Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,891
- 155,895
Kwa kweli mimi si mjuzi sana wa mambo ya simu, maana baada ya kuhama kutoka kwenye Siemens C25 nikahamia kwenye Research in Motion, na baada ya pale nikaenda Seoul, sikuwahi kurudi tena.
Sasa hapa mjini naona tu wazee wa rika langu wananifuata nyumbani eti niwaagizie simu mtandaoni maana wanachekwa kwa wajukuu zao sababu tu ya aina ya majina ya simu wanazotumia.
Mimi sijui tofauti kati ya iPhone, Samsung, Tecno, LG, Sony, HTC, Infinix, Google Pixel , itel nk naona zote ni smart.
Nikiwa na itel au tecno au infinix vicheko vyenu nitavidharau na kuvipuuza