Siku nilipotemwa, niliambiwa haya....

Siku nilipotemwa, niliambiwa haya....

Katika maisha ya mapenzi kuachwa ni jambo la kawaida japo lisilozoeleka, halina mzoefu, kuona umeachwa halafu mwanamke huyo akachukuliwa na mwanaume mwingine, ukipiga picha kinachoendelea wakiwa kitandani, inaumiza sana. Nimekuwa na bahati mbaya ya kuachwa kila wakati, katika kuachwa kote huyu dada sitamsahau kamwe:
...... nilidhani unajua mapenzi, kumbe kitandani hakuna unachokijua, hujanirdhisha kabisa. Nikadhani atanipatia nafasi nyingine niboreshe zaidi, kumbe ndo kaniacha.

Wewe uliachwa kwa maneno gani??????

Hata MUNGU alisema tuishi na hawa watu kwa akili sana! nakumbuka yuko aliyeniacha kisa nilirudi nyumbani kutoka kazini na barua ya kusimamishwa kazi, nakwambia siku hiyo hiyo aliniambia aisee mimi naenda nyumbani kunashida kidogo!! akaniacha na mawazo kibao, alipofika kwao sikumpata tena hewani mpaka nilipowasiliana na ndugu yake mmoja akaniambia niko nae hapa ngoja uongee nae, alipopokea simu aliniuliza wewe nani?? nikamwambia babe inamaana sauti yangu huijui? hee!! maneno aliyonipa aisee nilikonda hadi nikahisi nimeota mkia! alinijibu kuwa ilikuwa zamani na nisimtafute wala kumsumbua! sikukata tamaa kiukweli nilipoteza muda wangu mwingi kuhangaika kumrudisha kuliko kutafuta kazi sehemu nyingine maana ndiye binti aliyenifundisha hata nini maana ya kiss na mambo mengine ni miaka ya 2004-2005! ila kwa wakati huo niligundua kitu muhimu sana, MAMA ni nguzo muhimu sana katika maisha ya mtoto wake, mama yangu aligundua hili tatizo aliamua kunifungia nyumbani kwetu na kunipa malezi kama ya mtoto wa miaka mitano,naweza kusema nilikuwa napewa semina juu ya nidhamu ya maisha na kuheshimu maamuzi! na baada ya miezi mitatu akili ilinifunguka nikaanza kupita huku na kule kutafuta kazi,kwa kipindi chote hicho mama yangu mzazi alikuwa akiniwekea fedha kwenye wallet bila mimi kujua ili tu niwe huru kiuchumi kiasi fulani! siku ya siku nilimuaga mama naenda ku enjoy weekend, niliingia mahali nikaanza kucheza pool table, baada ya muda nikamuona yule binti aliye ni mwaga aisee yuko anapiga bia kama hana akili nzuri na baba mmoja hivi, bila aibu aliniita na kunitambulisha kwa yule baba akiniambia huyu ndiyo MR wangu, mimi nikasema asante na nikamsalimia yule baba shikamoo nae akaitikia marahabaa unakunywa nini? nikamjibu asante mimi niko sawa! nikarudi kuendelea na pool table sijui nini kilimleta tena yule binti kwenye pool table, akawa anashabikia kila niki score ball! nilijisikia vibaya kuwa naye karibu nikaaga kwa kijana mwenzangu niliokua nacheza nae lakini akasisitiza tuendelee kwani hata nikishindwa atalipa yeye! yule binti akaropoka akisema haaa!! unacheza pool table huna hela!!? iliniuma sana tena baada ya kukumbuka wakati nikiwa na kazi pesa zangu alizitumia vyema kazi ilipoisha alinitosa kisa alijua hatapata hela na hapa tena ananifuata kunikashfu?? ilikuja nguvu kama upepo ndani ya kifua changu nikajikuta namtamkia maneno ambayo hata sikujua yametokea wapi, yalikuwa machache kama hivi "Ber..tha, hutapata mwanamume wakutulia na wewe maishani" alinijibu kwendraaa huko umekuwa MUNGU wewe!!
Sehemu yenyewe tulipokuwa ni ya kitalii kidogo hivyo kulikuwepo na hawa wenzetu weupe au wazungu, baada ya muda nikiwa na yule kijana niliyekuwa nacheza naye pool table akiniambia na yeye alivyoumizwa awali alikuja dada mmoja wa kizungu akiomba kucheza pool table jamaa yangu akaniambia cheza naye, ile tunaanza kucheza tu yule binti aliye niumiza awali akaja tena na kuanza kukebehi kwa mbalii na vicheko vya dharau ila kwa sasa nilimpuuzia, yule dada wakizungu kwakweli alikuwa mstaarabu aliniuliza kama navuta sigara nikamjibu hapana basi akasema yeye anavuta hivyo anatoka nje ili akavute alafu atarudi tuendelee kucheza, aliporudi tuliendelea na ndio ukawa mwanzo wa maswali unaishi wapi, unafanya kazi gani na alipogundua niko kwenye fani anayofanyioa kazi ndipo akafunguka na kuniambia yeye ni assistance manager katika lodge moja ndani ya hifadhi moja maarufu hapa tanzania ila bado iko kwenye stage za mwisho kumalizika ujenzi ila kama niko tayari atanipa nafasi ya kazi, nilimjibu kwa haraka niko tayari hata kesho! huwezi kuamini nilipata ajira siku hiyo hiyo na nilianza kazi baada ya wiki moja! yule dada alinifundisha mambo mengi sana katika maisha hususani kazi na kujiendeleza, mume wake na huyu mzungu naye aliamua niwe mrithi wa umanager mkataba wao utakapo isha na ikawa hivyo. sasa siku moja mama yangu mzazi ananipigia simu na kuniambia kunawageni wangu nyumbani na mimi niko mbali porini huko kazini, hii ni baada ya miaka mitatu kupita, wageni wangu walikuwa ni binti aliye nikimbia baada ya kazi kwisha pamoja na mama yake mzazi, sababu ya ujio wao eti ni kwamba ameokoka na anatatizo hivyo anahitaji kuongea na mimi aniombe msamaha yaishe na tuoane maana mchungaji wake amemwambia kuwa mimi ndiye mume wake ambaye MUNGU alimpa!! nilimuomba mama awahifadhi mpaka nitakapofika nyumbani kesho yake, nilipofika kweli nilimkuta amepungua na maumbile niliyomuacha nayo kwakweli yamepotea nasasa anaonekana mtu mzima sana! niliumia moyoni maana naamini nilipokutana naye kwa mara ya kwanza ndio ilikuwa mwanzo wangu wa kujua kupenda hivyo nakiri ni kweli bado nilikuwa na chembechembe za kumpenda na huruma iliniingia nilipomuona anapiga magoti na kuniambia nisamehe yaishe mimi ni mwanadamu tu! nilihisi kulia, ila ghafla nilisikia kinyaa ndani ya moyo wangu hisia zangu zilipoleta picha ya yule baba aliyekuwa naye na kunitambulisha kuwa ndiyo MR wake! nimjibu kwa haraka nimekusamehe na uwe huru kuolewa sitakufunga tena ndani ya moyo wangu wala kukuombea mabaya na ninafuta laana niliyokutamkia siku ile. maana alishuhudia mbele yetu kuwa ameshaachwa na wachumba watatu tangu aniache na wote walisha toa posa kwao ila wachumba hao walibadili msimamo na kuoa wengine na ndipo alipo amua kuokoaka na kuweka kila kitu wazi. baada ya kukubaliana na mimi kuwa hatutaweza kuoana na atulie huenda akapata mume na kweli kwa sasa amepata bwana na ana mtoto wa kiume!
Nilichojifunza katika haya maisha ya mapenzi baada ya mateso matakatifu ni kusamehe na kumwachilia aliyekuumiza atoke moyoni mwako na ikibidi kama yuko uliye muumiza mtafute umuombe msamaha ili ufunguke kutoka katika gereza la kuachwa na kuumizwa na tuepuke kukimbilia mapenzi mapya tena haraka haraka ili tu kupunguza maumivu matokeo yake utajikuta unaongeza umivu juu ya maumivu.
 
Sasa kama umeshaachwa mara nyingi, huoni kama kuna tatizo na afadhali huyo amekuambia ukweli inabidi ujirekebishe mapungufu uliyonayo tena mshukru sana huyo ndo atakufanya upunguze kuachwa.

supu ya pweza inaweza ikasaidia au tumuite mzizmkavu?
 
Mm nadhani sio uhandsome kashindwa kuacha kula kitimoto.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom