Hahahahah
Mbona bado utampa pole mpaka uchoke
2Sehemu ya 2
Nikavuta kwa mkupuo mmoja na kutoa moshi mwingi kupitia tundu za pua na mdomo, kisha nikatoa pumzi ndefu huku kifua changu kikipanda juu na kurudi chini..
Akili yangu ilinieleza wazi kuwa mke wangu Nasra hakuwa mtu sahihi kwangu, lakini moyo wangu ulinionya kutofanya kitendo chochote kitakacho pelekea kuwa mbali na kiumbe yule mrembo.
Haja ya moyo wangu ikazidi matwaka ya utashi wangu, hali ile ikanifanya nizidi kuangamia nafsini, nikawa mtu wa kujilaumu na kujipinga mimi mwenyewe.
Lakini pamoja na mgogoro huo wa ndani kwa ndani uliokuwa ukinivuruga hata afya ya mwili wangu bado nafsi yangu ilijiapiza kufa Kijerumani na tai shingoni!!!!. Mambo yalianza hivi:
7SEHEMU YA 7
Nilimtekenya kwa siri kwenye kiganja chake nilichokuwa bado nimeking’anga’nia, tendo lile likamfanya anitizame, macho yetu yakagongana. Alishindwa kabisa kuhimili walau kwa sekunde mbili, alitizama chini lile tabasamu lake likigeuka kuwa katika sura nyingine.
Ni hapo nilipobaini ile ziada iliyonivuta katika sura na umbile la msichana huyu.
Aibu!
Alikuwa msichana mwenye aibu! Mmoja kati ya wasichana wachache kabisa duniani waliobakia na aibu. Wengi wao, toka walipoanza kuvaa suruali kama wanaume, kile kirusi kinachoitwa ‘aibu ’ kilitoroka zama za kale katika maumbile yao na hivyo kuwaacha wakavu kama wanaume.
Sifa zake hizo zikiwa zimepambwa kwa mavazi yenye heshima, sketi ndefu iliyovuka magoti na blauzi nyepesi iliyokifanya kifua chake kitoe picha ya uhai wa matiti yake. “Si…si..sija..sijambo,” alinijibu kwa kubabaika huku aibu yake ikiongezeka mara dufu.
“Karibuni sana,” nilisema huku nikiachia tabasamu. Tulielekea kwenye gari langu kisha safari ya kuelekea Kinondoni Studio ikaanza.
Lisaa limoja badaye, tuliwasili nyumbani kwangu, katika nyumba yangu kubwa ya kifahari, wageni wangu niliwapatia chumba kila mmoja na chake, ambapo niliwataka waoge na kubadilisha nguo ili kuchangamsha miili yao kabla ya kurudi mezani na kupata chakula cha usiku.
Mke wangu Nasra nilimwongoza hadi chumbani mwetu ambako pia nilimtaka aoge kabla ya kuungana na mjomba Majeed pamoja na shemeji Asha katika meza ya chakula.
“Faraji...” aliniita kwa sauti ya chini, uso wake ukionekana kuwa na jambo analotaka kunieleza. “Unasemaje mke wangu” akanitizama kisha akasema: “Nataka kuvua nguo” “Eeh, sawa vua tu.” “Unaweza kunipisha nibadili nguo?” mke wangu alisema huku uso wake ukionekana kujawa na haya.
Nilibaki nimeduwaa huku nikiwa sina jibu la kumpa, kwa mara nyingine nikabaini nilikuwa na mwanamke ambaye alikuwa na aibu nyingi.
Igawa awali nilivutiwa mno na hilo, lakini sikutaka tabia ya aibu kwa mke wangu ipite kiasi, kama ilivyokuwa wasaa ule. “Unanionea aibu?”nikamuuliza kwa sauti ya upole ilihali nikitambua hilo halikuwa swali bali jibu.
Alitikisa kichwa kukubali kwa
13Sehemu ya 13
Nilifanya vile makusudi ili mke wangu asibaini chochote kama kuna mambo yasiyo ya kawaida nimeanza kuyashitukia.
Jambo la mwisho nililofanya katika simu ile nilifungau faili lililoandikwa ‘Play store’, nikafungua, kisha nikapakua ‘program’ iitwayo ‘Voice recoder, nikaiseti simu ile kuwa inajirekodi yenyewe simu yoyote itakayokuwa inaingia na kutoka.
Baada ya hapo, nilitulia tuli, moyoni nikiweka nadhiri ya kulifuatilia jambo lile kimyakimya.
Muda mfupi badaye, mke wangu na nduguye walimaliza kupika, aliniandalia chakula, tukala wote pamoja. Wakati wote nilimwonesha tabasamu, sikumwonesha kama kuna kitu kisicho cha kawaida nimekibaini dhidi yake.
Baada ya mlo wa usiku, tulielekea chumbani mwetu kulala huku mdogo wake, Aisha naye akielekea chumbani kwake.
Tukiwa chumbani, kama kawaida tulipeana mapenzi motomoto na kama nilivyokwisha eleza awali, katika kipindi cha miezi sita, tangu nifungue usichana wake, mke wangu alikuwa mjuzi mno kitandani. Tulipeana mapenzi mazito hadi miili yetu iliporidhika.
“Ahsante mume wangu.” “…kwa?” “Penzi tamu, unajua sana kunikuna,” mke wangu alinambia baada ya kumaliza mmenyano. “Kweli?” “Sikudanganyi mume wangu.” “Lakini hata wewe siku hizi umekuwa fundi sana kitandani.”
“Mwongo.” “Kweli mke wangu, sijui nani amekufundisha.” “Nimefundishwa na wewe mwenyewe au umesahau?” “Nikumbushe.”
“Umesahau ‘ningali’ mwanamwali ulichonieleza?” “Nilikueleza vingi, kipi unachokusudia?” Kuhusu aibu.” “Alaa! Kumbe somo hilo.” “Ndio, siku hizi ninalifaulu kwa kiwango kikubwa, ndio maana unaona nimekuwa fundi kitandani,” alisema.
Tulizungumza na kufanyiana utani wa hapa na pale kisha usingizi mzito ukatuchukua. **** Ni asubuhi ya siku mpya, wingu la mvua lilikuwa limetanda, ngurumo za radi zilidhirisha uwepo wa mvua kubwa ambayo ingenyesha asubuhi hiyo.
Magari yalikuwa mengi barabarani, watu walikuwa wakihaha huku na kule kuhakikisha wanakuwa sehemu salama ili kujiepusha na kadhia ya matone ya mvua.
Ngurumo za radi zilizokwenda sambamba na miale mikali, ilifanya asubuhi ya siku hiyo kuwa nzito kwa wakazi wengi wa jiji la Dare es salam.
Mvua kubwa iliyoambatana na upepo ilianza kunyesha, upepo ulikuwa ukizoa
34Sehemu ya 34
“Usijali Faraji, hilo hesabu limekwisha, unajingine?” “Hapana ni hilo hilo.” Baada ya kuzungumza hayo, Dani alichukua laptop yake na kuanza kazi, aliingia kwenye ukurasa wa mke wangu, akachokonoa vile anavyojua yeye, dakika chache badaye, akaunti ile ikawa tunaweza kuiongoza tutakavyo. “Kazi imekwisha, sasa unaweza kuona kila kitu unachotaka,” aliniambia huku akinisogezea laptop ile.
Upesi nikaingia sehemu ya jumbe katika akaunti ya facebook ya mke wangu, mke wangu alikuwa akipokea jumbe nyingi za wanaume wanaomtaka kimapenzi.
Wanaume waliokuwa wakimfutilia mtandaoni walikuwa ni wengi mno, mambo yale yalizidi kuniumiza sana. Bado niliendea kutafuta jina la mtu aitwaye Ally.
Nikiwa naendelea kutafuta jina hilo mara ujumbe ukaingia, ujumbe huo ulitumwa na mtu aitwaye Abdul Ally. Naam! Alikuwa ni mtu yule yule niliyekuwa nikimsaka, Ujumbe uliotumwa na mtu huyo, ulikuwa ni mapenzi.
Ulisomeka hivi: “Vipi mpenzi, unafanya nini sasa hivi? nitumie basi kapicha.” Mate mepesi yalinijaa kinywani, ujumbe ule sikuujibu, nilichofanya ni kuingia kwenye ukurasa wa mtu huyo ili kumtambua vizuri.
“Mungu wangu!” nilipayuka baada ya kumwona mtu yule. Sikuamini macho yangu, nilihisi kutetemeka kwa hasira.
Mtu aliyekuwa akimzuzua mke wangu, alikuwa ni msanii wa muziki ambaye aliwahi kumtumia fedha miaka ya nyuma akitaka ashiriki kwenye video ya muziki. Nikiwa bado katika taharuki ile.
Mke wangu aliyekuwa ‘online’ nikaona anajibu ujumbe ule, akasema: “Niko chumbani, nakuwaza tu wewe, nakutumia kapicha,” nikazidi kutetemeka. Sijakaa sawa, mara picha ikatumwa.
Picha iliyotumwa, ilikuwa ya kifua cha mke wangu, alikuwa mtupu, matiti nje, alijifotoa matiti yake, akamtumia picha hiyo kwa hawala wake.
JE NINI KILITOKEA? TUKUTANE Kesho.
46Sehemu ya 46
Jamaa pamoja na mwonekano wa mwili wa mazoezi, umarufu, uliotokana na kazi zake za muziki, sanjari na fedha zilizompa kiburi hapa mjini, wasaa ule alikuwa zoba mtozeni.
Kwani, baada ya lile teke la tumbo nililomtandika Nasra na kumfanya ajitapikie matapishi, nilimgeukia huyo njemba mwenye misuli thabiti, nikaendelea kumshushia kipigo cha mbwa koko.
Wandishi wa habari wakazidi kurekodi, kufumba na kufumbua utitiri wa watu wakajaa kwenye gesti ile.
Hazikupita dakika nyingi askari polisi waliwasiri, walinituliza kisha wakawataka watu wale wavae nguo, gumzo kubwa kuzunguka gesti ile, ilikuwa ni juu ya fumanizi.
Baada ya mke wangu na mtu wake kuvaa nguo, walitolewa nje na kupakiwa ndani ya defender la polisi, wakati mambo yote yanafanyika picha ziliendelea kufotolewa, mimi, mwenyekiti wa mtaa, pamoja na mhudumu wa gesti, tukatakiwa kuongozana na polisi wale.
Kwa pamoja tuliingia ndani ya gari la polisi na safari ya kuelekea kituo cha Oystabay ikaanza.
Baada ya kuwasiri, mke wangu na yule bwana waliingizwa kwenye ofisi za wapelelezi.
Mimi nikabakia nje,walichukuliwa maelezo mule ndani, muda mfupi badaye wakatolewa, ikawa zamu yangu kuhojiwa na kutoa maelezo.
Nilitoa maelezo mbele ya askari mpelelezi, nikamweleza kila kitu juu ya usaliti wa mke wangu hadi kumfumania.
“Huyo mwanamke ni mkeo au alikuwa mkeo?” askari kanzu akauliza, baada ya kumpa maelezo.
“Ni mke wangu” “Mbona yeye anasema wewe siyo mume wake ila ulikuwa mume wake kwakuwa mlishapeana talaka kitambo sana?”
“Anasema mimi siyo mume wake!” niliuliza kwa mshangao “Ndio, kwa mujibu wa maelezo yake anasema mlikwisha achana muda mrefu tu, ila wewe ndio unamng’ang’ania” askari yule alinipasha, nilishusha pumzi ndefu nikaumia sana moyoni.
Je itakuaje?
No isiwatishe kuruka moja mtiririko upo sawa alisahau kuedit
67Sehemu ya 67
Awali nilidhani labda ni kwa kuwa siku hiyo nilimvamia chumbani kwake akiwa hana maandalizi, lakini hata nilipompa nafasi ya kujifanyia usafi bado alikuwa na harufu kali.
Kuanzia wakati huo, nilijikuta najuta sana kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na mfanya kazi wangu wa ndani, pamoja na kujuta huko, hali ilikuwa tofuati kwa Doren, yeye alikuwa amekufa ameoza juu yangu. Alinipenda mno msichana huyo.
Kitendo cha kupendwa na Doren niliona ingekuwa ni kashfa mbaya mbele ya mpenzi wangu Debora ambaye kwa wakati huo alikuwa safarini.
Doren kwa Debora alikuwa haingii hata robo, achilia mbali kwa mke wangu Nasra ambaye hadi wakati huo naye sikuwa najua habari zake zaidi ya kusikia tu anaishi Tabata.
“Shetani mbaya sana,” nilinong’ona. “Nawezaje kutembea na mwanamke kama Doren.” Nilikuwa nikiongea mwenyewe kila nilipokuwa nikimwangalia binti huyo.
**** Wiki mbili zikiwa zimesalia kabla ya Debora kurejea kutoka safari aliyokuwa amekwenda nje ya nchi, niliona nina kila sababu ya kutengeneza mazingira ya kutokuja kuumbuka mbele yake, dhidi ya uhusiano wa kimapenzi niliounzisha na msichana wangu wa kazi za ndani. Doren.
Nilichofanya ni kumwita na Doren na kuzungumza naye. “Doreen” “Abee” “Nahitaji urudi nyumbani kwa muda.”
“Kwa nini Dear?”akaniuliza huku akiniita jina la Dear, hilo likanitia kichefuchefu pia likachochea dhamira ya kumwondoa kabisa nyumbani kwangu.
“Mpenzi wangu Debora anakaribia kurudi,” nilimwambia waziwazi. “Debora ndiye nani?” Doren akauliza uso wake ukionesha kustajabishwa na kuchukizwa na kauli ile.
“Ni mwanamke niliyekuwa naye baada ya kuachana na mke wangu Nasra.” “Kumbe siku zote ulikuwa unanidanganya?” Doren akauliza huku machozi yakimlenga.
“Nisamehe bure.” “Shida yako ilikuwa ni penzi tu kwangu” “Siyo hivyo” “kumbe?” “Samahani.”
Nikaongea kibwege. “Kwa hiyo unataka kunirejesha nyumbani?” “Ndio.” nikajibu tena bila wasiwasi wowote.
“Hunitaki tena?” “Nasikitika sintaweza kuwa na wewe.” Nilimwambia waziwazi.
Doren alilia kama mtoto mdogo, uso wake ulionyesha ni kwa kiasi gani aliumizwa na jambo hilo, sikuwa na huruma na Doren, moyo wangu haukuwa kwake kabisa. Kilio chake hakikuwa na maana yoyote
80SEHEMU YA 80
Kimsingi ulikuwa ni utaratibu wenye kuudhi sana na kwa kweli Nasra alikuwa akiumizwa mno na utaratibu huo wa maisha, kuna wakati nilipokuwa nikimwangalia usoni niliona haiba ya majonzi na fadhaa kubwa.
Nilimwona mwanamke mwenye majuto maishani, uso wenye kunyanyasika kwa kukosa haki, nilimwona kiumbe mwenye machungu na maumivu makali.
Bahati mbaya au nzuri hakuwa na la kunifanya, wala pa-kunipeleka, alitambua kwamba, kama angaliamua kwenda mahakamani au kwenye taasisi mbalimbali za kirai, ili kudai haki ya kuwa huru na mtoto wake, kama mzazi. Kivyovyote Lazima ningemshinda tu. Pesa zangu zilifanya kazi ya kubatilisha sheria katika jambo hilo.
Nasra aliendelea kuishi katika madhila ya nafsi kwa muda mrefu tu. Wakati mke wangu wa zamani, Nasra Mfaume, akiwa kwenye hangaiko la kukosa haki zake za msingi, kama mama wa mwanangu. Uhusiano wangu na Debora uliendelea kuwa moto.
Nilinenepa nikaongezeka uzito. Msongo wa wa mawazo nilio kuwa nao mwanzo, ulitorokea Dirishani na kuishia zake. Debora naye alikuwa mwenye tabasamu wakati wote. Katikati ya furaha hiyo, likaongezeka jambo jingine lililotuongezea siku za kuishi, vicheko na tabasamu.
Mpenzi wangu Debora, alipandishwa cheo kazini, katika teuzi za rais, naye aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa Wilaya ya Misungwi, huko mkoani Mwanza.
Fursa ile ilitufurahisha. Halikuwa jambo dogo kuaminiwa na rais na kupewa mamlaka yale si jambo la kubeza. Nakumbuka baada ya uteuzi, mke wangu alitakiwa kusafiri hadi jijini Mwanza. Huko aliapaishwa. Siku iliyofuatia akaanza kazi.
Nikiwa nimeambatana naye kama ishara ya kumpa sapoti, baada ya kiapo, nilikaa naye Mwanza kwa kwa siku mbili tatu, kisha nikarejea Dar kuendelea na shughuli zangu.
Huo ukawa mwanzo wa kuwa mbali na Debora. Ile furaha ya kupanda cheo, ghafla ikawa mateso. Hii ni kutokana na umbali uliokuwepo baina yetu.
Maisha yetu yaliendelea. Umbali kati yangu na Debora ukawa ni mtihani mkubwa. Kwa siku za awali nilivumilia, lakini siku zilivyozidi kwenda mbele, nikawa nashidwa kustahimili kumkosa kiumbe yule mrembo.
98SEHEMU YA 98
“Mwanaume kujiua kwa sababu ya mpenzi ni udhaifu mkubwa sana Faraji.”
Afande Mirumbe alizidi kunipasha, kauli yake ilizidi kunifanya nijione mpuuzi. “Siwezi tena kufanya huo ujinga afaande”nilimjibu uso wangu ukionesha kujutia sana.
Alinifungulia pingu akanitaka niwe naripoti kila siku kituo cha polisi hadi pale atakaporidhishwa na mienendo yangu. Jioni ya siku hiyohiyo, niliruhusiwa, nikarudi nyumbani.
Suala langu likawa gumzo mtaani na kwa marafiki. Mama yangu pamoja na dada za zangu walipopata habari zile, kwa kweli walihuzinika sana. Ilikuwa ni aibu kubwa kwa upande wangu. Kutaka kujiua kisa kutoswa na mwanamke. Ilikuwa ni fedheha.
Siku zilikwenda, miezi ikayoyoma. Sikuwahi kumwona wala kuwasiliana tena na Debora, nilikuwa nikiugulia ndani kwa ndani, safari hii nilikuwa tayari kufa kijerumani, lakini sio kutwaa uhai wangu mwenyewe.
Katika hicho hicho kipindi, nikajikuta napata hasara kubwa kwenye miradi yangu ya biashara, nilifunga maduka yangu mawili ya nguo yaliyokuwa pale Kinondni studio, pia saluni zote za sinza nikafanga kutokana na hasaea kubwa.
Nikabakia na duka moja tu la vipodozi ambalo lilikuwa Posta mtaa wa Azikiwe. Mapenzi yalikuwa yamevuruga mno maisha yangu, hata haiba yangu nayo ilinyauka.
Katika kipindi hicho hicho mke wangu wa zamani Nasra, naye alikuwa akijaribu kunioneshea upendo mkubwa kila alipokuwa akija kumwona mwanawe pale kwangu.
Ajabu ni kwamba, moyo wangu kwakwe ulikuwa wa baridi mno, kila nilipofikiria kuwa chanzo cha matatizo yale kilitokana na yeye, sio tu sikumpenda bali nilimchukia!. “Siwezi kuwa na wewe Nasra, sina hisia tena juu yako.” Siku moja nilimwambia, baada ya kujaribu kunishawishi.
“Lakini mwanetu anahitaji malezi ya baba na mama.” “Hilo ulitakiwa ulifahamu tangu mwanzo.” “Usifikirie mabaya yangu tu Faraji, kumbuka mimi naye ni binadamu.” “Hata kama Nasra, lakini dhambi ya usaliti haivumiliki.” “Tafadhali niko chini yako.”
Kila wakati Nasra alisema neno nisamehe, ikafikia hatua nikahisi huenda Nasra anakazana kuniomba msamaha katika kipindi kile kigumu kwangu akiamini inaweza kuwa faida kwakwe kwa kuwa nilikuwa napitia nyakati ninazo hitaji faraja.
....Nimejikuta nikicheka kwa sauti, maana kama nakuona vile unavyoongea hayo....by the way asante sana Dada Shunie
BWANAHARUSI ALIYEJERUHIWA
SEHEMU YA MWISHO
ILIPOISHIA...
“Anahisi nikiwa mbali naye nitakuwa na mwanaume mwingine.”
“Whaat!!”nilimaka kwa hasira.
Nilimsihi sana nikimtaka aje nyumbani, lakini ndugu yangu aligoma, niliwasiliana na mumewe ambaye kwangu ni shemeji yangu, ili amruhusu mkewe aje kunisaidia kumuuguza mama, jamaa yule naye alinikatalia bila aibu. Dada yangu naye alimtii!
ENDELEA NAYO...
WATU huwa wanasema mtoto wa kike kwa mama, wa kiume kwa baba. Katika familia yetu ilikuwa kinyume chake. Ndugu zangu wa kike ambao ndio walitakiwa kuwa mstari wa mbele katika kumuuguza mama yetu wote walimpa kisogo.
Nadhani ni sahihi kusema dada zangu hawakuwa na uchungu na mama yao. Ukichilia mbali yule dada yangu wa Geita, kuna huyu aliyekuwa akiishi Tanga.
Yeye aliniambia hawezi kuja kumuuguza mama kwa kuwa mumewe alikuwa amekwenda nga’mbo kimasomo hivyo asingeweza kutoka kuja kijijini bila ruksa ya mumewe, akaongeza kuwa sheria ya dini ilikuwa hairuhusu yeye kutoka bila ruksa ya mumewe.
Kwa kweli nilikuwa napitia majaribu makubwa mno maishani. Kitendo cha dada zangu kushindwa kuja kumuguza mama yao kwa kuheshimu maslahi ya waume zao kiliniuma. Hata hivyo, kuna kitu nilijifunza kwenye jambo hilo, japokuwa niliumizwa na fikra zao.
Nilibakia na mama nikimuuguza. Mipango ya kilimo niliisimamisha. Niliendelea na kazi zangu za ufundishaji huku kila wiki nikiwa na kazi ya kumpeleka mama kwenye kliniki ya mazoezi.
Alikuwepo shangazi yangu mmoja ambaye mara nyingi alikuwa akija kunisaidia kumpa huduma muhimu kama kumwogesha, kumbadili nguo na kadhalika.
Kama ungepata bahati ya kumwona mama yangu, usingemtofautisha na mtu mwenye ugonjwa wa kiharusi. Mwanamke mnene mwenye mashavu makubwa, hakuwa yeye tena.
Alikuwa amekonda mashavu yamemnyauka na macho yenye makunyanzi yametumbukia kwa ndani.
Kila nilipokuwa nikimwangalia nilihisi uchungu.
Sikujua mipango ya Mungu ilikuwa ni nini, siri hiyo alibaki nayo yeye aliye juu. Mama ndiye faraja yangu iliyokuwa imesalia duniani.
Mama aliishi na maradhi yake kwa muda mrefu sana. Nadhani miezi karibu saba ama nane alikuwa akipambania uhai wake kitandani.
Kila baada ya ya wiki mbili nilikuwa nikimfanyia dua maalumu ili mwenyezi Mungu aweze kumfanyia wepesi katika maisha yake.
Katika kipindi fulani ilifika, yule shangazi aliyekuwa akinisaidia kumuuguza mama, naye aliugua, akawa haji tena nyumbani.
Ikabidi kazi alizokuwa akikifanya nimtafute mwanamke wa kuwa anamsaidia mama kwa malipo ya fedha.
Wakati ambao sikuwa na fedha, nilikuwa nikimuhudumia mwenyewe.
Nililazimika kungojea hadi giza liingie ndio nimwogeshe mama yangu.
Siku moja mwishoni mwa wiki, nilikuwa nimempeleka mama hospitali ni katika kliniki ya mazoezi. Wakati napita getini, nikasikia sauti ya mwanamke ikiniita nyuma yangu.
“Faraji!!”
Nikageuka kutizima. Lahaulaa!! Sikuamini kumwona Nasra Mfaume, mke wangu wa zamani.
Alikuwa amevaa sketi ndefu ya rangi ya zambarau ambayo iliburuza hadi chini. Juu alivaa blauzi nyeupe ya mikono mirefu, kichwani alijifunga ushungi wa rangi ya zambarau. Moyo wangu ulipiga kite baada ya kumwona mwanamke huyo.
“Ni wewe!!”
“Ni mimi...”alijibu uso wake ukiwa wenye tabasamu. Akaendelea kunichangamkia:
“Babari za siku?”
“Salama tu.” Nilimjibu nikiwa sina tashuishi yoyote usoni.
“Vipi kulikoni tena na mama?” alihoji huku akimwangalia mama aliye kuwa katika baskeli ya magurudumu.
“Anaumwa.”
“Ni nini na Tangu lini?”
“Mwaka sasa.”
“Nini tatizo?”
“Kiuno.”
“Poleni sana Faraji.” Alisema.
Nilimpa tabasamu jepesi lililosema: Ahsante.
“Mimi nimekuja jana.” Nasra aliendelea kusema.
Kimoyomoyo nikajisemea: Nani amekuuliza swali hilo?
“Kila la kheri Nasra.” Nilimwambia. Nikaondoka nikimwacha akinisinidkiza kwa macho.
****
Baada ya chakula cha usiku, nilikuwa nikifanya matayarisho kwa kwenda kumwogesha mama gizani. Maji ya moto nilikuwa nikiyapoza kidogo katika ndoo kubwa.
Wakati napeleka maji katika banda la uwani, nikaona kivuli cha mtu nyuma ya banda la kuku akiwa amejibanza. Kwa kuwa ilikuwa giza, nikahisi labda mwizi. Nikapaza sauti kuuliza:
“We nani?” niliuliza.
Nasra akatokeza kwa mwendo wa kunyata!!.
“Ni wewe tena umefuata nini!!” nilimaka.
“Nimekuja kukusaidia kumwogesha mama.”
“Hebu niondoke bwana.”
“Siendi popote.”
“Wewe si mke wa mtu!”
“Hata kama.” Alijibu, akanisogelea zaidi, uso wake mng’avu uling’aa gizani.
Alikuwa ananukia manukato ya mazuri.
“Kuwa mke wa mtu hainizuu kutoa msaada.” alisema.
“Sitaki matatizo hebu ishia zako.”
“Lau kama nisingekuwa chanzo cha mateso mengi maishani mwako, nisingekuwa hapa muda huu.”
“Kwa hiyo?”
“Nipo kulipa fadhila za mabaya niliyofanya kwako?”
“Kwa kumwosha mama yangu?”
Hakujibu. Nikaendelea kumzodoa.
“Kunisaliti, kumtelekeza mwanao na kuharibu maisha yangu. Inalipwa kwa kumwogesha mama yangu! Eti Nasra?” nilihoji huku nikimwangalia Nasra usoni.
Hakujibu alibakia ameghafirika, maneno yangu ni kama yalimgusa.
“Sikiliza Nasra,” nilisema tena.
“Hakuna jambo lolote la wema utakalofanya litakaloweza kunisahaulisha mabaya uliyonitendea, labda moyo wangu uamue tu kukusamehe. Weka akilini hilo.”
Nasra alishusha pumzi ndefu, akachutama na kuangua kilio cha chini chini.
“Huondoki?” nikamuuliza tena.
Alisimama, akataka kama kusema kitu, lakini akaghairi, akatembea kuelekea getini. Nikamfuata nyuma ili akitoka tu nifunge geti.
“Nimepewa talaka na mume wangu!” alisema huku akitembea.
“Kwa nini?”
“Ni kwa sababu sina kizazi!”
“Eeh!!! Kilikwenda wapi?”
Alisimama na kunigeukia kisha akaniuliza swali ambalo nililiona ni la kipumbavu. Akauliza:
“Unataka nikwambie?”
“Ulitegemea sintahoji kizazi chako kimekwenda wapi?”
Alitabasamu, sikujua kama tabasamu lake lilitokana na kufurahishwa na kauli yangu ama vipi.
Ninachokumbuka Nasra Mfaume alianza kunipa maelezo yaliyonikata maini. Alinisimulia:
“Wakati nakusaliti wewe dhidi ya yule sharobaro mwanamuziki, nilipata ujauzito....” alisema. Akasita kisha akaniangalia usoni, uso wangu ulisawijika kwa sentesi ile.
Nikawa kama nimewekwa kwenye theruji. Mwili wote ulipoa. Kumbe mke wangu aliwahi kupewa mimba na hawara wake. Loh!!.
Japokuwa nilikuwa nimekwisha achana na mwanamke yule lakini jambo lile liliniuma, maumivu yake utadhani tukio lilitokea jana tu.
“Eeh ikawaje?” nikamuuliza. Donge kavu lilinikaba kooni.
“Kwa kutotaka wewe kujua kama nina mwanaume mwingine, nilikwenda kuitoa mimba. Ilikuwa ni siri kati yangu na yule bwana.
Sikujua kama kwa kutoa ile mimba kulikuwa na athari, baada ya kuolewa na huyu bwana mwingine athari zake ndio nimeziona, sina kizazi.
Mume wangu huyo ameshindwa kabisa kuwa na simile na jambo hili, amenitaliki kwa kushindwa kumzalia mtoto. Nina siku nne tangu nitoke mikononi mwake.” Alimaliza.
Uso wa Nasra ulijawa machozi, nilishindwa kutathimini kilio chake kilitokana na nini hasa. Je ni kushindwa kupata mtoto?
Ama kupewa talaka? Aidha ni juu ya upumbavu wake wote kwa ujumla.
“Nimejifunza mengi maishani, nataka nisahihishe makosa yangu Faraji” alisema.
“Usiku mwema Nasra.”
Ndio kitu pekee nilichomwambia usiku ule.
Kauli hiyo ilifanya Nasra aangue kilio kama mtoto mdogo, sijui aliwaza kitu gani binti yule.
Labda alidhani naweza kuwa na huruma dhidi yake. Kwa kweli alikuwa mwanamke aliyevuruga maisha yake kwa ujuha wake mwenyewe.
Nilifunga geti na kurudi ndani kwa ajili ya kumwogesha mama yangu kipenzi.
Usiku ule nilipopanda kitandani, nilifikiria mambo yote aliyonieleza Nasra.
Pamoja na kwamba nafsi yangu ilikiri Nasra alikuwa mkosaji, lakini sauti moja ilinisihi kutomchukia daima mtu yule.
“Hakuna binadamu mkamilifu.
Wakati mwingine tunakosea ili tujifunze.” Sauti moja mawazoni iliniambia.
“Kwa makosa aliyoyafanya Nasra, kwa sasa atakuwa mwanamke bora pengine kuliko yeyote yule, maana amekwishakosea na kajifunza.
Mpe nafasi, ” sauti ile iliendelea kunishawishi.
Kwa kweli hadi kunapambazuka, lile donge kavu sijui hata lilipotelea wapi, nilikuwa na fikra tofauti kuhusu Nasra. Nilitaka niishi naye tena, ikiwezekana nimwoe upya!!!!!
*****
Ilikuwa ni siku mpya. Jumapili tulivu. Nilikuwa nimeamka tangu alfajiri nikifanya usafi wa hapa na pale.
Nilimwandalia mama stafutahi ya chapati za kumimina na mayai.
Akiwa anakunywa chai nikwamweleza kila kitu kilichotokea kwa Nasra. Pia nikamwambia nadhiri ya kurudiana na mwanamke huyo.
Masikini ya mungu mama yangu hakuwa na makuu, alikuwa radhi kwa kila kitu nitakacho.
Wakati tunaendelea na maongezi mara mlango wa geti uligongwa, nikamini kivyovyote vile mgongaji ni Nasra. Niliona itakuwa fursa nzuri kama nitazungumza na mrembo yule ili tuingie kwenye makubaliano ya kuanza maisha mapya pale kijijini.
Nilisimama na kwenda kufungua geti. Mara nilikutana na watu ambao sikuwategemea. Walikuwa ni askari polisi wawili waliovalia kijeshi.
“Wewe ndiye Faraji?”
“Kuna tatizo?” nilihoji. Ilikuwa ajabu, sikuwahi kufuatwa na polisi kwa miaka mingi sasa. Leo vipi tena. Kulikoni.
“Wewe ndiye Faraji!!” jamaa walirudia kuniuliza tena kwa amri.
“Ndio ni mimi, kuna nini?”
“Unahitajika kituoni.”
“Kuna tatizo gani?”
Jamaa hawakunipa jibu. Walinishika na kunipeleka kituoni. Hadi tunafika sikuwa nimejua kwa nini nikamatwe, ingawa kuna wakati nilihisi huenda kuonana kwangu na Nasra kuna uhusino fulani wa mimi kushikwa na polisi.
“Wewe ndiye Faraji Mpangalala?”mkuu wa kituo aliniuliza baada ya kuingizwa ofisini kwakwe.
“Ndio mimi. Kuna nini Afande?”
“Kwani hujaambiwa?”
“Sijaambiwa chochote!”
“Askari waliokuja kukukamata Ilibidi wakwambie wanakukamatia nini.”
“Hawakunieleza!” nilisema.
“Unahusishwa na kifo cha Nasra Mfaume” kamaanda alipasua jipu.
Lilikuwa ni bomu lililonifanya nilihisi ni ndoto inanipitia nikiwa nimelala usingizi.
“Nasra....Nasra ame....Nasra amekufa lini?”
“Jana usiku.”
“Jana usiku!!!!
“Ndiyo.”
“Nilikuwa naye!!!!”nilisema kwa wahaka huku nikimwangalia usoni yule kamanda.
“Tunajua ulikuwa naye, lakini baada ya kuachana naye ndipo alipokutwa na mauti?”
“Kivipi? Ilikuwaje? Kwa nini na wapi?”
“Hayo maswali nikuulize wewe!!”
“Whaat!!” nilimaka.
“Nisikilize bwana mdogo.” alisema kamanda akiwa ananiangalia kwa makini.
“Uchunguzi wa awali unanaonesha Nasra amejiua mwenyewe kwa kisu ndani ya chumba chake.”kamanda yule alisema huku akikuna ndevu zake zilizokuwa zimepunguzwa kwa mtindo wa mustachi.
“Hata hivyo Nasra kaacha ujumbe wenye maelezo yasiyojitosheleza sababu ya kujiua kwake, ujumbe huo unakutaja wewe kuwa moja ya sababu ya yeye kujiua, ndio maana uko hapa kusaidia polisi.”
“Uko wapi huo ujumbe?”
Alinipa kipande cha karatasi kilichoandikwa na Nasra. Nilisoma maneno yaliyoandikwa kwenye ujumbe ule yalinikata maini. Aliandika hivi:
“Faraji mpenzi...
Sioni, sababu ya kuendelea kuishi katika dunia kwa mateso makali ya nafsi. Dunia imenielemea na imenishinda. Hiki ndicho ninanistahili. Nisamehe kwa yote niliyokutendea maishani, angalau nakufa ili nikaungane na mwanetu Mwanda huko akhera.”
“Nooooo!” nilipiga kelele nikalia kama mtoto.
***
Siku mbili badaye niliachiwa huru baada ya uchunguzi wa kipolisi kuonesha sikuwa na kesi ya kujibu, niliwaomba polisi nikapaone mahali Nasra alipojiulia. Nikapelekwa kwao, mtaa wa Bweru.
Chumba cha Nasra kilikuwa kimefungwa kwa amri ya polisi, nilisukuma mlango nuru ya mwanga hafifu ikaangaza chumbani. Kitandani kulikuwa na mashuka yaliyotapakaa damu iliyokaukiana.
Damu ya Nasra Mfaume, damu ya Mwanamwali.
Nilimlilia Nasra hadi macho yakavimba, kifo chake kiliniuma mno, kwa kweli moyo wangu ulikuwa na majeraha makali sana.
Wiki moja badaye, Nasra alizikwa katika makaburi ya Lugongoni.
Mimi bado naishi kijiji cha Nguruka mkoani Kigoma, naendelea kumlea mama yangu ambaye bado hajaweza kusimama.
Mwisho kabisa nakushukuru kwa kusoma simulizi hii ya kweli ya maisha yangu. Naamini kuna funzo umepata maishani.
MWISHO.
Usikose kufutilia simulizi mpya
Huu ndio ushauri wa kumpa faraji kweli? Au unataniaOohoo bora hata ungemgonga house girl wako
Poa shunieMwisho wa Azra Malama - JamiiForums Simulizi: Niliyoyaona Darfur yanatisha - JamiiForums
Story nyingine hizo hapooo