Simu za Tecno, Infinix, Itel, n.k ni nzuri kwa bajeti lakini zinatumia soc zilizopitwa na muda, Ni sawa na kununua gazeti jioni,

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Tatizo la hawa ndugu zetu kina tecno hawatumii Soc (System on chip) mpya, soc huwa zinashikilia Ram, camera, modem za kunasa mtandao, wifi na vifaa vingine, soc ni kama roho ya simu.

Yani wao wanachofanya ni kusomba Soc za zamani zilizopitwa na muda ambazo huwa zimepungua bei, Tatizo sio soc za media tek bali ni wao kutumia soc zilizopitwa na wakati.

Watu wengi wamekariri simu ikiwa na media tek basi ina uwezo mdogo ila sio hivyo, kuna soc za mediatek za kisasa kama "MediaTek Dimensity 9200 Plus" ni ya tatu kwa ubora duniani kwa sasa lakini hawa ndugu zetu kina tecno hawaweki hizi soc mpya, wanaweka zilizopitwa na wakati,

simu chache sana za tecno zina Soc za kisasa,

hivyo tatizo hapa ni la Tecno na sio Mediatek.
 
Helio Ya G99 ni ya zamani mkuu maana camon 20 pro ndio inatumia
 
Mkuu hizo brand ulizo zitaja ni LAZIMA ziwepo ili watu wa vipato vidogo wamudu bei yake

Hebu fikiria iwapo simu zote zingekuwa zinatoa flagship kama za Samsung Iphone Huawei Pixel nk hizo bei za mamilioni mimi muuza mchicha ningemudu kununua?
Sana sana ningenunua matoleo ya nyuma sana ambapo tungerudi kule kule kwenye dhana ya kununua gazeti jioni

Hizo huwa ni marketing strategies na zipo kwenye magari, friji, saa, nguo nk nk

Na ndio maana hata hao akina Samsung nao inabidi watengeneze Midrange phone zenye soc ndogo ili bei iwe rafiki hata kwa wenye vipato vidogo
 
Naunga mkono hoja 👍👏
 
Back
Top Bottom