Sikujua kama kombe la dunia linaanza leo!

Sikujua kama kombe la dunia linaanza leo!

Hakika umetumia AI
Ni mawazo yako.
Hayo niliyo andika ni moja ya kumbukumbu zangu nzuri sana.
Kabla ya hilo kombe baba alikuwa na ukaribu sana na ubalozi wa ufaransa na alisoma hapo alliance de France kama sijakosea
Alipatta marafiki na tuliletewa tv na yeye kununua dish la DStv sasa kile kiwewe cha kujua kifaransa ilitulazimu tumfuate yeye
Hicho kikosi alikuwa shabiki na mpaka picha ya hao wachezaji mwaka 98 ipo na nimeitunza kama kumbukumbu.
Si ya kutoa mtandaoni Bali baba alipiga kupitia camera yake kwenye tv. Nikipata muda ntaweka.

Wengine tukikutana na jambo lenye kumbukumbu hisia zinapanda na kukumbuka mengi zaidi..
 
Katika michuano ambayo sipo interested nayo siku hizi ni world cup, mara ya mwisho kufuatilia ile yenyewe ni 2010, baada ya hapo hata sina mzuqa.

EPL na UCL kwa sasa ndio nafuatlia, napo sianglii, nimepoteza interest kuangalia mpira. Kweli uzee ni dawa!
 
Marahaba. Za huko Tanzania?
Nakaribia kuvuka mpaka wa tanzanzania ika kwa sasa Tanzania pako okay
Screenshot_20260611-225328_Google Earth.jpg
 
Katika michuano ambayo sipo interested nayo siku hizi ni world cup, mara ya mwisho kufuatilia ile yenyewe ni 2012, baada ya hapo hata sina mzuqa.

EPL na UCL kwa sasa ndio nafuatlia, napo sianglii, nimepoteza interest kuangalia mpira. Kweli uzee ni dawa!
2010 babu
 
😁😁😁
Nasikia bush mlikuwaga mnaletewa movie zile za ukimwi,,, ikifika saa tatu watoto wanafukuzwa mnaanza kuwekewa mauno ya yondo sister.
🤣🤣 Kabisaa. Nakumbuka wakati niko shule ya msingi kuna huyo baba alikuwa anatuwekea siku za sikukuu kiingilio 50 kijiji kizima mnajazana humo. Usiku wanafunzi hawaruhusiwi ukijitoa ufahamu ukaingia usiku shuleni kinakulamba
 
Nakumbuka zile sticker za big G (jojo) za wachezaji wa Brazil tulitamba nazo sana kwa kuzibandika kwenye madaftari, wengine maghetoni, hahahahha!

Ronaldo
Ronaldinho
Roberto Carlos
Dida
Gilberto
Na yale madaftari ya kina kaka unayakumbuka?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom