Simulizi:Biashara Ya Kifo

Simulizi:Biashara Ya Kifo

BIASHARA YA KIFO 11

Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa biashara ya kifo waliyokuwa wameianza, kazi kubwa ya Ethan ilikuwa ni kutafuta wanawake na suala zima la kuwachuna ngozi kwa wale waliokataa kuigiza filamu za ngono zilikuwa chini ya watu wengine kabisa.
Akaanza kupata mafanikio makubwa, hakutaka kurudi kule alipotoka, yaani kufanya starehe mpaka kuishiwa kabisa, hapo, akaanza kujipanga kwa kufanya biashara nyingine, akaanza kufungua maduka ambayo yalianza kumuingizia kiasi fulani cha fedha.
Hakuacha kuwatafuta wanawake, ilikuwa ni kazi kubwa iliyokuwa na malipo makubwa pia, alikuwa akisafiri huku na kule na kuonana na wanawake wengi na mwisho wa siku kuwalaghai kwa maneno mengi, ahadi za kufanya kazi kwa malipo makubwa na mwisho wa siku kuwatumikisha katika filamu za ngono.
Mara baada ya kutembea sana barani Ulaya, hapo ndipo alipoanza safari za kuelekea barani Afrika na nchi ya kwanza kabisa iliyokuja akilini mwake ilikuwa Nigeria. Alijua ni kwa jinsi gani Waafrika wengi walivyokuwa wakihangaika kwa ajili ya kufika nchini Marekani au hata barani Ulaya tu, alijua ni kwa jinsi gani watu wa huko walivyokuwa wakihangaika, hivyo, kwa upande wake aliona kwamba kusingekuwa na ugumu wowote ule.
Mara baada ya kuteremka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Murtala Muhammed uliokuwa jijini Lagos moja kwa moja akaanza kuelekea hotelini ambapo huko ndipo alipopanga kukutana na wasichana kwa ajili ya kufanya nao kazi za kugiza filamu za ngono pasipo kujua.
“Samahani,” alisema Ethan, alikuwa akimwambia mwanaume mmoja mara baada ya kukaa takribani wiki moja nchini humo.
“Bila samahani.”
“Ninahitaji wasichana kama kumi hivi.”
“Wa nini?”
“Ninahitaji kuzungumza nao, ila wawe wazuri ambao wanahitaji ajira ya kweli,” alisema Ethan, alikuwa akizungumza na mwanaume mmoja hotelini hapo.
“Hakuna tatizo! Kuna maslahi?”
“Hilo si tatizo.”
Kwa kijana yule, hiyo ikaonekana kuwa kazi ndogo mno. Kulikuwa na wanawake wengi nchini Nigeria ambao hawakuwa na kazi na walikuwa radhi kufanya kazi yoyote japokuwa walisoma sana na vyumbani walikuwa na vyeti vya chuo.
Alipoanza kuwatafuta, wala hakupata kazi kubwa, akafanikiwa kuwapata na kuwaambia kila kitu kilichokuwa kikiendelea na hivyo walitakiwa kuonana na huyo mtu hotelini kitu ambacho hakikuwa tatizo lolote lile, alipowakusanya, akaanza kuelekea nao hotelini huko.
“Vipi?”
“Wapo kumi, au unataka niongeze?’ aliuliza kijana yule.
“Hapana! Haohao wanatosha.”
“Sawa!”
Alichokifanya Ethan ni kutaka kuonana nao, wakaletwa chumbani mule na kuanza kuzungumza nao. Ethan alikuwa na uwezo mkubwa wa kuzungumza, alikuwa na uwezo wa kuziteka akili za mtu na kuzifanya alivyotaka yeye.
Alizungumza kipole, kwa umakini sana na uso wake aliuweka katika hali iliyowafanya wale wasichana kuona kwamba kweli mtu huyo alikuwa akihitaji wasichana kwa ajili ya kufanya kazi, alionekana kama mtu aliyekuwa na kiu ya kumsaidia mtu fulani.
“Kazi zipo, ila hotelini, malipo yake yanaanzia dola elfu moja kwa siku,” alisema Ethan maneno yaliyowafanya wasichana wale kushtuka.
“Dola elfu moja?”
“Ndiyo! Ni nyingi?”
“Ni nyingi mno!”
“Ni nyingi unapokuwa Afrika, unapokuwa Marekani, ni kiasi kidogo sana, tena inawezekana baada ya wiki mkalilia muongezwe mshahara,” alisema Ethan huku akichia tabasamu pana, wasichana wote wakacheka.
Kwa kumwangalia usingeweza kuamini kwamba alikuwa akijihusisha na kle kilichokuwa kikiendelea nyuma yake, alionekana kuwa kijana makini na mpole sana na aliaminika kutokana na jinsi alivyokuwa tu.
Wasichana wale wakatekwa, wakamwanmini Ethan na kuamini kila kitu alichokuwa akikizungumza, wakakubaliana naye kwamba walikuwa radhi kufanya kazi hiyo wakatakiwa kuwasiliana na wazazi wao au ndugu zao wakati yeye akifanya ishu zote za safari.
“Vipi?” aliuliza bwana Cook.
“Kuna Wanaigeria nimewapata, wazuriiii...”
“Haohao njoo nao.”
“Hakuna tatizo!’
Hiyo ndiyo ilikuwa kazi yake ya kila siku, alikuwa akizunguka huku na kule kwa ajili ya kazi hiyo tu. Aliendelea kulipwa vizuri, alijipatia kiasi kikubwa cha fedha kiasi kwamba kuna kipindi alihisi kwamba anaukaribia ubilionea.
Hakupata muda wa kupumzika, kila siku aliona kama muda umemtupa mkono hivyo alitakiwa kupambana kila siku mpaka kuhakikisha kwamba anafanikiwa na kuwa tajiri mkubwa maishani mwake.
Baada ya kuzunguka nchi nyingi za Afrika hapo ndipo alipoanza safari ya kwenda nchini Tanzania. Tayari alipewa taarifa kwamba huko kulikuwa na wanawake warembo, waliovutia mno na ambao hawakuwa na maisha mazuri kama walivyokuwa wanawake wengine barani Afrika.
Akatamani kwenda huko na kuianza safari hiyo. Alipofika ndani ya ndege, huku akiwa amevalia suti yake, macho yake yakatua kwa msichana mrembo mno, alipomwangalia, akatokea kumpenda lakini kwa kuwa alikuwa na kazi ya kufanya hasa na wasichana kama alivyokuwa msichana huyo, akataka kumuingiza katika biashara hiyohiyo.
“My name is Annabel,” (Ninaitwa Annabel) alijitambulisha msichana yule.
“Oooh! Annabel...myname is Ethan,” (Oooh! Annabel...jina langu ni Ethan,” alijitambulisha Ethan kwa msichana huyo.
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kufahamiana, walizungumza mengi huku wakionekana kama watu waliokwishaonana miaka miwili iliyopita. Kila mmoja alijitahidi kujifanya mchangamfu kwa mwenzake kitu kilichowafanya kutokuchokana kabisa.
Kichwani mwa Ethan kulifikiriwa vitu viwili tu, kumchukua msichana yule na kwenda kumchezesha filamu za ngono au kama angekataa basi angemchukua na kumpeleka kwa watu waliokuwa na kazi ya kuchuna ngozi tu.
Kwa muonekano wa sura, alikuwa binti mrembo mno zaidi ya wasichana ambao aliwahi kuwachukua kwa ajili ya kwenda nchini Mareani kwa lengo la kuigiza filamu za utupu. Kila alipomwangalia, hata yeye mwenyewe alihisi kumpenda ila kitu alichokisikitikia ni kwamba alikuwa akienda kuigiza filamu za utupu.
“Annabel...”
“Beee...”
“Hivi unajua kwamba wewe ni mrembo?”
“Hapana! Nipo kawaida!”
“Hakuna! Wewe ni mrembo mno, hivi umeuchukua kutoka wapi?”
“Kwa wazazi wangu!”
“Nimefurahi sana kukaa kiti kimoja nawe, hakika najisikia faraja.”
“Usijali,” alisema Annabel pasipo kujua lengo kubwa la kijana huyo ambaye aliendelea kumuonyeshea uchangamfu zaidi huku ikiwa njia mojawapo ya kufanya kumzoea ili hata kile alichokuwa amekipanga kiweze kufanikiwa.

Je nini kitaendelea?
 
BIASHARA YA KIFO 12

Annabel na Ethan walizoeana sana ndani ya ndege kiasi kwamba ndege hiyo ilipotua katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, waliongozana pamoja mpaka nje ya uwanja huo ambapo wakachukua taksi pamoja na kuondoka kuelekea hotelini.
Annabel hakutaka kabisa kuwaambia wazazi wake kwamba alikuwa amefika nchini Tanzania, alitaka kufanya siri kwani ni mara nyingi alijaribu kuwasiliana nao na kuwaambia kwamba angetamani sana kufika nchini humo lakini walimwambia asubiri.
Si yeye wala Ethan aliyekuwa mwenyeji nchini Tanzania, kitu walichomwambia dereva awapeleke katika moja ya hoteli kubwa, yenye hadhi ambapo huko Annabel angefanya mawasiliano na wazazi wake na kumwambia kwamba tayari alikuwa amekwishafika nyumbani.
“Ningependa tukae wote chumba kimoja,” alisema Ethan huku akimwangalia Annabel kwa macho yaliyojaa matamanio.
“Tukae chumba kimoja!! Hapana!” alisema Annabel huku akionekana kushtuka, ndita zikaanza kuonekana usoni mwake.
Japokuwa Ethan alimuomba sana Annabel akubaliane naye lakini binti huyo hakuonekana kuwa mwepesi hata mara moja, msimamo wake ulikuwa uleule kwamba hakutaka kukaa naye chumba kimoja kitu kilichomfanya Ethan kutokulazimisha sana kwani kwa jinsi hali ilivyoonekana, Annabel alianza kukasirika.
Baada ya dakika kadhaa, teksi ile ikaanza kupaki katika eneo la Hotel ya New Africa iliyokuwa Posta ambapo wote kwa pamoja wakatoka nje, wakamlipa dereva na kisha kuelekea ndani. Walipofika mapokezi, kila mmoja akachukua chumba chake.
“Nitawasiliana na baba kesho,” alisema Annabel na kulala kitandani.
Asubuhi ilipofika, mlango ukaanza kugongwa na mhudumu ambaye aliingia na kumpatia kifungua kinywa, wala hazikupita dakika nyingi, naye Ethan akagonga mlango na kukaribishwa. Macho yake yalipotua kwa Annabel aliyekuwa kitandani na nguo ya kulalia, akajikuta akimpenda zaidi msichana huyo.
Kwa kumwangalia machoni tu ingekuwa rahisi kugundua kwamba mwanaume huyo alikuwa kwenye mapenzi ya dhati kwa Annabel, alimwangalia kwa matamanio makubwa huku uso wake ukiwa kwenye tabasamu pana.
Ni kweli alikuwa amekutana na wasichana wengi lakini yule aliyekuwa mbele yake asubuhi hiyo alikuwa ni zaidi ya msichana mrembo. Akamsogelea pale kitandani na kutulia kitandani.
Muda wote huo Annabel alikuwa kimya, alimwangalia Ethan huku akigundua kile kilichokuwa kikiendelea moyoni mwa mwanaume huyo. Hakutaka kuzungumza chochote, alichokuwa akikitaka ni kuona angefanya nini.
“Mambo!” alimsalimia.
“Poa! Karibu.”
“Asante.”
Ethan akanyamaza kwanza, akameza fundo la mate na macho yake kwenda mapajani mwa Annabel. Alimtamani sana, alitamani kumsogelea zaidi na kumpapasa mapajani mwake, hakukuwa na kitu alichokuwa akikitaka kwa wakati huo zaidi ya kufanya ngono tu.
“Umependeza,” alisema Ethan.
“Kwa nguo hii ya kulalia?”
“Hahah! Ndiyo!” alijibu Ethan.
Mapenzi ni upofu, kupendeza kwa Annabel mbele ya macho ya Ethan ilikuwa kitu cha kawaida tu kwani hata kama angevaa magunia, bado mwanaume huyo angemwambia kweli kwamba alikuwa akimpenda.
“Naomba twende tukatembee leo.”
“Kwenda wapi?”
“Popote pale.”
“Wewe ni mwenyeji huku?”
“Hapa! Ila kama tukimwambia dereva, anaweza kutupeleka popote pale,” alisema Ethan.
“Ila sina muda, ninataka kuondoka kuelekea nyumbani,” alisema Annabel.
“Kwani unaishi huku?”
“Hapana! Naishi Marekani ila huku ndipo nilipozaliwa.”
“Sawa! Unaishi wapi?”
“Sifahamu! Natakiwa kuwasiliana na wazazi wangu kwanza,” alisema Annabel.
Ethan akashusha pumzi ndefu, bado moyo wake ulitamani sana kuwa na msichana huyo kwa siku nzima. Hata kile alichokuwa ameagizwa kikasahaulika kabisa, alitumwa nchini Tanzania kwa ajili ya kuja kuwachukua wasichana kwa ajili ya kwenda kucheza filamu za utupu ila badala ya kufanya hivyo, alikutana na msichana mrembo ambaye hakutaka kumuacha apite na kupotea.
Hakutaka kufanya kazi yake, alichokuwa akikifikiria kwa wakati huo ni kuwa na msichana huyo tu. Annabel alipowasiliana na baba yake, askofu Benedicto, askofu huyo alishtuka sana, hakuamini kama binti yake alifika nchini Tanzania, hivyo akataka kuonana naye.
“Upo wapi?” aliuliza baba yake simuni.
“Hotelini.”
“Hoteli gani?”
“New Africa,” alijibu Annabel.
“Nakuja.”
Annabel akakata simu na kutulia kitandani. Kidogo, moyo wake ukafurahi. Muda huo ulikuwa ni kuzungumza na Ethan mengi tu, alimuuliza maswali mengi juu ya kile alichokuwa akikifanya lakini kwa Ethan, sababu kubwa ya kuwa Tanzania ambayo alimwambia ni kwamba alikuwa amefika nchini Tanzania kama mtalii tu.
Ilipofika saa nne, Annabel akapokea simu kutoka kwa baba yake ambaye alikuwa nje ya hoteli hiyo na kumwambia atoke nje ili waweze kuondoka. Annabel alishangaa sana kwani alichokijua ni kwamba baba yake angekuja mpaka ndani ya hoteli na kumsubiria mapokezini, ila matokeo yake, alikuwa nje garini.
“Kwa nini usije mpaka ndani ya hoteli?”
“Wewe njoo tu Annabel.”
“Sawa nakuja.”
Annabel hakutaka kubaki ndani ya chumba hicho tena, akamwambia Ethan kwamba tayari baba yake alikuwa amekwishafika na hivyo alitaka kuondoka. Ethan hakutaka kukubali msichana huyo aondoke peke yake.
“Naweza kwenda na wewe?”
“Hapana!”
“Naomba niende nawe, nataka kuwa karibu na wewe zaidi. Nakuomba,” alisema Ethan kwa sauti ndogo na ya kubembeleza.
Aliomba kwa kunyenyekea sana kwamba alitaka kwenda naye huko kwao alipotaka kwenda. Japokuwa Annabel alikataa sana lakini mwisho wa siku akakubaliana naye na hivyo kutoka chumbani humo.
Walipofika nje, akapigiwa simu na baba yake na kuambiwa gari alilotakiwa kulifuta, alipoliona, akaanza kulifuata. Mpaka kipindi hicho alikuwa akijiuliza maswali yasiyokuwa na majibu kwamba ilikuwaje baba yake kukataa kumfuata ndani ya hoteli na matokeo yake kusimama nje kabisa, tena kwa mbali upande mwingine wa barabara?
Kila alichojiuliza, alikosa jibu. Hakujali sana, akaanza kulifuatan gari hilo na kuufungua mlango, akaingia ndani na Ethan.
“Huyu ni nani?” aliuliza askofu mara baada ya kumuona Ethan.
“Rafiki yangu!”
“Ulikuwa naye hotelini?”
“Ndiyo!”
“Chumba kimoja?”
“Hapana baba!”
Japokuwa Askofu Benedicto alikuwa amekasirika lakini hakutaka kuzionyesha hasira zake mbele ya binti yake, hakupenda kabisa kumuona akiwa na mwanaume tena akiwa hamfahamu kabisa.
Alikubaliana naye kwenda naye nyumbani lakini alitamani kumwambia Ethan arudi alipotoka kwani hakumpenda hata mara moja. Alifahamu kwamba alikuwa askofu, mtu aliyeheshimika Tanzania nzima,.
“Why didn’t you come inside of the hotel?” (Kwa nini hukuja ndani ya hoteli)
“I am very sorry, I had no more time, I had to leave very quickly,” (Samahani, sikuwa na muda zaidi, nilitakiwa kuondoka haraka sana) alijibu Askofu.
“And where is mom?” (Na mama yupo wapi?)
“She travelled to Zimbabwe, she will be back next week,” (Alisafiri kwenda Zimbabwe, atarudi wiki ijayo)
Alijulikana na watu wengi ndani ya Jiji la Dar es Salaam hivyo alijua kwamba endapo angeteremka kutoka garini na kumfuata binti yake ndani ya hoteli ile, watu wengi wangeshangaa na kusababisha maswali kadhaa kitu ambacho hakutaka kabisa kitokee.
Kitu cha pili ni kwamba aliamua kumdanganya binti yake kuhusu mama yake kwa sababu alijua kwamba endapo angemwambia ukweli kwamba alikuwa akisomea utawa katika chuo kimoja jijini Dar es Salaam, Annabel angeshtuka sana.
Walichukua muda mrefu mpaka kufika Chamazi ambapo gari ile ikapaki nje ya geti moja kubwa na kisha askofu kuteremka na kulifungua geti lile kisha kuliingiza gari ndani. Annabel alishangaa, kilichomshangaza ni kitendo cha baba yake kuteremka na kufungua geti, kwa nini hakuajiri mlinzi kwa ajili ya kufanya kazi hiyo na wakati jumba lenyewe lilikuwa la kifahari? Hakupata jibu.
“Karibuni,” aliwakaribisha mara baada ya kufungua mlango wa kuingilia ndani. Wote wakaingia, ila moyo wa askofu Benedicto bado ulijiuliza maswali mengi juu ya Ethan, hakupenda kabisa kuwa karibu na binti yake.

Je nini kitaendelea?
 
BIASHARA YA KIFO 12

Annabel na Ethan walizoeana sana ndani ya ndege kiasi kwamba ndege hiyo ilipotua katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, waliongozana pamoja mpaka nje ya uwanja huo ambapo wakachukua taksi pamoja na kuondoka kuelekea hotelini.
Annabel hakutaka kabisa kuwaambia wazazi wake kwamba alikuwa amefika nchini Tanzania, alitaka kufanya siri kwani ni mara nyingi alijaribu kuwasiliana nao na kuwaambia kwamba angetamani sana kufika nchini humo lakini walimwambia asubiri.
Si yeye wala Ethan aliyekuwa mwenyeji nchini Tanzania, kitu walichomwambia dereva awapeleke katika moja ya hoteli kubwa, yenye hadhi ambapo huko Annabel angefanya mawasiliano na wazazi wake na kumwambia kwamba tayari alikuwa amekwishafika nyumbani.
“Ningependa tukae wote chumba kimoja,” alisema Ethan huku akimwangalia Annabel kwa macho yaliyojaa matamanio.
“Tukae chumba kimoja!! Hapana!” alisema Annabel huku akionekana kushtuka, ndita zikaanza kuonekana usoni mwake.
Japokuwa Ethan alimuomba sana Annabel akubaliane naye lakini binti huyo hakuonekana kuwa mwepesi hata mara moja, msimamo wake ulikuwa uleule kwamba hakutaka kukaa naye chumba kimoja kitu kilichomfanya Ethan kutokulazimisha sana kwani kwa jinsi hali ilivyoonekana, Annabel alianza kukasirika.
Baada ya dakika kadhaa, teksi ile ikaanza kupaki katika eneo la Hotel ya New Africa iliyokuwa Posta ambapo wote kwa pamoja wakatoka nje, wakamlipa dereva na kisha kuelekea ndani. Walipofika mapokezi, kila mmoja akachukua chumba chake.
“Nitawasiliana na baba kesho,” alisema Annabel na kulala kitandani.
Asubuhi ilipofika, mlango ukaanza kugongwa na mhudumu ambaye aliingia na kumpatia kifungua kinywa, wala hazikupita dakika nyingi, naye Ethan akagonga mlango na kukaribishwa. Macho yake yalipotua kwa Annabel aliyekuwa kitandani na nguo ya kulalia, akajikuta akimpenda zaidi msichana huyo.
Kwa kumwangalia machoni tu ingekuwa rahisi kugundua kwamba mwanaume huyo alikuwa kwenye mapenzi ya dhati kwa Annabel, alimwangalia kwa matamanio makubwa huku uso wake ukiwa kwenye tabasamu pana.
Ni kweli alikuwa amekutana na wasichana wengi lakini yule aliyekuwa mbele yake asubuhi hiyo alikuwa ni zaidi ya msichana mrembo. Akamsogelea pale kitandani na kutulia kitandani.
Muda wote huo Annabel alikuwa kimya, alimwangalia Ethan huku akigundua kile kilichokuwa kikiendelea moyoni mwa mwanaume huyo. Hakutaka kuzungumza chochote, alichokuwa akikitaka ni kuona angefanya nini.
“Mambo!” alimsalimia.
“Poa! Karibu.”
“Asante.”
Ethan akanyamaza kwanza, akameza fundo la mate na macho yake kwenda mapajani mwa Annabel. Alimtamani sana, alitamani kumsogelea zaidi na kumpapasa mapajani mwake, hakukuwa na kitu alichokuwa akikitaka kwa wakati huo zaidi ya kufanya ngono tu.
“Umependeza,” alisema Ethan.
“Kwa nguo hii ya kulalia?”
“Hahah! Ndiyo!” alijibu Ethan.
Mapenzi ni upofu, kupendeza kwa Annabel mbele ya macho ya Ethan ilikuwa kitu cha kawaida tu kwani hata kama angevaa magunia, bado mwanaume huyo angemwambia kweli kwamba alikuwa akimpenda.
“Naomba twende tukatembee leo.”
“Kwenda wapi?”
“Popote pale.”
“Wewe ni mwenyeji huku?”
“Hapa! Ila kama tukimwambia dereva, anaweza kutupeleka popote pale,” alisema Ethan.
“Ila sina muda, ninataka kuondoka kuelekea nyumbani,” alisema Annabel.
“Kwani unaishi huku?”
“Hapana! Naishi Marekani ila huku ndipo nilipozaliwa.”
“Sawa! Unaishi wapi?”
“Sifahamu! Natakiwa kuwasiliana na wazazi wangu kwanza,” alisema Annabel.
Ethan akashusha pumzi ndefu, bado moyo wake ulitamani sana kuwa na msichana huyo kwa siku nzima. Hata kile alichokuwa ameagizwa kikasahaulika kabisa, alitumwa nchini Tanzania kwa ajili ya kuja kuwachukua wasichana kwa ajili ya kwenda kucheza filamu za utupu ila badala ya kufanya hivyo, alikutana na msichana mrembo ambaye hakutaka kumuacha apite na kupotea.
Hakutaka kufanya kazi yake, alichokuwa akikifikiria kwa wakati huo ni kuwa na msichana huyo tu. Annabel alipowasiliana na baba yake, askofu Benedicto, askofu huyo alishtuka sana, hakuamini kama binti yake alifika nchini Tanzania, hivyo akataka kuonana naye.
“Upo wapi?” aliuliza baba yake simuni.
“Hotelini.”
“Hoteli gani?”
“New Africa,” alijibu Annabel.
“Nakuja.”
Annabel akakata simu na kutulia kitandani. Kidogo, moyo wake ukafurahi. Muda huo ulikuwa ni kuzungumza na Ethan mengi tu, alimuuliza maswali mengi juu ya kile alichokuwa akikifanya lakini kwa Ethan, sababu kubwa ya kuwa Tanzania ambayo alimwambia ni kwamba alikuwa amefika nchini Tanzania kama mtalii tu.
Ilipofika saa nne, Annabel akapokea simu kutoka kwa baba yake ambaye alikuwa nje ya hoteli hiyo na kumwambia atoke nje ili waweze kuondoka. Annabel alishangaa sana kwani alichokijua ni kwamba baba yake angekuja mpaka ndani ya hoteli na kumsubiria mapokezini, ila matokeo yake, alikuwa nje garini.
“Kwa nini usije mpaka ndani ya hoteli?”
“Wewe njoo tu Annabel.”
“Sawa nakuja.”
Annabel hakutaka kubaki ndani ya chumba hicho tena, akamwambia Ethan kwamba tayari baba yake alikuwa amekwishafika na hivyo alitaka kuondoka. Ethan hakutaka kukubali msichana huyo aondoke peke yake.
“Naweza kwenda na wewe?”
“Hapana!”
“Naomba niende nawe, nataka kuwa karibu na wewe zaidi. Nakuomba,” alisema Ethan kwa sauti ndogo na ya kubembeleza.
Aliomba kwa kunyenyekea sana kwamba alitaka kwenda naye huko kwao alipotaka kwenda. Japokuwa Annabel alikataa sana lakini mwisho wa siku akakubaliana naye na hivyo kutoka chumbani humo.
Walipofika nje, akapigiwa simu na baba yake na kuambiwa gari alilotakiwa kulifuta, alipoliona, akaanza kulifuata. Mpaka kipindi hicho alikuwa akijiuliza maswali yasiyokuwa na majibu kwamba ilikuwaje baba yake kukataa kumfuata ndani ya hoteli na matokeo yake kusimama nje kabisa, tena kwa mbali upande mwingine wa barabara?
Kila alichojiuliza, alikosa jibu. Hakujali sana, akaanza kulifuatan gari hilo na kuufungua mlango, akaingia ndani na Ethan.
“Huyu ni nani?” aliuliza askofu mara baada ya kumuona Ethan.
“Rafiki yangu!”
“Ulikuwa naye hotelini?”
“Ndiyo!”
“Chumba kimoja?”
“Hapana baba!”
Japokuwa Askofu Benedicto alikuwa amekasirika lakini hakutaka kuzionyesha hasira zake mbele ya binti yake, hakupenda kabisa kumuona akiwa na mwanaume tena akiwa hamfahamu kabisa.
Alikubaliana naye kwenda naye nyumbani lakini alitamani kumwambia Ethan arudi alipotoka kwani hakumpenda hata mara moja. Alifahamu kwamba alikuwa askofu, mtu aliyeheshimika Tanzania nzima,.
“Why didn’t you come inside of the hotel?” (Kwa nini hukuja ndani ya hoteli)
“I am very sorry, I had no more time, I had to leave very quickly,” (Samahani, sikuwa na muda zaidi, nilitakiwa kuondoka haraka sana) alijibu Askofu.
“And where is mom?” (Na mama yupo wapi?)
“She travelled to Zimbabwe, she will be back next week,” (Alisafiri kwenda Zimbabwe, atarudi wiki ijayo)
Alijulikana na watu wengi ndani ya Jiji la Dar es Salaam hivyo alijua kwamba endapo angeteremka kutoka garini na kumfuata binti yake ndani ya hoteli ile, watu wengi wangeshangaa na kusababisha maswali kadhaa kitu ambacho hakutaka kabisa kitokee.
Kitu cha pili ni kwamba aliamua kumdanganya binti yake kuhusu mama yake kwa sababu alijua kwamba endapo angemwambia ukweli kwamba alikuwa akisomea utawa katika chuo kimoja jijini Dar es Salaam, Annabel angeshtuka sana.
Walichukua muda mrefu mpaka kufika Chamazi ambapo gari ile ikapaki nje ya geti moja kubwa na kisha askofu kuteremka na kulifungua geti lile kisha kuliingiza gari ndani. Annabel alishangaa, kilichomshangaza ni kitendo cha baba yake kuteremka na kufungua geti, kwa nini hakuajiri mlinzi kwa ajili ya kufanya kazi hiyo na wakati jumba lenyewe lilikuwa la kifahari? Hakupata jibu.
“Karibuni,” aliwakaribisha mara baada ya kufungua mlango wa kuingilia ndani. Wote wakaingia, ila moyo wa askofu Benedicto bado ulijiuliza maswali mengi juu ya Ethan, hakupenda kabisa kuwa karibu na binti yake.

Je nini kitaendelea?
Umeanza na fujo zako kupost mengimengi karim na post zako za fb ndefu jamani
 
Malizia mwenyewe na uwaambie watu wako hii lazima iishie njiani wajiandae kununua kitabu
Bwana imalizie upoje lakini inaonekana uko fb imefika mbali sana mbona nilimuuliza kama atatoa kitabu hajajibu
 
SEHEMU YA 13

“Nataka twende sehemu.”
“Wapi?”
“Kutembea! Unapenda kukaa hapa tu kwa siku zote tangu umefika?”
“Hapana! Ila sidhani, sijapazoea sana huku.”
“Unaogopa utapotea?”
“Ndiyo!”

Ethan alikuwa akizungumza na Annabel, alitaka kumchukua na kumtoa mtoko huku lengo lake kubwa likiwa ni kutaka kuzungumza naye juu ya kile kilichomfanya kuwa nchini Tanzania.

Bado Ethan aliona kulikuwa na ugumu wa msichana huyo kukubaliana naye kwani kila alipojaribu kumchombeza kwa maneno ya haya na yale, ugumu ulionekana dhahiri.

Annabel hakuwa na maamuzi ya maisha yake, alikuwa na umri chini ya miaka kumi na nane, kila kitu kilichotakiwa kuamuliwa maishani mwake kilikuwa chini ya wazazi wake.

Japokuwa kipindi hicho wazazi wake
hawakuwepo lakini hakutaka kulisahau hilo, hakutaka kuondoka nyumbani hapo.
Bado Ethan alikuwa akimchombeza kwa maneno matamu ya mahaba, alitaka msichana huyo awe mpenzi wake kwanza, alale naye na ndipo ampeleke nchini Marekani kwa ajili ya kucheza filamu ya ngono kama ilivyokuwa imepangwa.

Wanawake wale kumi walikuwa tayari, walijiandaa na wengine kuaga kabisa lakini tatizo likawa kwa Ethan tu. Hakutaka kuondoka nchini Tanzania pasipo Annabel, alimpenda mno msichana huyo na alimhitaji kuliko mtu yeyote yule, kila alipomwangalia, cha zaidi ya yote alihitaji kufanya naye ngono.

“Why are you here?” (Kwa nini upo hapa?) aliuliza askofu Benedicto mara baada ya kufika nyumbani.
“Me?” (Mimi?)

Askofu akakasirika, alijua fika kwamba Ethan alijua kuwa alikuwa akiongea na yeye sasa ilikuwaje aanze tena kumuuliza kama alikuwa akiongea naye. Akaanza kukunja ndita usoni mwake, hakumpenda kijana huyo na alimchukia mno.

“I’m sorry sir, I want to take your daughter out,” (Samahani mkuu, ninataka kumtoa binti yako mtoko) alisema Ethan huku akijivika ujasiri mkubwa.

“Impossible.” (Haiwezekani)
Askofu hakutaka kukaa mahali hapo, moja kwa moja akaelekea chumbani kwake kwa kuamini kwamba mara unapoamua kumuua nyani haukutakiwa kumwangalia usoni.

Ethan akanyong’onyea, hakuamini kama baba yake Annabel angekataa kumruhusu binti yake kuondoka naye.

Alimwangalia Annabel usoni, kila alipomwangalia, mapenzi yalizidi kuchomoza moyoni mwake kiasi kwamba kuna wakati

alijiona kutokujiweza kwa msichana huyo, aliamua tu kumchukua na kuwa naye huku lile lengo la kutaka kumpeleka nchini Marekani kwa ajili ya kuigiza filamu za ngono aachane nalo.

“Naomba unisamehe,” alisema Ethan.
“Umenifanyia nini kibaya?”
“Hakuna! Ila naomba unisamehe.”
Moyo wa Ethan ulikuwa kwenye maumivu makali mno, kutokana na mapenzi makubwa yaliyougubika moyo wake, hapo ndipo alipogundua kwamba alifanya kosa kubwa kutaka kumchukua Annabel na kumpeleka nchini Marekani kuigiza filamu zile za kikubwa.

Alijiona mkosaji na ndiyo maana wakati huo aliamua kumuomba msamaha msichana huyo kwa kile alichotaka kukifanya japokuwa hakumuweka wazi ni kitu gani.

“Utarudi Marekani?” aliuliza Ethan.
“Kurudi? Mmmh! Sijajua, ila sijui kama nitarudi, nitataka kukaa na wazazi wangu zaidi,” alisema Annabel.

Ethan hakutaka kurudi nchini Marekani peke yake, mtu aliyekuwa akimhitaji kurudi naye alikuwa Annabel tu. Kila siku akawa mtu wa kufika nyumbani hapo kwa ajili ya kumuona msichana huyo na kuzungumza naye mengi.

Japokuwa siku za nyuma askofu alikuwa akimchukia sana Ethan lakini mwisho wa siku akajikuta akimzoea kijana huyo na hatimaye chuki kuanza kupotea moyoni mwake.

Wakaanza kukaa chini na kuzungumza mengi huku kila mmoja akijaribu kumficha mwenzake kile kilichokuwa kikiendelea katika maisha yake, yaani askofu akimfichana Ethan kama alikuwa askofu wa Kanisa la Kiroma huku kijana huyo akificha kazi aliyokuwa akiifanya kipindi hicho.

akajikuta akimzoea kijana huyo na hatimaye chuki kuanza kupotea moyoni mwake. Wakaanza kukaa chini na kuzungumza mengi huku kila mmoja akijaribu kumficha mwenzake kile kilichokuwa kikiendelea katika maisha yake, yaani askofu akimfichana Ethan kama alikuwa askofu wa Kanisa la Kiroma huku kijana huyo akificha kazi aliyokuwa akiifanya kipindi hicho.

“Ninataka kumfanya Annabel kuwa mwanamke mwenye furaha kuliko wote duniani,” alisema Ethan huku akitoa tabasamu kubwa.

“Nyie vijana wa sasa hivi hamuaminiki kabisa.”
“Kwa nini tusaminike? Yaani hata wewe huniamini?”

“Hahaha! Siwezi kukuamini hivihivi.”
“Unataka nifanye nini ili uniamini?”
“Uanze kwenda kanisani.”
“Hahaha!”

Walizungumza kama marafiki, walizoeana mno na wakati mwingine walitaniana hapa na pale. Ethan alijisahau kabisa, akasahau kama alitumwa kwa ajili ya kuwachukua wanawake na kuwapeleka nchini Marekani, kwake, kile alichokuwa akikifikiria kwa kipindi hicho ni mapenzi tu.

Kutokana na ukaribu na familia hiyo, kila mmoja akamzoea Ethan kiasi kwamba hakukuwa na mtu aliyekuwa na hofu naye tena.

Kwa kuwa alizoeleka, hivyo alichokifanya ni kuendelea kumsisitizia Annabel jinsi alivyokuwa akimpenda na kumuhitaji maishani mwake.

Alikataa na kukataa lakini mwisho wa siku akaona kama usumbufu hivyo kukubaliana naye na hivyo kuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Ilikuwa ni siri kubwa, wazazi hawakujua chochote kile, walifanyiana mambo ya chumbani kila muda ambao wazazi hao hawakuwepo nyumbani hapo.

Wazazi walipokuwepo, waliishi kama kaka na dada kitu kilichowatia upofu wazazi hao. Japokuwa aliaminika sana lakini Ethan hakuwa mtu wa kulala nyumbani hapo, alikuwa akifika asubuhi na kuondoka usiku, kurudi hotelini na kucheza kamari, mchezo aliopenda sana kuucheza kipindi hicho.
*****

“Ninataka mniletee Ethan mahali hapa!” ilisikika sauti ya mwanaume mmoja kutoka ndani ya nyumba moja ya kifahari.

“Sawa.”
“Ninataka mkamilishe kila kitu, ikiwezekana, mmuue kama tu ataleta ubishi,” alisikika mwanaume huyoi.
“Hakuna tatizo mkuu.”

Yalikuwa ni mangezi baina ya bwana Cook na vijana aliokuwa amewaita ndani ya nyumba yake. Alichanganyikiwa mno, biashara zake zilisimama kwa muda.

Uchumi wake mkubwa ulitegemea biashara ya ngozi aliyokuwa akiiifanya, wasichana waliokuwa wakiletwa na kukataa ndiyo haohao ambao ngozi zao zilichunwa na kupelekwa nchini China.

Alichanganyikiwa, alijiona kama akikaribia Alichanganyikiwa, alijiona kama akikaribia kufilisika.

Kijana wake wa kazi ambaye alimtuma nchini Tanzania, alizamia, kwa kipindi cha mwezi mmoja na nusu hakuwa amerudi nchini Marekani, mbaya zaidi, hakuwa akiwasiliana naye kama alivyofanya wakati alipokuwa akienda katika nchi nyingine.

Alikuwa na hasira mno, alichohisi ni kwamba Ethan alitaka kuachana na biashara hiyo kitu ambacho hakutaka hata kukisikia kwa kuona kwamba ni lazima kijana huyo angekwenda kutoa siri juu ya biashara ile iliyokuwa ikiendelea.

Hakutaka hilo litokee, alikuwa radhi kulizuia kwa nguvu zote. Alichokuwa akikitaka mahali hapo, huyo Ethan aletwe kwake ili afanye uamuzi mmoja, kama kumuua au kumuonya kwa kile alichokuwa akikifanya.

“Kwa hiyo?” aliuliza kijana mmoja.
“Mmuue hukohuko.”
“Sawa mkuu!” alisema kijana mmoja na kuanza kuondoka.

“Subirini kwanza. Au kama vipi mleteni huku nimuue kwa mkono wangu! Wakati wa kuja huku, tumieni meli ya mizigo ya Mediteranian Cargo,” alisema bwana Cook.

“Hakuna tatizo!”
Kila kitu kikaanza kufanyika, vijana wale wakapatiwa dola laki tano kwa ajili ya safari yao ya kwenda nchini Tanzania ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kumtafuta Ethan na kwenda naye nchini Marekani.

Hawakujua wangempata wapi lakini kwa kuwa walijua kwamba Ethan alikuwa miongoni mwa watu waliohusudu sana michezo ya kamari, wakataka kuhakikisha wanatembelea sehemu zote za michezo hiyo na kumkamata.

Hawakutakiwa kurudi nchini Marekani pasipokuwa na Ethan mikononi mwao, walitakiwa kufanya juu chini mpaka mwanaume huyo anapatikana na kupelekwa nchini Marekani katika mikono ya bwana Cook.

Mawasiliano na Meli ya Mediteranian Cargo iliyokuwa Mombasa yakaanza kufanyika, mara baada ya Ethan kutekwa, hakutakiwa kupelekwa Marekani kwa ndege, alitakiwa kubebwa kwenye meli kiusalama zaidi.

Hilo halikuwa tatizo, nahodha alipopewa taarifa hiyo tu, akageuza meli hiyo ya mizigo na safari ya kuelekea nchini jijini Dar es Salaam kuanza. Kwa ujumla, kila kitu kilikamilika, kutokana na fedha nyingi alizokuwa nazo, alifanya chochote alichokitaka, hata baadhi ya viongozi wa serikali ya Marekani walikuwa chini yake.
*****

Hakukuwa na kitu alichokuwa akikipenda katika maisha yake kama kucheza kamari. Hakuanza kipindi hicho, tangu alipokuwa kijana mdogo aliyeishi katika mtaa wa kimasikini wa Manhattan, Ethan alikuwa mtu wa kushinda vijiweni na kucheza kamari tu.

Hayo ndiyo yalikuwa maisha yake, haikujalisha kama alikuwa na fedha au hakuwa nazo, alifilisika au la, kitu alichokuwa akikifanya pasipo kujihukumu moyoni mwake kilikuwa ni kucheza kamari tu.

Kila nchi aliyokwenda, kitu cha kwanza kilikuwa ni kupanga hoteli zilizokuwa na cassino ili humo ndani aweze kucheza kamari kama kawaida yake. Kwenye kamari hizo, alikuwa akila sana lakini kuna wakati mwingine aliliwa mpaka kuhisi kufakufa.

Hapo New Africa hotel alipofikia, kulikuwa na ukumbi mkubwa ambao ulitengwa kwa ajili ya cassino, ndani yake kulikuwa na michezo mbalimbali ya kamari.

Alipofika hotelini hapo siku ya kwanza, kitu alichokifanya hata kabla ya kula, ni kwenda cassino na kuangalia ni jinsi gani watu walikuwa wakicheza kamari hasa kwa kutumia karata ambao Wazungu waliuita Pokker.

Alijitahidi kucheza, alionekana kama mmoja wa vijana waliozaliwa na kipaji cha kucheza mchezo huo tu. Alipofika ndani ya ukumbi huo tayari kwa kucheza mchezo huo

Alipofika ndani ya ukumbi huo tayari kwa kucheza mchezo huo, aliwashinda wengi na kujikusanyia kiasi kikubwa cha fedha.
Kwa kipindi kifupi tu akajikuta akiwa mtu maarufu ndani ya cassino hiyo hali iliyomfanya kujiona kuwa bingwa wa mabingwa na kubatizwa jina la Mr Pokker.

Wacheza kamari wakaanza kupeana taarifa kwamba kulikuwa na mtu mmoja ambaye alikuja katika Hoteli ya New Africa na kisha kuzama katika cassino iliyokuwa mahali hapo na kucheza kamari, alikuwa moto wa kuotea mbali hivyo mabingwa wengi kukusanyika hotelini humo kuona makali ya huyo mtu aliyekuwa gumzo.

“Anajua kucheza sana Pokker, kuna wengi amewashinda,” alisema jamaa mmoja simuni, alikuwa akizungumza na rafiki yake.

“Anajua kweli?”
“Ni hatari aiseee...unamjua Muingereza
aliyetutesa yule kwenye kamari, Phillip Walker?”

“Ndiyo!”
“Amemla!”
“Duuh!”
“Unamjua Mc Regard, yule Mzungu kutoka Belgium?”
“Ndiyo!”
“Amemla!”
“Acha bwana!”
“Ni hatari sana.”

“Sasa hawezi kuja Las Vegas akutane na wakali wake?”
“Ngoja, nitazungumza naye.”
Watu waliotajwa hapo juu walikuwa hatari katika mchezo wa kamari, walijua kucheza kamari na kuweka gumzo kwa watu wengi waliokuwa wakienda katika Cassino mbalimbali jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kucheza kamari.

Hawakuwa wakiishi nchini Tanzania, walikuwa mabaharia ambao kila siku walisafiri kwa meli, walipofika nchi yoyote ile, kazi yao ilikuwa ni kucheza kamari kisha mizigo iliposhushwa au kupandishwa, waliendelea na kazi yao.

Waliwala fedha watu wengi, walikuwa Wazungu wenye uwezo mkubwa wa kucheza kamari, walijitengenezea majina na kuonekana hatari miongoni mwa wacheza kamari mbalimbali mpaka wengi kuogopa kucheza nao.

Pamoja na uwezo wao mkubwa wa kucheza kamari, kwa Ethan hawakufua dafu, wote hao walipokea vipigo mfululizo hali iliyowafanya kupoteza zaidi ya dola milioni moja kila mmoja.

Baada ya kucheza sana kamari na kujitengenezea jina kubwa ndani ya wiki mbili hapo ndipo alipoamua kuhama na kuhamia katika Cassino ya Las Vegas ambapo kuliaminika kuwa na wakali wa kucheza kamari.

Alipofika huko, bado moto wake ulikuwa uleule, aliendelea kuwala fedha zao na

na kujikuta akiwa biashara, yaani kila alipokuwa akicheza, watu walimpandia hela na kusema kwamba angeshinda, kweli alifanya hivyo.

Vijana wa bwana Cook walipofika nchini Tanzania, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kwenda katika kumbi za starehe kwa ajili ya kumtafuta Ethan kwani kwa jinsi walivyojua ilikuwa ni lazima kumkuta huko kwa kuwa ndiye alikuwa miongoni mwa watu waliopenda starehe katika vijana wote wa bwana Cook.

Walitembelea katika hoteli kubwa kwa lengo la kumtafuta lakini hawakuweza kumpata.

Ndani ya wiki mbili nzima kazi yao kubwa ilikuwa ni kwenda huku na kule katika kumbi na hoteli kubwa lakini hawakuweza kumpata mwanaume huyo.

Kikafika kipindi wote watatu wakaonekana kukata tamaa, hawakuona kama wangeweza kumpata Ethan aliyekuwa amepotelea nchini Tanzania.

Kuna kipindi wakahisi inawezekana Ethan hakuwepo nchini Tanzania hivyo walijadiliana kwenda sehemu nyingine kumtafuta hasa katika nchi jirani kama Kenya na Uganda.

“Mnaonaje?” aliuliza Thorn, mmoja wa vijana waliokuwa wametumwa.
“Nadhani twendeni Kenya, haiwezekani tukamkosa sehemu za starehe na wakati tunajua jinsi Ethan alivyo,” alisema Stephen.

“Sawa! Haina tatizo! Twendeni huko hata kesho!”
“Hebu subiri kwanza!” aliingilia Bruno.
“Una wazo?”
“Ndiyo! Kwa nini tusiendelee kumtafuta hapahapa?”

“Ila tumemkosa, na wewe umeona!”
“Bado! Kuna sehemu nyingi tunatakiwa kwenda,” alisema Bruno.

“Hatujakuelewa!”
“Kipi tena hamjanielewa hapo? Kwani tumemaliza sehemu zote?”

“Bado ila......”
“Jamani! Wote tunamjua Ethan kwamba alikuwa mtu wa kupenda starehe, si ndiyo?”

“Ndiyo!”
“Ila mnakumbuka kwamba hata kucheza kamari Ethan alikuwa balaa?”

“Ndiyo! Tena umenikumbusha, nahisi tukianza kumtafuta kwa staili hiyo itakuwa safi,” alisema Thorn.
“Hebu tujaribuni!”

Hawakuwa na jinsi, walikubaliana kwamba waendelee kumtafuta Ethan kama mcheza kamari. Walichokifanya ni kuanza kutembelea kumbi mbalimbali hasa kulipokuwa kwa wacheza kamari wengi kwa lengo la kumpata mtu waliyekuwa wakimtafuta.

Mpaka kufikia kipindi hicho, tayari mwezi ulikuwa umepita lakini bado hawakufanikiwa kumpata Ethan jambo lililowakera sana.

Waliwasiliana na bwana Cook na kumwambia kile kilichokuwa kikiendelea kwamba walikuwa na wazo la kumtafuta katika kumbi mbalimbali za kamari kwani walijaribu kwenda kwenye kumbi za starehe lakini hawakufanikiwa kumpata.

Bwana Cook akakubaliana nao hivyo kuanza kwenda huko. Haikuwa kazi kubwa, usiku hawakulala, muda wao wa kulala ulikuwa mchana, ulipoingia usiku, walikuwa na kazi ya kumtafuta Ethan tu.

Baada ya kukaa kwa kipindi cha miezi mwezi mmoja ndipo waliposikia kwamba kulikuwa na kumbi mbili tu ambazo zilikuwa na wacheza kamari wakubwa, kulikuwa na ile iliyokuwa New Africa na Las Vegas, hivyo wakaanza kwenda huko kwa kuanzia New Africa.

Kabla ya kuulizia, wakaanza kupita katika kila meza ya wacheza kamari wa mchezo wa Pokker na kuanza kuwaangalia wachezaji. Kila mmoja alikuwa makini kabisa kuwaangalia na katika meza kumi na nane zilizokuwa ndani ya cassino hiyo, Ethan hakuonekana kitu kilichowafanya kuuliza.

“Ethan! Who is he?” (Ethan! Ndiye nani?) aliuliza mwanaume mmoja aliyekuwa ameulizwa kuhusu Ethan.

Hapo ndipo walipoanza kumwambia kuhusu mwanaume huyo, walifafanua sana, jinsi alivyokuwa na utaalamu wake wa kucheza kamari lakini mwisho wa siku mtu huyo aliwaambia kwamba hakuwa akimfahamu kwani hapo kulikuwa na wacheza kamari wengi waliokuwa wakifika, hivyo kumfahamu ilikuwa ngumu.

“Tufanye nini?”
“Hebu tuwaulizeni wengine.”
Hapo ndipo wakaanza kuwauliza watu mbalimbali waliokuwa ndani ya cassino hiyo.

Jina walilokuwa wakiuliza lilikuwa Ethan kiasi kwamba ilikuwa ngumu sana kwa wengine kumfahamu.

“Unamuulizia mtaalamu wa kucheza kamari hapa?”

“Ndiyo!”
“Unataka kucheza?”
“Kama yupo mkali!”
“Unaweza nikuwekee dau?”

“Kiasi! Kuna wakali kwanza hapa?”
“Wakali wamepungua, wamehamia Las Vegas, kuna mmoja anaitwa Mr Pokker, huyo ndiyo balaa!” alisema mwanaume huyo.

“Hebu kwanza nianze na hawa, nikiwashinda utanipeleka kwa huyo Mr Pokker,” alisema Thorn na kupelekwa kwenye meza iliyojaa wacheza kamari, akapanda dau la dola elfu kumi kwanza kupima upepo.

Je, nini kitaendelea?
 
NYEMO CHILONGANI
BIASHARA YA KIFO

Sehemu ya Kumi na Moja.

Ili kumpata Ethan ilitakiwa kutumia fedha nyingi, wote walikubaliana kwamba Thorn aanze kucheza kamari, hata kama angeliwa sana hilo wasingejari kwani lengo lao mwisho wa siku lilikuwa kumpata mtu wao waliyemfuata nchini Tanzania.
Thorn hakuona hatari kumwaga fedha, alikuwa tayari kwa kila kitu. Alijua kucheza kamari ya Pokker lakini hakuwa na uwezo kama watu wengine ambao walionekana kuwa moto wa kuotea mbali.
Siku ya kwanza aliliwa sana, siku ya pili, hakukubadilika kitu, aliliwa kama kawaida kiasi kwamba akakaa chini na wenzake na kujadili ni kitu gani walitakiwa kufanya kwani hali ilionekana kuwa mbaya kwa upande wao.
“Tuwe wadhamini,” alisema Bruno.
“Kivipi?”
“Tuwe mabosi, kamari zetu ziwe za kuwapandia watu, ila kazi hiyo aifanye Stephen. Kila nikikaa na kufikiria, moyo unaniambia kwamba tutampata huyu mjinga,” alisema Bruno.
“Basi sawa. Kwa hilo hakuna tatizo.”
Wakapanga mipango yao, ilipopangika vizuri, kesho yake wakarudi tena katika cassino iliyokuwa kwenye Hoteli ya New Africa ambapo huko kama kawaida Stephen akaanza kufanya kama alichokuwa ameagizwa.
Kama inavyokuwa katika michezo mingi ya kamari hasa kunapokuwa na ushindani mkubwa huwa kunakuwa na watu wenye kazi ya kuwekeana madau pembeni ndivyo ilivyokuwa ndani ya cassino hiyo.
Wachezaji wanne walijikusanya katika meza moja ambayo walipenda sana kuitumia, pale, Stephen akaanza kazi ya kumwaga fedha huku akimuwekea kila mtu aliyemuona kuwa mkali kwamba angeibuka mshindi katika mchezo huo.
Wakati mwingine alikuwa akiliwa lakini wakati mwingine alikuwa akila. Kutokana na kiasi kikubwa cha fedha alichouwa akikiweka, wengi wakamuonea huruma na kumtaka kubadilisha mazingira kwa kuwawekea watu waliojua kucheza mchezo huo ili apate faida vinginevyo angeliwa kila siku.
“Unaliwa sana fedha zako,” alisema jamaa mmoja, alimsogelea kisiri.
“Daah! Sasa nifanye nini na wakati wachezaji wenyewe wanazingua?” alihoji Stephen.
“Unataka nikuonyeshe chimbo?”
“Itakuwa poa sana.”
“Twende sehemu fulani hivi kwenye Cassino ya Las Vegas, pale kuna jamaa anajua sana mpaka wakampa jina la Mr Pokker, muwekee huyo dau lako, utakuwa tajiri,” alisema jamaa huyo.
“Iko wapi hiyo?”
“Si mbali sana! Una usafiri?”
“Tunaweza kukodi.”
“Haina noma! Twende.”
Hakukuwa na haja ya kuendelea kusubiri mahali hapo, walichokifanya ni kuondoka kwenda huko Las Vegas, njiani, walikuwa wakizungumza kana kwamba walikuwa marafiki wa muda mrefu.
Katika kipindi chote cha safari, jamaa yule aliendelea kumwambia Stephen kwamba huyo jamaa ambaye walikwenda kumuwekea dau alikuwa mtu hatari sana, mtu asiyefungika, aliyekuwa akicheza sana mchezo wa Pokker kana kwamba kauanzisha yeye.
Kutoka Posta Mpya mpaka Upanga hakukuwa mbali sana, walitumia dakika tano tu wakawa wamekwishafika katika cassino kubwa iliyokuwa na umaarufu mkubwa jijini Dar es Salaam. Dereva akapaki gari katika sehemu ya maegesho na kisha watu hao wawili kuteremka na kuanza kuelekea katika Cassino hiyo ilikuwa na ukimya mkubwa kwa nje ila kwa ndani kulifunguliwa na mziki mkubwa ambao haukuwa ukisikika kwa nje.
Wakati wote walipokuwa wakielekea huko, Bruno na Thorn walikuwa kwa nyuma wakiwafuatilia. Hawakujua watu hao walipokuwa wakielekea lakini waliendelea kuwafuata mpaka gari liliposimama nje ya jengo kubwa lililoandikwa Las Vegas Cassino kwa nje.
Hapo ndipo walipogundua kwamba mbali na cassino nyingine nyingi walizowahi kuzitembelea, kumbe kulikuwa na cassino kubwa ambayo hawakudhani kama ingekuwa nchini Tanzania. Wakateremka na kuendelea kuwafuatilia ambapo wakapitia katika mlango mkubwa wa mbele na kisha kuteremka ngazi kwani cassino hiyo ilikuwa chini ya ardhi, hivyo wakaanza kwenda huko.
Walichokikuta, hakikutofautiana na cassino mbalimbali zilizokuwa nchini Marekani. Watu wengi walikuwa wamejazana, kulikuwa na meza zaidi ya thelathini, mbali na kamari ya Pokker, kulikuwa na kamari nyingine
Kulikuwa na idadi kubwa ya wanawake waliokuwa wakicheza utupu kwa kudanndia kwenye vyuma vilivyokuwa ndani ya cassino hiyo ambapo wanaume walikuwa na kazi ya kuwatunza fedha na kisha kuwashikashika tu.
Hawakutaka kufuatilia kitu chochote kile, hawakufika ndani ya cassino hiyo kwa ajili ya kucheza kamari au kuwaangalia wanawake wale, walchokuwa wakikitaka ni kuona mahali alipokuwa akipelekwa Stephen.
“Wako wapi?” aliuliza Bruno.
“Wale kule.”
“Hebu tuwahi wasije wakatupotea, watu wengi sana humu,” alisema Bruno na hivyo kupiga hatua za kasi zaidi.
Safari ya Stephan na mwanaume yule waliishia pembeni ya meza iliyokusanya wacheza kamari wanne waliokuwa wamezungukwa na watu wengi ambao walikuwa wakiufuatilia mchezo waliokuwa wakicheza.
Kila aliyekuwa akicheza kamari ya Pokker alikuwa na miwani myeusi usoni mwake ambayo waliitumia katika kuchungulia karata za wachezaji wengine pasipo kugundulika lakini pamoja na hayo, walitakiwa kuwa makini kutokana na miwani ile kuonyesha taswira ambayo ingezifanya karata zao kuonekana kwa wachezaji wengine.
“Unamuona yule?”
“Yupi?”
“Yule wa upande ule!”
“Aliyevaa miwani mikubwa?”
“Hapana! Yule wa pembeni yake.”
“Namuona! Ndiye nani?”
“Yule ndiye Mr. Pokker, ndiye mtaalamu mwenyewe wa kumuwekea hela. Hata wale watu waliokuwa nyuma yake, wamemuwekea yeye,” alisema jamaa yule.
Alichokifanya Stephen ni kumwangalia vizuri mwanaume yule aliyeonyeshewa, sura yake haikuwa ngeni kabisa, alionekana kushtuka lakini alitaka kujihakikishia zaidi kama ndiye yule aliyekuwa akimfahamu au alikuwa mtu mwingine.
“Ethan!” alisema Stephen mara baada ya kumuona vizuri mwanaume huyo.
Mapigo yake ya moyo yakamdunda mno, hakuamini kama mwanaume aliyekuwa akimwangalia kwa wakati huo alikuwa Ethan, mtu waliyekuwa wamemtafuta sana. Hakutaka kumwangalia kwa mbali, alitaka kujihakikishia kama alikuwa mwenyewe au alimwangalia kiwange, akasogea zaidi kule, Ethan hakuweza kumuona kwani muda wote macho yake yalikuwa kwenye karata tu.
“Ndiye yeye!” alisema Stephen huku akionekana kushtuka mno. Alichokifanya ni kugeuka nyuma ambapo macho yake yakatua kwa mwenzake waliokuwa wakimwangalia, hapohapo akawapa ishara ya kuangalia kule alipokuwa akiangalia, nao, wakamuona Ethan, mioyo yao ikafurahi, ikarukaruka kwa furaha, kazi kubwa waliokuwa nao, waliona ikiwa imekamilika.
*****
Mtu waliyekuwa wamemfuata nchini Tanzania, alikuwa mbele yao akiwa bize kucheza kamari ya karata. Walimwangalia huku wakati mwingine wakitaka kupata uhakika juu ya kile walichokuwa wakikiona, walichokifanya ni kumsogelea, wakaamini kwamba alikuwa yeye.
Wakashusha pumzi ndefu, wakafurahia kile walichokuwa wamekiona. Hawakuamini kwamba baada ya kipindi kirefu kupita hatimaye walikuwa wamefanikiwa kumpata mwanaume huyo aliyekuwa bize, hakuangalia hata pembeni, macho yake, muda wote yalikuwa yakiziangalia karata tu.
“Ndiye yeye! Kwa hiyo tumfuate?”
“Hapana! Hatutakiwi kuwa na presha, hapa ni cassino, lazima ukumbuke hilo,” Thorn alimwambia Bruno aliyeonekana kuwa na presha.
Walichokifanya ni kwenda pembeni, wakaanza kumfuatilia Ethan pasipo kugundulika, muda ulikuwa ukienda, walimwangalia jinsi alivyokuwa akicheza, kazi yake kubwa ilikuwa ni kukusanya hela kwani watu wote waliouwa wakikaa, aliwafunga kana kwamba alikuwa akicheza na watu wasiojua.
Ilipofika saa kumi alfajiri, Ethan akainuka, akachukua fedha zake na kuagizwa dereva aletwe mule ndani tayari kwa kuondoka, hakutaka kuzibeba fedha hizo bali alichokifanya ni kuziingiza kwenye akaunti zake kupitia kwa mtu wa mahesabu aliyekuwa hapo ndani, kiasi alichobaki nacho ni shilingi laki tano kwa ajili ya matumizi yake tu.
Dereva alipoletwa, akatoka naye na kwenda nje ya cassino hiyo ambapo huko akachukua teksi na kuondoka pasipo kujua kwamba kulikuwa na watu waliokuwa wakimfuatilia, walichotaka kujua ni mahali alipokuwa akiishi.
Waliendelea kuifuata teksi ile mpaka ilipofika katika Hoteli ya New Africa ambapo Ethan akateremka na kuelekea ndani. Wakaridhika, kwa kuwa walihitaji kuwa naye karibu zaidi, walichokifanya ni kuteremka.
“Kumbe alikuwa akiishi katika hoteli tunayoishi...daaah!” walishangaa kwani nao walichukua vyumba ndani ya hoteli hiyo.
Hawakutaka kuchelewa, walichokifanya ni kuelekea ndani ya hoteli hiyo na kisha kusubiria siku inayofuata ambapo waliamini kwamba ilikuwa ni lazima Ethan kutoka, hapo ndipo wangefanikiwa kumteka na kufanya walichotaka kukifanya, likiwemo suala la kumrudisha nchini Marekani.
Walichokifanya usiku huo ni kuwasiliana na bwana Cook na kumwambia ukweli kwamba tayari walikuwa wamefanikiwa kwani mtu waliyekuwa wameagizwa walifanikiwa kumuona na hivyo kilichokuwa kimebaki ni suala lao la kumteka na kumrudisha nchini Marekani.
“Mnajua kwamba meli imekwishafika huko?”
“Ndiyo bosi! Tulipewa taarifa.”
“Basi jueni mnaosubiriwa ni nyie tu, niwape muda gani?”
“Kama siku mbili, utapata majibu.”
“Sawa. Hakikisheni mnafanya kazi kwa wakati.”
“Hakuna tatizo bosi.”
Walichokifanya siku iliyofuata ni kuanza kumfuatilia mwanaume huyo. Wala haikuwa kazi kubwa sana kwa kuwa walikuwa katika hoteli moja. Alichokifanya Bruno ni kukaa kwenye makochi ya mapokezi na kuanza kumsubiria Ethan ambaye ilipofika saa sita mchana, akatoka huku akizungumza na simu.
Alichokifanya ni kuwashtua wenzake ambao wakatokea mahali hapo na kuanza kumfuatilia kwa nyuma. Hawakutaka kuwa naye karibu, walimuacha mpaka anafika umbali fulani na ndipo nao wakachukua teksi na kuanza kumfuatilia.
Walihisi kwamba kulikuwa na sehemu alipokuwa akielekea, hawakujua ni wapo na alikuwa akifuata nini huko. Hawakutaka kuacha, kwa sababu walikuwa wamedhamiri kumfuata, waliendelea kusonga mbele.
Walimfuatilia mpaka alipofika Gongo la Mboto ambapo mbele kabisa kama kilometa tatu wakafika Pugu Kajiungeni ambapo hapo kulikuwa na barabara iliyokata kushoto ambayo ilikuwa ikielekea Chanika na nyingine ilikuwa ikinyooka, huko ndipo kulipokuwaKisarawe.
“Where is he going?” (Anakwenda wapi huku?) aliuliza Thorn.
“I don’t know, ask him,” (Sijui! Muulize) alijibu Bruno, akimaanisha amuulize dereva ambapo Thorn akafanya hivyo.
“Kisarawe...”
“Okey!”
Safari ilikuwa ndefu lakini hawakukuwa na mtu aliyetaka kusimama, waliendelea mbele kwa kuamini kwamba ilikuwa ni lazima wampate mwanaume huyo na hivyo kumteka na kurudi naye nchini Marekani.
Katika njia hiyo waliyokuwa wakipita, kulikuwa na nyumba chache mno ambazo zilionekana kuwa mpya na nyingine zikiwa zinaendelea na ujenzi. Barabara haikuwa nzuri, hakukuwa na lami, hali iliyokuwepo ilionyesha kabisa kwamba wakati wa mvua kali, barabara ile ilichimbika sana.
Waliendelea mbele, walikuwa wakipandisha milimani, idadi kubwa ya minara ilikuwepo huko Kisarawe, kila mmoja alionekana kubabaika kwani kwa jinsi umbali ule ulivyokuwa, walifikiria jinsi hali itakavyokuwa endapo mafuta yangewaishia.
Waliendelea kumfuata mpaka alipofika sehemu iliyokuwa na nyumba nyingi nzuri, wakaona gari lile likisimama nje ya jumba moja kubwa kisha Ethan kumlipa dereva yule kiasi cha fedha alichotaka na kuingia ndani.
Nao hawakutaka kuendelea na safari, walichokifanya ni kuteremka na kuanza kuelekea katika nyumba ile ambapo Ethan alikuwa ameingia. Walichokipanga ni kumvamia kisha kumteka, hawakutaka kusikia kitu chochote kile, maelezo waliyokuwa wamepewa ni kumteka mwanaume huyo tu, maelezo mengine yangeelezwa mbele ya safari.
Walipolifikia geti kubwa la nyumba ile, wakatoa bastola zao na kuzishika vilivyo kisha kuanza kugonga geti lile. Walijifanya kuwa watu wema na hata ugongaji wa geti hilo ulikuwa ni wa kistaarabu sana, baada ya dakika moja, geti likafunguliwa na msichana, alikuwa Annabel.
“How are you!” (Habari yako!) alimsalimia Thorn.
“Cool! What can I help you?” (Salama! Niwasaidie nini?)
“We want the man who got in here,” (Tunamtaka mtu aliyeingia humu ndani) alijibu Thorn huku akiachia tabasamu pana.
“Who? Nobody got in here!” (Nani? Hakuna aliyeingia) alisema Annabel.
Hawakufika pale kupoteza muda, walikuja kwa ajili ya kufanya kazi moja tu, kumchukua mtu wao na kuondoka naye. Walichokifanya ni kumsukumia Annabel ndani kisha kuingia. Hawakutaka kumuacha mahali hapo kwa kuhisi kwamba angeweza kutoa taarifa kwa watu wengine kwa kupiga kelele, hivyo wakaanza kuondoka naye.
“Let’s get in, don’t shout out,” (Twende ndani, usipige kelele) alisema Thorn huku akionekana kumaanisha alichokuwa akikizungumza. Annabel akawa kimya, hofu ikamjaa moyoni.
Walipoufikia mlango wa kuingia sebuleni, Thorn akausukuma na Annabel kutangulia ndani, kitu kilichoonekana kumshtua hata Annabel mwenyewe, sebuleni hakukuwa na mtu yeyote yule, yaani yule Ethan aliyekuwa amemuacha pale kochini, hakujua alikwenda wapi.
Akapigwa na mshangao!

Je, nini kitaendelea?
Tukutane Jumanne.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sehemu ya 12.

Kila kitu kilichokuwa kikiendelea kilikuwa furaha kwake, hakuamini kama maisha yake yangebadilika na kuwa kama yalivyokuwa, kiasi ambacho kila siku alikuwa akikipata kutoka kwa wacheza kamari wenzake kilimfanya kuashau kabisa majukumu yaliyomfanya kuwa nchini Tanzania.

Alipokuwa akiishi nchini Tanzania, wakati mwingine alijisikia kuwa kama nchini Marekani, alikuwa akipata kila kitu alichokitaka, kuwaona wanawake wazuri na hata kuingiza kiasi kikubwa cha fedha, kwa kifupi, hakuwa na mawazo ya kurudi nchini Marekani, na hata ile kazi aliyokuwa amepewa, hakutaka kuendelea nayo tena.

Mara baada ya kuamka kutoka usingizini, kitu cha kwanza kabisa kilichokuja kichwani mwake ni msichana Annabel tu. Alimpenda mno binti huyo, alimthamini na hakuwa tayari kuona akimpoteza mikononi mwake, alichokuwa amekipanga kwa wakati huo ni kumfuata nyumbani kwao tu.

Akachukua simu yake na kumpigia kisha kumpa taarifa kwamba alikuwa akianza safari kuelekea nyumbani kwao. Alibaki akizungumza naye mpaka alipodhuka mapokezi ambapo akaacha funguo na kisha kuondoka.

Nje, akachukua teksi na safari kuanza. Ilikuwa safari ndefu, kila siku alikuwa akiitumia teksi hiyohiyo kwa ajili ya kumpeleka Kisarawe.

Muda wote huo, Ethan hakujua kama alikuwa akifuatiliwa, magari yote aliyoyaona nyuma, hayakumtia wasiwasi hata kidogo.

Walipofika Gongo la Mboto, wakaunganisha, walipoanza kuchukua barabara ya kuelekea Kisarawe, kwa mbali nyuma yake aliliona gari moja ndogo, hakuwa na wasiwasi nalo hata kidogo.

Baada ya kupita ile njia ya kuelekea Chanika, alipoona lile gari likizidi kuwafuata hapo ndipo alipoanza kuwa na wasiwasi kwamba inawezekana gari lile lilikuwa likiwafuata wao. Alichokifanya ni kumwambia dereva aongeze mwendo, nalo likaongeza.

Walipofika, akateremka na kuangalia nyuma kiwizi, aliliona gari lile likisogea taratibu na kisha kusimama, mpaka hapo alikuwa na uhakika kwamba watu waliokuwa ndani ya lile gari walikuwa wakimfuatilia, alichokifanya ni kumlipa dereva fedha zake kisha kwenda ndani huku akijifanya kutokuwa na wasiwasi.
“Nisikilize,” alisema Ethan mara baada ya kuingia ndani.

“Kuna nini?” aliuliza Annabel.
“Kama kuna yeyote atakuja kuniulizia, mwambie sipo,” alisema Ethan.
“Nani anakuja kukuulizia?”
“Wewe fanya kama nilivyokwambia.”
“Kwani ku...” alitaka kuuliza Annabel lakini hata kabla hajamalizia swali lake, akasikia mlango ukigongwa, Ethan akakaa kochini.

“Fanya kama nilivyokwambia.”
“Kwani ni nani?”
“Hatuna muda Annabel, fanya kama nilivyokwambia,” alisema Ethan huku akijiweka sawa kochini.

Annabel hakujali sana, alichokifanya ni kutoka nje na kisha kuelekea kule getini. Ethan akasimama na kuchungulia dirishani, alitaka kufahamu ni nani alikuwa akimfuatilia. Mara akaona Annabel akisukumiwa ndani kisha wanaume watatu kuingia, alikuwa akiwafahamu vilivyo.

“Thorn....” alisema Ethan, hapohapo akajua kilichokuwa kikiendelea.

Hakutaka kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuondoka sebuleni pale na kuelekea bafuni, alitaka kuruka kupitia katika kidirisha kidogo kisha kuelekea nje. Bafuni hapo, alikiangalia kidirisha hicho, kilikuwa kidogo mno, alichokifanya ni kutoka na kuelekea jikoni.

Kila kitu alichokuwa akikifanya, alikifanya kwa harakaharaka, alipofika jikoni mlango haukuwa umefungwa, hivyo alichokifanya ni kuuparamia ukuta na kurukia nje, akaanza kukimbia, hakujua alipokuwa akielekea, alichokiomba ni kukutana na usafiri wowote ule, hasa pikipiki.
*****

“Where is he?” (Yupo wapi?) aliuliza Thorn kwa sauti kubwa.

“Who is he?” (Ndiye nani huyo?)
“I give you the last chance, tell us where he is by now,” (Ninakupa nafasi ya mwisho, tuambie yupo wapi sasa hivi) alisema Thorn huku akionekana kukasirika.

Bado msichana Annabel hakutaka kuwapa jibu walilokuwa wakilitaka na badala yake alikuwa akiwauliza walimzungumzia nani kwani ndani mule alikuwa peke yake. Kila mmoja alikasirika, hawakutegemea kupata majibu kama yale, alichokifanya Thorn ni kukoki bastola yake.

Annabel hakuonekana kuhofia kitu chochote kile, hata alipowekewa bastola kichwani, bado aliendelea kuuliza watu hao walikuwa wakimzungumzi nani kwani humo ndani hakuwa na mtu yeyote zaidi yake, sasa wao walikuwa wakimuulizia nani?

“Unatuletea jeuri siyo!”
“Jeuri gani sasa? Nyie mnamuulizia nani?”
“Ethan!”
“Ndiye nani?”

“Mbona unamchelewesha Thorn! Hebu ngoja nikuonyeshee dawa ya kiburi,” alisema Bruno huku akichukua bastola yake, kwa mbali Annabel akaanza kuhofia kwani kwa jinsi Bruno alivyoonekana, hakuwa mtu wa kuletewa utani.

Bruno hakutaka kuchelewa, alionekana kuwa mwenye hasira mno, kitendo cha msichana Annabel kuwajibu kile alichokuwa akiwajibu kilimkasirisha mno. Alikuwa tayari kumpiga risasi kwani alileta jeuri na wakati walijua kwamba alifahamu kila kitu.

“Subiri kwanza Bruno.”
“Hatuna muda wa kupoteza Thorn, hataki kusema, unahisi tunatakiwa kufanya nini? Hakuna, bora tumuue tu,” alisema Bruno.

“Usiwe na wasiwasi, huyu ndiye wa kutuletea mtu huyo,” alisema Thorn.
Walichokifanya ni kumchukua Annabel na kisha kuondoka naye nyumbani hapo, japokuwa msichana huyo alikuwa akililia aachiwe lakini hawakutaka kufanya hivyo.

Walichokuwa wakikifahamu ni kwamba lingekuwa jambo jepesi sana kwa Ethan kuwafuata kule walipokuwa endapo tu wangemwambia kwamba walikuwa na msichana huyo.
Wakatoka nje ambapo wakachukua gari lile walilokuja nalo na kuondoka mahali hapo.

Njiani, Annabel aliendelea kulia, alitaka aachiwe ili arudi nyumbani kwani aliendelea kusisitiza kwamba hakuwa amemuona mtu aliyekuwa ameuliziwa.
“Hakuna tatizo, wala usijali, kuna kazi kubwa tunataka kufanya naye,” alisema Thorn.

Walikwishaambiwa kwamba tayari meli ile iliyotakiwa kumchukua Ethan ilikuwa imekwishawasili jijini Dar es Salaam hivyo wakaanza kuwasiliana na nahodha ambaye aliwaambia mahali alipokuwa amepaki, bandarini na kwenda huko.

Walichukua muda wa masaa mawili mpaka kufika, wakamchukua Annabel na kumuingiza ndani ya meli na kuwekewa ulinzi mkali.

Msichana huyo alilia na kulia huku akitaka aachwe lakini hakukuwa na mtu aliyemsikiliza, walichokuwa wakikitaka ni kumuona Ethan akijisalimisha tu.
“Jamani! Kwani nimefanya nini?” aliuliza Annabel.

“Haujafanya kitu, tumejisikia tu kukuteka,” alisema Thorn huku akiachia tabasamu pana.
“Naomba mniache niondoke, naomba mniache.”

“Kivipi? Hatujamaliza kazi yetu, hauwezi ukaondoka mpaka tumpate mtu tunayemtaka, wewe si umekataa kumtaja, sawa, hakuna tatizo, utakaa mpaka atakapopatikana, asipopatikana, tunakutupa baharini,” alisema Thorn huku uso wake tu ukionyesha nijinsi gani alikuwa akimaanisha alichokuwa akikizungumza.

Annabel hakutaka kuzungumza ukweli, kila alipoulizwa kuhusu Ethan alisema kwamba hakuwa akimfahamu mwanaume waliyekuwa wakimuulizia. Ethan hakutaka kujali sana, kwa kuwa msichana huyo alipinga kwamba hakuwa akimfahamu, walichokifanya ni kumfungia ndani ya chumba kilichokuwa na giza nene.

Kilikuwa ni chumba kilichokuwa na mateso makali, pamoja na giza lililokuwemo ndani humo lakini pia sakafu yake ilikuwa na unyevuunyevu huku kwa mbali zikisikika sauti za panya zilizomfanya Annabel kuogopa mno.

Alilia sana, hakujua ni kitu gani kingetokea, hakujua ni jinsi gani angeweza kujikomboa na kuondoka katika chumba kile kilichokuwa na giza nene. Alilia siku nzima, si Thorn wala wenzake waliokuja kumjulia hali, walimuacha mulemule chumbani akiendelea kuteseka.

“Umeshinda usiku mzima ndani ya chumba hiki, hii ni saa tisa usiku,” alisema Thorn, aliufungua mlango huo huku akiwa na tochi mkononi. Annabel alikuwa akilia tu.

“Sikiliza, tunahitaji tumpate Ethan, unaweza kutusaidia katika hilo?” aliuliza Thorn.

“Simjui, sijawahi kumuona mwanaume huyo.”
“Sawa. Hakuna tatizo,” alisema Thorn na kuufunga mlango.

Watu hao walikuwa wabaya, walionekana kuwa watu wenye roho mbaya, alijua fika kwamba walimtaka Ethan kwa kuwa walitaka kumuua.

Hakutaka kuona hilo likitokea, hakutaka kuona mwanaume aliyekuwa akimpenda akiuawa kwa kuwa tu alitaja mahali alipokuwa.

Moyo wake uliumia, alipata mateso makali kwa sababu ya mapenzi tu, gharama ya kupenda ndiyo iliyomfanya siku hiyo kuwa katika hali hiyo. Aliteseka, usiku kucha hakulala, alibaki akilia tu huku matumaini ya kutoka ndani ya chumba hicho yakiwa madogo.

Wakati akiwa kwenye indi la mawazo, mlango ukafunguliwa, tayari ilikuwa saa moja asubuhi ila kama kawaida chumba hicho kilikuwa na giza nene.

“Utatuambia yupo wapi?” aliuliza Thorn.
“Nani? Mimi simjui mtu yeyoteyule,” alisema Annabel.

“Sawa,” alisema Thorn na kufunga mlango ule. Annabel akaanza kulia kwa sauti kubwa.
 
Sehemu ya 13

“Utatuambia yupo wapi?” aliuliza Thorn.
“Nani? Mimi simjui mtu yeyoteyule,” alisema Annabel.
“Sawa,” alisema Thorn na kufunga mlango ule. Annabel akaanza kulia kwa sauti kubwa.
*****

Askofu Benedicto alionekana kuwa na furaha, kila kilichokuwa kikiendelea kilimfurahisha mno. Alimpenda sana binti yake zaidi ya kitu chochote kile, kila alipomuona amekaa sehemu yoyote ndani ya nyumba yake, alimfuata na kukaa karibu naye.

Japokuwa alikuwa na mapenzi makubwa kwake lakini kila siku alikuwa mkimya, msiri mkubwa ambaye hakutaka kumuweka wazi kwamba alikuwa askofu baada ya kupitia upadri kwa kipindi kirefu.

Siku hii, alikuwa akitoka nyumbani kwake, alijaribu kumpigia simu Annabel na kumpa taarifa kwamba alikuwa njiani, tatizo likatokea kwamba msichana huyo hakuwa akipokea simu.

Alishangaa, haikuwa kawaida hata kidogo, alijua kwamba wakati mwingine binti yake anakuwa bize na mambo mengine, lakini anapoona kwamba alipigiwa simu, ilikuwa ni lazima kupiga ili asikie alitaka kuambiwa nini.

Aliendesha gari kwa kasi huku kila wakati akijaribu tena na tena kumpigia simu lakini majibu yalikuwa yaleuale kwamba simu haikuwa ikipatikana.

Alichanganyikiwa lakini hakuwa na jinsi, alijiona kutokufika haraka nyumbani, foleni za kizushi zilizokuwa zikitokea njiani nazo zilimuongezea hasira zaidi.
“Ninakupenda binti yangu, pokea simu,” alisema Askofu huyo huku akiendesha gari kwa kasi.

Ilipofika saa saba mchana ndiyo muda ambao aliingia nyumbani, kama kawaida akateremka na kufungua geti. Aliuzoea ukimya, hata alipoona kukiwa kimya, hakujiuliza sana, akaingia ndani.

Hali ya ndani ndiyo ikamshtua zaidi, ukimya ulikuwa maradufu, televisheni ilizimwa, kitu ambacho haikuwa kawaida hata mara moja, aliopozunguka huku na kule, hakumuona mtu yeyote yule, alichokifanya ni kujaribu kumuita Annabel, majibu yalikuwa yaleyale, ukimya mkubwa ulitawala.

Jina la mtu aliyemjia kichwani lilikuwa moja tu, naye alikuwa Etha, alichohisi ni kwamba inawezekana binti yake alikuwa na mwanaume huyo, hivyo akaanza kumpigia simu. Simu iliita na kuita, haikupokelewa kitu kilichomchanganya sana.

Akashusha pumzi ndefu na kutulia kochini, alionekana kuwa na mawazo mengi mno juu ya binti yake. Huku akijifikiria kuhusu Annabel, mara akasikia simu yake ikiita, alipoichukua na kuangalia kioo, alikuwa Ethan, harakaharaka akaipeleka sikioni.
“Ethan...” aliita.

“Naaam!”
“Upo na Annabel?”
“Hapana! Sipo naye!”
“Yupo wapi?”
“Nyumbani hayupo?”

“Hayupo, sijakuta mtu yeyote yule.”
“Mmmh!”
“Ulikuja nyumbani?”
“Ndiyo, nilifika hapo!”
“Ulimkuta?”

“Ndiyo!”
“Yupo wapi sasa?”
“Naomba tukutane sehemu tuzungumze.”
“Tuzungumze kuhusu nini?”
“Annabel!”
“Yupo wapi?”

“Kuna mengi ya kuzungumza, naomba tukutane tuongee,” alisema Ethan na kukata simu huku akimpa maelekezo juu ya mahali walipotakiwa kuonana.

Askofu akachanganyikiwa, maneno ya Ethan yalimchanganya mno, hakujua ni kitu gani Ethan alitaka kuzungumza naye mpaka kuhitaji kuonana naye.

Akatulia kichwani, alichokifanya ni kujaribu kupiga simu ya binti yake, majibu hayakubadilika, yalikuwa yaleyale kwamba simu haikupatikana.
Alichokifanya ni kuondoka nyumbani hapo na kumfuata Ethan kule alipomwambia waonane, alitaka kusikiliza ni kitu gani alitaka kumwambia.

Hakutaka kumpa Irakoze taarifa kwani alijua kwamba angechanganyikiwa, alihitaji kumuona kwanza Ethan ili wajue ni kitu gani walitakiwa kufanya.

Alipofika katika Hoteli ya Kilimanjaro, akateremka garini na kuanza kupiga hatua sehemu iliyokuwa na meza nyingi, kulikuwa na mghahawa ambapo hapo akapiga macho huku na kule, yakatua kwa Ethan aliyekuwa akinywa juisi, akaanza kumfuata.

“Kwanza niambie nini kinaendelea,” alisema askofu mara baada ya salamu.
“Subiri kwanza, kuna jambo linaendelea ila tunatakiwa kulifanya kwa umakini sana.

“Jambo gani Ethan? Binti yangu yupo wapi?” aliuliza askofu Benedicto, alionekana kuchanganyikiwa.
“Yupo!”

“Wapi?”
“Ametekwa!”
“Ametekwa! Na nani?”
“Subiri kwanza, usiwe na presha.”
“Ni lazima niwe na presha, ni nani amemteka?”

Ethan hakuwa na jinsi, alichokifanya ni kumuelezea askofu kile kilichokuwa kimetokea, tangu maisha yake yalivyokuwa mpaka muda huo.

Askofu alibaki kimya, alimsikiliza Ethan kwa umakini, alionekana kuwa kijana mpole lakini mambo aliyokuwa akiyaeleezea kwa mzee huyo yalimsikitisha mno.

“Ethan!”
“Ndiyo!”
“Pole sana, ila nitampata vipi binti yangu? Huyo Cook ni nani?” aliuliza askofu.

“Huwezi kumfahamu! Wanaomtaka si binti yako bali ni mimi,” alijibu Ethan huku akimwangalia askofu huyo usoni.
“Nitampata vipi binti yangu?”
“Usijali, utampata, nitakwenda kumuokoa.”

“Naomba ufanye hivyo! Au tukatoe taarifa polisi?”
“Hahah! Huwezi kumpata, wale watu ni hatari, ukitoa taarifa polisi utakuwa unajisumbua tu, ule mtandao wao ni wa kimataifa,” alisema Ethan huku akimwangalia Askofu usoni.

Tumaini la askofu Bonedicto lilikuwa kwa Ethan tu, kila alipokaa alikuwa akimuomba kumsaidia kumpata binti yake tu, hakuwa na uhakika mahali alipokuwa, alitamani kwenda polisi kushtaki, ila kama aangekwenda huko ingekuwaje? Angemtambulisha Annabel kama nani? Binti yake? Lilikuwa jambo lisilowezekana hata mara moja.

“Naomba unisaidie,” alisisitiza aaskofu.
“Usijali, nitafanya hivyo,” alijibu Ethan.
*****
 
Back
Top Bottom