SEHEMU YA THEMANINI NA TISA
Mzee Mgaya alikaa kwenye kiti huku macho yakiwa kwa yule Binti mgeni, Mzee Mgaya hakuwa mtu mwenye kuwachangamkia wasichana wadogo, hivyo hakuweza kumsalimia Zena licha ya kuwa yeye ndiye kamkuta, Samson yeye alizuga kuingia chumbani kwake huku masikio yakiwa huku ili ajue kitazungumzwa Nini.
Shikamoo baba, Zena alisalimia kwa sauti yenye uchangamfu.
Marhaba mwanangu, japo napata shida kukutambua. alijibu salamu ile Mzee Mgaya huku akijenga tabasamu la kulazimisha ili asimtishe Binti wa watu.
Naitwa Zena, nasoma shule ya secondary ya (akitaja jina la shule)
Nasoma pamoja na Samson, Kuna zamu tulipangiwa kuja shuleni tarehe ya Leo, hivyo sikumuona Sam, nikadhani labda kasafiri kwenda mkoani lakini nashukuru nimemuona.
Zena alijua sana kudanganya hata Sam mwenyewe alijua ni uongo kwani hakukuwa na zamu yeyote.
Wewe Sam hebu njoo , huyu si unamfahamu Sasa mbona unaenda kujificha chumbani kwako?
Au hujui kama kakufuata wewe.
Mzee Mgaya alimuita Samson.
Samson alishusha pumzi huku akimshukuru MUNGU kwani Zena hakuja na Yale ambayo alikuwa anayafikiria kuwa kaja nayo.
Mzee Mgaya aliinuka na kuingia chumbani kwake akiwaacha Samson na Zena wakipiga stori pale sebuleni, japokuwa Zena alikuwa kachangamka huku akiwa anajiamini, lakini Samson hakupenda kwani alijikuta kama anabanwa, alitamani kumwambia Zena aondoke lakini aliona si jambo zuri, akaamua kuvumilia tu.
Jana nimekuona maeneo fulani ya mnada ulikuwa kwenye meza ya mama mmoja hivi Ukiwa unaangalia nguo za watoto wachanga, ujue ulishangaza sana watu, nilitamani nikushtue lakini tuliongozana na mama hivyo nikaona nisije kuamsha masuala mengine nikatulia, ila watu walikushangaa sana, pia yule muuzaji alikumaindi sana na ni afadhali uliondoka mapema nadhani ungezubaa pale ungehisiwa ni mshirikina. Zena aliweka kituo
Samson alitabasamu huku akishikwa na uoga fulani, kwani Kila akikumbuka tukio lile aligundua ilikuwa ni hatari kubwa kwake hata hivyo alishukuru kuwa salama hadi muda ule.
Zena alionesha kumpenda Samson sana , hivyo wakawa wanapiga stori zao za shule huku Zena aliyesifika kwa kuongea sana akifunga sebule ya Mzee Mgaya kwa muda.
Honi ilisikika ikiashiria mama Kulwa anarudi, Samson alienda kufungua geti na kumpokea mama yake pamoja na Rahma.
Wapi tena mume wangu, yaani siku hizi nimegundua hutaki hata kuniona,hutaki kukaa na Mimi , kwanza hushindi hapa, hulali , umekuwa kama mpitanjia tu kwanini mume wanguuuu, huyo Tausi kakupa Nini kiasi cha kushinda huko yaani hata humchoki, ndiyo najua Mimi ni Mzee , umri wangu unaenda lakini sijazeeka kihivyo, sijui nani atatangulia kufa Kati ya Mimi na wewe, lakini kama ukianza wewe unadhani msiba utakuwa wapi baba, kama siyo hapa,ukiumwa kidogo unakimbilia hapa kwangu,Ukiwa mzima wewe ni wa Tausi. Huyu mtoto mchanga wa Rahma anasumbuliwa na hapa tunatoka hospital,unajua fika mtoto kazaliwa kabla ya miezi hivyo lazima atakuwa na afya mgogoro lakini hata kukaa dakika tatu nikueleze mambo yanaendaje hutaki, shughuli zangu nyingi zinakwama kwaajili ya Rahma na Samson, Mimi nilishamaliza kulea watoto, nahitaji kupumzika lakini Samson kanipa ulezi mpya kabisa au kwakuwa hulali hapa, usichojua ni kwamba mtoto huyu analia sana nyakati za usiku kutokana na afya yake mgogoro.
Na Rahma mwenyewe ndiyo kwanza anazaa hajui hata kumbembeleza mwanaye, anajikuta na yeye analia tu hivyo mume wangu tambua kuwa silali kabisa. Nadhani napaswa kuhurumiwa, ni matatizo ambayo kaniletea mwanao Samson.
mama Kulwa licha ya kulalamika sana lakini Mzee Mgaya hakujibu chochote badala yake alidai afunguliwe geti atoe gari Kisha akatokomea.
Heee kumbe Kuna mgeni ndani , vipi hujambo Binti yangu, mama Kulwa alisalimia huku akiona aibu fulani kwa maneno aliyotoka kuropoka muda si mrefu akiwa nje.
Zena mtoto black beauty na mzuri wa sura mwenye kujenga tabasamu zuri ,wamezoeshwa kuitwa chocolate colour,aliitikia salamu ya mama Kulwa, huku akijitambulisha kuwa ni rafiki wa Samson.
Mama Kulwa aliguna kidogo Kisha akamwangalia Samson Kwa jicho fulani lenye Shari,
Karibu sana mwanangu Mimi sijawahi kukuona naona umemtembelea Samson, aliuliza mama Kulwa.
Yes mama unajua Samson ni mwanafunzi anayekubalika sana darasani kwetu, karibu Kila mwanafunzi anamkubali kwa uwezo wake kwahiyo nimejikuta napenda kumuona hasa ukizingatia zaidi ya wiki mbili sijamuona, najua anaishi hapa nikaamua kumcheki, Zena alifafanua.
Sura ya Rahma ilibadilika haraka sana, akionesha kachukia ghafla, akamchukua mtoto wake toka mikononi mwa mama Kulwa na kwenda kumkabidhi Samson.
Samson alishangaa, si yeye tu hata mama Kulwa na Sara walishangaa pia kwani hajawahi kufanya hivyo Rahma.
Vipi mbona unaninyang'anya mtoto na kumpa Sam vipi. aliuliza mama Kulwa.
Kwani Kuna kosa lolote, kwani huyu ni mtoto wa nani, Samson ni baba yake, anastahili kushinda naye hata kutwa nzima Wala hakuna shida. Rahma aliongea kwa hasira huku akionesha wivu wa kitoto.na kukimbilia chumbani kwake
Mama Kulwa aligundua kinachomsumbua Rahma ikabidi awe mpole akainuka na kwenda chumbani kwa Rahma ili akambembeleze.
Zena mwanafunzi mjanja aligundua picha ile, akamwangalia Samson na kutabasamu Kisha akampungia mkono wa bye Sam kuashiria anaondoka.
Sasa mwanangu Rahma unadhani Samson anakaa hapa, huyu anaendelea na masomo yake Tena bado siku chache anaenda kuripoti na atakuwa anakaa huko , na unanishangaza kweli mwanangu, wewe hukupaswa hata kukaribiana na Samson, kwani kuzaa na mtu bila ndoa ni aibu tu Wala siyo sifa nzuri , mbaya zaidi unaonesha wivu mbele yangu hii inadhihirisha hukujuta hata kosa lako, usifanye hivyo mwanangu . mama Kulwa aliongea kwa upole huku akimsihi Rahma atulie.
*************************************
Baada ya siku kadhaa kupita ilikuwa ni mida ya mchana Samson na mama Kulwa walikuwa barazani Samson akipokea ushauri fulani kutoka kwa mama Kulwa ,
Siku zote mwanangu unadhani nakuchukia ama sikupendi hapana, tambua hata yote aliyoyafanya baba yako, kuhamishwa shule na kupelekwa wanakosoma akina Kulwa bado Kuna baraka zangu pia, lakini Kaa ukijua kuwa umetufanyia visa na vituko vingi sana humu ndani, hakuna mwenye akili timamu angevumilia, lakini Kuna vitu tumeamua kuziba masikio na kufumba macho lengo wewe utimize ndoto zako, Sasa nakuomba mwanangu kaza kamba hii Dunia wala haina jipya utamaliza wasichana wote wa Kila aina lakini baadaye utajuta tu kwani watakuwa wamekucheleweshea muda wako bure tu.upo umri wa kusoma na ukikupita mara nyingi inakuwa ni basi tena, hivyo kwasasa zingatia masomo, una siku chache sana kuanzia Sasa utakuwa shule mpya tafadhali tabia zako zote za kijinga ziache hapa hapa nadhani itakusaidia wewe kujitengenezea tabia njema shuleni kwenu. mama Kulwa aliongea kwa hisia na sauti ya upole sana.
