Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,340
- 51,903
SIKU HIZI KILA FANI NA CHEO KINADHARAULIWA KWA SABABU HII
Anaandika, Robert Heriel.
Mtibeli
Siku hizi hata uwe Mfalme, sijui Waziri, sijui Hakimu, sijui Rais, sijui Kuhani, sijui Mwalimu, sijui Mwanasheria, sijui Mwanajeshi, sijui polisi, au hata uwe Nabii. Kote Huko Kwa kizazi hiki utadharauliwa tuu.
Zipo sababu za kizazi hiki kuwa na dharau.
Fikiria Kwa sasa unamiaka 30 hivi. Alafu ulisoma na marafiki zako kibao ambao unaujua uwezo wao. Unajua kabisa baadhi Yao walikuwa wadhaifu darasani, unajua kabisa Fulani alifeli kidato cha nne lakini Leo unaambiwa ati ni Mwalimu anafundisha Watoto. Automatic dharau itaingia
Fikiria unajua kabisa Fulani Wakati unasoma naye hakuwa mwadilifu, alikuwa mwizi na mtu asiye na uadilifu. Lakini Kutokana na connection unaambiwa Leo ni Mkurugenzi sijui WA nini Huko. Hivi utamheshimi mtu wa hivyo?
Fikiria Mchungaji au sheikhe Fulani ni mzinzi na anatoka na Wake za Watu. Sheikhe au Mchungaji huyohuyo kwenye matukio ya Gizani unakutana naye, hivi utaachaje kudharau fani na Cheo hicho?
Mtu unajua kabisa Fulani anauwezo mdogo wa shule lakini Kutokana na janjajanja za hapa na pale unamkuta paaap! Yule kule juu sijui ni Daktari WA nini Huko au Mwanasheria WA kitu gani sijui. Hivi mtu huyo na Cheo hicho utaacha kuvidharau.
Unajua kabisa Rafiki yako hakuenda jeshini Kwa mapenzi ya jeshi, isipokuwa alikosa option nyingine, na unajua kabisa amefuata Mshahara, hivi huo uanajeshi utauheshimu kweli?
Unajua kabisa marafiki zako baadhi wameingizwa Kwa connection na sio wito. Unafikiri utawaheshimu au kuheshimu hao Watu.
Unajua kabisa Mbunge Au Rais Fulani ameingia Kwa kuiba Kura, na anatumia nguvu ya Dola kulinda Cheo chake. Hivi Kwa Akili ya kawaida utamheshimu? Kwa maana kwa namna hiyo MTU yeyote hata mtoto Mdogo anaweza kuwa Mbunge au Rais ilimradi tuu Dola imlinde. Hivi hapo kuna heshima? Ni lazima Watu wadharau Cheo Hiko na fani husika.
Kizazi cha sasa kipi katika Njia sahihi. Kinaonekana hakina Maadili Kutokana na ukosefu WA uadilifu wa wale waliowatangulia. Huwezi mpa heshima MTU unayejua kabisa huyu sio muadilifu. Huwezi. Na katika Hilo Vijana WA sasa wapo wazi kabisa.
Heshima inatokana na uadilifu, maadili na nidhamu ya Watu Kwa Yale wanayoyafanya.
Utadharaulika tuu hata ungekuwa Nani kama iso mwadilifu. Pamoja na kuwa utajidanganya unaheshimika lakini ukitaka kujua kuwa wewe sio lolote wala chochote Subiri siku uwe nje ya hicho Cheo na hiyo fani ndio utajua kuwa wewe unadharaulika.
Hauhitaji kuwa na Cheo, Elimu, na utajiri ndipo uheshimike. Unahitajika kuwa tuu mwadilifu, kujiheshimu, nidhamu, na Maadili.
Kuna Watu wanaheshimika licha ya kuwa wapo Chini yako kifani, kielimu, kiutajiri na kicheo Kwa sababu ya uadilifu wao.
Unapodhulumu Haki za wengine wewe ni MTU uliyejidharau na kudhaulika tuu hata ujidanganye.
Nafasi uliyonayo unajua kabisa haustahili kuwa nayo na wapo wanaostahili. Hiyo pekee inakufanya ujidharau na kudharaulika.
Unaenda kuomba kazi, unatumia Rushwa Kupata kazi hiyo. Hakuna utakachopata zaidi ya kudharauliwa tuu. Utajidharau, utadharauliwa na familia yako hasa Mkeo na watoto, na Ndugu kisha na jamii.
Ninawajua Watu ambao wanakaribu kila kitu Kwa vitu vinavyoonekana lakini vitu hivyo ni vya dhulma, na wengi wao walidhani wangeheshimika lakini wanadharaulika hasa na familia zao wenyewe, mtu Hana furaha lakini anakila kitu. Huko ni kudharauliwa.
Mtu unakila kitu lakini Mkeo Hakupendi, anakupeleka peleka, Watoto wako wanakupasua kichwa. Hiyo pekee ni dharau. Ukidhulumu wengine na wewe utadhulumiwa na kudharaulika.
Tuwe waadilifu. Tenda Haki ikiwa ni pamoja na kujipa unayostahili na kuwapa wengine wanayostahili.
Usilazimishe mambo huo sio uadilifu, hiyo sio HAKI.
Sio lazima wewe uwe tajiri, sio lazima. Ukishafanya lazima ndipo unapoingia katika mazingira ya dhulma.
Sio lazima wewe uwe Waziri, Mbunge au Rais. Sio lazima. Ukishafanya lazima udhulumu wengine ambao hiyari imemchagua.
Sio lazima upate kazi unayoitaka, usilazimishe Mambo.
Sio lazima umpate Mwanamke ambaye umeshaona hakupendi. Hata utumie Pesa, Cheo au chochote. Hiyo Mwanamke sio wako. Hiyo ni dhulma. Na utadharaulika tuu Mimi Taikon nimesema.
Sio lazima mwanaume Fulani awe Mume wako ikiwa umeshaona hakutaki. Usitumie nguvu Sana. Hiyo ni dhulma. Ni kukosa uadilifu.
Acha nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam