Siku Mtanzania atakapotumia haki yake kumchagua kiongozi anayemtaka ndio tutaona Maendeleo ya Kweli Tanzania

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
14,840
31,583
Hello Great Thinkers....

Moja ya vitu vilivyojirudia kutoka kwa wachangiaji kwenye hii topic niliyoiandika siku chache zilizopita ni jinsi Tanzania kulivyo na Maigizo kwenye uchaguzi... unaweza kupitia Uchaguzi ujao, Kanda ya Ziwa isiwe ndio Kanda inayotuchagulia Rais

Kwamba kila Uchaguzi ni Maigizo tu, kwamba Kiongozi/Rais tayari anakua ameshawekwa, kinachoendelea ndani ya Uchaguzi ni Maigizo tuonekane na sisi tuna exercise demokrasia.

Wengine wakasema, Mafisadi yana Influence kubwa ndani ya nchi, wameiteka TISS, Mahakama, na vyombo vingine..ambavyo badala ya kuserve wananchi vinaserve Mafisadi.

Majina Mafisadi, wengine wanaita 'deep state' n.k siyo Mageni, LOL.

Huu ukiritimba ambao uko deep rooted kwenye Nchi yetu unatakiwa Uondolewe.

It makes me sick kuona bibi yangu kule Mazimbu,lol anajikongoja kwenda kupiga Kura ( sijui anamchagua nani, 😀 😀 😀 ), kumbe kuna lifisadi limoja limetulia kwake, linamsanifu tuu....:mad::mad::mad:

Mbaya zaidi Maendeleo kwa bibi huyu na wanaomzunguka ni hafifu!

Siku tutakapopata Uchaguzi huru, tukamchagua kiongozi mzalendo, Maendeleo Tanzania yataenda kwa speed ya Rocket!

Nakuja kwenu Great thinkers.

Tunaondoaje hizi tawala za kifisadi ambazo ziko deep rooted kwenye Jamii yetu.

Mimi sidhani watanzania wote hatujui kabisa jinsi ya ku deal na hawa Culprits!

Somewhere Mtanzania mmoja ana idea jinsi ya kutoka kwenye hii trap,

Come Foward please...lol

Any information is useful...lol

Karibuni, lol
 
Huenda ccm kikawa chama pekee "kiasisi" kitakachobaki kutawala kwa mda mrefu sana.

Akili yangu ni fupi mno kuona nani na kwa namna gani tukakiondoa hiki chama. Chama dola, dola yao, nec yao, mahakama yao...
Division within? Mbona ilitokea 2015 ila wapiii...
 
Huenda ccm kikawa chama pekee "kiasisi" kitakachobaki kutawala kwa mda mrefu sana.

Akili yangu ni fupi mno kuona nani na kwa namna gani tukakiondoa hiki chama. Chama dola, dola yao, nec yao, mahakama yao...
Division within? Mbona ilitokea 2015 ila wapiii...

Kwa kweli CCM influence yake ni kubwa mno, hata tukisema tupambane kwa mtutu bado wameishikilia TISS,Police, Mahakama, sana sana wachache wataishia kupewa kesi za Ugaidi...
 
Huenda ccm kikawa chama pekee "kiasisi" kitakachobaki kutawala kwa mda mrefu sana.

Akili yangu ni fupi mno kuona nani na kwa namna gani tukakiondoa hiki chama. Chama dola, dola yao, nec yao, mahakama yao...
Division within? Mbona ilitokea 2015 ila wapiii...



Pengine kuna makosa wanaweza kuyafanya katika uchaguzi ujao na mabadiliko yakaanzia hapo,
Lakini pia si wote katika hivyo vyombo ulivyotaja hapo wako pamoja kwa mapenzi,
Mabadiliko yapo na yatafikiwa
Kila chenye mwanzo kina mwisho,haitojalisha mwisho wa aina gani ila mwisho upo.
 
Pengine kuna makosa wanaweza kuyafanya katika uchaguzi ujao na mabadiliko yakaanzia hapo,
Lakini pia si wote katika hivyo vyombo ulivyotaja hapo wako pamoja kwa mapenzi,
Mabadiliko yapo na yatafikiwa
Kila chenye mwanzo kina mwisho,haitojalisha mwisho wa aina gani ila mwisho upo.
Mkuu, hao wachache wasiopenda ujinga wa ccm wakikohoa tu wanapumzushwa kwa amani.

Bahati mbaya kubwa tuliyonayo, watu hasa wakiwemo opposition wanajazwa matumbo yao na kuacha kuipigania nchi. Hilo ndio tatizo kubwa zaidi.
 
Kwan Mtanzania anahitaji kiongozi/Viongozi gani??

Hawa waliopo hawafai??

Huyo kiongozi au Viongozi wazuri ambao Mtanzania anawataka wako wapi?, Wana Sifa gani?, Wamejificha wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app

Mnhhhh, Mtanzania anahitaji Kiongozi Mzalendo atakayejali maslahi yake na ya watanzania kwa ujumla.

Hawa waliopo wote ni CCM wameoza!,

Viongozi wazuri wapo,

Wapo Tanzania,

Wana sifa ya Uzalendo,

Hawajajificha wamefichwa na Mafisadi,

Mbegu yao isichipue
 
Hapo umegusia moja ya vipera vya democrasia,Kisha ukamalizia na jawabu la "maaendeleo".
Lazima tutafakari na kufanya utafiti wa kina kuhusu democrasia(yes ndio democrasia ni nzuri) na maandeleo, JE Demokrasia huzaa/huleta"maandeleo" katika nchi "maskini"...???

Ukifanya tafiti ya kutosha demokrasia ni matokeo ya "maendeleo",hakuna nchi iliyopata "maaendelo" kwa kutumia demokrasia(hapa ni muhimu kufahamu historia ambayo haijachujwa ya demokrasia na maendeleo)... Hapa bado hatuchagusa sokohuria(wto )na imf & world,utatu mtakatifu huu unavyobana koo nchi maskini:

PATA BENEVOLENT DICTATORS(Intelligent,well informed kuhusu ulimwengu,)PLUS KUWEKA MFUMO WA ELIMU BORA WA MAZINGIRA YENU,,hapa walau mtapiga hatua moja kwenda mbele.
 
Akili yangu ni fupi mno kuona nani na kwa namna gani tukakiondoa hiki chama. Chama dola, dola yao, nec yao, mahakama yao...
Division within? Mbona ilitokea 2015 ila wapiii...
Kila marefu yana ncha, Ila ncha zingine zipo mbali mno....Ila zinafikika ( muhimu ziwepo).
 
Hapo umegusia moja ya vipera vya democrasia,Kisha ukamalizia na jawabu la "maaendeleo". Lazima tutafakari na kufanya utafiti wa kina kuhusu democrasia(yes ndio democrasia ni nzuri) na maandeleo, JE Demokrasia huzaa/huleta"maandeleo" katika nchi "maskini"...??? Ukifanya tafiti ya kutosha demokrasia ni matokeo ya "maendeleo",hakuna nchi iliyopata "maaendelo" kwa kutumia demokrasia(hapa ni muhimu kufahamu historia ambayo haijachujwa ya demokrasia na maendeleo)... Hapa bado hatuchagusa sokohuria(wto )na imf & world,utatu mtakatifu huu unavyobana koo nch maskini: PATA BENEVOLENT DICTATORS(Intelligent,well informed kuhusu ulimwengu,)PLUS KUWEKA MFUMO WA ELIMU BORA WA MAZINGIRA YENU,,hapa walau mtapiga hatua moja kwenda mbele.
Mnhh Accountants/Financial Analysts mna kazi sana,lol, Maendeleo hayaletwi na Demokrasia, ila Maendeleo yanaletwa na Mafisadi sio??!!!...hizo hela walizojimbikizia zingekuwa injected kwenye shughuli za Maendeleo, si tungekua tumefika mbali...?lol
 
Tuna matatizo makuu matatu yameshikana.
1. Demokrasia
2. Uzalendo
3. Mabeberu.
Sitaelezea wajuvi wanajua kuwa kuheshim sana kanuni za demokrasia kunatudumaza kufanya mabadiliko chanya.
Demokrasia huwafaa wenye nia moja ya kutawalana.
Anayetaka kukabiliana na walioiteka nchi kidemokrasia awazie mbinu zinazopingana na mabadiliko ya kidemokrasia!
Kuhusu mabeberu inafahamika ni ngumu mno kuchukua maamuz magum ya kubadili mfumo unaowanufaisha mabeberu wa nje wakishirikiana na wa ndan. Mwenye uchumi mzur ana nguvu sana. Mabadiliko tokea nje yanawezekana kirahis kuliko kuanzia ndan. Kila kitu ni pesa sio mihemko tu! Kunahitajika support ya nje kuelekezwa ndan, licha ya gharama zake.
Kuhusu uzalendo ni wazi hata tukiwa na katiba nzuri kama sheria mama na sheria zake ambata lakin kama wenyewe hatuna uzalendo hakuna kitakachobadilika zaid ya kubadili tu majina ya vibaka wanaotutunzia fuko la taifa!
Wananchi kwa ujumla wao bado hatujui tunataka kwenda wapi, tumetoka wap na tuko wapi. Wapatikane wenye nia ya dhat kubadiki mambo twende mbele na sio hawa wa sasa wamejichorea mstar mwisho ni kula wao. Siasa ajira! Tumegawanyika kutokana na uwepo wa tofaut za ufaham (informed)na uelewa(knowledgeable)!
Kwa sasa adui wa taifa ana nguvu zaid ya tujuavyo.
Afueni iliyopo ni moja tu kuwa sio ghost.
....Kwa anayehitaji nini kifanyike ukiachilia hizo porojo na u keyboard warriorship ni kanuni moja tu.....IF YOU WANT PEACE START WAR(The hard way!)
Namaanisha tunahitaji akina Jesus na tukio la msalaban!
Ikifikia hali ambapo walioiteka nchi na familia zao hawawez kutoka nje, hawawez kula na kunywa wamekaa, hawawezi kupitapita kudanganya, hawawez kukuibia na kukuita lofa, hawawezi kusali wala kustarehe hadharan.....
Hapo ndo kutakuwepo na kukaa mezan kwa mabadiliko halisi.
Hata hivyo kuna karata 3 zipo mkononi. Hata kama ziambatane na dua na sala.
A. Endapo giant party itaparanganyika wao kwa wao.
B. Endapo external pressure itakuwa kubwa.
C. Endapo mama mpenda haki na ustaarab kwa sabab ya kupewa elimu dunia na ahera, akiamua kuweka historia iliyosubiriwa na babu zake kuifanya zanzibar huru kwa kuruhusu katiba mpya na tume huru itakayozaa serkali ya mseto bara(hili litamsaidia kukaa zaid madarakan kwa kusubiri kipind cha mpito baada ya white paper!)
 
Back
Top Bottom