Simulizi: Bwana Harusi aliyejeruhiwa

Simulizi: Bwana Harusi aliyejeruhiwa

SEHEMU YA 59

Maneno ya Debora, ofisa ustawi wa jamii, yalinikata maini, nikawa nimezodoka kama tahira, nilimkata jicho Nasra na hawara wake, nikaona wakiwa kwenye uso wa tabasamu pana.

Debora, alitulia kidogo kuzungumza, naye ni kama alikuwa akisaili mwonekano wa nyuso zetu. Akaendelea kuongea.

“Sheria ya Tanzania inampa mtoto haki ya kuishi, tena kwa hadhi, heshima na uhuru, sambamba na kupatiwa elimu bora na maelezi.

“Hivyo basi, nahitimisha kwa kusema, mtoto wenu kwa kuzingatia umri wake, atakuwa chini ya malezi ya mama kuanzia sasa hadi pale atakapofikisha umri wa miaka saba, ndipo baba yake atakapokuwa na haki kisheria ya kuishi naye,” alimaliza kueleza.

Nilihisi uchungu mkali sana kufuani, hasira kali ikanipanda kichwani, nikatamani ningekuwa na bastola, ningewamalizia mbali watu wale.

Baada ya sakata hilo kuamuliwa katika mtindo ule, mchakato uliokuwa ubeakia ni mimi kupewa barua, ambayo ilinitaka kumkabidhi mtoto Nasra ndani ya siku saba.

Nilijikuta namchukia sana Debora, kitendo cha kutoa haki kwa Nasra, mwanamke alieisaliti ndoa yake bila haya wala staha, kisha kupewa haki zile, ilikuwa ni uonevu mkubwa sana nliotendewa.

Nilisimama na kuondoka, jasho lililowanisha maungo yangu. Wakati nakatiza kwenye, maegesho ya magari kulifuata gari langu, nikasikia sauti nyuma yangu ikiniita. “Faraji.” Nilipogeuka nyuma.

Alikuwa ni Debora.Ofisa Ustawi na rafiki wa zamani. Hakimu aliye nihukumu akimwacha mtesi wangu kwenye tabasamu la ushindi.

“Nakuomba tukutane Lamada Galden, nikuelekeze jambo unalotakiwa kufanya katika sakata hili,” aliniambia haraka haraka.

Ni kama hakutaka kuonekana akiwa na mimi eneo lile. “Unieleze jambo gani, nawe umekwisha kuwa mshenzi tu,” nilimjibu kwa ukali. “Kama unataka kuishi na mwanao nisikilizie ninachokueleza.”
 
SEHEMU YA 60

“Huna lolote mnafiki tu.” “…tafadhali” “TOKA,” nilibweka kwa sauti ya ukali.

Sikumwelewa kabisa Debora, niliona ni kama mtu aliyekuwa akinisanifu baada ya kupewa hukumu ile.

Niliingia kwenye gari langu na kuondoka. Nikamwacha amebung’aa haamini kama ningeweza kumtosa.

Nikiwa kwenye foleni ya mataa, pale Magomeni Kanisani, mara simu yangu ikaita, kucheki kwenye kioo, namba ngeni. Nikapokea. “Debora hapa,” sauti ya Debora ilisikika punde baada ya kupokea.

“Hivi we mwanamke unataka nini hasa? Umekwisha amua ninyang’we mtoto, hizi simu za nini hasa?”

“Sio mimi niliyeamua unyang’anywe mtoto bali sheria.” “Sasa unachokitaka kwangu ni kipi?”niliongea kwa ukali.

“Nataka nikupe mbinu ya kubaki na mwanao.”

“Kwa nini wewe hukuwa wa kwanza kuzitumia hizo mbinu, ukaniachia mwanangu.” “Ndio maana nataka tuzungumze.”

Kabla sijatia neno, taa ya kijani ikawaka kuruhusu magari ya upande wangu, sikuona haja ya kukinzana na Debora, niliona heri nimsikilize anachotaka kuniambia.

Nikamwambia aje La charse Pub majira ya jioni. Masaa machache badaye, Debora alifika La charse.

Tukiwa kwenye meza moja katika kona ndani ya bar ile alianza kuzungumza. “Kwanza nikutake radhi kwa maamuzi yote niliyoyafanya, ambayo kwa namna moja ama nyingine, yamekumiza.

“Namna kesi hii ilivyo, popote pale sheria haikupi haki ya moja kwa moja, lakini lipo jambo moja tu linaloweza kukupa haki ama matamanio uliyonayo.” “Jambo lipi?” nikauliza kwa kiherehere. “Pesa,” aliniambia.

Nilishusha pumzi kwa nguvu, nafsi yangu ikakiri pesa ndio mwarobaini wa wa kiu yangu.

Kama ni hivyo, hakuna tatizo, niambie tu ni kiasi gani unahitaji?” nilimuuliza. “Hujanielewa bado….” alisema akanyanyua glasi ya bia na kupiga funda moja kisha akaendelea.
 
SEHEMU YA 61

“Kesi hii ili imalizike salama, bila lapsha, sharti iende mahakamani, huko ndiko pesa itakapotumika na si kwangu.”

“Kwa nini?” “Kwa sababu huo ndio mhilimi wa mwisho unaotoa tafsiri ya sheria.” “Sawa, lakini wewe ulishidnwa nini kunisaidia?”

nikamuuliza “Pamoja na sheria zilizopo, lakini maamuzi haya hayakuwa ya kwangu peke yangu ni maofisa wote tuliona hukumu hii ndio inatakiuwa.”

“Kwa hiyo maofisa ustawi wote mlikubalina mimi nisibaki na mwanangu?” “Ni kwa mujibu wa sheria, pia naweza kukujibu ndivyo.” “Sasa kwa nini unawageuka wenzio?”

“Ni kwa sababau wewe ni rafiki yangu, na bosi wangu wa zamani Faraji, nisingependa urafiki wetu ukaingia doa.” Aliniambia kwa sauti ya kubembeleza.

Siku hiyo niliongea mambo mengi sana na Debora, napenda niseme chuki yote iliyokuwa imejazana kifuani mwangu dhidi yake, iliyeyuka kama bonge la barafu juani, sikuona sababu ya kumchukia mrembo yule.

Siku iliyofuatia, mchakato wa kufungua kesi mahakamani niliunza nikisaidiwa na wakili wangu, nikaucheza mchezo mchafu katika maeno yote muhimu. Pesa ikatumika kuwanunua maofisa wa mahakama akiwemo Hakimu Ndauka.

Ndani ya wiki mbili tu badaye, mahakama ikatoa hukumu, mimi ndiye nikatakiwa kubaki na mtoto na kumpa malezi yote muhimu!.

Ilikuwa ni siku nzuri sana, nakumbuka siku hiyo, Nasra alipatwa na taharuki kubwa sana baada ya hukumu hiyo kutolewa.

Nilimtusi moyoni na kumwona punguani anayejitia kusikitikia kuishi mbali na mtoto wake ilihali yeye ndiye chanzo cha hali hiyo.

Nilimpigia simu mama, pamoja na ndugu wengine kuwapa habari juu ya hukumu ya mahakama, ndugu wote walifurahi sana.

“Kwa hiyo nifurahi tu na mjukuu wangu kwa raha na amani?” mama aliniuliza simuni kwa furaha. “Kazi kwako mama.”
 
SEHEMU YA 62

Ilikuwa ni furaha kubwa. Siku hiyo nilikwenda bar, nikiwa pamoja na Debora, tukanywa pombe hadi usiku mkubwa, hapa nataka nikueleze kitu kimoja ndugu msomaji:

Kama nilivyosema awali, tangu nitengane na mke wangu, na kujiingiza kwenye tabia ya ulevi, nilikuwa mlevi haswaa. Kama utakumbuka vizuri, nilisema nilinjiingiza kwenye ulevi ili kuondokana na msongo wa mawazo niliokuwa nao baada ya kumfumania mke wangu.

Ukweli ni kwamba, pombe ilinipa starehe muda mfupi tu ambao nilikuwa nimelewa, lakini ikishaisha tu kichwani, mawazo ni kama yalizaliwa upya.

Maumivu ya usaliti yalijirudia kama mwanzo. Tukio la mke wangu akifanya mapenzi na Ally katika nyumba ya kulala wageni, ilikuwa ikijirudia.

Hali hii ni kutokana na akili yangu ilikuwa haiwaza mambo mapya, muda ambao ningetakiwa kufikiria namna ya kukabiliana msongo, ungekuta ubongo wangu umelewa pombe.

Tofauti na siku zingine, siku hiyo nikiwa na Debora, nilikunywa, ama tulikunywa nafsi yangu ikiwa na furaha, furaha ya ushindi. Ushindi wa kumbakiza Mwanda mikononi mwangu.

Baada ya masaa mengi kupita, nikiwa nimelewa chakari, nikamtaka Debora tuondoke.

“Leo nahitaji kulala na wewe, kitanda kimoja,” Debora aliongea kwa sauti ya kilevi.

Na muda huo huo, akaingiza mkono wake kifuani mwangu na kunichezea viyweleo. Ingawa nilikuwa nimelewa lakini kauli ile iliniingia, na mwili wangu ukapatwa na misisimko ya mapenzi kutokana na alivyokuwa akinipapasa.

Nikasahau kabisa uvumi nilowahi kuusikia. Kuhusu Debora kuishi na maambuki ya virusi vya Ukimwi, hisia za mapenzi zikanivaa, nikawa tayari kumpa penzi. Ofisa Ustawi wa Jamii.

JE NINI KITATOKEA?
 
SEHEMU YA 63

Na muda huo huo, akaingiza mkono wake kifuani mwangu na kunichezea viyweleo. Ingawa nilikuwa nimelewa lakini kauli ile iliniingia, na mwili wangu ukapatwa na misisimko ya mapenzi kutokana na alivyokuwa akinipapasa.

Nikasahau kabisa uvumi nilowahi kuusikia. Ni kuhusu mwanamke huyo kuishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi, hisia za mapenzi zikanivaa, nikawa tayari kumpa penzi.

Mwanamke yule akaendelea kunipapasa kifuani huku pumzi za huba zikimtoka. Viganja vyake vikashuka hadi ndani ya suruali yangu, akawa anamchezea mzee wa kazi aliyekuwa wima kama msumari.

Tendo lile likanifanya nitamani kumalizana naye palepale gizani, si nikaanza kufungua zipu ya sketi yake…. “No, no, nenda kachukue room,”alininong’oneza kwa sauti laini ya mahaba.

Nikaona isiwe tabu, wacha nikachukue chumba. Kwa kuwa palepale La charse pub huwa kuna huduma ya vyumba vya kulala wageni, nilimweka pembeni Debora, nikaenda kaunta kuulizia kama bado kuna nafasi ya vyumba.

Bahati ilikuwa upande wangu, nilipata chumba, nikalipia kisha nikamrudia Debora. Nilimshika mkono nikamwongoza chumbani kama kondoo aongozwaye machinjioni.

Baada ya kuingia ndani, nilisaula nguo zangu zote, Debora naye akafanya hivyo, kila mtu alikuwa na haraka ya kukata kiu ya penzi kwa mwenziye. Baada ya kuwa saresare maua, tukaanzishiana tena michezo ya kupashana joto.

Kwa kuwa mchezo wa kupashana joto ulikwishaanza tangu tukiwa nje, mule ndani haukudumu japo kwa dakika tatu, tukajikuta tumezama kwenye ulimwengu mwingine wa raha.

Asubuhi kulipokucha, mimi ndiye nilikuwa wa kwanza kuamka, Debora alikuwa bado anakoroma, akili ilipokaa sawa, nikajikuta napatwa na hofu kwa kitendo cha kuteembea na Debora.

Kama nilivyosema mwanzo, mwanamke yule amewahi kuhusishwa kuishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Nikiwa pale kitandani, nilikosa raha, nikajilaumu kwa kuzidisha ulevi kiasi cha kushindwa kuzidhibiti hisia zangu.

Nikajiambia kimoyomoyo, kama nitakuwa nimeambukizwa Ukimwi, mke wangu Nasra hawezi kukwepa lawama maana bila yeye, nisingefikia kuishi maisha yale. Nikiwa kwenye hali ile Debora aliamka.

“Mambo sweet,”akanisalimia. “Poa tu, umeamkaje?” “Niko fresh, yaani najisikia mwepesi!...Ugwadu nili
 
SEHEMU YA 64

“Ndio, nilikuwa na muda mrefu sana bila kuwa na mwanaume.”

“Kwa nini?” “Wanaume wengi wananiogopa. Wanadai nina ngoma,” Debora alisema, nikajiweka vizuri pale kitandani ili tuzungumze kuhusu jambo hilo.

Ukweli ni upi Debora, maana hata mimi nimewahi kusikia uvumi huo, na asubuhi hii nimejikuta nakosa raha sana juu ya jambo hilo.”

“Sina Ukimwi Faraji, ila nakiri nilikuwa na mpenzi wangu ambaye alifariki kwa Ukimwi, tangu wakati huo nimekuwa nikihusishwa kuwa nimeathirika, lakini ukweli ni kwamba, mimi sina Ukimwi.”

Maneno ya Debora yalinifanya nijisikie vizuri, japokuwa hakunionyesha uthibitisho wa kauli ile, hata hivyo angalau nilihisi ahueni nafsini.

Kuanzia wakati huo, mimi na Debora tukawa wapenzi, kila siku jioni tulikutana La charse pub, tulikunywa pombe, tukacheza muziki safari yetu ikawa inaishia kwenye chumba cha kulala wageni.

Penzi langu na Debora likafanya nimsahau mke wangu Nasra, yale maumivu niliyopewa na mke wangu yakawa yanayeyuka kifuani mwangu kama mshumaa uwakao.

Siku moja Debora alinieleza amepata safari ya kikazi, nje ya nchi, aliniambia atachukua takribani miezi miwili kuwa mbali na mimi.

Haikuwa taarifa nzuri kwa upande wangu hasa kwa kuwa mwanamke yule alikuwa ndiye mwarobaini wa maswahibu yangu ya moyo, sikuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana na jambo lile nililoelezwa.

Siku chache badaye, Debora akaondoka, nikabaki kama kinda la ndege lililoachwa na mama yake. Katikakati ya upweke huo, jioni moja baada ya kutoka kazini, nikiwa bar napata moja moto moja baridi, katika hali nisiyo itarajiwa, nikamwona hawara wa mke wangu, akiwa meza ya pembeni akinywa pombe kali.

Wakati huo ilikuwa yapata saa mbili usiku, jamaa huyo, hakuwa peke yake, alikuwa na jamaa wengine kama watatu ambao kwa mwonekano walikuwa pia wakijihusisha na sanaa ya muziki.

Hakuwa ameniona, na mimi sikupenda anione, ingawa kitendo cha mimi kumwona kiliniumiza sana, picha ya siku aliyokuwa akifanya mapenzi na mke wangu ikawa inajitengeneza akilini mwangu.
 
SEHEMU YA 65

Nikajikuta namchukia sana yule jamaa, uwepo wake katika bar ile ikanifanya nitamani kuondoka, nikajiambia moyoni, nikimaliza bia iliyokuwa mezani, lazima ningeondoka na kurudi nyumbani.

Baada ya kama dakika 20 tangu nibaini uwepo wa jamaa yule kwenye bar ile, mara Nasra nikamwona anaingia ndani ya bar ile.

Nilikuwa na siku nyingi sijamwona mwanamke huyo, siku hii ni kama alikuwa mpya machoni, nasema alikuwa mpya kutokana na namna alivyokuwa amebadirika.

Nasra alikuwa amependeza, alivaa suruali ya jinsi iliyombana na kufanya hipsi na wowowo lake lijidhihilishe waziwazi, wakati juu alivaa kiblauzi kilichomkaa vema kiasi cha kutoa taswira ya matiti yake.

Nywele zake ndefu alizibana kwa pamoja na kuacha kimkia kidogo kikining’inia. Rangi ya ngozi yake iling’ara, tembea yake iliwafanya baadhi ya wanaume wakware wageuke na kumtupia jicho la uchu.

Yule Nasra, mwanamke mpole na mchamungu, ambaye wakati wote alivaa hijabu na kuzihifadhi tupu zake, hakuwa yule niliyekuwa nikimwona umbali mdogo mbele yangu.

Nasra alitembea hadi katika meza ya bwana wake, akavuta kiti na kuketi, mambo yote hayo niliyashuhudia nikiwa umbali mchache sana kutoka mahali walipokuwa wao.

Moyo wangu uliniuma mno, wivu ulinishika hadi nikahisi kifua kinataka kupasuka, nilisimama nikiwa nimevurugwa vibaya sana, nikatoka nje na kurudi nyumbani.

Wakati huo ilikuwa yapata saa tatu usiku, Doreen alinifungulia geti nikapitiliza hadi sebuleni, nikaketi sofani nikitafakari maumivu ya moyo wangu.

Doreen, msichana wa kazi za ndani, akaniletea maji ya baridi katika glasi. Huwa nashindwa kuelewa, sijui kwa nini Doreeni huwa ananijali kwa kunipa huduma za hapa na pale pindi ninapokuwa katika madhila.

Wakati anaweka glasi ile mezani, niliona chuchu zake zikiwa wima, zimetuna kama vikombe vya kahawa, wakati anaondoka, macho yangu yakashuhudia wowo zuri likitikisika katika mtindo wa ‘Singida, Dodoma’ shetani wa ngono akanivaa, nikajikuta namtamani Doreen na kusahau habari za maumivu ya Nasra na Debora.

JE? NINI KITATOKEA. USIKOSE KUFUATILIA SIMULIZI HII YA KUSISIMUA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom