Sikutarajia kuumizwa namna hii!

Sikutarajia kuumizwa namna hii!

Anatafuta pa kujipoozea naye asahau machungu.

Mwache apambane na hali yake kama ambavyo wewe ulipambana na hali yako
 
Km asingetoswa huko wala usingemuona anarudi.
Huyo amekuja kwako sabb ametoswa huko na hana pa kukimbilia kwahiyo amekuja ili ajiponye then aendelee na safari yake.
Ukimkubalia huyo utakuja kulia sana zaid ya mwanzo
 
nasemaga kila siku dini sio ishu kwa wanopendana ! sijui kwann watu wanchukuliankmkigezo kikubwa namna hyo! huyu idada hakumpenda jamaa! kwanza jamaa ana moyo sana ht wa kukubali kumskiliza!.. wengne tungekuwa [HASHTAG]#mkono[/HASHTAG] wa mara sasa hv

Kuamini Mungu ni vyema. Ila kuanzisha mahusiano na mtu wa dini tofauti eti unampenda lakini hauko tayari kubadili dini Ni ujinga wa kiwango cha Airport kwani tangu mwanzo ulijua si ungeacha! Watu bahna
 
Huwa siamnini kama kuna wanaume wenzangu wanaumia kwa kiasi icho, eti kisa mapenzi hah hah ha labda mi sina chemba ya kupenda
 
Nahisi anapenda maumivu huyu jamaa, na atayapata.

Mimi nikigundua mwanamke ninaetaka kumwoa ana boyfriend nampiga chini. Jamaa dhaifu sana inakuwaje mwanaume unalilia penzi la mwanamke
hahaaaa muazme huo moyo wako mleta mada.
 
Nilikuwa na mpenzi ambaye tulikuwa tunapendana sana. Nilikutana nae jijini mwanza nilipokwenda kikazi July 2015.

Tukiwa tumukubalia kufunga ndoa hapo baadae. Tulifanya mambo mengi pamoja ikiwa kujenga nyumba na kununua gari pamoja, pia niliweza kufanikiwa kumuhamishia mor kikazi angalau awe karibu.

Hali ile ilinichukua miezi saba ndipo niliporudi normal.
Baadae Mungu akajalia nikapata kazi sehemu nyingine.

Baada ya mwaka mmoja kupita akaanza kunitafuta nakuomba turudiane maana jamaa amemtosa na kuoa mwanamke mwngine.

Hebu kwanza hii stori mbona kama timeline yake haijakaa sawa...

Umekutana na kujuana na mwanamke mwaka 2015 mwezi wa saba ( hii ina maana hadi leo ni takribani miaka 2 kamili)...

Leo hii unasema ni takribani mwaka mmoja umepita tangu muachane, binti ameanza kukutafuta ( Hii ina maana mliachana kama mwaka 2016 mwezi wa sita hadi wa nane hivi)...

Hadi hapo inaonesha mlikuwa katika mahusiano kwa kipindi cha mwaka mmoja tu pekee...

Sasa kweli ndani ya mwaka mmoja mmejenga nyumba, mkanunua gari, mkatambulishana kwa wazazi, mkahamishana kazi na zaidi mipango ya ndoa...really???? Ndani ya mwaka mmoja???
 
Ha ha ha ha ....story yako naipenda....kwa kweli hili suala la dini tofauti linatutesa wengi mnoooo ila ndo hvyo hakuna namna..............
Mkuu ipime nafsi yako tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unakuta hapo una gf mpya bado unawaza kwa huo msala ulishakuacha solemba
Hivi kweli wewe mwanaume unatumia akili hii ya kawaida au matope
 
Huyo hana ubinadamu kabisa,usimkubalie maana atakuja kuku umiza zaidi ya hapo,tafuta mwanamke mwingine
 
Naamini mko poa.
Niende kwenye mada moja kwa moja.

Nilikuwa na mpenzi ambaye tulikuwa tunapendana sana. Nilikutana nae jijini Mwanza nilipokwenda kikazi July 2015.
Safari yetu ya mapenzi ilipamba moto kila mmoja akiwa na mapenzi ya dhati kwa mwenzio.

Tukiwa tumekubaliana kufunga ndoa hapo baadae. Tulifanya mambo mengi pamoja ikiwa kujenga nyumba na kununua gari pamoja, pia niliweza kufanikiwa kumuhamishia Moro kikazi angalau awe karibu.

Hatukuwa wa imani moja, yeye alikuwa mkristo na mimi muislam lkn hili halikuwa tatizo la kutuzuia kupendana.

Tulitembeleana na kuwasiliana Mara kwa Mara bila kikwazo.
Baada ya kumwambia kuwa wakati umefika tuanze taratibu za kufunga ndoa tulikubaliana kuwa ndoa tutafungia serikalini lkn kila mtu atabaki na imani yake.

Alipowaeleza wazazi wake utofauti wa imani wazazi walilipinga kwa nguvu zote, nikamuuliza yeye mwenyewe anasemaje akajibu ananipenda na asingetamani tuachane lkn pia hawezi kufanya kinyume na wazazi wake.

Basi wakati tunaendelea kulitafakari hilo mwenzangu akabadilika, nikimpigia simu anakata meseji hajibu, baadae akaniblock kabsa.

Kitendo kile kiliniumiza sana, nikaamua kumfuata Moro nikakuta alipokuwa anaishi amehama, kwasababu nilikuwa najua shule aliyokuwa anafundisha nikaamua kumfuata shuleni.

Nilipofika shuleni sikuamini kile nilichojimbiwa...niliumia sana..nikamsihi na kumpigia magoti mbele ya walimu wenzie lakini yeye akanijibu hatoweza kuendelea na mimi tena kwani tofauti za dini hazivumiliki , pia kaendelea kusema kuwa alikuwa na mpenzi wake zamani walipotezana lakini wamekutana tena na kuamua kurudiana.

Maneno yale yalikuwa ni mkuki ndani ya moyo wangu, nillilia kama mtoto, sikuweza kula kwa siku kadhaa.

Nikaamua kujiua maana nilijisemea moyoni sitaweza kumuona mwanamke ninampenda akiolewa na mwanaume mwngine. Lkn nilikuwa nao wakanisihi nisifanye vile. Sikujua nini cha kufanya nilikuwa mtu wa kulia tu.

Sikwenda kazini kwa siku mbili mpaka rafiki yangu ambaye tunafanya nae kazi alipofanya kazi ya ziada.

Baada ya mwezi kupita nilifunga safari tena kumfuata nikiwa na lengo la kutaka kujua kuhusu gari na nyumba ambavyo tulinunua pamoja na vyote vilibaki kwangu.

Alichonijibu nikwamba vyote ameniachia kwasababu alichonitendea anajua kiliniumiza sana. Nikwamwambia achukue gari mimi nimeshapona na sina amani kumiliki Mali ambazo tulichuma pamoja akakubali nikamuachia gari .

Utendaji wangu wa kazi ukawa mbovu sana maana kila nilipokumbuka sikuweza kufanya chochote. Nilikuwa nafanya kazi kwenye NGO ya wa Marekani, kufuatia kuwa na ufanisi mbovu kazini nilisitishiwa mkataba wa kazi.

Mapenzi yanauma sana jamani usiombe ukimpenda mtu halafu akakuzingua.
Hapo ndipo shida ikazidi kuwa kubwa maana sikuwa na cha kunikeep busy ikafika wakati nikawa napoteza mpaka fahamu.

Wazazi walipofahamu shida yangu wakanitumia mtu wa kuwa nae maana nilikuwa naishi peke yangu. Hali ile ilinichukua miezi saba ndipo niliporudi normal. Baadae Mungu akajalia nikapata kazi sehemu nyingine.

Maisha yakaendelea tatizo ikawa ni ile nyumba kila nikiona namkumbuka , nikaamua kuiuza na kujenga sehemu nyingine. Maisha yakaendelea nikamtoa moyoni kabisa nikawa namuona wa kawaida sana. Baada ya mwaka mmoja kupita akaanza kunitafuta nakuomba turudiane maana jamaa amemtosa na kuoa mwanamke mwngine.

Nimemkatalia mara kadhaa lkn bado ananing'ang'ania , kila nikitaka kumkubalia nakumbuka mateso niliyopata kwasababu yake.

Naomba ushauri wenu wakuu nipo njia panda sitaki kuumia tena.
Bwana Majaliwa pole sana!hii binafsi imenigusa mno!kabla sijatoa sababu zangu/yangu ya uzoefu,'ACHANA NAE KABISA'Mshukuru Mungu umeweza kurudi kwenye mfumo wa maisha.Endelea na maisha yako na Mungu kakuwekea mke wako maalum atakae kukupa dunia unayotaka.
KISA CHANGU.Kwa ufupi sana.Nilimpata girlfriend mwislamu na mimi ni mkristo(mchanyiko wa mwarabu na borana .uta imagine kilichozaliwa hapo) miaka 2000 nikisoma Nairobi.Tukagombana na kuachana kwa muda wa miezi sita hivi.kwa namna nilivyompenda sikuwa na haja na girl mwingine.Baada ya hapo nadhani alijua kuwa kanikosea,akaamua kuja kuomba msamaha.Kwa namna nilivyompenda nilmfuta tu mchozi aliyotoa nikaendelea na mahusiano kama zuzu.Alinisihi sana nibadili dini ili asitengwe na familia yake kwa kuolewa na mkristo lkn nilgoma.Nilipo maliza college mwaka 2002 nikaamua kurudi nyumbani kupamambana na maisha ili nikamlete kuja kumtambulisha nyumbani afu tuendelee na mipango ya maisha.Nilikaa kama mwaka hivi tukiendelea na mawasiliano tu vizuri ila nlikua nakimbia mara chache kumuona.
Siku nilifunga safari rasmi kwenda Nairobi kumchukua kumleta Tz.Bahati nzuri nilifika na kesho yake nikafika kwao na kumkuta tena akiwa anashuka ghorfani kwenda mishe zake.Alistuka sana kuniona.Cha kushangaza hakutaka tuingie nyumbani.Ila kwa sababu alijua kusudio la safari yangu niliamweleza tu kuwa sasa niko tayari kumchukua kuja Tz.Alini jibu in short 'THAT IS AN IMPOSIBLE MISION'Mwanaume niliumia kushinda lkn sikutaka kuremba pamoja na mapenzi yote niliyokua nayo kwake nilienda strait kupanda gari na kuja zangu Arusha.Tangu hapo hadi sasa sijawahi kumwona tena ingawa nimeenda Nairobi mara kadhaa.Sasa nina familia yangu na nina furaha ya kutosha.Ingawa sijawahi kumsahau!
 
Forgiving those who hurts you is like giving them an extra weapon coz they missed you at first

Hiyo ndo kanuni yangu Ya maisha ya mahusiano, akiniumiza sisamehi kamwe

Jiulize Kama asingeachwa huko angekukumbuka?

My dear wanawake Wapo wengi tafuta mwingine, utofaut wa mwanamke na mwanaume ukiachilia jinsia ni MSIMAMO sasa jiendekeze, atakupelekesha ka gari bovu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Forgiving those who hurts you is like giving them an extra weapon coz they missed you at first

Hiyo ndo kanuni yangu Ya maisha ya mahusiano, akiniumiza sisamehi kamwe

Jiulize Kama asingeachwa huko angekukumbuka?

My dear wanawake Wapo wengi tafuta mwingine, utofaut wa mwanamke na mwanaume ukiachilia jinsia ni MSIMAMO sasa jiendekeze, atakupelekesha ka gari bovu

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu jamaa ni poyoyo la mwaka
 
Ndoa ni jambo LA kidini usifunge ndoa serkalini.Ukipenda penda kiasi na ukimchukia MTU iwe kiasi.Ukigombana na umpendae kupita kiasi utaumia sana pia unaweza kupatana na unaemchukia kama ikiwa chuki kupita kiasi mapatano yatapitia wkt mgumu.Lakini chuki ikiwa kiasi mapatano yanawezekana.Huyo hakufai kwa sababu tatizo LA dini mmeshindwa kulitatua.Chunga asiingie dini kufuata ndoa Bali awe na nia ya kuishi na imani yako.Wewe ndio kiongozi yeye aje kwako ukimfuata utakuwa umetuangusha wanaume wote duniani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom