Simu ya Hawa Ghasia yatumia Sh. 25 milioni

Simu ya Hawa Ghasia yatumia Sh. 25 milioni

Hata kama angeongea masaa yote 24 sidhani kama itafikia pesa hiyo?

Na sidhani kama naweza kuongea masaa 24...

Huu ni uzushi
 
Teh Teh uongo mbaya sana.
Hii TIN number ni Ya Airtel au Hawa GHASIA?
"Ghasia anatumia namba ya mlipa kodi
(TIN) TIN: 100-961.520.
"
 
Huu ni uongo na umbeya wa Kibavicha/ Chadema kutoka MF on line...huihitaji akili nyingi kubaini kuwa habari hii ni ya uongo...! Nitamshangaa mtu mwenye utimamu wa akili kama atasoma habari hiyo yote na kuamini ni ya kweli.
Huu ni uongo mtupu.
Huu uwongo unaelekea umeletwa na mumeo ambaye ni muongo kupindukia
 
Naona udaku wa Ngosha wa Mwana.halisi forum umehamia JF
 
Mtwara mjini?
Kumbuka alivyozomewa kwenye mkutano pale Soko Kuu alipokuwa na akina Kinana, Nape, Mkuchika na Chiza mpaka akasema "hata mkizomea mimi watu wangu ni Mtwara vijijini".

Mission yake ni Mtwara mjini.. Nasikia majuzi hapa alikuwa anataka ahonge bodaboda kwa madereva bodaboda wakamtoa mbio.. Sasa jiulize hizo bodaboda kwanini asipeleke vijijini??
 
KUNA mchwa ndani ya Serikali ya Rais Jakaya Kikwete. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Abdulrahman Ghasia (49), ni miongoni mwa wanaotafuna fedha za umma serikalini, mithili ya mchwa.


Anaripoti Mwandishi Maalum … (endelea).Katika kipindi kisichozidi siku 52, Ghasia ametumia kiasi cha Sh. 25.8 milioni kwa matumizi yake ya simu ya mkononi, tena kupitia kampuni moja ya Airtel.
Taarifa hizi za waziri kutumia kiasi cha Sh. 25.8 milioni kwa matumizi ya simu moja ya mkononi, ndani ya muda usiofikia miezi miwili, zinafichuka katika kipindi ambacho serikali imekuwa ikitumia nguvu kukusanya michango kutoka kwa wananchi.
Michango mingi ambayo serikali imekuwa ikikusanya, ni ile ya maabara kwenye shule za kata, madawati, ununuzi wa vitabu, madaftari na ujenzi wa nyumba za walimu na madarasa.
Taarifa zinasema, katika maeneo mengi, maagizo ya serikali, yaliambatana na vitisho, huku baadhi ya walioshindwa kutoa michango hiyo wakifikishwa mahakamani na kufungwa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya serikali na kampuni ya Aitel Tanzania Limited, waziri Ghasia ametumia mamilioni hayo ya shilingi kwa mawasiliano kati ya tarehe 1 Februari na 21 Machi mwaka huu.
“Kuna mambo ya ajabu sana ndani ya serikali hii. Taifa masikini kama hili, kuna viongozi wanaotumia kiasi cha Sh. 25 milioni kwa simu. Kwa kweli, umasikini tulionao ni wa kujitakia,” ameeleza Juma Said, mkaazi wa Kinondoni na mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii.

Nyaraka (Invoice) kutoka Aitel inamuonyesha Ghasia alipewa ankara ya malipo ya tarehe 1 Februri 2015, yenye Na.29906000001374, ikielekeza serikali – Tamisemi – kulipa kwa kampuni hiyo, jumla ya Sh. 25,878,335.86.

Kwa mujibu wa nyaraka hizo, Ghasia amejitambulisha kuwa ni waziri wa Tamisemi. Anatumia anuani ya S.L.P 23, jijini Dar es Salaam; huku namba ya mteja – Customer Id– ikitajwa kuwa 1219937034.
Ghasia anatumia namba ya mlipa kodi (TIN)TIN:100-961.520..

-----------Online linaweza kuripoti kuwa kila mwaka serikali inatumia mabilioni ya shilingi kwa njia za anasa, ikiwamo malipo ya simu, usafiri, nguo na fenicha za ndani, badala ya fedha hizo kuwekezwa kwenye maendeleo.
 
huyu mama si ndiyo wizara yake inahusika na Ajira za walimu huuyu? Hiyo pesa kama ni kweli si ingekua posho ya walimu wapya hata 20 hapo? Ndio maana ajira hakuna kama mawaziri wa wizara tu wana matumizi mabaya hivooo.

Ni vyema kabla ya kutoa comments za kumhukumu mtu, ufanye uchunguzi wa kina. Hii habari bila shaka ni ya kizushi,,toa uhalisia wa jambo na msijekukuta hakuna ukweli ndani yake,, eti ni bill ya siku 52, mna uhakika??????
Do the research,before coming to the conclusion.
Mtahaibika bure na uzushi wenu
 
ndio maana wameletea hii sheria ili masuala kama hayo yasijadiliwe hapa JF.
 
Jee, zimelipwa au ni Invoice iliyoletwa kimakosa? maana haiingii akilini.

Sitoshutumu mpaka nisikie 2nd and 3rd party (Airtel na Hawa Ghasia) wakitoa ufafanuzi.

Ni wale Wale, Serikali Inayoongozwa na Watu wetu.
 
Air tell kwa kubambikaaa bill...sometimes kwa kutojua kuna vitu kwenye simu Kama GPS etc usipo disable ....simu inakuwa charged full time na ukiwa roaming Ndio balaaaa ..........,Mimi pia ni Kati ya wateja wa post paid ambao taasisi yangu ...Ina mzozo wa bill .....,hizi Internet bundle Wakati tunapata kwa 30'000 kwa Mwezi Pre paid ....post paid wana kuchanga kwa dakika .....tena na hizi automatic downloads Tulizo subscribe ni balaa tena ....ni wizi mtupu.
Nadhani WANABAKI na wateja Kama Hao ambao bill ikija hakuna mwenye uchungu wa kuhoji Inalipwa tu ......Wakati ANAYETUMIa hapati value for money ...kwa dunia ya Sasa ....hata bill gate Hatakiwi kutumia Kiasi hicho Wakati free calls options kibao

Hiyo bill inawezekana kabisa, ukiweka data roaming , uakawa na data na ukasafiri na kupiga simu mradi unaona inapatikana inakula kwako, kuna jamaa alikwenda India akiwa mgonjwa, akaendelea kujipigia simu, internet kila kitu. ikaja bill millioni kumi na tatu.

Walimfuta kazi na kuuza gari yake Escudo.

lakini huwa kuna onyo either kwa contact person wu mwenye simu inapofika kiwango fulani ambacho wao Airtel wataona ni abnormal, lakini kwa mawaziri wetu inawezekana alisema hamna taabu nitalipa.

Kwa serikali makini, hii lazima alipe mwenyewe.
 
Unajuwa Kiingereza gaidi ni terrorist, sasa kama kuna polisi halafu awe hawezi kum terrorize mwizi huyo atakuwa si Polisi.

Waislam ni makhalifa hapa duniani, mkituona mnatuogopa "we terrorize you", hivyo ndivyo anatakiwa khalifa awe. Lazima umuogope.

terrorize,synonyms-persecute, victimize, torment, harass, tyrannize, intimidate, menace, threaten,bully, browbeat; scare, frighten, terrify, petrify




Try to replace the bolded green word with the bolded red words/terms....Do you really mean it or taken out of context?
Do Muslims harass/victimize/torment/persecute/bully etc?
 
Dada angu hilo ndo linatumaliza...........hata wanaotukata makoromeo Bukoba wamekutwa na visu vikali vina damu...na wakataka kukimbia wakapigwa risasi...kwa hiyo utataka mtuhumiwa akwambie kuwa ni damu ya kuku au binadamu?

Tazama post #95
 
Back
Top Bottom