MAREKANI: Urusi imefungiwa na Marekani kucheza Kombe la Dunia?

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
17,290
Reaction score
26,766
Kama USA imemrudisha refa wa Somalia, basi ile ni isue ndogo sana kwa Marekani, hili la Urusi Gen Z na millenia hamjui.

Urusi haishiriki Kombe la Dunia la 2026 kwa sababu FIFA iliweka kizuizi rasmi kinachozuia timu hiyo kushiriki katika mashindano yake yote tangu mwezi Februari 2022.

Hali hii ilitokana na uvamizi wa kijeshi wa nchi hiyo nchini Ukraine, ambao ulisababisha mashirikisho ya soka duniani kuitenga nchi hiyo kisiasa na kimichezo.

Kwa adhabu hiyo, timu ya taifa ya Urusi haikuruhusiwa kushiriki kwenye mechi za mchujo (qualifiers) za kuwania nafasi za kufuzu fainali hizi za 2026 zinazoandaliwa na nchi za Marekani, Mexico, na Canada.

Pia, Soma:
Hivi sasa (2026), hakuna wachezaji kutoka nchi ya Urusi wanaocheza kwenye Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) wala Ligi Kuu ya Hispania (La Liga). Kutokana na vikwazo vya kisiasa na mizozo ya kimataifa, wachezaji wengi wa kulipwa wa Urusi wanasakata soka lao katika Ligi Kuu ya nchini mwao (RPL) au ligi nyingine barani Ulaya kama Ufaransa (Ligue 1].

Mijadala mingine kuhusu Kombe la Dunia;

Safonov wa PSG alyewanyima uefa ni mrusi

Baada ya kuchukua ubingwa alikuwa analia tu familia yake hairuhusiwi kuingia ulaya so alkuwa mpweke wenzie wakat wapo na familia zao wakichukua snap
 
So huyo refa wa Somalia akirud kuchezesha World Cup atakua nae ni takataka tuu, mwanaume huwezi zungushwa hivyo km takataka
 
FIFA iko hivyo miaka zote, iinatumika kisiasa kukandamiza mataifa mengine huku wakijifanya siasa hairuhusiwi kwenye soka. Israel imevamia Palestina, inaua, inateka na kuua mamlioni ya ya raia lakini haijawahi kufungiwa. Mashindano yakifanyike nchi zingine wakizingua wanachapwa faini haraka sana au kufungiwa kama Indonesia ila Marekani huoni hata tamko tu
 
Kwani Marekani ina kosa gani kwa sababu kisheria kila nchi ina haki ya kujilinda kiusalama.

Na shida ya wanaoenda kuangalia mashindano ya kombe la dunia ni kwamba wengine wakifika huko hawataki kurejea makwao na badala yake watataka wazamie ili kukimbia shida katika nchi zao na Marekani wanalifahamu hilo.

Kila mwaka mamilioni kwa mamilioni ya watu hutafuta viza ya Marekani ili wakazamie huko.
 
Haikua na mpango wa kufatilia hao wazamiaji? Suala la mashabiki kuja kuzishangilia timu zao mbona ilo sio jambo geni. Yule refa msomali hata angezamia mbona kumpata ingekua rahisi tu
 
Hata mashindano ya ngazi ya club hawachezi mfano uefa champions league na ueropa timu za russia hazishiriki kama ikivyokua zamani
 
Kama USA imemrudisha refa wa Somalia, basi ile ni isue ndogo sana kwa Marekani, hili la Urusi Gen Z na millenia hamjui.

Urusi haishiriki Kombe la Dunia la 2026 kwa sababu FIFA iliweka kizuizi rasmi kinachozuia timu hiyo kushiriki katika mashindano yake yote tangu mwezi Februari 2022.

Hali hii ilitokana na uvamizi wa kijeshi wa nchi hiyo nchini Ukraine, ambao ulisababisha mashirikisho ya soka duniani kuitenga nchi hiyo kisiasa na kimichezo.

Kutokana na adhabu hiyo, timu ya taifa ya Urusi haikuruhusiwa kushiriki kwenye mechi za mchujo (qualifiers) za kuwania nafasi za kufuzu fainali hizi za 2026 zinazoandaliwa na nchi za Marekani, Mexico, na Canada.

Pia, Soma:
Hivi sasa (2026), hakuna wachezaji kutoka nchi ya Urusi wanaocheza kwenye Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) wala Ligi Kuu ya Hispania (La Liga). Kutokana na vikwazo vya kisiasa na mizozo ya kimataifa, wachezaji wengi wa kulipwa wa Urusi wanasakata soka lao katika Ligi Kuu ya nchini mwao (RPL) au ligi nyingine barani Ulaya kama Ufaransa (Ligue 1].

Mijadala mingine kuhusu Kombe la Dunia;

Ukifungiwa na Marekani umefungiwa Duni nzima
 
Marekani kavamia Iran, hajafungiwa! Ama utofauti uko wap kati ya Russia kuvamia Ukraine na USA kuvamia Iran?
 
Haikua na mpango wa kufatilia hao wazamiaji? Suala la mashabiki kuja kuzishangilia timu zao mbona ilo sio jambo geni. Yule refa msomali hata angezamia mbona kumpata ingekua rahisi tu
Marekani ni special case nchi zingine hizo hakuna watu wanaopenda kuzamiamo.
 
Walitakiwa kuongeza ulinzi sio kuzuia watu wasiingie nchini mwao. Ni matumaini yangu uko mbeleni mwenyeji mwingine akipiga hizi marufuku za timu, marefa na mashabiki kuingia kwenye nchi yake nae pia ataeleweka
 
Back
Top Bottom