Simu za Tecno, Itel, Infinix n.k zinatoa matoleo mapya mangapi kwa wiki?

Kaka yake shetani

JF-Expert Member
Feb 1, 2023
3,595
8,729
Wachina kwenye bidhaa wamesaidia sana ila upande wa usomi kama mfanyabiashara wametumaliza japo itakuwa na ubishi kwa wasiojua.

Sifanyi biashara ya kuuza simu ila nimeliona kwa wanaofanya biashara za kuuza simu. Kampuni hizi zinazotoka china kama tecno, itel, infix na n.k kifikra zaidi zimekaa kukuza mitaji yao binafsi sio muuzaji ambaye muuzaji wa duka la simu.

Utowaji wa matoleo kila wiki au mwezi una muumiza muuzaji ambaye ndio mwenye duka sababu mfululuzo wa matoleo usababisha simu nyengine kukosa soko,kuonekana ubora ni mdogo au kutokuwa na maana.

Msululu matoleo ya simu bila mda au kujali soko lake kama limenunulika linachanganya wanunuzi kuona ya zamani sio simu tena.

Wenye maduka wasipomaliza matoleo yaliyopita mnawapa tabu. Kwanini wasitulie wakatengeneza simu iliyokamilika kabisa, yani leo hizo simu mpaka spare zinaingiliana unaweza shangaa simu iliyotoka leo ikaingiliana spare na toleo la nyuma.

Wachina ni wazuri kwa leo ila ni vilio kwa kesho sababu wapo kwa ajili ya kuangalia uchumi wao sio wewe mfanyabiashara watakao kupa bidhaa zao ukiangaika nazo wakati washachukua pesa yako.
 
Kumbuka na wao ni wafanya biashara , Kwa Tanzania soko la hzo simu limeshuka Sana japo Kwa asilimia kubwa ndo waliochangamsha matumizi ya simu hapa bongo ikiwemo na wewe ... Hakuna mtu ambaye hatumii bidhaa za mchina hapa bongo na Africa Kwa ujumla, na wao pia wanapitia changamoto za biashara
 
Uzuri wa matoleo ya hizi simu zinaendana na bajeti ya mtanzania tofauti na matoleo ya flagship brands..

Tecno Anaweza kutoa toleo jipya wiki hii halafu ikatofautiana elfu 50 tu na toleo la zamani so mteja anakuwa na uhuru wa kupata atakacho kwa bajeti yake ukizingatia watu wengi wanaonunua hizi mtk phones wananunua specifically kwa ajili ya mahitaji really ya simu na sio kwa fashion kama wale wa iphones,samsung..

Hivyo kutokana na hili matoleo ya zamani ya Tecno yanaendelea kubaki na thamani sokoni hata kama kuna toleo jipya limetoka
 
Back
Top Bottom