miss nyanga
New Member
- Dec 18, 2023
- 4
- 8
Nimekaa kwenye ofisi na siyo ofisi ndogo,ofisi kubwa sana,Tena ninaimiliki mwenyewe iliyosheheni furniture za thamani na kila kitu nilichokuwa nakitamani muda wote wa maisha yangu,ninayo Amani ya moyo na ninaona Nina kila kitu ambacho niliomba muda wote kwa Mungu wangu yaani kiufupi nimebarikiwa.
Basi nikasema niperuzi kidogo mtandaoni, ghafla nakutana na account ya Remmy (mme wangu wa zamani) kwanza nikashtuka ndo kazeeka Hivi,baada ya kuona picha zake basi akili yangu ikarudi nyuma miaka 9 iliyopita wakati tuko kwenye mahusiano ya uchumba alivokuwa ananijali na kunithamini ilhali Hana kitu chochote kipindi tunasoma,na niliona Dunia imeumbiwa mapenzi jamani na Wa kuyaenzi ni Mimi na yeye na sio wengine maana wengine wanadanganyana tu,Yaani Kuna point jamii inawachagua nyie muwe mfano wa kuigwa na Tulipewa majina ya Wapenzi waliokufa pamoja fyuu huo utoto hapana aisee,Tukipeana sabuni na mafuta na vocha basi hakuna kingine kwenye mapenzi tulichohitaji zaidi penzi letu lifike mbali tu,na hatimaye tuzeeke pamoja.
Basi miaka ikapita Mimi nikamaliza chuo na yeye akabaki na Nikapata kijikazi cha kujishikiza kusukuma muda na kujipatia hata maisha,na baada ya muda na yeye akamaliza tukiwa tuko vizuri zaidi ya jana japo kukwaruzana kupo lakini tulikuwa vizuri sana,Tukatembeleana na baadae akaamua kuniamishia sehemu alipo kutokana na mkataba wangu kuisha nikarudi nyumbani kwetu na yeye alikuwa anafanyia kazi mkoa huo huo basi tukawa karibu zaidi,nikawa naenda kwake sana na katika kwenda kujiachia kukahusika, baada ya muda nikahisi siko sawa mara leo mgongo mara kichwa yaani tafrani nikaamua kupima mkojo, nikajikuta Nina ujauzito nisioupanga na matumaini yangu nikimwambia atafurahi sana lakini nilivomuambia alinijibu Sawa nitalea hebu fikiria picha iliyokuja kichwani,nikaumia lile jibu fupi nikalia nmevuruga mipango yangu na nikajipa jibu hapa hakuna muoaji hapa, kitu kizitoo.
Kwetu ni wakali sana wazazi, wananiamini,najiheshimu Leo nizalie nyumbani Mimi big nooo,
Wakati namuelezea Niko kwake akasema tuhakikishe kipimo kikanunuliwa mimba Ipo na kutoa haiwezekani sababu siko tayari yeye pia hayuko tayari lakini hapo nimeshapata majibu alivokuwa kapoa kuwa hakuna muoaji kabisa lakini Sina jinsi sababu mimba sio ugonjwa, ujasiri wa ajabu nikajikubali haraka sana na nikafanya Siri nyumbani nilivofika nyumbani Niko na Siri yangu na hakunitafuta Hadi Mimi niwe namtafuta,mpenzi kapeperushwa na habari za mimba,
Zikapita siku mtu hata mkipanga kitu ni kawa mkali sana na hataki mazoea,baada ya muda nikasema takufa Mimi ikabidi nimueleze mama yangu na mama akamtafuta sababu walikuwa wanajua ni Rafiki yangu ikabidi amuite na kumuuliza na Kumbuka hapo baba hajui na alivoulizwa na mama akakubali kweli mimba ni yake na Atalea hasemi atanioa,mama akamwambia sawa Tupange Mimi na yeye inakuwaje akajibu sawa.
Siku mbili hapokei simu zangu ikabidi niende kwake na hapo kaanza mapicha picha yaani anawasiliana na wadada ambao ni wanawake zake nikasema liwalo na liwe napambania penzi langu,nikamuomba tuishi pamoja yaani mwenzenu mimba ya nyumbani Tena mtu niliyokuwa najiheshimu Leo nizalie nyumbani Tena niwape mzigo wazazi hapana mwenye mzigo hajafa na yupo na najua ni yeye Bora anikatae lakini nyumbani sikai,basi katika kumlazimisha akatafuta mshenga na akaenda naye nyumbani na nikatolewa posa na kuchumbiwa wakatajiwa tarehe ya kuja na wazee kupangiwa maali yaani naona kabisa jamaa Hana furaha na sio muoaji ila ninalazimisha tu.
Kabla ya kupangiwa maali baba aligundua Hali yangu na ikabidi aitwe akabidhiwe mke,Kumbuka moyoni Nina furahi sababu natamani kudeka na kuishi na mpenzi wangu kumbe najitafutia shida tu.
Wazee wake walikuja wakapangiwe maali nyumbani kwetu na taratibu zifuatwe na walifanikisha na Jambo likapita,Nilikaa na yule mwanaume ugomvi ndio ugomvi na akaanza kubadilika kila siku,yaani nikawa mtu wa huzuni tu na sikuwahi kusema nyumbani kiufupi nilijuta na sikuwa na msaada kwa muda ule nikavumilia na kuvumilia Tena.
Unaishi na mtu Hana muda na wewe,dada yangu alinipa mtaji nikaanza kuuza nguo na viatu vya kike ndio ikawa ahueni hata nikawa nanunua nguo lakini Ukweli Sijui hata nguo yake,Mda ukawa unasonga na mtu amebadilika jumla,nilienda kujisubiria uzazi kwetu na siku zilivofika Nikapata mtoto na ndo mwanzo wa mateso yangu.
Nakumbuka Nina siku tatu nitoke uzazi,alikuja na akaniambia ana habari Nzuri za kuniekeza nikafurahi nilichoelezwa.
Ntaendelea
nyanga