Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,165
Mtunzi Nyemo Chilongani sehemu ya 01
SEHEMU YA 01
Mvua kubwa ilikuwa ikinyesha, mitaro midogo ikaanza kujaa maji huku baridi likianza kupiga kwa nguvu ndani ya jiji la Dar es Salaam.
Waliokuwa ndani ya nyumba zao, wakajifungia huku wale waliokuwa barabarani wakinunua miamvuli kwani mvua ile kubwa haikuonekana kuwa na dalili za kupungua hata mara moja.
Watu wengine walikuwa wakikimbilia sehemu zilizokuwa na uwezo wa kuzuia wasilowanishwe na mvua hiyo, wengine, walikubaliana na kile kilichokuwa kikiendelea hivyo kuendelea na kazi zao au safari zao huku wakiendelea kulowa.
Nje ya nyumba moja kubwa, msichana mrembo, mwenye sura nzuri, aliyekuwa na umbo lenye mvuto ambalo vijana wa sasa wangeliita namba nane alikuwa amesimama huku mkononi mwake akiwa ameshika furushi la nguo lililokuwa na nguo nyingi zilizofungwa kwa khanga.
Pale alipokuwa, macho yake yalikuwa mekundu, alikuwa na kitu moyoni mwake, hakuonekana kuwa mwenye furaha hata mara moja, baada ya dakika chache, machozi yale yaliyojikusanya machoni mwake yakaanza kumbubujika mashavuni mwake.
Msichana huyu aliitwa kwa jina la Irakoze, baba yake alikuwa Mnyarwanda na mama yake alikuwa Mnyaturu kutoka mkoani Singida.
Historia ya maisha yake ilianzia mbali, miaka miwili iliyopita, alikuwa akiishi mkoani Singida ambapo baadaye mwanamke aliyeitwa kwa jina la Hadija aliyetoka jijini Dar es Salaam akafika kijijini kwao na kumchukua kwa lengo la kwenda kufanya kazi katika nyumba yake iliyokuwa Magomeni jijini Dar.
Hilo ndilo lilikuwa lengo lake, aliporuhusiwa kumchukua, akaenda naye Dar ambapo huko baada ya kuishi kwa mwezi mmoja tu, wanaume wakaanza kumtongoza kwani ule urembo aliokuwa nao ulimvuta kila mtu aliyekuwa akimwangalia.
Uoga ulimjaa moyoni mwake, maneno aliyopewa na Bi Hadija kwamba kama angefanya ujinga na wanaume hao basi angefukuzwa na kurudishwa kijijini, ukamuogopesha na hivyo kila mwanaume aliyemfuata, alimwambia kwamba hamtaki.