SEHEMU YA SABINI NA MBILI
Siku moja wakati Samson anatoka zake shule, alimkuta Mzee Mgaya akiwa na mgeni fulani pale nyumbani kwao ambapo muda mwingi Mzee Mgaya alionekana kumsikiliza yule mgeni ambaye alikuwa anaongea vitu, huku Mzee Mgaya akiwa na kijikaratasi akiandika baadhi ya maelezo anayopewa.
Samson aliwasalimia Kisha akaingia zake ndani ili abadilishe nguo, Kisha akatoka na kumkuta mzee Mgaya peke yake yule mgeni akiwa kaondoka.
Mzee Mgaya alimuashiria Samson akae, kisha akaanza kupiga naye stori,
Enhee niambie, masomo yanaendaje huko, maana mpo kwenye kukaribisha mitihani ya kufungia muhula wa pili, na tayari wewe ni form four mtarajiwa. aliongea Mzee Mgaya huku akimwangalia Sam na kutoa tabasamu la kirafiki.
Ni kweli baba hata Mimi nafurahi kufika hapa nilipo, naamini mwenyezi MUNGU atatia wepesi kwenye kila ninalolifanya, hivyo kila kitu kitakuwa sawa tu. alijibu Samson.
Kwanza nafurahi kusikia hivyo, naweza kusema kwasasa umekuwa mtu mzima wa kutegemewa na hilo linanipa faraja sana, na nilichokuitia hapa ni kukutaarifu kuwa leo hii kesho nasafiri naenda mbali kidogo nje ya nchi, na ndiyo maana umenikuta hapa nilikuwa nafanya maandalizi yangu yanayohusu safari hii, hivyo Samson wewe si mtoto tena nakutegemea sana juu ya kuongeza ulinzi na msimamo thabiti kwenye hii nyumba.
Wewe ni mtoto wa kiume, unajua fika kwa taratibu za kabila letu mtoto wa kiume hupewa nguvu na mamlaka pindi akionesha anajitambua hata kama umri wake mdogo, lakini wewe hata umri wako si mdogo tena mwanangu.
Sitegemei kusikia habari za kijinga, mara Samson kafanya hiki mara hiki, haitapendeza, na mama yako unamjua kitu gani utafanya nisipate taarifa, hivyo kuwa makini sana ningependa uwe wewe na shule, shule na wewe, na hilo ndiyo limekuweka hapa mjini na si lingine.
Jambo lingine kule kwenye Karakana yangu unakujua vyema kabisa, hivyo naomba uwe unatembelea kule, na kucheki mazingira nadhani, itakupa nafasi ya kujifunza vitu vingi, lakini pia Kuna mama yako mdogo Tausi, usimsahau sana na wewe , amekuwa akilalamika mara kadhaa kwamba umemtupa huwa hutaki hata kumsalimia,siyo sawa ulishakaa kule hivyo siku moja moja si mbaya kumjulia hali ni mama yako yule.
aliweka kituo mzee Mgaya.
Sasa Mzee unaenda wapi na utakaa muda gani, aliuliza Samson.
Kwasasa nitakaa kama miezi miwili siyo mingi ila kwa watu tuliozoea kuonana zitakuwa ni siku nyingi.
Ila ninachosisitiza zaidi ni heshima, heshima, heshima.
Samson sitaki nirudi halafu badala ya watu tufurahi kwa kupoteana siku nyingi tuanze kugombana, haitakuwa sawa, hapa hakuna chakula na kama una njaa sana chukua hela ingia zako mtaani ukale maana dada na mama yako tangu asubuhi hawapo hapa. aliweka kituo mzee Mgaya huku Sam akiingia jikoni kujiandalia chakula chake licha ya kuonewa huruma kuwa akale mgahawani.
Jioni familia nzima iliungana huku Samson akiwa kafurahia sana safari ya mzee Mgaya aliona kama alikuwa anambana tu hivyo safari hii atakuwa huru kiasi.
**************************************
Jumamosi fulani Samson alipanda magari ya kuelekea shamba kuliko na Karakana za Mzee Mgaya kama alivyokuwa kaelekezwa, alifika na kujitambulisha huku wafanyakazi na mafundi wa pale wakimuita boss mtoto kama ilivyokawaida.
Samson alikaakaa pale, Kisha akashangaa kumuona Tausi mama yake mdogo, huku Kila mmoja akimshangaa mwenzake.
Hee vipi Sam umekuja na nani, na kama umekuja mwenyewe, hujapotea kweli? alitania Tausi huku akimuita fundi mkuu wa Karakana.
Naona maboss wote mmekuja, hii ni neema, najua watu tutashiba leo, aliongea kwa utani yule fundi huku akijifutafuta vumbi.
Mimi nimekuja kutembea tu lakini pia nadhani Kuna maagizo Mzee alikupa na ndiyo nimekuja. aliongea Tausi.
Ni kweli niliambiwa Kila jumamosi nitakupa kiasi fulani cha pesa, (akitaja kiasi kile)
Pia kinachobaki nitampa yule Mama mwingine. aliongea yule fundi Kisha akitoa burungutu la pesa kiasi cha kumshangaza Samson, maana zilikuwa pesa nyingi.
Hii ni zile kazi wanazoleta wateja wa kawaida yaani mmoja mmoja, na pia zile oda kubwa kubwa pesa zake niliambiwa nimkabidhi mama Kulwa
alifafanua yule fundi.
Sasa, nimekuelewa Mimi naona niwaache niwahi majukumu mengine, vipi Samson tunaongozana au bado upoupo? aliuliza Tausi huku Samson akisema naye anaondoka kwani hakukuwa na haja ya kuendelea kukaa pale, wakaanza kutembea kwa miguu huku wakitafuta kituo cha gari ambacho bado kulikuwa mbali.
Yaani baba yako ananionea sana, yeye si wakushindwa kununua usafiri angalau na Mimi niwe narahisisha safari zangu, si kwamba hana pesa anazo, ila ni bahili kupindukia,
Anashindwa kuelewa kuwa maisha ni hayahaya na Mimi napaswa kuwa na kitu fulani, labda ataninunulia nikiwa kaburini maana simuelewi hata kidogo. aliongea Kwa masikitiko Tausi huku Samson akiwa kimya tu kwani hakuwa na la kuchangia.
Walipata gari na safari ikaendelea huku wakiwa wanaongea vizuri tu.
Sasa mwanangu wewe nadhani utashukia hapo sokoni ili uchukue magari ya kwenu si ndiyo?
aliuliza Tausi.
Kwa unyonge Samson akaitikia huku akishangaa Tausi kumwambia vile kwani yeye alijua safari hii ni Hadi kwa Tausi,
Samson alishuka akatafuta sehemu akakaa licha ya magari ya kuelekea kwake yakipita yeye alikaa tu, huku akiwaza kwanini Tausi Hana hamu naye kama zamani
Kwa Tausi nayemjua angelazimisha niende kwake, lakini Kuna kitu gani nimemkosea? Alijiuliza Samson.
Akaona kwakuwa muda bado upo anapanda gari za kuelekea hukohuko kwa Tausi ili akamuulize mbona kabadilika sana.
Ndani muda fulani alikuwa getini kwenye nyumba ya tausi huku akigonga geti na kisha kufunguliwa,
Akafungua mwanamke fulani mzuri sana huku akiwa anaongea kiswahili cha mwambao kama ilivyo kwa Tausi.
Yule mwanamke alifungua sehemu ndogo sana huku akilishikilia geti, Kisha akauliza,
Wewe ni nani na unamtafuta nani?
Naitwa Samson, nimekuja hapa ni kwa mama yangu mdogo, alijibu Kwa kifupi Samson.
Ahaaa hili jina siyo geni, huwa nalisikia, kuhusu huyo unayemtafuta, ametoka, tangu asubuhi amesema anaenda sijui wapi Kuna miradi ya Mzee hivyo hajarudi bado, labda ingia ndani umsubiri. aliongea yule mwanamke huku akifunga geti Mara baada ya Samson kuingia.Huku Samson akiwa anawaza , Tausi alinitangulia muda Sasa atakuwa wapi tena, hata hivyo dili langu limeharibika kumbe hayupo peke yake Kuna mgeni tena? aaaaaargh Bora niondoke tu, tena tausi si tulikuwa wote akija hapa lazima ataniuliza nimefuata nini, mmmmh au niondoke tu? alijiwazia Samson.
Karibu ndani mgeni, naona umeganda tu mlangoni, ingia!
alikaribisha yule mwanamke Kisha wakaendelea na stori.
Huyo mama yako mdogo atachelewa, kwasababu aliniambia akitoka huko atapitia mjini kufunga mizigo yake ya kuweka dukani. alifafanua yule mwanamke.
Naitwa Samson Mgaya,
Huyu mzee Mgaya ni baba yangu mkubwa na hata hapa niliwahi kuishi kipindi fulani, samahani mwenzangu unaitwa nani? alianza uchokozi wake Samson
Mmmmh jamani kwani unataka nini, wewe si unamtaka mama yako mdogo Tausi? endelea kumsubiri maana jina langu hata nikikutajia halina msaada. alijibu kivivu yule mwanamke.
Hapana unakosea dada yangu, unajua Duniani kote watu huanza kwa kutambuana majina, ndipo mengine huendelea, Kuna ajali Kuna dharula na mengine mengi, kwa mfano Mimi hapa nadondoka ghafla, nimezimia au hata kama naongea lakini nikawa sijiwezi, huenda ukaomba msaada nikakimbizwa hospital, na ukiulizwa jina la mgonjwa utawatajia kuwa anaitwa Samson Mgaya,
Je, tufanye haya yamekuwa kinyume yamekupata wewe, je madaktari wakiniuliza jina, nitawaambiaje?
aliuliza Samson.
Mmmmh wewe mtoto umechangamka, hakika unanifurahisha sana, Ina maana hospital bila jina hutibiwi?
Ila nimependa sana ushauri wako ni mzuri,kifupi naitwa Latifa ni dada wa Tausi , yeye ni mtoto wa mkubwa Mimi mtoto wa mdogo, yaani mama zetu ni mtu na dada yake, bibi yetu ni mmoja, halafu umeniita dada unakosea Mimi ni mama yako mdogo. alijibu yule mgeni aliyejitambulisha kwa jina la Latifa.
Samson kutokana na tamaa zake tayari alivutiwa na yule mwanamke, na Samson alipenda sana mteremko , hakuwa na uwezo wa kumsimamisha mtu njiani na kumtongoza, yeye alikuwa na mbinu ya kuwateka watu ambao hawakuwa na utayari wa kufanya mapenzi huku wakikuta tayari wameshiriki ngono na Samson kama bahati mbaya tu.
Sasa Latifa mimi nikuage, maana mamdogo tulikuwa wote, ila sikujua kama ana ratiba nyingi anaenda mjini, akirudi mwambie Mimi nilikuja hapa. aliaga kimikwara.
Dah wewe mtoto kwanza usiniite Latifa, Mimi ni mama yako, Mzee Mgaya namuita shemeji yangu na Tausi ni mdogo wangu, Sasa nakuomba uwe unaniheshimu kama unavyomheshimu Tausi.
Ila nimependa uchangamfu wako hakika nimeenjoy huu muda mfupi uliokuwepo. aliongea Latifa.
Samson aliondoka huku moyo ukimdunda kwa tamaa za ngono, Latifa alikuwa mwanamke mwenye ushawishi, huku akigonga kichwa cha Samson maana ulimbukeni ulimsumbua.
Samson alirudi nyumbani kwao huku akilaumiwa kiasi na mama Kulwa baada ya kupitiliza muda ambao alipewa.
Halafu Samson naomba ule Chakula Kisha nakuomba uje huku nje barazani, aliongea mama Kulwa akiwa kashikilia Miwani mkononi na kitabu fulani, ilikuwa ni kawaida kwake kujisomea vitabu awapo nyumbani haswa vinavyohusu masuala ya uchumi ikiwa ni njia ya kujiongezea maarifa
Samson alimaliza kula Kisha akaja kwa mbwembwe alipo mama Kulwa akaketi chini .
Ahaa umekuja eeh, Sasa naomba unisikilize kwa umakini sana mwanangu, ni kuanzia juzi dada yako Rahma amekuwa ni mtu wa kulala , yaani amekuwa mvivu kupindukia.Na hata hapa ninapoongea yupo ndani amelala, juzi aliandaa Chakula vizuri lakini hakula, Jana pia hivyo hivyo, Leo nimempeleka dispensary, amekutwa ana ujauzito Sasa hii ni habari mbaya ndani mwetu , ni aibu katuletea huyu mtoto yaani nashindwa hata nimpeleke wapi, ila nakuomba mwanangu fanya uchunguzi huko mtaani ili tujue alikuwa na mahusiano na nani.
Lakini pia kama na wewe upo kwenye list japo sina uhakika, ni Bora ukasema mapema maana yule mbogo akirudi atakuja kuua mtu.
aliweka kituo mama Kulwa.
Samson aliruka futi mia huku akiomba asihusishwe na ule msala, lakini pia moyo ulimuuma kwani anajua kashafanya mapenzi na Rahma zaidi ya mara mbili kwenye wiki tatu zile.
Mama nimekusikia na nitafanya uchunguzi, alijibu Samson huku sauti yake ikibadilika na kuwa yenye uoga na mkwaruzo
Mama Kulwa alimwangalia Samson kitambo, huku akiwa anagundua kitu, maana uso wa Samson uliongea.
Itaendelea...................