Jamaa aliniharibia mbayaaaDaaaaa,huko ni kuzibiana
waoh. Hii stori n kaliSEHEMU INAYOFUATA,...................
Baada ya kutoka kukwazana na ESTA nilitulia huku msaada wangu pekee, au mtu aliyebaki ni Rose, licha ya kuwa alikuwa na umri wa mdogo sana kwangu, lakini bado alikuwa na busara za hali ya juu.
Hebu fikiria mchepuko kukupeleka hadi kwa wazazi wake si jambo jepesi mjue, niliendelea na michakato mingine huku kwa upande wa mahabusu yaani Shedy nilikuwa napokea simu na wale ndugu zake huku tukishauriana mambo tofauti tofauti.
Nakumbuka jumatatu Moja nilikuwa kwenye taasisi Moja ambayo baba yake Rose alinifanyia mpango, huku nikiwa nadhifu na mavazi safi, tofauti na kote nilikopita huku kulikuwa na watu wengi sana maarufu, wanasiasa wanaojulikana nchi nzima lakini , hata magari yaliyopark pale plate number za serikali ziliongoza.
Niliambiwa nikae sehemu nitulie, nisubiri wahusika waje, nakumbuka nilikaa kuanzia saa tatu asubuhi Hadi saa kumi huyo mlengwa hakutokea, nikaanza kuona utofauti Kati ya Sekta binafsi na serikalini, huku kulihitaji uvumilivu na subira haswa, baadaye muda ukikaribia kuisha alikuja mama fulani mtu mzima, sura haikuwa ngeni kwani namuonaga kwenye magazeti. hakika sehemu hii nilipaona pazito kila niliyemuona aliniona kama Sina hadhi ya kuongea na wewe.
How are you? alinisalimia kwa kimombo huku akiwa ananitazama usoni.
Nikaitikia salamu yake.
Unajua tangu saa tano nimekuona hapa kwani una shida gani kijana, au unataka kuchukua contract ya madaraja nini maana wengi wanachukua ili kufanya maboresho ya madaraja huko vijijini.
Akiongea kwa kejeli akitambua kabisa, sifanani na maboss wa aina hiyo.
Hapana boss Mimi hapa nimekuja kuwasilisha, maombi ya kazi hata hivyo Kuna mtu namsubiri hapa niliambiwa atakuja.nilimjibu.
Akawageukia wenzie huku wakicheka atakuwa anamsubiri (akitaja jina).
Huyo boss kaenda mkoani, na hii sikukuu hii hayo mambo sidhani kama yatatekelezwa Kirahisi aliongea
yule mama huku nikivunjika moyo .
Niliwasindikiza kwa macho, huku wakipanda kila mtu kwenye gari lake haoooo wakafunguliwa geti wakaishia, nilishindwa nifanyaje, ni kweli hata Mimi nilijua wazi kuanza kupeleka maombi ya kazi msimu ule wa sikukuu ikikuwa kama vitu vya kubahatisha tu.
Nilirudi hadi pale mapokezi nikamweleza yule mzee aliyenipokea kuwa naona muda umeisha na hakuna uhakika wa huyo mtu kutokea .
Yule mzee alinihurumia na kunisikitikia sana,
Umesema unaitwa nani,?
Ni kawaida mtu kujifanya kakusahau jina, iwe kwa bahati mbaya au makusudi, ila hupaswi kuchoka kumuelekeza jina lako, nikataja full name.
Akachukua simu yake akampigia huyo boss niliyemsubiri kutwa nzima, waliongea huku nikisikia vizuri
Maongezi yao,.
Aisee Kuna jamaa amekuja hapa anaitwa (akitaja jina langu)Sasa kwakuwa boss ulituahidi utafika leo, ikabidi nimwambie akusubiri. aliongea yule mzee huku akionesha hakuwa na uhakika wa huyo jamaa kurudi.
alikata simu Kisha akanieleza kuwa huyo ninayemsubiri yupo mkoani yaani alikozaliwa akiwa anaikaribisha sikukuu hata hivyo harudi leo wala kesho.
Tuliagana nikaondoka huku tayari mawazo yakirudi pale pale maana Kila nikichopanga kikawa hakiendi, nikiwa njiani nikamtafuta Rose maana ndiye mtu pekee aliyekuwa ananisikiliza lakini pia,
Eh niambie mpenzi wangu, vipi umefikia wapi, aliuza kwa pupa.
Mpenzi wangu wewe acha tu, huwezi amini masaa zaidi ya nane nimekaa pale lakini sijaongea na mtu jambo la maana, hivi my kwani yule mzee wako(nikimaanisha baba yake) alisema Kuna mtu anajuana naye lakini mbona kila nikipiga simu hapokei , na nikupe tu ukweli sioni dalili ya mafanikio pale.nilimwambia ukweli,.
Mmmh baby basi jaribu namba fulani ni za simu ya mezani, huenda atakupokelea kwakuwa ni simu ya kiofisi. Akanitumia zile namba,.
Nilisevu huku nikifika nyumbani nikiwa nimechoka najua si kwasababu ya kuzurura bali, kwakuwa sijafanikisha lengo langu. nilimsimulia Mke wangu akahuzunika sana,. nilifikiria Mara mbili huku nikitambua Kuna kitu hakipo sawa kwenye mfumo wa maisha yangu. Huku nikiwa naangaliana na Mke wangu hakuna aliyekuwa anajua mwenzake anawaza nini, maana najua hata yeye alikuwa kwenye lindi la mawazo.
Alifahamu fika jitihada zangu katika utafutaji wa maisha,. alifahamu fika juu ya balaa linalokuja mbele yetu ikiwa sina kazi, akavunja ukimya,
Mume wangu, naona huu si wakati wa kibweteka kumbuka Kuna kiakiba chetu kile ukiniambia niweke, unaonaje tukafungua hata kiduka fulani cha vyakula yaani mahitaji muhimu ya nyumbani, mume wangu lazima tuanze kwenye msingi tatizo wewe unaamini sana kwenye kuajiriwa, lakini kwenye ajira hizohizo naona huna bahati Nako kabisa. aliongea kwa sauti ya chini Sana iliyoonesha imekata matumaini.
Ni kweli maana najua hali itakayokuja mbele yetu si nzuri sana,. nilijibu huku nikimuonea huruma kwani sikupenda aumie Wala, apate shida.
Kila mwanaume hufurahi na kufarijika pale anapoiona familia yake ina furaha ila kinyume na hapo maumivu yake hayaelezeki.
Niliamka asubuhi, huku nikiwa sijakata tamaa bado nilikuwa na Imani, nikapanga ngoja niende Tena kule kwa Jana. Kabla ya yote nilipokea simu toka kwa jamaa mmoja akiwa ni sehemu ya wadhamini wa Shedy. Nilipokea simu tukasalimiana.
Akaanza kunikoromea
Ujue wewe Dani una dharau sana tulitegemea utatupigia simu lakini hukufanya hivyo, sisi ni majirani tu ujue lakini wewe ni ndugu yako kabisa mmetoka mkoa mmoja, lakini unajiweka nyuma wakati nyie ndiyo kila kitu. Na hapa tunapoongea nimeweka loud speaker Kila mtu anakusikia. aliongea kwa jazba yule jamaa.
Ikabidi nimwite Mke wangu kwa ishara ili asikie huku na Mimi nikiweka loud speaker.
Jamaa akaendelea kubwata.
Haya mshindi ni wewe maana uliamua kukaa kimya lengo tukutafute na ni kweli umeshinda maana, sisi ndiyo tumeshindwa ila Kaa ukijua kuwa ndugu yako anafungwa maana tumeenda jana tukaambiwa dhamana ni Hadi sikukuu ipite Sasa Kuna Nini Tena , aliongea kwa kujiamini sana.
Si kwamba sikuwa na uwezo wa kumjibu vibaya ila baada ya kuona watu wengi wananisikiliza nikakaa kimya huku nikimzuia Mke wangu ambaye alikuwa ameshakasirika mpaka namba ya mwisho.
Jamaa akakata simu.
Matusi ya nguoni aliyoyatukana mke wangu sikuwahi kumsikia tangu nimfahamu, ni kwamba siwezi kuyaandika hapa.
Sasa hapo unanitukana Mimi na wote tulioko kwenye hii nyumba. Maana hao hawakusikii. Nilimuonya
Mume wangu kwanini hawa wakugeuze kama choo cha stendi Ina maana wewe ndiye uliyemshawishi yule ms****aibe. tena kuanzia leo sitaki kusikia ukijihusisha na mambo ya watu, unajua ni mangapi umejihusisha nayo, na yakaleta matokeo mabaya, hizo huruma zako hizooo?
Ona Sasa yaani wewe miaka yote utakuwa mtu wa kutafuta kazi, badala ya kuiheshimu kazi uliyoipata ili ikuletee maendeleo unakuwa mtu wa kutembea na vihandbag Kila siku .
aliwaka mke wangu.
Nikaona kuendelea kukaa hapa nikujiletea matatizo nikaaga na kuondoka kuelekea kule kwa jana huku nikipanga kutokupiga simu.
Nikaona ni bora nikawaface moja kwa moja.
Kama kawaida niliingia kwenye ile yard huku nikitetemeshwa na Yale mandhari mazuri huku watu wakiwa wengi kila mtu akiwa busy na mambo yake.
Niliingia mapokezi, nikamkuta yule mzee na wafanyakazi wengi, akanikaribisha, chaajabu alinitoa nje nikashangaa, tunaongelea nje tena.
Bwana mdogo naona umerudi tena, bila shaka ni wewe uliyeambiwa uje na mzee(akitaja jina)ni baba yake Rose.
Akaendelea....
Samahani sana kijana wangu kwa usumbufu, ni kwamba Mimi na yule mzee tuliwahi kukutana kwenye baa moja, si unajua tena mambo ya pombe? (huku akicheka cheka)
Basi katika harakati za kufahamiana nikajikuta naropoka , nikimwambia Mimi ni afisa mwajiri hapa jambo ambalo si kweli. (Huku akitaja nafasi yake pale)
Hivyo Yule mzee mwenzangu aliniamini tukabadilishana namba,Sasa juzikati tu hapa alinipigia simu kuwa ana kijana wake, anataka nimfanyie mpango lakini tayari aliniweka kwenye wakati mgumu, hata Jana nilishindwa nifanyaje, lakini lazima nikwambie ukweli,
Mimi Sina cheo hicho lakini pia hapa ajira zikitoka huwa zinatangazwa kwenye vyombo vya habari na magazeti, hivyo wewe nenda mwaka wowote ukisikia tangazo la ajira usisite kuja kujaribu bahati yako,
Aliongea yule mzee huku nikigundua anaona aibu,.
Sasa dogo tafadhali naomba usimwambie yule mzee kuwa nilimdanganya wewe mwambie tu kuwa nafasi hakuna si unajua tena, huku akijichekesha.
Kwanza miguu ilikufa ganzi na tumbo likaanza kukata maana nilishakosa tumaini.
Sasa mzee wangu yaani hakuna namna yeyote Mimi kupata kazi. niliuliza nikiwa mnyonge.
Wewe kijana vipi bwana uambiweje huo ndiyo ukweli wenyewe mwanangu, alinijibu huku akirudi ofisini kwake.
Kweli pombe siyo chai, yaani baba yake Rose alipangwa akapangika.
niliwaza kisha nikielekea usawa wa getini, kabla sijatoka, Kuna Prado liliingia ni la kisasa ila linaonekana
Linapata suruba sana kutokana na kazi zao.
Mtu aliyekuwa upande wa kushoto kwa dereva alishusha kioo huku akiniangalia kwa muda , nilipigwa na butwaa kwani mhandisi mkubwa kabisa serikalini alikuwa akitazamana na Mimi.
Habari yako kijana ujue nimekufananisha na mfanyakazi fulani anaitwa Kelvini, Sasa nikashangaa yule tulimuacha Jana site ya mkoa huku kafikaje. aliongea yule injinia,
Aisee Boss ni kweli huyu jamaa kafanana kweli na kelvin alidakia yule dereva.
Kwahiyo wewe unaitwa nani na unataka Nini, aliuliza yule Injinia.
Naitwa(nikitaja full name)natafuta kazi.nilisema nikiwa nimenyooka kama nipo kwenye gwaride huku mkuu wa nchi akipita.
Hakujibu kitu alinishiria nisubiri huku akimwarisha dereva wake akamshushe karibu na mlango mkuu , nilichogundua ni kwamba siti za nyuma kulikuwa na njemba hata sikuziona zilipiga Jeans na fulana pamoja na buti ngumu, akaniashiria nimfuate ofisini, huku wale majamaa wakiniamuru nisiwe namkaribia boss wao,
Nilikaribishwa kwenye kiti huku, akiomba vyeti vyangu nikampatia.
Vipi mbona unahema boss vipi, aliniuliza huku wote wakicheka, ukweli ni kwamba nilimuona mtu mzito nadhani hakustahili kabisa kuongea na Mimi.
Cha ajabu hakuangalia vile vyeti ila alidili na vitambulisho vya makampuni binafsi nilikotoka.
Akaitwa afisa mwajiri ambaye alikuwa anaongea na yule mkuu huku kakusanya mikono, kwa heshima.
Huyu jamaa nimemkuta hapo nje eti anatafuta kazi, watu kama Hawa sijawahi kubahatika kuwaona huwa wanaishia kwenu tu, hivyo naomba kaangalie kama ana shahada kweli.
yule afisa akachukua akatoka, na Mimi nikaambiwa nitoke nikasubiri kule mapokezi,
Yule mzee ambaye kumbe ni tapeli tu alishtuka sana aliponiona,
Yaani wewe umepata nafasi ya kuitwa na Boss yule, huwa hadili na watu kabisa yule, sema,acha ALLAH aitwe ALLAH, kijana wewe mwenyezi MUNGU amekuona, hivyo ni vyema ukamtolea zaka na sadaka ALLAH maana Leo nimeona ukuu wa MUNGU.
Aliongea kwa kushangaza yule mzee anayedhani kila mtu ni muislamu.
Mara nikaitwa tena kule juu,
Vipi Ofisa anatufaa huyu, anatufaa tumpeleke mkoani maana kule huu mwaka ujao Kuna uhaba wakemia kule. aliuliza yule Injinia.
Anatufaa boss, ila ni vyema akabaki hapa hapa maana Kuna kitu nimegundua , huku akimsogelea na kusearch vitu kwenye desktop iliyokuwa pembeni ya boss , wakawa wanawianisha makaratasi yangu na vitu vilivyoko katika computer, wakacheka Kisha Injinia akakubali kwa kutingisha kichwa. basi utampa taratibu zote.
Huku yule mwajiri akiniambia nimfuate ofisini kwake, alikuwa ni mzee fulani wa makamo ila anajiweka kijana, kuanzia mavazi Hadi ongea yake ,
Bwana Danieliiiii we jamaa mganga wako ni yupi utuoneshe na sisi maana sikutegemea yule Boss akubali kuongea na wewe. aliongea kwa utani yule jamaa. Nikapewa taratibu zote huku baadhi ya vitu vikichelewa huku nikiambiwa kazi ni mwezi wa kwanza 2013.
hakuna Cha madam,
hakuna Cha ESTA
Hakuna Cha Shedy, nikiwa blacklist kwenye maisha yangu.
Niko na Rose sasa mtu aliyehusika nipate ajira ya heshima serikalini japo kwa ngekewa.
Itaendelea.......................
Nilikuwa mpya kama dhahabu.
Vipi
Hii inachangiwa na Hali ya kimaisha na wazazi gani wamemlea mkuu nadhani. Yanai Kuna mahusiano na Tabia zetu na hali za kimaisha tulizo nazo. Hata waliokuwa wanaofaulu shuleni enzi mkiwa shuleni nadhani ulikuwa unawaona walikuwa wako tofauti na wale waliokuwa guarantee to fail ama kufaulu kwa bahati mbaya ikitokea.umri wa mdogo sana kwangu, lakini bado alikuwa na busara za hali ya juu.
Kuitwa Boss Ni lugha ya kawaida town,sema Sasa mkuu ulikuwa na mawazo hata najaribu kuyavaa maisha yako Ni emotional pains sio ya kitoto.Akiongea kwa kejeli akitambua kabisa, sifanani na maboss wa aina hiyo.
SEHEMU INAYOFUATA,...................

Nakubali asilimia mia mkuuHii inachangiwa na Hali ya kimaisha na wazazi gani wamemlea mkuu nadhani. Yanai Kuna mahusiano na Tabia zetu na hali za kimaisha tulizo nazo. Hata waliokuwa wanaofaulu shuleni enzi mkiwa shuleni nadhani ulikuwa unawaona walikuwa wako tofauti na wale waliokuwa guarantee to fail ama kufaulu kwa bahati mbaya ikitokea.
Ungeishi shule like kibaha,mzumbe tabora boys na ilboru halafu ukaja Kama tanga technical,galanos,Moshi technical wanafunzi Tabia zao zilikuwa ziko tofauti.
Kuna tofauti ya waliozaliwa masikini wakapata pesa , waliozaliwa kwenye pesa wakaendelea kuwa nazo,walioelewa na wazazi waliosoma na wasiosoma Tabia zao ziko tofauti Kama umeishi na watu nadhani Ni rahisi kuwatambua.
Mfano mie nikija kwenye kazi yako ukiwa unanihudumua najua umeanza zero hata uwe na billions naweza nikajua kuwa ulipewa mtaji ama ulianza zero
Uongomara nyingi story za jamiiforum haziwahi kufika mwisho , hivyo tukeshe tukiomba maana lolote linaweza kutokea .
Babu m kipind niko kwenye msoto 2011-2017 nilikua muumin sana wa huo msemo, basi ikawa ndo kawaida yangu kuzunguka mashirika na tasisi ata kama Sina ahadi na yoyote, ingia huku na huko, tembea sana wapiii,Kutembea bure ndio Mana yake hii