Mkushi w jani
JF-Expert Member
- Oct 2, 2021
- 1,896
- 1,698
Sijui kakutwa na nini naona kapotea sanaMkushi w jani mwite basi Jack Daniel ashushe episode kadhaa hapa
Sijui kakutwa na nini naona kapotea sanaMkushi w jani mwite basi Jack Daniel ashushe episode kadhaa hapa
Sam anaenda kumgonga tena TausiSEHEMU YA SITINI NA SITA
Asubuhi na mapema Mzee Mgaya alikuwa nje huku akimsubiri Samson nje na kutaka kumpa kazi kadhaa,
Walisalimiana, Kisha Mzee Mgaya akaendelea,
Hapo kwenye parking ya gari naomba pasafishe, vizuri na hayo mapipa ya maji hamisha yote, peleka kule nyuma, ukimaliza wahi buchani maana dada yako ana kazi nyingi sana hivyo mpunguzie mzigo, aliongea Mzee Mgaya huku akiwa anajiandaa kutoka.
Kwanza Sam alishangaa, imekuwaje tena, Ina maana shule haendi tena? ikabidi aulize,
Sasa Mzee vipi mbona unanituma kazi hizi hatuendi shule? aliuliza Samson.
Sasa wewe umesimamishwa masomo, yaani unataka twende asubuhi hii yote? huko tunaenda kuanzia saa nne, kwanza lazima ujue kuwa tunaenda kuomba Kwanza, usitegemee majibu kirahisi hivyo, wewe fanya kazi nilizokueleza Mimi natoka narudi siyo muda, hebu fungua geti nitoe gari. aliweka kituo mzee Mgaya.
Samson aliendelea na kazi zile huku akiwa hana amani kabisa, kwani alihisi kama suala lake wanalichukulia poa, hisia za kuacha shule zilimjia kwa mbali, huku moyo ukimuuma Kila akikumbuka lile suala.
Rahma na Samson walikuwa wanafanya usafi kwenye eneo moja, lakini siku hiyo Rahma alikuwa kama kanuna akiwa hataki kuongea na Sam, licha ya Sam kujipendekeza kwa kuleta stori za hapa na pale lakini alijibiwa kimikato huku akijaribu kukumbuka ni wapi kakosea lakini hakupata majibu, akaamua kuwa bize na kazi zake.
Ndani ya masaa mawili Sam alikuwa kamaliza kazi zote na kukimbilia kwenda kuoga ikiwa ni kujiweka sawa na kumsubiri baba yake ili akifika tu Safari ya shule ianze.
We mwenzetu vipi chai leo, nakuona upo mbaaaali baba yangu? aliuliza mama Kulwa.
Niwe mkweli mama , hili suala la kusimamishwa shule kwa muda usiojulikana, linaniumiza sana mbaya zaidi wakati naenda buchani nimekutana na wanafunzi wenzangu huko mtaani, wanasema taarifa zangu zimezagaa na inaonesha Mimi shule basi, Sasa mama appetite ya kula inatokea wapi, yaani Kila nikiwaza kuhusu yanayokuja mbele yangu sina hamu mama . Alijibu Sam kwa uchungu sana.
Mama Kulwa alimwangalia Samson kisha akacheka kivivu, na kumwita Samson,
Mwanangu hebu acha kujipa mawazo hivyo, kwani hiyo shule ipo peke yake? halafu Ina maana Mimi na baba yako hutuamini?
Tunatambua wazi kuwa wazazi wako wanajua kuwa sisi tumejitolea kukusomesha, na sisi tumewaahidi kukutimizia kile tulichowaahidi wazazi wako, na pia ili utimize ndoto zako wewe mwenyewe, kwani hiyo shule aliitafuta nani, si ni sisi?
Nani analipa ada si ni sisi?
Sidhani kama unaweza kujibu maswali yangu, ila nakuomba Kaa chini, upate kifungua kinywa ili akili ikae sawa.
Halafu baba Jose naye karibu inaenda saa nne hii, gari hajarudisha wakati nilimwambia kuwa naenda mjini, Sasa sijui anawaza nini, yaani mambo yake anaonaga ni ya muhimu kuliko ya wenzake, loooh huyu naye ubahili kazidi watoto wetu wanaosoma kajitolea kaka yao kuwasomesha, Sasa sijajua ni wapi anatumia pesa zake, kwani pesa hapati, tena kipindi hiki ana hela nyingi sana, angeweza kununua gari jipya na la kisasa, lakini ubahili umemzidi mume wangu huyu , ila nashukuru watoto wetu wote kawapa Elimu nzuri tu, kwa hapa sina cha kumdai na hata yule aliyefeli bado alimpa mtaji, namshukuru kwa hilo.aliongea mama kulwa huku akiinuka na kwenda chumbani kwake.
Baada ya muda kidogo Mzee Mgaya alirudi huku akionekana mwenye haraka kidogo,
Ahaaa naona Sam umeshajiandaa siyo? aliuliza mzee Mgaya,
Sam aliitikia kwa kutikisa kichwa
Safi. Sasa mke wangu nakuomba kwanza unipe kile kiasi nilichokupa jana ili niende nacho huko shuleni kwa huyu jamaa (akimaanisha Samson)
Sasa huko uende na hela yanini baba Jose na wewe, alihoji mama Kulwa.
Mke wangu mkono mtupu haulambwi na nikuombe kitu, sidhani kama napaswa kukumbusha Kila siku , ila mnapaswa mjiongeze,
Kisheria huyu Hana kosa lolote na hata sisi hatuna kosa!
Swali ni njia ipi ifanyike ili Samson awahi kwenda shule,
Twende kwenye vyombo vya sheria, ambapo itachukua muda mrefu huyu kwenda shule, huku akiwa kachelewa masomo kwa kipindi kirefu,huku akichukiwa na walimu wake
au tutumie njia rahisi japo inaumiza ili awahi masomo na pia akiwa na uhusiano mzuri na walimu wake?
aliuliza mzee Mgaya.
Mama Kulwa hakujibu kitu huku akimshika mkono mumewe na kuingia naye chumbani, ndani ya dakika moja Mzee Mgaya alitoka huku akimuamrisha Samson watembee haraka, kwani kwa siku hiyo alikuwa na ratiba nyingi sana.
Walifika kwenye viunga vya shule huku wakiitafuta ofisi ya mwalimu mkuu ambapo walimkuta akiwa , ana barua nyingi mezani kwake akiwa na muhuri mkononi akiwa anagonga muhuri barua moja baada ya nyingine.
Karibu sana Mzee mwenzangu,
Mwalimu mkuu aliwakaribisha.
Mzee Mgaya alionesha kushukuru huku akiwa na uchangamfu fulani wa kujipendekeza kwani hakuwa na namna.
Enhee karibu ndugu yangu, kama una la kusema, sema nakusikiliza maana nipo bize sana kwa kutwa hii ya leo. Aliongea mwalimu mkuu huku akiwa kavalia Miwani puani, ambayo hata haikujulikana kama Ina kazi gani.
Ni kwamba ujumbe wako niliupata kupitia kwa huyu kijana wetu,sipingani na wewe kwa yale uliyosema kuwa taratibu hazikukamilika, ila nilikuwa nakuomba Mzee mwenzangu kuwa naomba basi kama ulivyofanya kipindi kile, fanya kama kawaida.
aliweka kituo mzee Mgaya huku akijichekesha.
Mzee Mgaya naona kama kijana wako hakukweleza vizuri, ni hivi huu utaratibu nadhani Mimi na wewe tulishamalizana na ndiyo maana kijana wetu aliendelea na masomo, yaani Mimi nilifanya lililo ndani ya uwezo wangu,
Lakini kwa hili, linatoka huko ngazi kubwa huko , limeratibiwa na waajiri wangu, je Mimi nikikusaidia huoni nitakuwa nimepishana na wakubwa zangu, na ikapelekea kuharibu kibarua changu?
Mzee mwenzangu, naomba usichanganye kujuana kwetu na kazi, Mimi na wewe tunajuana huko, nje ya ofisi, mambo haya naomba usinilazimishe nifanye kwa maslahi yako huku mimi nikiharibu, si vizuri hata kidogo. aliongea kwa ukali mwalimu mkuu huku akionesha hana masihara hata kidogo.
Samson alikuwa makini akisikiliza maongezi yale huku majibu ya mwalimu mkuu yakimkatisha tamaa zaidi.
Sawa naomba basi tuongee mengine kama hautojali mwalimu, tuachane na hayo.alishauri mzee Mgaya.
Mengine gani tena Mzee Mgaya, yaani kwenye hii ofisi ambayo wanaingia watu muhimu kila mara , halafu niwe napiga stori na wewe,
Hebu acha habari zako, kweli nimeamini yale nayosikiaga mtaani, kwamba wewe una shida kichwani kumbe ni kweli. aliongea mwalimu mkuu huku akitikisa kichwa kukubaliana na yale anayodai huwa anayasikia.
Mwalimu, najua umesikia mengi kunihusu Mimi, na sikatai kwakuwa ni mwanadamu lazima nitazungumziwa tu, Kuna watu wengi Duniani walifanya makubwa lakini bado wanazungumziwa vibaya, Sasa kwa kuyajua haya Mimi hainisumbui mtu kuniongelea aonavyo yeye.
Siwezi kulazimisha Dunia nzima inikubali au iniheshimu, Bali nitajitengeneza mwenyewe nipate walau Moja ya tisa ya heshima.
Tukiachana na hayo, mwalimu nimepita Jana kule saiti kwako nimekuta ujenzi unaendelea vizuri sana kwanza hongera, (huku akimpa mkono mwalimu mkuu)
Nashukuru sana, ile nyumba aliianzisha mke wangu tangu miaka mitano iliyopita Sasa ikamshinda, si unajua tena lakini nimeingia mwenyewe, alifafanua mwalimu mkuu.
Sawa lakini kile kibaraza, hakijakaa vizuri sana, kwanza kingetengenezewa nguzo za saruji Kali, ili kiwe cha kisasa zaidi. alishauri Mzee Mgaya.
Mzee mwenzangu wewe acha tu, ungejua ramani zote hizo tunazo kwani hata mafundi walitushauri hivyo lakini ni...... aliongea mwalimu mkuu huku akigonganisha vidole akimaanisha ni pesa inasababisha vitu viwe chini ya kiwango.
Usijali Mimi nitapabomoa pale pote na nitajenga upya kwa gharama zangu. alisema mzee Mgaya huku akimwangalia mwalimu mkuu usoni.
Mwalimu mkuu alikuwa nusu kuongea huku mdomo Ukiwa haufungi na akavua na Miwani kabisa, kisha kwa upole akauliza,
Unasema kweli unanitania, maana gharama zile ni kubwa ujue, aliongea huku akijichekesha yule mwalimu.
Sitanii tena nakuachia hela ya saruji mifuko kumi Sasa hivi, halafu kitakachoongezeka kama nondo na vitu vingine, utanitaarifu. aliweka kituo mzee Mgaya.
Mwalimu kusikia vile akamuamuru Samson atoke nje ili waongee wawili tu, Kisha baada ya dakika tano akaitwa tena.
Kama nilivyokwambia Kuna ugumu sana kwenye suala la Samson, na pia wewe ni jirani yangu Sina maana ya kukaa karibu hapana , namaanisha ujirani wa kipindi kirefu sana tumesaidiana vitu vingi hivyo na hili nitajaribu, nitaacha kazi zangu nitaenda kwaajili ya Samson tu kuhusu wanafunzi wengine hao nawaachia wazazi wao Mimi nitakusaidia wewe kwakuwa , tumefika mbali sana.
Kisha akamgeukia Samson,
Wewe kijana hivi ushukuru baba yako ana roho ya huruma sana na wewe, hakuna mtu akahangaika na mtoto asiye wake kwa kiasi hiki, hivyo naomba kuwa makini na masomo yako,
Wakati nafuatilia haya masuala ilitakiwa uwe nyumbani, lakini nimeona utapitwa na vingi, hivyo wewe kuanzia kesho utaendelea na masomo yako kama kawaida, sawa?
aliongea yule mwalimu kwa sauti kubwa akimtaka Samson kuwa na nidhamu shuleni pale.
Sasa mwalimu Mimi nikuage, nakutakia ufuatiliaji mwema maana wewe ndiye unayejua upite, njia zipi.
aliaga Mzee Mgaya huku akiondoka na Samson na kumuacha mwalimu akiwa na bashasha sana, alifanyiwa Nini, Samson hakujua.
Samson, inabidi ukabadilishe nguo uende Temeke kwa mama yako mdogo, Kuna kazi utamsaidia, usiwaze kuhusu shule, hayo yashaisha, Mimi naenda mjini Kuna gari nalifuata.alisema Mzee Mgaya.
Itaendelea...............
Namie niliwaza ivyo Ila akilegea tu Basi atakuwa mjinga sema kwa age sexual desire emotions are strong than himself.Sam anaenda kumgonga tena Tausi
Namie niliwaza ivyo Ila akilegea tu Basi atakuwa mjinga sema kwa age sexual desire emotions are strong than himself.
So to conquer them is inevitable.
Ila huo umri Ni hatari mno yaani vibaya mno Ila ukiupita salama shukuru highest power.Foolish age +temptations around him ndo znamfanya akose control over sexual emotions..!
Utafanikiwa kweli huyu kijana.kama anamtafuna mke wa baba yake mkubwa.anyway ngoja tuone mwisho wake.Sam anaenda kumgonga tena Tausi
ThanksSEHEMU YA SITINI NA SABA
Samson na Mzee Mgaya waliachana huku Samson akinyoosha moja kwa moja hadi kwenye kituo cha daladala na kwenda moja kwa moja kwa mama yake mdogo Tausi.
Aliikaribia nyumba na kumuona Tausi kwa mbali akiwa nje ya ile fence akiwa na wanaume watatu ambao walionekana wakibishana kiasi.
Jamani kwanza Mimi sikuwapa kazi, aliyewapa ni Mr, na hayupo hivyo kama hela hiyo no ndogo labda niwafanyie mpango muwasiliane naye,trip ya mchanga kidogo tu, mnataka hela nyiiiiingi nyie vipi?
aliongea Kwa hasira Tausi.
Mamdogo eeeh hizo dharau ujue, usiangalie sijui mchanga kidogo, Wala nini, sisi tunaangalia routes, wewe unajua mchanga umetoka wapi huo, au unaongea tu, na kwanza najuta kumkubalia yule mzee yaani, nimeacha kazi ya maana, nimekimbilia huku matokeo yake ndiyo haya, na Kuna jamaa aliniambia nyie ni watata kulipa. aliongea dereva wa gari lile huku akiwaambia wenzake wapande waondoke kwakuwa hakukuwa na nyongeza tena.
Kwani Hawa wanasemaje mamdogo mbona, kama mlikuwa mnalumbana?
aliuliza Samson.
Wee naye nini hujasalimia tayari unataka kujua yasiyokuhusu, hebu kwanza fuata yaliyokuleta. alijibu Kwa ukali Tausi kiasi cha kumstua Samson.
Ni Mzee kakuambia uje siyo? aliuliza Tausi huku akionesha kama mwenye hasira hasira sana, Samson alizoea utani toka kwa Tausi, lakini alishangaa mtu ambaye hawajaonana siku nyingi na ni kama maswahiba, vipi siku hiyo nini kimetokea, alijiuliza Samson asipate majibu.
Halafuuuuu mbona una sare za shule unawezaje kufanya hii kazi?
Unauona mchanga huu, inatakiwa wote uingie ndani kwasababu hapa nje utaanza kutawanyika kutokana na fujo za watoto na mengine mengi.
Chukua hiyo ndoo na anza kuchota ingiza ndani. alitoa maagizo Tausi Kisha akaingia ndani bila kumkaribisha Samson.
Samson alikuwa na njaa, kwani alishindwa kupitia nyumbani kwao ale akitegemea akifika kwa mama yake mdogo Tausi, atakula tu, lakini hali ilikuwa tofauti sana Tausi alikuwa mkalimkali huku akiwa hamjali Samson.
Samson alivua Shati la shule na kuanza kazi ile, huku akigundua ni ngumu tofauti na alivyouona ule mchanga, maana Kila akichota anaona hata haupungui, akajua Sasa kazi ipo, na alikuwa na kipindi kirefu hajafanya kazi ngumu hivyo ikawa ni changamoto kiasi.
Baba kazana uishe huo, Temeke hii tunaijua wenyewe, watu wanaiba hata vitu visivyowezekana, hivyo sitaki ulale hapo. Tausi alitoa maagizo yake huku akirudi ndani kwake ambako sijui alikuwa anafanya Nini maana Samson hakuingia, aliianza kazi juu kwa juu tu.
Samson alimsindikiza Tausi kwa macho huku akigundua mama yake mdogo anazidi kunenepa kwani namna alivyokuwa akitingisha mambo fulani yaliyo kwenye ile khanga huku miguu minene ambayo imechafuka chafuka kutokana na kazi fulani za pale ndani, kiufupi tayari mashetani ya Samson yalikuwa karibu mno, akajikuta anasisimka Kila akimuona Tausi, tatizo lilikuwa moja , kununa kwa Tausi, hapa Samson alijikuta anawaza mbali sana.
Baada ya kupiga kazi kwa muda mrefu sana, alijikuta walau anafikia nusu ya kazi huku akikata tamaa kama anaweza kumaliza, Mara Kuna gari fulani zuri la kutembelea, lililoonekana kuwa jipya kwa Samson kuanzia rangi yake nyeusi inayong'aa hadi tairi zake kubwa na njumu ambazo zinaonekana ndiyo kwanza zinakanyaga barabara.na hata hivyo gari lilikuwa jipya kweli kwani baadhi ya sehemu kulikuwa na makaratasi, alilitazama kwa muda huku akishangaa kwanini lipaki karibu na nyumbani kwao na muhusika hashuki, akaingiwa na woga akashangaa likisogea kuja alipo, wakati hofu yake ikiongezeka ndipo aliposhuka Mzee Mgaya huku akicheka kwani inaonesha alikuwa anamsoma Samson namna anavyoshangaa.
Ni gari letu hilo mwanangu. aliongea Mzee Mgaya huku akimwangalia Sam na kutoa tabasamu.
Dah hongera sana baba naona mambo yako yameenda kimya kimya hujamwambia mtu Wala nini hata ulivyonambia unaenda mjini kuchukua gari nilidhani labda gari lile la zamani, ila ni zuri sana baba, alisifia Samson huku wakiingia ndani.
Ila wewe ni kamanda nusu ya mchanga wote umeingia ndani, hebu pumzika kwanza na hongera kwa kazi nzuri, waliingia ndani na kumkuta Tausi yupo bize na TV huku akiwa si mchangamfu sana.
Mzee Mgaya aliingia chumbani huku akimwacha Sam pale sebuleni, na hakuna kilichoendelea kwani hawakuwa waliongea, Samson alimwangalia Tausi kwa kuibiaibia akagundua ni amekasirika zaidi baada ya kuingia Mzee Mgaya ila hakujua nini kinaendelea.
Mzee Mgaya alitoka huku macho yakiwa kwa Tausi, mke wangu mbona wale vijana walioleta mchanga wameniambia hujawapa hela yote kwanini, wakati nilijupa kiasi chote mke wangu, mbona unajishushia heshima kwa tamaa za vitu vidogo? Na sikia nikwambie mama, gari nimenunua na lazima ukubaliane nalo Mimi shughuli zangu nyingi zinahitaji uharaka unadhani nawezaje kwenda na muda bila usafiri wa uhakika.
Najua hujapenda kwakuwa tangu mwanzo ulisema ni anasa na najaribu hela na Mimi nikwambie tu ukweli kuwa siyo anasa bali ni kurahisisha mipango yangu tu. aliweka kituo mzee Mgaya huku Tausi akija juu.
Kwani gari lile dogo si lingetosha kurahisisha mambo yako, au unadhani Mimi ni mjinga sana niamini kuwa lile gari la Mama Kulwa,
Lile ni gari lako mama Kulwa hana uwezo wa kununua gari lile, usinifanye mjinga bwana. aliongea Kwa jazba Tausi.
(Huku akicheka)
Hebu futa ujinga wako hata robo tu,
Dada yako aliajiriwa serikalini sijui kama ulikuwepo Duniani, maana Mimi nilimuoa akiwa ana miaka miwili tangu apate kazi, huku akipanda madaraja kadri miaka ilivyosogea, Nini kununua gari unajua ana nyumba ngapi hapa mjini unazijua biashara zake? Tena nikwambie Mimi na harakati zangu zote za maisha asilimia nyingi ananiwezesha yeye.
Yule siyo chizi magari, tangu zamani hakupenda hivyo vitu ndiyo maana alichelewa kununua, Tena nikwambie yule akiamua kununua chombo Cha maana hata Sasa hivi anaweza, huu ni muda wa yeye kula starehe watoto wake wote Wana maisha yao.
Wewe huna Elimu wala ujuzi wowote nimejaribu kukufungulia biashara Mara kadhaa unashindwa tu , huku ukinifilisi, ni lini niliwahi onesha kukudai , si nilikaa kimya mwisho mwaka juzi tu hapa umeibiwa na huwa Sina uhakika sana kama uliibiwa maana huwa hainiingii akilini.unanidhalilisha kwa mambo mengi nanyamaza tu.
aliongea Kwa kufoka na sauti ya juu Mzee Mgaya.
Tausi alianza kudondosha machozi huku akiongea kwa sauti chini sana
,, Nayajua haya yote ni kwasababu sijazaa na wewe hivyo Sina haki ya kuhoji na kutaka kujua matumizi ya pesa zako, sawa hakuna shida baba. aliweka kituo Tausi.
Sasa ndiyo kufanyaje, kwani si kweli, haujazaa na mimi ndiyo, au Kuna mtoto umezaa na Mimi?
Hujawahi hata kuharibu mimba watu wakaona alibeba ujauzito lakini ni bahati mbaya, usinipande kichwani wewe binti. aliongea maneno makali sana Mzee Mgaya huku Tausi akilia kwa sauti akidai anadhalilishwa.
Samson kwa Mara ya kwanza alimshika mkono Mzee Mgaya na kumtoa nje huku akipiga magoti,,,
Baba samahani naona hapa kutatokea mambo mengine mabaya kwanini tusiondoke baba, epusha shetani. alishauri Samson.
Mzee Mgaya alitoka nje akawasha gari na kumuashiria kijana wake apande huku akitoa gari lake na kuingia nalo barabarani,
Unajua kijana wangu maisha yaone hivihivi, yule mama yako ana chokochoko fulani hivi tangu nimwambie nanunua gari alikuwa anapinga na nilipomwambia bei ndiyo kabisa , akaanza kunitukana eti nazeeka vibaya ile asubuhi, sikumuacha nilimnasa vibao, Sasa jioni hii bado kajifanya kuninunia na bado safari hii nataka ajue kuwa Mimi ndiye mwenye kuamua nini kifanyike mambo haya asipinge mama Jose, anapinga yeye ambaye ni sawa na mti wa porini ambao hauna faida, haikupi mbao, kuni Wala matunda atanisumbuaje. aliongea Mzee Mgaya huku akiwa anaovertake magari njiani huku akitabasamu nadhani gari yake ilikuwa ikimfurahisha sana.
Itaendelea...................
Endelea kuifuatilia simulizi mpaka mwisho.
Samson bana eti baba epusha shetani.......na kweli shetani kaepushwaSEHEMU YA SITINI NA SABA

Wakati shetani wake Ni mkubwa kuliko wa mzee mgayaSamson bana eti baba epusha shetani.......na kweli shetani kaepushwa![]()