Simulizi: Milango ya mafanikio

Simulizi: Milango ya mafanikio

Natamani hii simulizi ingekuja Kila siku walau two episodes, lakini inashindikana kwasababu muingiliano wa ratiba.

Mara nyingi huwa napenda kuandika nikiwa ofisini kwangu kwani ndiko nakopata muda sahihi na utulivu.nikiwa nje ya ofisi muda unabana sana kutokana na majukumu mengine.lakini nikipata muda Kila kitu kitakaa sawa.

Nawatakieni,
Kwaresma njema na Ramadhan njema.
We nae acha kujikuta unaomba msamaha kwani chakula hiki useme tukikosa tutakufa? Acha usitume tena
 
Tatizo hampendi ukweli, sasa anaomba msamaha wa nini hapo? Kias nnacho cha mboga mkuu je unataka?
Kila mtu ana aina fulani ya kuwajali watu, na unaona kabisa comments za watu wanavyoomba episode na Mwandishi kaja kuomba Msamaha kwa kusema kama ulivyom quote hapo. Jifunze kunyamaza au kuwa na majibu yenye staha Mkuu
 
Kila mtu ana aina fulani ya kuwajali watu, na unaona kabisa comments za watu wanavyoomba episode na Mwandishi kaja kuomba Msamaha kwa kusema kama ulivyom quote hapo. Jifunze kunyamaza au kuwa na majibu yenye staha Mkuu
We nae mbona wewe hujajifunza kunyamaza?!
 
We nae mbona wewe hujajifunza kunyamaza?!
Sijapendezwa na jinsi ulivyomjibu Jack Daniel Mkuu, Kwanini umjibu hivyo? Hata kama ungekuwa unamlipa mtu anapotoa udhuru uwe unaelewa. Nisamehe kama nimekukwaza 🙏🙏
 
Natamani hii simulizi ingekuja Kila siku walau two episodes, lakini inashindikana kwasababu muingiliano wa ratiba.

Mara nyingi huwa napenda kuandika nikiwa ofisini kwangu kwani ndiko nakopata muda sahihi na utulivu.nikiwa nje ya ofisi muda unabana sana kutokana na majukumu mengine.lakini nikipata muda Kila kitu kitakaa sawa.

Nawatakieni,
Kwaresma njema na Ramadhan njema.
Shukrani kwa ufafanuzi Mkuu basibkutuokoa na arosto kila ukipata muda andika ata episode sita au nne bila kupost. Halafu siku unaanza kutuwekea apa ata episode 3 kwa siku

Nadhani ilo litasaidia kutoondolea manunguniko
 
Natamani hii simulizi ingekuja Kila siku walau two episodes, lakini inashindikana kwasababu muingiliano wa ratiba.

Mara nyingi huwa napenda kuandika nikiwa ofisini kwangu kwani ndiko nakopata muda sahihi na utulivu.nikiwa nje ya ofisi muda unabana sana kutokana na majukumu mengine.lakini nikipata muda Kila kitu kitakaa sawa.

Nawatakieni,
Kwaresma njema na Ramadhan njema.
Hili linafahamika mzee we piga show ukiwa na muda shusha mzigo mkuu, vinginevyo kila kheri sir.
 
We nae acha kujikuta unaomba msamaha kwani chakula hiki useme tukikosa tutakufa? Acha usitume tena

Umechafukwa Keep cool buddy harakati nyingi mzee mtu unaamka toka kumi usiku kulala sita kasorobo, energy ya kuandika itoke wapi.

Vumilia ataweka tu.
 
Aiseee sehemu stori nzuri sana na yenye kufundisha sehemu ya 10 lini mkuu??
 
Natamani hii simulizi ingekuja Kila siku walau two episodes, lakini inashindikana kwasababu muingiliano wa ratiba.

Mara nyingi huwa napenda kuandika nikiwa ofisini kwangu kwani ndiko nakopata muda sahihi na utulivu.nikiwa nje ya ofisi muda unabana sana kutokana na majukumu mengine.lakini nikipata muda Kila kitu kitakaa sawa.

Nawatakieni,
Kwaresma njema na Ramadhan njema.
Sawa mkuu.ukipata muda usitusahau.
 
SEHEMU YA SABINI NA NANE

Watu wote walikusanyika pale barazani huku Samson akiwa pembeni.

Wewe Samson sogea huku mbele tumuone acha kuwa nyuma nyuma unaogopa nini.aliongea mzee Mgaya kisha akaendelea....

Mwanangu,Binti yetu kwanza tunashukuru kwa kuchukua nafasi ya kututembelea kwa Mara nyingine baada ya kupotezana kwa muda mrefu, na pia nikupe pole kwa majukumu yako huku nikikupongeza kwa uchapakazi wako, naamini Kila kitu kitakuwa sawa kwa uwezo wa MUNGU. aliweka kituo mzee Mgaya huku Glory akiitia na kuzipokea zile pongezi.

Lakini pia Kuna watu ambao ni wageni kwako nadhani hujawahi kuwaona, hapa tunaye ndugu yako huyu anaitwa Samson nadhani taarifa zake unazo. Ni kijana ambaye yupo smart kichwani na maendeleo yake yanatia faraja , yanaridhisha kiukweli licha ya kuwa na changamoto na tabia zake baadhi , lakini ni makuzi yenyewe najua Kila kitu kitakaa mahali pake....... Kabla hajamalizia Mzee Mgaya kuongea mama Kulwa akadakia

Binti yangu Mimi mama yako siwezi kuuvumilia unafiki wa mzee wako huyu sidhani kama alistahili kutoa utetezi kama huu,
Unamuona huyu {akimaanisha Rahma}huyu ni mjamzito, ni mgonjwa huyu siyo dada wa kazi kwa Sasa Bali ni mzigo.

Huyu alikuwa anaishi kwa mama yako mdogo Tausi lakini baada ya kugombana huyu akafukuzwa na kukosa pakwenda, akaja hapa kwa kivuli Cha Mzee Mgaya kama baba yake, Mimi Kwa huruma zangu nikaona ngoja akae hapa kwa muda nikiwa na moyo wa ubinadam, baadaye nikaona ni Binti mchapakazi na mwenye kujituma sana, tukakaa chini tukaongea kwamba kwakuwa Sina dada wa kazi basi ata replace hii nafasi na ni kweli amefiti kwa asilimia miamoja.

Lakini kwasasa ni mjamzito huyu, huku kazi yote ikifanywa na Samson , huyu ni kijana aliyekosa adabu inaonesha hakufundishwa huko kijijini kwao kwasababu ni mtu mwenye makosa yenye kujirudiarudia sana, siku moja aliweza kuja karibu na kile chumba chako ambacho kwasasa analala Rahma, bila heshima akaanza kugonga mlango hakika ni kitendo kilichukiza mno, tukaongea na baba yake huyu tukamsamehe, japokuwa binafsi sikutaka aendelee kukaa hapa kwasababu hata kipindi Cha kwanza akiwa kidato Cha kwanza tuliwahi kukosana lakini baadaye baba yake alinibembeleza kuwa kule anakokaa anahisi hakuna maadili mazuri nikamwambia amrudishe huku akarudi. Lakini bado ni mtu ambaye sijui aliugua ugonjwa gani, maana huwa haelewi chochote .

(Huku akimgeukia Samson Kwa jicho baya)au una laana wewe mtoto eeh Sasa kubwa zaidi kampa mimba huyu Binti, na kunipa Mimi mzigo, huu ni mzigo hana ndugu huyu Binti si kwa hapa mjini Wala kijijini . Hata nikimfukuza anaenda wapi?
Nilimuahidi mambo mazuri mwenyewe ni shahidi haya Sasa ni mjamzito itakuwaje?

Na hata huyu mjinga Samson Mimi nilimfukuza, si kwamba nilimtelekeza hapana, nilimpa nauli ya kurudi nyumbani kijijini, kwakuwa mbele ya Mzee wako huyu , tulikubaliana kuwa itakuwa mwisho wa masomo yake na mwisho wa kukaa hapa, lakini Mzee Mgaya baba yako alianza kunilaumu kuwa kwanini nimefanya hivyo , huku akinitisha kuwa akipotea na Mimi nipotee mara atishie kuniua. Kwasababu ya ujinga na upumbavu wa Samson ambaye leo hii anasema ni kijana smart.Mama Kulwa aliropoka akionesha kukerwa sana na tabia za Samson.

Pole mama lakini hayo yote muachie MUNGU kama mlijitolea kumsomesha huyu Sam basi mna jukumu la kumkumbusha mara kwa Mara kuwa azingatie kilichomleta hapa mjini na siyo mambo yasiyofaa.
aliongea Glory Kwa upole

Nani atasoma, huyu asome? Unajua ana mangapi huyu? hawezi huyu , nakumbuka kipindi kile huyu baba yako anasema huyu apelekwe boarding na akina Kulwa nikakataa, nikamwambia tumwangalie kwanza hizo shule za gharama tutatupa hela zetu bure . Lakini ni kweli Kila kitu kimejidhihirisha, huyu hawezi kuendelea ana mambo mengi.

Sasa Rahma shoga yangu umeshakuwa Boss na wewe (huku akimtingisha bega)

Natakiwa nilete Dada wa kazi mwingine, ambaye atasaidiana na wewe huku baadaye wewe ukipikiwa na kufuliwa nguo ikiwezekana Malaya mkubwa wewe, tena huenda ndiye uliyemshawishi Samson, mmeinajisi na kuitia mkosi nyumba yangu nyie wapumbavu, lazima nifanye Misa/ibada ili niitakase hii nyumba vinginevyo itakuwa kama kambi ya mashetani . mama Kulwa aliongea kwa uchungu huku ikionekana Kuna mambo aliwekeza muda mrefu sasa kapata pakutapikia.

Mamaaa hawa bado vijana wadogo walichokifanya ni kweli wamekosea tena sana ila ni vyema kukaa nao na kuwashauri mara kwa mara maana huna namna ni wanao tayari wasamehe tu my mom. aliongea Glory huku akionekana kutopenda kinachoongelewa na mama yake lakini hakuwa na namna.
Nani abishane na mama mzazi.
Haiwezekani.

Kuwasamehe, unaongelea kuwasamehe, niwasamehe mara ngapi? Vinginevyo usingewakuta hapa mwanangu.

Glory wewe tangu tumepanga kule mjini uliwahi kumuona kaka yako Jose akifanya vitendo vya kipuuzi na kukosa adabu?
Tuliishi na madada wa kazi wangapi, uliwahi kusikia au kuhisi tu anawanyemelea?
Wanangu nyinyi mpo bright toka zamani mlikuwa mnasikia mkionywa na siyo hii takataka (Samson)
Kwani unadhani mwanangu Jose hakuwa na wasichana, natambua sana hata wewe uliwahi kunishitakia kuwa mara nyingi halali hapa analala kwa yule mtoto wa mwanajeshi lakini nilimuonya akanisikia alikuwa na heshima mwanangu na ndiyo maana kafika hapo alipo ni mwanasheria mkubwa sasahivi , hakika najivunia sana, na alivyo yule hata haridhiki bado anasoma na kuhakikisha anafikia malengo yake. MUNGU amsaidie na matunda yake tunayaona kwani tangu Hawa wadogo zako mapacha waanze masomo ya upili Hadi Sasa wapi kidato Cha tatu sisi wazazi hatujawahi kutoa chochote, jukumu kalibeba yeye wote ninyi ni mashahidi.
Lakini hiki kitoto kisamson hiki huenda siyo binadamu kamili si tunasikia aliwahi kupotea huku akiitwa mganga wa kienyeji amrudishe Sasa mtu mpaka anarudishwa na dawa unadhani ni mtu huyo siyo mtu kamili nikwambie . Mama Kulwa aliamua siku ile.

Mama usiseme hivyo (huku akicheka kivivu)Sasa mtu afariki Dunia Kisha arudishwe Tena inawezekana vipi? Ukiona hivyo alikuwa sehemu tu hakufa mama. Gloria aliongeza.

Tuachane na hayo unanishauri vipi kuhusu huyu mzazi wa kujitakia,
Hapo alipo tena amekuwa mtu wa kulala tu , uvivu umemjaa, atafanya kazi gani? Familia imeongezeka huku akiwa anatuletea kiumbe kingine ambacho mwenye nacho naye bado analelewa tu, halafu nikiongea naonekana mama Kulwa mbaya, hafai , hataki watoto wa ndugu zake, Glory mwananguu, jua kuwa unakua na kuyaendea haya. Lazima utaniunga mkono, utakuja kusema mama aliniambia .
Siku hizi hata dukani kwangu nikienda nawahi tu kurudi, nipike mwenyewe Kila kitu nifanye mwenyewe halafu pia nimpeleke hospital panapobidi, si ndugu yangu Wala jamaa yangu ni mtu tu. Yaani siku hizi nikilala nawaza ama nikifukuze lakini roho ya huruma inanijia naahirisha maamuzi yangu kifupi Hawa watoto wawili wamenikinai mno.
alizidi kulalamika mama Kulwa.

Mama nadhani sisi si matajiri wala si masikini wa kiwango kikubwa, wewe Kaa nao Hawa huyo mkuu ajae mtunze tu, ukubwa ni jalala haya ndiyo matokeo yake, Mimi sidhani kama utakosa huduma za Hawa watu , hebu kwanza tuingie ndani mama yangu, maana tusije kuamsha mambo mengine zaidi. Glory aliingia na mama yake ndani.

Mzee Mgaya licha ya mkewe kuzungumza mambo mengi lakini hakujibu chochote, ni kama hakuwepo, haikujulikana kwanini asijibu chochote, au ni heshima ya uwepo wa Binti yake? Haikufahamika.

Samson moyo ulimuuma huku maneno ya mama Kulwa yakipenya vilivyo kwenye ngoma za masikio yake alisikia neno kwa neno , huku akijua fika kumbe mama Kulwa ndiyo chanzo cha yeye asisome shule yenye hadhi na taaluma bora.
alijihurumia sana.

Rahma yeye alikuwa analia muda mrefu sana, hata macho yake yalidhihirisha alikuwa na maumivu makubwa.

Mzee Mgaya aliinuka akawasha gari na kutoka , huku ujio wa mgeni mwingine pale nje ukimfanya Samson asifunge geti na kumwacha apite kwanza.

My friend Jii (G) yuko wapi nasikia amekuja, aliuliza Cathy huku baada ya kuonana na Glory walikimbiliana na kukumbatiana huku wakionesha wanafurahi baada ya kuonana , baada ya salamu, Glory alimkumbatia Rahma na kuanza kumbembeleza Rahma.

Glory na wewe, Nini bwana watu wanayataka mwenyewe, halafu unahangaiiiiika Mimi nimekuja kwaajili yako lakini cha kushangaza upo na hicho kitoto cha kazi gani Jii (G)wangu?

Lakini Glory alihakikisha Rahma anakaa sawa Kisha akaendelea na stori .

My classmate nilikumiss sana, yaani bado hata siamini yaani, kitambo unajua my. Sema unazingua jambo moja,nilitegemea kumkuta shemeji Sasa mbona umekuja mwenyewe?
Una kazi nzuri, una life si haba Sasa shida nini au hutaki kuolewa G.
aliongea Kwa bashasha Cathy.

(Huku akicheka)
Itakuwa hivyo my friend, sema nini ujue si jambo rahisi kumpata mume sahihi ambaye ni kiongozi, baba wa familia bora hapa ndipo kwenye mtihani kwani si Kila mwanaume anafaa kuwa baba wa watoto wako, japo atakachojalia mwenyezi MUNGU ndicho kitakachokuwa, aliongea Glory huku akimkonyeza Samson aingie ndani maana stori zile pengine aliona hapaswi kusikiliza.

Itaendelea...............
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom