nani mwingine zaidi ya Samir? Nampenda sana Samir naye ananipenda sana, mapenzi matamu ni kupendana. Asikudanganye mtu mdogo wangu, yani kupendana ni raha sana”
“Hongera sana dada”
“Asante na wewe ukikua utampata unayependana nae kama mimi nilivyompaya Samir”
“Mmmmh nishampata tayari”
“Niambie mdogo wangu, ni nani huyo?”
“Utamfahamu tu, jina lake linaanzia na E kama langu”
“Kheee umeanza kuchukua mtu kwa kufanana nae herufi ya jina!! Cha muhimu ni kupendana tu”
Erica alitabasamu tu na kuendelea na maongezi mengi sana na dada yake.

Kulipokucha, moja kwa moja Angel alienda kwa mama yake na kumuomba mama yake amnunulie simu,
“Ulisema nikiwa mkubwa ndio nitamiliki simu, naomba ninunulie simu mama”
“Usijali, hakuna tatizo. Simu yako ipo tu. Kwani unashida gani Angel?”
“nataka kuwasiliana na Samir”
“Tafadhari Angel usinitajie tena hilo jina hapa, nisije kufanya kitu kibaya, nakuomba sana usinitajie hilo jina”
Mama Angel alienda chumbani kwake, alijiuliza moyo wake na kuona kuwa anachotenda kumficha Angel sio kitendo sahihi ukizingatia Angel na huyo Samir wamependana, basi alijisemea,
“Nadhani ni wakati wa Angel kuutambua ukweli wa mambo kama baba yake mzazi ni Rahim, anatakiwa ajue kuwa huyo Samir ni ndugu yake maana ni mtoto wa baba mmoja. Asiniletee mambo ya mimi na Derrick bure!!”
Akawaza kwa muda kidogo ila bado hakujua ni jinsi gani aanze kumweleza mwane kuhusu ukweli halisi wa baba yake mzazi, alitambua kuwa mwanae anatakiwa kujua ukweli ila huo ukweli anausemaje? Hapo ndio palikuwa pagumu kwake, akajisemea tena,
“Inabidi nitafute wataalamu wa saikolojia ili wanishauri ni kitu gani naweza fanya ili binti yangu aufahamu ukweli kabla ya kuibua mengine”
Alifikiria sana ila aliamua tu kuendelea na mambo mengine.

Mchana wa siku hiyo, Erica alishaandaa keki aliyoambiwa na dada yake, kisha kuweka mezani halafu Angel aliwaita Vaileth na Junior, ili kwa pamoja wakate keki na kula ili kusherekea na kuwapongeza kwa ndoa yao.
Wakati wanafurahi pale, ndipo alipofika mgeni mahali hapo, mgeni huyo alikuwa ni Daima, ambapo aliuliza kwa makini,
“Kuna nini hapa?”
Alijibiwa na Erica bila ya kuficha kitu chochote kile,
“Tunampongeza Junior na Vaileth kwa hatua yao ya kufunga ndoa na kupata mtoto wao wa kwanza wa kiume”
Kwakweli Daima alihamaki kwa hasira sana,
“Kumbe ni kweli ndiomana ulikuwa hunitaki hapa wewe mtu mzima Vai”
Vaileth akajua tu pale lazima matusi yataanza kumtiririka Daima, hivyobasi aliamua tu kwenda chumbani, ikabidi Erick ndio amtoe nje Daima, ila Daima hakubisha na kutoka nae hadi nje ya geti kabisa kisha akamwambia,
“Naomba uondoke Daima”
Ila Daima alimuangalia Erick na kumwambia,
“Unajua sikuwahi kukuangalia vizuri ila leo nimekuangalia vizuri”
“Kivipi?”
“Kheee wewe kijana ni mzuri sana, yani leo ndio nimeuona uzuri wako”
“Kheee nenda zako bhana”
“Kwenda naenda ndio ila wewe ni mzuri sana, sio kama Junior, yani huyo mtu mzima atajuta tu kuolewa na Junior. Ila wewe ni mzuri sana, unafaa kuwa mume wa mtu”
Daima alitaka kumsogelea Erick ili ambusu ila muda huu, Erica alitoka ndani na kumvuta Erick kwa nyuma kisha akaingia nae ndani na kumuacha Daima akiwa mwenyewe pale nje, ambapo aliamua kuondoka tu kwa muda huo.

Erica aliingia ndani na Erick huku akimsema kwa kitendo cha kumsikiliza Daima,
“Ulikuwa ukimsikiliza wa nini yule lakini? Watu wengine sio wa kuwasikiliza kabisa, au alikuchanganya kukwambia anakupenda?”
“Hapana hajaniambia hivyo”
Mara simu ya Erick iliita kwa muda huo, akapokea ni baba yake ambaye alikuwa akipiga na alimuita mahali kuwa aende kwa muda huo. Basi alimweleza tu Erica pale kuwa anaenda kuonana na baba yao, basi Erica akamwambia,
“Naomba twende wote”
“Mmmh Erica, kaniita mimi lakini”
“Ndio kakuita wewe, najua kama leo sio siku ya kazi, kuna jambo ambalo baba kakuitia, naomba twende wote”
“Sawa hakuna tatizo”
Basi sababu walikuwa tayari, walienda tu kumuaga Angel na kuondoka zao, kwahiyo hata mama yao aliyekuwa chumbani hawakumwambia kuwa wanaenda wapi.
Moja kwa moja Erick alipofika sehemu ambayo baba yake kamuita, walienda na Erica na kumfanya baba yao ashangae kidogo,
“Kheee mmekuja wote?”
“Ndio, Erica kataka kuja pia”
“Kuna rafiki yangu alisema kuwa anahitaji kukufahamu ndiomana nimekuita hapa”
Muda kidogo yule rafiki wa baba Angel alifika, na alipoona wale watoto wapo wote alisema,
“Bila shaka hawa ndio Erick na Erica?”
“Ndio, umewaona eeeh!! Nilimwambia Erick aje mwenyewe ila na Erica akaja pia”
“Na nilijua tu kuwa lazima wangekuja wote”
Baba Angel alimuangalia rafiki yake kwa makini na kumuuliza,
“Umejuaje?”
“Aaaah hawa watoto wanapendana sana, nilijua tu kuwa lazima wangekuja wote”
Baba Angel alitabasamu kidogo na kusema,
“Ni mapacha hawa, lazima wapendane”
“Ila upendo wao ni zaidi ya unavyofikiria wewe”
Hii kauli baba Angel hakuielewa maana bado alijiuliza huyu rafiki yake kahisi nini kuwa hawa watoto watakuja wote? Kauli ya kupendana kupita na anavyofikiria yeye hakuielewa kwani kuna sehemu nyingi tu ambazo Erica na Erick hawaendi pamoja, basi aliwatambulisha pale na kuachana na ile mada asiyoielewa,
“Jamani huyu ni rafiki yangu mkubwa sana, anaitwa Mr.Noah”
Basi Erica na Erick walipena mikono na Mr.Noah na kisha kukaa pamoja ambapo waliagiza chakula na kuanza kula huku yule Mr.Noah akiwauliza Erick na Erica maswali kadhaa wakati wa kula chakula huku akionekana kuwaangalia sana watoto hawa kanakwamba kuna kitu kingine ambacho alihitaji kuongea halafu hakukiongea.
Walipomaliza, walijiandaa kwaajili ya kuondoka ambapo baba Angel alienda kupanda kwenye gari na watoto wake sababu yeye hakwenda na gari kwahiyo alichomuitia Erick kitu kingine ni kile kwenda pale na usafiri ili waweze kuondoka vizuri.

Usiku wa leo, Erica alimfata Erick chumbani kwake na kuanza kuongea nae kuhusu yule rafiki wa baba yao,
“Hivi yule rafiki wa baba umeweza kumuelewa kweli?”
“Sijamuelewa hata nimebaki kumshangaa tu”
“Anamaanisha nini kusema upendo wetu ni tofauti na baba anvyofikiria, au kaona kama tunapendana kwa namna tofauti?”
“kaonaje na yeye katufahamu leo”
“Mmmh sijui, usikute anatufahamu tangia zamani. Ila hii hali ya mimi na wewe kupendana zaidi imekuwa kubwa kwenye ukubwa wetu huu, kwahiyo yule sijamuelewa kabisa”
“Nadhani kuna kitu anajua kuhusu mimi na wewe, sijui ni kitu gani ila aaargh sijui ni kwanini jamani, mara nyingine najihisi hata kulia, kwanini nikupende hivi dada yangu? Ninakuwa na wivu na wewe, najikuta nikitamani unifanyie vitu vingi sana, najikuta nikitamani mimi niwe mpenzi wako na tuishi kama wapenzi wanavyoishi”
“Pole sana, mimi sasa ndio nimejikuta nikitamani hata Junior na Vaileth walivyoona iwe ni mimi na wewe”
“Aaaaarggh sisi ni ndugu ujue, kwanini lakini? Na kwanini wanazuia ndugu kuwa pamoja? Sitaki kukupoteza Erica na sitaki uwe na mwanaume mwingine, sijui nitafanyaje nikigundua”
Erica alihema kwa nguvu maana hakuwa na jibu kwani ni kweli hata yeye alijikuta akimpenda sana Erick kila siku inavyoenda ndivyo anavyozidi kumpenda.
Erick alimsogelea Erica na kumkumbatia, kwakwlei Erica alihisi akisisimka mwili mzima na kumtoa Erick pembeni,
“Mmmmh hapana, naogopa mimi naogopa”
Erica alitoka mule chumbani kwa Erick, basi Erick alikaa kitandani kwake na kujiinamia huku machozi yakimtoka na kujiuliza,
“Kwanini kila siku zinavyozidi kusonga mbele ndio hamu yangu ya kuwa na Erica inazidi? Kwanini Erica ni ndugu yangu? Nampenda sana, aaaarghh nadhani tutatengwa na ukoo, kwanini macho yangu yasitamani wasichana wengine yakaenda kumtamani Erica kweli!!! Aaaargggh”
Erisk alijikuta tu akitokwa na machozi, na mwisho wa siku aliamua tu kulala kwa muda huo maana hata angewaza sana bado asingepata jibu la mawazo yake.

Kulipokucha, baba Angel na mama Angel waliongea kuhusu Vaileth na Junior kuhamia kwenye hiyo nyumba ambayo Dora anataka kumzawadia Junior kama urithi wa kutoka kwa baba yake, ila mama Angel anaona kabla ya hilo watimize kwanza ahadi yao ya kufanya sherehe ndogo kijijini kwakina Vaileth ili kuwawezesha wazazi wa Vaileth nao kufurahi na binti yao,
“Ila mke wangu, sasa hivi unavyojua pesa imekuwa tatizo kidogo kwetu”
“Hakuna tatizo, yani hii namwambia Dora halafu utaona mambo yatakavyoenda, mbona ofisini kwa marehemu James wanachanga, hata wao walitaka kumfanyia sherehe kidogo Junior, basi tutawaomba tufanyie huko kijijini, halafu huko gharama haitakuwa shida, si unajua kijijini watu hata hawana makuu, raha ya sherehe wao ni wale na kunywa sio kama hapa mjini tulivyo na makuu, tunaweka hata vingine visivyokuwa na maana utakuta watu wanaviacha”
Baba Angel akacheka kidogo tu ila jukumu hilo aliona ni vyema kumuachia mke wake maana aliona akilibeba yeye basi litamshinda mara moja.
Baba Angel aliondoka zake kwenda ofisini, halafu mama Angel alimtafuta Dora na kuongea nae kuhusu hilo swala la sherehe ambapo Dora aliona hilo swala lipo sawa kabisa,
“Halafu uliongea na yule binti kitu anachoweza kufanya?”
“Ndio niliongea nae, alisema kuwa anaweza kufanya cherehani, ameomba kwenda kusomea hayo mambo ya kushona”
“Oooh hiyo haina kazi, najua utamsimamia, ili awe anashona halafu tumfungulie mahali ambapo atauza hata na vitambaa, vitenge na khanga huku akiwa fundi mwenyewe itamlipa sana hiyo”
“Kumbe Dora noma sana wewe, kuna muda unakuwa na akili timamu haswaaa”
Dora alicheka sana, na kupanga mipango mbalimbali haswaaa mipango ya kufanya sherehe nyumbani kwakina Vaileth.

Usiku wa leo, mama Angel alimueleza taarifa zote mumewe kuhusu hiyo sherehe na kila kitu alichoongea na Dora,
“Naona kaamua”
“Roho imemsuta, unajua alifanya vibaya, Junior ni mtoto halali kabisa wa James tena ni mtoto wa ndoa, sema tu mambo hapo kati yalitokea na kufanya baba na mama yake watengane, ila hilo haliwezi kukosesha Junior kupata haki zake. Ila mbaya mwingine ni yule shemeji Deo, yani ni mwanasheria ila hakutaka kujishughulisha na chochote kuhusu mali za Junior. Ila muache ataumbuka tu kwasasa, maana atashangaa kuona Junior amesharudi kwenye nyumba ya baba yake”
“Halafu hata kwenye harusi hakuja”
“Ndio hakuja, alimwambia mkewe kuwa mnajisumbua na huyo Junior, kwanza mnajipa mizigo maana mtahudumia watu watatu, Junior, mke wake na mtoto, akasema mtajuta sana. Badala mumkanye mtoto ndio mnahalalisha zinaa yake kwa kumfanyia harusi, mambo ya harusi mngemuacha agangamale nayo mwenyewe. Yani sijui kwanini Deo ana roho mbaya kiasi hiki, hampendi Junior hadi Junior mwenyewe anajua kama babake wa kambo hampendi”
“Yule nae sijui vipi, kama huyu Junior kuharibika hata na wao wamechangia kwa kiasi kikubwa sana. Mtoto hana uangalizi, kazi ya mama ni kulalamika tu na kusema mtoto amemshindwa tabia, yani Mungu amsaidie tu Junior aweze kupata akili ya maisha”
“Naamini Vaileth atamuweka sawa, kwani ni binti ambaye akili yake ipo vizuri, Vai atashughulika na Junior ndiomana nimefanya juu chini waoane tu.”
Wakajadiliana pale na kuamua tu kulala.

Siku hizi Dora na mama Angel walikuwa wakishirikiana vilivyo kuhakikisha kuwa sherehe kwenye kijiji cha wakina Vaileth inafanyika, na itakuwa nzuri tu, kwahiyo walifanikiowa kuweka kila kitu sawa na kushirikiana vyema na upande ule wa ndugu wa Vaileth katika maandalizi, kwanza na wao walifurahi sana, haswaa mama yake Vaileth ambaye a,ishajikatia tamaa ya binti yake kuolewa, kwahiyo ile ilikuwa ni furaha nyingine baada ya ile furaha ya kwanza ya mahari kupita.
Siku moja kabla ya shughuli, ilibidi mama Angel akaongee na mama mzazi wa Vaileth ili amwambie ukwlei kuhusu vaileth kuwa na mtoto maana walikuwa hawajui,
“Mama samahani, hatukuwaambia mwanzoni, ni hivi mtoto wenu Vaileth amezaa na kijana wetu”
“Oooh kumbe!! Ila kwanini hamkusema”
“Tuliogopa faini”
“Sasa faini tuwapige ya nini wakati mtoto mwenyewe alishazalia nyumbani tayari, tushindwe kumpiga faini aliyetuachia kuanzia mimba hapa kulea hadi mtoto halafu tuje kuwapiga faini nyie kweli!! Hilo ni jambo la kheri, tena tunashukuru sana mmetuambia, ni furaha sana kwetu kwani ni matunda mema”
Basi mama Angel alishukuru kwa yule mama kukubali tu bila ya tatizo lolote lile.

Siku ya sherehe, waliondoka familia nzima, mapema kabisa ili wawahi kule kijijini na pia waweze kuwahi kurudi, kwakweli ilikuwa ni furaha na shamra shamra nyingi tu.
Wakati sherehe ikiendelea, mama Angel alifatwa na mama Vaileth na kumwambia,
“Samahani mwanangu, kuna wazee pale wanahitaji maelezo pia uliyonipa mimi kuhusu Vaileth kuwa na mtoto”
Mama Angel hakuona tatizo, na moja kwa moja aliondoka na yule mama Vaileth ili kuwafuata wale wazee, ila kabla hajawafikia mama Angel alishikwa bega nyuma, alipogeuka alikutana macho kwa macho na dokta Jimmy.

Wakati sherehe ikiendelea, mama Angel alifatwa na mama Vaileth na kumwambia,
“Samahani mwanangu, kuna wazee pale wanahitaji maelezo pia uliyonipa mimi kuhusu Vaileth kuwa na mtoto”
Mama Angel hakuona tatizo, na moja kwa moja aliondoka na yule mama Vaileth ili kuwafuata wale wazee, ila kabla hajawafikia mama Angel alishikwa bega nyuma, alipogeuka alikutana macho kwa macho na dokta Jimmy.
Mama Angel alishtuka sana ila dokta Jimmy alimwambia kuwa asishtuke halafu akamuomba yule mama aliyekuwa ameongozana na mama Angel kuwa azungumze nae kidogo, yule mama hakukataa kwani yule dokta ni mtu ambaye aliheshimika sana pale kijijini.
Dokta Jimmy alisogea pembeni na mama Angel, kwakweli mama Angel alimfata tu na kujishangaa maana hakuwahi kufikiria kama siku akikutana na dokta Jimmy wazi kabisa atafanyaje nae.
Ila alivyozidi kusogea nae alimuuliza,
“Tatizo nini kwani?”
“Nisikilize Erica, kule na yule mama unaenda wapi?”
“Tatizo liko wapi? Unahisi naenda nae wapi?”
“Kijiji hiki unakifahamu vizuri Erica?”
“Hapana sikifahamu vizuri ila ninachojua ni kuwa hawa watu ni wakarimu sana”
“Mzee Mussa ndio ambaye alikuwa mshenga wenu, niliwahi kukutana nae na alinieleza kuhusu wewe, aliponiambia tu moja kwa moja nilitambua kuwa ni wewe. Swala la nyie kuja kuoa huku sio baya ila swala la nyie kuja kufanya sherehe huku ndio baya na msipokuwa makini litawagharimu sana”
“Sikuelewi”
“Kwani, muda huu yule mama kakuitia nini?”
Mama Angel aliamua tu kumwambia ukweli bila kujali kuwa huyu ni adui yao au la,
“Sasa hujawaambia kwani kuwa binti ana mtoto?”
“Nimeongea na mama yake kasema haina tatizo hilo ni swala la baraka ila sijajua kwanini leo kasema kuwa nikazungumze na wazee”
“Basi wale wazee watawaletea mlolongo usiotakiwa, na utajutia nakwambia, aiseee itawagharimu tena haswaaa, mimi nawajua wale wazee, yule mama hana tatizo ila wale wazee. Mimi ni kweli sio mtu mwema kwako, ila uliyopitia yanatosha, hakuna sababu ya kupitia mengine kwa wema wako ulioufanya kwa binti huyu. Mama wa huyu binti hana tatizo, hana tatizo kabisa, ni mtu mzuri, tatizo lipo kwa hao wazee waliokuita. Yani ukirudi nyumbani mwambie binti kuwa uliitwa na wazee, kwanza atatetemeka sana akisikia hivyo. Wale wazee wanaogopewa sana, na hivi hujaenda watafanya jambo”
“Kheee sasa nifanyeje?”
“Cha kufanya, nenda kakusanye familia yako hadi huyo binti na mtoto na mumewe, jifanye kama unaenda kuongea nae, zungukeni kwenye magari yenu muondoke hata msijisumbue kurudi wala nini kwa muda huu. Mimi nitaongea na yule mzee ambaye ni mshenga wenu ataenda kuwaombea ruhusa kuwa mmepatwa na dharula mmeondoka. Najua hata mlipokuja kutoa mahari hamkukutana na wale wazee”
“Hatukukutana nao ndio”
“Wale sio ndugu ila ni wazee wa kimila, wana mambo mabaya sana. Sio wa kuwaaga, nakuhurumia wewe na familia yako, ondoka muda huu na hivi umefanya sherehe wanajua wewe ni tajiri”
Kidogo mama Angel alishikwa na uoga, na hapo aliamua kufanya kamavile dokta Jimmy alivyomwambia, alivuta familia yake na kuondoka nayo huku akimwambia mumewe kuwa pale sio pazuri, wanatakiwa kuondoka halafu wanatakiwa wawahi ili wafike mjini mapema. Kwahiyo waliondoka bila wenyeji kujua maana hata Vaileth hakuaga, zaidi ya kuitwa kama kwa maongezi na kupandishwa kwenye gari, hapo ilikuwa ni safari tu ya kuondoka kurudi nyumbani.
Mama Angel alikuwa na mashaka sana ukizingatia alibeba familia yake yote na kwenda nayo huko, hakuelewa wala hakuwa na raha dhidi ya kile kitu kilichopo.

Walifika nyumbani wakiwa na uchovu kiasi, ila wote waliuliza ni kwanini wameondoka gafla vile ila mama Angel aliwaambia ni kwaajili waweze kuwahi, kwa upande mwingine alishukuru hawakwenda kule na wafanyakazi wa baba yake na Junior ambao walisema wataandaa tafrija fupi tu ya kumpongeza yule kijana, ila kule kijijini waliona kuwa ni mbali. Yani mama Angel hata kumuuliza Vaileth kwa siku hiyo alishindwa kabisa yani alikuwa hadi anatetemeka na kuamua tu kwenda kulala maana hata mumewe hakumwambia ukweli.
Kulipokucha, kitu cha kwanza kabisa, mama Angel alienda chumbani kwa Vaileth na kumtaka Vaileth kuongea nae,
“Samahani Vaileth, eti kwenu kuna mila gani?”
“Kivipi?”
“Mimi, niliongea na mama yako kuhusu wewe kupata mtoto, mamako hakuwa na tatizo lolote lile na alibariki tu lile swala. Ila toka tumefika jana kwenye ile sherehe nikashangaa tukiendelea na sherehe ila hakuna aliyeuliza mtoto wa Vaileth yuko wapi au mlete mtoto tumshike, hata wakati mtoto upo nae pale mbela, ila sikushangaa sana. Sema mama yako alikuja kuniita na kuniambia kuwa wazee wa kimila wanataka kuongea na mimi kuhusu swala la wewe kuwa na mtoto”
Vaileth alishtuka na kumuuliza mama Angel,
“Ulienda kuongea nao?”
“Hapana sikwenda, kuna mtu akanitonya kuwa niondoke na nisiende kuwasikiliza hao wazee wa kimila”
“Aaaarrrgh wale wazee wana mambo ya ajabu sana, sijui nani atakuwa kawaambia kuhusu shefrehe nyumbani kwetu. Ndiomana mimi wakati tumefika toka mwanzo nilimuachia mtoto akae na Erica tu hadi pale alipomleta ili anyonye, nawajua wale wazee yani lazima wamemsumbua mama ndiomana kakuita”
“Huwa wanataka nini?”
“Yani wale wazeee ungeenda kuwasikiliza, wangekutajia faini ya kulipa kwa kitendo cha mimi kuzaa kwanza kabla ya ndoa, halafu wana mtindo wa kuangalia uwezo wako kwahiyo wanakutajia faini kulingana na uwezo wako. Na hivi waliona tumeenda na magari basi hapo lazima wanajua ni matajiri kwahiyo wangetaja faini ndefu, ukikataa kulipa wanakwamisha safari yani unashangaa tu pale kijijini huwezi kuondoka, yani mnekuwepo pale na kuwaachia chochote mlichokuwa nacho, halafu wanawapa shida sana kwenye safari. Sikujua kama wale wazee wamerudi tena kijijini kwetu. Kuna kipindi waliondoka”
“Duh!! Kwahiyo ningewasikiliza ingekuwa balaa, kwahiyo wangenitajia ngapi?”
“Huwa wanataja wale, wakiona mtu ana gari wanaanza kutaja milioni ishirini”
Mama Angel alishtuka sana,
“Kheee jamani, hiyo hela ya mtaji kabisa wa biashara kubwa tu”
“Ndio hivyo, pole mama. Ashukuriwe huyo aliyekwambia mapema”
“Kwanini mama yako nae asiniambie?”
“Sijui ila najua pia hakupenda ila hakuwa na namna, ngoja nimpigie”
Muda huu Vaileth alimpigia simu mama yake na aliweka sauti kubwa na kuanza kumsalimia pale, ambapo mama yake alimuuliza,
“Mlifika salama jana?”
“Ndio mama tulifika salama, ila mama kulikuwa na tatizo gani?”
“Mmmmh si wale wazee jamani, mimi niliwaita wajomba zako na kuwaambia ukweli, sijui mjomba wako gani na kiherehere chake kaenda kuwaambia wale wazee wa mila, nikashindwa kufanya chochote kile. Nakumbuka hata mwanangu ulisema kuwa mahari tusipange kubwa ila wale wazee wa mila najua lengo lao lilikuwa ni kuwaumiza wageni wetu”
“Sasa mama, kwanini usingetutaarifu mapema”
“Jamani mwanangu, kwani siipendi familia yangu kuendelea kuishi huku!! Hii sehemu ni nzuri, ardhi inarutuba, tunakula na kuishi, nilivyoona vile niliamua kuongea na yule mshenga wao nikamueleza kuhusu wale wazee wa kimila, basi yule mshenga wao nae aliogopa jambo kulibeba yeye kama yeye, basi akasema kuna yule dokta mkubwa aliwahi kuongea nae na anaonekana kufahamiana na watu hao, akasema ataenda kumwambia, kwahiyo hata wakati naondoka na mama yako halafu dokta akamuita sikuwa na tatizo sana, ukizingatia karibia nilikuwa nafika nae kwa wazee wa kimila, kwahiyo wote waliona jinsi alivyoitwa na yule dokta. Si unajua yule dokta anavyooogopewa hapa kijijini, basi ndio ikawa rahisi, hata mlipoondoka na mshenga kuja kusema mmepata tatizo, na wenyewe walihisi mambo mbalimbali ila nani wa kumshikilia kasema? Watamshikilia yule dokta watamuweza yule? Nisamehe sana mwanangu, ila hawa wazee hata sikutaka wafike, ndiomana umeona hata sijafurahia ujio wenu, hata sijataka kumshika mjukuu wangu, yani hawa wazee hapana kwakweli. Nisamehe sana mwanangu”
Basi Vaileth alimaliza kuongea na mama yake na kukata ile simu huku akimuangalia mama Angel ambaye alipumua tu na kusema,
“Kweli duniani kuna mambo jamani, sikutegemea kama kuna sehemu kuna hayo mambo ya ajabu kama huko kijijini kwenu”
“Wenye mambo ya ajabu ni wale wazee ila wengine wapo salama tu”
“Au ndioama yule mwanaume wa mwanzo alikimbia kwa mambo kama haya?”
“Hapana, kipindi kile wale wazee wa kimila walikuwa vijiji vingine, wanazunguka wale sio kwamba wapo kijiji kimoja, wale ni watu wa kuzunguka. Sio watru wazuri”
“Duh!! Nimefahamu vitu vingi, mmmh sikutegemea kwakweli. Nilihisi mwili wote kusisimka”
Basi mama Angel alimaliza pale na kumuacha Vaileth huku akirudi chumbani kwake sasa ambapo mumewe alikuwepo tu amekaa kitandani huku akisoma gazeti, alianza kumwambia yale na kumfanya ashangae sana kwani ni kitu ambacho hata yeye hakukitegemea kabisa na aliona ni cha ajabu,
“Yani dokta Jimmy ambaye ndiye adui yetu namba moja halafu yeye ndio amekuwa msaada wetu!”
“Ndio hapo”
“Ila licha ya hayo, ila nahisi kuna mengi katikati hapo”
“Kama yapi mume wangu?”
“Nahisi dokta Jimmy hataki twende tena kule kijijini kumfatilia, kwahiyo ameshatutisha tayari na hatuwei kwenda tena maana tuna uoga”
“Ila mume wangu licha ya hivyo ametusaidia sana”
“Hata kama, bado sio mtu wa kumuamini dokta Jimmy, wala sio mtu wa kumshukuru kwani bado mabaya yake yanaendelea kucheza katika maisha yetu. Yeye na hao wazee wa kimila ni wako sawasawa, halafu hao wazee nadhani hawajawahi kukutana na watu wabishi, hivi nianze tu kutoa milioni ishirini mimi!! Labda sio mimi Erick”
Baba Angel alitabasamu tu, mama Angel alijua utata wa mumewe, alijua pale lazima lingezuka la kuzuka maana baba Angel asingekubali kutoa hiyo hela.
 
SIMULIZI INAELEKEA KUISHA...... ZIMEBAKI SEHEMU CHACHE SANA TUIMALIZE....

WEKA UTABIRI WAKO, NIKIPATA COMMENTS 5 TU, NAANGUSHA SEHEMU 10 KAMA BONUS.

HAMNA COMMENTS TUKUTANE KESHO SAA 12.
 
nimekua mlevi wa story zako kias mambo muhim baadhi siyafanyi kama saa hizi niko online jaman hebu eeka tunimalizie huu usiku, mimi sina wasap sina insta sipigi sim situmi msg yan me ndio natafutwa mana busy na story zako umeongeza kule kwa ndoa tatu zilizovunjwa?? usione sicoment chochote nasoma kimya kimya patakaponibamba ndio naweka mwandiko wangu, asante lakini umenifanya kuchangamsha akili
 
nimekua mlevi wa story zako kias mambo muhim baadhi siyafanyi kama saa hizi niko online jaman hebu eeka tunimalizie huu usiku, mimi sina wasap sina insta sipigi sim situmi msg yan me ndio natafutwa mana busy na story zako umeongeza kule kwa ndoa tatu zilizovunjwa?? usione sicoment chochote nasoma kimya kimya patakaponibamba ndio naweka mwandiko wangu, asante lakini umenifanya kuchangamsha akili

Asante sana mkuu kwa kuthamini kazi ninazozituma...!!!
 
SEHEMU YA 386


Leo, Angel aliamua kumfata mdogo wake Erick na kumukmba simu yake kwani alihitaji kuwasiliana na Samir ukizingatia hakuasiliana nae kwa muda kwani simu hakuwa nayo, ile simu yake ilikuwa kwa bibi yake.
Erick alimpatia simu, kisha Angel akaenda kuwasiliana nae, na kukubaliana nae kuwa Samir ataenda pale kwakina Angel siku hiyo.
Na kweli jioni yake, Samir alienda pale nyumbani kwakina Angel na kukaa na angel kwenye bustani huku akizungumza nae, kile kitendo mama Angel hakupendezea nacho kabisa, akaanza kijisemea,
“Wale ni ndugu, haya ni mambo ya ajabu kwakweli, inatakiwa Angel aufahamu ukweli. Lini nitamwambia ukweli Angel?”
Hapo ndio palikuwa na utata kwa upande wake, basi aliishia kuwaangalia tu ambapo Angel na Samir waliendelea na maongezi yao bila wasiwasi wowote ule.
“Unajua Angel kitendo cha sisi kukosa mawasiliano kinaniumiza sana”
“Ni kweli, hata mimi naumia ila nitaipata tu ile simu yangu au niende kwa bibi nikaichukue?”
“Nikupeleke kesho basi, mwambie bibi yako kuwa umekuwa mkubwa na unamaamuzi yako”
“Unadhini siku hizi hata mama namuogopa? Hakuna kitu kama hiko, kwasasa hata mama simuogopi wala nini, namwambia ukweli tu na yeye, ananielewa vizuri, nimeona uoga wetu ndio utakaovunja mapenzi yetu wakati Mungu anahitaji sana tuwe pamoja. Hebu angalia ni vikwazo vingapi tumepitia ila bado Mungu anatuweka pamoja”
“Kwakweli naamini hayo usemayo kuwa Mungu anataka gtuwe pamoja, kwahiyo wazazi lazima wakubaliane na matakwa yetu.”
“Vipi lakini wewe wazazi wako?”
“Aaaah mimi kwa mama yangu yupo sawa tu, ila baba sijawahi kumwambia wala nini, sema mama aliwaka tu kipindi kile cha mdogo wangu ila kwasasa naona yupo sawa tu, sababu nilikaa nae na kuongea nae na kumweleza ni jinsi gani nakupenda, basi alinielewa”
“Kwa upande wangu msumbufu ni mama, ila baba najua nikiongea nae ni mwelewe na atanielewa kwa haraka sana, nikiona mama haeleweki basi nitamwambia baba. Sisi hatuwezi kuwa mbalimbali kwani tunapendana”
Wakaongea mengi sana pale, ni mpaka Samir alipoamua kuondoka na kuondoka zake.
Mama Angel alimuita Angel na kuanza kuongea nae,
“Ila Angel mwanangu una nini lakini wewe?”
“Kwanini mama?”
“Si nilishakueleza kuwa huyu Samir simtaki na wala hakufai mwanangu, kwanini unakuwa hivyo lakini?”
“Mama, naomba unisikilize, mimi Angel ni binti mkubwa sasa, kama mzazi unatakiwa ukubali maamuzi yangu maana nimeyapima na kuona kuwa yanafaa, mama nampenda sana Samir, na yeye ananipenda sana, usitake kutuvuruga na kufanya tuachane, mimi na Samir tunapendana sana”
“Ni kweli mwanangu ila wewe na Samir hamfai kuwa pamoja”
“Kivipi mama, na kwanini hatufai kuwa pamoja ilihali tunapendana sana”
Mama Angel akapumua kidogo na kusema,
“Angel mwanangu, subiri umalize chuo ndio uanze hayo mambo ya mapenzi”
“Mama, kwani kuna muda ambao mtu anastahili kuanza kupenda? Mama Samir nampenda kweli tena, naomba tu mama niache niwe na Samir yani ukiniachanisha nae unanipa wakati mgumu sana. Naona wazi sitaweza kwenda mbele”
Ilionekana wazi kuwa mama Angel anashindwa cha kusema dhidi ya Angel na Samir, yani alijikuta akijiuma uma tu na kuachana na mtoto wake huku akifikiria vitu vingi sana.

Baada ya Samir kuondoka tu, ndio muda ambao Emmanuele na Emmanah waliwasili, na kumfanya Erica kwenda kumuita mama yao ili aweze kufahamiana na hao watu maana mama Angel alisema kuwa anahitaji kuwafahamu zaidi, kwahiyo Erica alifanya kila juhudi wale waweze kufika pale kwao.
Basi mama angel aliwakaribisha ndani kwake na kuwafurahia sana huku akiongea nao mambo mengi sana kwa wakati huo,
“Wazazi hawajambo”
“Hawajambo kabisa”
“Nimefurahi sana kuwafahu, kwa leo naomba tule chakula kwa pamoja kama hamtojali, tafadharini msikatae jamani”
Wote walitabasamu tu, na kwavile kwa siku hiyo mama Angel alikuwa amepika mapema, basi aliweka chakula na wote wakaenda mezani na kuanza kula kile chakula, kwakweli mama Angel alijikuta habandui macho yake kwa Emmanuel na Emmanah maana alijikuta akiwapenda sana wale watoto, vile walivyokuwa wakiongea ndio alizidi kuwapenda maana walionekana ni watoto wacheshi sana, kama alivyompenda Sarah basi ndivyo alivyowapenda na hawa watoto.
Walimaliza pale kula na kumshukuru, kisha alirudi kukaa nao sebleni ambapo kwa muda huo aliwaita watoto wake wote, kuanzia Angel, Junior, Vaileth, Sarah, Erick, Erica pamoja na wale Emmanuel na Emmanah na kusema,
“Jamani, kwasasa huyu Emmanuel na Emmanah nao ni ndugu zetu naomba tuwatambue kama ndugu zetu”
Wote walitabasamu na kufurahi tu huku maongezi mengine yakiendelea, hata Emmanuel na Emmanah walipoaga ni mama Angel ndio alijitoa kuwasindikiza watoto hawa maana alijikuta akiwapenda sana, njiani aliwaambia shauku yake ya kutaka kuwatambua wazazi wao,
“Natamani sana niwafahamu wazazi wenu, natamani sana kwakweli. Nahisi tu watakuwa ndugu zangu kwa namna moja au nyingine, maana naona damu yangu na damu zenu ikipatana sana”
“Haman tatizo, utawatambua tu wazazi wetu, hata sisi tumekupenda sana”
“Msiache kuja kunitembelea mara kwa mara, si mnaona watoto wangu pale nyumbani eeeh!! Pale kuna mmoja anaitwa Elly hayupo pale, na Ester amelala, nyie wote ni watoto wangu, nawapenda sana”
Emmanuel na Emmanah walitabasamu pia kwani waliweza kuona jinsi huyu mama alivyokuwa na moyo wa kipekee maana aliwapenda waziwazi bila kujificha kwa namna moja au nyingine, alionyesha wazi upenzo wake kwao.
Basi waliagana nae na kuondoka zao kuelekea nyumbani kwao.

Usiku wa siku hiyo, Erica alienda chumbani kwa dada yake na kumkuta kajiinamia tu, basi alikaa na kuongea nae huku akimuuliza kuwa tatizo ni kitu gani,
“Kwani vipi dada?”
“Mapenzi mdogo wangu, sijui kwanini mama hataki niwe na Samir ilihali ninampenda sana halafu na yeye ananipenda sana”
“Hivi dada, mapenzi ni mpaka mpendane?”
“Ndio, kupendana ndio raha ya mapenzi, yani umpende mwenzio halafu na yeye akupende wewe, hapo ndio raha ya mapenzi ilipo. Huyo uliyemtaja siku ile ni nani?”
“Aaaah nitakwambia tu dada”
“Au ndio huyu uliyemleta leo? Ni huyu Emmanuel?”
Erica alicheka na kusema,
“Hapana dada, yule ni rafiki yangu tu si unaona mama ameshatambulisha kuwa ni ndugu, yupo nimpendaye”
“Mmmh si uniambie dada yako”
“Nitakwambia tu dada”
“Halafu mama jamani kila mtu ni ndugu yetu yani na yeye anaanza kama wale mama wakubwa maana wale kila kijana nitakayesimama nae wakinikuta nae tu basi wanaleta sera za kusema ni ndugu yangu, jamani ukoo gani huu wenye ndugu kila kona? Kwakweli mimi kwa Samir hata sikubali, awe ndugu yangu au asiwe ndugu yangu siwezi kuachana nae kamwe. Mama kila siku anaongeza ukoo, rafiki zetu wote ni ndugu zake, anadhani itakuwaje kwetu”
“Ila dada, si hairuhusiwi kwa ndugu kuwa na mahusiano?”
“Unadhani ndio wakisema Samir ni ndugu yangu nitaachana nae! Thubutu, siachani nae hata kidogo kwanza duniani wote ni ndugu maana wote tumetoka kwenye uzao wa adamu na Eva”
“Aaaah kumbe, kweli ukifikiria hilo utapata jibu kuwa wote ni ndugu, kwahiyo swala la kuoana ndugu ni swala la kawaida, maana najiuliza kwani Adam na Eva ndio walikuwa wanadamu wa kwanza, haya sasa watoto wao walioana na wakina nani kama sio wenyewe kwa wenyewe?”
Angel na mdogo wake walicheka na kusema,
“Ni kweli hapo mdogo wangu, lazima walioana wenyewe kwa wenyewe, kwahiyo maswala ya kusema ndugu siwezi kukubali kuvunja mahusiano kwa kisingizio cha undugu”
Basi Erica alijadiliana vitu vingi na dada yake kwa usiku ule, kisha alimuacha mule chumbani kwake na kumuaga usiku mwema halafu yeye akaenda moja kwa moja chumbani kwa Erick ambapo alimkuta amejiinamia tu kwa wakati huo,
“Kheee Erick, nilijua umelala”
“Hapana, nina mawazo mengi sana Erica”
“Nini tena?”
“Unajua bado nafikiria ni kwanini mimi nakupenda kiasi hiki?”
“Pole, ila nilikuwa naongea na dada angel muda mfupi tu uliopita anasema kuwa sio tatizo kwa ndugu kupendana na kuanza kuwa wapenzi sababu hapa duniani wote ni ndugu”
“Kivipi?”
“Hebu fikiria Adam na Eva, waliumbwa peke yao na kuzaa watoto je wale watoto wao walioa wakina nani kama sio kuoana na dada zao ili kukuza kizazi?”
“Mmmh Erica, umefika hadi kwenye uumbaji?”
“Ndio, au tuseme ile dhana kuwa binadamu wa kwanza alikuwa nyani ni ya kweli? Kwahiyo kulikuwa na ukoo wa Adam na Eva halafu ukoo wa manyani, ndio watoto wa Adam na Eva wakaoa kutoka kwenye ukoo wa manyani?”
Hapa Erick alicheka sana, na Erica nae alicheka ila gafla walijikuta wakiangaliana kwa muda mrefu kidogo na kusogeleana, kila mmoja alianza kumbusu mwenzie, ila Erica alishtuka na kuinuka na kusema,
“Hapana Erick, sisi ni ndugu”
“Kumbuka umetoka kusema hapa kuwa ndugu si vibaya kupendana”
“Ni kweli ila hatutakiwi kupendana kupitiliza”
“Kwahiyo unatafuta ukoo wa manyani ndio uupende kupitiliza?”
Hapa wote walianza kucheka tena, kisha Erica aliamua tu kumuaga kaka yake na moja kwa moja kwenda chumbani kwake ila alimkuta Sarah amekaa tu, inamaana na yeye hakulala toka alipoondoka,
“Kheee Sarah hukulala kumbe!!”
“Kila siku unaniacha mwenyewe chumbani Erica, sio vizuri. Ningeenda kile chumba alichosema mama ila kulala bila simu siwezi, basi ongea na mama anipatie simu yangu niweze kulala nayo na kuichezea”
“Pole Sarah, nitaongea nae kwa hakika atakupatia tu hata usijali. Pole sana”
“Asante, sina raha mimi wala sina furaha. Ni kweli nimeondoka kwa mama yangu ila angalau ningewasiliana nae hata kidogo tu, nimemkumbuka pia”
Ni kweli Sarah alionekana kumkumbuka mama yake, ila Erica alielewa kuwa yote ile ni sababu mama Angel amekuwa akimbana Sarah sana mule ndani kwao kiasi kwamba Sarah kajiona kuwa hana uhuru tena wa kufanya chochote haswaa uhuru wa kuchezea simu yake, basi Erica alimbembeleza pale kisha wakaamua kulala tu.
 
SEHEMU YA 387

Baba Angel leo akiwa tu ofisini kwake, anapigiwa simu na rafiki yake Mr.Noah, na hapo anamuelekeza ofisini kwake ambapo rafiki yake huyo anaenda na kumkaribisha kisha kuanz akuongea nae,
“Karibu sana, hapa ndio ofisini kwangu, ila hii ofisi nilikaa mwaka mzima bila kuikanyaga sababu ya matatizo yaliyonipata”
“Duh pole sana, kwahiyo nani alikuwa akisimamia biashara yako sasa na kazi yako?”
“Namshukuru Mungu nimepata kijana mwenye akili na kujituma, yani mwanangu Erick yupo vizuri sana, ni yeye ndio alikuwa akisimamia kila kitu, kuanzia biashara yangu na kila kitu hadi hapa kazini”
“Oooh hongera kwa hili, kwahiyo mwanao yule anaweza kushinda asubuhi hadi jioni hapa?”
“Ndio, ila mara nyingi sana huwa anashinda kiwandani, yani kiwanda changu kimeendelea sababu yake, kwa jinsi nilivyoumwa vile, kile kiwanda kingekufa ila Erick kawa mtoto wa ajabu sana katika maisha yangu maana kasimamia kile kiwanda hadi ndio imekuwa biashara kubwa sana kwangu sababu ndio inaniingizia hela nzuri zaidi”
“Hivi mwanao huwa anakula chakula gani akishinda ofisini au huko kiwandani”
“Mmmh mwanangu yule ni mtihani mkubwa sana, alikuwa anaweza kushinda asubuhi hadi jioni bila kula chakula chochote kile eti hadi arudi nyumbani kula. Nilipiga nae kelele hadi nilikoma, ila badae nikaona kumbe kitu rahisi ni kumtuma Erica yani yule dada yake awe anampelekea chakula, basi akipelekewa chakula na Erica anakula ila asipopelekewa hali wala nini”
“Mmmh nilijua tu, watoto wako wale wanapendana sana”
“Ila sikuelewi, kwnai kupendana kwao na hayo maswali yako kuna husiana vipi?”
“Kuna siku utanielewa kuwa hao watoto kwanini nasema wanapendana sana, huoni kama maswali ninayokuuliza kuhusu hao watoto! Hayakupi maswali pia kwenye kichwa chako?”
“Napata maswali pia lakini sikuelewi”
“Basi kaa ukijua kuwa watoto wako wanapendana sana”
“Ila kama wanapendana ni vizuri maana upendo ndio kila kitu katika maisha”
“Kweli kabisa, siku moja jaribu kusema kuwa unahitaji kusafiri na Erick halafu utakaa nae wiki nzima huko unapohitaji kwenda nae, halafu sikiliza atakachokisema Erica baada ya wewe kusema hivyo”
“Mmmmh unajua sikuelewi”
“Kuna siku utanielewa, ila sina mengi sana kwa leo. Nilitaka tu kufahamu ofisi yako basi na si vinginevyo”
Mr.Noah alimuaga baba Angel na kuondoka zake, kwakweli baba Angel alibaki na baadhi ya maswali kichwani mwake.

Usiku wa siku hii, baba Angel alimueleza mke wake kile ambacho aliongea na rafiki yake ofisini kwake kuhusu watoto wake,
“Unajua sijaweza kumuelewa kwakweli, yani amekazana muda wote kuongea kuhusu watoto wetu mapacha kuwa wanapendana sana, yani sijaweza kumuelewa”
“Na yeye ana mambo ya ajabu, kwahiyo anataka watoto wachukiane? Ndugu wanachukianaje jamani! Mbona kuna watu wana mambo ya ajabu loh!!”
“Nimemshangaa sana kwa hilo, yani nimeona ni mtu wa ajabu kushangaa hilo jambo, sababu ndugu watachukianaje? Ndugu ni lazima kupendana”
“Huyo nae sijui ana mambo gani, yani hii familia jamani, likitoka hili linaingia lile khaa jamani!!”
Baba Angel alikumbuka kitu kingine,
“Halafu kesho natakiwa kwenda kwenye ofisi za yule mwarabu, kasema anataka mzigo nimpelekee mwenyewe halafu ana maongezi na mimi, sijui anataka kuongea nini na mimi”
“Itakuwa ni mambo ya biashara tu hayo maana nasikia yule ni mfanyabiashara mkubwa sana”
“Ndio, halafu anajuana na watu wengi ndiomana hata swala la kuumwa kwangu kaweza kulifanya vizuri sana”
Waliongea mengi tu, na kuamua kulala kwani muda nao ulikuwa umeenda.

Leo baba Angel kama ambavyo aliahidiana na yule mwarabu, basi alichukua mzigo ambao yule mwarabu aliutaka na kumfikishia moja kwa moja kwenye ofisi zake, kisha akampigia simu,
“Oooh Erick umekuja, njoo tu kwenye ofisi yangu hii ya chini nipo na kijana wangu huku”
“Sawa, nakuja hamna shida”
“Ndio njoo, umfahamu na kijana wangu”
Basi baba Angel moja kwa moja alienda kwenye ofisi aliyoelekezwa na mwarabu, ila alipofika pale ofisini alimuona kuna baba mwingine amekaa na yule mwarabu, alipomwangalia vizuri yule mtu aligundua kuwa yule ni Rahimu

Basi baba Angel moja kwa moja alienda kwenye ofisi aliyoelekezwa na mwarabu, ila alipofika pale ofisini alimuona kuna baba mwingine amekaa na yule mwarabu, alipomwangalia vizuri yule mtu aligundua kuwa yule ni Rahim.
Baba Angel alishangaa kwa muda, ila yule mwarabu alipomuona alimuita karibu na kusema,
“Sogea hapa karibu kijana wangu”
Kisha yule mwarabu alianza kumtambulisha baba Angel kwa Rahim,
“Huyu ni kijana wangu, ndio mtoto wangu wa kwanza anaitwa Rahim, halafu Rahim huyu ni kijana wangu pia ndio ambapo kiwandani kwake nachukua sana bidhaa kama unakumbuka ni kile kiwanda ulichonionyesha kipindi kile”
Kisha Rahim na baba Angel wakapeana mikono, ila baba Angel alielewa kuwa Rahim ndio alimuonyesha yule mwarabu kile kiwanda chake na kufanya awe mteja mzuri kwao.
Ila wakati wakipeana mikono, Rahim akasema kwa baba yake,
“Ila huyu ni rafiki yangu mkubwa sana”
“Aaaah kumbe”
“Ndio, kipindi kile nipo Marekani ndio nilikuwa nae. Ni rafiki yangu sana huyu, anaitwa Erick”
“Kweli inaonyesha mnafahamiana, ndiomana ulikazana kuniambia kuwa kile kiwanda kina bidhaa nzuri sana kumbe ulikuwa ukijuana vizuri na rafiki yako eeeh!! Ila hata hivyo ni kweli kuna bidhaa nzuri, hongera sana kijana”
“Asante sana”
Kisha Rahim akaamua kumuacha baba yake aweze kuongea na baba Angel maana hakujua ni kitu gani anataka kuongea nae, ila alimwambia baba Angel,
“Kabla hujaondoka naomba tuongee ndugu yangu, nitakuwa ofisi zile za juu nishtue tu”
“Sawa hakuna tatizo”
Rahim akaondoka na kumuacha baba Angel na yule mwarabu, ambapo cha kwanza kabisa yule mwarabu alianzakumsifia mtoto wake,
“Huyu kijana wangu yupo vizuri, ila tatizo lake uhuni, aaaarrgh mtoto kanisumbua huyu, najua unamjua sababu ni rafiki yako, mama yake alikuwa akimkatalia sana, hata kipindi nimemtafutia mwanamke aoe, bado mama yake alikuwa akikataa kuwa sio muhuni hadi pale wanawake zake walipoanza harakati za kubwaga watoto kwa bibi yao yani mama yake, kwakweli mimi nilikataa kabisa kuletewa watoto wa ajabu ajabu”
“Kwani mama yake Rahim huishi naye?”
“Aaaah sisi mila zetu zipo tofauti kidogo na kipindi kile zilikuwa kali sana, ni kweli nilizaa nae ila kumuoa ilishindikana kabisa kwani nyumbani walikataa na kutaka nioe mtu mwenye asili yangu, ndio sababu ikafanya nisiweze kumuoa na kutengana nae, yani tofauti ni asili tu na si kingine.”
“Ooooh mna mila kali”
“Eeeeh ndio kwetu kulivyo, ila siku hizi wanaoana tu ila napo ni kwa kulazimisha maana hairuhusiwi. Huyu Rahim mke wake wa kwanza nilimtafutia mimi mwenyewe, mwanamke aliyetulia, alikuwa ni mzuri tena alichanganya, lakini huyu kijana wangu sasa uwiiii alikuwa akimpiga sana na kumuacha mtoto wa watu na maalama kila kona, mwishowe wakashindwa kuishi wote. Ila nimepata shida maana mimi ndio niliingia dhamana ya kuoa yule mwanamke kwa niaba ya huyu mwanangu. Tuachane na hayo, tujadili nilichokuitia huku sasa”
“Sawa, nakusikiliza mzee”
“Yule kijana wako wa kuitwa Erick, kuna siku nimeongea nae kwakweli yule mtoto anaonekana kuwa na akili sana, kwakweli nimempenda kupita maelezo ya kawaida. Sasa nilikuwa naomba kitu moja, nipe ruhusa ya kufanya kazi na kijana wako kwa wiki moja tu halafu tutaongea zaidi”
“Aaaah sawa, hilo halina shida, nitaongea nae natumaini atakubali tu”
“Basi ongea nae juu ya hilo, kuna vitu nahitaji anaielekeze na anisaidie, kijana wako anaonekana kuwa vizuri sana. Kwakweli nimependa sana jinsi alivyo na akili ya tofauti, nitafurahi sana nikifanya nae kazi”
“Hakuna tatizo juu ya hilo mzee wangu”
Kisha waliongea mengi pale na kupanga mambo mbalimbali ya kuweza kumshawishi huyo Erick mdogo ili akubali kwenda kufanya kazi kwa huyo mwarabu japo kwa hiyo wiki moja.
Basi mwarabu alimaliza kuongea na baba Angel, na baba Angel akamuaga ila akamkumbusha kuhusu Rahim kuwa alihitaji kuongea nae pia,
“Ngoja nimshtue kwenye simu”
Huyu baba Alimpigia simu Rahim kisha baba Angel alitoka na kwenda kukutana na Rahim kwneye ofisi nyingine ilia pate kuongea nae.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom