Simulizi:Biashara Ya Kifo

Simulizi:Biashara Ya Kifo

Sehemu ya 28

“Kumbe una mtoto?” aliuliza askofu mmoja.

“Ndiyo! Najua nimemtenda Mungu wangu dhambi, ila ninaomba Mungu anisamehe,” alisema askofu Benedicto.

Huo ndiyo ulikuwa ukweli wenyewe, na haukubadilika, alipomaliza kusema maneno hayo, machozi yakaanza kumbubujika, akasimama na kuondoka zake.

Mapadri wote wakabaki katika chumba kile, walikuwa wakiulizana, kila mtu aliongea lake lakini ukweli uleule aliokuwa ameuzungumza ndiyo ulikuwa wenyewe, aliachia madaraka kwa kuwa tu alikuwa akifanya dhambi ya uzinzi.

Aibu kubwa ilionekana kuliogelea kanisa, hakukuwa na aliyeamini. Kwa kuwa lilikuwa ni jambo kubwa ambalo kanisa lilitakiwa kuambiwa, likatangazwa makanisani na hata kwenye vyombo vya habari.

Kila mtu aliyesikia hakuamini, kiongozi mkubwa, aliyeaminika, aliyeheshimika Tanzania nzima, leo hii alitangaza kujiuzulu tena kwa kashifa ya kuzaa mtoto kitu ambacho hakutakiwa kuwa nacho.
“Haiwezekani,” alisikika mwanamke mmoja.

“Jamani mwenzenu wala siamini,” alisema mwanamke mwingine.
“Kweli mwanaume mzuri si wa kumuamini,” aliingilia mwingine.

Baada ya wiki moja, Askofu Benedicto akaitwa Vatican ambapo huko alitakiwa kusimulia kilichokuwa kimetokea, hakuficha, alikuwa muwazi kwa kila kitu, alieleza vitu vyote vilivyotokea katika maisha yake.

Uongozi wa kanisa hilo kubwa duniani halikuwa na jinsi zaidi ya kumuondoa katika uongozi wa kanisa hilo nchini Tanzania na nafasi yake kuchukuliwa na mtu mwingine.

Watu walilizungumzia sana lakini hakujali, maneno ya watu, kashfa za watu hazikuwa zaidi ya furaha aliyokuwa nayo kuwa karibu na familia yake.

Baada ya miezi miwili, akiwa kama baba, akamfungisha ndoa binti yake, Annabel akaolewa na Ethan harusi iliyotangazwa sana kwani tayari umaarufu wa Benedicto ulikuwa mkubwa zaidi.

“Nilikuwa radhi kwa kila kitu, hakika uamuzi nilioufanya ulikuwa sahihi,” alisema Benedicto huku akionekana kuwa na furaha tele.

Kila kitu kilichotokea katika maisha yake kilibaki kubwa historia. Kwa bwana Cook, hakumtafuta tena Ethan, hakumfuatilia kwa kuwa alijua kwamba mwanaume huyo alikuwa amekufa baharini nchini Afrika Kusini.

MWISHO

Safi sana... inapendeza sana...

Chapter Closed...

Cc: mahondaw
 
Asante.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka sasa sijaona mahusiano ya heading "biashara ya kifo" zaidi ya kuwadhalilisha mapadri na kanisa
 
Back
Top Bottom