Simulizi: Kazi ya Kutengeneza Majeneza

Sehemu ya 82.

"Kaka nitoe mbao za kuanzia kuchonga jeneza?" mdogo wangu aliniuliza kwa ghafla kiasi kwamba nilishtuka na kujikuta nikiachana na wale watu na kumjibu yeye.
Nilipokumbuka na kurudisha macho kwao, nilibahatika kuona kama mguu wenye kanzu ukifutika ndani ya ile nyumba ya yule nama jirani yangu.

Je nini kitaendelea?
alafu mbona hii fupi kama vile umeniandikia sms
 
Sehemu ya 83.

Nilihamaki huku nikikazia macho pale mlamgoni kwa yule mama jirani.
Mdogo wangu naye aliniangalia kisha akageuza macho kuangalia kule nilikokuwa naangalia mimi.

"Vipi kaka?" mdogo wangu aliniuliza.
"Hata," nilimjibu nikiacha kuangalia kule.
"Kwani hawa jamaa wamekwenda wapi?"
"Sifahamu," nilimjibu kwa mkato ilu kukatisha mada aliyokusudia kuongea na mimi.

"Mh!" aliguna mdogo wangu kisha akaendelea na mambo yake mengine.
Nilisimama kwa muda nikitafakari tukio nililoliona kama ni la kweli au ni akili zangu kutokana na mawazo.

"He vijana wangu wamekuja?" yule mama jirani alisema akijifunga khanga huku akija pale kwenye banda langu la kazi.
"Shikamoo mama," nilimsalimia.

"Marahaba," aliitika akicheka
Sikujua alikuwa akicheka nini. Afadhali hata angetabasamu ningemwelewa kidogo kwani ni kawaida kwa binadamu.

Akilini nilimuwaza kuwa, huenda alicheka kwa sababu alijua ni jinsi gani alivyokuwa akituumiza au akiniumiza mimi kwa mambo yake aliyokuwa akinifanyia.

"Vipi mama, leo mbona umefurahi sana?" nilimuuliza nikiwa nimeacha kazi niliyokuwa nafanya.

"Hata, jamani nimewaona wanangu ni lazima nifurahi au nimefanya vibaya?" aliniuliza huku akiendelea kucheka sana.
Ilibaki kidogo sana nimtwange kwa nyundo ya kichwani kwani nilishajua nini kilikuwa kikiendelea kwa yule mama.

Hasa kutokana na kitendo cha kuona miguu ya mmoja wa wale watu ikizamia ndani kwake huku wakijifanya ni watu waliokuwa wamekuja kuweka oda ya kutengeneza jeneza.

Mara alinyamaza ghafla kucheka na kuniangalia. Najua kwanini aliniangalia vile. Nilikuwa nimekasirika sana kutokana na kitendo chake cha kucheka sana huku akinizunguka na kujifanya mimi na mdogo wangu ni wanawe.

"Kumbe una kazi sana, tena ya kutengeneza jeneza?" aliniuliza huku akiwa amesimama mbele yangu.

"Ndiyo," nilimjibu kwa mkato.
"Sawa, endelea baadaye basi," alinijibu na kuondoka.

Nilimfuatilia kwa macho mpaka anapanda ngazi za nyumba yake nikiamini kuwa, huenda angefanya chochote kile ambacho si cha kawaida.
Lakini hakufanya hivyo mpaka anaingia kwake.

"Kaka huyu mama huyu," mdogo wangu aliniambia huku akishika msumeno. Lakini hakuendelea kuniambia huyu mama nini kafanya.

Je nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 84.

Nilikumbuka ile ndoto yake aliyotaka kuniambia usiku, lakini eti nikajikuta nikupuuzia kwa sababu ya kuwahisha jeneza la watu.

Ilikuwa wakati nakata kata vipande vya jeneza kwa kufuata vipimo vya wale wateja, mara nilipogeuka nyuma yangu kama vile nilitekenywa, niliwaona wale watu wote watano wakiwa wamesimama nyuma yangu wakiniangalia ninavyofanya kazi.
Walikuja saa ngapi sikujua, walitokea wapi pia sikujua.

Je nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 85.

"Vipi bwana fundi tutawahi?" Mmoja kati ya wale wenye kanzu aliniuliza kwa hamu kubwa sana ya kusikia majibu yangu.
"Bila shaka mkuu," nilimjibu huku nikiingia ndani kuchukua futi.

Wakati natoka ndani sasa ambako sikuchukua zaidi ya dakika mbili, sikuona mtu hata mmoja na hata nilipoangaza kona zote za pale kazini sikuwaona. Moyoni nilikataa kwamba si kweli kwani kwa muda niliochukua ndani, lazima ningewaona walikokuwa wakimalizia kwenda.
"Hawa watu wameelekea uelekeo upi?" nilimuuliza mdogo wangu.

"Watu gani?" naye aliniuliza mimi akiwa na maana hajui lolote.
"Si hawa niliokuwa naongea nao sasa hivi?" nilimjibu.

"Kabla ya kuja mama au?" aliniuliza tena mdogo wangu.
"Baada ya mama kutoka hawajaja wale watu waliotaka jeneza wakasimama hapa mpaka yule mmoja mwenye kanzu akaniuliza kama wanaweza kuwahi?"

"Sijawaona na wala sijasikia kama uliongea na mtu yeyote yule," mdogo wangu alinijibu huku akiniangalia kwa macho ya kunishangaa sana kwa maneno yangu.
Ukweli ni kwamba nilibaki nimeduwaa kwa tukio lile.

Nilijionea huruma mwenyewe lakini sikuacha kuendelea na kazi ya kutengeneza lile jeneza ambalo wenyewe ndio hao walianza kunifanyia visa kama vile.
"Kwani wewe kaka umeona nini hapa?" aliniuliza mdogo wangu.
"Sijaona kitu kibaya ila kama niliwaona wale watu hapa," nilimjibu.

"Si saa zile?" alisema mdogo wangu.
"Hapana hata baada ya saa zile wamekuja tena," nilimjibu mdogo wangu huku nikimwangalia kwa kumtafakari kwanini na yeye asiyaone mambo niliyokuwa nikiyaona mimi?

Au ndiyo utaalam wa huyo mtu aliyekuwa akipambana na mimi?

Je nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 86.

"Unajua kaka inaonekana una mambo yanakusumbua kichwa sana, kama ulivyowaambia wazazi siku zile," alisema mdogo wangu.

"Ni kweli ni kweli kabisa," nilimjibu.
"Sasa leo umeona nini?" aliniuliza.
Pale pale nikasikia sauti masikioni mwangu ikiniambia.

"Ole wako usimulie chochote kuhusu yanayokupata nimekwambia."
"Sijaona kitu, nadhani ni hali tu," nilimjibu na kujipa kazi ya ghafla ili asiniulize tena kwani nilikwishaonywa kwa sauti ya ajabu asiyoonekana mtu wala kiumbe.

Nusu saa mbele, wale watu walikuja nikiwaona. Walitokea kwenye uchochoro mwingine kabisa huku wakiongea habari ambazo zilinishangaza mimi.

"Mimi siwezi kabisa nina huruma. Unajua kumdhuru binadamu mwenzako hivi hivi unamuona ni vibaya hata mbele ya Mwenyezi Mungu," mmoja mwenye kanzu aliwaambia wenzake.

"Hata mimi, yule mama iko siku atajua nini maana ya ubaya. Basi afadhali umtoe roho ijulikane moja, lakini unamweka mwenzako roho juu kila kukicha halafu eti unamuonya asiwaambie watu matatizo yanayomtokea," alisema mwingine naye ni yule mwenye kanzu wa pili.
Wale wasio na kanzu hakuna aliyesema neno wala kutoa sauti.

Nilisimama nikiwaangalia na kidogo niangushe nyundo niliyokuwa nimeshika. Kwani maneno yale yalionekana kama walikuwa wakimsema yule mama jirani na mambo ya ajabu aliyokuwa akinifanyia mimi.
"Jamani vipi tena?" niliwauliza kwa kuhamaki.

"Hata endelea na kazi tu, sisi tupo," mmoja ambaye hakuwa na kanzu alisema. Kwa mara ya kwanza ndiyo nilimuona akiongea.

Je nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 87.

Niliendelea na kazi, sasa nilikuwa nazibebanisha mbao ili kuzipigilia misumari kwa kuunganisha jeneza.

"Nasikia ilibidi kijana wa watu asafiri mpaka kwao Tanga kutoa taarifa na kuomba msaada lakini bado anamfuata tu," alisema, safari hii ni yule aliyenitaka kuendelea na kazi ambaye hakuwa na kanzu.

"Mh!" niliguna kwanza, nikasimama na kujinyoosha kiuno kisha nikaendelea kupigilia misumari.

"Yaani we acha tu. Kwa kweli anamtesa mtoto wa watu. Na sijui mwisho wao nini?" mwingine ambaye pia hana kanzu alisema.
Nilijikuta nikishindwa kufanya kazi. Si mimi tu, kwa mtu yeyote yule asingeweza kuendelea na kazi hasa nikizingatia kuwa, kila kilichoongelewa kilinihusu mimi japo kwa asilimia sabini na tano.

Vigezo kama kusafiri kwenda Tanga kutoa taarifa na kuomba msaada na vingine waliyoongea yalinihusu mimi.

"Halafu eti anafanya madudu yake ili kijana amuone bibi mwenye nyumba wake ndiye mhusika wa ubaya unaomtokea," mwenye kanzu alisema kisha wenzake wakacheka.
"Eeeh bwana utamaliza leo kweli, maana naona umeduwaa eti," yule yule mwenye kanzu aliyesema na wenzake wakacheka aliniambia akiniangalia.

"Ngojeni kwanza....ngojeni kwanza....huyo...." nilitaka kusema kitu lakini nikakwama sauti.
Lengo langu niwaambie huyo mnayemsema mbona kama ni mimi lakini nikaishia kwenye kusema huyo...!

Nilipokata sauti na wao waliendelea na maongezi yao bila kunijali wala kutaka kujua nilitaka kuongea nini mimi.
"Siku moja nasikia akamuingizia sanduku la kuzika ndani ya chumba chake mpaka kitandani kabisa," alisema mmoja mwenye kanzu.

Wakati wote huo mdogo wangu alikuwa akiendelea na kazi zake kwani hakuonekana kujihusisha na mazungumzo yao. Lakini waliposema alikwenda Tanga ndiyo kama nilimuona akishtuka lakini akarejea kawaida.
Na hii yote ni kwa sababu yote yaliyoluwa yakiongelewa mdogo wangu sikuwahi kumwambia hata siku moja.

Mfano tukio la kutokewa na jeneza chumbani. Japokuwa alikuwepo lakini hakujua nini kilitokea kwa hiyo isingekuwa rahisi kuunga mazungumzo ya wale watu na matukio yangu.

Waliendelea kukaa kwangu mpaka wakati nimemaliza jeneza likabaki kupakwa vanishi tu. Wakainiaga kwamba wanakwenda kuangalia uwezekano wa kupata gari la kubebea jeneza lao.

Je nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 89.

"Wala usipate tabu, mimi nitahakikisha anazeeka na haya maajabu. Na akidiriki kumwambia mtu siku moja namtoa uhai," yule mwanaume alisema akiangalia kama vile hakutaka kuona mbele alikokuwa akielekea.

"Tena usipate tabu, kwani mimi mwenyewe jana nilimfuata nyumbani kwake, nikamchezea lakini hakunitambua hata kidogo," yule mama jirani alisema.

"Hata sauti?" yule mwanaume aliuliza.
"Nini sauti inayoweza kubadilishwa hata miguu hakuitambua," yule mama jirani alimwambia yule mzee.

Walipofika usawa wa kwangu yule mama alimwambia yule mgeni wake wanisalimie mara moja.
"Enhe hujambo kijana?" yule mwanaume aliniambia.

"Sijambo, shi...!" sikumaliza kusema shikamoo, ghafla yule mzee aliweka kidole kimoja juu ya mdomo mmoja wa chini kama ishara ya kunipiga marufuku kumsalimia. Niliacha ghafla

"Hujambo kijana, naona unaandaa pa kumbebea marehemu," yule mama aliniambia akitabasamu huku mikono yote ameichomeka kwa mbele ndani ya kitenge alichojifunga.

Sikumjibu kitu zaidi ya kuendelea kushughulika na kazi ya watu ambayo ilifikia ukingoni sasa.

Mpaka saa kumi na moja na nusu, wale watu waliosema wanakwenda kuangalia uwezekano wa kupata gari la kubeba jeneza lao walikuwa hawajarudi.

Nilimtuma mdogo wangu aende upande wa pili wa mtaa ambako kuna barabara akajaribu kuwaangalia wale wafiwa huenda walikuwa huko wakitafuta uwezekano wa kupata gari. Akaenda na kuniacha peke yangu kazini.

Kwa siku hiyo mimi nilijiona siwezi kufanya kazi tena baada ya kumaliza ile ya jeneza la wale watu. Akili ilichoka sana hivyo nilichokuwa nahitaji ilikuwa ni kuoga na kupumzika kabla ya kula kisha kupanda kitandani kulala.

Wakati nikiendelea kuitafakari hali ya kuchoka mara nilimuona mdogo wangu anakuja huku akisema.

Je nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 90.

"Kaka, kaka mbona wanapakia jeneza kule?"
Nilishtuka kusikia hivyo, nikamuuliza.
"Una uhakika?"

"Nimewaona mwenyewe kaka, hakika ya nini?" alisema akihema wakati ameshafika.
Nilimshika ili kumtuliza kutokana na hali aliyokuwa nayo. Lakini alitulia akidai kuwa, yeye mawazo yake yalikuwa kwamba wameliiba jeneza nililokuwa nalitengeneza baada ya mimi kwenda mahali, lakini alipoliona akapata nguvu.

"Liko hivi hivi kama hili kaka," aliniambia.
Akashangaa imekuwaje sasa, watu waliokuwa wameagiza jeneza pale kwangu, wakalisubiri kwa muda mrefu, sasa inakuwaje waonekane wakiliingiza jeneza jingine ndani ya gari, wamelitoa wapi?
"Tunaweza kwenda kuwaona wote?" nilimuuliza mdogo wangu.

"Twende sidhani kama watakuwa wameondoka," alisema huku akiangalia kwa macho yenye woga.

"Au labda walipoona tunachelewa waliamua kununua jingine lililokwishatengenezwa nini?" mdogo wangu aliniuliza akijishika mikono.

"Wawe wamenunua kwa wapi?" na mimi nilimuuliza kwa sababu katika eneo lile hakuna mtu aliyekuwa akitengeneza majeneza zaidi yangu.

Tulirudisha mlango. Na mimi ndiye niliyerudishia mlango, kisha tukaenda wote hadi barabarani ambako hatukukuta wale watu wala dalili za kuwepo kwao.

"Lakini walikuwepo kaka," alisema mdogo wangu akidhani labda nitapunguza kumwamini baada ya kutowaona wale watu.
"Au tuulizie watu kama wamewaona wakiondoka?" aliniuliza mdogo wangu.
"Hakuna haja," nilimjibu.

Kisa cha mimi kumjibu hivyo ni kwamba, katika hali niliyokuwa nayo moyoni sikuwa napenda kuwajulisha watu mambo makubwa na mazito yaliyokuwa yakinitokea.
Nilimwona mdogo wangu akiangalia angalia chini nikajua alikuwa akiangalia sehemu ambazl labda alama za tairi za gari zingeonekana.

"Ona kaka, ona tairi si hizi?" aliniambia akiangalia bado chini.
Lakini njia ile ilikuwa na magari kila wakati japo si sana. Kwa hiyo haikuwa lazima tairi ziwe za gari hilo walilokuwa wakilitumia wale watu.

Nilimsihi tuondoke licha ya kwamba ufumbuzi ulikuwa hajapatikana.

Je nini kitaendelea?
 

Similar Discussions

7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom