Simu ya kinabii iliyopelekea Rais wa nchi kurudisha jengo la kanisa lililoporwa na wasaidizi wake

Championship

JF-Expert Member
Aug 7, 2019
5,499
10,538
Miaka fulani mkuu wa polisi, katibu wa chama tawala na jaji mkuu wa nchi moja kusini mwa jangwa la sahara waliamua kuchukua jengo la kanisa kupitia kesi ya kutengenezwa.

Askofu Oyedepo alipoambiwa akasema, "Mungu ni mkubwa na anaweza kujilinda na kujitetea yeye mwenyewe." Akawaambia viongozi wa pale watafute jengo lingine waendelee na ibada.

Sasa kitu kilichotokea ni cha kistaajabisha sana. Mungu alimtuma mtumishi mmoja katika nchi hiyo. Mtumishi huyo alikuwa maskini sana kiasi kwamba hata hakuwa na simu ya mkononi.

Akapewa namba katika maono na akaambiwa apige hiyo namba na asiulize ni nani amepokea ila ampe ujumbe kwamba kama hataacha kuabudu sanamu basi ndani ya siku saba mganga wake wa jadi atakufa.

Baada ya siku saba kweli mganga wake akafa. Ikabidi huyo mtu atume watu wafuatilie ile simu ilipigwa na nani. Wakafuatilia na kufahamu kwamba ilikuwa ni kwenye kituo cha kupigia simu. Bahati nzuri walikuwa wanarekodi kila anayekuja kupiga simu.

Hivyo wakafanikiwa kumpata yule mtumishi na kumuuliza kama alipiga simu na alimpigia nani. Akawaambia ndio nilipiga simu na sijui nilimpigia nani kwasababu Mungu ndiye aliyenipa ile namba.

Kumbe ile namba ilikuwa ni ya raisi wa nchi hiyo. Wakajaribu kumtishia akawaambia mimi ni mjumbe wa Mungu, sichukui vitisho kutoka kwa mtu yeyote.

Akawapa ujumbe wa pili kwamba wamfikishie raisi kwamba ile huduma ya winners (inayoongozwa na askofu Oyedepo) ni huduma inayomilikiwa na Mungu mwenyewe. Raisi ikabidi aunde tume maalumu kuchunguza lile tukio la kuwanyang'anya jengo lao.

Kamati ikafikia muafaka na lile jengo likarudishwa na wakaendelea kulitumia. Jamaa ambaye alikuwa mbele kupigania hilo jengo na akahamia hapo baada ya winners kunyang'anywa alifariki ghafla.

Sasa wale ambao mnampigania Mungu wenu badala ya yeye kuwapigania mnakaribishwa katika wokovu wa Yesu Kristo, Yehova, Yahweh, Mungu aliyehai.
 
Back
Top Bottom