Simulizi: Namtaka mpenzi wangu arudi

Simulizi: Namtaka mpenzi wangu arudi

Mungu wetu azidi kukupa wepesi, maana binafsi najifunza mengi sana kupitia simulizi zako, mfano, kumtumaini Mungu, mahusiano ya kifamilia, ujana, tamaa za utajiri, madsraka na Nguvu za giz kama kwenye story ya Malkia wa Ghoshen na ninaendelea kubarikiwa kwa kweli mpendwa. Naamini kwa Nandy na Dickson nitajifunza mengi zaidi. Barikiwe sana sana mpendwa.!!
 
Ameen [emoji120][emoji120]
Barikiwa mnooo mnoooo
 
Ipiii hiyo ya malkia wa goshen au

Kuna story moja uliileta humu, mie niliishia njiani kuisoma, anaitwa tatiana huyo binti alikuwa kipofu, then akapata uwezo wa kuona, kwao shinyanga vijijini (in masanja's voice)
 
Kuna story moja uliileta humu, mie niliishia njiani kuisoma, anaitwa tatiana huyo binti alikuwa kipofu, then akapata uwezo wa kuona, kwao shinyanga vijijini (in masanja's voice)
Story ya kipofu niliyeleta humu ni sarafina alikuwa mwimbaji akaja kuona akaaza kuwa naa majivuno badae Mungu akamrudisha kwenye upofu wake

Tatiana yupo kwenye malkia wa wagoshen badae alikuwa kipofu
 
Story ya kipofu niliyeleta humu ni sarafina alikuwa mwimbaji akaja kuona akaaza kuwa naa majivuno badae Mungu akamrudisha kwenye upofu wake

Tatiana yupo kwenye malkia wa wagoshen badae alikuwa kipofu

Mtunzi Shunie na wewe unajichanganya sasa, sarafina ni binti alikuwa anasoma udsm, akapata ujauzito wa david, then David akamwambia atoe, hakuutoa, akaenda kwa mwanza akafukuzwa, then akarudi dar, akawa omba omba akajifungua mtoto anaitwa malaika, maisha ya shida then sarafina kafariki kwa kansa ya titi n.k n.k

Tatiana ni binti alizaliwa shinyanga, kijiji cha chibe huko akiwa kipofu, alikuwa na sauti nzuri sana ya kuimba na sura nzuri, wazungu wakaja tanzania kwa ajili ya utalii then wakataka waimbaji kwenda kwenye shndano lao marekani, tatiana akawa mmojawapo, tatiana akaenda marekani, pamoja na yote akashida shindano, then wakawa wapenzi na mtoto wa muandaa shindano akampeleka hosp kafanyiwa op tatiana kaanza kuona, akamsahau Mungu wake akawa wa kidunia zaidi, niliishia pale amekuja Tanzania baada ya miaka mitatu, akachomwa kisu kwenye onyesho lake pale udsm...... niko deep Shunie, nadhani utakuwa umekumbuka..... nipe link sasa

Malkia wa gosheni sijawahi kuisoma
 
Story ya kipofu niliyeleta humu ni sarafina alikuwa mwimbaji akaja kuona akaaza kuwa naa majivuno badae Mungu akamrudisha kwenye upofu wake

Tatiana yupo kwenye malkia wa wagoshen badae alikuwa kipofu

Nimeikumbuka jina inaitwa "penzi bila maumivu"
 
Mtunzi Shunie na wewe unajichanganya sasa, sarafina ni binti alikuwa anasoma udsm, akapata ujauzito wa david, then David akamwambia atoe, hakuutoa, akaenda kwa mwanza akafukuzwa, then akarudi dar, akawa omba omba akajifungua mtoto anaitwa malaika, maisha ya shida then sarafina kafariki kwa kansa ya titi n.k n.k

Tatiana ni binti alizaliwa shinyanga, kijiji cha chibe huko akiwa kipofu, alikuwa na sauti nzuri sana ya kuimba na sura nzuri, wazungu wakaja tanzania kwa ajili ya utalii then wakataka waimbaji kwenda kwenye shndano lao marekani, tatiana akawa mmojawapo, tatiana akaenda marekani, pamoja na yote akashida shindano, then wakawa wapenzi na mtoto wa muandaa shindano akampeleka hosp kafanyiwa op tatiana kaanza kuona, akamsahau Mungu wake akawa wa kidunia zaidi, niliishia pale amekuja Tanzania baada ya miaka mitatu, akachomwa kisu kwenye onyesho lake pale udsm...... niko deep Shunie, nadhani utakuwa umekumbuka..... nipe link sasa

Malkia wa gosheni sijawahi kuisoma
Oooh ni penzi bila maumivu Penzi bila maumivu
 
SEHEMU YA 77

Wazazi wa Dickson walipewa taarifa juu ya kile kilichokuwa kimetokea, walishangaa, kwao lilionekana kuwa jambo geni kwa mtoto wao kukamatwa na kupelekwa polisi huku akishutumiwa kwa kosa la ubakaji alilokuwa amelifanya miezi mitatu iliyopita.

Wakaondoka na kuelekea katika kituo hicho ambapo huko wakajitambulisha kwa polisi na kutaka kujua kile kilichokuwa kimetokea.
Polisi hao waliwaambia kwamba kulikuwa na msichana mmoja aliyekwenda kituoni hapo kufungua kesi ya ubakaji aliyokuwa ameifanya miezi mitatu iliyopita.

Walichokitaka ni kuonana na msichana huyo na kuzungumza naye kwani kitu hicho kwao kilionekana kuwa kigeni na hawakuwa na uhakika kama mtoto wao alifanya kosa hilo kwa kuwa walimwamini, alikuwa mcha Mungu ambaye aliishi katika mazingira ya dini kila siku.

Linda akapigiwa simu na kuambiwa kwamba mwanaume aliyekuwa amemfungulia kesi tayari alikuwa amekamatwa na hivyo kwenda katika kituo hicho.

Msichana huyo aliposikia hilo, moyo wake ukawa na furaha, akawa na amani na kuona kwamba alikuwa amemaliza kila kitu na hivyo kitu kilichokuwa kimebaki kilikuwa ni kuzungumza na Amina ili amwambie kwamba alitakiwa kujiandaa.
“Kila kitu tayari, yule mwanaume amekamatwa,” alisema Linda.

“Mwanaume gani?”
“Dickson! Yaani umesahau?” aliuliza Linda.
Amina alisahau kila kitu kilichotokea, siku hiyo alipoambiwa kuhusu mwanaume huyo, kumbukumbu zake zikaanza kurudi nyuma na kuikumbuka sura ya mwanaume huyo.

Bado alikuwa mzuri, alihisi kabisa kwamba kama angekwenda mahakamani na kutoa ushahidi kwamba alibakwa kitu ambacho hakikuwa kweli, aliona kabisa maisha yake yasingekuwa kama yalivyokuwa, yangebadilika kwa kuwa nafsi yake kila siku ingekuwa ikimsuta.
“Siwezi! Siwezi kutoa ushahidi wa kumfunga,” alisema Amina.

Hilo ndilo alilopanga, hakutaka kumwambia Linda, mwanamke huyo alitumia kiasi kikubwa cha pesa kuhakikisha kila kitu alichopanga kinakwenda kama kilivyotakiwa hivyo kama angekataa kwamba hakubakwa basi alihisi kungekuwa na jambo baya ambalo lingetokea.

Wakati akifikiria kuhusu hayo, Linda akampigia simu na kumwambia kwamba walitakiwa kuonana kwa kuwa kuna mambo mengi walitakiwa kuyazungumza kabla ya kupanda mahakamani.
 
SEHEMU YA 78

Hilo halikuwa tatizo, haraka sana wakaonana Magomeni katika Mgahawa wa Young Boys na kuanza kunywa juisi. Waliongea mambo mengine mengi, walifurahia pamoja lakini mwisho wa siku Linda kumwambia kile kilichowafanya kuwa mahali hapo.

“Ninachohitaji ni kuona anafungwa gerezani tu,” alisema Linda huku akimwangalia Amina.
“Kwani tatizo hasa nini?”
“Ni mapenzi tu!”
“Na unampenda?”
“Sana tu!”

“Sasa kwa nini unataka kumfunga?” aliuliza Amina.
Kwa kipindi hicho hilo ndilo swali lililokuwa likimkasirisha moyoni mwake, hakutaka kuulizwa kuhusu sababu bali alichokuwa akikitaka ni kuona Dickson anafungwa gerezani tu kwa kuwa aliamua kumuacha na kumchukua mwanamke mwingine.

“Hilo hutakiwi kulifahamu! Shika hii bahasha, nadhani tutaonana mahakamani,” alisema Linda na kumpa bahasha ile.
Akaondoka, Linda akabaki peke yake mahali hapo. Alikiinamisha kichwa chake, alikuwa akipitia katika kipindi kigumu kupita kawaida.

Moyo wake ulikuwa umegawanyika, upande mmoja ulimwambia kwamba uamuzi wa kumfunga Dickson gerezani ulikuwa mbaya na hakutakiwa kuufanya hata siku moja katika maisha yake lakini upande mwingine wa moyo wake ulimwambia kwamba hakukuwa na tatizo, alitakiwa kufanya kile alichoambiwa kufanya.

“Mungu wangu! Nifanye nini mimi?” aliuliza.
Akaifungua bahasha ile kubwa ya kaki. Ndani, akakutana na noti za shilingi elfu kumi, vilikuwa vibunda vinne, kila kibunda kilikuwa na milioni moja.
“Pesa! Hizi pesa ni kwa lengo la kumfunga mtu?” alijiuliza.

Mpaka anaondoka mahali hapo hakuwa na jibu sahihi la kile alichotakiwa kufanya. Bado moyo wake ulikuwa kwenye wakati mgumu mno, wakati mwingine alitamani hata kutoroka na kwenda sehemu ambayo kusingekuwa na mtu mwingine ambaye angemuona.

Akiwa njiani, akapokea meseji kutoka kwa Linda na kumwambia kwamba alitakiwa kufanya kile alichotakiwa kwa kuwa zoezi hilo lilimfanya kutumia kiasi kikubwa cha pesa kuhakikisha mwanaume huyo anapotea.
 
SEHEMU YA 80

Alipofika, akateremshwa huku akiwa na pingu yake, akapelekwa ndani ya mahakama huku akiwa na watuhumiwa wengine. Alipokwenda kusimama kizimbani, akaanza kuangalia huku na kule.

Macho yake yalikuwa yakiangalia huku na kule, ghafla yakatua usoni mwa Linda aliyekuwa amekaa mbele kabisa. Msichana huyo hakuonekana kuwa na tatizo lolote lile, pale alipokaa uso wake ulikuwa na tabasamu pana kuonyesha kwamba kile kilichokuwa kikiendelea, kilimfurahisha kupita kawaida.

Siku hiyo ilikuwa ni ya kusomwa kwa kesi yake, alisimama kizimbani huku akiwa ameuinamisha uso wake chini. Alikuwa akilia, moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali na hakuamini kama siku hiyo alisimama mahakamani kusomewa mashitaka kwa kesi iliyokuwa ikimkabili.

Siku hiyo kesi ikaahirishwa na kupangwa tarehe ambayo ingeanza rasmi kusikilizwa. Linda aliondoka mahakamani hapo huku akijiona shujaa, alijiona bingwa kuliko watu wote katika dunia hii.

Alitembea kwa kujiamini mpaka alipolifikia gari lake na kuingia, hakutaka kubaki mahali hapo, akaondoka zake huku njiani akimpigia simu Amina na kumwambia kwamba kazi ilibaki kwake.
“Sijui kama nitaweza,” alisema Amina.

“Kwa nini ushindwe?”
“Mmh! Nitaweza kweli?”
Mpaka kufikia hapo tayari Linda akaona kama angegeukiwa na msichana huyo. Alitumia pesa nyingi kuhakikisha kila kitu kinawekwa sawa, wakati wakiwa wamemla ng’ombe mzima na kubaki mkia, akaanza longolongo kwamba aliona ugumu mbele yake.

Linda hakutaka kusubiri, hakutaka kuona akigeukiwa, akawapigia simu vijana wake na kuwaambia kwamba Amina alitakiwa kutekwa, apelekwe sehemu, ashikiliwe kwa siku mbili mfululizo huku akipewa vitisho kwamba kama asingefanya kile kilichotakiwa kufanywa basi angeuawa kwa kuchomwa moto.

“Hilo tu bosi?” alisikika jamaa akiuliza upande wa pili.
“Ndiyo! Yaani mumshikilie, mumpe vitisho, mumtese mpaka ashike adabu, na mmwambie kabisa kwamba kama hatofanya kile kinachotakiwa, basi mtamuua,” alisema Linda.

“Haina shida madam!”
“Sawa. Nawatumia milioni kumi!”
“Poapoa.”
Simu zikakatwa.

JE, nini kitaendelea?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom