Simulizi: Milango ya mafanikio

Simulizi: Milango ya mafanikio

SEHEMU YA SABINI NA NNE

Siku ya jumatatu wakati Samson anarudi nyumbani alimkuta mama Kulwa akiwa na Cathy wanaongea huku Cathy akiwa anacheka kila muda Samson hakujua nini kinamchekesha yule dada, aliwasalimia Kisha akaketi huku akitoa barua fulani waliyopewa shuleni na kumpa mama Kulwa.

Jamani vipi tena barua, umeharibu nini wewe, na kama ni hivyo siendi kwa mambo ya kipuuzi Mimi, mmezoea mambo ya kijinga utamsubiri baba yako nakwambia.
alilaumu mama Kulwa akiwa hata hajafungua barua ajue ina nini ndani.

Aliisoma kwa muda Kisha akaiweka pembeni, kumbe ni habari za mwaliko Mimi nikajua tayari kayazua huko. alisema mama Kulwa huku akimwangalia Cathy wote wakacheka.

Basi mama yangu fanya kama nilivyokuelekeza, umelea watoto wako vizuri kwa ethics safi kwanini aje akutese mtoto wa mtu , afanyiwe abortion tu ili kuepuka matatizo yasiyo ya lazima, kwanza huyu atakuwa mzazi wa kwanza Kuna vitu chungu mzima vitajitokeza kama operation, pia mtu kuumwa muda mrefu, na pia unakuta labda mtoto aliyezaliwa naye ana matatizo, eeh mama lazima hili suala uliangalie kuanzia muda huu, litakuletea shida baadaye utashindwa kufanya kazi zako ukiuguza mgonjwa. alishauri Cathy ambaye ni mtu wa karibu mno na mama Kulwa, pia ni born town akiwa anajua vitu vingi hususan bidhaa mpya na matoleo ya nchi mbalimbali hivyo ni mtu ambaye huwa anasikilizwa sana.

Samson akiwa anakula alisikia Kila kilichoongelewa na wawili wale lakini pia alitamani kujua Rahma yuko wapi maana hakumuona.

Sasa shoga yangu kwanza nimekusikia, japo kwa suala la kutoa huo ujauzito sijakuafiki bado, mimi nashauri aitwe Tausi hata kama hawana udugu wowote lakini ni mtu anayemfahamu Rahma tangu akiwa mdogo, Mimi nataka atoke hapa kwangu tu basi, wewe mwenyewe unaona amekuwa mtu wa kulala tu hafanyi kazi sijui hiyo mimba ndiyo inatafuta pakukaa hata sijui.na ndiyo maana nimemtuma sokoni aende kwa miguu ili apate kujinyoosha.
aliweka kituo mama Kulwa.

*************************************

Jioni ile kulikuwa na watu wanne wote wanawake, akiwemo mama mwenye nyumba
Mama Kulwa,
Tausi, pamoja na dada yake,
Na Rahma ambaye ndiye main character kwenye kikao kile, huku Samson akifukuzwa asishiriki hivyo ikawa ngumu kujua Nini kimezungumziwa.

Akiwa karibu na getini mithili ya mlinzi akiwa anajisomea nyakati zile, alisikia sauti ya mama Kulwa ikimuita ikabidi akusanye vitu vyake vyote, akaingia ndani, sura alizokutana nazo hazikuwa na tabasamu siyo mama Kulwa wala Tausi wote walimtazama Samson kwa macho mabaya sana.

Nilikwambia Sam,
Njia ya muongo sikuzote ni fupi nilikuuliza ukakataa na kuapa viapo vyote lakini ukweli umejulikana Sasa nakuomba uchukue vifaa vyako vyote nakuomba tu kwa ustaarabu uondoke sikuhitaji. hakuonesha masihara mama Kulwa.

Dada ni kweli kabisa huyu mtoto ni mshenzi, tena ni hafai hata kuwa naye karibu nakuomba fanya chochote dada Yangu. Tausi aliongea kwa uchungu kuliko mtu yeyote huku Samson pekee akijua kwanini Tausi anaumia kuliko wote, pengine ni baada ya kuujua ukweli aliokuwa anauhisi siku nyingi ila akawa hajathibitisha.

Samson alichukua begi lake huku akiwa haamini anachokiona, licha ya kuganda ganda pale getini lakini hakuna aliyemuonea huruma, wote walikuwa wa moto sana kiasi cha Samson kukosa mtetezi.
Mama Kulwa alifungua geti kwa nguvu huku akimsukuma Samson kwa nguvu ili atoke nje huku akimrushia kiasi fulani cha pesa ikiwa ni nauli ya kurudi kwao mkoani.

Mpuuzi sana wewe nimekuvumilia mangapi, tumekusaidia mangapi, kwahiyo ukakosa adabu ndani mwangu Mimi na baba yako tu********,halafu na wewe ufanye hivyo hivyo mtoto mwenye laana wewe, nasema hapa kwangu hutokanyaga na mzee Mgaya hawezi kunifanya chochote kwakuwa hapa ni kwangu na kama atakurudisha nitahakikisha hapa kwangu hukanyagi mpuuzi sana wewe. aliongea mama Kulwa akiwa anarusha maneno huku Samson akiwa nje ya fence majirani kadhaa walianza kutoka kwani ilikuwa si kawaida kwa mtaa wao kusikia matusi kama sehemu zingine.

Samson alikaa chini Kisha akacheka, si kicheko cha furaha bali akiwa haamini yaliyotokea kwani kwa muda huo ilikuwa kama ndoto kwake.

Muda ule aliwaza wapi aende, ingekuwa Tausi hayupo pale angeenda kwake, lakini alishajua Tausi kachukia zaidi, aliwaza huku akiwa hajui afanyaje .

Baadaye wazo likamjia, aende kwa mjumbe wa mtaa wao, alipofika pale alijieleza na kusikilizwa vizuri sana tu lakini mjumbe alikataa kumpa hifadhi.

Mwanangu siwezi kukuhifadhi hapa, wakati kwenu ni hapo tu na Dunia imebadilika mno, hatujui una matatizo gani kiafya, ukitufia kwa mawazo je, unataka kutusababishia matatizo, wewe nenda mbembeleze mama yako muombe msamaha , atakuelewa tu. alishauri yule mjumbe.

Mume wangu acha kuzunguka sisi wenyewe tuna watoto wa kike hapa na milango si mizuri akiamka usiku kwenda kuwabaka watoto wetu! Mtu mwenyewe anakwambia kampa mimba mtu, Mimi simuhitaji.
aliongea mke wa mjumbe aliyeonekana ni mwenye mdomo sana.

Samson aliwaza kitambo kidogo akaona suluhisho ni kwenda kwa Cathy tu, kwanza yule bwana wake Cathy ameshaondoka zake ughaibuni, alijua wazi Cathy atampokea tu, akaanza kupiga hatua za haraka huyooo mpaka kwa Cathy.

Aligonga geti muda mrefu sana lakini halikufunguliwa, baadaye sana alitoka dada wa kazi huku akimlaumu Samson kwa usumbufu kwani watu walishapumzika,

Simama hapohapo ngoja nikamwite na jua huwa haruhusu kumfungulia mtu usiku, subiri aje akufungulie mwenyewe, aliongea yule mdada.

Eeenhee sema wewe nini usiku huu mbona unatutisha, Cathy aliuliza.

Samson ikabidi ajieleze yale yaliyompata masaa machache yaliyopita.

Kwahiyo nikusaidie nini, mshamba mkubwa wewe, wazazi wako ni masikini, Mzee Mgaya kajitolea kukusomesha, badala ya kusoma unaendekeza mambo ya kijinga , halafu kumbe wewe ni malaaaayaaaa eeeh unaonekana mpole kumbe ni mshenzi, Sasa nikwambie kitu kunilala Mimi isiwe sababu ya kunizoea na kuja hapa ni marufuku , Mimi siyo ndugu yako. aliongea Cathy kwa sauti ya chini ili housemaid wake asisikie lakini ilikuwa sauti yenye amri kuu. Akafunga geti.

Samson alipoteza tumaini kwani sehemu aliyoitegemea ndiyo hivyo tena huku akiwa hana mtu yeyote anayemjua , alianza kutembea akiwa hajui aelekee wapi na usiku ulianza kuthibitika zaidi baada ya kuwa watu aliokuwa anapishana nao wanapungua na hata magari yalianza kupungua barabarani, huku hali ya utulivu ukianza kushamiri , hakuwa na saa akashindwa kujua ni saa ngapi, ila aligundua ni usiku mnene.

Aliamua kwenda kwenye baa moja ambako alikuwa anasikia makelele kwa mbali Lakini napo aligundua watu wanapungua huku gari fulani ndogo ikiwa inapakia vyombo vya muziki kuashiria kulikuwa na tafrija fulani kwenye baa ile na Sasa imeisha, akiwa yupo yupo hana la kufanya alisikia sauti ya mtu anayemfahamu, ikabidi asogee pengine atapata msaada.

Ila huyu alichotufanyia siyo kabisa yaani ndugu zanguni, Sasa kwanini atulete baa , kakosa hata viukumbi vidogo akaona aje huku, na sisi wengine hatulewi mapombe kama wao haoni kuwa hajatutendea haki? japokuwa Leo nimeonja na hapa inanitesa kweli hiyo wine,
alikuwa ni Madam Silvia akiwa na wanawake watatu wakilaumu jambo ambalo Samson hakulijua.

Wote watatu walishtuka baada ya kuona Kuna mtu anawasogelea,
Wewe ni nani na unamtaka nani ,
aliuliza mwanamke aliyekuwa mbele zaidi kuliko wenzake.

Naitwa Samson Mgaya nimeisikia sauti ya mwalimu wangu nilikuwa naomba msaada,alijibu Samson.

Wewe mtoto usiku huu unafanya nini hapa na ni mwanafunzi, huoni hata aibu jamani hebu njoo kwenye mwanga, alijibu Madam huku wengine wakicheka na kusanifu.

Samson alijieleza sana huku akipindisha ukweli maana alijua kwa kusema wazi kosa lake hatopata msaada hivyo akaamua kutunga kosa lingine lenye unafuu.

Mmmmh watu wengine bwana Sasa unamtoa mtoto wa mtu kwao Kisha unakuja kumzurulisha usiku huu eti kakukosea Sasa si Bora umrudishe kwao Tena kwa kumpandisha kabisa kwenye gari, sasa hapa akivamiwa na vibaka . walilaumu wanawake wale wawili.

Mara gari fulani ndogo ilikuja ikiwa Ina kazi ya kuwabeba watu wale na kuwapeleka makwao.

Sasa ndugu zanguni kwakuwa huyu kijana namfahamu naondoka naye na kwangu siyo mbali nyie pandeni gari Mimi naondoka naye taratibu.

Baada ya muda fulani walifika huku wakipiga stori mbalimbali pale sebuleni na muda mwingi Madam alimtoa hofu Samson kuwa asijali atamsaidia tu.

Sasa mwenzangu sijui hata utalala wapi maana chumba hiki kimejaa vyombo tu, na kingine kipo na kina kitanda japo hakuna godoro, sijui ujikunje hapa hapa kwenye kiti masikini, ni saa Saba hii ujue ,
wewe tena usitafute usingizi, wewe jali umepata tu hifadhi unataka kuniambia usiku huu ungeenda wapi,
aliongea madam huku akionesha naye ana usingizi maana muda nao ulienda (kulikuchwa)
Samson hakujibu neno, akawa anamwangalia tu madam,

Yule Madam aliingia ndani akakaa zaidi ya dakika kumi asitoke hii ikampa hofu Samson kuwa kwahiyo nitalala kwa kuegama tu, baadaye alisikia sauti ya Madam yenye usingizi na uchovu ikimuita, akaingia ndani akakuta Madam kalala huku akiwa kajitupa huku akiwa na harufu ya pombe kwa mbali.

Wewe Samson Mimi Sina namna ya kukusaidia kwanza nimechoka, we kung'uta miguu panda kitandani ulale. aliongea Madam Silvia huku akionesha pombe aliyokunywa inamzingua sana.

Itaendelea......................
Maskini Samson, ulivyo malaya sasa unaweza kumparamia madam usiku wakati matatizo yako ndio kwanza yameanza
 
Hizi ndio swaga za wanawake unapokuwa huna faida kwao.
Cathy hata hamu hanaye,tausi ,pia mama kulwa. Nadhani hapa Baba yake mdogo/mkubwa ndio anatakiwa aonyeshe uanaume ,hizi mambo Ni za kawaida. Huyo dada Ni mtu mzima ,binadamu wanahitaji nahitaji yao,wanawafungia wanadhani itakuwaje.
Rahma akaamua kuanika kila kitu wazi kisa dharau na biti za Samson Ila angeweza kumtetea.

Yaani akiachia umasikini uzidi kuenea kwa ndugu zake ,wakati Samson kitabu kinaweza kumfanya akabadili kwao mazima ikawa history.
Na Tena alivyo Kama mwarabu Koko atashobokewa kazini utashangaa anapendwa pendwa anapewa teuzi mpaka na sa100
Ahahahahah eti uteuzi.....huko ofisini samson atawafyeka wanawake wote
 
Purukushani moja hv enz za usichana Wang khaaa basi tu naogopa kusimulia hako kastor Mkuu
Hata mimi episode imenikumbusha mbali sana, enzi hizo niko fomu foothough sikufuzwa lkn nilisepa home saa sita usikutumetoka mbali na kupitia mengi
 
kidogo ifanane na ya kwang sema Huwa nkikumbuka nataman kujipiga vibao walahi vile
 
  • Kicheko
Reactions: ram
SEHEMU YA SABINI NA TANO

Samson aliwaza mambo mengi akiwa pale kitandani huku akiwa na mawazo mengi, alishindwa wa kumlaumu akijikuta kila lililoendelea hakuna aliyemuonea.

Aligeuka alimwangalia Madam ama mwalimu wake, akagundua usingizi umeshamchukua, akaamua kuinuka pale kitandani na kuja sebuleni lengo likiwa ni kutafakari upya nini kifanyike aliziangalia zile pesa akiamini ni kweli zingeweza kumfikisha nyumbani kwao mkoani lakini aende akafanye nini, wazazi wake wanategemea siku mtoto wao akirudi aje na habari njema Sasa itakuwaje ikiwa tofauti?
aliwaza sana Samson.
Usingizi ulimchukua saa ngapi hakujua, alishtuka akiamshwa na Madam pale kwenye kiti huku akishtuka baada ya kuona mandhari tofauti na akili ikirudi akigundua yupo ugenini na si kwa mama Kulwa.

Hujambo Samson,
Alisalimia Madam.

Samson akaitikia Salamu ile, huku akimpa heshima yake mwalimu wake.

Nakumbuka nilikwambia uje ulale ndani Sasa huku ulikujaje? aliuliza Madam.

Ni mawazo tu mwalimu, nadhani hata Jana sikukusimulia ipasavyo kifupi sioni nikiendelea na shule kwani watu ninaowategemea hawataki hata kuniona.
alijibu Samson.

Sawa, Sasa sijui itakuwaje maana usiku ule nimekuonea huruma ndiyo maana nikakupa hifadhi, lakini suala la wewe kukaa hapa haiwezekani, nadhani mchana huu inatakiwa utafute namna ya kuwasiliana na wazazi wako ili mjue mnayajenga vipi, lakini hapa kwangu haiwezekani tena kwanza mazingira yenyewe umeyaona tunawezaje kuishi wote lakini pia haiwezekani Mimi nikakaa na mtu ambaye sijui kafanya kosa gani, haiwezekani.na Sasa najiandaa kwenda shule na wewe inatakiwa uitumie siku hii ya leo vizuri uhakikishe unapata jibu aidha urudi kwenu kama unavyosema au upatane na walezi wako. Mimi sina cha kukusaidia na halafu familia yako wale wazee ni watata sana ni ngumu mtu kwenda kukuombea msamaha ni wajuaji sana. aliweka kituo Madam huku akimlazimisha Samson atoke akaangalie ustaarabu mwengine mbele.

Samson aliingia mtaani na begi lake huku mawazo yakizidi kumsonga, pengine umri na alichofanyiwa ilikuwa tofauti, aliendelea kuzunguka asijue anaenda wapi, aende kwa mama Kulwa ili aombe msamaha, akahisi hatasikilizwa, au aende basi kwa Tausi ili angalau apate utetezi lakini akikumbuka Tausi ndiye aliyekuwa anashikilia na kutoa msimamo wa yeye kufukuzwa.

Wazo likamjia kuwa Mzee Mgaya ana marafiki wengi sana tena wa maana anaweza kuwafuata baadhi awaeleze yanayomsibu pengine atasikilizwa, lakini Kila akijaribu kuvuta picha namna atakavyoulizwa maswali na ikiwa atasema ukweli basi ataonekana ni kijana asiyekuwa na adabu basi alikata tamaa hakutaka tena.

Hadi kufikia saa tisa alasiri hakuwa ametia kitu mdomoni, pesa alikuwa nayo lakini hakuwa na hamu ya kula mawazo yalimvuruga sana. alitafuta sehemu ajipumzishe baada ya kuzurula muda mrefu, akiwa hana hili Wala lile ghafla Kuna gari ilipaki karibu na yeye huku wakishuka watu watatu wanaume wawili na mwanamke mmoja huku dereva wa gari akiwa hajashuka kwenye gari.

Mwanaume mwenye miraba minne huku akiwa nadhifu kimavazi , alianza kumuuliza maswali kadhaa Samson.

Sihitaji salamu yako ni kwamba nataka kujua wewe ni nani na unafanya nini hapa, Kuna watu Wana wasiwasi na wewe kwani tangu asubuhi unazunguka mtaa mmoja kiasi cha kuwatisha wakazi wa eneo hili , hawakuelewi. aliongea jamaa huku akiwa makini .
Licha ya Samson kutaka kujibu lakini alitupiwa swali lingine ikawa ni ngumu kujibu, ajibu swali lipi aache lipi.

Unaona afande huyu ni mwizi Hawa wanatabia ya kuchora ramani mchana ili usiku iwe rahisi kuja kutuibia . alizidi kuchochea moto mwanamke aliyekuwa pale.

Wewe mama usijali, Hawa ndiyo tunawatafuta siku zote, alijibu yule afande ambaye alianza kupekua begi la Samson huku akizikuta nguo za shule,

Heee jamani majirani huu ni ushahidi hii sare ya shule ya (akitaja jina)

Ndiyo , masikini kumbe huyo mtoto mwizi eeeh, yaani ukute amesababisha mtoto wa mtu asiende shule kwa kumuibia. alizidi kuchochea moto mwanamke yule huku afande akimzuia Samson asijibu chochote, licha ya kujitetea mara nyingi lakini walimwambia ni mwizi na akae kimya, aliendelea kupekuliwa huku msala ukawa mkubwa zaidi baada ya kukutwa na kiasi fulani cha pesa, alianza kupigwa na yule afande huku wananchi wenye hasira Kali wakimtaka afande awaachie ili wadili naye maana wamechoka kuibiwa lakini walizuiliwa na afande mwingine ambaye alibaki ndani ya gari kama dereva lakini kwa kuokoa maisha ya Samson aliamua kushuka kwenye gari huku akiwa na silaha na kuwafanya baadhi ya raia warudi nyuma huku wakitukana matusi yote ya Duniani.

Mtoto mdogo umri huo ulipaswa uwe shule, lakini unaiba unadhani wizi utakufikisha wapi na leo hii ungekuwa ni marehemu mjinga wewe, mshukuru huyu afande , alishuka kwenye gari na kukutetea Mimi ningekuwa peke yangu ningewaachia wakugeuze kama nyama, aliongea yule afande huku Kila saa akimpiga vibao Samson., Huku Samson Kila akijaribu kuongea maafande wakimzuia na kumwambia akiendelea kuwasumbua watamshusha katikati ya raia ashughulikiwe.

Walifika naye kituoni huku wakimsukuma na kumwambia avue viatu tayari kuwekwa Lock up kama mahabusu, Samson aliomba MUNGU kimyakimya huku sauti ya mama yake mzazi ambaye yupo kwao kijijini ikimwambia mwanangu kumbuka kusali, kwenye Kila hatua ya maisha na masomo yako mshirikishe MUNGU. Kauli ile alipewa siku wakati akisindikizwa kwenye kituo cha basi tayari kuja jijini Dar es salaam mahali anakoishi baba yake mkubwa Mzee Mgaya.

Wewe mjinga vua viatu , unajiliza nini, unatafuta huruma , yaani unajifunza wizi ukitegemea nini, unadhani serikali imelala eeh hebu kwanza sogea huku mpumbavu wewe. aliongea mmoja wa maaskari waliokuwa pale huku wengine wakicheka sana. Wakati huo Kuna afande alishangaa kuona kumbe anayeambiwa ni mtu anayemfahamu.

Hebu afande subiri kwanza huyu mtoto mbona kama namfahamu, huyu anakaa kwa yule mzee wanamuita nani sijui, kwao siyo mbali ni kama robo saa tu, eti unaitwa nani wewe na kwanini uibe. aliuliza mmoja ya maafande waliokuwa pale kaunda

Ndipo Samson alipoanza kujieleza vizuri huku akiwa haachi neno maana alijua ukweli utamuweka huru.
maaskari waliangaliana huku wakiridhika na maelezo Yale kwa kiasi fulani hata wale ambao walimpa kichapo kwenye gari walianza kuona huruma huku wakitoka nje kwa kuzuga Wana majukumu mengine.

Lakini msiamini maneno yake huyu kijana lazima mzazi wake aje hapa aturidhishe kama ni kijana wake, hatuwezi kukubali kirahisi, au hamjui wezi na vibaka wanavyojua kugeuza maneno na kujieleza vizuri, alizidi kupigilia msumari afande mmoja aliyekuwa anahesabu hela za mahabusu fulani aliyetoka kupewa dhamana na jamaa zake.

************************************
Mama Kulwa alifika pale kituoni huku akimalizana na maafande na kumchukua Samson, mama Kulwa alimwangalia Samson huku wakiwa hawajasalimiana na hawajaongea lolote, mama Kulwa alitia gia huku Samson akishangaa mama Kulwa akiendesha gari kwa mkono mmoja mwingine akifuta machozi huku akiwa hataki Samson ajue kama analia. Gari ilikuwa inaelekea sehemu siyo lakini Samson hakuuliza kitu hatimaye wakafika kwenye zahanati moja iliyokuwa inasifika kwa huduma nzuri , baba tafadhali mwambie daktari Kila kitu usimfiche sehemu yeyote unahohisi una maumivu nayo. aliongea mama Kulwa huku akionesha ni mnyonge sana. Haswa baada ya kulaumiwa na polisi kuwa kwanini anachukua majukumu ya kumfukuza mtoto mdogo nyumbani Tena nyakati za usiku, na kusababisha raia wamuhisi mtoto vibaya hali ambayo ingepelekea kupoteza maisha ikiwa raia wangejichukulia sheria mkononi, huku polisi wakijivua na kudai wao hawana makosa.

Samson alipewa matibabu kisha akatoka huku daktari akimshauri kuwa akiona mabadiliko basi asisite kurudi tena,wakati anafika pale reception alishangaa kumuona Mzee Mgaya ambaye alimfuata Samson na kumkumbatia huku akimbusu kwenye paji la uso.

Mmmmh mke wangu, unajua huyu mtoto tungempoteza leo,aliongea Mzee Mgaya huku akiwa bado kakumbatiana na Samson.

Baba Jose naomba acha habari hizo utaniumiza mwenzio , hapa nilipo moyo unanienda mbio ningeanzaje kuwaambia kule kijijini, aliongea mama Kulwa huku safari hii machozi yakiwa hayajifichi.

Mzee Mgaya alipanda kwenye gari lake na kutokomea sehemu nyingine, huku Samson akipanda gari na mama Kulwa na kurudi nyumbani wakiwa hawaongei chochote njiani.

Milango ya mafanikio ipo mingi sana, kwa Dunia ya Sasa tunaamini katika Elimu ndiyo inaweza kufungua milango hiyo, je milango yenyewe ni rahisi kufunguka au Kila mlango una funguo zake?
Tiririka na Samson.

Itaendelea.........................
 
Hii imeniumiza mnooo jamani hadi chozi walahi
 
Nimelia kama mama kulwa🥲
 
Nimelia kama mama kulwa🥲
Mnakuwaga na machozi ama vilio vya furaha na vya huzuni ama maumivu na vingine vya kinafiki jamani. Yaani unalia kabisa inaonekana umeumia kumbe una act. Na kilio kingine Cha utamu ,eti unasema bebi nitwange taratibu unaniumiza kwa utam¥¥ so huwa hamueleweki.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom