Sikutarajia kuumizwa namna hii!

Sikutarajia kuumizwa namna hii!

We make mistakes in order to learn KWANZA KUFANYA KOSA SI KOSA BALI NI DARASA TOSHA KWA KUKUFUNDISHA USIRUDIE TENA naona hujajifunza kupitia hilo kosa na uzuri wa maisha we live under LAW OF KARMA AS "WHAT GOES AROUND COMES AROUND" pigo ama anguko la pili ni kubwa kuliko la kwanza fanya integration kama alikuacha kwa mara ya kwanza na ukatumia miezi saba kumsahau kuna hati hati ukatumia miaka miwil ama mwaka na nusu kumsahau kitu ambacho kingekuwa potential kufanya yale ya maendeleo ktk maisha yako, cha kukushauri songa mbele bwana mkubwa angalia maisha na future yako tambua wakati mwngne tunakutanishwa na tuwapendao sio kwamba wote tuwaoe ama tutawaoa bali wengine ni darasa ktk maisha yetu ili tujue makosa na kuwa makini nayo THAT WAS THE LESSON AND CLASSROOM TO YOU, GOING BACK IS AS SIMILAR AS REPEATING THE CLASS WHICH IS A SETBACK TO YOU SO LONG AS UMESHA GRADUATE FROM THE LESSON

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa Ndugu Majaliwa, unataka ushauri wa namna gani?? Kama mlifikia hatua ya kuchuma Mali pamoja, still akakuacha na kurudiana na mpenzi wake wa zamani, hakujali maumivu yako, wala ulivyojitoa kwake. Kweli Unaomba ushauri??? Au unataka tukutusi tuonekane hatuna busara?? Sikiliza moyo wako tu.
Si bure huyo kaka amerogwa tusiana naye sasa hivi lazima ujinyonge maumivu atakayokupa ni mara mbili ya mwanzo jitambue wewe kimbia huyo ni kama jini shauri yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya mapenzi ni ya mwendo kasi! Hata miaka miwili kupita mmependana, mmejenga nyumba, mmenunua gari,

uhamisho wa ualimu umefanikiwa, umepoteza kazi, umepona mapenzi miezi baada ya mmiezi saba, umeuza nyumba na kujenga nyingine katika kipindi cha mwaka mmoja, mmpenzii katoswa anataka mmrudiane...

Duh! hapa kwa mtiririko wa matukio haya lazima uchanganyikiwe tu... Ila hii stori ...ngoja ninyamaze tu
Labda kama nyumba alikuwa ananunua siyo kujenga, hata hivyo kwa muda huo hata hawakujuana vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkubalie kwa moyo mmoja na muanze kuishi maisha mapya.Muonyeshe unampenda zaidi ya mwanzoni.Hakikisha unampenda na kumuonyesha kuwa unamjali sana na yeye ndo kila kitu katika maisha yako.Hata ikibidi pangeni tarehe ya harusi haraka iwezekanavyo.Wakati maandalizi ya ndoa yakiendelea,tafuta kipindi hayuko ameenda safari uza kila kitu na uhame kabisa eneo.Then badilisha number zote za simu na uanze maisha mapya.

Tit for Tat is a fair game.
Ushauri mzuri lakini alivyo boya hawezi kufanya hayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikiliza moyo wako, watu hujifunza kutokana na makosa. Yawezekana kajifunza na akawa mke bora sana kwako.
 
Haya mapenzi ni ya mwendo kasi! Hata miaka miwili kupita mmependana, mmejenga nyumba, mmenunua gari,

uhamisho wa ualimu umefanikiwa, umepoteza kazi, umepona mapenzi miezi baada ya mmiezi saba, umeuza nyumba na kujenga nyingine katika kipindi cha mwaka mmoja, mmpenzii katoswa anataka mmrudiane...

Duh! hapa kwa mtiririko wa matukio haya lazima uchanganyikiwe tu... Ila hii stori ...ngoja ninyamaze tu
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
wakikubaliana kurudiana na yule mwenzake katika dini,maana that happened earlier kulingana na maelezo yako, pse b careful usije kurudi hapa na stori hii
 
Ukiona mtu unaanza kujiuliza/ kumuwaza mara mbili mbili basi bado unampenda...
Fuata moyo wako ila jifunze kutokana na makosa...

Mahondaw wa Smart911
Anatakiwa aangalie yaliyomkuta.
Huyo mwanamke akipata wa dini yake tena atamtosa jamaa.

Why alishindwa kumsaidia kipindi akiwa na shida ya upendo ? Je bila muoaji kumtosa angekurudi kwa jamaa?

Mi nashauri aendelee na maisha yake atampata mwingine tena mwenye mapenzi ya dhati na imara nae atamuona bora kuliko huyu aliyebwagwa ndo akarudi.
 
Naamini mko poa.
Niende kwenye mada moja kwa moja.

Nilikuwa na mpenzi ambaye tulikuwa tunapendana sana. Nilikutana nae jijini Mwanza nilipokwenda kikazi July 2015.
Safari yetu ya mapenzi ilipamba moto kila mmoja akiwa na mapenzi ya dhati kwa mwenzio.

Tukiwa tumekubaliana kufunga ndoa hapo baadae. Tulifanya mambo mengi pamoja ikiwa kujenga nyumba na kununua gari pamoja, pia niliweza kufanikiwa kumuhamishia Moro kikazi angalau awe karibu.

Hatukuwa wa imani moja, yeye alikuwa mkristo na mimi muislam lkn hili halikuwa tatizo la kutuzuia kupendana.

Tulitembeleana na kuwasiliana Mara kwa Mara bila kikwazo.
Baada ya kumwambia kuwa wakati umefika tuanze taratibu za kufunga ndoa tulikubaliana kuwa ndoa tutafungia serikalini lkn kila mtu atabaki na imani yake.

Alipowaeleza wazazi wake utofauti wa imani wazazi walilipinga kwa nguvu zote, nikamuuliza yeye mwenyewe anasemaje akajibu ananipenda na asingetamani tuachane lkn pia hawezi kufanya kinyume na wazazi wake.

Basi wakati tunaendelea kulitafakari hilo mwenzangu akabadilika, nikimpigia simu anakata meseji hajibu, baadae akaniblock kabsa.

Kitendo kile kiliniumiza sana, nikaamua kumfuata Moro nikakuta alipokuwa anaishi amehama, kwasababu nilikuwa najua shule aliyokuwa anafundisha nikaamua kumfuata shuleni.

Nilipofika shuleni sikuamini kile nilichojimbiwa...niliumia sana..nikamsihi na kumpigia magoti mbele ya walimu wenzie lakini yeye akanijibu hatoweza kuendelea na mimi tena kwani tofauti za dini hazivumiliki , pia kaendelea kusema kuwa alikuwa na mpenzi wake zamani walipotezana lakini wamekutana tena na kuamua kurudiana.

Maneno yale yalikuwa ni mkuki ndani ya moyo wangu, nillilia kama mtoto, sikuweza kula kwa siku kadhaa.

Nikaamua kujiua maana nilijisemea moyoni sitaweza kumuona mwanamke ninampenda akiolewa na mwanaume mwngine. Lkn nilikuwa nao wakanisihi nisifanye vile. Sikujua nini cha kufanya nilikuwa mtu wa kulia tu.

Sikwenda kazini kwa siku mbili mpaka rafiki yangu ambaye tunafanya nae kazi alipofanya kazi ya ziada.

Baada ya mwezi kupita nilifunga safari tena kumfuata nikiwa na lengo la kutaka kujua kuhusu gari na nyumba ambavyo tulinunua pamoja na vyote vilibaki kwangu.

Alichonijibu nikwamba vyote ameniachia kwasababu alichonitendea anajua kiliniumiza sana. Nikwamwambia achukue gari mimi nimeshapona na sina amani kumiliki Mali ambazo tulichuma pamoja akakubali nikamuachia gari .

Utendaji wangu wa kazi ukawa mbovu sana maana kila nilipokumbuka sikuweza kufanya chochote. Nilikuwa nafanya kazi kwenye NGO ya wa Marekani, kufuatia kuwa na ufanisi mbovu kazini nilisitishiwa mkataba wa kazi.

Mapenzi yanauma sana jamani usiombe ukimpenda mtu halafu akakuzingua.
Hapo ndipo shida ikazidi kuwa kubwa maana sikuwa na cha kunikeep busy ikafika wakati nikawa napoteza mpaka fahamu.

Wazazi walipofahamu shida yangu wakanitumia mtu wa kuwa nae maana nilikuwa naishi peke yangu. Hali ile ilinichukua miezi saba ndipo niliporudi normal. Baadae Mungu akajalia nikapata kazi sehemu nyingine.

Maisha yakaendelea tatizo ikawa ni ile nyumba kila nikiona namkumbuka , nikaamua kuiuza na kujenga sehemu nyingine. Maisha yakaendelea nikamtoa moyoni kabisa nikawa namuona wa kawaida sana. Baada ya mwaka mmoja kupita akaanza kunitafuta nakuomba turudiane maana jamaa amemtosa na kuoa mwanamke mwngine.

Nimemkatalia mara kadhaa lkn bado ananing'ang'ania , kila nikitaka kumkubalia nakumbuka mateso niliyopata kwasababu yake.

Naomba ushauri wenu wakuu nipo njia panda sitaki kuumia tena.
Yani
Mi ningemwambia kama umekubali twende kwanza kwa wazazi pande zote mbili tutafute mariadhiano na wakiridhia ndoa ifungwe mara moja

Na hii ni kama unampenda kweli na uangalie vizuri approach aliyorudi nayo usikute amekuja mapumzikonj maana kumbuka hata wakt mnaachana alikuambia anamrudia bf wake wa zamani.

Mungu ameshakuonyesha nazi mbovu wewe bado unaing'ang'ania jiongeze wanawake ni wengi kuliko wanaume duniani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom