Je, unafahamu nini kuhusu dira ya Maendeleo ya Tanzania?

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
626
938
1685896840027.png

Je, unafahamu nini kuhusu dira ya Maendeleo ya Tanzania?

Je, ni upi umuhimu wa kuwa na Dira ya Maendeleo ya Taifa inayotekelezeka kwa wakati na kwa kuzingatia rasilimali zilizopo?

Je, Dira ya Maendeleo ya Tanzania inahusu uelekeo wa nchi pekee au kuna zaidi ya hivyo?

Ungana nasi katika mjadala huu utakaofanyika kupitia Twitter Spaces ya JamiiForums Juni 8, 2023, kuanzia Saa 12 jioni hadi Saa 1 usiku.

Link ya Mjadala: https://twitter.com/i/spaces/1rmGPkABkmmKN

Pia unaweza kutoa maoni yako kupitia uzi huu, yatasomwa siku ya mjadala.

---

- Mjadala umeanza

DIRA YA MAENDELEO YA TANZANIA: Mjadala maalum kuhusu umuhimu wa kuwa na Dira ya Maendeleo ya Taifa inayotekelezeka kwa wakati na kwa kuzingatia rasilimali zilizopo unaendelea kupitia Twitter Spaces ambapo Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa pamoja na Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe ni sehemu ya wazungumzaji.

Dira ya Maendeleo ya Tanzania (Tanzania Development Vision-TDV) 2025 ilianzishwa Mwaka 1994 na kuzinduliwa rasmi Mwaka 1999 ambapo utekelezaji wake ulianza Mwaka 2000Lengo kuu ni kuongoza harakati za Maendeleo ya Uchumi na Jamii zitakazoiwezesha Tanzania kufikia Uchumi wa kati na kuondokana na Umasikini uliokithiri ifikapo Mwaka 2025 (Chanzo http://tanzania.go.tz)Shiriki kwenye Mjadala kuhusu Dira hii unaoendelea sasa kupitia Twitter Spaces ya JamiiForums.

- Malengo makuu matano yalioainishwa katika Dira ya Maendeleo 2025 ni:

- Kuboresha hali ya Maisha ya kila Mtanzania,

- Kuwepo kwa Mazingira ya Amani Usalama na Umoja

- Kujenga Utawala bora

- Kujenga Jamii iliyoelimika na kujenga uchumi imara unaokabiliana na ushindani.

MWAITENDA AHOBOKILE (Mtaalam wa Mambo Uchumi, Fedha, Uwekezaji): Malengo ya Dira ya Maendeleo wakati wa Utawala wa Rais Mkapa ilikuwa kuboresha maisha ya Watu, kudumisha Amani na Mshikamano, kuweka msingi imara wa Utawala Bora, kuboresha Mifumo ya Elimu na kuimarisha Uchumi Wetu. Utawala bora ni kitu kipana ili kutimiza hilo inatakiwa kuangalia maslahi ya Wananchi ikiwemo kuwa na maisha bora.

Mwaitenda Ahobokile: Tunapozungumzia maadili tunaanzia kwenye jamii, mfano kama kijana anaiba mitihani, unadhani huyo hawezi kuiba akiwa kwenye Ofisi ya Umma? Mambo ya Utawala Bora yanatakiwa kuanzia katika Sheria mama ambayo ni Katiba.

Baadhi ya Mawazo ya Zitto Kabwe
1686241570471.png

Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo): Dira ya Maendeleo kwa lugha nyepesi unaweza kujiwekea wewe mwenyewe binafsi kulingana na maendeo binafsi unayoyategemeaDira ya Taifa ni ile ambayo inakuwa na mambo makubwa ya Nchi, pia kila Nchi inaweza kujipangia Dira yake kwa kipindi maalum, mfano miaka mitano, kumi na zaidi.

Zitto Kabwe (ACT Wazalendo): Wakati tunaandaa Dira mpya lazima tuwe na mipango maalum-Moja ya mfano wa Dira ya Taifa ilikuwa na kuwezesha kipato cha Mtanzania kuwa na wastani wa kipato cha Dola 3,000 lakini hivi sasa pato la Mtanzania ni takriban Dola 1,400 kiasi ambacho hatujafika hata nusu ya dira tuliyojiwekea.

Zitto Kabwe (ACT Wazalendo): Katika maeneo ambayo hatujafanya vizuri kabisa kwenye Dira ya Maendeleo ni Utawala BoraMfano, Wasimamizi wa Uchaguzi hawakuwa Wakurugenzi, ilikuwa ni mtu yeyote anaomba kazi. Kwa sasa wasimamizi wengi ni Makada wa Uchaguzi.

Katika Dira ya Maendeleo ya Taifa upande wa Sheria ya Habari hatujafanya vizuri, angalau Sheria ya Ulinzi Binafsi imeonyesha kuna kitu, hapa namtolea mfano mtu kama Maxence Melo kwa mchango wake katika Sheria hiyo, lakini Sheria nyingine katika Utawala Bora hatujafanya vizuri.

Zitto Kabwe: Katika Dira ya Maendeleo ya Taifa upande wa Sheria ya Habari hatujafanya vizuri, angalau Sheria ya Ulinzi Binafsi imeonyesha kuna kitu, hapa namtolea mfano mtu kama Maxence Melo kwa mchango wake katika Sheria hiyo, lakini Sheria nyingine katika Utawala Bora hatujafanya vizuri.

Katika maeneo ambayo hatujafanya vizuri kabisa kwenye Dira ya Maendeleo ni Utawala BoraMfano, Wasimamizi wa Uchaguzi hawakuwa Wakurugenzi, ilikuwa ni mtu yeyote anaomba kazi. Kwa sasa wasimamizi wengi ni Makada wa Uchaguzi.

Zitto Kabwe: Dira ya Maendeleo kwa lugha nyepesi unaweza kujiwekea wewe mwenyewe binafsi kulingana na maendeo binafsi unayoyategemeaDira ya Taifa ni ile ambayo inakuwa na mambo makubwa ya Nchi, pia kila Nchi inaweza kujipangia Dira yake kwa kipindi maalum, mfano miaka mitano, kumi na zaidi.

Hatuwekezi vya kutosha kwenye mawasiliano ndio maana kunakuwa na utata wa baadhi ya hojaBunge likiridhia TPA na DP World wakajadiliane ikitokea wakashindwana itamaanisha kuwa mkataba hautakuwepo na wanaweza kufanya mazungumzo na kampuni nyingineKinachokwenda kujadiliwa na Bunge si kuwapa DP World ruhusa ya kuendesha Bandari bali ruhusa ya mazungumzo kati ya pande hizo mbili.

Kuelekea mkataba wa Bandari, Bunge linatakiwa kuzingatia suala la muda, isiwe mambo ya miaka 100 au hakuna ukomo. Pia, kila baada ya miaka mitano Bunge liweze kupewa taarifa kama Mkandarasi kafikia viwango vinavyotakiwa.

Baadhi ya Mawazo yaliyotolewa na Gerson Msigwa (Msemaji wa Serikali)

1686243598741.png
GERSON MSIGWA (Msemaji Mkuu wa Serikali): Mkataba ulioingiwa ni wa mashirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai. Baada ya makubaliano hayo mchakato huo utaenda Bungeni, baada ya kuridhiwa ndio itafuata mikataba ya utekelezaji.

Tusiwaambie watu kuwa tayari Tanzania imeshakamilisha mchakato huo wa mkataba wa Bandari, tusiwapotoshe WananchiBandari zetu ufanisi uko chini, Serikali imeamua kutumia utaalamu ulipo Duniani.

Mwaka jana mapato ya Bandarini yalikuwa Tsh. Trilioni 1.08 lakini kati ya hizo Tsh. Bilioni 900 na kitu zilitumika kwenye uendeshaji, faida iliyopatikana ni Tsh. Bilioni 100 na kitu, sisi hatustahili kupata faida kama hiyo tunastahili kubwa zaidi ya hapo.

Kuhusu mkataba wa Bandari, hatujazungumza na DP World peke yake, tumezungumza na makampuni mengi-Watu wanatakiwa kujua pia huko ambapo DP World walishindwana wajue walishindwana kwa sababu zipi. Watu wajue kuwa bado Serikali haijasaini mkataba na DP World
 
Back
Top Bottom