Habari,
Wananchi wenzangu ,Tanzania ni nchi Yetu ambayo tunapaswa kutambalia katika miongozo ya TANU mpaka CCM ya mwaka 1995,
Lakin kutokana na mmomonyoko wa maadili na tamaa ya baadhi ya watendaji wa serikali na mashirika binafsi wameyaweka kando maadili hayo,
Kila ofis imekuwa rushwa kila ofisi imekuwa kubaniana fursa kisa rushwa,
Tulipata faraja sana kwa kujitokeza sehem kama forum ambayo watu walipewa fursa ya kuongea bila woga na bila kubanwa, lakin suala la rushwa limekuwa hatari sana,
Naombeni tukomeshe huu mchezo, na ningeomba unisaidie suala moja tu we ndugu msomaji
Kama umewahi kutozwa RUSHWA, au unajua eneo ambalo liko na rushwa sana, taja hapa chini, au kama wahofia usalama wako niwekee katoka PM, mi najua pa kuyawasilisha hayo malalamiko,
Kumbuka kwamba habari ambayo utaleta PM Iwe ya uhakika na ukweli , na itabaki kuwa siri yangu na wewe uliyetuma hiyo PM, Nawasihi tutaje bila kuogopa, na haki yako utaipata, hakuna haja ya kujua jina lako mwanzoni wala hatuliitaji sana jina lako ila tunataka kisafisha sehem hiyo.
Tajeni hapa , kama waogopa njooni PM nafasi zipo za kutosha,
Sishangai kuona Uzi uu unaweza kunifanya kuzuiliwa maana habari nyingi zinaenda kugusa penyewe. Ila napata matumaini kuwa kwa kuwa hii ni jamii forums huu uzi utakuwa ,
Uzi uu tunaomba usiunganishwe na mwingine uache uwe huru,
Tuige mifano ya watu ambao au mataifa ambayo yanakemea rushwa kwa vitendo,
Britanicca