Sikujua, kumbe Bakhresa anakopa mikopo ya riba kwenye benki za biashara

Mkuu vyote ubepari na ujamaa ni unyonyaji ila katika namna tofauti, ubepari ni unyonyaji katika sekta ya uchumi na ujamaa ni unyonyaji katika sekta ya jamii, ujamaa ni unyonyaji kwa sababu kuna watu ambao hawafanyi kazi sababu wanajua watasaidiwa na ndugu, jamaa, wazazi au watoto

Yani watu wanaishi kwa ule msemo wa "maisha kusaidiana leo kwangu kesho kwako", mwisho wa siku unakuta wanaojitoa ni baadhi huku wengine wakipokea tu kwa kigezo cha kwamba ipo siku mambo yatabadilika, kwamba hao watoaji watakuwa wapokeaji na wapokeaji watakuwa watoaji (ambapo hiyo siku inaweza isifike kabisa)

Na huo ndio unyonyaji mbaya na unaoumiza kuliko ule wa kibepari kwa sababu ubepari ni all about survival for the fittest, ukiwa mjanja unatoboa ukiwa mzembe ndio basi tena huwezi kumlaumu mtu kwa kushindwa kutumia akili yako mwenyewe, ndio maana kuna tajiri alisema "kuzaliwa masikini siyo kosa lako ila kufa masikini ni ujinga wako"
 
Sio uelewa wangu bali huo ndio ufahamu wako na wenzio
Wewe ndio upeo wako wa kufikiri ulipoishia watu wanaongelea uislam unachosema kuhusu mikopo kwa riba wewe unaongelea habari za utajiri, mara mbona watu wanakopa mikopo kwa riba na bado ni masikini, aliyekuambia kwamba kukopa tu mikopo kwa riba ndio kuwa tajiri nani
 
Nilidhani ustadhi ni wale watu wa dini wasiojihusisha na riba kumbe ni mdau mzuri wa benki za biashara.

Ninapenda Bakhresa afanye kuwaelimisha wale wenye misimamo mikali tuwe na taifa endelevu.
Kwani hiyo inaitwa mikopo ya kiislaam unafikiri hakuna riba? Ni namna tu ya kuilipa wanabadili halafu wanaita eti mikopo ya kiislaam. Hebu fikiri benki gani itaweza kufanya kazi bila ya faida. Faida ndio msingi wa uwepo biashara yoyote. Na hakuna mantiki eti benki za kiislaam zipewe ruzuku. ..zipewe na na nani.. Labda na mungu🤣🤣. Tumeona serikali huweza kutoa ruzuku kwa biashara za shirika fulani nia ikiwa ni kutoza bei ndogo ili huduma iwafikie wananchi lakini kampuni binafsi isiporejesha gharama zake itaishia kufa.
 
Nilidhani ustadhi ni wale watu wa dini wasiojihusisha na riba kumbe ni mdau mzuri wa benki za biashara.

Ninapenda Bakhresa afanye kuwaelimisha wale wenye misimamo mikali tuwe na taifa endelevu.
Wewe hujaelewa kuwa benki wana facility au banking instruments nyingi kuwezesha biashara ambazo hazihusiani na mikopo ya riba.
Pili binaadamu hajaumbwa kamili anaerza kuterereka mahali.
Wewe umekalia kutafuta kasoro badala ya kutafuta kama yeye. Hiyo hapo benki nenda na wewe kama unadhani benki pekee ndio inaleta mafanikio ya biashara.
 
Hivi hata umesoma nilichoandika. Comprehension ni janga la Taifa.
Bila shaka wewe ndio hujaelewa kilichoandikwa usisingizie comprehension, wewe ndio umeshindwa kucomprehend umeamua kutunga hoja yako nyingine, kinachoongelewa hapo ni uislam na riba sasa niambie quran inasemaje kuhusu riba
 
Bila shaka wewe ndio hujaelewa kilichoandikwa usisingizie comprehension, wewe ndio umeshindwa kucomprehend umeamua kutunga hoja yako nyingine, kinachoongelewa hapo ni uislam na riba sasa niambie quran inasemaje kuhusu riba
Wewe umesema huwezi kukwepa riba za mabeberu, mimi nimekujibu bank za kiisilamu zipo very successful dunia nzima, hata ukienda nchi za Magharibi zipo, hebu niambie hio comment yangu na ulichonijibu vinahusiana nini. Nasubiria.
 
Watu wanakosoa dini kama wanavyokosoa ujinga mwingine uliopo kwenye jamii, kwani watu wa dini ni kina nani hadi wasikosolewe wewe ndio uache kusikiliza wakosoaji, komaa kushikilia dini yako kwa sababu watu hawataacha kukosoa hadi mwisho wa dahari
Hapa imekosolewa dini kwa vp? Mie nimeona wamesemwa Masheikh mara Bakhresa.
 
Nilichogundua bakhressa anawakosesha raha sana baadhi ya watu , dunia hii ya ajabu unaacha kufikiria mustakabali wako na familia yako unamuwaza bilionea ambae sasahivi level yake he feels sorry about the poor mtu analisha africa nzima wewe upo ileje huko unaleta umbea
Usikute hujasoma hata mada.
Kwa muhtasari: Mfia dini Said Bakresa analipa riba kwenye business. Ila mashekhee wanatuambia kukopa ni dhambi.
 
Back
Top Bottom