Cathy mwanamke mcharuko alifika pale nyumbani kwa mama Kulwa huku akiwa kachangamka fulani hivi.
Enhee hebu jitetee siku zote hizo hujaja kunisalimia mama yako ulikuwa na maana gani? alitania mama Kulwa.
Mama wewe acha tu huwezi amini mambo yangu mengi yamekwama, mwezi huu, na hapa nilipo ni kama nimechanganyikiwa tu, Mr nikiwasiliana naye anaonekana yupo bize sana, na Kuna tetesi nimepata kuwa Kuna mzigo alipeleka nchi fulani Sasa inaonesha kazidiwa ujanja na mafioso wa huko mbele kwahiyo December imekuwa mbaya sana kwangu, gari limeharibika na baada ya kupeleka garage bei niliyotajiwa MUNGU anajua , nimeamua kuliacha tu. aliweka kituo Cathy.
Kwahiyo Binti yangu umeona suluhisho la matatizo yanayokukabili ni kunywa pombe si ndiyo? Unajidanganya, pombe ni starehe inanywewa pindi mtu akiwa na amani na kamwe usijidanganye kuwa itapunguza matatizo yako badala yake itakushushia heshima tu.halafu mwanangu haya ni mavazi gani tena,wewe ulipofikia una heshima zako ujue,angalia mavazi ya kuvaa kulingana na mazingira.aliweka kituo mama Kulwa.
Wewe mama acha tu, kwanza nina kazi yangu pale nyumbani nilikuwa namuomba Sam akanisaidie, aliongea Cathy huku akiinuka
Samson, ongozana na dada yako ukamsaidie kazi anayosema nadhani pia itakuwa vizuri maana amelewa, na uwe makini kumsaidia huko barabarani. aliweka kituo mama Kulwa.
Dakika kadhaa walikuwa nyumbani kwa Cathy, huku dada wa kazi wa Cathy akiwa bize pale Nje, yule dada alimuita Sam kwa ishara Kisha akamtahadhalisha,
Tafadhali mdogo wangu naomba usiwe unakuja hapa ujue Cathy aligombana na mumewe kisa wivu wa mapenzi na mumewe huja hapa bila taarifa kwahiyo kuwa makini usije kuwa muhanga. alionya yule dada
Samson alikaa kwenye kiti akisubiri kazi aliyoahidiwa lakini Cathy alikuwa kimya mara akae mkao huu mara hivi ili mradi amtege Samson. Lakini Samson kwa siku ile alikaa imara kama ukuta wa Berlin kwani alishapewa onyo.
Sioni ukinielekeza kazi uliyoniitia na kama haipo Mimi naondoka, aliongea Samson akitaka kuinuka.
Halafu wee naye una miaka mitatu Sasa hapa mjini lakini ushamba haujakutoka tu eeh, hebu njoo kwanza huku, Cathy alimshika Samson mkono na kumkokotea chumbani kwake, lakini Sam alimzidi nguvu na kukimbia lakini hakuwa na pakwenda kwani milango ilifungwa .
Ahaaaaa kwahiyo unanikimbiaaaaa nenda basi, si unataka kutoka?
Nenda mshamba wewe,
Kwanza najilaumu sana mtu hujiongezj, yaani nitaongea na mama Kulwa wakufukuze mpumbavu wewe
Na hujui tu kuwa neno lolote nikimwambia mama Kulwa huwa ananikubali Sasa tutaona. aliongea Cathy kwa sauti ya kilevi huku akifungua mlango na kumsukuma Samson kwa nguvu huku akimtukana.
Itaendelea......... ...............
Hahahaha tatizo Sam bwana ujana unampeleka sanaaahapana daaaah usiombee iwe hivyo
SEHEMU YA TISINI
Tena afadhali umerudi maana nakosa mtu wa kumtuma hapa, vipi ni kazi gani alikuitia ukamfanyie Cathy? mama Kulwa aliuliza.
Sijafanya kazi yoyote kwasababu dada Cathy alipata dharula.
alijibu Kwa kudanganya Samson.
Mmmmh huyu Cathy pombe zinampeleka vibaya ukute hajapata dharula yoyote bali kaenda kulewa tu lazima nitaongea naye, na kibaya zaidi akipata changamoto kidogo kwenye mambo yake hukimbilia kunywa pombe hajui kama ndiyo anaweza kujipoteza.
aliongeza mama Kulwa.
Sasa Sam mwanangu naomba uende kwenye ile grocery ya yule mama kule karibu na barabara kuu Kuna mzigo wangu atakupa, tafadhali kuwa makini njiani si unajua sikukuu hii inakaribia unaweza kuporwa
nashindwa kumtuma Sarah, kwasababu ana kazi nyingi lakini pia ni mtu mzima nashindwa kum direct moja kwa moja baadhi ya vitu.
Samson alitoka na kuelekea alikotumwa, huku akipita kwenye Chochoro alizoona kwake ni shortcut,
Hivi yule Cathy Mimi huwa ananionaje, kwa Mara ya kwanza niliweza lala naye na kudhani labda alinipenda, lakini mbona ile siku mama kanifukuza niliomba nilale kwake alikataa huku akisema nisikanyage kwake na nipunguze mazoea? Halafu leo kalewa pombe zake anakuja kumuomba mama eti nikamfanyie kazi kumbe kanitoa kijanja kusudi nikamtizie haja zake,
Ina maana moja kwa moja hanipendi na huwa namuona jinsi anavyonidharau, Sasa leo bwana wake hayupo ananiita Mimi. Siwezi kwasasa sitakubali na ikiwa atanichongea kwa mama , na Mimi nitaeleza ukweli wote hawezi kunifanya nikawa mtumwa wake.
Nikimtaka Mimi ananidharau na kuniita mshamba, yeye akinitaka basi anataka nimkubalie tu siwezi na sitaweza. alijiwazia Samson huku alichanja mbuga na kuelekea alikotumwa na hatimaye akafika sehemu husika.
Enhee vipi kijana kwahiyo unasema yeye anafanya nini? aliuliza yule mwenyeji wa Samsoni mara baada ya kumsalimiana.
Mama yupo tu nyumbani, kaniambia nije Kuna mzigo utanipa .
alijibu Samson huku akiona kama anachelewa.
Mume wangu nakuomba kwanza ujue huyu rafiki yangu huwa ana masikhara sana na sijui ni dharau hata sijui, eti ndo amemtuma huyu kijana nimpe zile pesa, akipoteza?
Pesa zenyewe ni nyingi kiasi, Sasa hizi ni dharau mno, Mimi nimekuita ili tushauriane tumpe au tutafute namna nyingine ya kufikisha huu mzigo maana huyu kijana sijui mtoto nakuwa na mashaka naye.
Yule mama alimweleza mumewe ambaye ni mwalimu mkuu wa shule anayohama Samson.
Mmmh mke wangu, umefanya vizuri kuniita, huyu ni mwanafunzi wangu namjua vizuri ni mtukutu mno na hizo pesa usimkabidhi badala yake tutapeleka wenyewe. Halafu hii familia ya mzee Mgaya Wana dharau sana tena mno, pesa nyingi kama hii unafanyaje utani na kumtuma mtu ili mradi, ndiyo maana mke wangu tangu siku ile sikupenda kusikia umeazima hela kwa yule mwanamke yaani ni watu wanajionaje sijui, na yule kijana niliyekusimulia asubuhi kuwa wanamuhamisha shule ndiye huyu yaani ana records chafu na mbaya sana shuleni kwangu.
Tena nikwambie tu kuwa yule msichana ambaye nusura amfunge mtoto wetu Sadick kwa kumsingizia eti alitaka kumbaka, Sasa hivi ana mtoto na baba wa mtoto ndiye huyu kijana,Wenyewe wamefichaficha lakini taarifa nimepata.
aliongea yule mwalimu mkuu akionesha chuki za wazi kwa Samson.
Mume wangu jambo lenyewe ni la Siri basi, mbona Kuna Binti anaitwa Catherine (Cathy)alikuwa anakunywa
Pombe hapa tangu saa nne asubuhi nilikuwa naye kaniambia mambo mengi tu kuwahusu hawa, kiufupi familia ya mzee Mgaya imekosa adabu sana tu, na mwenyewe anavyoonaga kayapatia maisha,
Na hata shoga yangu mwenyewe, yale maduka yake mawili tayari hujiona ni nani sijui lakini kifupi ni familia iliyokosa msimamo.
Mwalimu mkuu wa shule iliyo karibu na nyumbani kwa Mzee Mgaya aliinanga ile familia huku wakipokezana na mkewe na wakionesha hawajapendezwa na kitendo cha mama Kulwa kumtuma Samson mtu ambaye hawamwamini hata kidogo.
Kwahiyo huo mzigo naupata au niondoke, Samson aliuliza baada ya kuona wale wenyeji wake wanaendelea na shughuli nyingine.
Wewe nenda tu kamwambie nitaleta mwenyewe tena leo hii hii,
Yaani mpaka natetemeka , eti nikupe hii hela wewe ili uipoteze halafu nionekane sikukupa ili nilipe mara mbili eeh, ni kitu hakiwezekani,
aliongea kwa dharau yule mama na kumruhusu Samson aondoke.
***************************************
Ujue Samson umeingia hapa naona unafanya mambo yako tu hunipi majibu ya kule nilikokutuma vipi,
Kwanza mbona upo mbali mwenzetu huli Chakula leo, hebu kamuamushe na mzazi mwenzio huko, maana naye anadeeeeka sijui hata kitanda hakimchoshi! Lakini kwanza ya yote nipe mzigo wangu niliokutuma.
aliweka kituo mama Kulwa.
Ujue mama ndiyo maana unaona nakosa hata hamu ya kula, yaani mwalimu mkuu na mkewe wamenikatalia katakata kuwa hawawezi kunipa chochote eti hawaniamini, mara sitafikisha mara nini yaani kifupi sijawaelewa, na yule mama kaniambia atakuja mwenyewe atakuletea. Samson alifafanua Kisha akaenda kumuita Rahma na kurudi naye sebuleni.
Haya mama mwenye mtoto asiye na jina,nikisema mumpe jina langu hamtaki na vipi umekuwa boss humu ndani siyo, siku nyingine ujikaze mtoto wa kike bwanaa au kwakuwa Sarah yupo ndiyo unataka Chakula awe anakuletea chumbani kwako.
aliongea kiutani mama Kulwa lakini ujumbe ukifika.
Unajua Sarah wewe ni mgeni humu ndani kwakuwa huna siku nyingi sana, niseme tu kuwa huyu Samson licha ya mambo yake ya kipuuzi mengi aliyotufanyia lakini ni mtu mwenye nidhamu sana na pesa kwanza siyo mwizi, nimeshamtuma sehemu nyingi sana, lakini pia amekuwa akitumwa na baba yake kule saiti afuate pesa kiasi kikubwa Wala siyo vijisenti nilivyomtuma leo, Lakini anafikisha salama kabisa Sasa yule shoga yangu sijamuelewa?
mama Kulwa aliongea huku akiegama kwenye kiti akishindwa hata kula.
Mimi nadhani hajakosea sana, Kuna mawili aidha hana hiyo hela kaamua kuleta visingio tu, au ni kweli hamuamini Samson hasa ukizingatia wanamfahamu kama mtoto mkorofi hivyo inakuwa ngumu kumwamini.
Sarah aliongea naye kwa mtazamo wake.huku akiinuka na kwenda kumchukua mtoto wa Rahma chumbani.
Lakini geti lilisikika likigongwa kwa fujo na Kwa nguvu sana , Samson aliinuka na kwenda kufungua huku akimuuliza jina mgongaji kama ulivyo utaratibu wa watu wengi kabla ya kufungua.
Itaendelea............................

Mama Kulwa ana mdomo jamani lol!SEHEMU YA TISINI NA MOJA
Mgongaji wa geti alikuwa ni Cathy,
aliingia huku akimwangalia Samson Kwa jicho baya na kubinua midomo ya dharau, kwakuwa Samson alijua haikumpa taabu badala yake alijiona ni wa thamani huku akijisifu kimoyomoyo kwa msimamo wake.
Enhee vipi mwanangu mbona usiku hivi kuna nini, nauliza hivi kwasababu si kawaida yako kuja mara mbili hapa na saizi inaelekea saa nne kasoro hii.
aliuliza kwa mshangao mama Kulwa.
