NEMC imetoa mwezi mmoja kwa viwanda vinavyozalisha Chupa za plastiki zenye rangi kuweka utaratibu wa kukusanya na kuhifadhi chupa hizo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Baraza la Usimamizi na Utunzaji Mazingira Nchini NEMC imetoa mwezi mmoja kwa viwanda vinavyozalisha chupa za plastiki zenye rangi kuweka utaratibu wa kukusanya na kuhifadhi chupa za rangi ambazo zimekuwa zinachafua mazingira kwa kuzagaa maeneo mbalimbali.

Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samweli Gwamaka amewataka wamiliki wa viwanda hivyo kuweka utaratibu wa ambavyo vinatumia chupa za rangi kuweka utaratibu wa kurejeleza chupa hizo ili kuepuka uchafuzi wa mazingira

Dkt. Gwamaka amesema NEMC itafungia lile eneo tu linalofanya uzalishaji wa chupa za rangi mpaka watakapoweka mpaka wa kurejereza chupa hizo kwa ajili ya kutunza mazingira.
WhatsApp Image 2023-11-07 at 4.55.04 PM.jpeg

DKT. SAMWELI GWAMAKA - Mkurugenzi Mkuu NEMC

Kuhusu chupa za rangi kuchafua mazingira hasa pale zinapotupwa kwenye mitaro ya maji hasa katika maeneo mbalimbali hasa jiji la Dar es salaam, Baadhi ya wananchi wamesema wamiliki wa viwanda wanalo jukumu la kulinda mazingira kwa kutengeneza chupa ambazo ni rafiki kwa mazingi.

Utupaji wa chupa za rangi au plastiki katika mazingira unatajwa kama uchafuzi wa mazingira ambao unaweza ukaleta atahari kwa jamii kama vile mlipuko wa magonjwa na Ili kuendelea kutunza na kuhifadhi mazingira dhidi ya taka hizo jamii imezitaka mamlaka kuhakikisha wamiliki wa viwanda wanazalisha chupa rafiki.

Katika hatua nyingine Dkt. Gwamaka ametoa tahadhari kwa wachimbaji wa madini ambao wanamiliki visima vya tope sumu kuchukua tahadhari mapema ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza pindi mabwawa yatakapojaa hasa kipindi hiki cha mvua ambazo zinaendelea kunyesha.
WhatsApp Image 2023-11-07 at 4.55.07 PM (1).jpeg

DKT. SAMWELI GWAMAKA - Mkurugenzi Mkuu NEMC
3511d3e95dd54dbab6e7af0c679b0252.jpg
ffa5f99855a44e9caa359249b703c963.jpg
 
Energy drink zenyewe zifutwe tu vijana wa Ovyo wamebadilisha matumizi siku hizi. Vile siyo vinywaji vya kawaida
 
Nasikua vijana wanatumia hii kinywaji kupandishia mnara ili wakanyooshe pipe☹️
 
Back
Top Bottom