Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,763
- 40,990
Najua baadhi ya watu hawajawahi kutoa rushwa wala kupokea rushwa, sitashangaa kuna watu ambao hawajawahi kuona mtu akipokea au kutoa rushwa na hivyo kwao rushwa ni kitu wanachokiangalia kutoka mbali na kwa kutumia mantiki tu.
Kwa muda mrefu tumekuwa tukiambiwa kuwa rushwa ni adui ya haki na hivyo tuipige vita; lakini nikiwa nimetulia na kujaribu kujiuliza kama nimewahi kutoa rushwa na nilijisikiaje nilijikuta narudishwa nyuma miaka kadhaa hadi siku ile nilipojikuta natoa rushwa na yote yalipomalizika sikuhisi au kuona kuwa rushwa niliyotoa ilikuwa ni "Adui" ya haki yangu na kimsingi nilioona ni rafiki, msaada, na njia rahisi ya kupata haki yangu.
Kuna kiwanja ambacho nilikuwa nakipania kwa muda mrefu sana lakini watu wa Halmashauri hawakutaka kuniuzia. Eneo lenyewe wakati huo lilikuwa halijajengwa sana na bado jipya na viwanja ndiyo vimepimwa tu. Tayari hapo mtaani kulikuwa na viwanja vya majaji wawili, kamanda mmoja wa JWTZ na Daktari wa Mkoa fulani... sasa nilipotoka kiwanja ambacho kilikuwa karibu na huyo jaji ndiyo ilikuwa kasheshe na jamaa walijua kuwa eneo hilo lilikuwa "hot" hasa huko mbeleni (liko karibu za ufuko wa bahari)... Sasa viwanja vilikuwa vinauzwa kwa wakubwa hawa kwa kati ya milioni 3 hivi na kuendelea lakini hakuna kilichozidi milioni tano (at that time).
Lakini kwa sababu wanazozijua hao jamaa wakawa wananizungusha kweli kukipata wakati waliniquotia Shs milioni 3.5. Ikawa ni kuzungushana kila kukicha na kunipoteza muda wangu mwingi. Nikawa najitahidi kuwa mwadilifu na nikisema kuwa sitatoa rushwa... bahati mbaya muda wangu wa kurudi kijijini ukawa umefika na pressure ilikuwa kubwa nikamilishe hilo kabla ya kuondoka. Ndipo nilipojikuta nikichukua uamuzi wa "kupenyeza rupia pale penye udhia" na matokeo yake kesho yake nikapigiwa simu kuwa kibali na makaratasi mengine viko tayari. (nilipenyeza shs 500,000 ingawa mwanzoni walitaka kama 200,000).
Tangu wakati huo hadi leo, nimekuwa nikijiuliza kama rushwa kwa watu wengi inaonekana kweli ni adui wa haki au inaharakisha haki kupatikana. Nimetumia neno kuonekana kwa sababu kama adui haonekani kama ni adui basi yawezekana kuwa ni rafiki.
Swali langu, je wewe umewahi kujikuta unalazimika kupenyeza rupia ili upate unachostahili au ulifanya nini kukwepa kufanya hivyo na ukapata unachotaka katika muda na namna unavyotakiwa? Je, wale wanaopokea rushwa na wanaotoa rushwa ni nani hasa anachochea vitendo vya rushwa? Je, mfanyakazi wa Tanzania anaweza kweli kuishi kwa kipato chake bila "njia" hizi za pembeni na kufanya kazi kwa uadilifu? Je tufweza twa asante baada ya kufanikiwa au kupewa unachotaka kunachochea rushwa?
Je, ni mazingira gani yanaweza kukufanya kweli ukubali kutoa rushwa kidogo hata kama wewe mwenyewe hukubaliani nayo?