Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,165
- Thread starter
- #121
Sehemu ya 22
“Vipi?”
“Tayari! Jiandae, yafunge maboksi hayo vizuri, kuna boti itakuja upande wa huku, tutatakiwa kutoka kisha kuingia botini,” alisema Ethan.
Upande wa pili, Thorn na wenzake walikuwa wakiendelea kuimba na kupiga kelele, walikuwa wamekunywa mno na walionekana kuzidiwa na ulevi, muda wote, mizinga ya pombe kali ilikuwa mikononi mwao, nyimbo walizoimba, hazikueleweka kabisa.
Hakukuwa na wafanyakazi waliokuwa wakiwafahamu wale walikuwa wakina nani, kadiri walivyoendelea kuwa ndani ya meli ile walizidi kuwa na maswali zaidi, hawakuonekana kuwa watu wazuri hata mara moja kutokana na yale waliyokuwa wakiyafanya.
Baada ya dakika kama kumi, ghafla wakaanza kuhisi kwamba meli ile ilianza kuzama. Wafanyakazi wote wakashtuka, hawakuwa na uhakika juu ya kile walichokuwa wamekihisi, walichokifanya ni kwenda kwenye vyumba vyote kuangalia.
Walipokuwa wakielekea katika chumba kile, ghafla wakaona maji mengi yakitoka kutokea mlangoni na walipoufungua mlango tu, chumba kizima kilikuwa kimejaa maji, hivyo kitendo cha kuufungua tu, maji yakawa kama yameruhusiwa.
Kila mtu alichanganyikiwa, maji yaliendelea kuingia na kadiri muda ulivyozidi kwenda mbele na ndivyo meli ile ilivyoendelea kuzama. Kila mmoja akaanza kuhangaika huku na kule, walikuwa wamefika mbali mno na nchi kavu hakukuonekana, walikuwa wakiukaribia mpaka wa bahari mbili za Indi na Atlantiki.
“Chukueni maboya,” alisema nahodha huku akionekana kuchanganyikiwa, giza lilikuwa limetanda kila kona.
Kilichofanyika, wafanyakazi wakachukua maboya, kijana yule ambaye alikuwa amekwishafanya mipango na Ethan, akachukua boti iliyokuwa imefungwa nyuma ya meli ile, akaifungua kamba, ikaelekea baharini, hapohapo hakutaka kuchelewa, alichokifanya ni kujirusha majini na kuanza kupiga mbizi kuifuata boti ile, alipoifikia, akaipanda, akaiwasha na kuelekea katika upande ule aliokuwepo Ethan na Annabel ambapo napo chumba chao kilianza kujaa maji, maboksi yale matano yaliyojaa hela yalianza kuelea.
*****
Hawakutaka kupoteza muda, tayari meli ile ilianza kuzama hivyo ilimaanisha kwamba kama wasingefanya haraka kutoka, nao wangeweza kufa.
Alichokifanya Ethan ni kuchuka yale maboksi matano yaliyojaa hela huku akisaidiana na Annabel na kuanza kutoka nje.
Hayakuwa maboksi makubwa sana, na wala hayakuwa mazito sana. Walipotoka nje, tayari meli ililala upande mmoja, maji yalijaa na kadiri muda ulivyokuwa ukizidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo maji yalizidi na meli kuendelea kuzama zaidi.
Hakukuwa na mwanga wa taa yoyote ile, maji yaliingia katika mtambo wa umeme uliokuwa chini na umeme kuzima. Walikuwa wakipishana na wafanyakazi ambao wote hao walikuwa kwenye harakati za kuyaokoa maisha yao.
Huku wakiwa na maboksi yao, wakaelekea katika upande ambao walikubaliana na kijana yule kwamba wangeonana, kuangalia kule baharini, wakaiona boti kwa mbali ikielea, bila wasiwasi wakajua kwamba huyo ndiye alikuwa yule kijana ambaye mpaka muda huo hawakujua aliitwa nani.
Walichokifanya, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kuyatupa mabegi yale baharini, walitaka wayatangulize hayo na ndipo nao wafuate. Walipoyatupa yote na kuyaona yakielea, Ethan akamgeukia Annabel.
“We have to jump,” (tunatakiwa turuke) alisema Ethan.
“What?” (Unasemaje?)
“We have to jump right now,” (Ni lazima turuke sasa hivi) alisema Ethan.
“I am afraid,” (Naogopa)
“What are you afraid of?” (Unaogopa nini?)
“Pleasee! I can’t jump,” (Tafadhali! Siwezi kuruka) alisema Annabel huku akionekana kuogopa.
Maji yalizidi kujaa, watu waliendelea kukimbia huku na kule kuyaokoa maisha yao, wale waliokuwa na maboya, tayari wakaanza kujirusha baharini kwani kwa namna moja au nyingine walikwishajua kwamba meli ile ilikuwa ni lazima izame.
Alichokifanya Ethan ni kuanza kumbembeleza Annabel kwamba asingeweza kufa japokuwa maji yalionekana kuwa mbali. Alizungumza naye, walipokubaliana, akamshika mkono na kumwambia sasa ulikuwa wakati wa kuruka.
“Jump.....” (Ruka...) alisema Ethan huku akimshika Annabel mikono kisha kujitupa ndani ya maji.