Simulizi: Milango ya mafanikio

Simulizi: Milango ya mafanikio

SEHEMU YA SABINI NA SITA

Mama Kulwa aliingiza gari lake ndani Kisha Samson akawa wa kwanza kushuka ili afunge geti kabisa,
Aliingia ndani na huku akishangaa shangaa kama mgeni, wakati huo mama Kulwa hakuongea chochote na Samson akaingia tu chumbani kwake . Samson aliingia ndani kwake na kuweka begi lake chini kabisa kwasababu lilikuwa chafu sana kutokana na misukosuko aliyoipata.

Alirudi pale sebuleni akiwa kama mgeni mpya licha ya njaa kumuandama, lakini hakuthubutu kumuuliza yeyote Wala kulisogelea poti la Chakula kuona kama kuna chochote kitu ili apoze njaa, akabaki katulia tu.huku akishangaa mbona Rahma haonekani lakini hakuwa na jibu ikabidi atulie tu, huku akitafakari juu ya lile tukio ambalo huenda asingekuwepo Duniani maana aliponea kwenye tundu la sindano.

Akiwa kwenye lindi la mawazo huku akiwa hajui kwanini mama Kulwa anamkwepa na kwenda chumbani kwake akasikia honi nje na kwenda kufungua alikuwa ni Mzee Mgaya kushoto akiwa ni Rahma, walishuka huku gari likiachwa nje kabisa ya fence, wakaja ndani huku Mzee Mgaya akipitiliza Moja kwa moja hadi chumbani kwake.

Pole sana Samson, pole kwa yale yaliyokukuta jana, vipi ulilala wapi kwani? Na nimemsikia baba anasema eti polisi walikukamata wakidhani ni mwizi kwani ulifanyaje? aliuliza maswali Rahma huku wakitoka nje ili wawe huru kuongea

Lakini juu ya yote nikupe pole sana hata Mimi nilifukuzwa jana ileile , nashukuru baba alinikuta hapo nje akiwa anatoka kwenye safari yake, ndipo aliponirudisha ndani akauliza sababu ya kufukuzwa, sikumficha nilisema Kila kitu, kwa muda ule alikuwa na hasira sana pengine ungekuwepo angekuumiza sana. Maana alianza kuuuliza uko wapi huku akiingia chumbani kwako kwa kupiga teke mlango, ndipo alipoambiwa umefukuzwa huku akitukana na kusema una bahati na usirudi tena ndani mwake,

Na Mimi nikaambiwa nilale kisha ikifika asubuhi nitafute pa kwenda, lakini ilipofika , alfajiri ya leo nikasikia makelele Kati ya baba na mama huku baba akimwambia mama atoke nje akutafute ulipo, na mama naye akidai atakutafutia wapi kwakuwa hajui ulipoelekea kifupi wamegombana sana, ilipofika asubuhi mama akasema hataki anione ikabidi baba anipeleke kwa mamdogo Tausi ambako Nako nimekataliwa akidai hawezi kuuguza mgonjwa.

Hivyo nilikuwa sehemu tu nimetulia kwa wauza Chakula karibu na pale kwa mamdogo, ni jioni hii nimeshangaa nikiitwa na baba na kuniambia nipande kwenye gari eti mama Kulwa ananiita wakati ni yeye alidai hanitaki. aliweka kituo Rahma.

Wewe Rahma ni mjinga sana, na matatizo yote yaliyonipata chanzo ni wewe kwanini ulinitaja Mimi kwanza una uhakika gani kama ujauzito ni wa kwangu mimi? Ni afadhali ungesingizia kuwa ulibakwa na mtu usiyemfahamu ili utunze siri.aliongea Kwa ukali kidogo Samson.

Weweee ukweli utabaki kuwa ukweli Mimi namuogopa MUNGU licha ya kuwa nimemkosea kwa kuifanya zinaa, lakini aliyenipa ujauzito ni wewe na si mwingine,
Samson, upendo wangu kwako haupimiki haya yaliyotokea ni matunda ya kile ambacho tulionywa kabla , unadhani walezi wetu wangefurahia na kuhalalisha vitendo visivyo vya kimaadili?

Tambua kuwa nakupenda Samson, na najua unanipenda, na tunapendana,Mimi si mwanafunzi kwamba labda umekatisha ndoto zangu, hapana!
Wewe utaendelea na masomo na Kila kitu chako kitakuwa sawa kama ulivyopanga, wewe ni baba mtarajiwa hivyo.............. Kabla hajamalizia sentensi yake Rahma alichapwa kibao.

Yaani wewe sijui nikuiteje, mbona unakuwa kama kichaa namna hii, umeshindwa hata kujua hatari tuliyoitengeneza wewe unataja vitu visivyokuwa na msingi kwanini,
Yaani unawaza juu ya kuzaliwa kwa mtoto usiye na uhakika naye.

Je , umewaza juu ya hatma ya wewe kukaa humu ndani?
Huna hata huruma yaani, unawaza juu yangu baada ya kuvuruga masomo, wazazi wangu ni masikini, angalau nilidhani naweza kuja kuwakomboa kwenye hili janga lakini ndiyo zangu zimefutika , halafu kuanzia leo sitaki unishirikishe juu ya hilo tumbo lako, jua sitaki wa sikuhitaji, aliongea Kwa kujikaza Samson.

Mimi siyo mjinga ila wewe ndiye mjinga kwani ulivyotoka kijijini kwako hukujua kilichokuleta huku,
Unaongea vitu Ukiwa sahihi na Ukiwa timamu ila unasahau kuwa hakuna aliyekushikia panga kunipenda mimi, ulinipenda na kunitamkia wazi unateseka juu yangu, yaani badala uteseke na masomo ujue ni namna gani utaikomboa familia yako kama ulivyosema.

Miezi kadhaa iliyopita nani alikutwa kwenye chumba cha mwenzie , ni Mimi au wewe, jitahidi kuchunga mdomo wako Mimi siyo mtoto mdogo kama wewe. aliongea Rahma huku na yeye akiwa na hasira muda ule ikabidi Samson aondoke, lakini wakati anageuka alishangaa kumuona Mzee Mgaya nyuma yao ambaye anaonekana alisikiliza maongezi yao kwa muda mrefu sana.

Nakuhurumia sana mwanangu, nashindwa kujua una chaguo gani hadi sasa, unachekesha sana juu ya ulichokifanya, sidhani kama una kumbukumbu nzuri sana, halafu mbona ukiambiwa jambo huelewi? unakuwa mwenye kurudia makosa yaleyale kwanini?

Nitawasiliana na wazazi wako ili nijue hatua za ukuaji wako zilikuwaje, isije kuwa nalea mtoto mwenye matatizo ya akili, kwasababu hata usiku wa leo sikulala nikiwaza juu ya mwenendo wako, shida siyo kosa ulilofanya shida ni hali ya kurudia mambo yale yaleyale.

Nina mengi ya kuongea na wewe naijua familia yako, namjua mdogo wangu Elias baba yako wewe, nawajua dada zangu wote asili yetu sisi ni masikini.

Hata mimi bado ni masikini kwakuwa siishi maisha niyatakayo licha ya kuwa ni Mimi pekee niliyebahatika angalau kujaribu kupambana na hawa maadui watatu japo sijafikia hata moja ya kumi siishi maisha wanayoishi watu.
Lakini bado nina nafuu mara mia kuliko yeyote kwenye familia yetu.
aliweka kituo mzee Mgaya. Huku akionesha upole ambao si kawaida yeye kuwa nao.

Samson alipiga magoti kama ishara ya kuomba msamaha na kuonesha kujutia kosa lake lakini Mzee Mgaya akamwambia ainuke huku akimpa swali lingine,

Vipi utaendelea na masomo yako au unawaza nini, au unataka kuwa baba wa familia maana nimemsikia mwenzio anasema wewe ni baba mtarajiwa, aliuliza huku akicheka kivivu Mzee Mgaya.

Kwanza Samson miguu yake ilitetemeka, huku akionesha yupo tayari masomo na asingependa kuwa karibu na Rahma hata kidogo.

Mzee Mgaya akawataka wote waingie ndani, huku mama Kulwa akiamshwa ili aje kwenye kile kikao cha dharula.

Mke wangu kwanza pole sana, ila usiwaze kuhusu yaliyotokea chukulia ni kawaida tu, ni majukumu tumeyabeba wenyewe kwa hiari , kwenye maisha huwezi kuwa sawa kwenye Kila kitu,mambo yenyewe ndiyo haya huyu mtoto ni mjamzito hivyo tuna jukumu la kuhakikisha afya na usalama wake,
Hali kadhalika Samson, tumeshatoa pesa nyingi kwaajili yake, je tunaweza kula ng'ombe mzima ukatushinda mkia? Mzee Mgaya alimuuliza mkewe.

Mama Kulwa hakujibu bali aliitikia kwa kichwa akimaanisha lazima Samson asome.
Hali ya wazazi wake, kuwa wapole vile ni jambo lilimshangaza sana Samson alihisi Kuna kitu kinajificha ambacho hakijui huku akiamini atajua tu kwani wazee wake aliwajua vyema hawawezi kukaa na jambo muda mrefu.

Mzee Mgaya alifunga mjadala huku akimsihi mkewe atulie wala asiwaze badala yake ashukuru MUNGU Kila mtu yupo hai , akatoka huku akimwambia Samson afunge geti kwakuwa hatorudi.

Samson aligundua kuwa mama Kulwa anamkwepa hataki kuwa karibu naye , hakujua sababu ni nini lakini ilikuwa hivyo, aliendelea kutulia pale sebuleni huku Rahma akiwa jikoni akiandaa dinner kwa usiku huo.

Itaendelea....................
 
ila Abdala kichwa chini ni mpumbavu Sana.

unakuta sam anaendelea na kakosa kama kawaidai.

ila yote Tisa la kumi familia ya Mzee mgaya kuanzi yeye mwemyewe Hadi mkewe mama kulwa wanaonekana kuwa na busara Sana achilia mbali makosa madogo ya kibinadamu.

ila swali Kwa mama kulwa alikuwa analilia Nini Baada ya kumuona Sam?

point ya kushika.

wanaume tuwe na maamuzi ya kiume kama Mzee mgaya hapo inaonekana kalazimisha mama kulwa akubali matokeo
 
ila Abdala kichwa chini ni mpumbavu Sana.

unakuta sam anaendelea na kakosa kama kawaidai.

ila yote Tisa la kumi familia ya Mzee mgaya kuanzi yeye mwemyewe Hadi mkewe mama kulwa wanaonekana kuwa na busara Sana achilia mbali makosa madogo ya kibinadamu.

ila swali Kwa mama kulwa alikuwa analilia Nini Baada ya kumuona Sam?

point ya kushika.

wanaume tuwe na maamuzi ya kiume kama Mzee mgaya hapo inaonekana kalazimisha mama kulwa akubali matokeo
Mama kulwa atakuwa anampigia mahesabu Samson.inavyoonekana Tausi na Cathy watashika Mimba ya Samson.mtazamo wangu.
 
Mtunzi amewachora wahusika kwa ufundi mkubwa hasa Tabia ya mwanamke ktk jamii wengi ni wabinafsi wenye kufikiri mafanikio ya mda mfupi ya haraka na pia manyanyaso ya watu ambao siyo wa upande wao hasa watoto wasio wao.(tukokuwakubali). Na pia kuwa wadadisi na si rahisi kujua wanataka Nini na Ndo maana mzee mgaya anapata shida ya kujua Tabia za wake zake ni Kama vinyonga,wandishi umetisha
 
SEHEMU YA SABINI NA SABA

Habari nyepesi nyepesi zilizagaa shuleni kuhusu suala la Samson kunusurika kuumizwa na waliodhani si raia mwema.

Akiwa anafika shuleni kwao mida ya asubuhi , alishangaa kila mwanafunzi akimwangalia, wapo walioonesha huruma kwani walimwangalia kwa kutikisa vichwa vyao na wapo walioonesha kucheka kama ilivyo kawaida kwa sisi binadamu mioyo kutofautiana.
Samson alianza kuona noma kwa kiasi fulani kwani kitendo cha watu kukaa vikundi vikundi, huku akijua anajadiliwa yeye kilimuumiza sana.

Muda wa wanafunzi kuingia madarasani ulifika, huku Samson kabla hata hajakaa akaambiwa anaitwa na mwalimu mkuu, japokuwa alipata hofu kidogo lakini alijua anachoitiwa hivyo haikumpa taabu sana.
*************************************

Hivi unajua kama tayari umekuwa na matukio na mwenendo mbaya hapa shuleni kwetu?
Hivi kwanini siku tusiongelee masuala ya wewe juu ya taaluma yako au kukuza upeo wako, ama siku ukapewa taarifa nzuri labda kuhusu kuonesha kipaji na uwezo fulani ukajikuta wewe ni miongoni wa wanaochaguliwa kwenda shule fulani kubwa kubwa, yaani tuwe tunaongelea mambo positive yenye faida kwako. Kuna wakati natamani sana nifanye maamuzi magumu sana lakini ubinadam unachukua nafasi yake. hebu niambie mwanangu kwanini unajaribu kujihusisha na makundi mabaya , mpaka taarifa zinazagaa kuwa umenusurika kufa kwanini? mwalimu mkuu alimuuliza Samson huku akiwa kama ana uhakika kuwa Samson ni mwizi au kibaka.

Mwalimu, tofauti na nafasi yako ya kuwa mwalimu wangu, naomba basi tuzungumze kama mtu na mwanaye au mtu na baba yake,

Ndipo Samson alipojiekeza mambo mengi huku mwalimu mkuu alimsikiliza kwa umakini sana, ingawaje Samson alificha juu ya mimba ya Rahma, maana kusema vile yangeibuka maswala mengine na kujikuta anapoteza masomo. hivyo akasingizia ananyanyasika kivingine tu huku akifanikiwa kumteka mwalimu mkuu.

Mmmmh kumbe Mzee mwenzangu naye familia yake haina msimamo hivi, Sasa mtoto wa ndugu yake unawezaje kulala nje, hata kama hakuwepo pindi unafukuzwa lakini kitendo cha mkewe kuwa na mamlaka kama hayo ni dhahiri Mzee mwenzangu Kuna mahala kakamatwa. aliongea mwalimu mkuu huku akionesha dharau kwa Mzee Mgaya kwa kile ambacho ameshindwa kusimamia.

Baada ya maelezo yale Samson aliruhusiwa aende darasani huku akipewa pole na mwalimu mkuu, kwa kile alichodai anateswa, laiti mwalimu naye angejua Wala asingesema.

Samson aliingia darasani huku wanafunzi wachokozi wakimuita marehemu, wengine wakidai kwanini alinusurika maana wangepewa hata likizo ya wiki nzima kwa kuomboleza msiba wake, maneno ya utani wa kawaida na wenye kuudhi yalikuwa mengi, lakini yote Yale hayakumsumbua Samson, yeye alishukuru kuwa anaendelea na masomo yake basi hakuwa na lingine.

Muda wa mapumziko pia alitafutwa na Madam Silvia,

Wewe vipi tena kwa habari nilozisikia jana, maana niliumia lakini sikuwa na namna ya kuweza kufanya chochote, nilitamani kufika kwenu kuuliza lakini........... any way tuachane na hayo, ilikuwaje hadi kuhisiwa mwizi? aliuliza Madam.

Samson alieleza mkanda mzima huku Madam Silvia akiridhika na majibu Yale.

Mdogo wangu pole sana, inatakiwa umuombe sana MUNGU juu ya haya mambo yako, maana ipo siku utaingia kwenye magumu zaidi, vipi ulivyoitwa na Headmaster hujasema ulilala kwangu?
aliuliza Madam.

Hapana Madam Sasa Mimi ningewezaje kusema nimelala kwako huoni kama ningeleta matatizo, Mimi nimemwambia nililala kwenye mtaro tu
alijibu Samson.

Kumbe una akili mi nikajua tena utafunguka ukidhani Mimi nitaonekana Nina moyo mzuri kumbe watu wangehisi vibaya, yote kwa yote Ishi kwa heshima hapo kwenu na omba sana MUNGU maana matatizo yako si ya kawaida.
Samson aliingia darasani huku akiwa busy sana na mambo yake, japo Kila mwalimu aliyeingia kwenye kipindi alitaka Samson ajieleze ilikuwaje akahisiwa kibaka jambo ambalo lilimnyima raha.

Maisha ya shule na kitabu kwa Samson viliendelea kama kawaida huku akiacha baadhi ya vijitabia na kujenga Imani kwa kiasi fulani kuwa huenda Samson kaachana na mambo ya kijinga.

Miezi mitatu baada ya ule upepo mbaya kupita, Samson alirudi nyumbani akitoka shule akamkuta mgeni,
Si mwingine alikuwa ni binti wa Mzee Mgaya aitwaye Glory akiwa anaongea na mama yake barazani.
Samson alisalimia, Kisha akatambulishwa yule mgeni ambaye hajawahi kumuona.

Huyu ni dada yako anaitwa Glory ni Daktari kama Mimi japo yeye ni wa kisasa zaidi kwani Elimu yake simfikii kaniacha mbali sana. aliongea mama Kulwa huku wote wakifurahi.

Karibu Samson, kama alivyokuelekeza mama Mimi ni second born kwenye hii familia , au dada mkuu.halafu Mimi ni mmbea hata sijui kwanini,nitahitaji kuona mitihani yako kama hutojali.Glory aliongea kwa utani huku wote wakicheka kwa furaha.

Hapana dada, kwanza nitafurahi subiri niingie ndani nakuletea, pia usisite kukosoa pale unapohisi nilichemka. Samson alijibu Kwa kujiamini na kuwafanya watu wote wacheke.

(Glory akaanza kumuita Rahma)
Dada, Dadaaa , eti mama anaitwa nani huyu, nataka aniletee maji ya kunywa jamani dah.
aliongea Glory.

Atakuwa amelala, wewe Sam hebu mletee maji dada yako, alijibu Mama Kulwa huku akimtuma Samson.

Mamaa , mbona sielewi dada wa kazi analala? Why alale anaumwa?
aliuliza Glory.

Mwanangu wewe acha tu ni mjamzito hivyo muda mwingi namwacha apumzike, na mimba yake inavyomtesa hadi huruma maana mwanzo tulijua labda ni nanii tu lakini kwa sasa dah. aliweka kituo mama Kulwa.

(Glory akacheka kwanza)
Sasa my mom, ndiyo mmefanyaje kumleta housemaid mjamzito?
Mbona sielewi? Mwanzo nilikuuliza kuwa yule Mary yuko wapi ukasema alishaondoka na uko na msichana mpya ambaye ndiye yule uliyenitambulisha, Sasa kuwa na msichana wa kazi mjamzito tenaaaaa......... glory alishindwa kumalizia sentensi yake huku akimwangalia mama yake.

Mama Kulwa alitabasamu huku akionesha ana hasira kwa mbali Kisha akamuashiria Samson aingie ndani. Samson akajua fika Nini kitazungumzwa pale, akaingia chumbani kwake huku akitoa makaratasi yake ya mitihani huku akichagua yale aliyopata alama za juu tu , ili muhusika asije kukosoa sana.

alitoka nje na kumkuta mama Kulwa hayupo Bali yupo dada yake glory pamoja na baba yake Mzee Mgaya, Samson alisalimia Kisha akawaacha Daddy and Daughter wakiongea na kufurahi kwani hawakuonana kwa kipindi kirefu sana .

Alirudi ndani na kumkuta mama Kulwa akiwa yupo na Rahma wakiwa wanakuja nje pale barazani, huku mama Kulwa akimuita Sam kwa ishara kuwa naye anahitajika kule nje.

Itaendelea............... ...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom