Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,076
- 463,978
- Thread starter
- #561
SEHEMU YA 104
Mpenzi msomaji,mikasa yote hiyo ilinitokea kwa muda mchache mno, kama utakuwa ulinifatilia kwa makini, utabaini kwamba, kupolomoka kwangu kiuchumi kulitokea ndani ya masaa 72 tu.
Na sasa niliona natakiwa kuuza nyumba niliyokuwa nikiishi ili mtoto wangu apone.
Naam! ilikuwa ni lazima akafanyiwe upasuaji wa moyo nchini India. Zaidi ya milioni 22 za matibabu ilitakiwa ili mwanangu aendelee kuishi. Nifanye nini mimi!.
Nilijiuliza kimoyomoyo, mwanangu nilimwitaji sana maishani, lakini hata nyumba yangu pia sikupenda kuipoteza kabisa.
Nilikwenda kwenye ATM ya pale pale Muhimbili nikangalia kiasi cha fedha kilichosalia kwenye akaunti yangu.
Nikakuta nina milioni nane peke yake. Kwa hesabu za harakaharaka, nilikuwa bado nahitaji angalau milioni 15 ili kuyanusuru maisha ya Mwanda.
Niliwafikiria ndugu na marafiki zangu, nikaona naweza kujaribu kuomba msaada hata kwa kukopeshwa ili niweze kupata kiasi kile cha fedha.
Nilichofanya ni kuwasilina na watu wangu wa karibu. Waswahili wanao msemo usemao, siku ya kufa nyani, miti yote hueteleza.
Kila rafiki na ndugu niliyekuwa nikimgusa, naye alinibwagia matatizo yake lukuki.
Hadi jioni inatimu sikuwa nimepata mtu yeyote wa kunisaidia. Nilirudi wodini alipokuwa amelazwa mwanangu, nikaketi kando ya kitanda chake.
Mtoto wangu mzuri, alikuwa katika usingizi wa nusu kaputi. Alikuwa akipumua kwa kutumia Mashine maalumu za Oxjen, hata kula alitumia mipira.
Nikiwa pale, niliwasiliana na mama yangu, nikampa taarifa juu ya hali ya mtoto wangu na maamuzi ya mke wangu wa zamani Nasra.
Kunitelekezea mtoto na kwenda kuolewa na mwanaume mwingine huko visiwani pemba. “Mwanamke punguani kweli huyo, kaamua tena kumkimbia mwanaye!”
“Ndiye mke mliyekuwa mmenichagulia mama.” Kauli yangu ilimuumiza mno mama. Kupitia simu nikamsikia akinung’unika kwa makosa waliyoyafanya yeye na marehemu baba kunitafutia mke mpumbavu.