Sehemu ya 44
Sikuamini macho yangu. Nasra Mfaume, mke wangu wa ndoa, alikuwa amekunjwa na mwanaume mrefu mwenye misuli, wakiwa kama walivyozaliwa, waliikuwa wakifanya mapenzi, jamaa alikuwa amemkunja mke wangu kwa mtindo ambao mimi sikuwa kumfanyia mwanamke yule.
Nilijikuta nalia kama mtoto mdogo aliyetelekezwa na mzazi wake, mke wangu mrembo, niliyempenda kwa dhati, alikuwa amenipa pigo takatifu.
Baada ya kuona wameingiliwa, walishituka mno, hakuwategemnea kabisa tukio lile, wakiwa kwenye hali ya kuzubaa na taharuki kubwa, Issa na wenzake walikazana kufotoa picha.
Yule mwanaume alikuwa wa kwanza kugutuka na kuona alitakiwa afanye kitu kijificha na aibu ile, haraka alivuta shuka na kujifunika, hata hivyo alikwisha chelewa sana, picha nyingi zilikwisha ingia kwenye kamera za waandishi.
Mke wangu naye, baada ya kugundua alitakiwa ajistiri akavuta shuka jingine na kujifunika. “Tusameheni jaman,” hatimaye jamaa akasema, kauli ile ilikuwa ni mthili ya petrol katika moto, iliniudhi sana, hasira zilinipanda, nikiwa bado kwenye kilio cha uchungu, nilimsogelea na kutandika ngumi mbili za uso.
Kufumba na kufumbua uso wake ukajaa damu, tukio hilo likamliza mke wangu kwa hofu. Naye akaanza kuomba msamaha, tendo hilo likachochea chuki, nilimvaa na kutandika teke la tumbo akatapika chipsi kuku alizolishwa na yule bwana.
Mambo yote hayo yalikuwa yakirekodiwa na wale waandishi wa habari chakaramu.
Ndugu msomaji, nakusihi sana, kama unatabia za kutembea na wake za watu acha kabisa mchezo huo, nasema hivyo kwa sababu najua hali utakayokutana nayo siku ukifumaniwa.Na nakuhakikishia ndugu yangu, kama umezoea kula vya watu, ipo siku utakamatwa, usiombe kabisa ukutwe na tukio la kufamaniwa.
Haijalishi unazo nguvu nyingi, pesa, ama mamlaka katika serikali, ukifumaniwa na mke wa mtu, ndugu yangu, utapata tabu sana, hutowezi kabisa kupambana na mwenye mali wasaa huo.
Na sio siri, pamoja na sifa zote hizo ulizonazo, lakini mbele ya mume aliyekufuma na mkewe, huna la kufanya, unaweza jikuta unauawa na mwanaume dhariri, ambaye hajai kiganjani mwako, ikiwa tu, atakufumania na mkewe. Waswahili wanasema mke wa mtu ni sumu