Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,815
- 11,992
Katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 5 mwezi Juni, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limetembelea na kutoa misaada ya kulinda mazingira katika Hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kukabidhi misaada hiyo ya Mapipa ya kuhifadhi taka, Hamad Taimur ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria wa NEMC amesema “Kaulimbiu ya Mwaka 2023 inasema ‘Pinga uchafuzi wa Mazingira Utokanao na Mifuko ya Plastiki’.
Amesema “Kanuni zimekataza matumizi ya mifuko ya plastiki Nchini lakini zipo plastiki baadhi ambazo zinaendelea kutumika katika utaratibu mzuri wa kutumika.
“Tumetoa baadhi ya vifaa vinavyoweza kusaidia kutenganisha taka kwa kuwa zinatakiwa kutengwa kulingana na aina yake.
“Mfano taka hatarishi zinapatikana kwa wingi maeneo ya hospitali, tunawakabidhi mapipa makubwa ya kutunzia taka na pia tunawapongeza Muhimbili kwa kuwa na utaratibu mzuri wa kutunza mazingira.
“Timu yao inafanya vizuri, tunaomba taasisi nyingine au hospitali kufuata mfano wa Muhimbili, hatutarajii kuona taka za hospitali zikipatikana mtaani.
“Kuna sehemu maalum Muhimbili ya kuteketeza taka kulingana na aina ya taka husika, kabla ya kufika hatua hiyo zinatenganishwa kupitia mapipa yanayotumika kama haya tunayogawa leo.”
Neno la Muhimbili
Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi na Matengenezo Muhimbili, Domiana John akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi, amesema wanashukuru NEMC kwa msaada huo kwa kuwa tunu kubwa ya taasisi hiyo ni usalama.
Amesema “Tunaunga mkono kauli mbiu ya Mwaka huu isemayo ‘Pinga uchafuzi wa Mazingira Utokanao na Mifuko ya Plastiki’, ili kuendelea kulinda mazingira ya watu wote wanaofika eneo la Muhimbili.”