Mifuko ya Plastiki yazuiwa Muhimbili

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili umepiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kwa watoa huduma na ndugu wa wagonjwa katika mazingira ya hospitali (Upanga na Mloganzila) ikiwemo wodini na maeneo mbalimbali ya kutolea huduma.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma (MNH), Bw. Aminiel Aligaesha katazo hilo linatolewa kufuatia uwepo wa mifuko ya plastiki kwenye mazingira ya hospitali iliyopigwa marufuku na Serikali nchini.

“Mifuko hii inaletwa na baadhi ya ndugu wa wagonjwa ambao huitumia kama vibebeo vya chakula wanapokuja kutembelea ndugu zao waliolazwa wodini na baadhi ya watoa huduma hospitalini hapa” amesema Bw. Aligaesha.

Ameongeza kuwa katazo hilo linaanza mara moja na ni kwa kampasi zote mbili za Hospitali ya Taifa Muhimbili ambazo ni Upanga na Mloganzila.

Bw. Aligaesha ameiomba jamii kutoa ushirikiano katika kukabiliana na matumizi ya mifuko ya plastiki hospitalini hapa kwa kuwa lengo ni kulinda na kutunza ustawi wa mazingira ya eno hilo na watu wake.

Ikumbukwe kuwa, kauli mbiu ya Siku ya Mazingira Duniani mwaka huu ni Pinga uchafuzi wa mazingira utokanao na mifuko ya plastiki.
 
Back
Top Bottom