Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,076
- 463,978
- Thread starter
- #421
SEHEMU YA 85
Siyo makazini kwao hata majumbani mwao, ni viumbe wasiogopa lolote, sio watu wa kujishusha hata kama wao ndio wakosaji, wakati wote hujiona wako sahihi. Wanawake viongozi huathiriwa sana na mazingira.
Pamoja na kwamba ni watu wanaojua kupenda wakiwa wamezama penzini, lakini ni viumbe hatari na wajanja sana pale wanaokuwa wamekinaiwa na wapenzi wao. “Sikiliza wewe mwanamke…”nilisema.
Nikaendelea. Usiniletee siasa ndani mwangu, kimsingi kama hutaki kunipa maelezo ya kina juu ya mipira ya kiume iliyotumika humu ndani mimi na wewe basi.” “Kila la kheri Faraji.” Debora alikazia “Eeh!!” “Ndio ondoka.”
“Unanifukuza!!” “Kwani hapa ni kwa nani?” Debora alisema akiwa amenikazia macho. Nilishikwa na kizunguzungu, nikawaza sijui nimtandike vibao ila nikaona kwa wadhifa wake, nitaishia Jela. “Kumbe nawe ni mshenzi tu kama viruka njia wengine,”
Nikaunguruma. “Ni maoni yako juu yangu, nimeyapokea.” Alinijibu kwa pozi. Halafu akaniuliza tena. “Huondoki?” Ebwana wee! Nilipagawa. Uhusiano wangu na Debora ulikuwa unavunjika kama mzaha.
“Hustahili kuwa kiongozi, mnafiki na mkatili mkubwa, hustahili kuwa kioo cha jamii wewe.” “Hata hilo pia nalipokea. Haya ondoka kabla sijapiga simu moja tu, ukaishia lockup siku ya leo.” “Usinitishe wewe!”
“Sikutishi!” Debora alindelea kuongea kwa pozi tena kwa sauti ya kawaida ila iliyobeba ujeuri wa kiwango kikubwa. Akaendelea kunieleza. “Leo ni ijumaa, nikikutupa selo hutotoka hadi jumatatu, hilo usilisahau Faraji….Ishia zako.”
Ilikuwa halmanusura nicheke, mambo yalikuwa yamebadirika kama utani tena kwa kasi sana, mwanamke niliyemwamini na kumpa mapenzi yote leo alikuwa akinitishia ‘kuniswenteka’ ndani, kwa sababu tu alikuwa amepewa mamlaka. Ama kweli dunia uwanja wa fujo.
Sikuwa na namna Niliondoka. Nilikwenda kituo cha tax nikajitoma kwenye moja katika nyingi zilizokuwepo. “Twende.” Nikwambia dereva kwa amri “Wapi bosi?” “Buhongwa…kwenye Lodge yoyote nzuri.”
Tukaanza safari. Nusu saa badaye, tukafika Buhongwa kwenye lodge moja inaitwa Maganga. Baada ya kumlipa dereva, pia nikafanya malipo ya chumba, nikaingia ndani, huko nikalia kama mtoto.