Siku nilipotoa rushwa

Siku nilipotoa rushwa

C=P+D-T-A - I
Corruption = Power +Discretion - Transparency - Accountability -Intergrity

Kukiwa na force ya kuweka proper policies, kukawa na Transparency katikia policy then accountability itakuwako penda usipende,
Discretion itaondoka, Integrity italazimishwa kuja, power haitakuwa tena power.

So we change the policies, but how to that is a mystery as the change itself will be infuenced by coruption!!!
 
HAIKA...
You are right ..ila nadhani the starting point is "self"....Kila mmoja angeaza kujibadilisha... fikra na mwenendo.. we could reach somewhere.... tatizo..hata the way tunavyoongea hapa ni kuangali wengine.. na si sis wenyewe.

Remember Leo Tolstoy aliwahi kusema hivi
" Everyone thinks of changing the world but no one thinks of changing himself"....
Food for thought..how can I change myself?
 
Kwa kweli na mimi nimeshakutana nayo mara nyingi kweli. Nimepata taabu kweli both kupokea na kutoa rushwa. Nafsi yangu haikubali kabisa ila saa zingine unajikuta unalazimika.

Alivyosema Womanofsubstanc na Haika, ni sahihi kabisa lazima watu tubadilike na tuanze na sisi wenyewe kwanza. Sasa hivi hilo ndilo jambo nahubiri kila siku kwa wanangu kwani madhara ya rushwa nayajua, nimeyaona na naendelea kuona yanavyodidimiza watu, jamii na taifa. Wengine walionizunguka nashindwa kwani kila mara utetezi wao ni kuhusu hali halisi. Na hilo mimi naliona, na kama nilivyosema awali. Nilishatoa rushwa mara nyingi tu pamoja na ufahamu wangu na nafasi nilizowahi shika. Siko proud hata kidogo, lakini ndio hivyo, vinginevyo leo nisingekuwa na kiwanja au sehemu ya biashara.

Jamani, tuendelee na uzi huu wa kubadili tabia zetu kwenye hili jambo la rushwa. Naamini tutafanikiwa kwani litatusukuma kutaka kuona yaliyo sahihi yanafanyika, yanafanyika kwa wazi na inavyostahili.
 
in a matter of life and death ... bwana nasasambua ... i.e hospitals bila hiyari natoa ... bila kujua idadi .... kwenye mahospitali yetu haya anaetaka kupata hela ya mlala hoi aende tu ... maana za kwangu ni lazima
Siyo tu hapo hata mahakamani mtoto mdogo wa miaka saba anabakwa ... mbakaji anamwaga senti ... kesi inaenda miaka tatu na beyond hata tarehe zinapangwa kwa kukubabaisha anaeshitaki isipokuwa makini kwa kula na PP then kesi inafutwa ... unaenda kwa vyombo vya kutetea haki za binadamu ... also as hopeless ni taasisi za kuuza sura tu .... AM SPEAKING THRU EXPERIENCE HERE

SOME SITUATIONS cannot be avoided they are mostly to your advantage ukitaka kupata ushindi

This is because ... rushwa ni kitu cha kiza i.e. cha kujificha sana ... ni sifa za shetani maana ni tamu kupindukia .. ni kama kutembea na mke wa mtu na huku unamjua ... kwani unanunua haki yako kwa mapeni.

Yakikukuta ndiyo utafahamu ... advantages and disadvantages za rushwa .... wameshazoea hawaachi ngo.. hata waongezewe mshahari ya mamilioni .. kwani udhaifu wa binadaamu ni kwamba hatutosheki
 
Naima... kupunguza rushwa inawezekana; lakini kwanza ni lazima tuiangalia kwa usahihi. Kwa miaka mingi tumekuwa tukiingalia "intellectually" kwambi ni kinyume na haki. Mifano iliyojadiliwa na bila ya shaka mingine inaonesha wazi kuwa watu wanaikataa rushwa intellectually kama kitendo cha aibu lakini linapokuja suala la wao wenyewe wanaona haiwahusu.

Nakumbuka tulikulaga viapo vya "Sitapokea wala kutoa rushwa"... wangapi kati yao wamekishika kiapo hicho? Ni lazima tubadili kupambana na rushwa from an intellectual angle... hii tumeshindwa.
 
Naimaomari..
Umegusa pale penyewe haswaaaaa......rushwa hutolewa kwa kificho... ni kama alivyosema Naimaomari... kuifananaisha na.......
Kila mtub almost anafanya lakini hafurahiii... analalamika pembeni tu..na kesho anatoa tena maana huduma anaitaka... wameshika mpini sie tumeshika makali... ukijitia kuvuta... utabata habari yako!
Nadhani hii vita ya ufisadi ..ambapo watu wana name and shame.. tusiishie kwa akina EPA na KAGODA tu...tushuke chini tuendeleee kuwataja... wataona haya... polepole tutashinda..tutumie multi-pronged approach kupambana nao wanaodai rushwa... MAHAKAMANI, MAHOSPITALINI, TAASISI MBALIMBALI... LETS NAME AND SHAME THEM! Tuandike majina yao hata hapa kwenye forum...utakuwa mwanzo mzuri... MAANA RUSHWA NI SIRI... TUITOE HIYO SIRI HADHARANI...
 
Ndio sababu nasema policies ndio zianze, kuanza nafsini ni vizuri sana, lakini kwa sababu ni kitu cha kujificha, tena wakati wa mahitaji muhimu ya haraka, then ushawishi kidogo tu unatosha kukulegeza msimamo wako au wangu.
Lakini ukijua kuna support ya policy inayotekelezeka, bila kisingizio, product inayotakiwa iliyo wazi, uwezekano upo unajulikana kwa uwazi, kabisa, then ushawishi utakuwa mgumu.
Mfano kama foleni ikipungua hospitali, then kunishawishi nikupe helea uniingize kwa dokta mapema itakuwa ngumu kidogo.
 
Haika lakini hivi kweli mfanyakazi wa Tanzania anaweza kuishi kwa kutumia mshahara wake kweli?
 
MKK hilo ndio swali.
Tumuulize nani? mimi nitasema ...................
sasa tufanyeje????

Mimi bahati nzuri niko kampuni binafsi, na sipokei rushwa, KABISA hata ulie. Sina mshahara mkubwa ila pia hakuna mianya mingi kwa hio wazo pia nalo liko mbali. (too risky)
Ila wafanyakazi wa kipato cha chini serikalioni wanajiendekeza, lakini hao wenye kutupwa sehemu za ajabu, wanaposhindwa kula na wakubwa, mbona wanaishi?
unajua hii rushwa ikipungua seriakalini, na warsha na semina elekezi pia zikipungua, hela zitaongezeka na mishahara itongezeka pia. (labda)
mi nadhani swala na mtu mmoja, kiongozi kuamua kujitoa sadaka na kulivalia njuga.
mi nadhani ni attitude ya kiongozi, commitment yake na upeo wake, bado hatuna kiongozi aliepania kuitoa rushwa, rushwa inaweza kupungua kwa 60% kwa muda mfupi, hiyo itakayobaki 40% ndio inahitaji nguvu kubwa
 
MKK hilo ndio swali.
Tumuulize nani? mimi nitasema ...................
sasa tufanyeje????

Mimi bahati nzuri niko kampuni binafsi, na sipokei rushwa, KABISA hata ulie. Sina mshahara mkubwa ila pia hakuna mianya mingi kwa hio wazo pia nalo liko mbali. (too risky)
Ila wafanyakazi wa kipato cha chini serikalioni wanajiendekeza, lakini hao wenye kutupwa sehemu za ajabu, wanaposhindwa kula na wakubwa, mbona wanaishi?
unajua hii rushwa ikipungua seriakalini, na warsha na semina elekezi pia zikipungua, hela zitaongezeka na mishahara itongezeka pia. (labda)
mi nadhani swala na mtu mmoja, kiongozi kuamua kujitoa sadaka na kulivalia njuga.
mi nadhani ni attitude ya kiongozi, commitment yake na upeo wake, bado hatuna kiongozi aliepania kuitoa rushwa, rushwa inaweza kupungua kwa 60% kwa muda mfupi, hiyo itakayobaki 40% ndio inahitaji nguvu kubwa

Haika,
There is more than kipato katika kufanya mtu apokee rushwa.Unajua kwa mfano taasisi zenye kulipa vizuri wafanyakazi wake wanakula rushwa kama hawana akili nzuri.Mfano kwenye mashirika ya kutoa misaada au grants... hao ma programme officers ambao mishahara yao inazidi milioni 3 kwa mwezi unaambiwa kuna baadhi yao haya vijana wanaograduate siku hizi hawatoi grant mpaka mshiko... TRA na kwingineko wanapata angalau kipato kinachowezesha kumudu maisha..nao rushwa utadhani ni sehemu ya fringe benefits zao... nadhani ni sahihi kusema rushwa imeshakuwa culture ya watanzania! Utashangaa watu wanapopata kazi hasa kwenye taasis za serikali..wengine hudiriki hata kuuliza.." huko kunalipa?" maana yake ni kuwa kuna opportunity ya kupata kitu kidogo?..haya..fikiria kipindi kile kulipokuwa na sheria inayohalalisha takrima... maana yake ni nini?? thank God NGOs zilifight a case in high court mpaka ikawa scrapped off!...inatia kizunguzungu ukifikiria sana.. haya walipokea vijisenti... je walikuwa wanapokea mshahara kichele??..
 
Sasa hamuoni kuwa kama tukikataka kukomesha rushwa tutakuwa tunakata jinsi ya watu wanaishi na kula na kulea familia zao. Hata hivyo swali langu ni je mkulima anaweza vipi kuishi mwaka mzima bila kula rushwa?
 
Sasa hamuoni kuwa kama tukikataka kukomesha rushwa tutakuwa tunakata jinsi ya watu wanaishi na kula na kulea familia zao. Hata hivyo swali langu ni je mkulima anaweza vipi kuishi mwaka mzima bila kula rushwa?

MKJJ,
Kufuatilia pia life styles za watu inaweza isilete tija sana... kumbuka kuna wanaotafuta pesa kihalali maana wanataka kuishi vizuri... na pia mkulima hana jinsi maana s/he has to make with what s/he has..bare minimums to survive... issue pia sio kufanya watu waishi maisha ya ufukara...may be katika kufuatilia huko ndo kuna codes of ethics ambazo hazifuatwi...labda tuendelee kulijadili hili tupate maoni zaidi...
 
Ni kiasi gani cha fedha ya mshahara kinaweza kumfanya mfanyakazi wa Tanzania akate rushwa ya shilingi elfu 10 au kuomba rushwa ya aina yoyote ile?
 
Hakuna kiasi chochote cha chini au juu kinachoweza kumfanya ahitajike kupokea au aweze kukataa rushwa.
Kinachoweza kumfanya mtu akatae rushwa ni mazingira.
je ataonekanaje? jamii itamchukuliaje? familia itamchukuliaje? kazini itakuwaje? mteja atamuonaje? kazi itabaki? future prospects zitakuwaje? mke/mpenzi atamuonaje?
sasa kama mazingira yote hayo yanamkumbatia huyo mtu kwa upendo, basi lazima atakuwa anaitafuta kila kona.
Mfano: Mume wangu angekubali kuvumilia foleni ya kufungiwa umeme, na familia nzima ingemuona shujaa na kuvumilia naye. Asingekuwa na haja ya kuharakisha.
LAkini alipofanya tu ujanja, tukapata umeme, alionekana shujaa hata na majirani na ndugu wote.
Mkulima wa kiwango chochote anaweza kukataa kuota rushwa akiamua. wapo wengi tu hasa wazee hawataki kabisa na ni watu wenye misimamo, na wanaumbua watu hadharani.
Nadhani its high time kuweka policies ambazo zitatusuport wenye kania kadogo kakupiga vita rushwa.
 
Ila watz na sisi tumezidi unakuta mtu anakuja ofisin kwako kisa kazoea kutoa rushwa uko kwingine unamhudumia anaaza mzee ambuli ya SODA basi.
Most of the time huwa nazikataa na kuwaambia ni wajibu wangu kufanya hayo and am paid for that.
Sasa imagine mtu kama huyo anakuletea mkwanja alafu umechacha si waweza kuuchukua!
Rushwa itaendela kushamili tuu juzi tuu nilioverspeed trafic akalamba 5000 yangu ivi ivi tena bila ata haya.Naona matrafic rushwa kwao ni halali tena wengi wametajirika kwa ilo na mbaya zaidi collection ya izo ruswa lazima uwakilishe fungu kwa bosi vinginevyo anakupeleka FFU
 
watu wenye kupokea rushwa si wa kipato cha chini kuliko wote.
Wenye kutoa rushwa ndio wenye kipato kidogo zaidi.
mfano nesi anakipato cha chini kuliko mhudumu wa duka la mswahili? au shoe shiner?
au walimu wanavyongangania tuisheni, ni mishahara au basi tu? mashindano?
 
Kumbe Bongo kuna rushwa mi nilijua ni ka utaratibu tu kakusaidia au kusukuma shughuli zako ziende kwa haraka na vizuri.
Kautaratibu haka kakushikana mikono jamani si ni kautamaduni ka siku nyingi.Kwani Kumwambia mwanao Ukifaulu vizuri mwaka huu nitakununulia baiskeli ni kumpa rushwa?
 
Mwanakijiji,

Mimi jana nimetoa rushwa BRELA, ndio, nasema kweli, hakuna haja ya kuficha wala kuona aibu.

Walificha file letu huku wanaokuja nyuma wanashughulikiwa na kuondoka. Baada ya wiki niliyemtuma akasema wanataka pesa, nikamwambia hao ni majambazi, ni sawa na majambazi kukuvamia na kusema usipotoa pesa tutakuua, je utafanya nini? Nikamwambia wapatie wanachotaka tuendelea na mihangaiko mingine. Alipowapatia pesa, file likaonekana, baada ya saa certificate yetu ikawa tayari.

Ndio maana RICHMOND, Norconsult, makampuni ya EPA yanapeta tu Tanzania kwasababu wao kutoa rushwa sio shida.

Kwa mwendo huo rushwa kuisha itakuwa shida sana. Kinachotakiwa ni kuwa na process
ambayo inaonyesha toka file la mtu linaingia mpaka mwisho pamoja na trigers zake, kwa mfano kama file halijashughulikiwa siku tatu, aliye nalo inatakiwa akajieleze kwa boss, kwanini imekuwa hivyo.

Mimi nina hasira sana na hawa wataalamu wetu wengi wa TZ. Wasije wakakosea kunipa cheo, nitakula nao sahani moja, wala hiyo sio siri.

Hao akina Jk na wenzake sina uwezo nao, lakini kwenye idara au kwenye kampuni, huko tutabanana mpaka kieleweke.

Hivi huyo mkuu wa BRELA ni yule yule ndugu yake MKAPA?
 
mzee Mtanzania wenzio watakuuliza...kwanini hukutega mtego wa TAKUKURU ili kuwaumbua hao jamaa?
 
mzee Mtanzania wenzio watakuuliza...kwanini hukutega mtego wa TAKUKURU ili kuwaumbua hao jamaa?

Mzee Mwanakijiji,

Kwanza sikuwa mimi na sio wote wana courage kiasi hicho cha kuwakamatisha wala rushwa.

Ningekuwa mimi nisingetoa labda kwenye mazingira magumu sana. Mimi wote wanaofanya kazi zangu huko maofisini huwa nawapa asante wakimaliza kazi kulingana na ufanisi wao lakini sio kabla ya kazi. Huenda natoa hata pesa ya maana kuliko ambayo wangeomba kama rushwa. Hata kule kwetu kijijini mtu akikufanyia kazi huwa tunasema ndaga fijo lakini hatutoi ndaga kabla ya kazi maana inaweza ku influence utendaji wa huyo mhusika.

Kama unatumia watu wengine TZ ni ngumu sana kuwataka wafuate principles zako zote, wengine tuko tayari kuumia lakini je hiyo sacrifice unaweza kuitumbukiza kwa mtu mwingine pia?

Pia sijui kama kwa mtu mmoja kumkamatisha mfanyakazi mmoja mmoja wa BRELA kunaweza
kusaidia sana.

Nikifanya kazi zangu mimi mwenyewe tunaweza hata kushikana mashati.
 
Back
Top Bottom