Kwanza mama Mimi nina njaa sana kama kwenye poti Kuna chakula, ngoja nile kwanza halafu nitasema ujue Leo kutwa nzima nilikuwa hivi (akionesha ishara kuwa alilewa)
Sasa vitu vimepungua ninaisikia njaa vilivyo. aliongea Cathy huku akimzuia Sarah asipakue chakula.
Aisee shoga yangu wala usijisumbue Mimi hapa ni nyumbani na huyu hapa ni mama yangu mlezi tangu miaka hiyo, hivyo nikiwa na njaa huwa napika kabisa siyo tu kula , hapa ndiyo kwa mama Jose, au mama mkwe ingawaje mwanaye Jose alinikataa mchana kweupe lakini sikuwa na namna. aliongea Cathy na kufanya watu wacheke.
Mwanangu Jose angekuweza wapi na hizo pombe, yule tangu utotoni aliipiga vita pombe licha ya baba yake na Mimi kuwa ni watumiaji lakini hajamrithi yeyote haya niambie usiku huu una shida gani.
Kwanza mama nina furaha ya mambo mawili , la kwanza nimewasiliana na Mr anasema kumbe alipata na matatizo kidogo ndiyo maana nikawa simpati, kwa maana hiyo mambo yangu yatanyooka.
Lakini pia Jambo la pili ni kuhusu gari langu , mafundi wamehangaika nalo likakubali japo kiasi walichonitajia kwa kazi waliyofanya ni kikubwa(akitaja bei) lakini nashukuru gari limepona, kwahiyo hapa nadaiwa nusu ya hela nimelipa nusu ya hela nikawadanganya kuwa hela nyingine ipo nyumbani kwahiyo wameniachia gari kwakuwa wananijua vinginevyo nisingechukua na yule fundi mkuu navyomjua kesho saa kumi na mbili asubuhi atakuwa getini ana njaa kama nini yaani Sasa mama naomba niokoe maana Mr atarekebisha wiki hii hii.
alifafanua Cathy.
Sawa nimekuelewa lakini Mimi mwenyewe kwenye akiba yangu harakaharaka hivyo Sina ila Kuna kijipesa changu kwa mtu mmoja na nilimtuma Samson jioni hii lakini ameshindwa kumpa kwa visingizio vya kijinga kwahiyo na Mimi nikuahidi kuwa njoo asubuhi saa tatu na Mimi nitaenda kuchukua asubuhi. aliongea mama Kulwa Kwa sauti yenye usingizi ikionesha mida nayo imeenda.
Yaani mama sijui twende wote kwa huyo mtu, au labda nitakuja hapa asubuhi kwa lengo la kuwakimbia wale halafu wewe ukichukua utanikuta hapahapa maana sitaki wale mafundi nionane nao nikiwa Sina hela. aliongea Cathy kwa uoga akiona labda mama Kulwa anampa Imani tu.
Siku inayofuata mida ya asubuhi sana kama ambavyo ratiba za kazi zilivyo Kila mtu alikuwa bize na shughuli zake muda ule huku Rahma na mama Kulwa wakiwa vyumbani bado, labda kwasababu Rahma ni mgonjwa na mama Kulwa ni boss.
Geti liligongwa kufungua akaja yule mwanamke ambaye alimnyima hela Samson ile Jana yake, walisalimiana.
Wewe kijana hapa hata ndani siingii, naomba niitie mama yako maana nikiingia ndani tutaanza stori na hii asubuhi Nina mambo mengi ya kufanya. alisisitiza yule mama.
Mama Kulwa alitoka huku akijifunga kitenge chake vizuri na kuja usawa alipo mgeni wake,
Mwenzangu, Jana umetulaza na njaa maana nilimtuma kijana wangu ukamnyima mzigo bwana, na ilikuwa nije asubuhi hii afadhali umeniwahi.alitania mama Kulwa.
Weeee hapana kwa taarifa tunazosikia kuhusu kijana wako huyu hakuna anayeweza kumwamini kirahisi, tena Kuna taarifa zingine tumesikia jana tu kuwa humu Kuna watoto wanaishi kama wanandoa ni huyu mtoto na binti fulani yule kama mwarabu sijui mmanga, na tunaambiwa hilo jambo mmeridhia na mmebariki kabisa, tunajua huwa Kuna bahati mbaya nyingi sana kwa watu wengi kukuta madada wa kazi wanazalishwa na mashambaboy au watoto wa wenye nyumba na hata mababa wenyewe, lakini kamwe hakuna mama mwenye nyumba hata mmoja anaweza kufurahia haya masuala, lakini kwa taarifa nilizosikia
Jana mmmmh sidhani kama unapaswa kufurahia haya mambo. nimeamua kukwambia yasiyonihusu kwakuwa wewe ni mtu mzima mwenzangu, msiri, mstiri wangu na mzigo wetu ni huu hapa. yule mama alikabidhi kiasi fulani cha pesa kwa mama Kulwa huku akitaka afunguliwe geti atoke.
Hapanaaaa, hapana Sam mwanangu usifunge geti, halafuu unaona unavyonidhalilisha wewe mtoto, ama kweli ukubwa ni jalala kwa kukuonya na kukukanya kote, leo hii naonekana nafurahia mambo yako uliyoyafanya mwanangu, loooh haya yote nitamlaumu Mzee Mgaya ndiye aliyenidhalilisha kwa kukuleta wewe lakini yote haya nasamehe na kuwasamehe wote wewe na Rahma.
Enhee na wewe mwenzangu hizi taarifa ni nani kamwambia kuwa Mimi Nina akili za kuweza kufurahia ujinga na upumbavu uliotokea humu ndani,? Mama Kulwa aliuliza kishari kiasi cha kumtisha yule mama mgeni ama mke wa mwalimu mkuu.
Mmmh dada yangu Mimi utanionea bure jambo zuri ni kwamba mambo haya nimeyasikia Jana toka kwa msichana fulani huwa nakuona naye mara nyingi anaitwa Catherine, na hajaniambia Mimi tu kulikuwa na watu wengi, hivyo Mimi usinichukie Mimi ni kama mjumbe tu. alijitetea yule mama baada ya kuona mama Kulwa anapaniki.
Wakati Sarah akijaribu kumuelewesha mama Kulwa kuwa asimchukie yule mama ambaye kwanza kwa kuongea ule ukweli ni jambo jema na kizuri zaidi muhusika katajwa kuwa ni Cathy, ilisikika honi ya gari nje, kufungua geti alikuwa ni Cathy akiwa anashuka kwenye gari kwa mbwembwe na kuingia ndani,
Cathy alionesha kushangaa uwepo wa mama ambaye ni mmiliki wa grocery ambako Jana yake alikuwa katoka kulewa hapo, sura yake ilibadilika huku akiwasalimia akina mama wale Kwa upole kwani alishagundua jambo.
Samson funga geti na jamani wote nawaombeni basi tukaribie ndani maana Kuna stori sizielewi vizuri.
Mama Kulwa aliwakaribisha wageni wake ndani.
Mdaiwa ambaye analipa deni aliingia ndani huku akilalamika kuwa anachelewa kazi zake.
Lakini pia mkopaji Cathy ambaye aliahidiwa kuwa atatimiziwa asubuhi suala lake, alionesha yupo kwenye wakati mgumu kwani alinywea ghafla.
Lakini pia Samson alijikuta anapoteza furaha ghafla kwani yale mambo kila yakiibuka basi mishale mikali kutoka kwa mama Kulwa ilimchoma yeye kwani ndiye aliyekuwa msababishaji.
Pia hata Binti mrembo na mzazi kwa kipindi hicho huku akizaa mapema kutokana na kuwa na Presha ile ya kusemwa mara kwa mara na mama Kulwa, huku afya yake ikiporomoka siku hadi siku kwani mdomo wa mama Kulwa ulimnyima raha, naye alitoka chumbani kwake taratibu huku akitambua mishale na mawe yote watatupiwa yeye na Samson, kuliko hata wale wambeya na wasengenyaji.
Itaendelea,kuifuatilia...........................
😂😂😂 Mbona Jack Daniel alishasema akiwa yupo ofisini ndio huwa anapata muda wa kuandika. Halafu huyu ni Engineer wa mabarabara inawezekana yupo site anajenga daraja la Kigongo BusisiInachelewa hadi tunaisahau tulipo ishia
Mbona Jack Daniel alishasema akiwa yupo ofisini ndio huwa anapata muda wa kuandika. Halafu huyu ni Engineer wa mabarabara inawezekana yupo site anajenga daraja la Kigongo Busisi



kazi na dawa mzee
