Simulizi: Bwana Harusi aliyejeruhiwa

Simulizi: Bwana Harusi aliyejeruhiwa

SEHEMU YA 32

Nikatega sikio. Jambo alilokuwa akiliongea na mtu wa upande wa pili, lilinitisha sana. Mapigo yangu ya moyo yakanienda kasi hadi nikaogopa.

NILIENDELEA kubana pale koridoni, mwili wote ukitetemeka. Mazungumzo kati ya mke wangu na mtu wa upande wa yalikuwa hivi:

“Mume wangu amegundua kama natoka nje ya ndoa,” alisema. “Wacha wewe!” sauti ya mwanaume upande wa pili ikahamaki. “Ndio, amekwishajua kila kitu.” “Kajuaje. Ameona akaunti yako ya facebook?”mtu yule akauliza.

“Hapana. Amejua kutokana na kuzorota kwa afya ya mwanangu. Kumbe ile michezo tuliyokuwa tukifanya ilikuwa sumu kwa mtoto” “Kivipi?” “Nilikuwa nikimbemenda…”

“Mimi si’ nilikwambia umwachishe ukabisha.” “Sasa kama ningemwachisha, ningemwambiaje mume wangu?” “Sababu ziko nyingi Nasra.” Jamaa alimwambia mke wangu, kimya kifupi kikapita, kisha wakaendelea na maongezi “Sasa tunafanyaje?”

“Wallah Ally mie bado nakupenda,”maneno yale yalitoka kinywani mwa mke wangu. “Najua, lakini hujapewa talaka bado.”

“Nitahakikisha wiki hii naipata hiyo talaka, nahitaji kushi na wewe Ally.” Yalikuwa ni maneno mabaya sana kusikika masikioni mwangu, pale nilipokuwa nimesimamaa nilihisi kizunguzungu, nilijiona nipo angani naeleea. Akili ilinizunguka.

Dunia kwangu ilikuwa kubwa mno. Nilijiona kiumbe mdogo mithili ya sisimizi. Nikiwa pale kiridoni, nikawaza, nimvae mke wangu na nimfanye kitu mbaya, ama nimpe talaka kisha niachane naye kiroho safi.

Wazo la kumwacha kwa amani, niliona nitakuwa siitendei haki nafsi yangu, nikaamini, hatua nzuri kabla ya kumwacha ni kumkomesha. Kadhalika. Nikaamini kumkomesha mke wangu peke yake ilihali yupo mjinga mwingine aliyenichoma kijiti jichoni, bila kumuadabisha nitakuwa nimeidhulumu nafsi yangu.

Kabla mke wangu hajashitukia uwepo wangu, nikanyata na kurudi nje, bahati nzuri hapakuwa na yeyote aliyeniona. Nilitembea kwa mguu hadi katika kituo cha madereva bodaboda, nikachukua usafiri huo, nikamtaka dereva anipelekea Mbezi Temboni.

Niliazimia kwenda Temboni kumwona jamaa yangu mmoja aitwaye Daniel Mwansasu, watu hupenda kufupisha jina lake na kumwita Dani, huyu alikuwa ni mtaalamu wa mambo ya ‘Information Technology’ (IT)ambaye alikuwa
 
SEHEMU YA 33

Lengo la kumfuata huyu mtu nilitaka anisaidie kuingilia mawasiliano ya Facebook ya mke wangu (HALK), ili niweze kumtambua mtu niliyemjua kwa jina moja la Ally, niliamini ndiye kirusi kilicho iharibu ndoa yangu.

Baada ya kufika nyumbani kwa jamaa huyo, ambaye hadi wakati huo alikuwa akiishi nyumbani kwa wazazi wake, bahati nzuri nilimkuta, siku hiyo alikuwa ni ya mapumziko kazini kwake.

“Ooh! Faraji…” Dani alinilaki baada ya kuniona. “Karibu, naona leo umenifanyia uvamizi wa kimyakimya” “Ahsante sana Dani, nisamehe kwa kukuvamia.” “Sio kitu Faraji, karibu sana, pita ndani.”

Dani ni mtu mmoja mcheshi na makarimu sana, aliendelea kunikaribisha, usoni mwake akiwa katika tabasamu pana.

“Tangu uachane na ukapela umenitupa sana mwanao.” “Hapana Dani, si kwa sababu nilioa, ni mihangaiko tu ya maisha.” “Kweli, haya leta habari.

Uso wako unaonesha unalo jambo tata sana,” Dani alisema. “Ndio. Hujakosea Dani.” “Kuna nini tena?” Nilivuta pumzi, nikazitoa kwa nguvu, nikaanza kumuhadithia mkasa wote, nilimweleza kila kitu bila kumficha.

“Loh! Pole sana Faraji.” “Ndio ukubwa, nimekwisha poa Dani.” “Mimi naogopa sana ndoa, wanawake ni viumbe washenzi sana, hasa wanapozongwa na mihemko ya kiwendawazimu,” Dani alisema kwa kulalama, maswahibu yangu yalimgusa sana.

“Sana Dani,” nikashadadia. “Ulikuwa kipofu Faraji, haya mambo ungekwisha yatambua mapema tangu mama yako alipokuwa akikueleza. “Ni kweli nilikuwa kipofu,” nilisema kwa huzuni.

“Kwa hiyo ulikuwa unataka msaada wa gani hasa?” “Swali zuri…”nilimwambia, nikaendelea. “Kwanza kabisa nataka niachane na huyu mwanamke, pili nataka niwakomeshe yeye na hawara wake.”

“Kuwakomeshaje?” “Nataka niwadhalilishe.” “Duh! Sasa mimi naingiaje hapo?”

“Kama nilivyokwambia, sijamtambua moja kwa moja mwanaume anayemzuzua mke wangu, lakini inavyoonyesha mawasiliano yao yapo zaidi facebook.”

“Kwa hiyo unataka ni-hack akaunti ya mkeo ili kumnasa huyu mtu?” “Ndio. Hilo ndio kubwa ninalolitaka kutoka kwako.”
 
Sehemu ya 34

“Usijali Faraji, hilo hesabu limekwisha, unajingine?” “Hapana ni hilo hilo.” Baada ya kuzungumza hayo, Dani alichukua laptop yake na kuanza kazi, aliingia kwenye ukurasa wa mke wangu, akachokonoa vile anavyojua yeye, dakika chache badaye, akaunti ile ikawa tunaweza kuiongoza tutakavyo. “Kazi imekwisha, sasa unaweza kuona kila kitu unachotaka,” aliniambia huku akinisogezea laptop ile.

Upesi nikaingia sehemu ya jumbe katika akaunti ya facebook ya mke wangu, mke wangu alikuwa akipokea jumbe nyingi za wanaume wanaomtaka kimapenzi.

Wanaume waliokuwa wakimfutilia mtandaoni walikuwa ni wengi mno, mambo yale yalizidi kuniumiza sana. Bado niliendea kutafuta jina la mtu aitwaye Ally.

Nikiwa naendelea kutafuta jina hilo mara ujumbe ukaingia, ujumbe huo ulitumwa na mtu aitwaye Abdul Ally. Naam! Alikuwa ni mtu yule yule niliyekuwa nikimsaka, Ujumbe uliotumwa na mtu huyo, ulikuwa ni mapenzi.

Ulisomeka hivi: “Vipi mpenzi, unafanya nini sasa hivi? nitumie basi kapicha.” Mate mepesi yalinijaa kinywani, ujumbe ule sikuujibu, nilichofanya ni kuingia kwenye ukurasa wa mtu huyo ili kumtambua vizuri.

“Mungu wangu!” nilipayuka baada ya kumwona mtu yule. Sikuamini macho yangu, nilihisi kutetemeka kwa hasira.

Mtu aliyekuwa akimzuzua mke wangu, alikuwa ni msanii wa muziki ambaye aliwahi kumtumia fedha miaka ya nyuma akitaka ashiriki kwenye video ya muziki. Nikiwa bado katika taharuki ile.

Mke wangu aliyekuwa ‘online’ nikaona anajibu ujumbe ule, akasema: “Niko chumbani, nakuwaza tu wewe, nakutumia kapicha,” nikazidi kutetemeka. Sijakaa sawa, mara picha ikatumwa.

Picha iliyotumwa, ilikuwa ya kifua cha mke wangu, alikuwa mtupu, matiti nje, alijifotoa matiti yake, akamtumia picha hiyo kwa hawala wake.

JE NINI KILITOKEA? TUKUTANE Kesho.
 
Kwa hali hii Shunie naanzaje sasa????
 
Usiache kuoa sababu ya changamoto ya ndoa nyingine

Sio kila ndoa ina changamoto nipo2

Faraji katafutiwa mke na mama yake hawajuani hawajasomana tabia kabisa

Ndo ni wito usikurupuke kama moyo umekutuma kuoa oa sio sababu mwanamke analazimisha umuoe kingine msomane tabia mjuane kama mwaka hivi au zaidi

Dadeki ndoa isinisogelee " Sitaki kushiriki kitu kama hicho " kabisaaa
 
Usiache kuoa sababu ya changamoto ya ndoa nyingine

Sio kila ndoa ina changamoto nipo2

Faraji katafutiwa mke na mama yake hawajuani hawajasomana tabia kabisa

Ndo ni wito usikurupuke kama moyo umekutuma kuoa oa sio sababu mwanamke analazimisha umuoe kingine msomane tabia mjuane kama mwaka hivi au zaidi
Mh asanteh!
 
Kwa msisitizo huu, nipo2 asipokuelewa itabidi afanyiwe maombi ya radi na moto..
 
SEHEMU YA 35

Nikiwa bado katika taharuki ile. Mke wangu aliyekuwa ‘online’ nikaona anajibu ujumbe ule, akasema: “Niko chumbani, nakuwaza tu wewe, nakutumia kapicha,” nikazidi kutetemeka. Sijakaa sawa, mara picha ikatumwa.

Picha iliyotumwa, ilikuwa ya kifua cha mke wangu, alikuwa mtupu, matiti nje, alijiftoa matiti yake, akaitumia picha kwa hawara yake.

Bila kutarajia, machozi yalinibubujika. nilihisi kifua kikiwaka moto kutokana na hasira, kitendo cha kusalitiwa na mwanamke yule, niliona ni uonevu mkubwa mno maishani.

Nikaendelea kufuatilia mawasiliano yao, nikaona namna mke wangu alivyokuwa amekolea kwenye penzi la jamaa yule.

Kila ambacho Ally alitaka kwa mke wangu, mwanamke huyo alitii. Walitumiana picha chafu kadiri walivyojisikia. Wakaambiana maneno yote ya kimapenzi vile walivyoweza. Mambo yote hayo niliyashuhudia kwa macho yangu mawili.

Kwa kweli niliumia mno, nakumbuka siku ile, nililia kama mtoto chumbani kwa rafiki yangu Dani. Uchungu nilioupata ulishinda hata ule msiba wa marehemu baba yangu.

“Pole sana Faraji,” Dani alisema huku akinishika bega. “Waswahili husema, dunia tambara bovu. Mambo yote ambayo mkeo anakutendea ni matokeo ya ulimbukeni wa kutoitambua vema ulimwengu. Wajibu wako ni kumpuuza.”

“Kumpuuza!..” nilibweka kwa hasira. “Nawezaje kupuuza tukio la kusalitiwa na mke wangu? Unajua uchungu wa mke wewe?” “Mantiki ya kauli yangu sivyo hivyo Faraji bali….” “Nisikilize Dani,”nilimkatisha. Uso uliniiva

“Nashukuru kwa msaada wako ndugu, nasikitika siwezi kusikiliza falsafa na siasa zozote juu ya hili, najua nitakachofanya” nilisema. Nikasimama na kutoka nje.

Daniel ama Dani kama alivyopenda kuitwa, hakuwa na chochote cha kufanya kunituliza. Niliondoka na kuelekea Sinza. Muda mfupi badaye nilikuwa La_cherse Hoteli, bado nilikuwa kwenye mkanganyiko mkubwa sana.

Nikiwa pale, mhudumu alipofika mezani, nikaagiza maji ya Kilimanjaro ya baridi sana, yalipoletwa, nikayafakamia na kuyanywa yote, angalau nikahisi ahueni nafsini.

Kwa mujibu wa saa yangu ya mkononi, ilikuwa yapata saa saba kasoro mchana, hadi wakati huo, yalikuwa yamepita masaa 17 nikiwa sijatia chochote tumboni, njaa sikuisikia kutokana na mfululizo wa matuki
 
Sehemu ya 36

Kwa kuwa niliazimia kuwafanyia kitu mbaya, mke wangu na hawala yake, nilianza kuseti mipango muda ule ule.

Nilimpigia simu mwandishi mashuuri wa Gazeti la Uwazi, Issa Mnally, ili nimweleze kisanga chote sambamba na lengo la kuweka hadhalani uchafu wote wa mke wangu na hawara yake ambaye, Ally.

Simu iliita muda mrefu bila kupokelewa. Sikuchoka. Nikapiga tena. Hali ikabaki vilevile, simu ya mwandishi yule haikupokewa.

Moyo ukaniuma mno kwa kutompata Issa, mwandishi asifikikaye kwa habari za kichunguzi, nikaona mipango ya fumanizi lile linaanza kuingia doa.

Nikajiuliza, sasa nifanyeje endapo sintampata mwandishi Issa na kutengeneza lile fumanizi? Nimwache mke wangu kiroho safi kwa kumpa talaka? Ama nitumie njia gani nyingine ya kumwadabisha?

Baada ya kufikiri kwa kina, bado nafsi yangu iligoma kabisa kumpa talaka mke wangu bila kumwachia maumivu maishani mwake. “Sasa nimkomeshe vipi?” nikano’ngona peke yangu.

Suala la kuua nikakiri lingenisababishia misukosuko maishani, hivyo nikalifutilia mbali. Sasa nifanye nini? Swali hili likaendelea kutembea kwenye kuta cha ubongo wangu bila majibu.

Akili ilichoka. Muda ulizidi kwenda bila kupata majibu. Nilimwita mhudumu wa jikoni na kumtaka anitayarishie ugali wa dona na nyama choma, nikaendelea kufikiri ni kitu gani nimfanye mwanamke yule.

Muda mfupi badaye, chakula kilikuwa tayari, wakati mhudumu ananinawisha maji, mara simu yangu iliita, nilipocheki kwenye kioo cha simu, mpigaji alikuwa ni Issa, mwandishi wa gazeti.

Niliinyakua simu na kuweka sikioni. “Mnally.” “Nambie bosi.” “Nakutafuta sana. Hupokei simu yangu.” “Samahani aisee, nilikuwa kikaoni.” “Ninayo habari.” “Acha wewe! Habari gani?”

“Njoo La_charse, ni stori nyeti, siyo ya kuongelea kwenye simu.” “Nidokeze kwa ufupi ili nimshirikishe mhariri wangu.” “Ni habari ya fumanizi” “Acha wewe!” Issa alimaka.

Mwandishi yule anapenda sana habari za namna ile. “Ndio ukweli wenyewe.” “Nani tena?” “Mke wangu” “Shemeji huyu huyu!!” “Hakuna mwingine”nilimwambia.

Kwa mbali nilimsikia mwandishi yule akizidi kifurahia kupata habari ile ambayo ingemfanya apate sifa kemkem kwa uhodari wake.
 
Sehemu ya 37

Baada ya kukata simu. Nilianza kukishmbulia kile chakula. Dakika chache badaye, Issa aliwasili, alikuwa ameongozana na mwandishi mwenzie, ambaye alinitambulisha kuwa ni ‘partner’ wake kwenye kazi zao.

Nilimsimulia mwandishi yule mwanzo mwisho. Nikamwonyesha picha na ‘screenshort’ za mazungumzo kati ya mke wangu na hawala yake.

“ Wamepanga kukutana lini kwa ajili ya kufunya uachafu wao?” hatimaye Issa aliniuliza baada ya kutumia muda mwingi kunisikiliza.

“Kwa mujibu wa mazungumzo yao inaonesha ni kesho saa nne.” “Wapi?” “Kuna lodge moja inaitwa Madrid, ipo Kinondoni studio, jirani na anapoishi mzee Beka Mfaume” “Sasa nisikilize…” alisema, akaendelea.

Kuanzia sasa, unachotakiwa kufanya ni kutomwonyesha kama kuna mpango umeusuka. “Na itabidi kuanzia kesho asubuhi tutakuwa mitaa yako kuweka kambi ili kufuatilia nyendo zote za mkeo bila kumpoteza hata point moja” “Sawa”

Tukakubaliana. Tukazungumza mawili matatu, kisha tukaagana. Wakati huo ilikuwa imetimu saa kumi na mbili jioni.

Nilichukua usafiri wa bodaboda nikarudi nyumbani, nilimkuta mke wangu akiwa ameketi sofani, alikuwa bize na simu kama ilivyo kawaida yake.

Nilizidi kuugulia ndani kwa ndani kwa kuaminii wasaa ule mwanamke yule alikuwa akichati na hawara yake. Nilitamani nimvae kisha nifanye kitu mbaya, lakini sauti moja kichwani ilinishi kutofanya hivyo.

Pamoja na kuniona nimeingia, wala hakunijali, si salamu wala kujishughulisha na chochote. Yeye na simu, simu na yeye.

Nilipitiliza hadi chumbani, nikaoga na kubadili nguo, nikarudi sebuleni ambako niliwacha. Nilimkuta akiendelea kucheza na simu yake, hakunisemesha chochote, mimi pia sikumsemesha lolote.

Masaa machache badaye, nilitayarishiwa chakula na dada wa kazi. Niliona yamesalia masaa machache kabla ya kukamilika kwa tukio baya na la aibu nililopanga kumtendea mwanamke yule na hawala wake.

Nilisahau kabisa methali isemayo: Jambo isilolijua ni sawa na usiku wa giza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom