SEHEMU YA SITINI NA TISA
Baada ya kijana kubanwa kwa maswali kadhaa kuhusu aliyempa hela, lakini pia kwanini akose adabu na kugonga mageti ya watu nyakati za usiku, kijana alijitetea huku akiomba sana msamaha, huku akishindwa kumtaja kabisa aliyempa hela kwa madai eti hamfahamu.
Mzee Mgaya kama baba mwenye nyumba akaamuru kijana aachwe aende zake licha ya wengine kutaka kumbana zaidi.
Mke wangu, unajua hapa tayari tuna mtoto wa kike halafu vijana wamegundua hasomi, haya yote lazima yatakojitokeza tu, halafu jaribu kukaa na huyo Binti umbane vizuri kuhusu ni nani anayewasiliana naye, si rahisi mtu kutoa pesa kwa mwanamke ambaye anakukataa kwa vyovyote vile, ni lazima kuna muhusika tu, na pia ushauri wangu ni kwamba kama Kuna yeyote ambaye Binti anaridhika kuwa naye, basi amlete atutambulishe ili kama anaolewa basi taratibu zifuatwe...........
Kabla hajamalizia Mzee Mgaya, Rahma akadakia,,,,,,
Baba mimi sitaki kuolewa!
na Sina mahusiano na mtu yeyote,
Hata mimi nashangaa kuona mtu analeta pesa zake ikiwa hatujaongea.
alifafanua Rahma.
Mzee Mgaya na mkewe waliangaliana wakionekana wenye maswali mengi, huku Mzee Mgaya akiendelea..............
Ujue tangu ufike hapa, nyumba imekosa adabu, watu wasioeleweka wanagonga geti na kujikuta wanaingia ndani kama vile sokoni,
Pia umri wako nao siyo haba ni mkubwa kiasi cha kuweza kuwa na mume, unadhani utakaa hivyo hadi muda gani? aliuliza mzee Mgaya
Eti mke wangu, tumeishi na wasaidizi wa kazi tofauti tofauti kwa miaka mingi, huku Kila mmoja akitoka hapa kwa staili yake, wapo walioshindwa kazi au mazingira, lakini pia wapo ambao walipata wapenzi/wachumba wao huku tukiwapa baraka kwa uamuzi wao, eeh mke wangu unajua vyema sana, hivyo hata huyu kama Kuna namna ya kuweza kuolewa, tuwasiliane na walezi Wake kama ana wazazi alikotoka, ili Kila kitu kikae kwenye eneo sahihi, sihitaji kuona mtu akishika ujauzito ndani mwangu, japokuwa kwa wenzangu yanatokea sana, lakini kwangu nashukuru aibu hiyo haijaja ndani mwangu.
akamgeukia Rahma,,,
Mama yangu, siku ukijihisi una ujauzito sitakuhitaji hapa kwangu, hapa ni kwangu siyo danguro la kupatia mimba zilizokosa baba.
alichimba mkwara Mzee Mgaya.
Mimi niongezee jambo langu, ni kwamba Rahma wewe huna Elimu yeyote, yaani hata ile kufuta ujinga wewe huna, na Hawa wanaokudanganya sidhani kama Kuna yeyote atakaye kuoa,
Wanaume ni watu wa tamaa zaidi umbo lako na rangi yako, ndivyo vinavyowapa tamaa zaidi hao mabaradhuli na si kingine.
Utapata mimba na magonjwa kama alivyosema baba yako na kuishia kubwagwa huku ukikosa msaada na mzee hapa kashasema ukiona una hali hiyo basi hapa pamekushinda, uhame, utaenda wapi sisi hatutohitaji kujua, nyinyi ndiyo mnasababishaga majirani watuone tuna roho mbaya,
Wewe hapa tambua si ndugu yetu, halafu kwa upelelezi wangu nimegundua hata Tausi si ndugu yako, sasa kwa maana hiyo lazima utateseka sana, utatafuta huruma lakini hutoipata mwanangu jichunge, kama Kuna mtu umempenda basi niambie sisi tutamtazama kama anafaa Kisha tutafanya taratibu zote Tena na harusi tutakugharamia wewe ni sehemu ya hii familia. aliweka kituo mama Kulwa.
Mamaaa mbona hamunielewi nasema Mimi sipo tayari kuolewa, na hakuna mtu ambaye nina mahusiano naye licha ya wanaume wengi kunisumbua, naomba nieleweke hivyo . Wewe umeniahidi biashara. Hicho ndicho kitu nakiwaza zaidi kuliko kingine. alizidi kukataa Rahma.
Sawa kama ni hivyo nimependa msimamo wako, na tambua heshima na nidhamu utakayoonesha hapa ndiyo taa itakayonishawishi nikufungulie biashara yako.
naona muda unaenda Mimi naingia zangu kupumzika.
alifunga mjadala ule mama Kulwa huku wakigawana vyumba Kila mtu akiingia zake kulala.
Samson aliingia chumbani kwake huku voltage za wivu zikiwa juu sana, kitendo cha Mzee Mgaya kusema Rahma akipata mchumba aolewe, huku akirudiarudia Kila muda vilimchanganya Samson sana tu, hakupenda Rahma aolewe, pamoja na kwamba alishaonjaonja kwa wanawake tofauti tofauti, lakini Rahma alimkaa kifuani mno hakutamani aje amkose wala kumpoteza , aliiona alarm ya hatari kwa Rahma namna alivyoambiwa na mzee Mgaya kuwa kwanza si ndugu yao na pia ikitokea amepata ujauzito ndiyo ticket ya kuhama.
pia alimsikia Rahma kuwa amekuwa akisumbuliwa na wanaume kibao, huku kauli ile ikichoma moyo wa Samson, maana akili zake zilimwambia kuwa Rahma atakataa ndiyo, lakini hawezi kukataa Kila mtu itafikia muda atawakubali tu baadhi ya wengine, kwa akili zake za kitoto alijaribu kuvuta picha ya Nini kinaendelea akajikuta ni kama miguu inakufa ganzi kwa wivu, mithili ya mtu aliyechapiwa mkewe na kigogo au mtu mwenye pesa nyingi huku Ukiwa huna uwezo wa kumfanya chochote kutokana na ukubwa wake. unabaki na hasira kifuani au ujifariji.
Samson hakuwaza kujisomea wala kushika chochote kwa muda ule, alijikuta anamuwaza Rahma tu, akisahau kuwa wiki kadhaa tu alikuwa katoka kupigwa kwa jaribio lake baya la kutaka kwenda kwa Rahma.
Kauli pekee iliyo mvutia Samson ni vile Rahma alivyokataa kuwa hayupo tayari kuolewa huku akionesha hataki kweli, hii angalau ilimpa amani na Imani Samson, akatoka nje kabisa ili apoteze muda maana hata usingizi hakuwa nao.
Akiwa pale nje aliwaza mambo mengi sana,
MUNGU anisaidie nimalize masomo yangu vyema Kisha nipate kazi nitengeneze maisha yangu, nitaoa mwanamke wa ndoto zangu, sidhani kama Kuna mwanamke atanipenda kama Rahma, sidhani kama nastahili kuwa na mwanamke tofauti na Rahma, Rahma ni mpenzi wangu,
Sasa kwanini Mzee Mgaya anamruhusu eti aolewe na mwanaume mwingine kirahisi?
Mimi ananikataza, eti nasoma basi angenilindia mpenzi wangu.
alijiwazia Samson huku akitoa lawama kwa mzee Mgaya kutojali hisia zake kana kwamba Mzee Mgaya anajua.
Aaaarrrgh,au nimwambie Mzee Mgaya kuwa nampenda Rahma hivyo akae anisubiri nimalize masomo Kisha nimuoe? sihitaji kumpoteza kabisa Rahma wangu, lakini hili zee nikiliambia tu, najua kitakachotokea nitakuwa nimethibitisha kile ambacho wao wanabahatisha na itakuwa mwanzo wa kupokea kipigo matusi na kurudishwa kijijini. alijiwazia Samson.
Akainuka akirudi zake ndani kwani alijua kukaa pale nje kutamletea matatizo maana wakigundua wale wazee wake wangembana maswali asiyajibu.
Wakati anaingia ndani hamadi alikutana na Rahma sebuleni,
Heee Sam unatoka wapi muda huu mbona hujalala? aliongea Rahma kwa sauti ya chini.
Mbona na wewe hujalala, umefuata nini hapa? alinong'ona Samson
Mimi nimefuata nguo zangu hizi aliniletea mama mchana wakati anatoka mjini, hivyo wakati yule Cathy anakuja mama akasema nizifiche chini ya kiti kwani angeanza kuzodoa na tabia yake ya kudharau vitu vya wengine hivyo nikasahau ,
saizi naingia zangu kupumzika ndiyo nakumbuka. aliongea Rahma huku akigeuka arudi chumbani kwake.
Samson akamdaka na kuanza kumkokotea chumbani kwake,
Samson Mimi sitaki bwanaa, unajua haya mambo yanavyokatazwa humu ndani nitapiga kelele nimwamshe mama, aliongea Rahma huku akiwa ameshachelewa kwani alikuwa kwenye chumba cha Samson muda huo.
Samson akamuacha Rahma Kisha akarudi sebuleni kusikiliza kama wazazi wake wanaamka kwani alivyomburuza Rahma kama mtu hana usingizi angeweza kusikia lakini alijiridhisha baada ya kuona kimya, akarudi chumbani kwake.
Samson kwanini umenifungia mlango nisitoke, kwanza Mimi Leo sijisikii kufanya chochote naomba niache bwana, aliongea Rahma kwa kumaanisha.
Samson hakutaka kusikia habari zile, akatumia nguvu na kujiridhisha mwenyewe, kisha akakaa pembeni huku akigundua Rahma hajapenda kwa alichofanyiwa lakini hakujali kwani alikidhi haja zake na kupoza machungu huku akiwa anaikagua kwa kuigeuza pakiti fulani ya nguo za ndani za Rahma huku akijichekesha
Hebu lete huko hizi nguo za kike wewe zinakuhusu nini, alimpora zile nguo Kisha akatoka huku akimwacha Samson aliufurahia ushindi wa ile mechi ya ghafla.
Itaendelea...,..............................